Sura ya 73

Maneno Yangu yanatimizwa mara tu yanaposemwa; hayabadiliki kamwe na ni sahihi kabisa. Kumbuka hili! Kila neno na kirai kutoka katika kinywa Changu lazima yafikiriwe kwa uangalifu. Kuwa makini zaidi, usije ukapitia upotezaji na kupokea hukumu Yangu, ghadhabu Yangu na moto Wangu pekee. Kazi yangu sasa inasonga mbele kwa kasi ya haraka sana, ingawa si ya haraka haraka; imesafishwa kwa ustadi sana kwamba haiwezi kabisa kuonekana kwa macho tu, na haiwezi kushikwa na mikono ya wanadamu. Ni iliyofanywa kwa uangalifu hasa. Mimi huwa Sitamki maneno matupu; kila Ninachosema ni kweli. Unapaswa kuamini kwamba kila neno ni la kweli na sahihi. Usiwe mzembe; huu ni wakati muhimu! Ikiwa utapata baraka au bahati mbaya itaamuliwa katika wakati huu hasa, na tofauti iko hivyo kati ya mbingu na dunia. Iwapo unaenda mbinguni au Kuzimuni yote iko katika udhibiti Wangu kikamilifu. Wale wanaokwenda Kuzimuni wanajihusisha na mapambano yao ya mwisho ya kufa, wakati wale wanaoenda mbinguni wanapitia mateso yao ya mwisho na kutumika kwao kwa mwisho kwa ajili Yangu, na kila kitu wanachofanya katika siku zijazo ni kufurahia na kusifu, bila vitu vyote visivyo vya maana vinavyowasumbua watu (ndoa, kazi, utajiri wenye kukera, hadhi, na kadhalika). Lakini kwa wale wanaoenda Kuzimuni, mateso yao ni ya milele (hii inahusu roho, nafsi, na mwili wao), kamwe wasitoroke kutoka kwa mkono Wangu wa adhabu. Pande hizi mbili hazipatani kama moto na maji. Hakuna kutatizana: Wale wanaopatwa na bahati mbaya wataendelea kupatwa na bahati mbaya, wakati wale waliobarikiwa watafurahia hadi watosheke.

Matukio yote na vitu vinadhibitiwa na Mimi, bila kutaja kwamba ninyi—wanangu, wapendwa Wangu—ni Wangu hata zaidi. Ninyi ndio dhihirisho la mpango Wangu wa usimamizi wa miaka 6,000, hazina Zangu. Wale wote Ninaowapenda wanapendeza macho Yangu, kwa sababu wananidhihirisha; wale wote Ninaowachukia Ninawadharau bila hata kuwatazama, kwa sababu wao ni wazawa wa Shetani na ni wa Shetani. Leo, kila mtu anapaswa kujichunguza mwenyewe: Kama nia zako ni sahihi na unanipenda kwa kweli, basi hakika utapendwa na Mimi. Lazima unipende kweli na lazima usinidanganye! Mimi ni Mungu anayechunguza ndani zaidi ya mioyo ya watu! Kama nia zako ni mbaya na wewe ni baridi na usiye mwaminifu Kwangu, basi bila shaka utachukiwa na Mimi na hukuwa umechaguliwa au kuamuliwa kabla na Mimi. Wewe subiri tu kwenda kuzimu! Watu wengine wanaweza kukosa kuona mambo haya, lakini ni wewe tu na Mimi—Mungu anayetazama kwa kina ndani ya mioyo ya wanadamu—tunaoyajua. Yatafichuliwa kwa wakati fulani. Waaminifu hawahitaji kuwa na wasiwasi na wasio waaminifu hawahitaji kuwa na hofu. Yote ni sehemu ya mpango Wangu wa hekima.

Kazi hii ni ya dharura na nzito, na inawahitaji kutumia kwa ajili Yangu mara moja ya mwisho kukamilisha kazi hii ya mwisho. Mahitaji Yangu siyo ya juu: Nawahitaji tu kuweza kuratibu nami vizuri sana, kuniridhisha katika kila kitu, kufuata uongozi Wangu ndani yenu. Msiwe vipofu; muwe na lengo, na kuhisi nia Zangu kutoka kwa kila kipengele na katika kila kitu. Hii ni kwa sababu Mimi si Mungu aliyefichwa kwenu tena. Lazima muwe wazi sana juu ya hili ili muelewe nia Zangu. Katika muda mfupi sana, hamtakutana tu na wageni wanaotafuta njia ya kweli, kilicho cha muhimu zaidi ni kwamba ninyi mnapaswa kuwa na uwezo wa kuwaongoza. Hiyo ndiyo nia Yangu ya dharura. Haikubaliki iwapo hamwezi kuona hili. Hata hivyo, lazima uamini katika kudura Yangu. Mradi tu watu wako sahihi, hakika Nitawafundisha kuwa askari wema. Kila kitu kimepangwa na Mimi ipasavyo. Lazima mtamani kuteseka kwa ajili Yangu. Huu ndio wakati muhimu. Msiukose! Sitakumbuka mambo kutoka katika siku zenu za nyuma. Lazima uombe na kusihi mbele Zangu mara nyingi; Mimi Nitakupa neema ya kutosha kwa furaha na matumizi yako. Neema na baraka si kitu kimoja. Kile mnachofurahia sasa ni neema Yangu na hakifai kutajwa machoni Pangu, ilhali baraka ni kile mtakachofurahia milele katika siku zijazo. Hizo ni baraka ambazo watu hawajafikiria na hawawezi kufikiria. Nasema mmebarikiwa kwa sababu hii—ni baraka ambayo mwanadamu hajafurahi tangu uumbaji.

Tayari Nimefichua yote Yangu kwenu. Natumaini tu kwamba ninyi mtakuwa wenye huruma kwa moyo Wangu, kufikiria kwa ajili Yangu katika kila jambo, na kuwa wenye huruma Kwangu katika kila kitu, ili kila Ninachoona kila mara ni nyuso zenu zenye kutabasamu. Kuanzia sasa kuendelea, wale wanaopata hadhi ya wazaliwa wa kwanza ni watu ambao watatawala kama wafalme pamoja nami. Hawatadhulumiwa na ndugu yeyote, wala hawataadibiwa au kushughulikiwa na Mimi, kwa sababu kanuni Yangu ya kufanya mambo ni: Wale walio katika kikundi cha wazaliwa wa kwanza ni watu wanaodharauliwa na kudhulumiwa na wengine na wamepitia mabadiliko yote ya maisha. (Wameshughulikiwa na kuvunjwa na Mimi mapema, na wamefanyika wakamilifu mbeleni.) Watu hawa tayari wamefurahia pamoja na Mimi baraka wanazopaswa kupokea mapema. Mimi ni mwenye haki na Simpendelei yeyote.

Iliyotangulia: Sura ya 72

Inayofuata: Sura ya 74

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp