Sura ya 76

Matamshi Yangu yote ni maonyesho ya mapenzi Yangu. Ni nani anayeweza kuudhukuru mzigo Wangu? Nani anayeweza kuelewa nia Yangu? Je, mmefikiria kila moja ya maswali Niliyoibua kwenu? Uzembe ulioje! Unathubutu vipi kuvuruga mipango Yangu? Wewe Wewe umevuka mipaka! Kazi kama hii ya pepo wabaya ikiendelea, Nitawatupa mautini mara moja katika shimo lisilo na mwisho! Kwa muda mrefu Nimeona waziwazi matendo mbalimbali ya pepo wabaya. Na watu wanaotumiwa na pepo wabaya (wale wenye nia mbaya, wale wanaotamani mwili au utajiri, wale wanaojikuza, wale wanaolivuruga kanisa, nk.) kila mmoja wao pia amebainika na Mimi. Usifikiri kwamba kila kitu kimemalizika punde pepo wabaya watatupwa nje. Hebu Nikwambie! Kuanzia sasa na kuendelea, Nitawaondoa watu hawa mmoja baada ya mwingine, nisiwatumie kamwe! Yaani, mtu yeyote aliyepotoshwa na pepo wabaya hatatumiwa na Mimi, na atafukuzwa! Usifikiri kuwa Sina hisia! Fahamu jambo hili! Mimi ndimi Mungu mtakatifu, na Sitakaa katika hekalu chafu! Mimi huwatumia tu watu waaminifu na wenye hekima ambao ni waaminifu kabisa Kwangu na wanaoweza kuudhukuru mzigo Wangu. Hii ni kwa sababu watu kama hao walijaaliwa na Mimi, na bila shaka hakuna pepo wabaya wanaowafanyia kazi hata kidogo. Hebu Nieleze wazi jambo moja: Kuanzia sasa na kuendelea, wale wote ambao hawana kazi ya Roho Mtakatifu wana kazi ya pepo wabaya. Hebu Nirudie: Simtaki hata mtu mmoja ambaye pepo wabaya humfanyia kazi. Wote watatupwa kuzimuni pamoja na miili yao!

Matakwa Yangu kwenu hapo zamani yalikuwa malegevu kidogo, na mmekuwa wapotovu inapohusu mwili. Kuanzia siku hii na kuendelea, Sitawaruhusu mwendelee hivi. Ikiwa maneno na vitendo vyako havinidhihirishi katika kila namna, au kama haviko katika mfano Wangu hata kidogo, basi bila shaka Sitawasamehe kwa urahisi. Vinginevyo, mngekuwa mkicheka na kufanya utani kila mara, mkivunja mbavu zenu kwa vicheko, bila kizuizi chochote. Unapotenda jambo baya, je, huhisi kuwa Nimekuacha? Kwa kuwa unajua, kwa nini bado u mpotovu? Je, bado unasubiri mguso wa mkono Wangu wa hukumu? Kuanzia leo, Nitamwadhibu mara moja mtu yeyote asiyekubaliana na nia Yangu hata kwa wakati mmoja. Mkikaa pamoja mkipiga umbeya, basi Nitakuacha. Usizungumze ikiwa hutoi ruzuku ya kiroho. Sisemi hivi ili kuwazuia, lakini Ninamaanisha kwamba kwa kuwa kazi Yangu imeendelea hadi hatua iliyopo sasa, Nitaendelea mbele kulingana na mpango Wangu. Mkiketi pamoja mkiwasiliana kuhusu mambo ya kiroho katika maisha, basi Nitakuwa pamoja nanyi. Sitamtendea yeyote kati yenu pasi na haki. Ukifungua kinywa chako, Nitakupa maneno yanayofaa. Unapaswa kufahamu moyo Wangu kutoka ndani ya maneno Yangu. Siwaambii mjifanye kuwa bubu, wala Siwaambii mshiriki katika porojo.

Kwa nini Ninaendelea kusema kwamba hakuna muda mwingi uliobaki, na kwamba siku Yangu haipaswi kucheleweshwa? Je, mmefikiria kuhusu jambo hili kwa makini? Je, mnaelewa maana ya maneno Yangu kweli? Yaani, Nimekuwa nikifanya kazi tangu nilipoanza kuzungumza. Kila mmoja wenu amekuwa lengo la kazi Yangu, si mtu yeyote hasa; na zaidi ya hayo, si mtu mwingine yeyote. Mna wasiwasi tu kuhusu kutofurahia baraka, lakini hamfikirii juu ya maisha yenu. Ninyi ni wapumbavu kweli! Mnasikitisha sana! Hamuufikirii mzigo Wangu hata!

Juhudi Zangu zote za mchwa na gharama ambayo Nimelipa vimekuwa kwa ajili yenu. Ikiwa hamuufikirii mzigo Wangu, basi hamjafikia matarajio Yangu kwa ajili yenu. Mataifa yote yanawasubiri mmiliki, na watu wote wanawasubiri mtawale. Nimeweka kila kitu mikononi mwenu. Sasa, wale wote walio mamlakani wameanza kujiuzulu na wameanguka, na wanasubiri tu hukumu Yangu iwafike. Angalia waziwazi! Dunia inaanguka sasa, huku ufalme Wangu umejengwa kwa mafanikio. Wanangu wameonekana na wazaliwa Wangu wa kwanza wanatawala pamoja na Mimi kama wafalme, wakitawala mataifa na watu mbalimbali. Usifikiri hili ni jambo lisilo yakini; ni ukweli ulio dhahiri. Je, sivyo? Mara tu mtakapoomba na kunisihi, Nitachukua hatua mara moja na kuwaadhibu wale wanaowatesa, kuwashughulikia wale wanaowasumbua, kuwaharibu wale mnaowachukia, na kuwatawala watu hao, matukio, na vitu ambavyo huwatumikia. Nimesema mara nyingi: Sitamletea wokovu mtu yeyote anayemtumikia Kristo (yaani, mtu yeyote ambaye hutoa huduma kwa Mwanangu). Kumhudumia Mwanangu hakumaanishi kuwa wao ni watu wema; ni kutokana na nguvu Zangu kuu na matendo ya ajabu tu. Msitilie umuhimu sana katika binadamu. Hakika watu kama hao hawana kazi ya Roho Mtakatifu na hawaelewi mambo ya kiroho kabisa. Hawatakuwa na manufaa yoyote baada ya Mimi kumaliza nao. Kumbuka hili! Huu ni uthibitisho Wangu kwenu. Msielewe tu bila mpango, mnafahamu?

Kuna watu wachache zaidi na zaidi, lakini washiriki wanazidi kusafishwa zaidi na zaidi. Hii ni kazi Yangu, mpango Wangu wa usimamizi, na zaidi ya hayo hekima Yangu na kudura Yangu. Ni uratibu wa ubinadamu Wangu wa kawaida na uungu Wangu kamili. Je, mnaona jambo hili waziwazi? Je, mna ufahamu wowote wa kweli kuhusu jambo hili? Nitatimiza moja baada ya lingine, kupitia uungu Wangu, kila kitu ambacho Nimenena kutoka kwa ubinadamu Wangu wa kawaida. Hii ndiyo sababu Ninaendelea kusema kuwa kile Ninachosema kitafanyika bila ya utata wowote; badala yake, yote yatakuwa wazi na dhahiri sana. Kila kitu Ninachosema kitatimizwa, na hakika hakitatendeka ovyoovyo. Sizungumzi maneno matupu na Sifanyi makosa. Yeyote atakayethubutu kunipima atahukumiwa, na hakika hataweza kuponyoka kiganja cha mkono Wangu. Mara maneno Yangu yanapozungumzwa, ni nani anayethubutu kupinga? Ni nani anayethubutu kunirairai au kunificha chochote? Nimesema hapo awali: Mimi ni Mungu mwenye hekima. Ninatumia ubinadamu Wangu wa kawaida kuwafichua watu wote na tabia ya shetani, kuwafichua wale wenye nia mbaya, wale wanaotenda kwa njia moja mbele ya wengine na kwa njia nyingine bila wao kufahamu, wale wanaonipinga, wale wasio waaminifu Kwangu, wale wanaotamani fedha, wale ambao hawaudhukuru mzigo Wangu, wale wanaojihusisha na ulaghai na udanganyifu pamoja na ndugu zao, wale wanaozungumza kwa maneno matamu ili kuwafanya watu wafurahi, na wale ambao hawawezi kuratibu na ndugu zao kwa umoja kwa kujitolea. Kwa sababu ya ubinadamu Wangu wa kawaida, watu wengi sana hunipinga kwa siri na kushiriki katika ulaghai na udanganyifu, wakidhani kuwa ubinadamu Wangu wa kawaida haujui. Na watu wengi sana wanatilia maanani maalum ubinadamu Wangu wa kawaida, wakinipa vitu vizuri nile na kunywa, wakinitumikia kama watumishi, na wakininenea yaliyo ndani ya mioyo yao, huku wakati wote wakitenda kwa njia tofauti kabisa pasi na ufahamu Wangu. Binadamu vipofu! Mnajua kidogo sana kabisa—Mungu ambaye huangalia kwa kina sana ndani ya moyo wa mwanadamu. Bado hamnijui Mimi hata sasa; bado mnafikiri Sijui kile unachonuia. Fikiria jambo hilo: Ni watu wangapi ambao wamejiangamiza kwa sababu ya ubinadamu Wangu wa kawaida? Amka! Usinidanganye tena. Lazima uweke tabia na mwenendo wako wote, kila neno na tendo lako mbele Yangu, na ukubali ukaguzi Wangu wa hilo.

Iliyotangulia: Sura ya 75

Inayofuata: Sura ya 77

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp