XI Maneno Bora Zaidi Juu ya Kuingia Katika Uhalisi wa Ukweli

(III) Maneno Juu ya Kumtegemea na Kumwaminia Mungu

19. Mwenyezi Mungu Hutawala mambo yote na matukio yote! Ili mradi mioyo yetu inamheshimu Yeye wakati wote na tuingie katika roho na kushirikiana naye, basi Atatuonyesha mambo yote tunayotafuta na mapenzi Yake kwa hakika yatafichuliwa kwetu; mioyo yetu kisha yatakuwa katika furaha na amani, thabiti kwa uwazi kamili. Ni muhimu kuwa na uwezo wa kutenda kulingana na maneno Yake; kuwa na uwezo wa kuelewa mapenzi Yake na kuishi katika utegemezi wa maneno Yake—hii tu ndiyo kupitia kwa kweli.

kutoka katika “Sura ya 7” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

20. Mwenyezi Mungu, Mkuu wa vitu vyote, hushika madaraka Yake ya kifalme kutoka kwa kiti Chake cha enzi. Yeye hutawala ulimwengu na vitu vyote Naye Anatuongoza katika dunia yote. Mara kwa mara tutakuwa karibu Naye, na kuja mbele Zake kwa utulivu; kamwe hatutakosa wakati mmoja, na kuna mambo ya kujifunza wakati wote. Mazingira yanayotuzunguka pamoja na watu, mambo na vitu, yote yameruhusiwa na kiti Chake cha enzi. Usiwe na moyo wa kunung’unika, au Mungu hatatupa neema Yake juu yako. Wakati ugonjwa hutokea ni kwa sababu ya upendo wa Mungu, na nia Yake nzuri kwa hakika inaiunga mkono. Hata wakati mwili wako unavumilia mateso, usichukue ushauri kutoka kwa Shetani. Sifu Mungu katikati ya ugonjwa na furahia Mungu katikati ya sifa yako. Usikate tamaa unapokabiliwa na ugonjwa, endelea kutafuta na kamwe usisalimu amri, na Mungu Ataangaza nuru Yake kwako. Ayubu alikuwa mwaminifu kiasi gani? Mwenyezi Mungu ni daktari mwenye nguvu zote! Kukaa katika ugonjwa ni kuwa mgonjwa, lakini kukaa katika roho ni kuwa mzima. Kama unayo pumzi moja tu, Mungu hatakuacha ufariki.

Uzima wa Kristo Aliyefufuka uko ndani yetu. Kwa kweli tunakosa imani mbele ya Mungu, na hebu Mungu Atie imani ya kweli ndani yetu. Neno la Mungu ni tamu kweli! Neno la Mungu ni dawa yenye nguvu! Tilia aibu mapepo na Shetani! Kama sisi tutafahamu neno la Mungu tutakuwa na msaada na neno Lake litaokoa mioyo yetu kwa haraka! Linaondoa vitu vyote na kuweka yote kwa amani. Imani ni kama daraja moja la gogo la mti, wale ambao hushikilia maisha kwa unyonge watakuwa na ugumu katika kulivuka, lakini wale ambao wako tayari kujitolea wenyewe wanaweza kulivuka bila wasiwasi. Kama mtu ana mawazo ya uoga na ya kuogofya, wao wanadanganywa na Shetani. Ina hofu kwamba tutavuka daraja la imani ili kuingia katika Mungu. Shetani hubuni kila njia iwezekanayo kututumia mawazo yake, tunapaswa daima kuomba kwamba nuru ya Mungu itatuangazia sisi, na ni lazima daima tumtumainie Mungu kututakasa kutoka kwa sumu ya shetani. Daima tutakuwa tukitenda katika roho zetu kuja karibu na Mungu. Tutamruhusu Mungu kuwa na utawala juu ya asili yetu yote.

kutoka katika “Sura ya 6” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

21. Si kwamba imani yako ni nzuri au safi, lakini badala yake, kazi Yangu ni ya ajabu! Kila kitu ni kwa sababu ya rehema Zangu! Hupaswi kuwa na tabia potovu ya ubinafsi au kiburi hata kidogo, vinginevyo kazi Yangu kwako haitaendelea. Lazima uelewe wazi kwamba iwapo watu wanaanguka au kusimama imara si kwa sababu yao, ni kwa sababu Yangu. Leo, kama huelewi vizuri hatua hii, hutaweza kuingia katika ufalme! Lazima uelewe kwamba kile kinachofanywa[a] leo ni kazi ya ajabu ya Mungu; hakina uhusiano na mwanadamu. Je, matendo ya mwanadamu yana umuhimu gani? Wakati si mwenye ubinafsi, wenye kiburi, na mwenye majivuno, anakatiza usimamizi wa Mungu na kuharibu mipango Yake. Eh, ninyi wapotovu! Lazima unitegemee Mimi leo; usipofanya hivyo, leo Nitakuambia kwamba hutafanikisha chochote kamwe! Yote yatakuwa bure na shughuli zako hazaitakuwa na maana!

kutoka katika “Sura ya 38” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

22. Lazima usikilize maneno yote ambayo Roho Mtakatifu anafundisha; usimpuuze. Mara nyingi umesikia maneno Yangu na kisha ukayasahau. Ee wasio na fikra! Umepoteza baraka nyingi sana! Lazima usikilize kwa makini sasa na utilie maanani maneno Yangu, ufanye ushirika zaidi na Mimi na kusogea karibu na Mimi zaidi. Nitakufundisha juu ya chochote ambacho haukielewi, nami Nitawaongoza kwenye njia inayoendelea. Uzingatie sana kushirikiana na watu wengine maana kuna watu wengi sasa wanaohubiri maandishi na mafundisho, na wachache ambao wana uhalisia Wangu kwa kweli. Kusikiliza ushirika wao kutakufanya uchanganyikiwe na uwe asiyejali, bila kujua jinsi ya kuendelea. Hata ukiwasikiliza, unaishia tu kuelewa kidogo zaidi kuhusu maandishi na mafundisho. Lazima muangalie hatua zenu, mlinde mioyo yenu na kuishi mbele Yangu daima, muwasiliane na Mimi, mnikaribie na nitakuwezesha kuona ambayo huyaelewi. Lazima uangalie kile unachosema, uangalie kwa karibu moyo wako nyakati zote na kutembea katika njia Ninayotembelea.

kutoka katika “Sura ya 26” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

23. Lazima uwe wa vitendo katika kushirikiana na Mimi; kuwa na bidii na usiwe mvivu kamwe. Daima uwe katika ushirika na Mimi na uwe na urafiki wa kina sana na Mimi. Ikiwa huelewi, usikose subira kwa ajili ya matokeo ya haraka. Sio kwamba sitakuambia, Ninataka kuona ikiwa unanitegemea Mimi wakati unapokuwa katika uwepo Wangu na ikiwa unanitegemea Mimi kwa ujasiri. Lazima ubaki karibu na Mimi daima na kuweka mambo yote katika mikono Yangu. Usirudi nyuma. Baada ya kuwa karibu na Mimi kwa kipindi cha muda bila kujua, nia Zangu zitafichuliwa kwako. Ikiwa utazielewa, basi kweli utakuwa uso kwa uso na Mimi, na utakuwa umeupata uso wangu kweli. Utakuwa dhahiri na imara ndani na utakuwa na kitu cha kutegemea, na utakuwa na nguvu na ujasiri pia. Pia utakuwa na njia ya kusonga mbele na kila kitu kitakuja kwako kwa urahisi.

kutoka katika “Sura ya 9” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

24. Usione haya, usivunjike moyo au kuwa dhaifu. Fanya ushirika na Mimi moja kwa moja katika roho yako, subiri kwa ustahimilivu na Mimi kwa hakika Nitakufichulia kulingana na wakati Wangu. Wewe kweli, lazima kabisa utahadhari na usiache juhudi Zangu zipotelee bure kwako, na usipoteze wakati. Wakati moyo wako una ushirika na Mimi daima, wakati moyo wako huishi daima mbele Yangu, basi hakuna mtu, hakuna tukio hakuna kitu, hakuna mume, hakuna mwana au binti anayeweza kuvuruga ushirika wako na Mimi ndani ya moyo wako. Wakati moyo wako unawekewa mipaka daima na Roho Mtakatifu na wakati unafanya ushirika na Mimi kila wakati, mapenzi Yangu kwa hakika yatafichuliwa kwako. Wakati unapojongea karibu na Mimi daima kwa njia hii, bila kujali mazingira yako au upo kwa wakati upi maalum, basi huwezi kuvurugika bila kujali ni nani au ni nini unachokabili, na wewe utakuwa na njia ya kwenda mbele.

kutoka katika “Sura ya 8” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

25. Unapomtegemea Mungu, inawezekana kwamba Yeye hakupi hisia au maoni yoyote yaliyo dhahiri, sembuse mwelekeo wowote ulio wazi, lakini Yeye hukuruhusu upate ufahamu kiasi. Au labda wakati huu hujaelewa chochote, lakini ni sahihi umtegemee Mungu. Watu kutenda kwa njia hii hakufanywi ili kufuata sheria, lakini badala yake ni hitaji la mioyo yao na ndivyo mwanadamu anavyopaswa kutenda. Si kwamba unaweza kupata nuru na mwongozo kila wakati unapomtegemea Mungu na kumwita Mungu; hali hii ya kiroho katika maisha ya mwanadamu ni ya kawaida na ya asili, na kumtegemea Mungu ni mwingiliano wa kawaida na Mungu katika mioyo ya watu.

Wakati mwingine, kumtegemea Mungu hakumaanishi kumwomba Mungu afanye kitu kwa kutumia maneno maalum, au kumwomba uongozi au ulinzi maalum. Badala yake, ni kwamba watu wanapokabiliwa na suala fulani, wanaweza kumwomba Mungu kwa kweli. Hivyo, Mungu anafanya nini pale watu wanapomwita? Wakati ambapo moyo wa mtu unatikisika na ana wazo hili: “Ee Mungu, siwezi kufanya hili mimi mwenyewe, sijui jinsi ya kufanya hivyo, na ninahisi mwenye udhaifu na uhasi,” je, Mungu anajua kuhusu hilo? Mawazo haya yanapotokea ndani ya watu, je, mioyo yao ni ya kweli? Wanapomsihi Mungu kwa kweli kwa njia hii, Mungu anakubali kuwasaidia? Licha ya ukweli kwamba huenda hawakusema neno, wanaonyesha uaminifu, na hivyo Mungu anakubali kuwasaidia. Mtu anapokabiliwa na tatizo ambalo ni gumu hasa, wakati ambapo hana mtu anayeweza kumwomba msaada na anahisi asiyejiweza, yeye huweka matumaini yake ya pekee kwa Mungu. Maombi yake yako vipi? Hali yake ya akili iko vipi? Je, ni mwaminifu? Je, kuna ughushi wakati huo? Ni wakati tu ambapo unamwamini Mungu kana kwamba ni matawi ya mwisho unayokamata ili kuokoa maisha yako, ukitumai kwamba Atakusaidia, kwamba moyo wako ni wa kweli. Ingawa huenda hujasema mengi, moyo wako tayari umesisimuka. Yaani, unatoa moyo wako wa kweli kwa Mungu, na Mungu anasikiliza. Mungu atakapoona matatizo yako, Atakupa nuru, Atakuongoza, na kukusaidia.

kutoka katika “Waumini Wanahitaji Kwanza Kubaini Mielekeo Mibaya ya Dunia” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

26. Bila kujali jinsi kimo cha mtu kilivyo kikubwa au kidogo, au ni aina gani ya mazingira aliyomo mtu, na bila kujali mtu anaelewa ukweli kiasi gani, ni kiasi kipi cha wajibu ambacho mtu ametimiza, au ni kiasi gani cha uzoefu ambacho mtu amepata wakati wa kutekeleza wajibu huo, jambo moja ambalo hawezi kulikosa ni kwamba katika kila kitu anachofanya, lazima amtegemee Mungu na kumtumainia Mungu. Hii ndiyo aina kubwa zaidi ya hekima. Kwa nini nasema kuwa hii ndiyo hekima kubwa zaidi? Hata kama mtu amekuja kuelewa ukweli kiasi, je, atafanikiwa iwapo hamtumainii Mungu? Watu wengine, baada ya kumwamini Mungu kwa muda mrefu kidogo, wamekuja kuelewa ukweli kiasi na wamepitia majaribu machache. Huenda wana uzoefu mdogo wa kiutendaji, lakini hawajui jinsi ya kumtegemea Mungu, na hawaelewi jinsi ya kumtumainia Mungu. Je, watu kama hawa wana hekima? Wao ndio watu wapumbavu zaidi, na ni aina ya watu ambao hujiona kuwa mahiri; hawamwogopi Mungu na kuepuka uovu. Watu wengine husema: “Ninaelewa ukweli mwingi na nina uhalisi wa ukweli. Ni sawa kufanya tu vitu kwa njia yenye maadili. Mimi ni mwaminifu kwa Mungu na ninajua jinsi ya kumkaribia Mungu. Je, si inatosha kwamba mimi natumainia ukweli?” “Kutumainia ukweli” ni sawa, kulingana na mafundisho. Lakini kuna nyakati nyingi na hali nyingi ambapo watu hawajui ukweli ni nini au kanuni za ukweli ni nini. Wote walio na uzoefu wa vitendo wanajua jambo hili. Unapokumbana na masuala fulani, ikiwa hujui jinsi ambavyo ukweli unaohusika katika suala hili unapaswa kutendwa au jinsi unavyotakiwa kutumika, unapaswa kufanya nini nyakati kama hizi? Bila kujali una uzoefu wa vitendo kiasi gani, huwezi ukawa na ukweli katika hali zote. Bila kujali umemwamini Mungu kwa miaka mingapi, umepitia vitu vingapi, umepitia upogoaji, ushughulikiwaji, au kufundishwa nidhamu kiasi gani, je, wewe ndiye chanzo cha ukweli? Watu wengine husema: “Nimekariri maneno na vifungu vinavyojulikana sana katika kitabu cha Neno Laonekana katika Mwili. Sihitaji kumtegemea Mungu au kumtumainia Mungu. Wakati utakapofika, nitakuwa sawa tu nikitegemea maneno haya ya Mungu.” Maneno ambayo umeyakariri hayabadiliki, lakini mazingira unayokumbana nayo na hali zako hubadilika. Kuwa na ufahamu kuhusu maneno halisi na kuongea juu ya mafundisho mengi ya kiroho si sawa na ufahamu wa ukweli, sembuse kuwa sawa na wewe kuelewa mapenzi ya Mungu katika kila hali. Kwa hivyo kuna somo la muhimu sana la kujifunza hapa. Ni kwamba watu wanahitaji kumtegemea Mungu katika mambo yote. Kwa kumtegemea Mungu katika mambo yote, watu wanaweza kufanikisha imani katika Mungu, na ni wale tu wanaomtegemea Mungu ndio wana njia ya kufuata. Vinginevyo, unaweza kufanya kitu kwa usahihi na kwa kufuata kanuni za ukweli, lakini usipomtegemea Mungu, basi kile unachofanya ni tendo la mwanadamu tu, na si sharti kuwa linamridhishi Mungu. Kwa sababu watu wana ufahamu wa juu juu sana kuhusu ukweli, huenda wakafuata sheria na kushikilia kwa ukaidi maandiko na mafundisho kwa kutumia ukweli huo huo wanapokabiliwa na hali tofauti. Inawezekana kwamba mambo mengi yanaweza kukamilishwa kwa kawaida kwa kufuata kanuni za ukweli, lakini mwongozo wa Mungu haupo, wala kazi ya Roho Mtakatifu. Kuna tatizo kubwa hapa, ambalo ni kwamba watu hufanya mambo mengi kwa kutegemea uzoefu wao na sheria ambazo wameelewa, na mawazo fulani ya binadamu. Wanaweza kufikia matokeo bora kabisa kwa shida, ambayo hutokana na kuelewa mapenzi ya Mungu kwa wao kumtegemea Mungu na kumwomba Mungu, na kisha kwa kutumainia kazi na mwongozo wa Mungu. Kwa hivyo Nasema: Hekima kuu zaidi ni kumtegemea Mungu na kumtumainia Mungu katika mambo yote.

kutoka katika “Waumini Wanahitaji Kwanza Kubaini Mielekeo Mibaya ya Dunia” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Tanbihi :

a. Makala ya asili hayana neno “kile kinachofanywa.”

Iliyotangulia: (II) Maneno Juu ya Kumwomba na Kumwabudu Mungu

Inayofuata: (IV) Maneno Juu ya Tofauti Kati ya Kazi ya Mungu na ya Mwanadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

Shida Kubwa Sana: Usaliti (2)

Asili ya mwanadamu ni tofauti kabisa na kiini Changu, kwa sababu asili potovu ya mwanadamu hutoka kwa Shetani kabisa; asili ya mwanadamu...

Sura ya 15

Wanadamu wote ni viumbe wasio na ufahamu kujihusu, na hawezi kujijua mwenyewe, yeye hata hivyo anajua kila mwanadamu mwingine kama kiganja...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki