265 Nitatumikia Maisha Yangu Pamoja na Hukumu na Adhabu ya Mungu

1 Ee Mungu! Upendo wako ni wenye thamani na wa kupendeza; jinsi gani mimi ningetaka kuishi katika mikono ya yule mwovu? Je, mimi sikuumbwa na Wewe? Ningewezaje kuishi chini ya miliki ya Shetani? Ningependa nafsi yangu nzima iishi chini ya adabu Yako. Sitaki kuishi chini ya miliki ya yule mwovu. Kama mimi ninaweza kutakaswa, na ninaweza kutoa yote niliyonayo Kwako, mimi niko tayari kutoa mwili wangu na akili kwa hukumu na adabu Yako, kwa maana mimi nachukizwa na Shetani, na sina nia ya kuishi chini ya uwanja wake. Kupitia hukumu Yako kwangu, umenionyesha tabia Yako ya haki; Nina furaha, na sina malalamiko hata kidogo. Kama mimi nina uwezo wa kutekeleza jukumu la kiumbe, mimi niko tayari kuwa maisha yangu yote yaambatane na hukumu Yako, kwa njia ambayo mimi nitapata kujua tabia Yako ya haki, na kujiondolea ushawishi wa yule mwovu.

2 Hata ingawa ninaishi katika adabu Yako, na huku kukiwa na hukumu Yako, bila kujali ugumu unaohusiana na maisha, bado mimi sina nia ya kuishi chini ya miliki ya Shetani, sina nia ya kuteseka na hila za Shetani. Mimi nina furaha kuishi kwenye laana Yako, na ninapata uchungu kwa kuishi katika baraka za shetani. Nakupenda kwa kuishi katika hukumu Yako, na hii huniletea furaha kuu. Adabu Yako na hukumu ni yenye uadilifu na takatifu; ni vyema ukinitakasa, na hata zaidi kuniokoa. Ninapenda niishi maisha yangu yote katika hukumu Yako na kuwa chini ya uchungaji Wako. Sina nia ya kuishi chini ya mamlaka ya Shetani hata kwa dakika moja; Napenda kutakaswa na Wewe; hata kama ninapitia taabu, sina nia ya kutumiwa na kuhadaiwa na shetani.

3 Mimi, kiumbe hiki, nafaa nitumike na Wewe, nijazwe na Wewe, nihukumiwe na Wewe, na kuadibiwa na Wewe. Nafaa hata nipokee laana kutoka Kwako. Moyo wangu hufurahi wakati Uko tayari kunibariki, kwa maana nimeona upendo Wako. Wewe ni Muumba, na mimi ni kiumbe: Sifai kukusaliti Wewe na kuishi chini ya himaya ya Shetani, wala sifai kutumiwa na Shetani. Mimi nafaa kuwa farasi wako, au ng’ombe, badala ya kuishi kwa ajili ya Shetani. Afadhali niishi katika adabu Yako, bila neema ya kimwili, na hii itanipa raha na starehe hata kama ningepoteza neema Yako. Ingawa neema Yako haiko nami, mimi nafurahia kuadibiwa na kuhukumiwa na Wewe; Hii ndiyo baraka Yako nzuri zaidi, neema Yako kuu.

Iliyotangulia: 264 Siwezi Kumudu Bila Hukumu na Kuadibu kwa Mungu

Inayofuata: 266 Upendo Wa Petro Kwa Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp