1. Umuhimu wa Kazi ya Mungu ya Maneno

Maneno Husika ya Mungu:

Katika Enzi ya Ufalme, Mungu hutumia maneno kuikaribisha enzi mpya, kubadilisha njia ambayo kwayo Yeye hufanya kazi, na kufanya kazi ya enzi nzima. Hii ndiyo kanuni ambayo kwayo Mungu hufanya kazi katika Enzi ya Neno. Alikuwa mwili ili Anene kutoka katika mitazamo tofauti, ili mwanadamu aweze kumwona Mungu kweli, ambaye ni Neno kuonekana katika mwili, na angeweza kuona hekima na ajabu Yake. Kazi kama hiyo inafanywa ili kufikia malengo ya kumshinda mwanadamu, kumkamilisha mwanadamu, na kumwondoa mwanadamu vyema zaidi, ambayo ndiyo maana ya kweli ya matumizi ya maneno kufanya kazi katika Enzi ya Neno. Kupitia katika maneno haya, watu huja kuijua kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, kiini cha mwanadamu, na kile ambacho mwanadamu anapaswa kuingia katika. Kupitia katika maneno, kazi ambayo Mungu anataka kufanya katika Enzi ya Neno inafanikiwa kwa ukamilifu. Kupitia katika maneno haya, watu wanafunuliwa, kuondolewa, na kujaribiwa. Watu wameyaona maneno ya Mungu, kuyasikia maneno haya, na kutambua uwepo wa maneno haya. Kama matokeo, wameamini katika uwepo wa Mungu, katika kudura na hekima ya Mungu, na pia katika upendo wa Mungu kwa mwanadamu na tamanio Lake la kumwokoa mwanadamu. Neno "maneno" linaweza kuwa rahisi na la kawaida, lakini maneno yanayonenwa kutoka katika kinywa cha Mungu mwenye mwili yanautikisa ulimwengu, kuibadilisha mioyo ya watu, kubadilisha fikira zao na tabia zao za zamani, na kubadilisha jinsi ambavyo ulimwengu wote ulikuwa ukionekana. Katika enzi zote, ni Mungu wa leo tu ndiye Aliyefanya kazi kwa njia hii, na ni Yeye Anayezungumza kwa namna hii na kuja kumwokoa mwanadamu hivi. Kuanzia wakati huu na kuendelea, mwanadamu anaishi chini ya mwongozo wa maneno ya Mungu, akichungwa na kuruzukiwa na maneno Yake. Watu wanaishi katika ulimwengu wa maneno ya Mungu, kati ya laana na baraka za maneno ya Mungu, na kuna hata watu wengi zaidi ambao wamekuja kuishi chini ya hukumu na kuadibu kwa maneno Yake. Maneno haya na kazi hii vyote ni kwa sababu ya wokovu wa mwanadamu, kwa sababu ya kutimiza mapenzi ya Mungu, na kwa sababu ya kubadilisha kuonekana kwa asili kwa ulimwengu wa uumbaji wa zamani. Mungu aliuumba ulimwengu kwa kutumia maneno, Anawaongoza watu ulimwenguni kote kutumia maneno, na Anawashinda na kuwaokoa kutumia maneno. Hatimaye, Atatumia maneno kuutamatisha ulimwengu mzima wa zamani, hivyo kuukamilisha mpango Wake mzima wa usimamizi. Katika Enzi nzima ya Ufalme, Mungu hutumia maneno kufanya kazi Yake, na kufikia matokeo ya kazi Yake. Hatendi maajabu au kufanya miujiza, lakini hufanya kazi Yake kupitia katika maneno tu. Kwa sababu ya maneno haya, mwanadamu hulishwa na kuruzukiwa, na hupata maarifa na uzoefu wa kweli. Katika Enzi ya Neno, mwanadamu amebarikiwa kwa njia ya pekee. Hapitii uchungu wa mwili na hufurahia tu ruzuku nyingi ya maneno ya Mungu; bila kuhitaji kwenda kutafuta bila kufikiri au kusafiri mbele bila kufikiri, kutoka katikati ya utulivu wake, huiona sura ya Mungu, humsikia Akinena kwa kinywa Chake mwenyewe, hupokea kile ambacho Yeye hutoa, na humtazama Akifanya kazi Yake binafsi. Hivi ni vitu ambavyo watu wa enzi zilizopita hawakuweza kufurahia, na ni baraka ambazo hawangeweza kupokea kamwe.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Enzi ya Ufalme Ni Enzi ya Neno

Wakati huo, Yesu alifanya kazi kubwa ambayo haikueleweka kwa wanafunzi Wake, na kusema mengi kwamba watu hawakuelewa. Hii ni kwa sababu, wakati huo, Hakutoa maelezo. Kwa hivyo, miaka kadhaa baada ya Yeye kuondoka, Mathayo aliunda kizazi chake, na wengine pia walifanya kazi kubwa ambayo ilikuwa ya mapenzi ya mwanadamu. Yesu hakuja kumkamilisha na kumpata mwanadamu, lakini kufanya awamu moja ya kazi: kuleta injili ya ufalme wa mbinguni na kukamilisha kazi ya kusulubiwa—na punde tu Yesu Aliposulubishwa, kazi Yake ilifika mwisho kamili. Lakini kwa awamu iliyoko sasa—kazi ya ushindi—maneno mengi zaidi lazima yasemwe, kazi nyingi zaidi lazima ifanywe, na lazima kuwe na hatua nyingi. Hivyo pia ni lazima siri za kazi ya Yesu na Yehova zitafichuliwa, ili wanadamu wote waweze kuwa na ufahamu na uwazi wa imani yao, kwa kuwa hii ni kazi ya siku za mwisho, na siku za mwisho ni mwisho wa kazi ya Mungu, wakati wa kuhitimisha kazi hii. Hii awamu ya kazi itakufafanulia sheria ya Yehova na ukombozi wa Yesu, na ni hasa ili uweze kuelewa kazi nzima ya mpango wa usimamizi wa Mungu wa miaka elfu sita, na kuelewa kusudi la kazi zote Alizozifanya Yesu na maneno Aliyoyasema, na hata upofu wako wa imani kwenye na katika ibada ya Biblia. Yote haya yatakuwezesha kuelewa kabisa. Wewe utakuja kufahamu kazi anayoifanya Yesu na kazi ya Mungu leo; utaelewa na kushuhudia ukweli wote, uzima, na njia. Katika awamu ya kazi Aliyoifanya Yesu, kwa nini Yesu Aliondoka bila kufanya kazi ya ukamilishaji? Kwa sababu awamu ya kazi ya Yesu haikuwa kazi ya kukamilisha. Wakati Yeye Alisulubishwa msalabani, maneno Yake pia yalifika mwisho; baada ya kusulubiwa kwake, kazi Yake kwa hivyo ilimalizika. Awamu ya sasa ni tofauti. Ni baada tu ya maneno hayo kusemwa hadi mwisho na kazi nzima ya Mungu iwe imehitimika ndipo kazi yake itakapokuwa imemalizika. Wakati wa awamu ya kazi ya Yesu, kulikuwa na maneno mengi yaliyobakia bila kusemwa, au ambayo hayakuwa yameelezwa kikamilifu kwa ufasaha. Waama, Yesu hakujali Alichosema au kile ambacho hakusema, kwa kuwa huduma yake haikuwa huduma ya maneno; na hivyo baada ya Yeye kusulubishwa msalabani Aliondoka. Awamu hiyo ilikuwa hasa kwa ajili ya kusulubiwa, na ni tofauti na awamu ya sasa. Awamu ya kazi hii ni hasa kwa ajili ya kukamilisha, kufumbua, na kuleta kazi yote kwenye hitimisho. Kama maneno hayasemwi hadi tamati yake kabisa, hakutakuwa na mbinu ya kuhitimisha kazi hii, kwa kuwa awamu hii ya kazi yote inafikishwa mwisho na kukamilika kwa kutumia maneno. Wakati huo, Yesu Alifanya kazi kubwa isiyoeleweka na mwanadamu. Akaondoka kimyakimya, na leo bado kunao wengi wasioelewa maneno Yake, ambao ufahamu wao ni potofu lakini bado unaaminika nao kwamba ni sahihi, ambao hawajui kuwa wao si sahihi. Mwishoni, awamu hii ya sasa itafikisha kazi ya Mungu mwisho ulio kamilifu, na kutoa hitimisho Lake. Wote watakuja kufahamu na kujua mpango wa usimamizi wa Mungu. Dhana zilizo ndani ya mwanadamu, nia yake, fahamu yake potofu, dhana zake kuhusu kazi ya Yehova na Yesu, maoni yake kuhusu watu wa Mataifa mengine na michepuko yake ingine na makosa yake yatarekebishwa. Na mwanadamu ataelewa njia yote ya haki ya uzima, na kazi yote anayofanya Mungu, na ukweli wote. Wakati hayo yatafanyika, awamu hii ya kazi itafikia kikomo.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (2)

Katika hatua hii ya mwisho ya kazi, matokeo yanapatikana kupitia kwa neno. Kupitia kwa neno, mwanadamu anaelewa mafumbo mengi na kazi ya Mungu katika vizazi vilivyopita; kupitia kwa neno, mwanadamu anapewa nuru na Roho Mtakatifu; kupitia kwa neno, mwanadamu anapata kuelewa mafumbo ambayo hayajawahi kuelezwa na vizazi vilivyopita, na pia kazi za manabii na, mitume wa enzi zilizopita, na kanuni ambazo walitumia kufanya kazi; kupitia kwa neno, mwanadamu anatambua tabia ya Mungu Mwenyewe, na pia uasi na pingamizi ya mwanadamu, na anakuja kujua dutu yake mwenyewe. Kupitia kwa hatua hizi za kazi na maneno yote yaliyonenwa, mwanadamu anatambua kazi ya Roho Mtakatifu, kazi ya mwili wa Mungu, na zaidi ya hayo, tabia Yake yote. Maarifa yako ya kazi ya usimamizi wa Mungu wa kupita miaka elfu sita ulitwaliwa kupitia kwa neno. Je, maarifa yako hayakuwa ya fikira zako za awali na mafanikio kwa kuyaweka kando pia yalipatikana kupitia neno? Katika hatua ya awali, Yesu Alifanya ishara na maajabu, lakini sio hivyo katika hatua hii. Je si kuelewa kwako kwa nini Mungu hafanyi ishara na maajabu pia kulipatikana kupitia neno? Kwa hivyo, maneno yanenwayo katika hatua hii, yanashinda kazi iliyofanywa na mitume na manabii wa vizazi vilivyopita. Hata unabii uliotabiriwa na manabii haungeweza kupata matokeo haya.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)

Wakati wa siku za mwisho, Mungu Amekuja mahususi kwa ajili ya kuzungumza maneno Yake. Anazungumza kutokana na mtazamo wa Roho, kutokana na mtazamo wa mwanadamu, na kutokana na mtazamo wa nafsi ya tatu; Anazungumza kwa namna tofauti, Akitumia njia moja kwa kipindi fulani, na Anatumia njia za kuzungumza ili kubadilisha dhana za mwanadamu na kuondoa taswira ya Mungu yakini katika moyo wa mwanadamu. Hii ndiyo kazi kuu iliyofanywa na Mungu. Kwa sababu mwanadamu anaamini kwamba Mungu Amekuja kuponya wagonjwa, kutoa mapepo, kufanya miujiza, na kumpatia mwanadamu baraka za vitu, Mungu Anatekeleza hatua hii ya kazi—kazi ya kuadibu na hukumu—ili kuweza kuondoa mambo hayo kutoka katika dhana za mwanadamu, ili mwanadamu aweze kuuelewa uhalisia na ukawaida wa Mungu, na ili kwamba taswira ya Yesu iweze kuondolewa moyoni mwake na kuwekwa taswira mpya ya Mungu. Mara tu taswira ya Mungu ndani ya mwanadamu inapozeeka, basi inakuwa sanamu. Yesu alipokuja na kutekeleza hatua hii ya kazi, Hakuwakilisha Mungu kikamilifu. Alifanya baadhi ya ishara na maajabu, Alizungumza maneno kadhaa, na hatimaye Akasulubishwa, na Aliwakilisha upande mmoja wa Mungu. Hakuweza kuwakilisha yale yote ambayo ni ya Mungu, bali Alimwakilisha Mungu katika kufanya upande mmoja wa kazi ya Mungu. Hiyo ni kwa sababu Mungu ni mkuu, na ni wa ajabu sana, na Haeleweki, na kwa sababu Mungu Anafanya upande mmoja tu wa kazi Yake katika kila enzi. Kazi inayofanywa na Mungu katika enzi hii ni hasa ya kutoa maneno kwa ajili ya uzima wa mwanadamu; kufunuliwa kwa tabia potovu ya mwanadamu na kiini cha asili ya mwanadamu; na uondoaji wa fikira za kidini, fikra za kinjozi, mitazamo iliyopitwa na wakati, vilevile maarifa na utamaduni wa mwanadamu. Hii ni lazima iwekwe wazi na kusafishwa kupitia maneno ya Mungu. Katika siku za mwisho, Mungu Anatumia maneno na siyo ishara na maajabu ili kumfanya mwanadamu kuwa mkamilifu. Anatumia maneno Yake kumweka wazi mwanadamu, kumhukumu mwanadamu, kumwadibu mwanadamu, na kumkamilisha mwanadamu, ili katika maneno ya Mungu, mwanadamu aje kuona hekima na wema wa Mungu, na aje kuelewa tabia ya Mungu, ili kupitia maneno ya Mungu, mwanadamu aone matendo ya Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuijua Kazi ya Mungu Leo

Katika siku za mwisho, Mungu hasa hutumia neno kumfanya mwanadamu kuwa mkamilifu. Hatumii ishara na maajabu kumdhulumu mwanadamu, ama kumshawishi mwanadamu; hii haiweki wazi nguvu za Mungu. Iwapo Mungu angeonyesha tu ishara na maajabu, basi hakungekuwa na uwezo wa kuweka wazi ukweli wa Mungu, na hivyo haingewezekana kumfanya mwanadamu mkamilifu. Mungu hamfanyi mwanadamu mkamilifu kwa kutumia ishara na maajabu, ila Anatumia neno kunyunyizia na kumchunga mwanadamu, na baada ya haya kunapatikana utiifu kamili wa mwanadamu na ufahamu wa mwanadamu kuhusu Mungu. Hili ndilo lengo la kazi Anayofanya na maneno Anenayo. Mungu hatumii mbinu ya kuonyesha ishara na maajabu ili kumfanya mwanadamu kamili—Anatumia maneno, na Anatumia mbinu nyingi za kazi kumfanya mwanadamu kamili. Iwe ni usafishaji, kushughulikia, upogoaji, ama kupewa maneno, Mungu hunena kutoka taswira nyingi tofauti kumfanya mwanadamu kamili, na kumpa mwanadamu maarifa kuu ya kazi, hekima na ajabu ya Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu

Katika siku za mwisho, Mungu anapokuwa mwili, kimsingi Anatumia neno kukamilisha yote na kufanya yote yawe wazi. Katika maneno Yake pekee ndipo unaweza kuona kile Alicho; ni katika maneno Yake pekee ndiyo unaweza kuona kwamba yeye ni Mungu Mwenyewe. Mungu katika mwili Anapokuja duniani, hafanyi kazi nyingine ila kuongea maneno—hivyo basi hakuna haja ya kutumia uhakika; maneno yanatosha. Hii ni kwa sababu Amekuja kimsingi kufanya kazi hii, kumruhusu mwanadamu aone nguvu Zake na ukuu ulio kwenye neno Lake, kumruhusu mwanadamu kuona kupitia kwa maneno Yake jinsi Alivyojificha kwa unyenyekevu, na kumruhusu mwanadamu kujua ukamilifu Wake kupitia kwa maneno Yake. Kila kitu Alicho nacho na kile Alicho kiko katika maneno Yake, hekima Yake na ajabu yako katika maneno Yake. Katika hii ndipo unapofanywa kuona mbinu nyingi ambazo Mungu anatumia kuongea maneno Yake. Kazi ya Mungu nyingi katika wakati huu wote imekuwa kutoa, ufunuo, na kushughulika mwanadamu. Hatoi laana kwa mwanadamu kijuu juu, na hata Akifanya hivyo, ni kupitia kwa neno. Na hivyo, katika enzi hii ya Mungu kuwa mwili, usijaribu kuona Mungu akiponya wagonjwa na kufukuza mapepo tena, usijaribu kila mara kuona ishara—hakuna haja! Ishara hizo haziwezi kumfanya mwanadamu kamili! Kuongea wazi: Leo Mungu wa kweli Mwenyewe wa mwili Anaongea tu, na hatendi. Huu ni ukweli! Anatumia maneno kukufanya mkamilifu, na Anatumia maneno kukulisha na kukunyunyizia. Pia Anatumia maneno kufanya kazi, na Anatumia maneno badala ya uhakika kukufanya ujue ukweli Wake. Kama una uwezo wa kutazama aina hii ya kazi ya Mungu, basi itakuwa vigumu kuwa wa kutoonyesha hisia. Badala ya kulenga vitu vilivyo vibaya, mnapaswa tu kulenga yale yaliyo mazuri—hivyo ni kusema, bila kujali kama maneno ya Mungu yamekamilika au la, ama iwapo kuna majilio ya ukweli ama haupo, Mungu anamfanya mwanadamu kupata uzima kutoka kwa maneno Yake, na hii ndiyo ishara kuu kushinda zote, na hata zaidi, ni ukweli usiopingika. Huu ndio ushahidi bora wa kupata ufahamu kumhusu Mungu, na ni ishara hata kuu kushinda ishara. Maneno haya pekee yanaweza kumfanya mwanadamu kamili.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu

Ingawa maneno Yangu yanaweza kuwa makali, yote yanasemwa kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu, kwa kuwa Ninazungumza tu maneno na sio kuuadhibu mwili wa mwanadamu. Maneno haya humsababisha mwanadamu kuishi katika nuru, kujua kwamba mwanga upo, kujua kwamba mwanga ni wa thamani, hata zaidi kujua jinsi maneno haya yalivyo na manufaa kwa mtu, na kujua kwamba Mungu ni wokovu. Ingawa Nimesema maneno mengi ya kuadibu na hukumu, hayajafanywa kwako katika vitendo. Nimekuja kufanya kazi Yangu, kuzungumza maneno Yangu na, ingawa maneno Yangu yanaweza kuwa magumu, yanasemwa kwa hukumu ya upotovu na uasi wako. Madhumuni Yangu ya kufanya hili yanabaki kumwokoa mtu kutoka kwa utawala wa Shetani, kutumia maneno Yangu ili kumwokoa mwanadamu; Kusudi Langu sio kumdhuru mwanadamu kwa maneno Yangu. Maneno Yangu ni makali ili matokeo yaweze kupatikana kutoka katika Kazi Yangu. Ni katika kufanya kazi kwa njia hii tu ndipo mtu anaweza kujijua na anaweza kujitenga mbali na tabia yake ya uasi. Umuhimu mkubwa zaidi wa kazi ya maneno ni kuwaruhusu watu kuweza kutia katika matendo ukweli baada ya kuuelewa ukweli, kutimiza mabadiliko katika tabia yao, na kutimiza maarifa kuhusu wao wenyewe na kazi ya Mungu. Mbinu za kufanya kazi tu kupitia kwa kuongea ndizo zinazoweza kuleta mawasiliano kuhusu uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu, maneno tu ndiyo yanayoweza kuelezea ukweli. Kufanya kazi kwa njia hii ndiyo mbinu bora zaidi ya kumshinda mwanadamu; mbali na matamko ya maneno, hakuna mbinu nyingine inayoweza kumpatia mwanadamu uelewa wa wazi zaidi wa ukweli na kazi ya Mungu, na hivyo basi katika awamu Yake ya mwisho ya kazi, Mungu anazungumza naye mwanadamu ili kuweza kuwa wazi kwa mwanadamu kuhusu ukweli na siri zote ambazo haelewi, na hivyo basi kumruhusu kufaidi njia ya kweli na uzima kutoka kwa Mungu na kisha kutosheleza mapenzi ya Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mnapaswa Kuweka Pembeni Baraka za Hadhi na Kuelewa Mapenzi ya Mungu ya Kumletea Mwanadamu Wokovu

Katika enzi hii, na miongoni mwenu, Mungu atatimiza ukweli ufuatao: kwamba kila mtu ataishi kwa kuyadhihirisha maneno ya Mungu, ataweza kuuweka ukweli katika vitendo, na atampenda Mungu kwa dhati; kwamba watu wote watatumia maneno ya Mungu kama msingi na kama uhalisi wao, na watakuwa na mioyo inayomcha Mungu; na kwamba, kupitia kutenda maneno ya Mungu, mwanadamu kisha atashikilia mamlaka ya kifalme pamoja na Mungu. Hii ndiyo kazi inayopaswa kufanikishwa na Mungu. Je, unaweza kuishi bila kusoma maneno ya Mungu? Leo, kuna wengi ambao wanahisi kuwa hawawezi kuishi hata siku moja au mbili bila kusoma maneno Yake. Lazima wayasome maneno Yake kila siku, na ikiwa muda hauruhusu, kuyasikiza kutatosha. Hii ndiyo hisia ambayo Roho Mtakatifu huwapa watu, na ndiyo njia ambayo Anaanza kuwagusa. Yaani, Yeye huwatawala watu kupitia maneno, ili kwamba waweze kuingia katika uhalisi wa maneno ya Mungu. Ikiwa, baada ya siku moja tu bila kula na kunywa maneno ya Mungu, unahisi giza na kiu, na huwezi kustahimili hali hiyo, hili linaonyesha kwamba umeguswa na Roho Mtakatifu, na kwamba Hajakukuacha. Wewe basi, ni mtu aliye kwenye mkondo huu. Hata hivyo, ikiwa baada ya siku moja au mbili bila kula na kunywa maneno ya Mungu, huhisi kitu, ikiwa huna kiu, na hujaguswa hata kidogo, hili linaonyesha kwamba Roho Mtakatifu amekuacha. Hili linamaanisha, basi, kwamba kuna kitu kibaya na hali yako; hujaingia katika Enzi ya Neno, na wewe ni mmoja wa wale ambao wamebaki nyuma. Mungu hutumia maneno kuwatawala watu; unahisi vizuri ukila na kunywa maneno ya Mungu, na usipokula na kunywa maneno ya Mungu, huna njia ya kufuata. Maneno ya Mungu huwa chakula cha watu, na nguvu inayowaendesha. Biblia inasema “Mwanadamu hataishi kwa mkate pekee, lakini kwa kila neno linalotoka kinywani mwa Mungu”. Leo, Mungu ataikamilisha kazi hii, naye Ataukamilisha ukweli huu ndani yenu. Ni vipi kwamba hapo zamani, watu wangeweza kwenda siku nyingi bila kusoma maneno ya Mungu na bado waweze kula na kufanya kazi kama kawaida, lakini hivi sivyo ilivyo leo? Katika enzi hii, Mungu haswa hutumia maneno kutawala vyote. Kupitia katika maneno ya Mungu, mwanadamu anahukumiwa na kukamilishwa, kisha hatimaye kupelekwa katika ufalme. Maneno ya Mungu tu ndiyo yanayoweza kuyaruzuku maisha ya mwanadamu, na ni maneno ya Mungu tu yanayoweza kumpa mwanadamu mwangaza na njia ya kutenda, hasa katika Enzi ya Ufalme. Alimradi hupotei kutoka katika ukweli wa maneno ya Mungu, kula na kunywa maneno Yake kila siku, Mungu ataweza kukufanya mkamilifu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Enzi ya Ufalme Ni Enzi ya Neno

Iliyotangulia: 5. Kwa Nini Yasemekana Kwamba Kuzijua Awamu Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kujua Mungu?

Inayofuata: 2. Umuhimu wa Kazi ya Mungu ya Kushinda

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp