Sura ya 77

Kutokuwa na hakika ya maneno Yangu ni sawa na kushikilia mtazamo wa kukanusha kuelekea matendo Yangu. Yaani, maneno Yangu yamebubujika kutoka ndani ya Mwanangu, lakini hamyatilii maanani. Ninyi hamko makini! Maneno mengi yamebubujika kutoka ndani ya Mwanangu, lakini ninyi ni wenye mashaka, hamyajui sana. Ninyi ni vipofu! Hamwelewi madhumuni ya kila kitu ambacho Nimefanya. Je, maneno Ninayoyaeleza kupitia kwa Mwanangu si maneno Yangu? Kuna mambo mengine ambayo Siko tayari kuyasema moja kwa moja, kwa hiyo Nazungumza kupitia kwa Mwana Wangu. Lakini kwa nini ninyi ni wenye upuuzi sana kiasi kwamba mnasisitiza Ninene moja kwa moja? Hunielewi Mimi, na kila mara una mashaka kuhusu vitendo na matendo Yangu! Je, Sijasema hapo awali kwamba kila hatua Yangu na kila kitendo Changu ni sahihi? Watu wanapaswa kuacha kuyachunguza. Ondoa mikono yako michafu! Hebu Nikuambie: Watu wote ambao Mimi huwatumiwa waliamuliwa kabla ya Mimi kuumba ulimwengu, na pia wanaidhinishwa na Mimi leo. Ninyi daima mnatia bidii kwa mambo kama hayo, mkichunguza mtu Niliye na kuyachunguza matendo Yangu. Ninyi nyote mna mawazo ya wafanyabiashara. Hili likitokea tena basi hakika mtaangushwa kwa mkono Wangu Ninachosema ni: Usinishuku, na pia usichanganue au kufikiri juu ya mambo ambayo Nimeyatenda. Aidha, usiingilie mambo kama hayo. Ni kwa sababu hii inahusiana na amri Zangu za utawala. Hili sio jambo dogo!

Tumia wakati kufanya yote Niliyoyaagiza. Hebu Niseme tena, na pia kama onyo: Wageni wako karibu kufurika nchini China. Hii ni kweli kabisa! Najua watu wengi wana mashaka juu ya jambo hili na hawana hakika, kwa hivyo Nawakumbusha tena na tena ili kwamba muweze kutafuta ukuaji wa maisha kwa haraka na kuweza kuyaridhisha mapenzi Yangu mapema iwezekanavyo. Kuanzia sasa, hali ya kimataifa itakuwa na fadhaa hata zaidi, na nchi mbalimbali zitaanza kuanguka kutoka ndani. Hakutakuwa tena na siku za furaha nchini China. Yaani, wafanyakazi watagoma, wanafunzi wataacha masomo yao, wafanyabiashara wataacha masoko, na viwanda vitafungwa vyote na havitaweza kudumu. Wale maofisa wa jeshi wataanza kuandaa fedha za kutoroka (hii, pia, itatumikia mpango Wangu wa usimamizi), na viongozi wa serikali kuu katika ngazi zote pia watakuwa na shughuli nyingi sana wakizingatia mambo fulani huku wakiacha mengine yaharibike huku wote wakifanya maandalizi (hii ni ili kutumikia hatua ifuatayo). Angalia hili vizuri! Hili ni jambo linalohusisha ulimwengu wote, si tu China, kwa maana kazi Yangu inaelekezwa kwa ulimwengu wote, lakini pia inatumika kulifanya kundi la wazaliwa wa kwanza kuwa wafalme. Je, mnaona hili waziwazi? Harakisha mtafute! Sitawatendea pasi na haki; Nitawaruhusu mpate furaha hadi mridhike.

Matendo Yangu ni ya ajabu. Wakati ambapo kuna maafa makubwa ulimwenguni, wakati ambapo waovu wote na wakuu wanapokea adhabu—au kuwa wazi, wakati ambapo waovu walio nje ya jina Langu wanateseka—Nitaanza kuwapa baraka Zangu. Hii ndio maana halisi ya maneno “Bila shaka hamtapitia uchungu au madhara ya maafa” ambayo Nimesema mara kwa mara hapo zamani. Je, mnaelewa hili? “Wakati huu” Ninaozungumzia unahusu wakati ambapo maneno yanatokana kinywani Mwangu. Kazi ya Roho Mtakatifu ni ya haraka sana; Sitakawia au kupoteza dakika au sekunde, lakini badala yake Nitafanya kulingana na maneno Yangu mara tu yanaponenwa. Nikisema kuwa leo Ninamwondoa mtu au Namdharau mtu, yote yatakwisha kwa mtu huyo mara moja. Hiyo ni kusema kwamba Roho Mtakatifu Wangu ataondolewa mara moja kutoka kwake na atakuwa mfu anayetembea, mtu asiye na maana. Anaweza kuwa bado anapumua, kutembea na kuzungumza, na anaweza bado kuomba mbele Yangu, lakini hatawahi kutambua kwamba Nimemwacha. Yeye hasa ni mtu asiye na maana. Hii bila shaka ni kweli na halisi!

Maneno Yangu yanamwakilisha mwanadamu niliye. Kumbuka hili! Msiwe na shaka; lazima muwe na hakika kabisa. Haya ni mapambano ya kufa na kupona! Hili ni jambo zito sana! Katika wakati ambapo maneno Yangu yanazungumzwa, kile Ninachotaka kufanya kimefanyika. Lazima maneno haya yote yanenwe kupitia kwa Mwanangu. Ni nani kati yenu ametafakari jambo hili kwa uzito? Ninaweza kuelezea jambo hili vipi tena? Msiwe wenye kutishwa na waoga kila mara. Je, Mimi ni mtu Asiyewafikiria wengine? Je, Nitawatupa nje wale ambao Ninawaidhinisha bila mpango? Kila kitu Ninachofanya kina kanuni. Sitalivunja agano Nililoliweka Mimi Mwenyewe; Sitauvuruga mpango Wangu Mwenyewe. Mimi si mjinga kama ninyi. Kazi Yangu ni jambo kuu; ni kitu ambacho hakuna mwanadamu anayeweza kufanya. Nimesema kuwa Mimi ni mwenye haki, na kwamba Ninawapenda wale wanaonipenda. Je, huamini kuwa hii ni kweli? Unaendelea kuwa na shaka! Iwapo dhamiri yako iko wazi kuhusu kila kitu, basi kwa nini bado unaogopa sana? Yote ni kwa sababu umejifunga. Mwanangu! Nimekukumbusha mara nyingi usiwe na huzuni na usitoe machozi, nami Sitakutupa. Je, bado huwezi kuniamini? Mimi Nitakushikilia na Sitakuachilia. Nitakukumbatia daima katika upendo Wangu. Nitakutunza, kukulinda, na katika kila jambo kukupa ufunuo na ufahamu wa kukuwezesha kuona kwamba Mimi ni Baba yako, msaada wako. Najua kuwa daima wewe hutafakari jinsi ambavyo unaweza kupunguza mzigo ulio juu ya mabega ya Baba yako. Huu ndio mzigo Niliokupa. Usijaribu kuudharau! Ni wangapi leo wanaweza kuwa waaminifu Kwangu? Natumaini unaweza kuongeza kasi ya mafunzo yako na kukua haraka ili kuukidhi moyo Wangu. Baba humfanyia mtoto kazi kwa bidii usiku na mchana, hivyo pia lazima mwana aufikirie mpango wa usimamizi wa Baba kila dakika na kila sekunde. Huu ndio ushirikiano wa shauku pamoja na Mimi ambao Nilikuwa na mazoea ya kuuzungumzia.

Haya yote ni shughuli Yangu. Nitaweka mzigo juu ya watu Ninaowatumia leo na kuwapa hekima, ili yale yote wanayoyatenda yatakubaliana na mapenzi Yangu, ili ufalme Wangu utimizwe, na mbingu na nchi mpya zitatokea. Watu ambao Siwatumii ni kinyume kabisa. Kila mara wao huwa wametunduwaa, wao hulala baada ya kula, na hula baada ya kulala, bila kujua kabisa maana ya mzigo. Watu hawa wanakosa kazi ya Roho Mtakatifu na wanapaswa kusafishwa kutoka katika kanisa Langu haraka iwezekanavyo. Sasa Nitawasiliana kuhusu baadhi ya mambo juu ya kipengele cha maono: Kanisa ni sharti la kwanza la ufalme. Watu wanaweza tu kuingia katika ufalme mara kanisa linapojengwa kwa kiwango fulani. Hakuna mtu anayeweza kuingia katika ufalme moja kwa moja (ikiwa hakuahidiwa na Mimi). Kanisa ni hatua ya kwanza, ilhali ufalme ni kusudi la mpango Wangu wa usimamizi. Kila kitu kitakuwa katika hali nzuri watu watakapoingia katika ufalme na hakutakuwa na chochote cha kuogopa. Sasa, ni wazaliwa Wangu wa kwanza pekee na Mimi ambao tumeingia katika ufalme na tumeanza kutawala mataifa yote na watu wote. Yaani, ufalme Wangu unaanza kuwa na mpangilio, na wote ambao watakuwa wafalme au watu Wangu wametangazwa hadharani. Mtaambiwa matukio ya baadaye hatua kwa hatua na kwa utaratibu. Hupaswi kuwa na wasiwasi au wahaka sana. Je, unakumbuka kila neno ambalo Nimekumbia? Ikiwa kwa kweli uko upande Wangu, basi Nitazungumza kwako kwa uaminifu. Kwa mintarafu ya wale wanaotenda ulaghai na udanganyifu, Nitawachukulia kwa namna isiyo ya dhati pia, na kuwaacha waone vizuri kabisa ni nani atakayeangamizwa na mwenendo kama huo!

Iliyotangulia: Sura ya 76

Inayofuata: Sura ya 78

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp