Utendaji (4)

Amani na furaha Nizungumziayo leo sio sawa na kile ambacho unaamini na kufahamu. Ulikuwa ukifikiri kwamba amani na furaha yalimaanisha kuwa na furaha siku nzima, kutokuwako kwa magonjwa au misiba katika familia yako, kuwa mwenye furaha kila mara ndani ya moyo wako bila hisia hata kidogo za huzuni, na kuwa na furaha isiyoelezeka bila kujali kiasi ambacho maisha yako yamekua. Hilo lilikuwa ni pamoja na kupata nyongeza na mwanao kuingia katika chuo kikuu karibuni. Ukiwa unayafikiria mambo haya, ulimwomba Munguna, ulipoona kwamba neema ya Mungu ilikuwa kuu sana, ulikuwa na furaha sana, ukitabasamu kutoka sikio hadi sikio, na hungeacha kumshukuru Mungu. Amani na furaha kama hiyo siyo ndiyo amani na furaha halisi itokanayo na kuwa na uwepo wa Roho Mtakatifu. Badala yake, ni amani na furaha itokanayo na kuridhika kwa mwili. Unapaswa kufahamu enzi ya leo ni gani; siyo Enzi ya Neema, na si tena wakati ambapo unatafuta kulijaza tumbo lako kwa mkate. Unaweza kufurahi mno kwa sababu mambo yote yanaendelea vyema katika familia yako, lakini maisha yako yamo katika hali mahututi—na hivyo, haijalishi vile furaha yako ilivyo kuu, Roho Mtakatifu hayuko nawe. Kupata uwepo wa Roho Mtakatifu ni rahisi: fanya unachopaswa kufanywa kwa kufaa, tekeleza wajibu na kazi ya binadamu vizuri, na uweze kujiandaa na vitu unavyohitaji ili kufidia upungufu wako. Ikiwa kila mara una mzigo kwa ajili ya maisha yako na unafurahi kwa sababu umetambua ukweli au umefahamu kazi ya Mungu ya sasa, huku kweli ni kuwa na uwepo wa Roho Mtakatifu. Au, iwapo wakati mwingine unapatwa na wasiwasi kwa sababu unapitia tatizo fulani ambalo hujui namna ya kulipitia, au kwa sababu huelewi ukweli unaoshirikiwa, hili linathibitisha kwamba Roho Mtakatifu yuko nawe. Hizi ni hali za kawaida katika tukio la uzoefu wa maisha. Lazima uelewe tofauti kati ya kuwa na uwepo wa Roho Mtakatifu na kuukosa, na usiwe wa kawaida mno katika mtazamo wako wa hili.

Hapo awali, ilisemwa kwamba kuwa na uwepo wa Roho Mtakatifu na kuwa na kazi ya Roho Mtakatifu ni tofauti. Hali ya kawaida ya kuwa na uwepo wa Roho Mtakatifu inadhihirishwa katika kuwa na mawazo ya kawaida, mantiki ya kawaida, na ubinadamu wa kawaida. Tabia ya mtu itabaki kama ilivyokuwa, lakini ndani yake kutakuwa na amani, na nje atamstahi mtakatifu. Hivi ndivyo atakavyokuwa wakati ambapo Roho Mtakatifu yuko naye. Wakati ambapo mtu yuko na uwepo wa Roho Mtakatifu, kufukiria kwake ni kwa kawaida. Anapokuwa na njaa yeye hutaka chakula, anapoona kiu yeye hutaka kunywa maji. … Udhihirisho kama huu wa ubinadamu wa kawaida si nuru kutoka kwa Roho Mtakatifu; ni kufikiria kwa kawaida kwa watu na hali ya kawaida ya kuwa na uwepo wa Roho Mtakatifu. Watu wengine huamini kimakosa kwamba wale walio na uwepo wa Roho Mtakatifu huwa hawaoni njaa, kwamba huwa hawahisi uchovu, na huwa hawaifikirii familia, wakiwa takribani wamejitenga kabisa kutoka kwa mwili. Kwa kweli, kadiri Roho Mtakatifu alivyo na watu, ndivyo wanavyokuwa wa kawaida zaidi. Wanajua kuteseka na kujitolea kwa ajili ya Mungu, kujitumia kwa ajili ya Mungu, na kuwa waaminifu kwa Mungu; zaidi ya hayo, wao hufikiria kuhusu chakula na mavazi. Kwa maneno mengine, hawajapoteza chochote cha ubinadamu wa kawaida wanachopaswa kuwa nacho na, badala yake, wanakuwa hasa na mantiki. Wakati mwingine, wao husoma maneno ya Mungu na kuitafakari kazi ya Mungu; kuna imani ndani ya mioyo yao na wako radhi kufuatilia ukweli. Kwa kawaida, kazi ya Roho Mtakatifu inategemezwa juu ya msingi huu. Kama watu hawana fikira za kawaida, basi hawana mantiki—hii si hali ya kawaida. Watu wanapokuwa na fikira za kawaida na Roho Mtakatifu yuko nao, hakika wao huwa na mantiki ya mtu wa kawaida na hivyo, wao huwa na hali ya kawaida. Katika kupitia kazi ya Mungu, kuwa na kazi ya Roho Mtakatifu hutokea mara chache, ilhali uwepo wa Roho Mtakatifu uko takribani nyakati zote. Maadamu mantiki na fikira za watu ni za kawaida, na maadamu hali zao ni za kawaida, basi Roho Mtakatifu yuko nao kwa hakika. Wakati ambapo mantiki na fikira za watu si za kawaida, basi ubinadamu wao sio wa kawaida. Ikiwa, wakati huu, kazi ya Roho Mtakatifu iko ndani yako, basi Roho Mtakatifu atakuwa nawe pia kwa hakika. Lakini ikiwa Roho Mtakatifu yuko nawe, si lazima kwamba Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yako, kwani Roho Mtakatifu hufanya kazi katika nyakati maalumu. Kuwa na uwepo wa Roho Mtakatifu kunaweza tu kudumisha kuishi kwa kawaida kwa watu, lakini Roho Mtakatifu hufanya kazi tu katika nyakati fulani. Kwa mfano, kama wewe ni kiongozi au mfanyakazi, unapofanya kazi ya unyunyizaji au kuruzuku kwa ajili ya kanisa, Roho Mtakatifu atakupa nuru kufikia maneno fulani ambayo ni ya kuwaadilisha wengine na yanayoweza kutatua baadhi ya matatizo ya utendaji ya kina ndugu—katika wakati kama huo, Roho Mtakatifu anafanya kazi. Wakati mwingine, unapokuwa ukila na kunywa maneno ya Mungu, Roho Mtakatifu hukupa nuru kwa maneno fulani ambayo yanahusiana na matukio uliyopitia hasa, yakikuruhusu upate ufahamu mkubwa zaidi wa hali zako; hii pia ni kazi ya Roho Mtakatifu. Wakati mwingine, Ninapozungumza, ninyi husikiliza na huweza kupima hali zenu wenyewe dhidi ya maneno Yangu, na wakati mwingine ninyi huguswa au kutiwa moyo; hii yote ni kazi ya Roho Mtakatifu. Watu wengine husema kwamba Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yao nyakati zote. Hili haliwezekani. Ikiwa wangesema kwamba Roho Mtakatifu yuko nao kila mara, hilo lingekuwa la kweli. Ikiwa wangesema kwamba fikira na hisia zao ni za kawaida nyakati zote, hilo pia lingekuwa la kweli, na lingeonyesha kwamba Roho Mtakatifu yuko nao. Ikiwa wanasema kwamba Roho Mtakatifu hufanya kazi ndani yao kila mara, kwamba wamepata nuru kutoka kwa Mungu na kuguswa na Roho Mtakatifu kila wakati, na wanapata ufahamu mpya kila wakati, basi hili si la kawaida hata kidogo! Ni la kupita uwezo wa binadamu kabisa! Bila tashwishi yoyote, watu kama hao ni pepo wabaya! Hata wakati ambapo Roho wa Mungu huja ndani ya mwili, kuna nyakati ambapo lazima Ale, na lazima apumzike—sembuse mwanadamu. Wale ambao wamemilikiwa na pepo wabaya huonekana kutokuwa na hisia na udhaifu wa mwili. Wanaweza kutelekeza na kuacha kila kitu, ni wasio na hisia, ni wenye uwezo wa kustahimili mateso na hawahisi uchovu hata kidogo sana, kana kwamba wamevuka mipaka ya mwili. Je, hili silo la kupita uwezo wa binadamu kabisa? Kazi ya pepo waovu ni ya kupita uwezo wa binadamu—hakuna mwanadamu anayeweza kutimiza mambo kama haya. Wale wasio na utambuzi huwa na wivu wanapowaona watu kama hao; Wao husema kwamba wana nguvu mno katika imani yao katika Mungu, wana imani kubwa na kamwe hawaonyeshi ishara yoyote ya udhaifu! Kwa kweli, hili lote ni dhihirisho la kazi ya pepo mwovu. Kwa sababu watu wa kawaida bila kuzuilika huwa na udhaifu wa binadamu; hii ni hali ya kawaida ya wale walio na uwepo wa Roho Mtakatifu.

Maana ya kusimama imara katika ushuhuda wa mtu ni ipi? Watu wengine husema kwamba wao hufuata tu jinsi wanavyofanya sasa na hawajishughulishi na kama wana uwezo wa kupata uzima; wao hawafuatilii uzima, lakini hawajiuzulu pia. Wanakubali tu kwamba hii hatua ya kazi hutekelezwa na Mungu. Je, huku si kushindwa katika ushuhuda wao? Watu kama hao hata hawashuhudii kuhusu kushindwa. Wale ambao wameshindwa hufuata haijalishi mengine yote na wanaweza kuufuatilia uzima. Wao hawaamini tu katika Mungu wa vitendo, lakini pia hujua kuifuata mipango yote ya Mungu. Hao ndio huwa na ushuhuda. Wale wasiokuwa na ushuhuda hawajawahi kuufuatilia uzima na bado wanafuata kwa kumaliza jambo kwa kubahatisha. Unaweza kufuata, lakini hili halimaanishi kwamba umeshindwa, kwani huna ufahamu wowote kuhusu kazi ya Mungu leo. Masharti fulani lazima yatimizwe ili kushindwa. Sio wote wanaofuata wameshindwa, kwani ndani ya moyo wako hufahamu chochote kuhusu kwa nini ni lazima umfuate Mungu wa leo, wala hujui vile ambavyo umefaulu hadi leo, nani amekusaidia mpaka leo. Utendaji wa imani katika Mungu wa watu wengine huwa wenye kuchanganyikiwa na kukanganyikiwa; hivyo, kufuata si lazima kumaanishe kwamba unakuwa na ushuhuda. Ushuhuda wa kweli ni nini hasa? Ushuhuda uliozungumziwa hapa una sehemu mbili: Mojawapo ni ushuhuda wa kushindwa, na nyingine ni ushuhuda kwa kuweza kufanywa mkamilifu (ambako, kwa kawaida, utakuwa ushuhuda unaofuata majaribio makuu zaidi na majonzi ya siku za usoni). Kwa maneno mengine, ikiwa unaweza kusimama imara wakati wa majonzi na majaribio, basi utakuwa umekuwa na hatua ya pili ya ushuhuda. Kilicho cha maana sana leo ni hatua ya kwanza ya ushuhuda: kuweza kusimama imara wakati wa kila namna ya majaribu ya kuadibu na hukumu. Huu ni ushuhuda wa kushindwa. Hilo ni kwa sababu sasa ni wakati wa ushindi. (Unapaswa kujua kwamba sasa ni wakati wa kazi ya Mungu duniani; kazi kuu ya Mungu mwenye mwili duniani ni kushinda hili kundi la watu duniani wanaomfuata Yeye kupitia hukumu na kuadibu.) Kama una uwezo wa kushuhudia kuhusu kushindwa au la hakutegemei tu kama unaweza kufuata hadi mwisho, lakini, la muhimu zaidi, kama, unapopitia kila hatua ya kazi ya Mungu, unakuwa ba uwezo wa kuelewa kweli kuadibu na hukumu ya Mungu, na kama wewe kweli wewe unaitazama kazi hii yote. Hutaweza kupenyeza kwa kufuata tu hadi mwisho kabisa. Lazima uweze kusalimu amri kwa hiari wakati wa kila nafasi ya kuadibu na hukumu, lazima uwe na uwezo kuelewa kweli kila hatua ya kazi upitiayo, na lazima uweze kupata ufahamu wa, na utiifu kwa tabia ya Mungu. Huu ndio ushuhuda wa mwisho wa kushindwa ambao wewe unatakiwa kuwa nao. Ushuhuda wa kushindwa kimsingi unahusu ufahamu wako wa kupata mwili kwa Mungu. Cha msingi, hatua hii ya ushuhuda ni kwa kupata mwili kwa Mungu. Haijalishi kile ambacho unafanya au kusema mbele ya watu wa ulimwengu au wale wanaotawala; kilicho na maana kuliko vyote ni kama unaweza kuyatii maneno yote kutoka kinywani mwa Mungu na kazi Yake yote. Kwa hivyo, hatua hii ya ushuhuda inaelekezwa kwa Shetani na maadui wote wa Mungu—pepo na wenye uadui ambao hawaamini kwamba Mungu atakuwa mwili mara ya pili na kuja kufanya kazi hata kubwa zaidi, na zaidi ya hayo, hawaamini katika ukweli wa kurudi kwa Mungu kwa mwili. Kwa maneno mengine, inaelekezwa kwa wapinga Kristo wote—maadui wote wasioamini katika kupata mwili kwa Mungu.

Kumfikiria Mungu na kumtamani sana Mungu hakuthibitishi kwamba umeshindwa na Mungu; hili linategemea kama unaamini kwamba Yeye ni Neno lililopata mwili, kama unaamini kwamba Neno limepata mwili, na kama unaamini kwamba Roho amekuwa Neno, na Neno limeonekana katika mwili. Huu ndio ushuhuda muhimu. Haijalishi jinsi wewe unafuata, wala vile unavyojitumia mwenyewe; kilicho muhimu ni kama wewe unaweza kugundua kutoka kwa ubinadamu huu wa kawaida kwamba Neno limepata mwili na Roho wa kweli amepatikana katika mwili—kwamba ukweli wote, njia, na uzima umekuja katika mwili, na Roho wa Mungu hakika amewasili duniani na Roho amekuja katika mwili kwa kweli. Ingawa, kijuujuu, hili linaonekana kuwa tofauti na utungaji mimba kwa Roho Mtakatifu, katika kazi hii mnaweza kuona dhahiri zaidi kwamba Roho tayari amedhihirika katika mwili, na, zaidi ya hayo, kwamba Neno limepata mwili, na Neno limeonekana katika mwili. Unaweza kufahamu maana ya kweli ya maneno haya: “Mwanzoni kulikuwa na Neno, na Neno alikuwa na Mungu, na Neno alikuwa Mungu.” Zaidi ya hayo, lazima ufahamu kwamba Neno la leo ni Mungu, na utazame Neno likiwa mwili. Huu ni ushuhuda bora zaidi unaoweza kuwa nao. Hili linathibitisha kwamba una ufahamu wa kweli wa Mungu kupata mwili—mbali na kumjua Yeye, lakini pia unajua kwamba njia unayoifuata leo ni njia ya uzima, na njia ya ukweli. Hatua ya kazi ambayo Yesu alitekeleza ilitimiza tu kiini cha “Neno alikuwako kwa Mungu”: Ukweli wa Mungu ulikuwako kwa Mungu, na Roho wa Mungu alikuwa na mwili na alikuwa asiyetenganishwa kutoka katika mwili huo. Yaani, mwili wa Mungu mwenye mwili ulikuwa na Roho wa Mungu, ambalo ni thibitisho kuu zaidi kwamba Yesu mwenye mwili alikuwa kupata mwili wa kwanza wa Mungu. Hatua hii ya kazi hasa inatimiza maana ya ndani ya “Neno lakuwa mwili,” ilichangia kwenye maana ya kina zaidi ya “naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu,” na inakuruhusu wewe uamini kwa uthabiti maneno “Hapo mwanzo kulikuwako na Neno.” Ambalo ni kusema, wakati wa uumbaji Mungu alikuwa na maneno, Maneno Yake yalikuwa na Yeye na yasiyotenganishwa kutoka Kwake, na katika enzi ya mwisho, Yeye anafanya nguvu na mamlaka ya maneno Yake yawe hata wazi zaidi, na kumruhusu mwanadamu kuziona njia Zake zote—kuyasikia maneno Yake yote. Hiyo ndiyo kazi ya enzi ya mwisho. Lazima uelewe mambo haya yote kabisa. Si suala la kuujua mwili, bali la jinsi unavyouelewa mwili na Neno. Huu ndio ushuhuda unaopaswa kuwa nao, kile ambacho kila mtu lazima akijue. Kwa sababu hii ni kazi ya kupata mwili kwa pili—na mara ya mwisho ambapo Mungu anapata mwili—inakamilisha kwa ukamilifu umuhimu wa kupata mwili, inatekeleza kabisa na kutoa kazi yote ya Mungu katika mwili, na kuitamatisha enzi ya Mungu kuwa katika mwili. Hivyo, lazima ujue maana ya kupata mwili. Haijalishi unavyokimbia huku na huko, au vile unavyotekeleza vizuri masuala mengine ya nje; kilicho muhimu ni kama unaweza kutii kwa kweli mbele ya Mungu mwenye mwili na kuitoa nafsi yako yote kwa Mungu, na kutii maneno yote yatokayo kinywani Mwake. Hili ndilo unalopaswa kufanya, na unalopaswa kutii.

Hatua ya mwisho ya ushuhuda ni ushuhuda wa kama unaweza kufanywa mkamilifu au la—ambako ni kusema, kwa kuwa umeelewa maneno yote yaliyonenwa na kinywa cha Mungu mwenye mwili, umekuja kupata ufahamu wa Mungu na kuwa na hakika kumhusu Yeye, unaishi kwa kudhihirisha maneno yote kutoka kinywani mwa Mungu, na kutimiza masharti ambayo Mungu anakwambia—mtindo wa Petro na imani ya Ayubu—kiasi kwamba unaweza kutii hadi kufa, kujitoa mwenyewe kabisa Kwake, na hatimaye kutimiza mfano wa mtu ambaye anafikia kiwango kilichowekwa, kinachomaanisha mfano wa mtu ambaye ameshindwa na kufanywa mkamilifu Baada ya kupitia hukumu na kuadibu kwa Mungu. Huu ndio ushuhuda wa mwisho—ni ushuhuda ambao mtu ambaye hatimaye amefanywa mkamilifu anapaswa kuwa nao. Hizi ni hatua mbili za ushuhuda mnaopaswa kuwa nao, na zinahusiana, kila moja ni ya msingi. Lakini kuna jambo moja unalotakiwa kujua: Ushuhuda Ninaotaka kutoka kwako leo hauelekezwi kwa watu wa ulimwengu, wala kwa mtu yeyote mmoja, lakini kwa kile ambacho Nitakacho kutoka kwako. Kinatathminiwa na kama unaweza kuniridhisha Mimi, na kama unaweza kutimiza kabisa viwango vya masharti Yangu kwa kila mmoja wenu. Hili ndilo mnalopaswa kufahamu.

Iliyotangulia: Utendaji (3)

Inayofuata: Utendaji (5)

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp