C. Jinsi ya Kujijua Mwenyewe na Kufikia Toba ya Kweli

358. Baada ya miaka elfu kadhaa ya upotovu, mwanadamu amekuwa asiyehisi na mpumbavu, pepo anayempinga Mungu, kwa kiasi kwamba uasi wa mwanadamu kwa Mungu umeandikwa katika vitabu vya historia, na hata mwanadamu mwenyewe hana uwezo wa kutoa ripoti kamili ya tabia zake za uasi wake—kwa kuwa mwanadamu amepotoshwa sana na Shetani, na amehadaiwa na Shetani kiasi kwamba hajui ni wapi pa kugeukia. Hata wa leo, mwanadamu bado anamsaliti Mungu: Wakati mwanadamu anamwona Mungu, anamsaliti, na wakati yeye hawezi kumwona Mungu, bado anamsaliti. Kuna hata wale ambao, baada ya kushuhudia laana ya Mungu na ghadhabu ya Mungu, bado wanamsaliti. Na hivyo Nasema kwamba hisia ya mwanadamu imepoteza kazi yake ya awali, na kwamba dhamiri ya mwanadamu, pia, imepoteza kazi yake ya awali. Mwanadamu Ninayemtazamia ni mnyama katika mavazi ya binadamu, yeye ni nyoka mwenye sumu, haijalishi jinsi anavyojaribu kuonekana mwenye kuhurumiwa machoni Pangu, Sitawahi kamwe kuwa na huruma kwake, kwa kuwa mwanadamu hana ufahamu wa kutofautisha kati ya nyeusi na nyeupe, tofauti kati ya ukweli na yasiyo ya kweli. Hisia ya mwanadamu ni usiohisi chochote, ilhali bado anataka apate baraka; ubinadamu wake si wa kuheshimika lakini bado anataka kumiliki ukuu wa mfalme. Ataweza kuwa mfalme wa nani, na hisia kama hiyo? Jinsi gani yeye na ubinadamu kama huo ataweza kukaa kwenye kiti cha enzi? Mwanadamu kwa kweli hana aibu! Yeye ni mdhalili wa kujivuna tu! Kwa wale kati yenu mnaotaka kupokea baraka, Ninawashauri kwanza mtafute kioo na kuangalia picha zenu mbaya—je, una kile kinachohitajika kuwa mfalme? Je, una uso wa mwanadamu ambaye anaweza kupata baraka? Hakujawa mabadiliko hata madogo katika tabia yako na wewe hujaweka ukweli wowote katika vitendo, ilhali bado unatamani kuona siku ifuatayo ikiwa ya ajabu. Unajihadaa mwenyewe! Kwa sababu ya kuzaliwa katika nchi ya uchafu vile, mwanadamu ameangamizwa kabisa na jamii, amekuwa akishawishiwa na maadili ya kikabaila, na amefundisha katika “taasisi za elimu ya juu.” Fikra zilizo nyuma kimaendeleo, maadili potovu, mtazamo mbaya juu ya maisha, falsafa za kudharauliwa za kuishi, uwepo usio na thamani, na hali potovu za maisha na desturi—mambo yote haya yameuingilia moyo wa mwanadamu, na kudhoofisha na kushambuliwa dhamiri yake pakubwa. Matokeo yake, mwanadamu kamwe yuko mbali kutoka kwa Mungu, na kila mara anampinga. Tabia ya mwanadamu inakuwa matata zaidi kila siku, na hakuna hata mmoja ambaye kwa hiari yake atatoa chochote kwa ajili ya Mungu, hakuna hata mmoja ambaye kwa hiari atamtii Mungu, wala, zaidi ya hayo, mwanadamu mmoja ambaye kwa hiari yake atatafuta uso wa Mungu. Badala yake, chini ya umiliki wa shetani, mwanadamu hafanyi kitu ila kukimbiza anasa, kujitoa mwenyewe kwa upotovu wa mwili katika nchi ya matope. Hata wanaposikia ukweli, wale wanaoishi gizani hawafikiri kuuweka katika vitendo, na wala kuelekea kumtafuta Mungu hata kama wameuona mwonekano Wake. Jinsi gani wanadamu wapotovu kiasi hiki wawe na nafasi yoyote ya wokovu? Jinsi gani wanadamu waovu kiasi hiki kuishi katika mwanga?

Kubadilisha tabia ya mwanadamu huanza na maarifa ya kiini chake na kupitia mabadiliko katika mawazo yake, asili, na mtazamo wa akili—kwa njia ya mabadiliko ya msingi. Ni kwa njia hii tu ndio mabadiliko ya kweli yatapatikana katika tabia ya mwanadamu. Tabia ya upotovu ya mwanadamu inatokana na hali yake ya kupewa sumu na kukanyagwa na Shetani, kutokana na madhara mabaya sana ambayo Shetani ameweka katika mawazo yake, maadili, ufahamu, na hisia. Ni hasa kwa sababu mambo ya msingi ya mwanadamu yamepotoshwa na Shetani, na ni tofauti kabisa na jinsi Mungu aliwaumba kwa asili, kwamba mwanadamu humpinga Mungu na haelewi ukweli. Hivyo, mabadiliko katika tabia za mwanadamu lazima yaanze na mabadiliko katika mawazo yake, ufahamu na hisia ambayo yatabadilisha maarifa yake ya Mungu na maarifa yake ya ukweli. Wale waliozaliwa katika nchi potovu zaidi ndio wasiojua zaidi kumhusu kile Mungu Alicho, au kunamaanisha nini kumwamini Mungu. Jinsi watu walivyo wapotovu zaidi, ndivyo wanavyokosa kujua kuwepo kwa Mungu na ndivyo hisia zao na utambuzi huwa duni. Chanzo cha upinzani wa mwanadamu na uasi dhidi ya Mungu ni kupotoshwa kwake na Shetani. Kwa sababu amepotoshwa na Shetani, dhamiri ya mwanadamu imekuwa bila hisia, yeye ni mwovu, mawazo yake yamepotoka, na ana mtazamo duni. Kabla ya kupotoshwa na Shetani, mwanadamu kawaida alimfuata Mungu na alitii maneno Yake baada ya kuyasikia. Alikuwa kawaida mwenye akili timamu na dhamiri, na wa ubinadamu wa kawaida. Baada ya kupotoshwa na Shetani, hali yake ya awali, dhamiri, na ubinadamu vilidhoofika sana na viliharibiwa na shetani. Hivyo, yeye amepoteza utii wake na upendo kwa Mungu. Akili ya mwanadamu imekuwa potovu, tabia yake imekuwa sawa na ile ya mnyama, na uasi wake kwa Mungu kabisa umekuwa wa mara kwa mara na wa kuhuzunisha zaidi. Hata hivyo mwanadamu bado hajui wala kutambua hili, na kwa upofu anapinga na kuasi. Ufunuo wa tabia ya mwanadamu ni udhihirisho wa hisia zake, utambuzi na dhamiri, na kwa sababu hisia yake na utambuzi si timamu, na dhamiri yake imezidi kuwa ndogo zaidi, hivyo tabia yake ni ya uasi dhidi ya Mungu. Kama hisia ya mwanadamu na utambuzi hauwezi kubadilika, basi mabadiliko katika tabia yake hayawezekani, sawa na kuwa baada ya moyo wa Mungu. Kama hisia ya mwanadamu sio timamu, basi hawezi kumhudumia Mungu na hafai kutumiwa na Mungu. “Hisia za Kawaida” inaashiria kutii na kuwa mwaminifu kwa Mungu, kuwa mwenye imani kamili kwa Mungu, na kwa kuwa na dhamiri kwa Mungu. Inamaanisha kuwa na moyo mmoja na akili kwa Mungu, na si kwa kumpinga Mungu kwa makusudi. Wale ambao ni wa akili potovu hawako hivi. Tangu mwanadamu aharibiwe na Shetani, ametunga dhana kuhusu Mungu, na yeye hajakuwa na uaminifu au kumtamani Mungu, pia hana dhamiri kwa Mungu. Mwanadamu kwa makusudi anapinga na huweka hukumu juu ya Mungu, na, zaidi ya hapo, anatupa shutuma Kwake nyuma Yake. Mwanadamu anajua vizuri kuwa Yeye ni Mungu, lakini bado humhukumu nyuma ya mgongo wake, hana nia ya kumtii, na hufanya madai ya kipofu na maombi kwa Mungu. Watu wa aina hii—watu walio na akili potovu—hawana uwezo wa kujua tabia zao za kudharauliwa au ya kujuta uasi wao. Kama watu wana uwezo wa kujijua wenyewe, basi wao wamerudisha kiasi kidogo cha akili zao; Zaidi ya vile watu wanavyomuasi Mungu lakini hawajui wenyewe, ndivyo walivyo zaidi wenye akili isiyo timamu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu

359. Mpaka watu wawe wamepitia kazi ya Mungu na kupata ukweli, ni asili ya Shetani inayotwaa madaraka na kuwatawala kwa ndani. Ni nini, hasa, kilicho ndani ya asili hiyo? Kwa mfano, kwa nini wewe ni mchoyo? Kwa nini wewe hulinda nafasi yako mwenyewe? Kwa nini una hisia kali sana namna hiyo? Kwa nini unafurahia hivyo vitu visivyo vya haki? Kwa nini unapenda maovu hayo? Msingi wa kupenda kwako vitu hivi ni upi? Mambo haya hutoka wapi? Kwa nini unafurahia sana kuyakubali? Kufikia sasa, nyote mmekuja kuelewa kwamba sababu kuu ya mambo haya yote ni kwamba sumu ya Shetani iko ndani yenu. Kuhusu sumu ya Shetani ni nini, inaweza kuelezwa kwa ukamilifu kwa maneno. Kwa mfano, ukiwauliza baadhi ya watenda maovu kwa nini walitenda jinsi walivyotenda, watajibu, “Kwa sababu kila mwamba ngoma huvutia upande wake.” Msemo huu mmoja unaonyesha asili ya shida. Mantiki ya Shetani imekuwa maisha ya watu. Wanaweza kutenda mambo kwa ajili ya madhumuni fulani au mengine, lakini wanajifanyia tu. Kila mtu hudhani kwamba kwa kuwa ni kila mwamba ngoma huvutia upande wake, watu wanafaa kuishi kwa sababu yake mwenyewe tu, na kufanya kila awezalo kupata wadhifa mzuri kwa ajili ya chakula na mavayi mazuri. “Kila mwamba ngoma huvutia upande wake”—haya ndiyo maisha na falsafa ya mwanadamu, na pia inawakilisha asili ya binadamu. Maneno haya ya Shetani ni sumu ya Shetani hasa, na watu wanapopoiweka moyoni, inakuwa asili yao. Asili ya Shetani hufunuliwa kupitia maneno haya; yanamwakilisha yeye kabisa. Sumu hii inakuwa maisha ya watu pamoja na msingi wa kuwepo kwao; na wanadamu waliopotoshwa wametawaliwa kwa uthabiti na sumu hii kwa maelfu ya miaka. Kila kitu ambacho Shetani hufanya ni kwa ajili yake. Anatamani kumpita Mungu, kujiondoa Kwake na kushika mamlaka mwenyewe, na kumiliki vitu vyote ambavyo Mungu ameumba; kwa hivyo, asili ya mwanadamu ni asili ya Shetani. Kwa kweli, wito wa watu wengi unaweza kuwakilisha na kuakisi asili yao. Haijalishi jinsi watu hujaribu kuificha, katika kila kitu wafanyacho na kila kitu wasemacho, hawawezi kuificha asili yao. Kuna wengine ambao huwa hawasemi ukweli kamwe na wanajua sana kujifanya, lakini punde tu wengine wanapoingiliana nao kwa muda, asili yao ya udanganyifu na wao kutokuwa waaminifu kabisa kutagunduliwa. Muda utafichua yote. Baada ya kuwajua kwa muda, asili yao itagunduliwa. Mwishowe, wengine hufikia hitimisho hili: Mtu huyo kamwe hasemi neno lolote la ukweli na ni mdanganyifu. Kauli hii ni ukweli wa asili ya mtu wa aina hiyo; ni ushahidi na kielezo cha asili yake; falsafa yake ya maisha ni kutomwambia yeyote ukweli, na pia kutomwamini mtu yeyote. Asili ya kishetani ya mwanadamu ina kiwango kikubwa cha falsafa. Wakati mwingine wewe mwenyewe huna hata habari ya hilo na hulielewi, ilhali kila muda wa maisha yako unategemea hilo. Isitoshe, unafikiri kuwa falsafa hii ni sahihi sana, yenye mantiki na isiyo na kosa. Falsafa ya Shetani imekuwa ukweli wa watu, na wanaishi kulingana na falsafa ya Shetani kabisa, bila kumpinga hata kidogo. Kwa hivyo, kila mara wanaonyesha asili yao ya kishetani. mwanadamu daima hufichua asili ya Shetani, na katika vipengele vyote, wanaishi daima kulingana na falsafa ya ya kishetani. Asili ya Shetani ni maisha ya mwanadamu.

Kimetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kuitembea Njia ya Petro” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

360. Inapofikia kujua asili ya wanadamu, kitu cha muhimu zaidi ni kuijua kutoka kwa mtazamo wa maoni yao ya dunia, maoni ya maisha, na maadili. Wale wote walio wa ibilisi wote huishi kwa ajili yao wenyewe. Mitazamo yao ya maisha na kanunizinatoka kwa misemo ya Shetani, kama vile, “Kila mtu kivyake, na ibilisi achukue ya nyuma kabisa.” Maneno yaliyonenwa na hao ibilisi wafalme, wakuu, na wanafalsafa wa dunia yamekuwa maisha yao. Hasa, maneno mengi ya Konfyushasi, ambaye anatangazwa na watu wa Kichina kuwa “mtu mwenye hekima” yamekuwa maisha ya watuyamekuwa maisha ya watu. Pia kuna methali maarufu ya Ubudha na Utao, na misemo maarufu zaidi ya inayosemwa mara kwa mara ya watu mbalimbali mashuhuri; haya yote ni muhtasari wa falsafa ya Shetani na asili ya Shetani. Pia ni vielezo vizuri sana na maelezo ya asili ya Shetani. Sumu hizi ambazo zimetiliwa mioyoni mwa wanadamu zote hutoka kwa Shetani; hakuna hata chembe yao inayotoka kwa Mungu. Uongo na upuuzi kama huu pia ni upinzani wa moja kwa moja kwa neno la Mungu hasa. Ni wazi kabisa kuwa uhalisi wa vitu vyote vyema hutoka kwa Mungu, na vitu vyote hivyo hasi ambavyo huwatia sumu wanadamu hutoka kwa Shetani. Kwa hivyo, unaweza kumaizi asili ya mtu na yeye yu wa nani kutoka kwa maoni yake ya maisha na maadili. Shetani huwapotosha watu kwa kupitia masomo na ushawishi wa serikali za kitaifa na walio mashuhuri na wakuu. Upuuzi wao umekuwa uzima wa mwanadamu na asili. “Kila mtu kivyake na ibilisi achukue ya nyuma kabisa” ni msemo wa kishetani unaojulikana sana ambao umeingizwa ndani ya kila mtu na umekuwa maisha ya watu. Kuna maneno mengine ya falsafa ya kuishi ambayo pia ni kama haya. Shetani hutumia utamaduni mzuri wa kila taifa kuwaelimisha watu, akisababisha wanadamu kuanguka ndani na kumezwa na lindi kuu lisilo na mipaka la uharibifu, na mwishowe watu wanaangamizwa na Mungu kwa sababu wanamtumikia Shetani na kumpinga Mungu. Hebu fikiri kumwuliza mtu ambaye amekuwa mtendaji katika jamii kwa miongo swali lifuatalo: ‘Kuona kwamba umeishi duniani kwa muda mrefu sana na umetimiza mengi sana, je, ni misemo ipi mikuu maarufu unayofuata katika maisha yako?’ ‘Ule ulio muhimu zaidi ni “Wenye madaraka hawawapigi wanaowapa zawadi, na wale wasiojipendekeza hamna wanachofanikisha.’” Je, maneno haya hayaiwakilishi asili ya mtu huyo? Kutumia kila mbinu ili kupata cheo imekuwa asili yake na, kuwa na madaraka rasmi ndiko kunakompa uzima. Bado kuna sumu nyingi za kishetani maishani mwa watu, katika mienendo yao na shughuli zao na wengine; hawana ukweli wowote hata kidogo. Kwa mfano, falsafa zao za kuishi, njia zao za kufanya vitu, na kanuni zao zote zimejazwa sumu za joka kuu jekundu, na zote zinatoka kwa Shetani. Hivyo, vitu vyote vinavyopita katika mifupa na damu ya watu ni vitu vyote vya Shetani. Wale maafisa wote, wale wanaoshikilia mamlaka, na wale waliofaulu wana njia zao na siri za kufaulu. Je, si siri kama hizo ni uwakilishi mzuri zaidi wa asili yao? Wameyafanya mambo makubwa sana duniani, na hakuna anayeweza kung’amua njama ambazo ziko katika mambo haya. Hili linaonyesha jinsi asili yao ilivyo yenye kudhuru kwa siri na yenye uovu. Wanadamu wamepotoshwa kwa kina zaidi na Shetani. Sumu ya Shetani inabubujika kwa damu ya kila mtu, na inaweza kuonekana kwamba asili ya mwanadamu imepotoka, ni yenye uovu, na ya kupinga maendeleo, ikijawa na kuzamishwa katika falsafa za Shetani—kwa jumla ni asili inayomsaliti Mungu. Hii ndiyo maana watu humkataa Mungu na humpinga Mungu. Asili ya mwanadamu inaweza kujulikana na kila mtu ikichanguliwa hivi.

Kimetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kujua Asili ya Mwanadamu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

361. Mnaelewa vipi asili ya mwanadamu? Kuifahamu asili yako kunamaanisha kugawanya vina vya nafsi yako kwa kweli; kunahusu kile kilicho katika maisha yako. Ni mantiki ya Shetani na mitazamo ya Shetani ambayo umekuwa ukiishi kulingana nayo; yaani, ni maisha ya Shetani ambayo umekuwa ukiishi kulingana nayo. Ni kwa kufukua tu sehemu za kina kabisa za nafsi yako ndio unaweza kuifahamu asili yako. Vitu hivi vinaweza kufukuliwa namna gani? Hayawezi kufukuliwa au kugawanywa kupitia tu tukio moja au matukio mawili; wakati mwingi, baadaa ya kukamilisha kufanya jambo, bado hutakuwa umepata kuelewa. Inaweza kuchukua miaka mitatu au mitano kabla Kuweza kupata hata chembe kidogo cha ugunduzi na ufahamu. Katika hali nyingi, lazima ujitafakari na ujijue, na ni wakati tu unapofanya mazoezi ya kuchimba kwa kina ndipo utaona matokeo. Kadiri ufahamu wako wa ukweli unavyozidi kuwa wa kina, pole pole utapata kujua asili na kiini chako mwenyewe kupitia kujitafakari na kujitambua. Ili kujua asili yako, lazima utimize vitu vichache. Kwanza, lazima uwe na uelewa dhahiri wa kile upendacho. Hili halihusu vitu unavyopenda kula au kuvaa; bali, linamaanisha aina ya vitu unavyofurahia, vitu unavyohusudu, vitu unavyoabudu, vitu unavyotafuta, na vitu unavyozingatia moyoni mwako. Aina ya watu unaofurahia kuwasiliana nao, aina ya vitu unavyopenda kufanya, na aina ya watu unaopenda mno ndani ya moyo wako. Kwa mfano, watu wengi huwapenda watu mashuhuri, watu ambao ni wa madaha katika usemi wao na tabia zao, au kama wale ambao huzungumza kwa lugha ya ushawishi yenye sifa mno au wale ambao hujifanya. Lililotajwa hapa mbeleni linahusu watu ambao wanapenda kushirikiana nao. Kuhusu vitu ambavyo watu hufurahia, hivi vinajumlisha kuwa radhi kufanya vitu fulani ambavyo ni rahisi kufanya, kufurahia kufanya vitu ambavyo watu wengine hufikiri ni vizuri na ambavyo vitasababisha watu kuimba sifa na kupeana taadhima. Katika asili za watu, kuna sifa zenye usawa kuhusu vitu ambavyo wao hupenda. Yaani, wanapenda watu, matukio na vitu ambavyo watu wengine wanahusudu kwa sababu ya mwonekano wa nje, wanapenda watu, matukio na vitu vinavyoonekana vizuri na vya anasa, na wanapenda watu, matukio na vitu ambavyo huwafanya watu wengine kuwaabudu kwa sababu ya sura zao za nje. Hivi vitu ambavyo watu hupenda ni vizuri, vya kung'aa, vya kupendeza, na vya fahari. Watu wote huabudu vitu hivi. Inaweza kuonekana kwamba watu hawana ukweli wowote, wala hawana mfano wa wanadamu wa kweli. Hakuna kiwango hata kidogo cha umuhimu katika kuabudu vitu hivi, ilhali watu bado huvipenda. … kila unachopenda, kile unachozingatia, kile unachoabudu, kile unachohusudu, na kile unachofikiria ndani ya moyo wako kila siku vyote ni viwakilishi vya asili yako. Inatosha kuthibitisha kwamba asili yako inapenda udhalimu, na katika hali mbaya, asili yako ni mbovu na isiyotibika. Unapaswa kuichambua asili yako kwa njia hii; yaani, chunguza kile unachopenda na kile unachoacha katika maisha yako. Unaweza kuwa mzuri kwa mtu fulani kwa muda, lakini hili halithibitishi kwamba unampenda. Kile unachopenda sana kweli ndicho hasa kilicho katika asili yako; hata kama mifupa yako ingekuwa imevunjwa, bado ungekifurahia na hungeweza kukiacha. Hili si rahisi kubadilisha.

Kimetoholewa kutoka katika “Unachopaswa Kujua Kuhusu Kuigeuza Tabia Yako” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

362. La muhimu katika kufikia badiliko katika tabia ni kujua asili ya mtu mwenyewe, na hili ni lazima lifanyike kulingana na ufunuo kutoka kwa Mungu. Ni katika neno la Mungu tu ambapo mtu anaweza kujua asili yake mbaya, afahamu katika asili yake mwenyewe sumu mbalimbali za Shetani, atambue kuwa yeye ni mjinga na mpumbavu, na atambue dalili dhaifu na hasi katika asili yake. Baada ya haya kujulikana kikamilifu, na unaweza kwa hakika kujichukia na kunyima mwili, daima kutekeleza neno la Mungu, na kuwa na mapenzi ya kujiwasilisha kikamilifu kwa Roho Mtakatifu na kwa neno la Mungu, basi utakuwa umeianza njia ya Petro. Bila neema ya Mungu, na bila nuru na mwongozo kutoka kwa Roho Mtakatifu, ingekuwa vigumu kuitembea njia hii, kwa sababu watu hawamiliki ukweli na hawawezi kujisaliti wenyewe. Kuitembea njia ya Petro ya ukamilisho inaegemea kuwa na azimio, kuwa na imani, na kumtegemea Mungu. Mbali na haya, mtu lazima ajiweke chini ya kazi ya Roho Mtakatifu; katika mambo yote, mtu hawezi kutenda bila maneno ya Mungu. Hivi ndivyo vipengele muhimu, Kupata kujitambua mwenyewe kupitia uzoefu ni vigumu sana bila kazi ya Roho mtakatifu, ni vigumu sana kuingia ndani. Kuitembea njia ya Petro mtu lazima azingatie juu ya kujijua mwenyewe na kubadili tabia yake.

Kimetoholewa kutoka katika “Kujijua Mwenyewe Hasa Ni Kujua Asili ya Binadamu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

363. Kwa upande mmoja, wakati wa majaribio ya Mungu mwanadamu huja kujua kasoro zake, na huona kwamba yeye ni mdogo, wa kudharauliwa, na duni, kwamba hana chochote, na si kitu; kwa upande mwingine, wakati wa majaribio Yake Mungu humuumbia mwanadamu mazingira tofauti yanayomfanya mwanadamu aweze zaidi kupitia kupendeza kwa Mungu. Ingawa maumivu ni makubwa, na wakati mwingine yasiyoshindika—na hata hufikia kiwango cha huzuni ya kuseta—baada ya kuyapitia, mwanadamu huona vile kazi ya Mungu ndani yake ni ya kupendeza, na ni juu ya msingi huu tu ndiyo ndani ya mwanadamu huzaliwa upendo wa kweli kwa Mungu. Leo mwanadamu huona kwamba na neema, upendo na rehema ya Mungu pekee, hana uwezo wa kujijua mwenyewe kweli, sembuse kuweza kujua kiini cha mwanadamu. Ni kupitia tu usafishaji na hukumu ya Mungu, ni wakati tu wa usafishaji kama huo ndiyo mwanadamu anaweza kujua kasoro zake, na kujua kwamba hana chochote.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu

364. Umuhimu wa kujitafakari na kujijua ni huu: Kadiri unavyozidi kuhisi kuwa katika sehemu fulani umefanya vizuri au umefanya jambo linalofaa, na kadiri unavyofikiri kuwa unaweza kuyaridhisha mapenzi ya Mungu au kuweza kujivunia katika sehemu fulani, basi ndivyo inavyofaa zaidi kwako kujijua katika sehemu hizo na inavyofaa zaidi kwako kuzichunguza zaidi ili kuona ni uchafu gani uko ndani yako, pamoja na mambo gani ndani yako hayawezi kuyaridhisha mapenzi ya Mungu. Hebu tumchukue Paulo kama mfano. Paulo alikuwa mwenye maarifa mno, na alivumilia mengi katika kazi yake ya kuhubiri. Alipendwa hasa sana na Wengu. Kama matokeo, baada ya kumaliza wingi wa kazi, alidhani kungekuwa na taji lililowekwa kando kwa ajili yake. Hili lilimfanya atembee zaidi na zaidi kwenye njia isiyo sahihi, hadi mwishowe akaadhibiwa na Mungu. Ikiwa, wakati huo, angetafakari juu yake mwenyewe na kujichambua, basi asingefikiria hivyo. Kwa maneno mengine, Paulo hakuwa amelenga kutafuta ukweli katika maneno ya Bwana Yesu; alikuwa tu ameamini mawazo na fikira zake mwenyewe. Alikuwa amedhani kwamba almradi afanye mambo machache mazuri na kuonyesha tabia nzuri, angesifiwa na kutuzwa kupewa tuzo na Mungu. Mwishowe, mawazo na fikira zake zilipofusha roho yake na kufunika hali yake ya kweli. Hata hivyo, watu hawakujua hili, na bila Mungu kuliweka wazi, waliendelea kumweka Paulo kama kiwango cha kufikia, mfano wa kuishi kulingana naye, na wakamwona kama ambaye walitamani kuwa kama na kama kitu cha kufuatilia kwao na kama mtu wa kuigwa nao. Hadithi hii kumhusu Paulo inatumika kama onyo kwa kila mtu amwaminiye Mungu, ambalo ni kwamba wakati wowote tunapohisi kuwa tumefanya vizuri zaidi, au kuamini kwamba tuna vipawa zaidi katika mambo fulani, au kufikiria kwamba hatuhitaji kubadilika au kushughulikiwa katika jambo fulani, tunapaswa kujitahidi kutafakari na kujijua wenyewe zaidi katika suala hilo; jambo hili ni muhimu. Hii ni kwa sababu bila shaka hujafichua, kutilia maanani au kuchanganua vipengele kujihusu ambavyo unaamini kuwa mzuri, ili kuona kama kweli vina chochote kinachompinga Mungu au la.

Kimetoholewa kutoka katika “Ni kwa Kutambua Maoni Yako Yaliyopotoka Tu Ndipo Unapoweza Kujijua Mwenyewe” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

365. Kwa hivyo kama ujuzi wa watu juu yao wenyewe ni wa juujuu sana, watapata kuwa haiwezekani kutatua matatizo, na tabia zao za maisha hazitabadilika kabisa. Ni muhimu kujijua mwenyewe kwa kiwango cha kina kabisa, ambayo inamaanisha kuijua asili yako mwenyewe: ni vipengele vipi ambavyo vimejumuishwa katika asili hiyo, jinsi vitu hivi vilivyoanza, na kule vilipotoka. Aidha, unaweza kuchukia mambo haya kweli? Je, umeona nafsi yako mwenyewe mbaya na asili yako mbovu? Ikiwa kwa hakika unaweza kuuona ukweli kujihusu mwenyewe, basi utaanza kujichukia mwenyewe kabisa. Wakati unapojichukia mwenyewe kabisa na kisha unatenda neno la Mungu, utakuwa na uwezo wa kunyima mwili na kuwa na nguvu ya kutekeleza ukweli bila shida. Kwa nini watu wengi hufuata tamaa zao za kimwili? Kwa sababu wanajiona kuwa wazuri kabisa, wakihisi kuwa vitendo vyao ni viadilifu na vya haki, kwamba hawana makosa, na hata kwamba wako sahihi kabisa, kwa hiyo wao wana uwezo wa kutenda kwa dhana kuwa haki iko upande wao. Wakati mtu anapotambua asili yake ya kweli ilivyo—jinsi ilivyo mbaya, jinsi inavyostahili kudharauliwa, na jinsi ilivyo ya kusikitisha—basi yeye si mwenye majivuno sana, hajigambi ovyo ovyo sana, hajifurahii kama hapo awali. Mtu kama huyo huhisi, “Lazima niwe mwenye ari na mpole, na nitende baadhi ya maneno ya Mungu. Kama sivyo, basi siwezi kufikia kiwango cha kuwa mwanadamu, na nitaona aibu kuishi mbele ya Mungu.” Kwa hakika mtu hujiona kuwa hafifu, kama kweli asiye na maana. Wakati huu, inakuwa rahisi kwake kutekeleza ukweli, naye ataonekana kwa kiwango fulani kuwa kama mwanadamu anavyopaswa kuwa. Ni pale tu ambapo watu kwa hakika hujichukia kabisa ndipo wanaweza kunyima mwili. Kama hawajichukii, hawataweza kunyima mwili. Mtu kujichukia kweli kunajumuisha mambo machache: Kwanza, kujua asili yake mwenyewe; na pili, kujiona kama yeye ni mwenye shida na wa kudharaulika, kujiona kuwa mdogo kupindukia na asiye na maana, na kuona nafsi yake kuwa yenye kudharaulika na chafu. Mtu anapoona kikamilifu kile alicho kwa hakika, na matokeo haya yakafikiwa, basi yeye kweli hupata ufahamu juu yake mwenyewe, na inaweza kusemwa kwamba amekuja kujijua mwenyewe kikamilifu. Ni hapo tu ndipo anaweza kwa hakika kujichukia mwenyewe, kufikia hata kujilaani mwenyewe, na ahisi kwa kweli kwamba amepotoshwa sana na Shetani kiasi kwamba hafanani tena na mwanadamu. Kisha, siku moja, wakati tishio la kifo linapoonekana, mtu kama huyu atafikiri, “Hii ni adhabu ya haki ya Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye haki; Kwa hakika mimi lazima nife!” Wakati huu, yeye hatalalamika, wala kumlaumu Mungu, akihisi tu kwamba yeye ni wa kudharaulika, mchafu sana na mpotovu, kwamba anapaswa kuangamizwa na Mungu na roho kama yake haifai kuishi duniani. Wakati huu, mtu huyu hatampinga Mungu, sembuse kumsaliti Mungu. Iwapo mtu hajijui mwenyewe, na bado hujiona kuwa mzuri sana, basi wakati kifo kinapokuja kubisha, mtu huyu atafikiria, “Nimetenda vyema sana katika imani yangu. Jinsi nimetafuta kwa nguvu! Nimejitolea mengi sana, nimeumia sana, ilhali hatimaye, Mungu sasa ananiuliza nife. Sijui haki ya Mungu iko wapi. Kwa nini Ananitaka nife? Ikiwa hata mtu kama mimi anafaa kufa, basi ni nani atakayeokolewa? Je! Si jamii ya wanadamu itafikia mwisho?” Kwanza kabisa, mtu huyu ana dhana juu ya Mungu. Pili, mtu huyu analalamika, na hatii hata kidogo. Hii ni kama tu Paulo: Wakati alipokaribia kufa, hakujijua mwenyewe, Na kufikia wakati adhabu ya Mungu ilipokaribia, hakukuwa na muda wa kutubu.

Kimetoholewa kutoka katika “Kujijua Mwenyewe Hasa Ni Kujua Asili ya Binadamu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: B. Juu ya Kutekeleza Ukweli, Kuelewa Ukweli na Kuingia katika Uhalisi

Inayofuata: D. Juu ya Jinsi ya Kupitia Hukumu na Kuadhibiwa, na Majaribu na Usafishwaji

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp