Sura ya 72

Sharti unitegemee kuondoa upungufu ama udhaifu mara tu unapougundua. Usichelewe; vinginevyo kazi ya Roho Mtakatifu atakuwa mbali sana nawe, na utaanguka nyuma mbali sana. Kazi ambayo Nimekuaminia inaweza kutimizwa kwa kupitia tu kukaribia kwako mara kwa mara, kuomba, na kuwa na ushirika katika uwepo Wangu. Kama sivyo, hakuna matokeo yoyote yatakayofikiwa, na kila kitu kitakuwa bure. Kazi Yangu leo si kama ilivyokuwa awali. Kadiri ya maisha kwa watu Ninaowapenda si kama ilivyokuwa mbeleni. Wote wanayaelewa maneno Yangu kwa hakika, na wana umaizi mwelekevu juu yake. Hiki ndicho kipengele dhahiri kabisa; kinaweza zaidi kuakisi ajabu la kazi Yangu. Mwendo wa kazi Yangu unaongeza kasi, na kazi Yangu bila shaka ni tofauti na iliyopita. Ni vigumu kwa watu kudhania, na zaidi ya hayo ni vigumu kwa watu kuelewa. Hakuna kilicho fumbo kwenu tena; badala yake, kila kitu kinajulishwa na kujitokeza. Ni wazi, kinatolewa, na, hata zaidi, ni cha bure kabisa. Wale Ninaowapenda kwa hakika hawatazuiliwa na mtu yeyote, tukio, kitu, ama na kipindi ama jeografia; watavuka mipaka ya udhibiti unaotolewa na mazingira na wataibuka kutoka katika miili. Huu ndio ukamilisho wa kazi Yangu kuu. Hakutakuwa na yoyote itakayosalia; itakuwa imemalizika kabisa.

Ukamilisho wa kazi kuu unasemwa kwa kurejelea wazaliwa wote wa kwanza wa kiume na watu wote ambao Ninawapenda. Kuanzia sasa kuendelea hutadhibitiwa na mtu yeyote, tukio, ama kitu. Mtasafiri kotekote katika mataifa mbalimbali ya ulimwengu, mpite katika ulimwengu mzima, ili kwamba nyayo zenu zisalie kila mahali. Msifikiri hili kuwa mbali sana; ni kitu ambacho kitatokea hivi punde mbele yenu. Kile Ninachokifanya kitaaminiwa kwenu, na pahali ambapo miguu Yangu itakanyaga patakuwa na nyayo zenu. Hii ndiyo maana ya kweli ya Mimi na nyinyi kutamalaki kama wafalme. Je, mmetafakari kwa nini ufunuo ambao Ninatoa daima u wazi zaidi, u dhahiri zaidi na zaidi, pasipo kufichwa hata kidogo? Kwa nini Nimeshuhudia ushuhuda mkuu zaidi, na kuwaambia kuhusu mafumbo yote na maneno yote? Sababu si nyingine ila kazi ambayo imetajwa hapo juu. Maendeleo ya kazi yenu kwa sasa ni ya polepole sana, hata hivyo. Hamna uwezo wa kuenda kwa mwendo sawa na Ninavyopiga hatua, hamwezi kushirikiana na Mimi vyema zaidi, na kwa sasa bado hamna uwezo wa kutimiza mapenzi Yangu. Lazima Niwafunze kwa nguvu zaidi, Nizidishe kasi ya ukamilisho Wangu kwenu, ili kuwaruhusu kuuridhisha moyo Wangu haraka iwezekanavyo.

La wazi zaidi sasa ni kwamba kundi la wazaliwa wa kwanza limeundika kabisa, wote wakiidhinishwa na Mimi, ambao walikuwa hata wameamuliwa kabla na kuchaguliwa na Mimi tangu uumbaji wa dunia, kila mmoja akikuzwa na mkono Wangu mwenyewe. Hakuna nafasi ya kufikiria kwa mwanadamu katika hili, na haliwezi kudhibitiwa nawe. Usijivune; yote ni ukarimu Wangu na huruma. Machoni Pangu, kila kitu tayari kimetimizwa. Ni kwa sababu tu macho yenu yana ukungu, na hata sasa huwezi kuona wazi ajabu la vitendo Vyangu. Hamko wazi kikamilifu na hamuelewi kabisa kuhusu kudura Yangu, hekima Yangu, kila kitendo Changu, na kila neno Langu na tendo. Kwa hivyo Nazungumza dhahiri. Kwa wana Wangu, wapendwa Wangu, Niko radhi kulipa gharama, Niko radhi kufanya kazi kwa bidii, na Niko radhi kujitumia Mwenyewe. Je, unanijua kupitia kwa maneno Yangu? Je, unahitaji kwamba Niseme wazi zaidi? Usiwe mpotovu tena; fikiri juu ya moyo Wangu! Sasa kwa kuwa fumbo kuu limefumbuliwa kwenu, mna lipi la kusema? Je, bado mna malalamiko yoyote? Msipolipa thamana na kutia bidii, je, mnaweza kustahili shida yote ambayo Nimepitia?

Siku hizi watu hawawezi kujidhibiti. Nisipompendelea mtu, hataweza kunipenda, ingawa anaweza kutaka kufanya hivyo. Watu ambao Nimewajaalia na kuwachagua, hata hivyo, hawataweza kuepuka ingawa wangetaka kufanya hivyo; bila kujali popote waendapo hawataweza kuepuka kiganja cha mkono Wangu. Hivyo ndivyo ulivyo uadhama Wangu, hata zaidi ilivyo hukumu Yangu. Watu wote sharti wafanye shughuli zao kulingana na mpango Wangu, na kulingana na mpenzi Yangu. Kila kitu kutoka hapa hadi nje hurejea mikononi Mwangu kabisa, na hawawezi kukidhibiti wenyewe. Kimedhibitiwa na Mimi kikamilifu, kimepangwa na Mimi. Mtu asiposhiriki kwa kiasi kidogo, Sitamwacha aende kwa urahisi. Kuanzia leo, Nitawaruhusu watu wote waanze kunijua—Mungu wa pekee wa kweli aliyeviumba vyote, aliyekuja miongoni mwa watu na kukataliwa na kukashifiwa nao, anayedhibiti na kupanga kila kitu, mfalme anayesimamia ufalme, Mungu Mwenyewe anayesimamia ulimwengu, hata zaidi Mungu anayedhibiti maisha na mauti ya watu, mwenye ufunguo wa Kuzimu. Nitawaruhusu watu wote (wazima, watoto, bila kujali ikiwa wana roho au la, ama ikiwa ni wapumbavu ama walemavu, nk.) wanijue. Simwachilii yeyote kutoka kwa kazi hii; ni kazi inayohitaji ustadi kabisa, kazi ambayo Nimetayarisha vema, kazi ambayo inatekelezwa kuanzia sasa hivi. Ninalosema litafanyika. Yafungue macho yako ya Kiroho, ziache dhana zako, na utambue kuwa Mimi ndimi Mungu wa kweli wa pekee Anayetawala ulimwengu! Sijafichwa kwa yeyote, na Mimi hutekeleza amri Zangu za utawala kwa kila mtu.

Viweke kando vitu vyako vyote. Je, si vitu vyote unavyovipata kutoka Kwangu ni vya thamani kubwa na vyenye umuhimu mkuu? Je, hakuna tofauti kubwa mno kati ya hayo na takataka yako? Usipoteze wakati wowote katika kuviacha vitu vyote vya bure! Imeamuliwa sasa iwapo baraka zinapatikana ama kukumbana na msiba. Sasa ni wakati muhimu; hata zaidi ni wakati wa umakinifu. Je, unaweza kuona hili?

Iliyotangulia: Sura ya 71

Inayofuata: Sura ya 73

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp