Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu

Mwanadamu anaelewa sehemu ndogo ya kazi ya leo na kazi ya baadaye, lakini hafahamu hatima ambapo mwanadamu ataingia. Kama kiumbe, mwanadamu anapaswa kutekeleza wajibu wa kiumbe: Mwanadamu anapaswa kumfuata Mungu kwa lolote afanyalo; mnapaswa muendelee mbele kwa njia yoyote ambayo Nitawaambia. Wewe huna mbinu ya kusimamia vitu mwenyewe, na huna ustadi juu yako mwenyewe; yote ni lazima yaachwe kwa rehema za Mungu, na kila kitu kinashikiliwa katika mikono Yake. Kama kazi ya Mungu ilimkimu mwanadamu kwa kumpa hatima, hatima ya ajabu, kabla ya wakati, na kama Mungu alitumia hii kumshawishi mwanadamu na kusababisha mwanadamu kumfuata Yeye—kama Yeye alifanya mpango na mwanadamu—basi huu haungekuwa ni ushindi, wala haingekuwa kufanya kazi katika maisha ya binadamu. Kama Mungu angetumia hatima ya mambo kumtawala au kumdhibiti mwanadamu na kupata moyo wake, basi kwa hii Hangekuwa anamkamilisha mwanadamu, wala Hangeweza kumpata mwanadamu, lakini badala yake angekuwa akitumia hatima kumdhibiti. Mwanadamu anajali tu kuhusu hatima ya siku zijazo, hatima, na kama kuna ama hamna kitu kizuri cha kutumainia. Iwapo mwanadamu angepewa matumaini mazuri wakati wa kazi ya ushindi, na kama, kabla ya kushindwa kwa mwanadamu, yeye angepewa hatima ifaayo ya kufuata, basi kushindwa kwa mwanadamu kusingekosa kuwa na athari tu, bali athari za kushindwa zingeshawishika pia. Hivi ni kusema kwamba, kazi ya ushindi inafanikisha mazao yake kwa kuchukua hatima na matarajio ya mwanadamu na kuhukumu na kuadibu uasi wa tabia ya mwanadamu. Haifanikishwi kwa kufanya mpango na mwanadamu, yaani, kwa kumpa mwanadamu baraka na neema, lakini ni kwa kufichua uaminifu wa mwanadamu kwa kumnyang’anya “uhuru” wake na kukomesha matarajio yake. Hiki ni kiini cha kazi ya ushindi. Kama mtu angepewa matumaini mazuri hapo mwanzoni sana, na kazi ya kuadibu na hukumu zingefanywa baadaye, basi mwanadamu angekubali kuadibu huku na hukumu kwa msingi kwamba alikuwa na matarajio, na mwishowe, utiifu na ibada ya Muumba isiyo na masharti ya viumbe vyote vyake haingetimizika; kungekuwepo tu na utiifu wenye upofu na wa ujinga, au pengine mwanadamu angetoa madai yasiyo na msingi kwa Mungu, na ingekuwa ni vigumu kushinda moyo wa mwanadamu. Kwa hivyo, kazi kama hii ya ushindi haingekuwa na uwezo wa kumpata mwanadamu, wala, zaidi ya hayo, ya kuwa na ushuhuda kwa Mungu. Viumbe kama hawa hawangeweza kutekeleza jukumu lao, na wangeweza tu kufikia makubaliano na Mungu; hii haitakuwa ushindi, lakini huruma na baraka. Tatizo kubwa mno kwa mwanadamu ni kuwa yeye hufikiria tu kuhusu hatima yake na matarajio, na kuyaabudu. Mwanadamu humfuata Mungu kwa ajili ya hatima yake na matarajio; yeye hamwabudu Mungu kwa sababu ya upendo wake kwake. Na kwa hivyo, katika ushindi kwa mwanadamu, ubinafsi wa mwanadamu, uroho na vitu ambavyo sana sana huzuia ibada yake kwa Mungu ni sharti vishughulikiwe na hapo viondolewe. Kwa kufanya hivyo, matokeo ya ushindi kwa mwanadamu yatatimizwa. Hivyo, katika ushindi wa kwanza wa mwanadamu ni muhimu kuondoa matarajio makubwa na udhaifu mkubwa kabisa wa mwanadamu, na, kupitia hili, kufichua upendo wa mwanadamu kwa Mungu, na kubadilisha maarifa yake kuhusu maisha ya binadamu, mtazamo wake kwa Mungu, na maana ya kuwepo kwake. Kwa njia hii, upendo wa mwanadamu kwa Mungu unatakaswa, ambapo ni kusema, moyo wa binadamu unashindwa. Lakini katika mtazamo wake wa viumbe vyote, Mungu hashindi kwa sababu ya kushinda; badala yake, Yeye anashinda ili kumpata mtu, kwa sababu ya utukufu wake mwenyewe, na ili kuokoa ufanano wa kwanza wa awali wa mwanadamu. Kama angeshinda kwa ajili ya kushinda, basi umuhimu wa kazi ya ushindi ungepotea. Hiyo ni kusema kuwa ikiwa, baada ya kumshinda mwanadamu, Mungu alikata tamaa kwa ajili ya mwanadamu, na hakuzingatia maisha au kifo chake, basi hii haitakuwa usimamizi wa mwanadamu, wala kumshinda mwanadamu haitakuwa ni kwa ajili ya wokovu wake. Ni upato wa mwanadamu tu kufuatia ushindi wake na ujio wake wa mwisho katika hatima ya ajabu ndiyo yaliyomo katika kiini cha kazi yote ya wokovu, na ni hii tu ndio inayoweza kufikia lengo la wokovu wa mwanadamu. Kwa maneno mengine, ni ufikaji wa mwanadamu katika hatima nzuri na kuingia kwake katika mapumziko tu ndiyo matarajio ambayo yanatakiwa yamilikiwe na viumbe vyote, na kazi ambayo lazima ifanywe na Muumba. Kama mwanadamu ndiye ambaye angefanya kazi hii, basi kazi hii ingekuwa kidogo sana. Ingemchukua mwanadamu hadi kiwango fulani, lakini haingekuwa na uwezo wa kumleta mwanadamu katika hatima ya milele. Mwanadamu hana uwezo wa kuamua hatima ya mwanadamu, wala, zaidi ya hayo, hana uwezo wa kuhakikisha matarajio na hatima ya baadaye ya binadamu. Kazi inayofanywa na Mungu, hata hivyo, ni tofauti. Tangu Yeye amuumbe mwanadamu, Yeye anamwongoza; kwa sababu Yeye humwokoa mwanadamu, atamwokoa mwanadamu kwelikweli, na atampata kikamilifu; kwa kuwa Yeye humwongoza mwanadamu, atamleta kwenye hatima inayofaa; na kwa kuwa Yeye alimuumba mwanadamu na humsimamia mwanadamu, ni sharti Achukue jukumu la hatima ya mwanadamu na matarajio yake. Ni hii ndio kazi ambayo hufanywa na Muumba. Ingawa kazi ya ushindi inatimizwa kwa kutakasa matarajio ya mwanadamu, hatimaye ni lazima mwanadamu aletwe kwenye hatima ifaayo aliyotengenezewa na Mungu kwa ajili yake. Ni kwa sababu hasa kuwa Mungu hufanya kazi katika mwanadamu ndiyo maana mwanadamu ana hatima na hatima yake ni ya uhakika. Hapa, hatima ifaayo inayoangaziwa sio matumaini na matarajio yaliyotakaswa katika nyakati za zamani, hizi mbili ni tofauti. Kitu ambacho mwanadamu hutumainia na kufuata ni tamaa za harakati ya hamu ya kimwili iliyo badhirifu, badala ya hatima ya mwanadamu anayotazamiwa. Kile ambacho Mungu amemwandalia mwanadamu, wakati huo huo, ni baraka na ahadi alizoandaliwa mwanadamu mara baada ya kutakaswa, ambayo Mungu alimtayarishia mwanadamu baada ya kuumba ulimwengu, na ambayo haitiwi doa na uchaguzi, dhana, mawazo au mwili wa mwanadamu. Hatima hii haitayarishwi kwa ajili ya mtu fulani, lakini ni mahali pa kupumzikia pa wanadamu wote. Na kwa hivyo, hii hatima ni hatima inayofaa zaidi kwa wanadamu.

Muumba anakusudia kupanga viumbe vyote. Wewe ni lazima usitupe au kutokaidi chochote ambacho Yeye anakifanya, wala usiwe na uasi kwake. Wakati ambapo kazi ambayo Yeye hufanya hatimaye inatimiza nia Yake, katika hii atapata utukufu. Leo, ni kwa nini haisemwi kwamba nyinyi ni wa uzao wa Moabu, au watoto wa joka kuu jekundu? Je, ni kwa nini hakuna mazungumzo ya wateule, na mazungumzo pekee ni ya viumbe? Kiumbe—hili lilikuwa jina la asili la mwanadamu, na ni hili ndilo utambulisho wake wa asili. Majina yanatofautiana tu kwa sababu nyakati na vipindi ni tofauti; kwa kweli, mwanadamu ni kiumbe wa kawaida. Viumbe wote, ikiwa ni wapotovu zaidi ama ni watakatifu sana, ni lazima watekeleze wajibu wa kiumbe. Wakati Yeye anafanya kazi ya ushindi, Mungu hakudhibiti kwa kutumia matarajio yako, majaliwa au hatima. Kwa kweli hakuna haja ya kufanya kazi kwa namna hii. Lengo la kazi ya ushindi ni kumfanya mwanadamu atekeleze wajibu wa kiumbe, kumfanya aabudu Muumba, na ni baada ya hii tu ndivyo ataweza kuingia kwenye hatima ya kustaajabisha. Majaliwa ya mwanadamu yanadhibitiwa na mikono ya Mungu. Wewe huna uwezo wa kujidhibiti mwenyewe: Licha ya mwanadamu yeye mwenyewe daima kukimbilia na kujishughulisha, anabakia bila uwezo wa kujidhibiti. Kama ungejua matarajio yako mwenyewe, kama ungeweza kudhibiti majaliwa yako mwenyewe, ingekuwa wewe bado ni kiumbe? Kwa kifupi, bila kujali jinsi Mungu hufanya kazi, kazi yote yake ni kwa ajili ya mwanadamu. Chukua, kwa mfano, mbingu na nchi na vitu vyote ambavyo Mungu aliviumba ili kumhudumia mwanadamu: mwezi, jua, na nyota ambazo Yeye alimuumbia mwanadamu, wanyama na mimea, majira ya machipuko, majira ya joto, vuli na baridi, na kadhalika—yote yametengenezwa kwa ajili ya kuwepo kwa mwanadamu. Na kwa hivyo, bila kujali ni jinsi gani anavyoadibu na kuhukumu mwanadamu, yote ni kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu. Japokuwa yeye humnyang’anya mwanadamu matumaini yake ya kimwili, ni kwa ajili ya kumtakasa mwanadamu, na utakaso wa mwanadamu ni kwa ajili ya kuishi kwake. Hatima ya mwanadamu iko mikononi mwa Muumba, hivyo ni jinsi gani mwanadamu anaweza kujidhibiti mwenyewe?

Punde tu kazi ya ushindi imekwisha kamilika, mwanadamu ataletwa katika dunia nzuri. Haya maisha, bila shaka, bado yatakuwa duniani, lakini yatakuwa tofauti kabisa na jinsi maisha ya mwanadamu yalivyo leo. Ni maisha ambayo mwanadamu atakuwa nayo baada ya wanadamu kwa ujumla kushindwa, itakuwa mwanzo mpya kwa mwanadamu hapa duniani, na kwa wanadamu kuwa na maisha kama hii ni ushahidi kwamba wanadamu wameingia katika milki jipya na nzuri. Itakuwa mwanzo wa maisha ya mwanadamu na Mungu duniani. Nguzo ya maisha mema kama haya ni lazima iwe hivyo, hivi kwamba baada ya mwanadamu kutakaswa na kushindwa, anajiwasilisha mbele za Muumba. Na kwa hivyo, kazi ya ushindi ni awamu ya mwisho ya kazi ya Mungu kabla ya wanadamu kuingia katika hatima ya ajabu. Maisha kama haya ni maisha ya baadaye ya mwanadamu duniani, ni maisha yanayopendeza zaidi duniani, aina ya maisha ambayo mwanadamu ametamania, aina ambayo mwanadamu hajawahi kamwe kutimiza katika historia ya ulimwengu. Ni matukio ya mwisho ya miaka 6,000 ya kazi ya usimamizi, na ndicho wanadamu wanatamani sana, na pia ni ahadi ya Mungu kwa mwanadamu. Lakini ahadi hii haiwezi timika mara moja: Mwanadamu ataingia katika hatima ya mbeleni punde tu kazi ya siku za mwisho zitakapokuwa zimemalizika na yeye amekwisha kushindwa kikamilifu, yaani, punde tu Shetani atakapokuwa ameshindwa kabisa. Mwanadamu atakuwa hana asili ya kutenda dhambi baada ya kusafishwa, kwa sababu Mungu atakuwa amemshinda Shetani, ambayo ina maana kuwa hakutakuwepo na kuvamiwa na vikosi vya uhasama, na hakuna vikosi vya uhasama ambavyo vinaweza kushambulia mwili wa mwanadamu. Na kwa hivyo mwanadamu atakuwa huru, na mtakatifu—yeye atakuwa ameingia ahera. Ni kama tu vikosi vya uhasama wa giza vitakuwa vimefungwa ndipo mwanadamu atakuwa huru kokote aendako, na bila uasi au upinzani. Shetani ni sharti afungwe katika utumwa, and kila kitu kitakuwa sawa kwa mwanadamu; hali ya sasa ipo kwa sababu Shetani bado huchochea shida kila mahali hapa duniani, na kwa sababu kazi nzima ya usimamizi wa Mungu bado haijafika mwisho wake. Punde tu Shetani anaposhindwa, mwanadamu atakuwa amekombolewa kikamilifu; wakati mwanadamu anampata Mungu na anatoka katika kumilikiwa na Shetani, atatazama jua ya haki. Maisha atakayolipwa mwanadamu wa kawaida yatarejeshwa; yote yale ambayo ni lazima yamilikiwe na mwanadamu wa kawaida—kama uwezo wa kupambanua mema na mabaya, na kufahamu jinsi ya kula na kujivisha mwenyewe, na uwezo wa kuishi kama kawaida—yote haya yatarejeshwa. Hata kama Hawa hakuwa amejaribiwa na nyoka, mwanadamu ni lazima angekuwa na maisha kama haya ambayo ni ya kawaida baada ya kuumbwa hapo mwanzo. Ni lazima angekula, angevishwa, na kuendelea na maisha ya mwanadamu wa kawaida hapa duniani. Ila baada ya mwanadamu kupotoshwa, maisha haya yakawa ndoto, na hata leo mwanadamu hathubutu kufikiri mambo kama haya. Kwa kweli, maisha haya ya kupendeza ambayo mwanadamu anatamani ni haja yake: Iwapo mwanadamu angekuwa hana hatima kama hii, basi maisha yake ya duniani yaliyopotoshwa kamwe hayangekoma, na kama hakungekuwepo na maisha yakupendeza kama haya, basi hakungekuwa na hitimisho la majaliwa ya Shetani au kwa enzi ambayo Shetani ana utawala duniani kote. Mwanadamu ni sharti awasili kwenye ufalme ambao huwezi kufikiwa na nguvu za giza, na wakati atawasili, hii itathibitisha ya kwamba Shetani amekwisha shindwa. Kwa njia hii, punde tu hakuna usumbufu wa Shetani, Mungu mwenyewe atamdhibiti mwanadamu, na Yeye ataamuru na kudhibiti maisha yote ya mwanadamu; hii tu ndiyo itahesabika kama kushindwa kwa Shetani. Maisha ya mwanadamu leo ni sanasana maisha ya uchafu, na bado ni maisha ya kuteseka na mateso. Hii haingeitwa kushindwa kwa Shetani; mwanadamu bado hajatoroka kutoka katika bahari ya mateso, bado hajatoroka kutoka katika ugumu wa maisha ya mwanadamu, ama ushawishi wa Shetani, na bado yeye ana maarifa ya Mungu lakini kidogo sana. Taabu zote za mwanadamu ziliumbwa na Shetani, ni Shetani ndiye alileta mateso katika maisha ya mwanadamu, na ni baada tu ya Shetani kufungwa ndipo mwanadamu ataweza kutoroka kikamilifu kutoka katika bahari ya mateso. Na bado utumwa wa Shetani unahitimika kupitia kushindwa na kupatwa kwa moyo wa mwanadamu, kwa kumfanya mwanadamu mabaki ya vita dhidi ya Shetani.

Leo, harakati ya mwanadamu ya kukuwa mshindi na kufanywa mkamilifu ni vitu ambavyo vinafuatwa kabla yeye hajakuwa na maisha ya mtu wa kawaida duniani, na ndiyo malengo ambayo mwanadamu hutafuta kabla ya utumwa wa Shetani. Kwa kiini, harakati ya mwanadamu ya kukuwa mshindi na kufanywa kamili, au kufanywa wa kutumika vilivyo, ni kutoroka kutoka katika ushawishi wa Shetani. Harakati ya mwanadamu ni kuwa mshindi, lakini matokeo ya mwisho yatakuwa ni kutoroka kutoka kwa ushawishi wa Shetani. Ni kwa kutoroka kutoka kwa ushawishi wa Shetani tu ndipo mwanadamu ataweza kuishi maisha ya mtu wa kawaida duniani, maisha ya kumwabudu Mungu. Leo, harakati ya mtu ya kukuwa mshindi na kufanywa kamilifu ndiyo mambo ambayo yanafuatwa kabla ya kuwa na maisha ya mtu wa kawaida duniani. Haya yanafuatwa kimsingi kwa ajili ya kutakaswa na kuweka ukweli katika vitendo, na ili kufanikisha ibada ya Muumba. Kama mwanadamu anamiliki maisha ya mtu wa kawaida duniani, maisha ambayo hayana taabu na matatizo, basi mwanadamu hawezi kushiriki katika harakati za kuwa mshindi. “Kuwa mshindi” na “kufanywa kamili” ni malengo ambayo Mungu humpa mwanadamu kufuatilia, na katika ufukuziaji wa malengo haya, Yeye husababisha mwanadamu kuweka ukweli katika vitendo na kuishi kwa kudhihirisha maisha yenye umuhimu. Lengo ni kumkamilisha mtu na kumpata yeye, na harakati ya kukuwa mshindi na kufanywa kamili ni njia tu. Kama, hapo mbeleni, mwanadamu ataingia kwenye hatima ya ajabu, hakutakuwepo na kurejelea kuwa mshindi na kukamilika, kutakuwepo tu na kila kiumbe kikitekeleza wajibu wake. Leo, mwanadamu anafanywa kufuata mambo haya tu ili kufafanua upeo wa mwanadamu, ili harakati ya mwanadamu ilengwe zaidi na iwe ya utendaji zaidi. La sivyo, mwanadamu angeishi katikati ya dhahania isiyo dhahiri, na kufuatilia kuingia katika uzima wa milele, na kama ingekuwa hivyo, je, si mwanadamu hata angelikuwa hafifu hata zaidi? Kufuata njia hii, bila malengo au kanuni—je, hii sio kujidanganya? Hatimaye, harakati hii ingekuwa kama kawaida bila mazao; na mwishowe, mwanadamu bado angemilikiwa na Shetani na hangeweza kujinasua mwenyewe kutokana nayo. Mbona ajikabili mwenyewe kwenye harakati kama hii isiyo na sababu? Wakati mwanadamu ataingia kwenye hatima ya milele, mwanadamu atamwabudu Muumba, na kwa sababu mwanadamu amepata wokovu na kuingia ahera, mwanadamu hawezi kimbiza malengo yoyote, wala, zaidi ya hayo, yeye hatakuwa na haja ya kuhangaika kuwa atazingirwa na Shetani. Kwa wakati huu, mwanadamu atajua nafasi yake, na atatekeleza wajibu wake, na hata kama hataadibiwa au kuhukumiwa, kila mtu atatekeleza jukumu lake. Kwa wakati huo, mwanadamu atakuwa kiumbe katika sura na hadhi pia. Hakutakuwepo tena na tofauti ya juu na chini; kila mtu atatekeleza tu kazi tofauti. Bado mwanadamu ataishi katika hatima ya wanadamu yenye utaratibu na ifaayo, mwanadamu atatekeleza wajibu wake kwa ajili ya kumwabudu Muumba, na wanadamu kama hawa ni wanadamu wa milele. Kwa wakati huo, mwanadamu atakuwa amepata maisha yaliyoangaziwa na Mungu, maisha chini ya utunzaji na ulinzi wa Mungu, na maisha pamoja na Mungu. Wanadamu wataishi maisha ya kawaida duniani, na wanadamu wote wataingia katika njia sahihi. Mpango wa usimamizi wa miaka 6,000 utakuwa umemshinda Shetani kabisa, ambayo ina maana kuwa Mungu atakuwa amerejesha sura ya awali ya mwanadamu kufuatia kuumbwa kwake, na kwa hivyo, nia ya awali ya Mungu itakuwa imetimizwa. Hapo mwanzo, kabla mwanadamu hajapotoshwa na Shetani, mwanadamu aliishi maisha ya kawaida duniani. Baadaye, alipopotoshwa na Shetani, mwanadamu alipoteza maisha haya ya kawaida, na kwa hivyo kazi ya Mungu ya usimamizi ikaanza, na vita dhidi ya Shetani ikaanza ili kurejesha maisha ya kawaida ya mwanadamu. Ni wakati tu ambapo usimamizi wa kazi ya Mungu wa miaka 6,000 utafikia kikomo ndipo maisha ya mwanadamu yatakapoanza rasmi hapa duniani, ni wakati huo tu ndipo mwanadamu atakapokuwa na maisha mazuri, na Mungu atarejesha lengo la kumuumba mwanadamu hapo mwanzoni, na pia kufanana kwake kwa asili na mwanadamu. Na kwa hivyo, punde tu atakuwa na maisha ya kawaida ya mwanadamu duniani, mwanadamu hatafuatilia kuwa mshindi ama kuwa kamili, kwa kuwa mwanadamu atakuwa mtakatifu. “Washindi” na “kukamilishwa” ambako watu huzungumzia ni malengo yaliyopewa mwanadamu ili kufuata wakati wa vita kati ya Mungu na Shetani, na yapo tu kwa sababu mwanadamu amepotoshwa. Ni kwa kukupa lengo na kukufanya wewe kufuata lengo hili, ndipo Shetani atashindwa. Kukuambia uwe mshindi au ufanywe kamili ama utumike kunahitaji ya kwamba uwe na ushuhuda ili umwaibishe Shetani. Mwishowe, mwanadamu ataishi maisha ya mwanadamu wa kawaida duniani, na mwanadamu atakuwa mtakatifu, na wakati hii itatendeka, je, watatafuta kuwa washindi? Je, wote si viumbe wa uumbaji? Kuzungumza kuhusu kuwa mshindi na kuwa yule aliyekamilika, maneno haya yanaelekezwa kwa Shetani, na uchafu wa mwanadamu. Je, hii “mshindi” si kuhusu ushindi dhidi ya Shetani na majeshi ya uhasama? Unaposema kuwa wewe umefanywa mkamilifu, nini hicho ndani yako ambacho kimekamilishwa? Je, si kuwa umevua mwenyewe tabia potovu ya kishetani, ili uweze kufaulu kupata upendo mkuu wa Mungu? Mambo kama haya yanasemekana kuhusu mambo machafu ndani ya mtu, na kuhusu Shetani; na hayasemwi kuhusu Mungu.

Leo, kama haufuatilii kuanza kuwa mshindi na kukamilishwa, basi mbeleni, wakati mwanadamu ataishi maisha ya kawaida duniani, hakutakuwa na nafasi ya harakati kama hizo. Wakati huo, hatima ya kila aina ya mtu itakuwa imefichuliwa. Wakati huo, itakuwa wazi wewe ni kitu cha aina gani, na kama unataka kuwa mshindi au unataka kukamilishwa haitawezekana. Ni hivyo tu kwa sababu ya uasi wake mwanadamu ataadhibiwa baada ya kufichuliwa. Wakati huo, harakati za mtu hazitakuwa za juu kuliko za watu wengine, kwa wengine kuwa washindi na wengine kukamilika, au kwa wengine kuwa wazaliwa wa kwanza wa Mungu na wengine kuwa wana wa Mungu; hawatafuatilia vitu hivi. Wote watakuwa viumbe vya Mungu, wote wataishi duniani, na wote wataishi duniani pamoja na Mungu. Sasa ni wakati wa vita kati ya Mungu na Shetani, ni wakati ambapo vita hivi havijahitimishwa bado, wakati mwanadamu bado hajapatwa kikamilifu, na ni kipindi cha mpito. Na kwa hivyo, mwanadamu anatakiwa afuatilie kuwa mshindi au mmoja wa watu wa Mungu. Leo kuna tofauti baina ya hadhi, lakini wakati utawadia ambapo hakutakuwepo na tofauti kama hizo: Hadhi ya wote hao ambao wamekuwa washindi itakuwa sawa, wote watakuwa wamehitimu kuwa wanadamu, na wataishi duniani kwa usawa, kwa maana kuwa wote watakuwa viumbe wenye sifa zinazostahili, na chochote watapewa kitakuwa sawa. Kwa kuwa nyakati za kazi ya Mungu ni tofauti, na madhumuni ya kazi yake ni tofauti pia, kama kazi hii inafanyika ndani yenu, nyinyi mnafaa kufanywa kamili na kuwa washindi; kama ingefanyika ng’ambo, basi wangekuwa na stahiki ya kuwa kundi la watu la kwanza kushindwa, na kundi la watu la kwanza la kufanywa kamilifu. Leo, kazi hii haifanywi kule ng’ambo, na kwa hivyo hawastahiki kufanywa wakamilifu ama kuwa washindi, na haiwezekani wao kukuwa kundi la kwanza. Kwa kuwa nia ya kazi ya Mungu ni tofauti, enzi ya kazi ya Mungu ni tofauti, na upeo wake ni tofauti, hivyo kuna kundi la kwanza, yaani, kuna washindi, na pia vile vile kutakuwa na kundi la pili ambalo ni la kufanywa kamilifu. Punde tu kunapokuwa na kundi la kwanza lililokamilishwa, kutakuwa na kiolezo na mfano, na hivyo mbeleni kutakuwa na kundi la pili na la tatu la wale wanakamilishwa, lakini ahera wote watakuwa sawa, na hakutakuwa na uainishaji wa hadhi. Wote watakuwa tu wamefanywa wakamilifu katika nyakati tofauti, na hakutakuwa na tofauti katika hadhi. Wakati utakapofika kila mtu amefanywa wakamilifu, na kazi ya ulimwengu mzima imehitimishwa, hakutakuwa na kulinganisha kwa hadhi, na wote watakuwa wa hadhi sawa. Leo, kazi hii inafanywa kati yenu ili muweze kuwa washindi. Kama ingefanyika nchini Uingereza, basi Uingereza ingekuwa kundi la kwanza, kwa njia sawa na vile mtakavyokuwa kundi la kwanza. Ni kwamba tu mmebarikiwa hasa na neema kwa njia ambayo kazi inatekelezwa ndani mwenu leo, na kama kama kazi hii haingefanywa ndani yenu, basi mngekuwa kundi la pili, au la tatu, au la nne, au la tano. Hii ni kwa sababu tu ya utofauti katika utaratibu wa kazi; kundi la kwanza na kundi la pili haliashirii kuwa moja ni la juu au la chini kuliko lingine, inaashiria tu utaratibu ambao upo wa watu hawa kufanywa wakamilifu. Leo maneno haya yanawasiliwa kwenu, lakini mbona hamkuwa mmefahamishwa mapema? Kwa sababu, bila mchakato, watu huwa wanakaa kuenda kuzidi kiasi. Kwa mfano, wakati huo Yesu alisema kwamba: “Kama Nilivyoondoka, ndivyo Nitakavyowasili.” Leo, wengi wamepumbazwa na maneno haya, na wanataka tu kuvaa mavazi meupe wakisubiri kuchukuliwa kwenda mbinguni. Kwa hivyo, kuna maneno mengi ambayo hayawezi kusemwa mapema mno; kama yangesemwa mapema mno, mwanadamu angeenda kuzidi kiasi. Kimo cha mwanadamu ni kidogo mno, na hana uwezo wa kuona kuanzia mwanzo hadi mwisho wa ukweli wa maneno haya.

Wakati mtu anafanikiwa kupata maisha ya ukweli ya mwanadamu duniani na vikosi vizima vya Shetani vimefungwa, mwanadamu ataishi kwa urahisi katika ardhi. Mambo hayatakuwa magumu kama yalivyo sasa: Mahusiano ya binadamu, mahusiano ya kijamii, mahusiano changamani ya kifamilia…., haya ni ya kusumbua, machungu mno! Maisha ya mwanadamu hapa ni duni! Punde tu mwanadamu anaposhindwa, moyo wake na akili yake vitabadilika: atakuwa na moyo unaomcha Mungu na moyo ambao unampenda Mungu. Punde tu wote walio ulimwenguni ambao wanatafuta upendo wa Mungu wanaposhindwa, ambayo ni kusema, punde tu Shetani anaposhindwa, na punde tu Shetani—nguvu zote za giza—zimekwisha fungwa, basi maisha ya mwanadamu duniani yatakuwa yasiyotaabishwa, na ataweza kuishi huru duniani. Kama maisha ya mwanadamu hayana mahusiano ya kimwili, na hayana changamani za mwili, basi itakuwa rahisi mno. Mahusiano ya kimwili ya mwanadamu ni changamani mno, na kwa mwanadamu kuwa na mambo kama hayo ni thibitisho kuwa yeye bado hajajikomboa kutoka kwa ushawishi wa Shetani. Kama ungekuwa na uhusiano sawa na kila mmoja wa ndugu na dada, kama ungekuwa na uhusiano sawa na kila mmoja wa wanafamilia wako, basi hungekuwa na wasiwasi, na hungekuwa na haja ya kuhofia kuhusu mtu yeyote. Hakuna kitakachoweza kuwa bora zaidi, na kwa njia hii mwanadamu atapunguziwa nusu ya mateso yake. Kuishi maisha ya kawaida ya binadamu duniani, mwanadamu atakuwa sawa na malaika; ingawa atakuwa bado na mwili, atakuwa sawa na malaika. Hii ni ahadi ya mwisho, ni ahadi ya mwisho ambayo mwanadamu amezawadiwa. Leo mwanadamu anapitia kuadibu na hukumu; Je, unafikiri matukio kama haya ya mwanadamu hayana maana? Je, kazi ya kuadibu na kuhukumu inaweza kufanywa bila sababu. Hapo awali ilisemekana kuwa kuadibu na kuhukumu mwanadamu ni kumweka katika shimo lisilo na mwisho, ambayo ina maana ya kuchukua majaliwa na matarajio. Hii ni kwa ajili ya jambo moja: utakasaji wa mwanadamu. Mwanadamu hawekwi kwenye shimo lisilo na mwisho kimakusudi, ambapo baadaye Mungu hukata tamaa juu yake. Badala yake, ni ili kushughulika na uasi ndani ya mwanadamu, ili hatimaye mambo ndani ya mwanadamu yaweze kutakasika, ili aweze kuwa na ufahamu wa kweli wa Mungu, na awe kama mtu mtakatifu. Iwapo hii itafanywa, basi yote yatakuwa yametimia. Kwa kweli, wakati mambo hayo ndani ya mwanadamu ambayo yanapaswa kushughulikiwa yameshughulikiwa, na mwanadamu anakuwa na ushuhuda wa mwangwi, Shetani pia atashindwa, na hata ingawa kunaweza kuwa na mambo machache ambayo awali ndani ya mwanadamu hayakuwa yametakasika kabisa, punde tu Shetani ameshindwa, Shetani hawezi tena kusababisha taabu, na wakati huo mwanadamu atakuwa ametakaswa kabisa. Mwanadamu hajawahi kupitia maisha kama haya, lakini wakati Shetani anashindwa, yote yatakuwa yametulizwa na mambo hayo pumbavu ndani ya mwanadamu yatatatuliwa yote; matatizo mengine yote yataisha punde tu tatizo kuu litakapokuwa limetatuliwa. Wakati wa kupata kwa mwili kwa Mungu duniani, wakati Yeye binafsi anafanya kazi miongoni mwa watu, kazi yote ambayo Yeye hufanya ni kwa ajili ya kumshinda Shetani, na Yeye atamshinda Shetani kupitia kumshinda mwanadamu na kuwafanya kamili. Wakati nyinyi mtakuwa na ushuhuda wa ajabu, hii, pia, itaonyesha kushindwa kwa Shetani. Kwanza mwanadamu anashindwa na hatimaye anafanywa kamili kabisa ili kumshinda Shetani. Kwa kiini, hata hivyo, pamoja na kushindwa kwa Shetani hii pia vilevile ni wokovu wa wanadamu wote kutoka kwa shimo la bahari hii ya mateso. Bila kujali kama kazi hii inatendeka katika ulimwengu mzima au katika nchi ya China, yote ni kwa ajili ya kumshinda Shetani na kuleta wokovu kwa wanadamu wote ili mwanadamu aweze kuingia pahali pa kupumzika. Mungu mwenye mwili, mwili huu wa kawaida, ni kwa usahihi kwa ajili ya kumshinda Shetani. Kazi ya Mungu mwenye mwili ni kuleta wokovu kwa wale wote walioko chini ya mbingu wanaompenda Mungu, ni kwa ajili ya kushinda wanadamu wote, na, zaidi ya hayo, kwa ajili ya kumshinda Shetani. Msingi wa kazi yote ya Mungu ya usimamizi haitengani na kushindwa kwa Shetani ili kuleta wokovu kwa watu wote. Kwa nini, katika mengi ya kazi hii, daima inasemekana kwenu kuwa na ushuhuda? Na ushuhuda huu unaelekezewa nani? Je, si unaelekezwa kwa Shetani? Ushuhuda huu unafanyiwa Mungu, na unafanywa ili kushuhudia kuwa kazi ya Mungu imetimiza matokeo yake. Kuwa na ushuhuda inahusiana na kazi ya kumshinda Shetani; kama hakungekuwa na vita dhidi ya Shetani, basi mwanadamu hangetakiwa kuwa na ushuhuda. Ni kwa sababu kwamba Shetani lazima ashindwe, kwa wakati huo huo kama kuokoa mwanadamu, Mungu anataka kwamba mwanadamu awe na ushuhuda wake mbele ya Shetani, ambao Yeye hutumia kufanya vita na Shetani. Kwa hivyo, mwanadamu ni mlengwa wa wokovu na chombo cha kumshinda Shetani, na kwa hivyo mwanadamu yumo katika msingi wa usimamizi mzima wa Mungu, na Shetani ni mlengwa wa uharibifu, adui. Unaweza kuhisi kuwa haujafanya kitu chochote, lakini kwa sababu ya mabadiliko katika tabia yako, umekuwa na ushuhuda, na ushuhuda huu unaelekezwa kwa Shetani na haufanywi kwa mwanadamu. Mwanadamu hajafaa ili afurahie ushuhuda kama huu. Je, jinsi gani yeye ataweza kuelewa kazi inayofanywa na Mungu? Mlengwa wa vita vya Mungu ni Shetani; mwanadamu, wakati huo huo, ni mlengwa wa wokovu. Mwanadamu ana tabia potovu ya kishetani, na hana uwezo wa kuelewa kazi hii. Hii ni kwa sababu ya kupotoshwa na Shetani and asili kwa mwanadamu, bali inaelekezwa na Shetani. Leo, kazi kuu ya Mungu ni kumshinda Shetani, yaani, kumshinda mwanadamu kabisa, ili kwamba mwanadamu awe na ushuhuda wa mwisho wa Mungu mbele ya Shetani. Kwa njia hii, mambo yote yatatimika. Kwa matukio mengi, kwa macho yako pekee inaonekana kwamba hakuna chochote ambacho kimefanyika, lakini kwa kweli, kazi tayari imekamilika. Mwanadamu anahitaji kwamba kazi yote iliyokamilika iwe ya kuonekana, bali bila kuifanya inayoonekana wazi kwako, Nimemaliza kazi yangu, kwa kuwa Shetani ametii, ambayo ina maana kuwa yeye ameshindwa kabisa, ya kuwa busara yote ya Mungu, nguvu na mamlaka yamemshinda Shetani. Huu ndiyo ushuhuda mahsusi ambao ni lazima mtu awe nao, na ingawa haijidhihirishi kwa uwazi katika mwanadamu, ingawa haionekani kwa macho pekee, Shetani tayari ameshindwa. Ujumla wa kazi hii lazima uelekezwe dhidi ya Shetani, na inafanyika kwa ajili ya vita dhidi ya Shetani. Kwa hivyo, kuna mambo mengi ambayo mwanadamu haoni kuwa ni mafanikio, lakini ambayo, machoni pa Mungu, yalikuwa na mafanikio kwa muda mrefu uliopita. Hii ni moja ya ukweli wa ndani wa kazi yote ya Mungu.

Punde tu Shetani anaposhindwa, yaani, punde tu mwanadamu anaposhindwa kabisa, mwanadamu ataelewa kwamba kazi hii yote ni kwa ajili ya wokovu, na kuwa mbinu ya wokovu huu ni kurejesha kutoka kwa mikono ya Shetani. Miaka 6,000 ya kazi ya Mungu ya usimamizi imegawanywa katika hatua tatu: Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Hatua hizi zote tatu za kazi ni kwa ajili ya wokovu wa wanadamu, yaani, ni kwa ajili ya wokovu wa wanadamu ambao wamepotoshwa na Shetani kwa kiasi kikubwa. Wakati uo huo, hata hivyo, pia ni ili kwamba Mungu afanye vita na Shetani. Hivyo, kama kazi ya wokovu ilivyogawanywa katika hatua tatu, kwa hivyo pia vita dhidi ya Shetani vimegawanywa katika hatua tatu, na vipengele hivi viwili vya kazi ya Mungu vinafanywa sawia. Vita dhidi ya Shetani kwa kweli ni kwa ajili ya wokovu wa wanadamu, na kwa kuwa kazi ya wokovu wa wanadamu silo jambo linaloweza kukamilishwa kwa mafanikio katika hatua moja, vita dhidi ya Shetani pia vimegawanywa katika hatua na vipindi, na vita vinapiganwa dhidi ya Shetani kulingana na mahitaji ya mwanadamu na kiwango cha kupotoshwa kwa mwanadamu na Shetani. Pengine, katika mawazo ya mwanadamu, anaamini kuwa katika vita hivi Mungu atajiandaa kupigana na Shetani, katika njia sawa na vile ambavyo majeshi mawili yangepigana. Hili tu ni jambo ambalo akili ya mwanadamu ina uwezo wa kukisia, na ni wazo lisilo dhahiri kupita kiasi na lisiloweza kutendeka, na bado ndilo mwanadamu analiamini. Na kwa sababu Nasema hapa kuwa njia ya wokovu wa mwanadamu ni kupitia vita na Shetani, mwanadamu anawaza ya kwamba hivi ndivyo vita vinavyoendeshwa. Katika kazi ya wokovu wa mwanadamu, hatua tatu zimefanywa, ambayo ni kusema kuwa vita na Shetani vimegawanyika katika hatua tatu kabla ya kushindwa kabisa kwa Shetani. Na bado ukweli wa ndani wa kazi yote ya vita dhidi ya Shetani ni kwamba matokeo yake yanatimizwa kupitia kwa hatua kadhaa za kazi: kumpa mwanadamu neema, na kuwa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, kuzisamehe dhambi za mwanadamu, kumshinda mwanadamu, na kumfanya mwanadamu akamilishwe. Kusema ukweli, vita na Shetani hajiandai kupigana na Shetani, bali ni wokovu wa mwanadamu, kuyashughulikia maisha ya mwanadamu, na kubadilishwa kwa tabia ya mwanadamu ili kwamba aweze kumshuhudia Mungu. Hivi ndivyo Shetani anashindwa. Shetani anashindwa kwa kubadilisha tabia potovu ya mwanadamu. Wakati Shetani ameshindwa, yaani, wakati mwanadamu ameokolewa kabisa, basi Shetani aliyeaibika atafungwa kabisa, na kwa njia hii, mwanadamu atakuwa ameokolewa kabisa. Na kwa hivyo, kiini cha wokovu wa mwanadamu ni vita dhidi ya Shetani, na vita na Shetani vitajitokeza kimsingi katika wokovu wa mwanadamu. Hatua ya siku za mwisho, ambapo mwanadamu atashindwa, ni hatua ya mwisho katika vita dhidi ya Shetani, na pia kazi ya wokovu kamili wa mwanadamu kutoka kwa miliki ya Shetani. Maana ya ndani ya ushindi wa mwanadamu ni kurudi kwa mfano halisi wa Shetani, mtu ambaye amepotoshwa na Shetani, kwa Muumba baada ya ushindi wake, kwa njia ambayo atamwacha Shetani na kurejea kabisa kwa Mungu. Kwa njia hii, mwanadamu atakuwa ameokolewa kabisa. Na kwa hivyo, kazi ya ushindi ni kazi ya mwisho katika vita dhidi ya Shetani, na hatua ya mwisho katika kazi ya Mungu ya usimamizi kwa ajili ya kushindwa kwa Shetani. Bila kazi hii, wokovu kamili wa mwanadamu hatimaye haungewezekana, kushindwa kikamilifu kwa Shetani kusingewezekana, na wanadamu kamwe hawangekuwa na uwezo wa kuingia kwenye hatima ya ajabu, ama kuwa huru kutoka kwa ushawishi wa Shetani. Kwa hivyo, kazi ya wokovu wa mwanadamu haiwezi kukamilishwa kabla vita dhidi ya Shetani havijahitimishwa, kwa kuwa msingi wa kazi ya Mungu ya usimamizi ni kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu. Mwanadamu wa kwanza kabisa alikuwa kwa mikono ya Mungu, lakini kwa sababu ya majaribu ya Shetani na upotovu wake, mwanadamu alifungwa na Shetani na kuanguka katika mikono ya yule mwovu. Kwa hivyo, Shetani akakuwa mlengwa wa kushindwa katika kazi ya Mungu ya usimamizi. Kwa sababu Shetani alichukua umiliki wa mwanadamu, na kwa sababu mwanadamu ndiye kiini cha usimamizi wote wa Mungu, kama mwanadamu ni wa kuokolewa, basi ni lazima anyakuliwe kutoka mikononi mwa Shetani, yaani mwanadamu ni lazima achukuliwe baada ya kutekwa nyara na Shetani. Hivyo, Shetani lazima ashindwe kupitia mabadiliko ya tabia ya mwanadamu ya zamani, mabadiliko ambayo hurejesha hisia zake za awali, na kwa njia hii, mwanadamu, ambaye ametekwa nyara, anaweza kunyakuliwa kutoka mikononi mwa Shetani. Kama mwanadamu anawekwa huru kutokana na ushawishi wa Shetani na utumwa wake, Shetani ataaibika, mwanadamu hatimaye atarejeshwa, na Shetani atakuwa ameshindwa. Na kwa sababu mwanadamu amewekwa huru kutoka kwa ushawishi wa giza wa Shetani, mwanadamu atakuwa mabaki ya vita hivi vyote, na Shetani atakuwa ndiye mlengwa ambaye ataadhibiwa punde tu vita hivi vitakapokamilika, na baada ya hapo kazi nzima ya wokovu wa mwanadamu itakuwa imekamilika.

Mungu hana nia mbaya kwa viumbe na anataka tu kumshinda Shetani. Kazi yote Yake—iwe ni kuadibu ama hukumu—inaelekezwa kwa Shetani; inafanyika kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu, yote ni kwa ajili ya kumshinda Shetani, na ina lengo moja: kufanya vita na Shetani mpaka mwisho kabisa! Na Mungu kamwe hatapumzika kabla ya kuwa mshindi dhidi ya Shetani! Atapumzika tu punde atakapomshinda Shetani. Kwa sababu kazi yote ambayo inafanywa na Mungu inaelekezwa kwa Shetani, na kwa sababu wale waliopotoshwa na Shetani wote wanadhibitiwa na milki ya Shetani na wote wanamilikiwa na Shetani, bila kupigana dhidi ya Shetani na kuwa huru dhidi yake, Shetani hangepumzisha kushika kwake kwa watu hawa, na hawangeweza kupatwa. Kama hawangepatwa, ingethibitisha kwamba Shetani hajashindwa, ya kwamba hajatiishwa. Na kwa hivyo, katika miaka 6,000 ya mpango wa usimamizi wa Mungu, katika hatua ya kwanza Yeye alifanya kazi ya sheria, wakati wa hatua ya pili Yeye alifanya kazi ya Enzi ya Neema, yaani, kazi ya kusulubiwa, na wakati wa hatua ya tatu Yeye alifanya kazi ya kumshinda mwanadamu. Kazi hizi zote zinaelekezwa kwa kiwango ambacho Shetani alikuwa amewapotosha wanadamu, yote ni kwa ajili ya kumshinda Shetani, na hakuna hatua hata moja ambayo si kwa ajili ya kumshinda Shetani. Kiini cha miaka 6,000 ya kazi ya Mungu ya usimamizi ni vita dhidi ya joka kubwa jekundu, na kazi ya kusimamia watu pia ni kazi ya kumshinda Shetani, na kazi ya kufanya vita na Shetani. Mungu amepigana vita kwa miaka 6,000, na hivyo kufanya kazi kwa miaka 6,000, ili hatimaye kuleta mwanadamu katika ulimwengu mpya. Wakati Shetani atashindwa, mwanadamu atakuwa amewekwa huru kabisa. Je, huu si mwelekeo wa kazi ya Mungu hivi leo? Huu kwa hakika ni mwelekeo wa kazi ya leo: ukombozi kamili na kuwekwa huru kwa mwanadamu, ili kwamba asiwe chini ya sheria yoyote, wala asiwekewe mipaka na vifungu au vikwazo vyovyote. Kazi hii yote inafanywa kwa mujibu wa kimo chenu na kwa mujibu wa mahitaji yenu, kwa maana kuwa nyinyi mnapewa chochote mnachoweza kutimiza. Siyo namna ya “kumpeleka bata kwenye kitulio cha ndege,” ya kuwalazimishia chochote; badala yake, kazi hii yote inafanywa kwa mujibu wa mahitaji yenu ya kweli. Kila hatua ya kazi ni kwa mujibu wa mahitaji halisi na matakwa ya mwanadamu, na ni kwa ajili ya kumshinda Shetani. Kwa kweli, hapo mwanzo hapakuwa na vikwazo kati ya Muumba na viumbe Vyake. Vyote vinasababishwa na Shetani. Mwanadamu amegeuka asiyeweza kuona au kugusa chochote kwa sababu ya usumbufu wa Shetani na upotovu wake. Mwanadamu ndiye mwathiriwa, yule ambaye amedanganywa. Punde tu Shetani anaposhindwa, viumbe watamtazama Muumba, na Muumba ataangalia viumbe na kuweza kuwaongoza binafsi. Haya ndiyo tu maisha ambayo mwanadamu anapaswa kuwa nayo duniani. Na kwa hivyo, kazi ya Mungu kimsingi ni kwa ajili ya kumshinda Shetani, na punde tu Shetani anaposhindwa, mambo yote yatakuwa yametatuliwa. Leo, umeona kwamba kweli ni jambo kuu kwa Mungu kuja miongoni mwa wanadamu. Yeye hajakuja kutumia kila siku akitafuta makosa kwenu, kusema hivi au vile, au kuwawezesha tu kuona vile Yeye anavyofanana, na vile ambavyo Yeye huongea na kuishi. Mungu hajapata mwili ili kuwaruhusu mmtazamie Yeye tu, au kufungua macho yenu, ama kuwaruhusu kusikia mafumbo ambayo amenena kuhusu na mihuri saba ambayo amefungua. Badala yake, amepata mwili ili amshinde Shetani. Yeye binafsi amekuja miongoni mwa watu katika mwili ili amwokoe mwanadamu, kufanya vita na Shetani, na huu ndio umuhimu wa Yeye kupata mwili. Kama haingekuwa ni kwa ajili ya kumshinda Shetani, basi asingefanya kazi hii binafsi. Mungu amekuja duniani kufanya kazi Yake miongoni mwa watu, kujifichua Mwenyewe kwa mwanadamu na kumruhusu mwanadamu kumtazamia; je, hili ni jambo dogo? Kwa kweli ni kuu! Si kama jinsi mwanadamu anavyofikiria kwamba Mungu amekuja ili mwanadamu aweze kumtazamia, ili mwanadamu aweze kuelewa kwamba Mungu ni wa ukweli na wala si yule asiye yakini ama mtupu, na ya kuwa Mungu ni wa fahari lakini pia mnyenyekevu. Je, inawezekana kuwa rahisi hivyo? Ni hasa kwa sababu Shetani amepotosha mwili wa mwanadamu, na mwanadamu ndiye Mungu anakusudia kuokoa, ya kuwa Mungu ni sharti achukue mwili ili afanye vita na Shetani na amchunge mwanadamu binafsi. Hii pekee ndiyo yenye manufaa kwa kazi Yake. Miili hiyo miwili ya Mungu ya nyama imekuwepo ili kumshinda Shetani, na pia imekuwepo ili imuokoe mwanadamu kwa njia bora zaidi. Hilo ni kwa sababu yule anayefanya vita na Shetani anaweza tu kuwa Mungu, awe ni Roho wa Mungu au ni mwili wenye nyama wa Mungu. Kwa kifupi, yule anayefanya vita na Shetani hawezi kuwa ni malaika, sembuse kuwa mwanadamu, ambaye amepotoshwa na Shetani. Malaika hawana uwezo wa kuifanya, na mwanadamu ni dhaifu hata zaidi. Kwa hivyo, ikiwa Mungu anataka kufanyia kazi maisha ya mwanadamu, kama Yeye anataka kuja duniani binafsi kumwokoa mwanadamu, basi ni lazima Yeye binafsi apate mwili—yaani, lazima Yeye binafsi achukue mwili, na kwa utambulisho Wake wa asili na kazi ambayo ni lazima afanye, aje miongoni mwa wanadamu na kumwokoa mwanadamu binafsi. La sivyo, kama ingekuwa ni Roho wa Mungu au mwanadamu ndiye aliyefanya kazi hii, basi vita hivi daima vingeshindwa kutimiza matokeo yake, na kamwe havingekwisha. Wakati tu Mungu anapata mwili ili Yeye binafsi aende kwa vita dhidi ya Shetani miongoni mwa watu ndipo mwanadamu anapata nafasi ya wokovu. Aidha, hapo tu ndipo Shetani anaaibishwa, na kuwachwa bila nafasi zozote za kutumia au mipango yoyote ya kutekeleza. Kazi inayofanywa na Mungu aliyepata mwili haiwezi kutimizwa na Roho wa Mungu, na hata zaidi haiwezi kufanywa na mtu yeyote mwenye mwili kwa niaba ya Mungu, kwa kuwa kazi ambayo Yeye hufanya ni kwa ajili ya maisha ya mwanadamu, na ili kubadilisha tabia potovu ya mwanadamu. Kama mwanadamu angeshiriki katika vita hivi, yeye angekimbia tu kwa vurugu ya huzuni, na hangekuwa na uwezo kabisa wa kubadilisha tabia potovu ya mwanadamu. Angekuwa hana uwezo wa kumwokoa mwanadamu kutoka msalabani, ama wa kushinda wanadamu wote waasi, lakini angeweza tu kufanya kazi kidogo ya zamani ambayo haiendi zaidi ya kanuni, au vinginevyo kazi ambayo haihusiani na kushindwa kwa Shetani. Kwa hivyo, mbona ujisumbue? Kuna umuhimu gani wa kazi ambayo haiwezi kuwapata wanadamu, sembuse kumshinda Shetani? Na kwa hivyo, vita dhidi ya Shetani vinaweza kufanywa tu na Mungu Mwenyewe, na itakuwa tu vigumu kwa mwanadamu kupigana vita hivyo. Wajibu wa mwanadamu ni kutii na kufuata, kwa kuwa mwanadamu hana uwezo wa kufanya kazi kama vile kuumba mbingu na dunia, wala, zaidi ya hayo, hawezi kutekeleza kazi ya kupigana na Shetani. Mwanadamu anaweza tu kumtosheleza Muumba chini ya uongozi wa Mungu Mwenyewe, ambapo Shetani hushindiwa; hili ndilo jambo pekee ambalo mwanadamu anaweza kulitenda. Na kwa hivyo, kila wakati vita vipya vinapoanza, kila wakati kazi ya enzi mpya inapoanza, kazi hii inafanywa na Mungu binafsi, ambapo kupitia kazi hiyo Yeye huongoza enzi nzima, na kufungua njia mpya kwa ajili ya wanadamu wote. Pambazuko la kila enzi mpya ni mwanzo mpya katika vita na Shetani, ambapo kupitia hiyo mwanadamu anaingia akiwa mpya zaidi, ulimwengu wa kupendeza zaidi na enzi mpya ambayo inaongozwa na Mungu Mwenyewe. Mwanadamu ni bwana wa vitu vyote, lakini wote ambao wamepatwa watakuwa matunda ya vita dhidi ya Shetani. Shetani ndiye mpotoshaji wa vitu vyote, na ndiye mshindwa katika mwisho wa vita vyote, na pia ndiye atakayeadhibiwa kufuatia vita hivi. Miongoni mwa Mungu, mwanadamu na Shetani, ni Shetani pekee ndiye atachukiwa na kukataliwa. Wale waliopatwa na Shetani lakini hawarejeshwi na Mungu, wakati huo huo, watakuwa wale ambao watapokea adhabu kwa niaba ya Shetani. Kati ya hawa watatu, Mungu pekee ndiye anapaswa kuabudiwa na vitu vyote. Wale waliopotoshwa na Shetani lakini wanarejeshwa na Mungu na wale wanaofuata njia ya Mungu, wakati huo huo, wanakuwa wale ambao watapokea ahadi ya Mungu na kuhukumu wale waovu kwa niaba ya Mungu. Bila shaka Mungu atakuwa mshindi na Shetani bila shaka atashindwa, lakini miongoni mwa wanadamu kuna wale watakaoshinda na wale watakaoshindwa. Wale ambao watashinda ni wa washindi, na wale ambao watashindwa ni wale wa washindwa; huu ni uainishaji wa kila mmoja kufuatana na aina, na ni hitimisho la mwisho la kazi yote ya Mungu. Pia ni lengo la kazi yote ya Mungu, na kamwe haitabadilika. Msingi wa kazi kuu wa mpango wa usimamizi wa Mungu unalenga wokovu wa mwanadamu, na Mungu anakuwa mwili kimsingi kwa ajili ya msingi huu, kwa ajili ya kazi hii, na ili kumshinda Shetani. Mara ya kwanza Mungu kuwa mwili ilikuwa ili kumshinda Shetani: Yeye binafsi akawa mwili, na akasulubiwa msalabani binafsi, ili kukamilisha kazi ya vita vya kwanza, ambayo ilikuwa kazi ya ukombozi wa mwanadamu. Aidha, awamu hii ya kazi ilifanywa na Mungu binafsi, ambaye amekuwa mwili ili kufanya kazi yake miongoni mwa wanadamu, ili kusema neno lake binafsi na kumwezesha mwanadamu kumwona. Bila shaka, ni hakika kwamba Yeye hufanya kazi nyingine njiani, lakini sababu kuu ya kufanya kazi yake binafsi ni ili kumshinda Shetani, kushinda wanadamu wote, na kuwapata hawa watu. Na kwa hivyo, kazi ya Mungu kuwa na mwili ni jambo kuu kweli. Kama kusudi lake lilikuwa tu kumwonyesha mwanadamu kuwa Mungu ni mnyenyekevu na aliyefichika, na kuwa Mungu ni wa ukweli, kama ingelikuwa ni kwa ajili ya kufanya kazi hii, basi hakungekuwa na haja ya kuwa mwili. Hata kama Mungu hakuwa mwili, yeye angefichua unyenyekevu na usiri wake, ukuu wake na utakatifu, kwa mwanadamu moja kwa moja, lakini mambo kama hayo hayana uhusiano wowote na usimamizi wa mwanadamu. Mambo kama hayo hayana uwezo wa kumwokoa mwanadamu au kumfanya awe kamili, na hata hayawezi kumshinda Shetani. Kama kushindwa kwa Shetani kungehusisha Roho tu akipigana vita dhidi ya roho, basi kazi kama hii ingekuwa na thamani ndogo ya ukweli; haingeweza kumpata mwanadamu na ingeharibu hatima na matarajio ya mwanadamu. Kwa hivyo, kazi ya Mungu leo ni moja ambayo ina umuhimu kupindukia. Sio hivyo ili kwamba mwanadamu aweze kumwona, au ili macho ya mwanadamu yaweze kufunguliwa, au ili ampe msukumo kiasi na kutiwa moyo; kazi kama hii haina umuhimu. Kama unaweza tu kuongea kwa hekima ya sampuli hii, basi inathibitisha kuwa wewe haujui umuhimu wa ukweli wa Mungu kupata mwili.

Kazi mzima ya mpangilio wa usimamizi wa Mungu inafanywa binafsi na Mungu mwenyewe. Awamu ya kwanza—uumbaji wa ulimwengu—ilifanywa binafsi na Mungu Mwenyewe, na kama haikuwa hivyo, basi hakuna yeyote ambaye angekuwa na uwezo wa kumuumba mwanadamu; awamu ya pili ilikuwa ukombozi wa wanadamu wote, na pia ilifanywa binafsi na Mungu Mwenyewe, awamu ya tatu inaenda bila kusemwa: Kuna haja kuu zaidi ya mwisho wa kazi ya Mungu kufanywa na Mungu Mwenyewe. Kazi ya ukombozi, ushindi, kumpata, na kumkamilisha wanadamu wote inafanywa binafsi na Mungu Mwenyewe. Kama hangefanya kazi hii Yeye binafsi, basi utambulisho wake hauwezi kuwakilishwa na mwanadamu, au kazi kufanywa na mwanadamu. Ili kumshinda Shetani, ili kumpata mwanadamu, na ili kumpa mwanadamu maisha ya kawaida duniani, Yeye binafsi humwongoza mwanadamu na hufanya kazi binafsi miongoni mwa wanadamu; kwa ajili ya mpangilio mzima wa usimamizi, na kwa kazi yake yote, ni lazima Yeye binafsi afanye kazi hii. Kama mwanadamu anaamini tu kuwa Mungu alikuja kuonekana naye na kumfurahisha, basi imani kama hizo hazina thamani, na hazina umuhimu. Maarifa ya mwanadamu ni ya kijuujuu mno! Ni kwa Mungu kutekeleza kazi Yeye mwenyewe ndivyo Mungu anaweza kufanya kazi yake vizuri na kikamilifu. Mwanadamu hana uwezo wa kuifanya kwa niaba ya Mungu. Kwa kuwa yeye hana utambulisho wa Mungu ama kiini Chake, hana uwezo wa kufanya kazi hii, na hata kama mwanadamu angekuwa na uwezo, haingekuwa na matokeo yoyote. Wakati wa kwanza Mungu kuwa mwili kwa ajili ya ukombozi, ilikuwa ni ili kuwakomboa wanadamu wote kutoka kwa dhambi, ili kufanya mwanadamu aweze kutakaswa na kusamehewa dhambi zake. Kazi ya ushindi pia inafanywa na Mungu binafsi miongoni mwa wanadamu. Kama, katika awamu hii, Mungu angekuwa wa kusema tu ya unabii, basi nabii au mtu ambaye ana kipawa angepatikana wa kuchukua nafasi Yake; kama unabii pekee ungesemwa, mwanadamu angechukua nafasi ya Mungu. Lakini ikiwa mwanadamu binafsi angefanya kazi ya Mungu Mwenyewe na angefanya kazi kwa maisha ya mwanadamu, haingewezekana kwake kufanya kazi hii. Ni lazima ifanywe na Mungu Mwenyewe binafsi: Ni lazima Mungu binafsi awe mwili ili kufanya kazi hii. Katika Enzi ya Neno, kama unabii pekee ungesemwa, basi Isaya au nabii Eliya wangepatikana wakifanya kazi hii, na hakungekuwepo na haja ya Mungu Mwenyewe kuifanya kazi hii binafsi. Kwa sababu kazi ambayo inafanywa katika awamu hii si tu ya kuongea kuhusu unabii, na kwa sababu ni ya umuhimu mkubwa zaidi kuwa kazi ya maneno inatumiwa kumshinda mwanadamu na kumshinda Shetani, kazi hii haiwezi fanywa na mwanadamu, na ni lazima ifanywe na Mungu Mwenyewe binafsi. Katika Enzi ya Sheria Yehova alifanya sehemu ya kazi ya Mungu, ambapo baadaye alinena baadhi ya maneno na kufanya baadhi ya kazi kupitia kwa manabii. Hiyo ni kwa sababu mwanadamu angemwakilisha Yehova katika kazi yake, na waonaji wangeweza kutabiri mambo na kutafsiri baadhi ya ndoto kwa niaba Yake. Kazi iliyofanyika hapo mwanzo haikuwa kazi ya kubadilisha tabia ya mwanadamu moja kwa moja, na ilikuwa bila uhusiano na dhambi ya mwanadamu, na mwanadamu alitakiwa tu atii sheria. Kwa hivyo, Yehova hakuwa wa kuwa na mwili na kujifichua Mwenyewe kwa mwanadamu; badala yake Yeye aliongea moja kwa moja na Musa na wengine, akawafanya wao kusema na kufanya kazi kwa niaba yake, na kusababisha wao wafanye kazi moja kwa moja miongoni mwa wanadamu. Awamu ya kwanza ya kazi ya Mungu ilikuwa uongozi wa mwanadamu. Ilikuwa ndio mwanzo wa vita dhidi ya Shetani, lakini vita hivi vilikuwa bado kuanza rasmi. Vita rasmi dhidi ya Shetani vilianza na kupata mwili kwa Mungu kwa mara ya kwanza, na vimeendelea hadi leo. Tukio la kwanza la vita hivi ni wakati Mungu aliyepata mwili alisulubishwa msalabani. Kusulubiwa kwa Mungu aliyekuwa mwili kulimshinda Shetani, na ilikuwa mafanikio ya awamu ya kwanza katika vita. Wakati Mungu mwenye mwili alianza kufanya kazi kwa mwanadamu moja kwa moja, huu ulikuwa mwanzo rasmi wa kazi ya kumrejesha mwanadamu, na kwa sababu hii ilikuwa kazi ya kubadilisha tabia ya zamani ya mwanadamu, ilikuwa kazi ya kufanya vita na Shetani. Awamu ya kazi iliyofanywa na Yehova hapo mwanzo ilikuwa tu ya uongozi wa maisha ya mwanadamu duniani. Ilikuwa ndio mwanzo wa kazi ya Mungu, na hata ingawa ilikuwa bado haijashirikisha vita vyovyote, au kazi kuu yeyote, ilikuwa imeweka msingi kwa ajili ya kazi ya vita vijavyo. Baadaye, awamu ya pili ya kazi wakati wa Enzi ya Neema ilihusisha kubadilisha tabia ya zamani ya mwanadamu, ambayo ina maana kuwa Mungu Mwenyewe alitengeneza kwa ustadi kazi ya mwanadamu. Hii ilikuwa ni lazima ifanywe na Mungu: ilihitaji kuwa Mungu binafsi awe mwili, na kama hangekuwa mwili, hakuna mwingine angeweza kuchukua nafasi yake katika awamu hii ya kazi, kwa kuwa iliwakilisha kazi ya kupambana dhidi ya Shetani moja kwa moja. Kama mtu angekuwa amefanya kazi hii kwa niaba ya Mungu, wakati mwanadamu alisimama mbele ya Shetani, Shetani hangeweza kutii na haingewezekana kumshinda yeye. Ilibidi iwe Mungu aliyepata mwili aliyekuja kumshinda, kwa kuwa kiini cha Mungu mwenye mwili bado ni Mungu, Yeye bado ni maisha ya mwanadamu, na bado Yeye ni Muumba; chochote kitakachotokea, utambulisho Wake na kiini havitabadilika. Na kwa hivyo, Yeye alivaa mwili na alifanya kazi ili kusababisha kujisalimisha kwa Shetani. Katika awamu ya kazi ya siku za mwisho, kama mwanadamu angefanya kazi hii na angefanywa kusema maneno moja kwa moja, basi hangeweza kusema maneno hayo, na kama unabii ungesemwa, basi haungekuwa na uwezo wa kumshinda mwanadamu. Kwa kuchukua mwili, Mungu huja kumshinda Shetani na kusababisha kujisalimisha kwake kamili. Wakati Yeye atamshinda Shetani kabisa, kumshinda mwanadamu kikamilifu, na kumpata mwanadamu kabisa, awamu hii ya kazi itakamilika na mafanikio kutimizwa. Katika usimamizi wa Mungu, mwanadamu hawezi kuwa naibu wa Mungu na kuwa Mungu wakati hayupo. Hasa, kazi ya kuongoza enzi na kuzindua kazi mpya ina haja kubwa zaidi kufanywa binafsi na Mungu Mwenyewe. Kumpa mwanadamu ufunuo na kwa kumpa yeye unabii kunaweza kufanywa na mwanadamu, lakini kama ni kazi ambayo ni lazima ifanywe na Mungu binafsi, kazi ya vita kati ya Mungu Mwenyewe na Shetani, basi kazi hii haiwezi kufanywa na mwanadamu. Katika awamu ya kwanza, wakati hakukuwepo na vita dhidi ya Shetani, Yehova binafsi aliongoza wana wa Israeli kutumia unabii uliosemwa na manabii. Baadaye, awamu ya pili ya kazi ilikuwa vita na Shetani, na Mungu Mwenyewe binafsi akawa mwili, kuja katika mwili, ili kufanya kazi hii. Chochote ambacho kinahusisha vita na Shetani pia kinahusisha kupata mwili kwa Mungu, ambayo ina maana kuwa vita hivi haviwezi kufanywa na mwanadamu. Kama mwanadamu angekuwa wa kufanya vita, hangeweza kumshinda Shetani. Jinsi gani yeye angekuwa na nguvu ya kupambana dhidi ya Shetani wakati bado yumo chini ya utawala wake? Mwanadamu yumo katikati: Kama wewe utaegemea kuelekea kwa Shetani wewe ni wa Shetani, lakini wewe ukimridhisha Mungu wewe ni wa Mungu. Kama mwanadamu angeweza kuwa mbadala wake Mungu katika kazi ya vita hivi, je, yeye angekuwa na uwezo wa kufanya hivyo? Kama angekuwa na uwezo, je, hangeangamia kitambo sana? Je, yeye si angekuwa ameingia katika ulimwengu wa jahanamu muda mrefu uliopita? Na hivyo, mwanadamu hana uwezo wa kuchukua nafasi ya Mungu katika kazi yake, ambayo ni kusema kwamba mwanadamu hana kiini cha Mungu, na kama ungepambana na Shetani hungeweza kumshinda Shetani. Mwanadamu anaweza tu kufanya baadhi ya kazi; anaweza kushinda baadhi ya watu, lakini hawezi kuwa mbadala wa Mungu katika kazi ya Mungu Mwenyewe. Je, ni jinsi gani mwanadamu atafanya vita na Shetani? Shetani ataweza kukushika mateka kabla hata hujaanza. Ni wakati Mungu Mwenyewe hufanya vita dhidi ya Shetani na mwanadamu kufuata na kutii Mungu katika msingi huu tu ndipo mwanadamu anaweza kupatwa na Mungu na kutoroka kutokana na vifungo vya Shetani. Kile mwanadamu anaweza kufikia kwa hekima yake na uwezo wake mwenyewe ni kidogo sana; hana uwezo wa kufanya mwanadamu akamilike, kumwongoza mwanadamu, na, zaidi ya hayo, kumshinda Shetani. Akili na hekima ya mwanadamu haviwezi kuharibu miradi ya Shetani, hivyo je, ni jinsi gani mwanadamu awezavyo kufanya vita na Shetani?

Wale wote ambao wamo tayari kufanywa kamili wana nafasi ya kukamilishwa, kwa hivyo kila mtu ni sharti apumzike: katika siku zijazo ninyi wote mtaingia kwenye hatima. Lakini kama huko tayari kufanywa kamili, na huko tayari kuingia katika ufalme wa kustaajabisha, basi hilo ni tatizo lako mwenyewe. Wale wote ambao wako tayari kufanywa kamili na ni waaminifu kwa Mungu, wale wote ambao hutii, na wale wote ambao hufanya kazi yao kwa uaminifu watu wote kama hawa wanaweza kufanywa kamili. Leo, wale wote ambao hawatekelezi majukumu yao kwa uaminifu, wale wote ambao si waaminifu kwa Mungu, wale wote ambao hawajiwasilishi kwa Mungu, hasa wale ambao wamepokea kupata nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu lakini hawaweki mafundisho hayo kwenye vitendo—watu wote kama hawa hawawezi kufanywa kamili. Wote wale ambao wako tayari kuwa waaminifu na kumtii Mungu wanaweza kufanywa kamili, hata kama ni wapumbavu kwa kiasi kidogo, wote hao ambao wako tayari kufuatilia wanaweza kufanywa kamili. Hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kuhusu hili. Ili mradi umo tayari kufuata mwelekeo huu, unaweza kufanywa kamili. Mimi sina nia ya kuwacha au kuondoa chochote kati ya hizo miongoni mwenu, lakini ikiwa mwanadamu hajitahidi kufanya vyema, basi utakuwa unajiangamiza mwenyewe; siyo Mimi ndiye ninakuondoa, lakini ni wewe mwenyewe. Kama wewe mwenyewe hutajitahidi kufanya vyema—ikiwa wewe ni mvivu, au hutekelezi jukumu lako, au si mwaminifu, au hufuati ukweli na daima unafanya unavyotaka, ukitenda bila kujali, ukipigania umaarufu wako na bahati yako mwenyewe na huna maadili katika kushirikiana na jinsia tofauti, basi utabeba mzigo wa dhambi zako mwenyewe; hustahili huruma ya yeyote. Lengo langu ni kwa ajili ya nyinyi nyote mfanywe kamilifu, na kuwa angalao muweze kushindwa, ili awamu hii ya kazi iweze kumalizika kwa mafanikio. Mapenzi ya Mungu ni kuwa kila mtu aweze kufanywa kamili, na kupatwa naye hatimaye, na kutakaswa naye kabisa, na kuwa mmoja anayependwa na Yeye. Haijalishi kama Ninasema nyinyi ni wa fikra za kurudi nyuma au wa kimo cha umaskini—hii yote ni ukweli. Huku kusema kwangu hakuthibitishi kuwa Mimi nina nia kukuacha wewe, kwamba Mimi Nimepoteza matumaini kwenu, au kwa kiasi kidogo kwamba sina nia ya kuwaokoa. Leo Nimekuja kufanya kazi ya ukombozi wenu, ambayo ni kusema kuwa kazi ambayo Mimi hufanya ni mwendelezo wa kazi ya ukombozi. Kila mtu ana nafasi ya kufanywa kamili: Ili mradi uko tayari, ili mradi ufuate, na mwishowe wewe utaweza kutimiza matokeo haya, na hakuna hata mmoja wenu ambaye ataachwa. Kama wewe ni mtu wa kimo cha umasikini, mahitaji Yangu kwenu yatakuwa kwa mujibu wa kimo chako cha umaskini; kama wewe ni wa kimo cha juu, mahitaji Yangu kwako yatakuwa kwa mujibu wa kimo chako cha juu; kama wewe ni mjinga na hujui kusoma na kuandika, mahitaji Yangu kwako yatakuwa kwa mujibu wa ujinga wako; kama wewe unajua kusoma na kuandika, mahitaji Yangu kwako yatakuwa kwa mujibu wa ukweli kwamba wewe unajua kusoma na kuandika; kama wewe ni mkongwe, mahitaji Yangu kwako yatakuwa kwa mujibu wa umri wako; kama wewe una uwezo wa kutoa ukarimu, mahitaji Yangu kwako yatakuwa kwa mujibu wa hilo; kama wewe unasema huwezi kutoa ukarimu, na unaweza tu kufanya kazi fulani, iwe ni kueneza injili, au kuchunga huduma ya kanisa, au kuhudhuria mambo mengine kwa ujumla, Ukamilifu Wangu kwako utakuwa kwa mujibu wa kazi ambayo wewe hufanya. Kuwa mwaminifu, kutii hadi mwisho kabisa, na kutafuta upendo mkuu wa Mungu—mambo haya ni lazima uyakamilishe, na hakuna vitendo vizuri zaidi kuliko mambo haya matatu. Hatimaye, mtu anatakiwa kuyafikia mambo haya matatu, na kama anaweza kuyafikia hayo atafanywa kamili. Lakini, zaidi ya yote, ni lazima ujitahidi na kuendelea kwa bidii, na usiwe wa kukaa tu kuelekea hapo. Nimesema kwamba kila mtu ana nafasi ya kufanywa mkamilifu, na ana uwezo wa kukamilishwa, na hili ni kweli, lakini hujaribu kuwa bora zaidi katika ufuatiliaji wako. Kama huwezi kuvifikia vigezo hivyo vitatu, mwishowe lazima uondolewe. Nataka kila mtu afaulu kufikia wengine, nataka kila mtu awe na kazi na kupata nuru wa Roho Mtakatifu, na kuwa na uwezo wa kutii hadi mwisho kabisa, kwa sababu huu ni wajibu wa kila mmoja wenu ambao mnapaswa kufanya. Wakati nyinyi wote mmetimiza wajibu wenu, mtakuwa wote mmefanywa kamili, mtakuwa pia na ushuhuda wa kustaajabisha. Wale wote walio na ushuhuda ni wale ambao wamekuwa na ushindi juu ya Shetani na wanapewa ahadi ya Mungu, na wao ndio watakaobaki kuishi katika hatima ya ajabu.

Iliyotangulia: Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni

Inayofuata: Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp