4. Uhusiano Kati ya Kila Mojawapo ya Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

Maneno Husika ya Mungu:

Kutoka kwa kazi ya Yehova mpaka ile ya Yesu, na kutoka kwa kazi ya Yesu hadi kwa kazi iliyoko kwa awamu hii ya sasa, awamu hizi tatu zinajumlisha upana wote wa usimamizi wa Mungu, na zote ni kazi za Roho mmoja. Kutoka Alipoumba ulimwengu, Mungu Amekuwa Akisimamia wanadamu. Yeye ndiye Mwanzo na ndiye Mwisho; Yeye ndiye wa Kwanza na wa Mwisho, na Yeye ndiye mwanzilishi wa enzi na Yeye ndiye huleta enzi kwenye kikomo. Awamu tatu za kazi, katika enzi tofauti na maeneo mbalimbali, hakika yanafanywa na Roho mmoja. Wote ambao wanatenganisha awamu hizi tatu wanampinga Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)

Kazi ifanywayo katika siku za mwisho haiwezi kuwekwa mbadala wa kazi ya Enzi ya Sheria ama ile ya Enzi ya Neema. Ingawa, hatua zote tatu zinaungana kuwa kitu kimoja na yote ni kazi iliyofanywa na Mungu mmoja. Kawaida, utekelezaji wa kazi hizi umegawanyishwa katika enzi tofauti. Kazi iliyofanywa katika siku za mwisho inaleta kila kitu mpaka tamati; ile iliyofanywa katika Enzi ya Sheria ilikuwa ya mwanzo; na ile iliyofanywa katika Enzi ya Neema ilikuwa ya ukombozi. Na kuhusu maono ya kazi katika mpango wote wa usimamizi wa miaka elfu sita, hakuna anayeweza kupata ufahamu au kuelewa. Maono kama hayo yamebaki kuwa mafumbo kila wakati. Katika siku za mwisho, kazi ya neno pekee inafanyika ili kuukaribisha Wakati wa Ufalme lakini haiwakilishi enzi zile zingine. Siku za mwisho sio zaidi ya siku za mwisho na sio zaidi ya Enzi ya Ufalme, na haziwakilishi Enzi ya Neema au Enzi ya Sheria. Siku za mwisho ni wakati ambapo kazi zote ndani ya mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita inafichuliwa kwenu. Mafumbo kama hayo hayawezi kufichuliwa na mwanadamu yeyote. …

Kazi katika siku za mwisho ni hatua ya mwisho kati ya hizo tatu. Ni kazi ya enzi nyingine mpya na haiwakilishi kazi ya usimamizi mzima. Mpango wa miaka elfu sita umegawa katika hatua tatu za kazi. Hakuna hatua moja pekee itakayowakilisha kazi ya enzi hizo tatu ila inaweza tu kuwakilisha sehemu moja ya yote. Jina Yehova haliwezi kuwakilisha tabia yote ya Mungu. Ukweli kuwa Alitekeleza kazi katika Enzi ya Sheria sio ushahidi kuwa Mungu Anaweza tu kuwa Mungu chini ya sheria. Yehova alitengeneza sheria kwa mwanadamu na kutoa amri, Akimuuliza mwanadamu ajenge hekalu na madhabahu; kazi Aliyofanya inawakilisha tu Enzi ya Sheria. Kazi Aliyoifanya haidhibitishi kuwa Mungu ni Mungu Anayemwamuru mwanadamu kufuata sheria, Mungu Aliye hekaluni, ama Mungu Aliye mbele ya madhabahu. Haya hayawezi kusemwa. Kazi chini ya sheria inaweza tu kuwakilisha enzi moja. Kwa hivyo, kama Mungu Alifanya kazi katika Enzi ya Sheria pekee, mwanadamu angemfafanua Mungu na kusema, “Mungu ni Mungu Aliye hekaluni. Ili kumtumikia Mungu, lazima tuvae mavazi ya kikuhani na tuingie hekaluni.” Iwapo kazi katika Enzi ya Neema haingetekelezwa na Enzi ya Sheria ingeendelea mpaka wakati huu wa sasa, mwanadamu hangefahamu kuwa Mungu pia ni mwenye huruma na upendo. Iwapo kazi katika Enzi ya Sheria haingefanywa, na badala yake kazi katika Enzi ya Neema pekee, basi yote ambayo mwanadamu angefahamu ni kwamba Mungu Anakomboa tu mwanadamu na kumsamehe dhambi zake. Wangefahamu tu kuwa Yeye ni mtakatifu na asiye na hatia, kwamba Anaweza kujitoa kafara na kusulubishwa kwa ajili ya mwanadamu. Mwanadamu angejua tu kuhusu haya na asiwe na ufahamu wa mambo mengine yoyote. Kwa hivyo kila enzi inawakilisha sehemu moja ya tabia ya Mungu. Enzi ya Sheria inawakilisha vipengele vingine, Enzi ya Neema vipengele vingine na enzi hii vipengele vingine. Tabia ya Mungu inaweza tu kuonekana kwa mchanganyiko wa hatua zote tatu. Ni wakati tu mwanadamu anajua hatua hizi tatu ndipo anaweza kuipokea kikamilifu. Hakuna hatua kati ya hizo tatu ambayo inaweza kuachwa. Utaiona tu tabia ya Mungu kwa ukamilifu wake mara tu utakapozijua hatua hizi tatu za kazi. Ukweli kamba Mungu alikamilisha kazi yake katika Enzi ya Sheria sio ushahidi kwamba Yeye ni Mungu chini ya sheria tu, na ukweli kamba alikamilisha kazi Yake ya ukombozi haimaanishi kuwa Mungu Atamkomboa mwanadamu milele. Hizi zote ni hitimisho zilizofanywa na mwanadamu kuhusu jambo hilo. Enzi ya Neema ikiwa imefika mwisho, huwezi basi kusema kuwa Mungu ni wa msalaba tu na kuwa msalaba pekee unawakilisha wokovu wa Mungu. Ukifanya hivyo, basi utakuwa unamfasili Mungu. Katika hatua hii, Mungu Anafanya zaidi kazi ya Neno, lakini huwezi kusema kuwa Mungu hajawahi kuwa Mwenye huruma kwa mwanadamu na kwamba yote Aliyoleta ni kuadibu na hukumu. Kazi katika siku za mwisho inaonyesha wazi kazi ya Yehova na ile ya Yesu na mafumbo yote yasioeleweka na mwanadamu. Hii inafanywa ili kuonyesha hatima na mwisho wa binadamu na kukamilisha kazi yote ya wokovu miongoni mwa wanadamu. Hatua hii ya kazi katika siku za mwisho huleta kila kitu kufika mwisho. Mafumbo yote yasiyoeleweka na mwanadamu yanapaswa kufunuliwa ili kumpa mwanadamu ufahamu na kuweza kuelewa kwa kina katika mioyo yao. Hapo tu ndipo wanadamu wataweza kuainishwa kulingana na aina. Baada tu ya mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita kukamilishwa ndipo mwanadamu atapata kuelewa tabia ya Mungu kwa ukamilifu wake, kwani usimamizi Wake utakuwa umefika mwisho.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)

Kazi inayofanywa kwa sasa imesukuma mbele kazi ya Enzi ya Neema; yaani, kazi katika mpango mzima wa usimamizi wa miaka elfu sita imesonga mbele. Ingawa Enzi ya Neema imeisha, kazi ya Mungu imeendelea mbele. Kwa nini Ninasema mara kwa mara kwamba hatua hii ya kazi inajengwa juu ya Enzi ya Neema na Enzi ya Sheria? Hii ina maana kwamba kazi ya siku hii ni mwendelezo wa kazi iliyofanyika katika Enzi ya Neema na maendeleo ya kazi iliyofanyika katika Enzi ya Sheria. Hatua hizi tatu zinaingiliana kwa karibu na kuunganika moja kwa inayofuata kwa karibu. Kwa nini pia Ninasema kwamba hatua hii ya kazi inajengwa juu ya ile iliyofanywa na Yesu? Tuseme kwamba hatua hii haingejengwa juu ya kazi iliyofanywa na Yesu, ingebidi kusulubiwa kwingine kufanyike katika hatua hii, na kazi ya ukombozi ya hatua iliyopita ingelazimika kufanywa upya tena. Hii isingekuwa na maana yoyote. Kwa hiyo, sio kwamba kazi imekamilika kabisa, bali ni kwamba enzi imesonga mbele, na kiwango cha kazi kimewekwa juu kabisa kuliko kilivyokuwa kabla. Inaweza kusemwa kwamba hatua hii ya kazi imejengwa juu ya msingi wa Enzi ya Sheria na kwenye mwamba wa kazi ya Yesu. Kazi hii inajengwa hatua kwa hatua, na hatua hii sio mwanzo mpya. Ni muungano tu wa hatua tatu za kazi ndio unaweza kuchukuliwa kuwa mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili

Hatua ya kazi ya mwisho haisimami peke yake, ila ni sehemu ya yote iliyounganishwa pamoja na hatua mbili za awali, ambayo ni kusema kwamba haiwezekani kukamilisha kazi nzima ya wokovu kwa kufanya kazi ya hatua moja pekee. Ingawa hatua ya mwisho ya kazi inaweza kumwokoa mwanadamu kabisa, hii haimaanishi kwamba ni muhimu tu kutekeleza hatua hii pekee, na kwamba hatua mbili za hapo awali hazihitajiki kumwokoa mwanadamu kutokana na ushawishi wa Shetani. Hakuna hatua moja kati ya zote tatu inayoweza kuwekwa kama maono ya kipekee ambayo lazima yajulishwe mwanadamu, kwa kuwa ukamilifu wa kazi ya wokovu ni hatua tatu za kazi, wala si hatua moja kati ya tatu. Ilimradi kazi ya wokovu bado haijakamilishwa, usimamizi wa Mungu utashindwa kufikia kikomo. Nafsi ya Mungu, tabia, na hekima zimeonyeshwa katika ukamilifu wa kazi ya wokovu, wala hazikufichuliwa kwa mwanadamu hapo mwanzo, lakini zimeonyeshwa hatua kwa hatua katika kazi ya wokovu. Kila hatua ya kazi ya wokovu huonyesha sehemu ya tabia ya Mungu, na sehemu ya nafsi Yake: si kila hatua ya kazi inayoweza moja kwa moja kuonyesha kabisa na kwa ukamilifu nafsi ya Mungu. Kwa hivyo, kazi ya wokovu inaweza tu kuhitimishwa hatua tatu za kazi zitakapokamilika, na kwa hivyo, maarifa ya mwanadamu ya ukamilifu wa Mungu hayawezi kutenganishwa na hatua tatu za kazi ya Mungu. Kile ambacho mwanadamu hupokea kutoka kwa hatua moja ya kazi ni tabia ya Mungu inayoonyeshwa katika sehemu moja ya kazi yake tu. Haiwezi kuwakilisha tabia na nafsi inayoonyeshwa katika hatua ya awali na ijayo. Hii ni kwa sababu kazi ya kumwokoa mwanadamu haiwezi kumalizika mara moja katika kipindi kimoja, ama katika eneo moja, lakini hukuwa kwa kina hatua kwa hatua kulingana na kiwango cha kukua kwa mwanadamu katika wakati na maeneo tofauti. Ni kazi inayofanywa hatua kwa hatua, na haikamilishwi katika hatua moja. Na kwa hiyo, hekima yote ya Mungu imejumuishwa katika hatua tatu, badala ya hatua moja. Nafsi yake yote na hekima yake yote zimewekwa wazi katika hatua hizi tatu, na kila hatua ina nafsi Yake, na ni rekodi ya hekima ya kazi Yake. Mwanadamu anapaswa kujua tabia yote ya Mungu iliyoonyeshwa katika hatua hizi tatu. Nafsi hii ya Mungu ndiyo ina maana zaidi kwa wanadamu wote, na ikiwa watu hawana maarifa haya wanapomwabudu Mungu, basi hawana tofauti na wale wanaoabudu Budha. Kazi ya Mungu kati ya wanadamu haijafichiwa mwanadamu, na inapaswa kujulikana na wale wote wanaomwabudu Mungu. Kwa sababu Mungu ametekeleza hatua tatu za kazi ya wokovu kati ya wanadamu, mwanadamu anapaswa kujua maonyesho ya kile Anacho na alicho wakati wa hatua hizi tatu za kazi. Hili ndilo ambalo ni lazima lifanywe na mwanadamu. Kile ambacho Mungu anamfichia mwanadamu ni kile ambacho mwanadamu hawezi kutimiza, na kile ambacho mwanadamu hapaswi kujua, ilhali yale Mungu anayomfunulia mwanadamu ni yale ambayo mwanadamu anapaswa kujua na yale ambayo mwanadamu anapaswa kumiliki. Kila moja ya hatua tatu za kazi huendelea juu ya msingi wa hatua iliyopita; haitekelezwi peke yake, tofauti na kazi ya wokovu. Ingawa kuna tofauti kubwa katika enzi na aina ya kazi ambayo inafanywa, katika kiini chake bado ni wokovu wa mwanadamu, na kila hatua ya kazi ya wokovu ina kina kuliko iliyopita.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu

Usimamizi mzima wa Mungu umegawika katika hatua tatu, na katika kila hatua, mahitaji yanayofaa yanatakiwa kutoka kwa mwanadamu. Aidha, kadri enzi zinavyopita na kuendelea, mahitaji ya Mungu kwa wanadamu wote huwa ya juu hata zaidi. Kwa hiyo, hatua kwa hatua, kazi hii ya usimamizi wa Mungu hufikia kilele chake, hadi mwanadamu aamini ukweli wa “kuonekana kwa Neno katika mwili,” na kwa njia hii mahitaji ya mwanadamu huwa ya juu hata zaidi, na mahitaji ya mwanadamu kutoa ushuhuda huwa ya juu hata zaidi. Kadiri mwanadamu alivyo na uwezo wa kushirikiana na Mungu kwa kweli, ndivyo anavyozidi kumtukuza Mungu. Ushirikiano wa mwanadamu ndio ushuhuda anaohitajika kuwa nao, na ushuhuda alio nao ndio matendo ya mwanadamu. Na kwa hivyo, kazi ya Mungu iweze au isiweze kuwa na matokeo yanayohitajika, na paweze ama pasiweze kuwa na ushuhuda wa kweli, ni mambo ambayo yameunganishwa yasiyochanganulika na ushirikiano na ushuhuda wa mwanadamu. Wakati kazi itakapokwisha, yaani, wakati usimamizi wote wa Mungu utakapofikia kikomo chake, mwanadamu atahitajika kuwa na ushuhuda wa hali ya juu, na wakati kazi ya Mungu itakapofika mwisho wake, matendo na kuingia kwa mwanadamu vitafikia upeo wake. Wakati wa kale, mwanadamu alihitajika kutii sheria na amri, na alihitajika kuwa mwenye subira na mnyenyekevu. Leo, mwanadamu anahitajika kutii mipango yote ya Mungu na awe na upendo mkuu wa Mungu, na hatimaye bado anahitajika kumpenda Mungu katika taabu. Hatua hizi tatu ndizo Mungu anazozitazamia kutoka kwa mwanadamu, hatua kwa hatua, katika usimamizi Wake wote. Kila hatua ya kazi ya Mungu huzidisha kina kuliko iliyopita, na katika kila hatua, mahitaji kwa mwanadamu ni makubwa kuliko yaliyopita, na kwa njia hii, usimamizi mzima wa Mungu huonekana. Ni hasa kwa sababu mahitaji ya mwanadamu kila mara huwa ya juu kiasi kwamba tabia yake kila mara inafikia viwango anavyovihitaji Mungu, na ni hapo tu ambapo wanadamu wote wanaanza kujiondoa polepole kutoka kwa ushawishi wa Shetani hadi, ambapo kazi ya Mungu itafikia kikomo kabisa, ndio wanadamu wote watakuwa wameokolewa kutoka kwa ushawishi wa Shetani.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu

Kazi mzima ya mpangilio wa usimamizi wa Mungu inafanywa binafsi na Mungu mwenyewe. Awamu ya kwanza—uumbaji wa ulimwengu—ilifanywa binafsi na Mungu Mwenyewe, na kama haikuwa hivyo, basi hakuna yeyote ambaye angekuwa na uwezo wa kumuumba mwanadamu; awamu ya pili ilikuwa ukombozi wa wanadamu wote, na pia ilifanywa binafsi na Mungu Mwenyewe, awamu ya tatu inaenda bila kusemwa: Kuna haja kuu zaidi ya mwisho wa kazi ya Mungu kufanywa na Mungu Mwenyewe. Kazi ya ukombozi, ushindi, kumpata, na kumkamilisha wanadamu wote inafanywa binafsi na Mungu Mwenyewe. Kama hangefanya kazi hii Yeye binafsi, basi utambulisho wake hauwezi kuwakilishwa na mwanadamu, au kazi kufanywa na mwanadamu. Ili kumshinda Shetani, ili kumpata mwanadamu, na ili kumpa mwanadamu maisha ya kawaida duniani, Yeye binafsi humwongoza mwanadamu na hufanya kazi binafsi miongoni mwa wanadamu; kwa ajili ya mpangilio mzima wa usimamizi, na kwa kazi yake yote, ni lazima Yeye binafsi afanye kazi hii.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu

Iliyotangulia: 3. Kusudio na Umuhimu wa Kila Mojawapo ya Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

Inayofuata: 5. Kwa Nini Yasemekana Kwamba Kuzijua Awamu Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kujua Mungu?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp