Maneno ya Mungu Hufanya Miujiza ya Maisha

26/01/2021

Na Yang Li, Mkoa wa Jiangxi

Mama yangu alifariki nilipokuwa msichana mdogo, na kwa hivyo ilinibidi nibebe mzigo mzito wa majukumu ya kaya kuanzia umri mdogo. Baada ya kufunga ndoa, majukumu yangu yalianza kuwa mazito sana kiasi kwamba sikuweza kupumzika chini ya uzito wao. Baada ya kupata matatizo mengi na taabu nyingi za maisha, polepole nilianza kufadhaika na kuwa mwenye huzuni, mnyamavu na asiyeonyesha hisia kwa urahisi, na nilipoteza wakati siku moja baada ya nyingine. Mnamo mwaka wa 2002, baadhi ya ndugu waliposhiriki nami injili ya kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho, niliipokea kwa furaha na kisha nikaandamana pamoja na mume wangu na watoto kwenda mbele za Mungu. Kuanzia wakati huo kuendelea, mara kwa mara ndugu wangekuja nyumbani kwetu kwa ajili ya mikutano na tungeshirikiana kuhusu neno la Mungu, tuimbe, tucheze na kumsifu Mungu; haya yaliniletea raha ya ajabu na sikuhisi tena mwenye huzuni au wasiwasi. Watoto wangu walisema kwamba nilionekana kuzidi kuwa mchanga na mchangamfu kila wakati. Mara nyingi tulisoma maneno ya Mungu pamoja kama familia na, kupitia maneno Yake, tulikuja kufahamu ukweli mwingi, pamoja na mapenzi ya Mungu ya dharura ya kuwaokoa wanadamu. Nilisafiri kote, nikieneza injili na kushuhudia kwa Mungu ili kulipiza upendo wa Mungu na kuwawezesha wale ambao, kama mimi, wamepitia mateso ya Shetani kuja mbele za Mungu na kuokolewa Naye haraka iwezekanavyo. Sikuwahi kufikiri kwamba, kwa sababu ya haya, ningekuwa mlengwa wa mateso ya kikatili ya serikali ya CCP.

Mnamo tarehe 23 Novemba, mwaka wa 2005 takriban saa moja jioni nilipokuwa kwenye mkutano na dada wawili, ghafla nilisikia mbisho wa nguvu nyingi mlangoni na, nilipogundua kuwa inawezekana kuwa ni polisi, nilikusanya haraka vitabu vyote vya maneno ya Mungu. Kama vile nilivyotarajia, mlango ulipigwa teke haraka sana; maafisa watano wa polisi waliingia ghafla kwa nguvu na kutuzunguka. Afisa mkuu alisema kwa sauti kubwa: “Hakuna kutoroka! Pekueni mahali pote!” Muda si muda, vitu vyote katika nyumba vilikuwa vimeangushwa katika mchafuko usiopendeza. Kisha wakachukua ngawira mifuko yetu yote na kitabu cha nyimbo, na wakatutia pingu mikononi na kutupeleka hadi kwenye kituo cha polisi. Nilishtuka sana baada ya kukumbana na onyesho hili la nguvu na nilimwomba Mungu kwa dhati atulinde. Wakati huo, nilikumbuka kifungu cha maneno ya Mungu: “Unapaswa kujua kwamba vitu vyote vilivyo katika mazingira yanayo wazunguka vipo hapo kwa ruhusa Yangu, Mimi napanga yote. Oneni wazi na muridhishe moyo Wangu katika mazingira Niliyokupa. Msiogope, Mwenyezi Mungu wa majeshi hakika atakuwa pamoja nawe; Yeye anawasaidia na Yeye ni ngao yenu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 26). Maneno ya Mungu yalinipa nguvu na imani kubwa, yakaniondolea woga wangu na kuingiza polepole umakinifu na busara ndani yangu. Hiyo ni kweli! Matukio yote na vitu vyote viko mikononi mwa Mungu na polisi wako chini ya mfumbato na mipango ya Mungu pia. Nikiwa na Mungu kama tegemeo langu thabiti, hakukuwa na chochote cha kuogopa. Nilihitajika tu kulenga kutafuta mapenzi ya Mungu na kumtegemea Mungu ili niweze kuwa shahidi katika hali yoyote ninayoweza kumbana nayo.

Katika kituo cha polisi, maafisa kumi kutoka Ofisi ya Usalama wa Umma ya Manispaa na kituo cha polisi cha eneo hilo walituhoji kwa zamu katika vikundi vya watu wawili. Walitaka kujua majina yetu, anwani zetu na viongozi wa kanisa letu walikuwa kina nani. Tulipokosa kutoa majibu yoyote, kero lao liligeuka kuwa hasira na walitutia pingu kwenye benchi za chuma za mateso. Nilipoona sura katili kwenye nyuso za askari hao woga mdogo uliingia moyoni mwangu; nilijiuliza ni aina gani ya mbinu mbaya ambazo wangetumia kwetu na sikuwa na uhakika ikiwa ningeweza kusimama kidete. Walipoona kwamba sikuwa nikizungumza, afisa mmoja alisema kwa sauti nyororo: “Usiku unakaribia. Tuambie tu jina lako na anwani yako na tutakuruhusu kwenda moja kwa moja hadi nyumbani.” Niliweza kufikiria waziwazi wakati huo kwa sababu nilikuwa na ulinzi wa Mungu, na nikajiwazia, “Hii ni mojawapo ya hila za Shetani. Nikiwapa jina langu na anwani yangu, bila shaka watakwenda na kupekua nyumba yangu, jambo ambalo litaleta madhara makubwa sana kwa kanisa.” Kwa hivyo, bila kujali jinsi polisi hao wabaya walivyonihoji, sikusema lolote, lakini nilimwomba Mungu tu kwamba anipe maneno yanayofaa ya kusema. Siku iliyofuata, walirudi wakiuliza maswali yale yale na tena sikusema lolote. Jioni hiyo, afisa wa kike aliyevalia nguo zisizofaa alikuja, akanikazia macho na kuniuliza kwa ukali, “Jina lako ni nani? Unaishi wapi?” Sikumjibu na kwa hivyo alinifokea kwa hasira: “Ninyi watu hula shibe lenu na kukaa kwa uvivu tu, bila kushughulika kwenda kuchuma pesa yoyote. Kwa nini mnataka kumwamini Mungu fulani?” Kisha, alitembea kwa hatua kubwa akija kwangu na kuanza kupiga miguu yangu na nyaya zangu mateke kwa viatu vyake vyenye visigino virefu huku akifoka, “Kutenda kulingana na imani ni upuuzi! Usiponipa jibu la kweli, nitakuua!” Miguu yangu na nyaya zangu ziliuma kwa namna isiyovumilika na nililemewa na wimbi la udhaifu moyoni mwangu, nisijue wangeweza kunifanyia nini baadaye. Nilimwomba Mungu haraka sana, nikimtaka alinde moyo wangu. Baada ya kumaliza ombi langu, woga wangu ulipungua. Kwa sababu mahojiano yao yalishindwa kutoa majibu yoyote, polisi walitupekeka sote watatu kizuizini.

Usiku huo, kulianguka theluji nzito na kukawa na baridi sana. Maskari hao wakali sana walichukua ngawira nguo zote za majira ya baridi tulizokuwa nazo ndani ya mifuko yetu, wakitulazimisha kuvalia tu safu moja ya nguo laini iliyotuacha tukitetemeka kwa ajili ya baridi safari hiyo nzima. Tulipofika kizuizini, walitupeleka katika chumba cha gereza la chini lenye giza na la kutisha. Wakati mwingine sauti za matusi na vilio vya wafungwa wengine zilienea chini, zakinitisha sana—nilihisi kana kwamba nilikuwa nimeingia katika aina fulani ya jehanamu hapa duniani. Sote watatu tulisukumwa ndani ya seli lenye wafungwa wengine takriban ishirini, ambako wimbi baada ya wimbi la uvundo wenye harufu ya uozo lilitokea. Seli hiyo ilikuwa imejazwa pande zote na majukwaa ya kulala ya saruji na wafungwa wote waliketi kandokando ya meza ndefu wakipenyeza nyaya za balbu. Mara tu tulipoingia, afisa alimwambia mfungwa mkuu: “Hakikisha unawakaribisha vizuri!” Mfungwa mkuu, mfungwa wa dawa za kulevya, hakuwa hata amefikisha umri wa miaka thelathini; mara tu aliposikia maagizo ya afisa, aliniangusha sakafuni kwa kunipiga teke la kikatili kabla hata sijayajua mazingira yangu. Iliuma sana kiasi kwamba niligaagaa sakafuni nikipiga mayowe. Baada ya hapo, walirarua mavazi yetu yote, wakatuvuta kwa nguvu hadi bafuni na kutulazimisha kuoga kwa maji baridi. Maji baridi sana yaliyoumiza yalinifanya kupatwa na mutukutiko wa maungo na meno yangu yalikereza bila kukoma. Mwili wangu wote ulikuwa katika maumivu yasiyovumilika kana kwamba nilikuwa nimekatwa kwa kisu na nilipoteza fahamu haraka sana. Nilipopata fahamu tena, niligundua kuwa tayari nilikuwa nimerudishwa kwenye seli. Mfungwa mkuu alipoona kwamba nilikuwa macho, bado hakupunguza ukali kwangu, lakini aliendelea kunipiga mateke na kunipiga makonde. Ni baada tu ya kuchoshwa mwenyewe ndipo alinitupa kando. Hao dada wangu wawili walikuja na kunishikilia kwa karibu, machozi yao yakitiririka usoni mwangu. Nikisikia dhaifu sana moyoni mwangu, nilijiwazia: “Je, mbona Mungu asiniachie nife? Mara tu nitakapokufa, nitakuwa huru, lakini nikiendelea kuishi, ni nani anayejua jinsi mapepo hao watanipiga na kunitesa, na ikiwa nitaweza kustahimili yote au la.” Kadiri niilivyofikiria zaidi juu ya jambo hilo ndivyo nilivyozidi kuhuzunishwa, na machozi yalikuwa yakitiririka usoni mwangu. Katikati ya mateso yangu, Mungu alinipa nuru ili nifikirie wimbo wa maneno Yake: “Chini ya mwongozo wa mwangaza Wangu, mtapenya katika utawala wa nguvu za giza. Hakika, katikati ya giza, hamtaupoteza mwangaza unaowaongoza. … Hakika mtasimama imara na thabiti katika nchi ya Sinimu. Kupitia katika mateso mnayoyavumilia, mtarithi baraka zinazotoka Kwangu, hakika mtaonyesha utukufu Wangu katika ulimwengu mzima(“Wimbo wa Washindani” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Moyo wangu ulijawa na uchangamfu mara moja—ahadi ya Mungu na upendo Wake ulinigusa sana, vikaniwezesha kugundua kuwa, hata ingawa Shetani alikuwa akinitesa kwa ukatili wake, ilimradi tu nimtegemee Mungu kwa dhati na kumheshimu, kwa hakika Mungu angeniongoza kushinda ukandamizaji wa nguvu za giza na kuingia katika nuru. Mateso niliyokuwa nikipitia yalikuwa ya thamani na yenye maana; yalikuwa baraka kutoka kwa Mungu, na yalikuwa mateso niliyohitaji kupitia katika harakati ya kufuatilia ukweli na kupata wokovu wa Mungu. Yalikuwa pia ushuhuda thabiti wa ushindi wa Mungu dhidi ya Shetani. Shetani alikuwa akiniumiza vibaya na kunitesa ili kujaribu kunifanya nimkane na kumsaliti Mungu; ni kwa kubaki thabiti katika kujitolea kwangu kwa Mungu, kuvumilia mateso yote ambayo nilipaswa kuvumilia na kuwa shahidi kwa Mungu ndivyo tu ningeweza kulipiza kisasi kwa njama ya Shetani, kumdhalilisha Shetani ili kuleta utukufu kwa Mungu. Punde nilipofikiria haya yote, nilitubu sana kwa Mungu na kufanya azimio: “Ee Mungu Mwenyezi! Umeteseka zaidi kuliko mtu yeyote wa kawaida angeweza kuvumilia ili kutuletea wokovu, sisi watu wapotovu sana. Umefanya juhudi kubwa sana kwa ajili yetu na upendo Wako kwetu kweli ni mkubwa sana! Ninapaswa kulipiza upendo Wako, lakini leo, wakati ninakabiliwa na majaribu, wakati nilipaswa kuwa na ushuhuda mbele ya Shetani, nilichagua kutoroka. Wakati niliteseka kidogo tu katika mwili, nilianza kuwa hasi na nikapinga, nikitamani tu kufa na hatimaye kumalizana na yote. Mimi ni mwoga na mwenye upungufu wa dhamiri kaisi gani! Kuanzia sasa kuendelea, bila kujali nitakabili hali gani mbaya, ninaahidi kuwa shahidi Kwako.” Nilihisi imani yangu ikiimarika wakati huo na niliushika mkono wa dada yangu kwa uthabiti, nikiwa tayari kuendelea kuishi ili kuwa shahidi kwa Mungu.

Baada ya kuzuiliwa kizuizini kwa muda wa siku ishirini na moja, polisi walinipeleka katika Ofisi ya Usalama wa Umma ya Kaunti. Walinifunga kwa ugwe kwenye benchi ya mateso na kunihoji. Kwa sababu nilikataa katakata kusema lolote, usiku huo walinitia pingu mikonoi kwa pingu zilizopigiliwa misumari na kunining’iniza kutoka kwa kiunzi cha nondo cha chuma cha dirisha, na kuacha mwili wangu ukining'inia hewani ili niweze kugusa chini kwa ncha za vidole tu. Afisa alinizungumzia kwa kiburi, akisema, “Ikiwa kuna jambo moja ambalo ninalo, ni stahamala. Nitakufanya unisihi na uniambie kiongozi wako ni nani kwa hiari yako mwenyewe!” Kisha, akatoka chumbani, akifunga mlango kwa kishindo alipokuwa akiondoka. Muda si muda, nilianza kuhisi maumivu makali sana kwenye vifundo vya mikono yangu ambayo yaliniacha nikiteseka isivyoelezeka. Wakati huo, ghafla niliwaza kuhusu wimbo wa maneno ya Mungu: “Mmewahi kuzikubali baraka mlizopewa? Mmewahi kuzitafuta ahadi mlizofanyiwa? Hakika, chini ya mwongozo wa mwangaza Wangu, mtapenya katika utawala wa nguvu za giza. Hakika, katikati ya giza, hamtaupoteza mwangaza unaowaongoza. Hakika mtakuwa bwana wa viumbe vyote. Hakika mtakuwa washindi mbele ya Shetani. Hakika, wakati wa maangamizi ya ufalme wa joka kubwa jekundu, mtasimama miongoni mwa umati mkubwa kushuhudia ushindi Wangu. Hakika mtasimama imara na thabiti katika nchi ya Sinimu. Kupitia katika mateso mnayoyavumilia, mtarithi baraka zinazotoka Kwangu, hakika mtaonyesha utukufu Wangu katika ulimwengu mzima(“Wimbo wa Washindani” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Nikiwa na machozi machoni mwangu, niliimba wimbo huo tena na tena. Kadiri nilivyoimba, ndivyo nilivyozidi kuchangamshwa na niliweza kuhisi nishati ya uhai ya maneno ya Mungu ambayo iliimarisha moyo wangu na kunipa imani madhubuti kwamba hakika Mungu ataniongoza kushinda ukandamizaji wa nguvu za giza, na kunisaidia kuvumilia mateso haya yote ya kikatili ili kusimama kidete katika ushahidi wangu. Baada ya kutiwa moyo na maneno ya Mungu, maumivu yangu ya mwili yalitoweka na kwa kweli nilihisi mimi mwenyewe nikimkaribia Mungu na kuwa karibu zaidi na Mungu. Nilihisi kana kwamba Mungu alikuwa kando yangu, Akiandamana nami. Maneno Yake yaliugusa moyo wangu na niliazimia kwamba nitakuwa shahidi ili kumridhisha Mungu na kamwe sitajisalimisha kwa Shetani!

Baada ya hapo, nilipelekwa katika chumba cha mahojiano ambapo kitu cha kwanza kilichoonekana kilikuwa seti nzima ya vifaa tofauti vya mateso: Virungu vikubwa na vidogo vya polisi vilikuwa vikining’inia katika safu kwenye ukuta, na karibu na ukuta palikuwa virungu vya ngozi, mijeledi ya ngozi na benchi ya mateso. Maafisa wachache walikuwa katikati ya kumpiga mfungwa wa kiume mwenye umri wa miaka ishirini na kitu kwa kutumia virungu vya umeme na mijeledi ya ngozi. Alikuwa amekatwa na kuvilizwa vibaya na alikuwa amelemazwa kwa kiwango asichoweza kutambuliwa. Afisa wa kike aliingia wakati huo tu na bila kusema lolote, alinipiga mateke mara kadhaa kabla ya kunivuta nywele kwa nguvu na kukigongesha kichwa changu ukutani, jambo ambao lilitoa sauti ya mshindo mbaya. Nilipatwa na kizunguzungu, nikahisi kisulisuli na kichwa changu kiliuma sana kiasi kwamba nilidhani kingepasuka. Alipokuwa akinipiga, alisema kwa karipio bovu: “Usiposema ukweli leo, nitahakikisha kwamba hutaishi kuona siku nyingine!” Maafisa wengine wawili wa kiume waliongezea kwa kelele, wakitishia: “Tumewaita maafisa kutoka vituo vyote vya polisi vilivyo karibu. Tuna wakati mwingi sana wa kukuhoji, mwezi mmoja, miezi miwili…. Muda wowote utakaohitajika kupata majibu tunayotaka kutoka kwako.” Niliposikia wakisema hayo, pamoja na kuwaza kuhusu mbinu za kikatili ambazo wahalifu hao walikuwa wametumia kwangu hapo awali na tukio ambalo lilikuwa limetokea karibuni kwa yule mfungwa wa kiume, moyo wangu ulianza kupiga kwa kasi na nilijawa na wimbi baada ya wimbi la woga na hofu. Nilichoweza tu kufanya ni kumwomba Mungu haraka. Katika wakati huo, maneno ya Mungu yaliniongoza, “Watu wanapokuwa tayari kuyatoa maisha yao, kila kitu huwa hafifu, na hakuna anayeweza kuwashinda. Ni nini kingekuwa muhimu zaidi kuliko uzima? Hivyo, Shetani anakuwa hawezi kufanya chochote zaidi ndani ya watu, hakuna anachoweza kufanya na mwanadamu. Ingawa, katika ufafanuzi wa ‘mwili’ inasemekana kwamba mwili hupotoshwa na Shetani, kama watu watajitoa kweli, na wasiendeshwe na Shetani, basi hakuna anayeweza kuwashinda—na wakati huu, mwili utatekeleza kazi yake nyingine, na kuanza kupokea rasmi mwongozo wa Roho wa Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufafanuzi wa Mafumbo ya “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima”, Sura ya 36). Maneno ya Mungu yalinipa njia ya utendaji. Nilifikiria, “Kweli, Shetani ametumia udhaifu huu wangu, woga wangu wa kifo, ili anifanye nimsaliti Mungu, na Mungu anatumia hali hii kujaribu uaminifu wa imani yangu Kwake. Nikifikiria hili vizuri, maisha yangu yamo mikononi mwa Mungu, kwa hivyo mbona nimwogope Shetani? Sasa ni wakati wangu wa kuwa shahidi kwa Mungu; ni kwa kutoa maisha yangu tu na siyo kuzuiliwa na kifo ndivyo ninavyoweza kutoroka ushawishi wa Shetani na kuwa shahidi kwa Mungu.” Baada ya kufikiria jambo hili, sikuogopa kifo tena na niliamua kutoamaisha yangu ili kumridhisha Mungu. Wakati polisi mmoja mwovu aliona kwamba sikuwa naogopa, alifoka kwa ghadhabu, “Tusipokuadhibu sasa kama onyo, utadhani kuwa hatujui cha kukufanyia!” na kisha mara moja walinitia pingu mikononi kwa pingu zilizopigiliwa misumari, wakanining’iniza kwenye kiunzi cha nondo cha chuma cha dirisha, na kuanza kunidukua kwa kirungu cha umeme. Mkondo mkali wa umeme uliingia mwilini mwangu mwote mara moja, ukinisababisha nitetemeke na kusukasuka bila kukoma. Kadiri nilivyong’ang’ana zaidi, ndivyo pingu zilibana zaidi vifundo vya mikono yangu; ziliumiza sana kiasi kwamba nilidhani mikono yangu ilikuwa karibu kung’okaanguka na mwili wangu wote uliteseka sana kwa maumivu makali. Polisi hao wawili waovu waliendelea kuchukua zamu kunitesa kwa virungu ambavyo vilichakarika kila mara. Kila nilipopitishiwa shoti za umeme, mwili wangu wote ulipatwa na mkazo wa ghafla wa misuli na kutetemeka na polepole nilianza kufa ganzi. Taratibu, nilianza kupoteza fahamu na mwishowe, nilizirai. Wakati fulani baadaye, sijui ni baada ya muda gani, niliamshwa na baridi. Kikundi hicho cha maafisa waovu, walipoona kwamba nilikuwa nimevalia mavazi laini tu, walikuwa wamefungua madirisha yote makusudi ili kunigandisha. Upepo baridi ulikuwa ukivuma wakati wote kutoka dirishani; nilikuwa nahisi baridi sana hivi kwamba mwili wangu ulikuwa wenye mavune na niliweza kujihisi nikipoteza fahamu tena, lakini hapo hapo niliweza kufiria waziwazi: “Siwezi kufa moyo. Lazima nikuwe shahidi kwa Mungu hata ikiwa itamaanisha nife!” Wakati huo huo, nilimwonara Bwana Yesu akisulubiwa akilini mwangu ili kuwaokoa wanadamu: Bwana Yesu alipigwa sana na kisha akapigiliwa msumari msalabani ili kuhitimisha kazi ya ukombozi wa wanadamu. Ikiwa Mungu angeweza kutoa maisha Yake ili kuwaokoa wanadamu, kwa nini mimi singeweza kulipiza kidogo tu upendo wa Mungu? Upendo wa Mungu ulinitia moyo na nikamwomba Mungu: “Ee Mungu! Umenipa maisha haya ninayoishi, kwa hivyo ikiwa ungetaka kuyachukua, nimejisalimisha kwa hiari. Itakuwa fahari na heshima yangu kubwa kufa kwa ajili Yako!” Kisha nikapata fahamu kamili polepole. Nikifikiria jinsi Peter, Stefano na wanafunzi wengine walivyokufa katika mateso ya kishahidi, sikuweza kujizuia kuimba kimoyomoyo wimbo huu wa kanisa ambao niliufahamu vizuri: “Kwa mpango Wake mtakatifu na enzi kuu, ninakabiliwa na majaribu yaliyokusudiwa kwangu. Ninawezaje kufa moyo au kujaribu kuficha? Kitu cha kwanza ni utukufu wa Mungu. Wakati wa shida, maneno ya Mungu yananiongoza na imani yangu inakamilishwa. Nimejitoa kabisa na kikamilifu, kujitoa kwa Mungu bila hofu ya kifo. Mapenzi Yake daima yako juu ya yote. Bila kujali mustakabali wangu, bila kufikiria faida au hasara, Natamani tu Mungu aridhike. Nashuhudia ushuhuda mkubwa sana na kumwaibisha Shetani kwa ajili ya utukufu wa Mungu. Naahidi kabisa kulipa upendo wa Mungu. Namsifu bila pingamizi moyoni mwangu. Nimeona Jua la haki, ukweli unadhibiti vitu vyote vilivyo duniani. Tabia ya Mungu ni ya haki (na inastahili sifa za wanadamu). Moyo wangu utampenda Mwenyezi Mungu milele, na nitaliinua jina Lake juu” (“Ninaomba tu Kwamba Mungu Aridhike” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Kadiri nilivyoimba, ndivyo nilivyozidi kuguswa na kutiwa moyo na nikawa na sauti ya kwikwi. Niliweza kumhisi Mungu akiwa kando yangu, Akisikiliza kwa makini nilipokuwa nikizungumza naye kwa siri. Nilikuwa na hisia za uchangamfu moyoni mwangu na nilijua kuwa Mungu alikuwa akinisaidia wakati huu wote kwa mkono Wake wenye nguvu ili nisiogope baridi au kuogopa kifo changu mwenyewe. Moyoni mwangu, nilifanya azimio lifuatalo: Bila kujali ni aina gani za mateso au taabu zinanisubiri, ninaapa kwa maisha yangu kusalia mwaminifu hadi mwisho kabisa na kuwa shahidi ili kulipiza upendo wa Mungu!

Asubuhi ya siku iliyofuata, polisi mmoja alinitishia kwa nguvu, akisema, “Una bahati hukuganda hadi kufa jana usiku, lakini usipozungumza leo, nitahakikisha Mungu wako hataweza kukuokoa!” Nilijichekea mwenyewe, bila kushtuka. Niliwaza “Mungu ndiye Muumba wa mbingu na nchi na vitu vyote, Anatawala kila kitu, ni muweza na amejawa mamlaka. ‘Maana alizungumza na ikawa. Aliamuru na ikasimama imara.’ Maisha yangu pia yamo mikononi mwa Mungu; ikiwa Angetaka kuniokoa sasa, je, halingekuwa jambo rahisi zaidi Kwake? Ni vile tu anataka kukutumia, wewe pepo, kumtumikia.” Wakati huo, yule polisi mwovu alinidukua tena kwa kirungu chake cha umeme na mkondo mkali wa umeme uliingia mwilini mwangu mwote, ukisababisha maumivu makubwa ambayo yalinifanya ning’ang’ane na kulia bila hiari. Polisi huyo alicheka tu kwakwakwa na kusema: “Endelea, piga mayowe! Mwite Mungu wako akuokoe! Ukinisihi nikuokoe, nakuahidi nitakuruhusu uondoke!” Kusikia ufidhuli wa kuchukiza wa maneno ya afisa huyo kulinijaza chuki ya muda mrefu sana na nilimwomba Mungu kimoyomoyo: “Ee Mungu! Ibilisi Shetani ni katili kiasi gani! Anakukashifu na kukukufuru; ni adui Wako asiyeweza kupatanishwa na hasa ni adui wangu wa jadi. Bila kujali jinsi Shetani atakavyonitesa, sitakusaliti. Ningependa tu moyo wangu upatwe Nawe. Pepo hawa wanaweza kuumiza mwili wangu, lakini kamwe hawawezi kuangamiza azimio langu la kukuridhisha. Ningependa unipe nguvu.” Askari huyo katili na mkali sana alinidukua kwa kirungu chake cha umeme bila huruma; kirungu cha umeme cha kwanza kilipoisha batri, alibadilisha kwa kingine kipya na akaendelea kunidukua. Nimepoteza hesabu ya virungu alivyovitumia kwa jumla. Nilihisi kwamba kifo kilikuwa kikinikaribia na kwamba hakukuwa tumaini la kuishi. Nikiwa nimejawa uhasi na kufa moyo, nilichoweza kufanya tu ni kumwomba Mungu bila matumaini, nikimsihi anilinde na kuniokoa. Wakati huo, nilikumbuka kifungu cha neno la Mungu: “Nguvu za Mungu za maisha zinaweza kutawala juu ya nguvu zozote; zaidi ya hayo, inazidi mamlaka yoyote. Maisha Yake ni ya milele, nguvu zake za ajabu, na nguvu Zake za maisha haziwezi kuzidiwa na kiumbe yeyote au nguvu za adui. Nguvu za maisha ya Mungu zipo, na hung’aa mwangaza wake ulio mzuri sana, bila ya kujali muda au mahali. Mbingu na dunia zinaweza kupitia mabadiliko makubwa, lakini uzima wa Mungu ni ule ule daima. Mambo yote hupita, lakini maisha ya Mungu hubaki, kwa maana Mungu ni chanzo cha kuwepo kwa mambo yote, na mizizi ya kuwepo kwao(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele). Maneno ya Mungu yalinijaza nguvu isiyo na mpaka na mara moja yakanipa imani yenye nguvu sana katikati ya udhaifu wangu. Nilijiwazia: “Ndiyo, ninamwamini Mwenyezi Mungu mmoja na wa pekee. Nishati ya uhai ya Mungu ni ya milele na yasiyo ya ulimwengu, na nguvu ya maisha ya Mungu inavuka mipaka ya vitu vyote na inashinda yote. Yote yaliyoko yamekuwa kupitia maneno ya Mungu. Vipengele vyote vya mwanadamu, yakiwemomaisha na kifo chake yako chini ya maamuzi ya Mungu. Maisha yangu, hata zaidi, yako mikononi mwa Mungu na kwa hivyo Shetani anawezaje kudhibiti hali yangu ya kuweza kufa? Kwa mfano, fikiria jinsi Bwana Yesu alivyomwita Lazaro, ambaye mwili wake ulikuwa tayari umeanza kuoza katika kaburi lake, akisema, “Lazaro, kuja nje(Yohana 11:43) naye Lazaro alitoka kaburini, akafufuka kutoka kwa wafu. Maneno ya Mungu yana mamlaka na uwezo; Aliumba ulimwengu kwa maneno Yake na Yeye hutumia maneno Yake kuongoza kila kizazi. Leo, Mungu anatumia maneno Yake kutuokoa na kutukamilisha. Sipaswi tena kutafsiri mambo kulingana na maoni na mawazo yangu, lakini lazima niishi kulingana na maneno ya Mungu. Leo, ikiwa Mungu hataniruhusu nife, bila kujali Shetani anatenda kikatili jinsi gani, hawezi kuchukua maisha yangu. Ilimradi tu ninaweza kumletea Mungu heshima, nitakufa kwa furaha na kwa hiari.” Mara tu nilipoanza kuishi kulingana na maneno ya Mungu na kuacha kuwa na wasiwasi kuhusu hali yangu mwenyewe ya kufa, muujiza ulifanyika: Bila kujali polisi huyo mwovu alinidukua jinsi gani, sikuhisi tena taabu yoyote au maumivu yoyote na niliweza kufikiria waziwazi. Nilikuwa na uhakika kuwa huu ulikuwa ulinzi wa Mungu na utunzaji Wake—ulikuwa mkono wa Mungu wenye uwezo ukinisaidia. Kweli nilijionea mwenyewe uwezo wa kustaajibisha wa maneno ya Mungu, na vile vile asili ya nishati ya uhai ya Mungu isiyo ya ulimwengu na ya pekee. Maneno ya Mungu ni ukweli na uhalisi wa maisha. Nishati Yake ya uhai haiwezi kukandamizwa na nguvu yoyote ya giza. Bila kujali jinsi polisi walivyonitesa kwa kila aina ya mateso na ukatili, wakichukua zamu kunipa adhabu yao ya kikatili, niliweza kuvumilia hayo yote. Huo haukuwa uwezo wangu mwenyewe, bali wote ulikuwa nguvu na mamlaka ya Mungu. Isingalikuwa maneno ya Mungu kunipa nguvu na imani, ningalikufa moyo muda mrefu uliopita. Nilikuwa na utambuzi wa kina kwamba, mwili wangu ulipokuwa dhaifu zaidi na nilikuwa nimetumbukia katika lindi la taabu, Mungu alikuwa kando yangu kila wakati, akinihimili kwa maneno Yake ya maisha yaliyo thabiti na yenye uwezo, na akinilinda kila wakati, ili imani yangu iwe thabiti zaidi ndani yangu na azimio langu liimarike.

Usiku huo, walitumia mbinu tofauti ya mateso kwangu. Walinitia pingu mikononi mbele ya dirisha, wakiniweka wazi kwa hewa baridi ya nje na kisha walinilinda kwa zamu ili kuhakikisha kuwa sikulala. Mara tu macho yangu yangeanza kufifia, wangenizaba makofi usoni. Sikuwa nimekunywa hata tone moja la maji au kula funda la chakula kwa muda wa siku mbili, mwili wangu wote haukuwa na nguvu, na macho yangu yalikuwa yamevimba sana kiasi kwamba nilishindwa kuyafungua. Nilihisi nimejawa na aina fulani ya taabu isiyoelezeka na nilijiuliza mateso hayo yangeendelea kwa muda gani zaidi. Upepo mkali baridi ulivuma kwangu bila kukoma na nilitetemeka kila wakati kwa ajili ya baridi. Polisi, wakiwa wamevalia koti aina ya anoraki zilizofika magotini, walikaa kimarufaa kwenye viti mbele yangu, wakisubiri kujisalimisha kwangu. Wakati huo, ulikuwa ni kana kwamba onyesho la pepo wakimtesa mtu kuzimuni lilikuwa likichezwa mbele yangu, na sikuweza kuzuia hasira yangu: Mwanadamu aliumbwa na Mungu na ni kawaida na haki amwabudu, lakini serikali ya CCP iliyo duni, na isiyo na haya haiwaruhusu watu kumwabudu Mungu wa kweli. Ili kuanzisha ukanda wa ukanaji wa Mungu katika ulimwengu na kufikia lengo lao mbovu la kuwadhibiti watu bila kukoma na kuwafanya wafuate na kuwaabudu wao, wanapinga vikali, kuvuruga na kuharibu kazi ya Mungu, wakitumia kila mbinu ya kudharauliwa chini ya mamlaka yao kuwatesa kikatili wafuasi wa Mwenyezi Mungu. Pepo huyo mzee amefanya makosa makubwa zaidi—anapaswa kulaaniwa na kuhukumiwa! Ghafla, wimbo wa maneno ya Mungu ulinijia akilini, “Kwa maelfu ya miaka hii imekuwa ni nchi ya uchafu, ni chafu sana, shida zimejaa, mizimu wanakimbia kila mahali, wakihadaa na kudanganya, wakitoa tuhuma zisizokuwa na msingi,[1] wakiwa katili na waovu, wakikandamiza mji huu ulio mahame na kuuacha ukiwa umetapakaa maiti; harufu ya uozo inaijaza nchi na kuenea hewani, na inalindwa isivyo kawaida.[2] Nani awezaye kuuona ulimwengu kupita anga? Inawezekanaje watu wa mji wa mahame kama huu wawe wamewahi kumwona Mungu? Je, wamekwishawahi kufurahia uzuri na upendo wa Mungu? … Kwa nini uweke kikwazo hicho kisichopenyeka katika kazi ya Mungu? Kwa nini utumie hila mbalimbali kuwadanganya watu wa Mungu? Uhuru wa kweli na haki na matakwa halali vipo wapi? Usawa uko wapi? Faraja iko wapi? Wema upo wapi? Kwa nini utumie mbinu za hila kuwadanganya watu wa Mungu? Kwa nini utumie nguvu kukandamiza ujio wa Mungu? Kwa nini umsumbue Mungu hadi Anakosa sehemu ya kupumzisha kichwa Chake? hii inawezaje kukosa kuamsha hasira? Maelfu ya miaka ya chuki ikiwa imejaa kifuani, milenia ya dhambi imeandikwa katika moyo—inawezekanaje hii isichochee chuki? Kumlipiza Mungu, kuuondoa kabisa uadui wake, Sasa ndio wakati: Mwanadamu ana muda mrefu tangu akusanye nguvu zake zote, amejitolea nguvu zake zote, amelipa kila gharama, kwa hili, kuchana uso uliojificha wa pepo hili na kuwafanya watu, ambao wamepofushwa na kuvumilia kila aina ya mateso na taabu, kuinuka kutoka katika maumivu na kurudi kwa ibilisi huyu wa zamani(“Walio Gizani Wanapaswa Kuinuka” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Niliimba wimbo huo tena na tena moyoni mwangu. Nilipokuwa nikiimba, nilikasirika sana na ghadhabu kali ikaibuka ndani yangu; niliapa kwa maisha yangu kumwacha Shetani, pepo huyo mzee, na nikasema kwa huzuni moyoni mwangu: “Wewe pepo! Ikiwa unafikiri kwamba nitamsaliti Mungu na kuiacha njia ya kweli, umekosea, fikiria tena!” Nilifahamu fika kuwa ni Mungu aliyekuwa amenipa nguvu, kwamba maneno ya Mwenyezi Mungu yalikuwa yametegemeza roho yangu.

Siku ya tano, mikono yangu ilikuwa imejaa damu kwa wingi, yenye ganzi na kuvimba sana vibaya kwa sababu ya pingu. Nilihisi kana kama mwili wangu ulikuwa katika hali mbaya sana, kwamba maelfu ya wadudu walikuwa wakinila kutoka ndani kuelekea nje. Hakuna maneno ya kuelezea maumivu na masumbuko hayo makali. Nilisali bila kukoma moyoni mwangu, nikimsihi Mungu anipe nguvu ya kushinda udhaifu wa mwili wangu. Muda ulipita polepole sana na taratibu, usiku ulianza kuingia. Nilikuwa mwenye kiu na njaa, nilikuwa nikihisi baridi na kutetemeka kote, na nilikuwa nimechoshwa na nishati yangu iliyokuwa imebaki ilikwisha—nilihisi kuwa sitaweza kuvumilia kwa muda mrefu zaidi. Ikiwa haya yangeendelea kwa muda mrefu zaidi, hakika ningekufa kwa ajili ya njaa au kiu. Ni wakati huo tu ndipo nilielewa kile afisa mwovu alikuwa amemaanisha aliposema, “Nitakufanya unisihi.” Alikuwa akijaribu kutumia mbinu zake za kudharauliwa ili anilazimishe nimsaliti Mungu. Singenaswa na ujanja wake; ilinibidi nimtegemee Mungu. Kwa hivyo, nilimwomba Mungu tena na tena: “Ee Mwenyezi Mungu! Ninaomba unipe nguvu, ili niweze kukutegemea kushinda adhabu na mateso ya kikatili ya Shetani. Hata ikiwa itamaanisha kifo changu, sipaswi kukusaliti na kuwa Yuda.” Wakati huo, maneno ya Mungu yalinipa nuru: “Asili ya maisha ya mwanadamu hutoka kwa Mungu, kuwepo kwa mbingu ni kwa sababu ya Mungu, na kuwepo kwa ardhi kunatokana na nguvu ya uhai wa Mungu. Hakuna kitu kinachomiliki nguvu kinachoweza kuzidi ukuu wa Mungu, na hakuna kitu chenye nguvu kinachoweza kuvunja mipaka ya mamlaka ya Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele). Maneno ya Mungu yenye mamlaka yalinipa imani na nguvu. “Ni kweli,” nilijiwazia, “Mungu ndiye chanzo cha maisha yangu: ilimradi Mungu hajaondoa pumzi hii kwangu, bila kujali jinsi Shetani anavyonitesa na kutoniruhusu kula au kunywa, bado sitakufa. Maisha yangu yamo mikononi mwa Mungu, kwa hivyo nina nini cha kuogopa?” Wakati huo niliona haya na kuaibika kwa ajili ya ukosefu wangu wa imani katika Mungu na ufahamu wa Mungu. Niligundua pia kuwa Mungu alikuwa akitumia hali hii ngumu kunifunza kidogo kidogo ukweli ufuatao: “Mwanadamu hatadumu kwa mkate pekee, lakini kwa kila neno linalotoka kinywani mwa Mungu(Mathayo 4:4). Kwa hivyo nilimwomba Mungu: “Mwenyezi Mungu, Mtawala wa yote! Maisha yangu yako mikononi Mwako kusimamia na niko tayari kutii mipango na utaratibu wako. Bila kujali iwapo nitaishi au kufa, nitakubali mipango Yako yote.” Baada ya kumaliza maombi yangu, nilihisi mwili wangu ukiwa umejawa nguvu na sikuhisi njaa au kiu kama nilivyokuwa nimehisi. Ilipofika saa mbili usiku huyo askari mwovu alirudi. Alifinya kidevu changu na kwa tabasamu mbovu, aliniambia, “Kwa hivyo unaendeleaje, unafurahia? Uko tayari kunisihi na kuniambia ninachotaka kukijua? Usipozungumza, nina njia nyingi za kukushughulikia!” Nilifunga macho yangu na kumpuuza, na jambo hili lilimfanya aghadhabike—alinitupia matusi na maneno machafu alipokuwa akinikamata kwa nguvu kwenye kola kwa mkono mmoja na kunizaba makofi vibaya pande zote za uso wangu kwa mkono huo mwingine. Niliweza kuuhisi uso wangu ukivimba ghafla, na uliuma kwa ajili ya maumivu. Ukatili wa polisi huyo mwovu uliniwezesha nitambue waziwazi asili yake ya kishetani; nilimchukia hata zaidi na nilihisi hata zaidi kutojisalimisha kwa udhalimu wa Shetani. Nilikuwa imara katika azimio langu la kuwa shahidi kwa Mungu na kumridhisha. Wakati huo, sikujali tena maumivu yangu ya mwili, lakini nilimkazia macho huyo polisi kwa hasira, nikijiwazia, “Unadhani kuwa unaweza kunilazimisha nimsaliti Mungu? Acha kuota!” Nikiwa na mwongozo wa Mungu, moyo wangu ulijawa imani na nguvu; bila kujali jinsi afisa huyo alivyonipiga, sikuwahi kukubali kumpa alichotaka. Mwishowe, ni baada tu ya afisa huyo kujichosha kabisa ndipo hatimaye alikoma.

Baada ya hapo, polisi hao walidumisha ulinzi mkali hata zaidi kwangu. Walifanya kazi kwa zamu, wakinichunga wakati wote na ikiwa macho yangu yangeanza kufifia hata kidogo, wangenipiga ili kuniamsha kwa kutumia gazeti lililokunjwa. Nilielewa waziwazi kuwa walikuwa wakiyafanya haya ili kudhoofisha azimio langu na kutumia hali yangu ya kiakili iliyokuwa imedhoofishwa ili kupata habari kuhusu kanisa. Wakati huo, nilikuwa tayari dhaifu sana kimwili na nilikuwa nimeanza kuchanganyikiwa. Mchanganyiko wa baridi, njaa na uchovu ulizidi sana kiasi kwamba nilitamani kifo. Nilihisi kana kwamba singeweza kuvumilia kwa muda mrefu zaidi; niiliogopa kwamba singeweza kuvumilia maumivu na kuwa ningemsaliti Mungu bila kukusudia. Nikiwa na wazo hili, nilitamani kifo, nikidhani kwamba angalau ikiwa ningekufa, singelisaliti kanisa na kumsaliti Mungu. Kwa hivyo nilimwomba Mungu: “Mungu wangu, siwezi kustahimili kwa muda mrefu zaidi. Ninaogopa kwamba nitakubali kushindwa na kukusaliti. Ninaomba Uulinde moyo wangu. Afadhali nife kuliko kuwa Yuda.” Baada ya hapo, nilianza kupoteza fahamu polepole, na katika hali hiyo ya kutunduwazwa ghafla mwili wangu ulihisi mwepesi, kana kwamba upepo baridi ulikuwa umeupuliza na kuukausha. Pingu zilihisi kulegea katika vifundo vya mikono yangu na singeweza kujua ikiwa nilikuwa hai au mfu. Asubuhi mapema ya siku ya sita ndipo nilizabwa kofi na afisa mmoja hadi nikapata fahamu; niligundua kuwa bado ningali hai na bado nilikuwa nikining’inia hapo kwa pingu zangu. Polisi huyo mwovu alinifokea: “Umetuchosha kweli. Hakuna hata mmoja wetu ambaye amelala unono, tukiandamana nawe kwenye mchezo huu mdogo wakati huu wote. Usipozungumza leo, nitahakikisha kwamba hutawahi kuzungumza tena!” Kwa kuwa kile nilichotaka tu kilikuwa kufa, nilimjibu kwa hasira bila woga: “Ikiwa unataka kuniua au kunikatakata vipande vipande, endelea!” Hata hivyo, polisi huyo mwovu alicheka kwa dharau tu na kusema: “Kwa hivyo unataka kufa? Hilo halitatendeka! Hilo litakurahishia mambo sana! Nitakutesa vibaya na polepole mpaka urukwe na akili, ili kila mtu ajue kuwa kumwamini Mwenyezi Mungu kutamfanya arukwe na akili, na kisha kila mtu atamuacha Mungu wako!” Nilipomsikia akiropoka najisi hii ya kishetani, nilishikwa na bumbuazi na kuduwaa kabisa: Shetani huyu alikuwa mkatili na mbaya sana! Mara tu baada ya hapo, askari huyo mwovu alimwamuru mdogo wake alete bakuli lenye majimaji meusi. Nilijawa na hofu nilipoliona na nikamwomba Mungu kwa dharura: “Ewe Mwenyezi Mungu! Polisi huyu mwovu anakaribia kuninywesha dawa ya kulevya ili kunifanya nirukwe na akili. Ninakusihi unilinde. Afadhali nilishwe sumu hadi kufa kuliko kutiwa wazimu.” Wakati huo, maneno ya Mungu yaliingia polepole akilini mwangu: “Matendo Yake yamo kila mahali, nguvu Zake ziko kila mahali, busara Zake ziko kila mahali na mamlaka Yake yako kila mahali. … Kila kitu kinaishi chini ya uangalizi Wake, zaidi ya hayo, kila kitu huishi chini ya ukuu Wake. Matendo na nguvu Zake huwaacha wanadamu bila chaguo ila kutambua ukweli kwamba ni Yeye pekee Anayeishi na Ana ukuu juu ya kila kitu. Hakuna kitu chochote ila Yeye kinachoweza kuamuru dunia, wala kuwajibikia wanadamu bila kukoma(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 3: Mwanadamu Anaweza tu Kuokolewa Katikati ya Usimamizi wa Mungu). Maneno ya Mungu kwa mara nyingine yaliniingiza polepole imani na nguvu. Niligundua kuwa mamlaka ya Mungu, nguvu na matendo Yake yapo kila mahali. Anaongoza ulimwengu wote na zaidi ya hayo, Anatawala kuenea kwa viumbe vyote ulimwenguni. Mungu ndiye Mtawala wa milele wa vitu vyote na nguvu aliyo nayo katika kutawala vitu vyote imezidi ufahamu wa mwanadamu. Maisha ambayo Mungu humpa mwanadamu hayazuiliwi na anga au wakati. Ibilisi Shetani anaweza tu kuumiza miili ya wanadamu, lakini anakosa kabisa udhibiti wa maisha yetu na roho zetu. Wakati wa majaribu ya Ayubu, Shetani aliweza tu kumtesa Ayubu na kuumiza mwili wake, lakini kwa sababu Mungu hakumruhusu achukue uhai wake, Shetani hakuwa na uwezo wa kufanya hivyo hata kidogo. Nilijiwazia: “Leo, Ibilisi Shetani wanajaribu kutumia mbinu zao mbaya kuharibu mwili wangu na kunifanya nimsaliti na kumwacha Mungu. Anatarajia bila mafanikio kutumia dawa za kulevya ili kunigeuza kuwa kichaa mwenye wendawazimu au zuzu ili kuliabisha jina la Mungu, lakini Shetani ana mamlaka gani? Bila idhini ya Mungu, kila tendo lake haliwezi kufanikisha jambo—Shetani ametabiriwa kushindwa mikononi mwa Mungu!” Nilipogundua haya nilibaki na hisia za amani na utulivu. Wakati huo huo, askari huyo katili alishika taya yangu na kuninywesha kwa nguvu dawa hiyo, ikiwa na ladha chungu na tamu na kunilazimsha niimeze. Ilifanya kazi haraka; nilihisi ni kama viungo vyangu vyote vya ndani vilikuwa vikisongamana, vikibanana, kana kwamba vilikuwa vinararuka. Maumivu hayo hayawezi kulinganishwa na chochote. Nilianza kuwa na tatizo la kupumua na nilivuta pumzi kubwa, nzito, nihema kwa shida. Sikuweza kusogeza macho yangu na nilianza kuona vitu vikiwa viwili viwili. Muda mfupi baadaye, nilipoteza fahamu. Mwishowe, baada ya muda fulani nisiojua, nilipata fahamu na nilidhani nilimsikia mtu akisema kwa namna isiyo dhahiri: “Jike hilo litakuwa mwendawazimu au kuwa zuzu baada ya kunywa dawa hiyo.” Niliposikia hilo, nilijua kuwa nilikuwa nimendelea kuishi tena. Nilishangaa sana kwa furaha kwamba sikuwa nimerukwa na akili hata kidogo; badala yake, niliweza kufikiria waziwazikabisa. Hakika haya yote yalitokana na uweza na ustaajabishaji wa Mungu. Nilihisi kuwa haya yalikuwa maneno ya Mwenyezi Mungu yakifanya kazi ndani yangu na kwamba, kwa mara nyingine, Mungu alikuwa amenyoosha mkono Wake wenye uweza wote na kunirudisha kutoka kwa mifumbato ya ibilisi, akiniwezesha kuendelea kuishi katika hali hii hatari. Wakati huo, nilijionea mwenyewe hali ya kuaminika na uhalisi wa maneno ya Mungu na kushuhudia nguvu na mamlaka Yake kuu. Zaidi ya hayo, niliona jinsi Mungu ni Muumba wa vitu vyote, na Mungu Mwenyewe wa pekee, Mtawala wa vitu vyote. Niliona jinsi maisha yangu, vitu vyote vyangu, vikiwemo kila neva mwilini mwangu, vyote vinadhibitiwa na Mungu. Bila idhini ya Mungu, hakuna hata unywele mmoja utakaotoka kichwani mwangu. Mungu ndiye tegemeo langu na wokovu wangu kila wakati, kila mahali. Siku hiyo katika pango lenye giza la pepo, maneno ya Mwenyezi Mungu yalionyesha nguvu yao ya kustaajabisha, yakinionyesha jinsi Mungu anavyofanya miujiza ya maisha tena na tena, na yaliniwezesha kutoroka kutoroka ukingo wa kifo. Niliimba kwa ari sifa za Mwenyezi Mungu moyoni mwangu na kuapa kumtegemea Mungu kuwa na ushuhuda katika vita hivi nzima vya kufa kupona.

Polisi walinitesa kwa muda wa siku sita mchana na usiku. Kwa kuwa sikuwa nimekula hata chembe kimoja cha chakula au kunywa hata tone moja la maji wakati huo wote, nilikuwa dhaifu sana, na walipoona kwamba nilikuwa katika hali mahututi, walinifunga katika seli ya gereza. Siku hizo sita za mateso zilikuwa kama safari ya kupitia jehannamu, na ukweli kwamba niliweza kuendelea kuishi ulikuwa ni kwa sababu tu ya rehema na ulinzi wa Mungu, na ulikuwa mfano wa uwezo na mamlaka ya maneno Yake. Baada ya siku chache kupita polisi walikuja kunihoji tena. Kwa sababu nilikuwa nimeshuhudia matendo ya Mungu ya kustaajabisha mara kadhaa, na nilikuwa nimejionea mwenyewe jinsi Mungu ni msaada wangu na vitu vyote viko mikononi mwa Mungu, nilihisi utulivu na jasiri katika mahojiano mengine. Katika chumba cha kuhojiwa, nilipata habari kutoka kwa afisa mmoja kwamba walikuwa wamejua jina langu na anwani yangu na walikuwa wamekwenda kupekua nyumba yangu. Hata hivyo, kwa sababu mume wangu alikuwa amewachukua watoto wetu zamani na kutoroka kutoka nyumbani, hawakupata kitu chochote. Kisha kwa mara nyingine tena alijaribu kunishurutisha nifumbue habari kuhusu kanisa, lakini kwa kuwa sikusema lolote, alikasirika na kusema: “Wewe ni kiongozi na mgumu kushughulikia! Kwa sababu yako, sijapata usingizi mzuri kwa siku sita na bado hujatupa lolote la manufaa.” Alipoona kwamba hangeweza kupata habari yoyote kutoka kwangu, alionekana kupoteza shauku baada ya hapo na alimaliza mahojiano hayo kwa haraka na uzembe na walichoweza kukifanya tu ni kunirudisha kwenye seli yangu. Nilipoona kwamba Mungu alikuwa ameshinda na Shetani alikuwa ameshindwa nilibaki nimefurahi isivyoelezeka—nilimshukuru na kumsifu Mungu. Nilijua kuwa sababu niliyoweza kuwa shahidi mbele ya Shetani ni kwamba Mungu alikuwa ameniongoza hatua kwa hatua, na neno la Mungu lilikuwa limenipa nuru mara kwa mara, likinipa nguvu, na kunipa hekima, na kunipa uwezo wa kumshinda Shetani na kutojisalimisha kwa udhalimu wake.

Baada ya kufungwa kizuizini kwa miezi minne, serikali ya CCP ilitunga mashtaka ya kuamini katika ‘xie jiao’ na ikanihukumu kifungo cha mwaka mmoja unusu gerezani. Nilipelekwa katika gereza la wanawake mnamo Machi mwaka wa 2006 ili kutumikia kifungo changu. Nilipokuwa gerezani, hata ingawa nilitendewa kama mnyama na mara nyingi niliwaona wafungwa wengine wakipigwa hadi kuuawa bila sababu dhahiri, nikiwa na kinga ya Mungu na ulinzi Wake na vile vile mwongozo wa maneno Yake, niliweza kuendelea kuishi kwa muda wa mwaka mmoja unusu wa kuteswa na kuweza kutoka katika gereza hilo la kishetani nikiwa hai. Baada ya kuachiliwa, askari wabaya waliendelea kuwatuma maafisa ili kunifuatia. Mara nyingi walikuja nyumbani kwangu kunisumbua na kwa sababu hiyo, hakuna hata mmoja wetu katika familia yangu angeweza kutenda imani yetu au kutekeleza wajibu wetu kwa kawaida. Baadaye, kwa ajili ya utunzaji na msaada wa ndugu zetu kanisani, tuliweza kuacha nyumba yetu na kuhamia nyumba mpya iliyomilikiwa na dada mmoja. Kwa ajili ya kutegemea hekima tuliyopewa na Mungu, tuliweza kwa mara nyingine kutekeleza wajibu wetu.

Kupitia mateso ya kikatili ya serikali ya CCP kulinipa mtazamo dhahiri na kamili wa asili mbovu sana ya Shetani ya udhalimu wa kikatili, udanganyifu wa shari, na upinzani mkali dhidi ya Mungu. Zaidi ya hayo, nilijionea nguvu tendaji ya Mungu ya kushangaza na isiyo ya ulimwengu. Hata ingawa polisi waovu walinipiga na kunitesa, wakaniadhibu kikatili na kunijeruhi bila huruma tena na tena, wakitafuta kuniibia maisha yangu, maneno ya Mwenyezi Mungu yalifichua nguvu yao tendaji isiyo ya ulimwengu, yakaniwezesha kuendelea kuishi kimiujiza. Katikati ya shida hizi zote na mateso haya, niliona kweli jinsi Mungu ni chanzo cha maisha yangu na neema ya Mungu na riziki Yake ndiyo kiini cha maisha yangu kuendelea. Bila mkono wa Mungu wenye nguvu kunisaidia, ningekuwa nimeangamizwa na pepo hao hapo zamani. Mungu aliandamana nami wakati huo wote, akiniongoza kumshinda Shetani mara nyingi na kuwa shahidi Kwake! Ingawa nilipitia mateso ya kinyama ya pepo hao na mwili wangu uliteseka sana, yote haya kwa kweli yalikuwa ya manufaa sana kwa maisha yangu. Yaliniruhusu kuona kwamba Mungu sio tu riziki ya maisha ya wanadamu, lakini pia anatupa msaada na fadhila ya kila wakati. Ilimradi tu tuishi kulingana na maneno ya Mungu, tunaweza kushinda nguvu zozote za giza za kihetani. Maneno ya Mungu kwa kweli ni ukweli, njia na uzima! Yana mamlaka ya juu zaidi na nguvu ya kushangaza zaidi na yanaweza kufanya miujiza ya maisha! Utukufu, heshima na sifa zote zimwendee Mungu wa hekima yenye uweza wote!

Tanbihi:

1. “Wakitoa tuhuma zisizokuwa na msingi” inahusu mbinu ambazo ibilisi hutumia huwadhuru watu.

2. “Inalindwa isivyo kawaida” inaonyesha kuwa mbinu ambazo ibilisi hutumia huwatesa watu ni mbovu hasa, na kuwadhibiti watu sana kiasi kwamba hawana nafasi ya kusogea.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp