3. Wokovu Unawezekana Tu Kupitia Imani kwa Mwenyezi Mungu

Maneno Husika ya Mungu:

Yesu Alipokuja katika ulimwengu wa mwanadamu, Aliikaribisha Enzi ya Neema na Akatamatisha Enzi ya Sheria. Wakati wa siku za mwisho, Mungu kwa mara nyingine Alipata mwili, na kwa mwili huu, Alitamatisha Enzi ya Neema na Akaikaribisha Enzi ya Ufalme. Wale wote wanaoweza kukubali kupata mwili kwa Mungu mara ya pili wataongozwa kuingia katika Enzi ya Ufalme, na zaidi ya hayo watakuwa na uwezo wa kukubali kibinafsi uongozi wa Mungu. Hata ingawa Yesu Alikuja miongoni mwa wanadamu na akafanya kazi nyingi, Alimaliza tu kazi ya kuwakomboa wanadamu wote na Akawa kama sadaka ya dhambi ya mwanadamu; Hakumwondolea mwanadamu tabia yake yote ya upotovu. Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuwa kama sadaka ya dhambi tu na kuchukua dhambi za mwanadamu, lakini pia kulimlazimu Mungu afanye hata kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake iliyopotoshwa na Shetani kikamilifu. Na kwa hivyo, baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake, Mungu Alirudi katika mwili kumwongoza mwanadamu kuingia katika enzi mpya, na Akaanza kazi ya kuadibu na hukumu. Kazi hii imemleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi. Wale wote wanaonyenyekea chini ya utawala Wake watapata kufurahia ukweli wa juu na kupata baraka nyingi mno. Wataishi katika mwanga kwa kweli, na wao watapata ukweli, njia na uzima.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji

Kupata mwili mara ya kwanza kulikuwa kumkomboa mwanadamu kutoka katika dhambi kupitia mwili wa Yesu, yaani, Alimwokoa mwanadamu kutoka msalabani, lakini tabia potovu ya kishetani bado ilibaki ndani ya mwanadamu. Kupata mwili mara ya pili si kwa ajili ya kuhudumu tena kama sadaka ya dhambi ila ni kuwaokoa kikamilifu wale waliokombolewa kutoka kwa dhambi. Hii inafanyika ili wale waliosamehewa wakombolewe kutoka kwa dhambi zao, na kufanywa safi kabisa, na kupata mabadiliko ya tabia, hivyo kujikwamua kutoka kwa ushawishi wa Shetani wa giza na kurudi mbele za kiti cha enzi cha Mungu. Hivyo tu ndivyo mwanadamu ataweza kutakaswa kikamilifu. Baada ya Enzi ya Sheria kufika mwisho, na kuanzia Enzi ya Neema, Mungu alianza kazi ya wokovu, ambayo inaendelea hadi siku za mwisho ambapo, katika kuhukumu na kuiadibu jamii ya binadamu kwa ajili ya uasi wao, Atawatakasa wanadamu kikamilifu. Ni hapo tu ndipo Mungu atakamilisha kazi Yake ya wokovu na kuingia katika pumziko.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)

Kazi katika siku za mwisho ni kunena maneno. Mabadiliko makuu yanaweza kusababishwa kwa watu kupitia katika maneno hayo. Mabadiliko yanayosababishwa sasa kwa watu hawa kwa sababu ya kukubali maneno haya ni makubwa kuliko yale ya watu katika Enzi ya Neema kwa kukubali ishara na maajabu hayo. Kwa maana, katika Enzi ya Neema, mapepo yalitolewa kutoka kwa mwanadamu kwa kuwekewa mikono na maombi, lakini tabia potovu ndani ya mwanadamu bado zilibaki. Mwanadamu aliponywa ugonjwa wake na kusamehewa dhambi zake, lakini kuhusu jinsi tu mwanadamu angesafishwa na tabia potovu za kishetani ndani yake, kazi hii ilikuwa bado kufanywa. Mwanadamu aliokolewa na kusamehewa dhambi zake kwa imani yake, lakini asili ya dhambi ya mwanadamu haikuchukuliwa na ikabaki naye. Dhambi za mwanadamu zilisamehewa kupitia mwili wa Mungu mwenye mwili, lakini hili halikumaanisha kuwa mwanadamu hakuwa na dhambi ndani yake. Dhambi za mwanadamu zingesamehewa kupitia sadaka ya dhambi, lakini mwanadamu hajaweza kutatua suala la vipi hangeweza kutenda dhambi na vile asili Yake ya dhambi ingetupiliwa mbali kabisa na kubadilishwa. Dhambi za mwanadamu zilisamehewa kwa sababu ya kazi ya Mungu ya kusulubiwa, lakini mwanadamu akaendelea kuishi katika tabia yake potovu ya zamani ya kishetani. Hali hii ikiwa hivyo, mwanadamu lazima aokolewe kabisa kutoka kwa tabia yake potovu ya kishetani, ili asili yake ya dhambi iweze kung’olewa kabisa, isiweze kukua tena, hivyo kuwezesha tabia ya mwanadamu kubadilishwa. Hii inampasa mwanadamu kuelewa njia ya kukua katika maisha, njia ya maisha, na jinsi ya kubadilisha tabia yake. Inamhitaji pia mwanadamu kutenda kulingana na njia hii ili tabia ya mwanadamu iweze kubadilika hatua kwa hatua na aishi chini ya nuru inayong’aa, na aweze kufanya mambo yote kulingana na mapenzi ya Mungu, atupilie mbali tabia potovu za kishetani, na kutoka kwa ushawishi wa Shetani wa giza, hivyo kutoka kabisa katika dhambi. Ni hapo tu ndipo mwanadamu atapokea wokovu kamili.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)

Yesu Alipokuwa Akifanya kazi Yake, maarifa ya mwanadamu juu Yake yalikuwa bado hayakuwa bayana na hayakuwa wazi. Mwanadamu aliamini kila wakati kuwa Alikuwa Mwana wa Daudi na kumtangaza kuwa nabii mkuu na Bwana mwema Aliyezikomboa dhambi za mwanadamu. Wengine, wakiwa na msingi wa imani, wakaponywa tu kwa kugusa vazi Lake; vipofu wakaona na hata wafu kurejeshwa katika uhai. Hata hivyo, mwanadamu hangeweza kutambua tabia potovu za kishetani zilizokita mizizi ndani yake na pia mwanadamu hakujua jinsi ya kuitoa. Mwanadamu alipokea neema nyingi, kama amani na furaha ya mwili, baraka ya familia nzima juu ya imani ya mmoja, na kuponywa magonjwa, na mengine mengi. Yaliyobaki ni matendo mema ya mwanadamu na kuonekana kwa kiungu; kama mtu angeishi katika huo msingi, angechukuliwa kama muumini mzuri. Waumini hao tu ndio wangeingia mbinguni baada ya kifo, ambayo ilimaanisha kuwa walikuwa wameokolewa. Lakini katika maisha yao, hawakuelewa kamwe njia ya maisha. Walitenda tu dhambi, na kisha kukiri kila wakati bila njia yoyote ya kubadili tabia yao; hii ndiyo ilikuwa hali ya mwanadamu katika Enzi ya Neema. Je mwanadamu amepokea wokovu kamili? La! Kwa hivyo, hatua ilipokamilika, bado kuna kazi ya hukumu na kuadibu. Hatua hii ni ya kumfanya mwanadamu awea safi kupitia neno, na hivyo kumpa njia ya kufuata. Hatua hii haingekuwa na matunda ama ya maana kama ingeendelea na kukemea mapepo, kwani msingi wa dhambi wa mwanadamu haungetupwa mbali na mwanadamu angekoma tu baada ya msamaha wa dhambi. Kupitia kwa sadaka ya dhambi, mwanadamu amesamehewa dhambi zake, kwani kazi ya kusulubisha imefika mwisho na Mungu Ametawala juu ya Shetani. Lakini tabia potovu ya wanadamu bado imebaki ndani yao na mwanadamu anaweza kutenda dhambi na kumpinga Mungu; Mungu hajampata mwanadamu. Hiyo ndio sababu katika hatua hii ya kazi Mungu Anatumia neno kufichua tabia potovu ya mwanadamu na kumuomba mwanadamu kutenda kulingana na njia sahihi. Hatua hii ni ya maana zaidi kuliko zile za awali na pia yenye mafanikio zaidi, kwani wakati huu ni neno ambalo linatoa maisha moja kwa moja kwa mwanadamu na linawezesha tabia ya mwanadamu kubadilishwa kabisa; ni hatua ya kazi ya uhakika kabisa. Kwa hivyo, Mungu kupata mwili katika siku za mwisho imekamilisha umuhimu wa Mungu kupata mwili wa Mungu na kukamilisha usimamizi wa Mungu katika mpango wa kuokoa mwanadamu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)

Unajua tu kwamba Yesu atashuka wakati wa siku za mwisho, lakini je, Atashuka kwa njia gani hasa? Mwenye dhambi kama wewe, ambaye umetoka tu kukombolewa, na haujabadilishwa bado, ama kukamilishwa na Mungu, je, unaweza kufuata nia za Mungu? Kwa wewe, wewe ambaye ni wa nafsi yako ya zamani, ni kweli kuwa uliokolewa na Yesu, na kwamba huhesabiwi kama mwenye dhambi kwa sababu ya wokovu wa Mungu, lakini hii haithibitishi kwamba wewe si mwenye dhambi, na si mchafu. Unawezaje kuwa mtakatifu kama haujabadilishwa? Ndani, umezingirwa na uchafu, ubinafsi na ukatili, na bado unatamani kushuka na Yesu—huwezi kuwa na bahati namna hiyo! Umepitwa na hatua moja katika imani yako kwa Mungu: umekombolewa tu, lakini haujabadilishwa. Ili uweze kuwa sawa na nia za Mungu, lazima Mungu Mwenyewe afanye kazi ya kukubadilisha na kukutakasa; ikiwa umekombolewa tu, hautakuwa na uwezo wa kufikia utakatifu. Kwa njia hii hautahitimu kushiriki katika baraka nzuri za Mungu, kwani umepitwa na hatua kwa kazi ya Mungu ya kumsimamia mwanadamu, ambayo ni hatua muhimu ya kubadilisha na kukamilisha. Na basi wewe, mwenye dhambi uliyetoka tu kukombolewa, huna uwezo wa kurithi urithi wa Mungu moja kwa moja.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Majina na Utambulisho

Katika kazi ya siku za mwisho, neno lina nguvu zaidi kuliko udhihirisho wa ishara na maajabu, na mamlaka ya neno hushinda yale ya ishara na maajabu. Neno linaweka wazi tabia zote potovu katika moyo wa mwanadamu. Huwezi kutambua binafsi wewe mwenyewe. Yatakapofunuliwa kwako kupitia kwa neno, utakuja kujua mwenyewe; hutaweza kuyakataa, na utashawishika kikamilifu. Je haya si mamlaka ya neno? Haya ndiyo matokeo yanayopatikana kwa kazi ya wakati huu ya neno. Kwa hivyo, mwanadamu hawezi kuokolewa kikamilifu kutoka kwa dhambi zake kwa kuponya magonjwa na kukemea mapepo na hawezi kufanywa mkamilifu kabisa kwa udhihirisho wa ishara na maajabu. Mamlaka ya kuponya na kukemea mapepo yanapatia mwanadamu neema tu, lakini mwili wa mwanadamu bado ni wa Shetani na tabia potovu za kishetani zitabaki ndani ya mwanadamu. Kwa maneno mengine, yale ambayo hayajatakaswa bado inahusu dhambi na uchafu. Ni baada tu ya mwanadamu kufanywa safi kupitia kwa maneno ndipo mwanadamu atakapopatwa na Mungu na kutakaswa. Wakati mapepo yalikemewa kutoka kwa mwanadamu na alikombolewa, hii ilimaanisha tu kwamba alipokonywa kutoka kwa mikono ya Shetani na kurudishwa kwa Mungu. Hata hivyo, hajafanywa msafi ama kubadilishwa na Mungu, anabaki kama mpotovu. Ndani ya mwanadamu bado kuna uchafu, pingamizi na uasi; mwanadamu amerudi tu kwa Mungu kupitia kwa ukombozi Wake, lakini mwanadamu hana maarifa hata kidogo kumhusu Mungu na bado anaweza kumpinga na kumsaliti. Kabla ya mwanadamu kukombolewa, sumu nyingi za Shetani zilikuwa tayari zimepandwa ndani yake na, baada ya maelfu ya miaka ya kupotoshwa na Shetani, ndani yake ana asili inayompinga Mungu. Kwa hiyo, mwanadamu alipokombolewa, haikuwa chochote zaidi ya kisa cha ukombozi. Yaani, mwanadamu ananunuliwa tena kwa gharama ya juu, lakini asili ya sumu ndani yake haikuwa imeondolewa. Mwanadamu ambaye ni mchafu sana lazima apitie mabadiliko kabla ya kuwa mwenye kustahili kumtumikia Mungu. Kupitia kazi hii ya kuadibu na hukumu, mwanadamu atakuja kujua kikamlifu kiini cha uchafu na upotovu kilicho ndani yake, na ataweza kubadilika kabisa na kutakasika. Ni kwa namna hii tu ndivyo mwanadamu ataweza kustahili kurudi mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Kazi yote ifanywayo siku hii ya leo ni ili mwanadamu afanywe msafi na kubadilika; kupitia hukumu na kuadibiwa na neno, na pia kutakaswa, mwanadamu anaweza kuacha nje upotovu wake na kufanywa safi. Badala ya kuichukua hatua hii ya kazi kuwa ile ya wokovu, itafaa zaidi kusema kuwa ni kazi ya utakaso. Kwa kweli hatua hii ni ile ya ushindi na pia hatua ya pili ya wokovu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)

Mungu Anapopata mwili mara hii, kazi Yake ni kuonyesha tabia Yake, kimsingi kupitia kuadibu na hukumu. Akitumia haya kama msingi, Analeta ukweli zaidi kwa mwanadamu, kuonyesha njia zaidi za matendo, na hivyo Hufikia lengo Lake la kumshinda mwanadamu na kumwokoa mwanadamu kutokana na tabia yake potovu. Hili ndilo liko katika kazi ya Mungu katika Enzi ya Ufalme.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji

Wanaoweza kusimama imara wakati wa kazi ya Mungu ya hukumu na kuadibu siku za mwisho—yaani, wakati wa kazi ya mwisho ya utakaso—watakuwa wale watakaoingia katika raha ya mwisho na Mungu; kwa hivyo, wanaoingia rahani wote watakuwa wametoka katika ushawishi wa shetani na kupokewa na Mungu baada tu ya kupitia kazi Yake ya mwisho ya utakaso. Hawa watu ambao hatimaye wamepokewa na Mungu wataingia katika raha ya mwisho. Sababu ya kazi ya Mungu ya kuadibu na hukumu katika kiini ni ili kuwatakasa binadamu kwa ajili ya pumziko la mwisho; bila utakaso wa aina hii, hakuna binadamu yeyote angeainishwa katika makundi tofauti kulingana na aina yake ama kuingia katika pumziko. Hii kazi ni njia ya pekee ya binadamu kuingia rahani. Kazi ya Mungu ya utakaso pekee ndiyo itatakasa udhalimu wa binadamu, na kazi Yake ya kuadibu na hukumu pekee ndiyo itadhihirisha hayo mambo yasiyotii miongoni mwa binadamu, hivyo kutenga wanaoweza kuokolewa kutoka wale wasioweza, na wale watakaobaki kutoka wale ambao hawatabaki. Kazi Yake itakapoisha, wale watu watakaoruhusiwa kubaki wote watatakaswa na kuingia katika hali ya juu zaidi ya ubinadamu ambapo watafurahia maisha ya pili ya binadamu ya ajabu zaidi duniani; kwa maneno mengine, wataingia katika siku ya binadamu ya raha na kuishi pamoja na Mungu. Baada ya wasioweza kubaki kupitia kuadibu na hukumu, umbo zao halisi zitafichuliwa kabisa; baada ya haya wote wataangamizwa na, kama Shetani, hawatakubaliwa tena kuishi duniani. Binadamu wa baadaye hawatakuwa tena na aina yoyote ya watu hawa; watu hawa hawafai kuingia eneo la raha ya mwisho, wala hawafai kuingia siku ya raha ambayo Mungu na mwanadamu watashiriki, kwani ni walengwa wa adhabu na ni waovu, na si watu wenye haki. … Kusudi lote la kazi kuu ya Mungu ya kuadhibu maovu na kuthawabisha mema ni kuwatakasa kabisa wanadamu wote ili Aweze kuleta ubinadamu mtakatifu katika pumziko la milele. Hatua hii ya kazi Yake ni kazi Yake muhimu zaidi. Ni hatua ya mwisho ya kazi Yake yote ya usimamizi.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja

Kristo wa siku za mwisho huleta uzima, na huleta njia ya kweli ya kudumu na ya milele. Ukweli huu ndiyo njia ambayo kwayo binadamu anapata uzima, na ndiyo njia pekee ambayo mwanadamu atamjua Mungu na kukubaliwa na Mungu. Kama hutatafuta njia ya maisha inayotolewa na Kristo wa siku za mwisho, basi kamwe hutapata kibali cha Yesu, na kamwe hutastahili kuingia lango la ufalme wa mbinguni, maana wewe ni kikaragosi na mfungwa wa historia. Wale ambao wanadhibitiwa na kanuni, na maneno, na minyororo ya historia kamwe hawataweza kupata uzima wala kupata njia ya kudumu ya uzima. Hii ni kwa sababu yote walio nayo ni maji machafu ambayo yameshikiliwa kwa maelfu ya miaka badala ya maji ya uzima yanayotiririka kutoka kwenye kiti cha enzi. Wale ambao hawajaruzukiwa maji ya uzima daima watabakia maiti, vitu vya kuchezewa na Shetani, na wana wa Jehanamu. Je, basi jinsi gani wanaweza kumtazama Mungu? Ukitafuta tu kushikilia yaliyopita, ukisimama tu bila kusonga na kuweka mambo jinsi yalivyo, na usitafute kubadilisha hali iliyopo na kuitupilia mbali historia, hivyo hutakuwa ukimpinga Mungu kila wakati? Hatua za kazi ya Mungu ni zenye nguvu na kuu, kama kufurika kwa mawimbi na mngurumo wa radi—lakini wewe unakaa tu bila kufanya chochote ukisubiri maangamizo, ukikwamilia yale ya zamani na kusubiri vitu vikuangukie miguuni. Kwa njia hii, unaweza kuchukuliwaje kama mtu anayefuata nyayo za Mwanakondoo? Unaweza kuonyeshaje kwamba Mungu unayeshikilia ndiye Mungu ambaye ni mpya daima na kamwe si wa zamani? Na maneno ya vitabu vyako vilivyochuchuka yanawezaje kukubeba hadi katika enzi mpya? Yanawezaje kukuongoza katika kutafuta hatua za kazi ya Mungu? Na jinsi gani yanaweza kukuchukua wewe kwenda mbinguni? Unayoshikilia mikononi mwako ni maneno tu ambayo yanaweza tu kukupa furaha ya muda mfupi, wala sio ukweli unaoweza kukupa uzima. Maneno ya maandiko unayosoma yanaweza tu kuuimarisha ulimi wako; hayo siyo maneno ya hekima ambayo yanaweza kukusaidia kujua uzima wa binadamu, sembuse hayo kuwa njia zinazoweza kukuongoza kuelekea kwenye ukamilifu. Je, tofauti hii haikupi sababu ya kutafakari? Je, haikupi umaizi ndani ya siri zilizomo ndani? Je, una uwezo wa kujiwasilisha mwenyewe mbinguni kukutana na Mungu? Bila kuja kwa Mungu, je, unaweza kujipeleka mwenyewe mbinguni kufurahia pamoja na familia ya Mungu? Je, wewe bado unaota sasa? Ninakusihi, basi, uache kuota na uangalie ni nani anayefanya kazi sasa—tazama uone ni nani sasa anayetekeleza kazi ya kumwokoa mwanadamu katika siku za mwisho. Kama huwezi, kamwe hutapata ukweli, na kamwe hutapata uzima.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele

Wale ambao wanataka kupata uzima bila kutegemea ukweli wa neno la Kristo ni watu wenye mzaha mno duniani, na wale ambao hawawezi kukubali njia ya maisha inayoletwa na Kristo wamepotea ndotoni. Na hivyo nasema kwamba wale ambao hawamkubali Kristo wa siku za mwisho watachukiwa milele na Mungu. Kristo ni lango la binadamu kwa ufalme katika siku za mwisho, na hakuna ambaye anaweza kumpita Yeye. Hakuna anayeweza kukamilishwa na Mungu ila kwa njia ya Kristo. Unamwamini Mungu, na hivyo ni lazima ukubali neno Lake na kulitii neno Lake. Usifikiri tu kuhusu kupata baraka huku ukikosa kuweza kupokea ukweli na ruzuku ya uzima. Kristo Anakuja katika siku za mwisho ili Aweze kuwatolea uzima wale wote ambao wanamwamini kwa dhati. Kazi hii ipo kwa ajili ya kuhitimisha enzi ya zamani na kuiingia enzi mpya, na kazi hii ndiyo njia ambayo lazima ifuatwe na wale wote ambao wataingia katika enzi mpya. Kama humtambui Kristo, na zaidi ya hayo umhukumu, umkufuru au kumtesa Yeye, basi wewe umefungwa kuchomwa milele na kamwe hutaingia katika ufalme wa Mungu. Hii ni kwa sababu Kristo huyu Mwenyewe ni onyesho la Roho Mtakatifu, onyesho la Mungu, Yule ambaye Mungu amemkabidhi kufanya kazi Yake hapa duniani, na hivyo nasema kwamba kama huwezi kukubali yote yanayofanywa na Kristo wa siku za mwisho, basi unamkufuru Roho Mtakatifu.Adhabu inayostahili kwa wale wanaomkufuru Roho Mtakatifu ni dhahiri kwa wote. Pia nakuambia hili: Ukimpinga Kristo wa siku za mwisho, ukimkataa Kristo wa siku za mwisho, basi hakuna mtu mwingine anayeweza kubeba matokeo ya hili kwa niaba yako. Zaidi ya hayo, kuanzia wakati huo na kuendelea hutawahi kuwa na nafasi ya kupata kibali cha Mungu kamwe; hata ukitaka kujikomboa, hutaweza kuutazama uso wa Mungu tena. Hii ni kwa sababu unayempinga si mwanadamu, unayemkataa si mtu asiye na maana, bali ni Kristo. Je, unajua matokeo ya hili ni yapi? Hufanyi kosa dogo, bali unatenda dhambi mbaya sana. Na kwa hivyo namshauri kila mtu asitoe kucha na meno au kutoa maoni kiholela mbele ya ukweli, kwa maana ukweli pekee ndio unaoweza kukuletea uzima, na hakuna chochote isipokuwa ukweli kinachoweza kukuwezesha kuzaliwa upya na kuutazama uso wa Mungu tena.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele

Iliyotangulia: 2. Mwenyezi Mungu Ndiye Bwana Yesu Aliyerudi

Inayofuata: 1. Kwa Nini Mungu Hutajwa Majina, na Jina Moja Linaweza Kuwakilisha Uzima wa Mungu?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp