Kumpa Mungu Moyo Wangu

24/01/2021

Na Xinche, Korea ya Kusini

Miaka miwili iliyopita, nilifanya mazoezi ya maonyesho ya kwaya ya Wimbo wa Ufalme. Nilihisi kwamba niliheshimiwa na nilijivunia kuimba jukwaani, nikimsifu na kumshuhudia Mungu. Nilimwomba Mungu pia na kuahidi kufanya mazoezi na kufanya wajibu wangu vizuri. Nilipoanza kufanya mazoezi mara ya kwanza, nilikuwa mwangalifu na nilijitahidi sana, lakini kwa kuwa sikuwa na tajriba ya kuimba na kucheza, maonyesho yangu hisia yalikuwa yaliyoshupaa kidogo na uwezo wangu haukuwa sawa na wa wengine. Mwalimu wetu alikuwa akitaja matatizo yangu kila mara. Baada ya muda fulani nilianza kukata tamaa na nikahisi kana kwamba bila kujali jinsi nilivyojitahidi, nisingewahi kuwa bora; tulipopewa nafasi, kina ndugu waliokuwa hodari katika kuimba na kucheza walikuwa mbele, na nilijaza tu kule nyuma. Nilianza kutotia juhudi katika mazoezi na nikaanza kuchelewa kuhudhuria mazoezi kila nilipoweza. Wakati wetu wa kwanza kupiga picha za filamu, niliwekwa kwenye safu ya nyuma, upande mmoja. Nilifadhaika kidogo, “Mimi si hodari katika hili na siwezi kushindana na wale ambao ni waimbaji na wachezaji hodari. Bila kujali jinsi ninavyojitahidi, sitawahi kuwa sawa nao na sitawahi kuonekana kwenye kamera. Kwa nini nifanye bidii wakati wa mazoezi? Jitihada kidogo itakuwa sawa.” Kuanzia wakati huo, motisha yangu ilipungua. Nilijua kwamba miondoko yangu haikuwa sawa lakini sikujaribu kuirekebisha. Wakati mwingine mwalimu alitwambia tujaribu zaidi na kwamba iwapo mtu mmoja angekosea, jambo hilo lingeathiri programu nzima na kuchelewesha upigaji picha za filamu. Hilo liliniathiri na nilihisi kwamba nilipaswa kuzingatia matokeo ya jumla. Nilianza kufanya bidii na kisha nikazama tena katika hali ya kutokuwa na motisha. Nilijizoeza tena wimbo huo na miondoko kwa shauku kidogo bila kuhisi mwongozo wa Mungu. Nilijizoeza miondoko mingine lakini sikuweza kuielewa vizuri. Kila mtu alishiriki juu ya jinsi alivyoelewa maneno ya wimbo ule, lakini mimi sikuweza. Pia, sikuguswa nilipokuwa nikiimba, na kwenye filamu, sikuonyesha hisia. Hakuna mtu aliyefurahia kunitazama. Nilihisi kwamba mazoezi yalichosha na nilisubiri kwa hamu yaishe ili niweze kufanya wajibu mwingine.

Chati ya nafasi za jukwaani ilipotokea, niligundua kwamba nilihusika katika maonyesho mengine ambayo hayakupigwa picha na nilihuzunika zaidi. Niliwaza, “Mimi si hodari, lakini pia si kwamba sina uwezo kabisa. Hata kama siwezi kuwa kwenye safu ya mbele, angalau napaswa kupigwa picha. Kwa nini nimetengwa? Je, nimekuwa nikifanya mazoezi bure? Kama ningejua, nisingejizoeza miondoko hii.” Baada ya hapo, kila nilipoonekana kwenye kamera nilishirikiana kwa furaha, vinginevyo, nilifanya mazoezi kwa namna isiyo ya dhati. Upigaji picha za filamu ulipomalizika, nilifadhaika nilipomskia kila mtu akizungumza mkutanoni juu ya yale waliyoyapata. Nilifanya wajibu huo huo na walipata kitu, hivyo kwa nini moyo wangu ulihisi mtupu kana kwamba sikupata chochote? Nilihisi hofu, nikijiuliza iwapo nilikuwa nimemchukiza Mungu. Baada ya hayo nilimtafuta na kumwomba Mungu, nikimsihi Anipe mwongozo. Kisha nikasoma maneno haya kutoka kwa Mungu: “Kila wakati, watu husema kwamba Mungu huangalia ndani ya moyo wa mtu kwa kina na huona kila kitu. Hata hivyo, watu hawajui kamwe kwa nini wengine huwa hawapati nuru kutoka kwa Roho Mtakatifu, kwa nini hawapati neema kamwe, kwa nini hawana furaha kamwe, kwa nini wao huwa hasi na wenye huzuni kila mara, na kwa nini hawawezi kuwa chanya? Hebu angalia hali za kuwepo kwao. Nakuhakikishia kwamba kila mmoja wa watu hawa hana dhamiri inayofanya kazi au moyo mwaminifu(“Mpe Mungu Moyo Wako wa Kweli, Na Unaweza Kupata Ukweli” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). “Vipengele vya msingi na muhimu zaidi vya ubinadamu wa mtu ni dhamiri na mantiki. Mtu asiye na dhamiri na ambaye hana mantiki ya ubinadamu wa kawaida ni mtu wa aina gani? Kwa ujumla, ni mtu asiye na ubinadamu, mtu mwenye ubinadamu mbaya. Acha tuchambue hili kwa makini. Je, mtu huyu huonyeshaje ubinadamu potovu kiasi kwamba watu waseme hana ubinadamu? Watu kama hawa huwa na tabia gani? Ni maonyesho gani mahususi ndiyo wao hudhihirisha? Watu kama hawa ni wazembe katika matendo yao na wanajitenga kutoka kwa chochote ambacho hakiwahusu wao binafsi. Hawafikirii masilahi ya nyumba ya Mungu wala hawazingatii mapenzi ya Mungu. Hawabebi mzigo wowote wa kumshuhudia Mungu au kutekeleza wajibu wao, na hawawajibiki. Ni kitu gani ambacho wao hufikiri kuhusu wakati wowote wanapofanya kitu? Kile wanachofikiria kwanza ni, ‘Je, Mungu atajua nikifanya jambo hili? Je, linaonekana kwa watu wengine? Watu wengine wasipoona kuwa ninatumia hii juhudi yote na ninatenda kwa kweli, na ikiwa Mungu haioni pia, basi hakuna haja ya mimi kutumia juhudi kama hii au kuteseka kwa ajili ya hili.’ Je, huu si ubinafsi? Wakati huo huo, pia ni aina duni sana ya dhamira. Wanapofikiria na kutenda kwa njia hii, je, dhamiri ipo katika jambo hili? Je, kuna sehemu yoyote ya dhamiri katika hili? Hata kuna watu ambao wanapoona tatizo wanapotekeleza wajibu wao, wanabaki kimya. Wanaona kwamba wengine wanakatiza na kuvuruga, lakini hawafanyi chochote kuwakomesha. Wao hawajali maslahi ya nyumba ya Mungu hata kidogo, wala hawafikirii kabisa wajibu wao au majukumu yao. Wanazungumza, kutenda, kuwa tofauti, kujitahidi, na kutumia nguvu tu kwa ajili ya ubatili, fahari, nafasi, maslahi, na heshima zao wenyewe. Matendo na nia za mtu kama huyo ni wazi kwa kila mtu: Yeye hujitokeza wakati wowote ambapo kuna fursa ya heshima au kufurahia baraka. Lakini, wakati ambapo hakuna fursa ya heshima, au punde tu kuna wakati wa kuteseka, yeye hutoweka kama kobe afichavyo kichwa chake. Je, mtu wa aina hii ana dhamiri na mantiki? Je, mtu asiye na dhamiri na mantiki ambaye hutenda kwa njia hii hujilaumu kweli? Dhamiri ya mtu wa aina hii haina maana, na hajawahi kujilaumu. Kwa hivyo, anaweza kuhisi kusuta au kufundisha nidhamu kwa Roho Mtakatifu? Hapana, hawezi(“Mpe Mungu Moyo Wako wa Kweli, Na Unaweza Kupata Ukweli” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Niliguswa niliposoma maneno ya Mungu. Sikuweza kupata kazi ya Roho Mtakatifu kwa sababu sikuwa mwaminifu ndani ya moyo wangu. Nilizingatia tu heshima na hadhi yangu badala ya masilahi ya nyumba ya Mungu. Mungu huchukia mtazamo huu katika wajibu wa mtu. Ninapokumbuka mazoezi hayo, nilipoona kwamba nilikuwa na uwezo mdogo kuliko wengine, na nilipowekwa kule nyuma, nilianza kuwa hasi na sikuonyesha hisia na sikutaka kufanya mazoezi ya hisia nilizoonyesha nikiimba na miondoko yangu. Niliridhishwa na jitihada ndogo sana, na sikuwa nikifikiria jinsi ya kufanya vizuri zaidi. Picha zangu ambazo hazikuonekana kwenye kamera zilinifanya nihisi kulalamika na kubishana, nikifikiri kwamba kujitahidi kwangu kulikuwa bure. Sikutaka kufanya mazoezi. Nilipokuwa nikipigwa picha za filamu, nilifanya wajibu wangu, lakini wakati ambapo sikuwa nikipigwa, nilizembea na kumaliza wajibu kwa kubahatisha. Niliona hatia nilipofikiria hayo. Sisi hupiga picha za kazi za kwaya ili kumshuhudia Mungu, kwa hivyo kushiriki kwangu kulikuwa Mungu kuniinua. Nilipaswa kutia juhudi za mchwa ili kufanya wajibu wangu vizuri. Badala yake, tamaa yangu ya heshima na hadhi ilinifanya niwe mzembe, hasi na mvivu. Sikuwa na dhamiri au mantiki. Nilikuwa mtu mbinafsi na mwenye kujishughulisha na mambo madogo. Mungu huchunguza mioyo ya watu, kwa hivyo Angewezaje kutochukizwa na mtazamo wangu? Nilijuta na kuhisi hatia nilipogundua haya na nikamwomba Mungu: “Ee Mungu! Nilikosea. Ninajutia nafasi yangu katika programu hii na sasa siwezi kuifidia. Sasa, nitafuatilia ukweli na nitaacha kufikiria heshima na hadhi. Nataka kufanya wajibu wangu vizuri.”

Wakati huo, nilidhani kwamba nilichoweza tu kufanya kilikuwa kujawa na majuto, lakini kwa mshangao wangu, tulihitaji kupiga picha za ziada za filamu. Hisia za kila aina ziliibuka niliposikia hayo. Nilihisi kwamba hii ilikuwa nafasi yangu ya kutubu. Niliazimia kufanya wajibu wangu vizuri ili nimridhishe Mungu. Nilifanya mazoezi kwa bidii mno na baada ya muda fulani, niliona maendeleo katika uwezo wangu. Tulikuwa karibu kuanza kupiga picha za filamu, lakini shughuli hiyo ilibidi iahirishwe kutokana na sababu fulani. Mwelekezi alituambia tuendelee kufanya mazoezi. Mwanzoni, niliweza kufanya mazoezi kwa bidii kila siku, lakini baadaye nilianza kuwaza, “Hatujui tutakapopiga picha au tutafanya mazoezi kwa muda gani. Kama wakati uliopita, labda sitaonekana katika picha nyingine. Nina ufahamu wa msingi kuhusu wimbo huu na miondoko, kwa hivyo kufanya mazoezi tu kunapaswa kutosha.” Mwalimu alituonya tusipunguze juhudi za kufanya mazoezi kabla ya kupiga picha za filamu na kwamba mipangilio ya jukwaa inaweza kubadilika. Lakini sikuzingatia hayo, nikifikiri, “Hakuna uwezekano kwamba nitawekwa mbele, kwa hivyo hata nikitia bidii, si lazima kwamba nitakuwa kwenye filamu. Kwa nini nisumbuke?” Mwalimu alipotaja matatizo yangu, sikuwa tayari kuyashughulikia na nilitoa visingizio: “Kina ndugu ambao wapo mbele wataonekana kwenye filamu, kwa hivyo ni vyema wao wafanye mazoezi sana. Lakini mimi nitakuwa kule nyuma na sitatambulika. Hakuna haja ya kuhangaika sana.” Baada ya hapo, nilihisi uchovu wakati wa mazoezi, kana kwamba yalihitaji bidii nyingi. Sikutaka kwenda mara nyingi. Niligundua kwamba tatizo langu la zamani lilikuwa limerudi na sikuhisi vizuri. Nilijiuliza, “Kwa nini mimi ni mzembe katika wajibu wangu? Kwa nini siwezi kulenga kumridhisha Mungu?” Nilimwomba Mungu kuhusu hali yangu ya kweli, nikimsihi Anipe mwongozo.

Nilisoma maneno ya Mungu: “Kwa miaka mingi, mawazo ambayo watu wametegemea kwa ajili ya kuendelea kuishi kwao yamekuwa yakiharibu mioyo yao hadi kiwango ambapo wamekuwa wadanganyifu, waoga, na wenye kustahili dharau. Hawakosi tu ushupavu na uamuzi, lakini pia wamekuwa walafi, wenye kiburi, na wa kudhamiria. Kabisa wanakosa uamuzi wowote upitao sana ubinafsi, na hata zaidi, hawana ujasiri hata kidogo wa kuondoa shutuma za ushawishi huu wa giza. Fikira na maisha ya watu ni mabovu sana kiasi kwamba mitazamo yao juu ya kuamini katika Mungu bado ni miovu kwa namna isiyovumilika, na hata watu wanaponena kuhusu mitazamo yao juu ya imani katika Mungu haivumiliki kabisa kusikia. Watu wote ni waoga, wasiojimudu, wenye kustahili dharau, na dhaifu. Hawahisi maudhi kwa nguvu za giza, na hawahisi upendo kwa nuru na ukweli; badala yake, wanafanya kila wanaloweza kuvifukuza. … Sasa nyinyi ni wafuasi, na mmepata ufahamu fulani wa hatua hii ya kazi. Hata hivyo, bado hamjaweka kando tamaa yenu ya hadhi. Wakati hadhi yenu iko juu mnatafuta vizuri, lakini wakati hadhi yenu iko chini hamtafuti tena. Baraka za hadhi daima ziko katika fikira zenu. Kwa nini watu wengi hawawezi kujiondoa katika uhasi? Je, si jibu bila shaka ni kwa sababu ya matarajio ya kuvunja moyo?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mbona Huna Hiari ya Kuwa Foili?). “Usizingatie kile asemacho mtu kama huyo; lazima uone kile anachoishi kwa kudhihirisha, kile anachofunua, na mtazamo wake ni upi anapotekeleza wajibu wake, na vile vile hali yake ya ndani ni ipi na kile anachopenda. Ikiwa upendo wake wa umaarufu na utajiri wake mwenyewe unashinda kujitolea kwake kwa Mungu, ikiwa upendo wake wa umaarufu na utajiri wake mwenyewe unashinda masilahi ya Mungu, au ikiwa upendo wake wa umaarufu na utajiri wake mwenyewe unashinda wema anaomwonyesha Mungu, basi yeye si mtu aliye na ubinadamu. Tabia yake inaweza kuonekana na wengine na Mungu pia; kwa hivyo, ni vigumu sana kwa mtu kama huyo kupata ukweli(“Mpe Mungu Moyo Wako wa Kweli, Na Unaweza Kupata Ukweli” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Maneno ya Mungu yalifichua nia zangu thabiti zilizostahili dharau, na yakanionyesha kwa nini nilikuwa mzembe wakati ambapo sikuweza kujionyesha katika wajibu wangu na kwa nini sikujali na jukumu langu. Tamaa yangu ya heshima na hadhi ilikuwa kubwa mno. Kwa sababu sikuwa na kipaji kwanza kabisa, haikuwa dhahiri kwamba nilikuwa nikifuatilia fursa ya kujionyesha. Nilitaka kujionyesha licha ya ukosefu wangu wa kipaji. Nilipoona kwamba hakukuwa na nafasi ya kuwapiku wengine, kwamba nisingekuwa katika safu ya mbele, nilianza kuwa na mtazamo hasi kwa jambo hilo lote na nikatia juhudi kidogo katika wajibu wangu. Nilifanya wajibu kwa njia isiyo ya dhati bila kufanya vizuri kadiri nilivyoweza. Nilidhani kwamba kwa kuwa sikuweza kujionyesha, sikuhitaji kuteseka sana, ili nisishindwe kwa njia hiyo. Sumu za Shetani kama vile “Kila mwamba ngoma huvutia upande wake” tayari zilikuwa zimekita mizizi ndani yangu. Nilikuwa nikidhibitiwa nazo kiasi kwamba nilifikiria faida yangu mwenyewe katika kila nilichofanya. Ningekifanya tu kwa ajili ya sifa na faida. Hiyo ilikuwa kweli hata katika wajibu wangu. Nilijitahidi wakati ambapo niliweza kujionyesha, lakini wakati ambapo sikuweza kutimiza tamaa zangu, nilifanya kwa njia isiyo ya dhati, bila kuzingatia mapenzi ya Mungu au nyumba ya Mungu hata kidogo. Nilikuwa nikiishi kulingana na asili yangu ya ujanja, nikipanga njama kwa ajili ya sifa na cheo changu. Nilikuwa mzembe na mdanganyifu katika wajibu wangu, bila kuwajibika au kuwa na dhamiri, mantiki, au hadhi yoyote. Sikuwa mtu wa kutegemewa hata kidogo. Nilifikiria jinsi ambavyo ndugu wengi niliowajua walikuwa safi na waaminifu, kwamba bila kujali nafasi yao jukwaani ilikuwa wapi, walimfanyia Mungu kazi vizuri zaidi kadiri walivyoweza. Baada ya muda fulani, kuimba na kucheza kwao kuliboreka na waliweza kuona baraka na mwongozo wa Mungu. Aidha, kuna wale waliokuwa nyuma ya jukwaa, ambao walifanya wajibu wao kimyakimya ingawa wasingewahi kuonekana. Walisema kwamba kazi yao yote ilikuwa ya maana ilimradi programu hiyo ilichapishwa mtandaoni. Lakini wakati ambapo sikuweza kujionyesha sikufanya wajibu wangu vizuri. Nilikosa ubinadamu. Tabia ya Mungu ni yenye haki, kwa hivyo Yeye hudharau na kuchukia binadamu kama mimi na ufuatiliaji kama wangu. Sikuweza kupata kazi ya Roho Mtakatifu katika wajibu wangu na maendeleo maishani. Nilijua kwamba nisingetubu, kamwe nisingepata ukweli wowote. Ningeondolewa na Mungu! Nilihisi hofu nilipotafakari na nikamwomba Mungu. “Ee Mungu, naona jinsi ambavyo nimekuwa wa aibu, nikiishi kulingana na tabia yangu potovu na bila ubinadamu. Mungu, nataka kutubu na kubadilika. Tafadhali niongoze ili nibadilishe tabia yangu na nizingatie wajibu wangu.”

Baadaye nilisoma maneno ya Mungu: “Ikiwa unataka kujitolea kuyaridhisha mapenzi ya Mungu katika kila kitu unachofanya, huwezi kutekeleza wajibu mmoja tu; lazima ukubali agizo lolote akupealo Mungu. Liwe linalingana na upendeleo wako au halilingani na lipo ndani ya maslahi yako, ni kitu ambacho hufurahii au hujawahi kukifanya hapo awali, au ni ki kigumu, bado unapaswa kulikubali na kutii. Sio tu kwamba lazima ulikubali tu, lakini pia lazima ushirikiane kwa bidii, na ujifunze kulihusu na ufikie uingiaji. Hata ukiteseka na hujaweza kuonekana na kung’aa, bado lazima utende kujitolea kwako. Lazima ulione kama wajibu wako wa kutimiza; si kama kazi yako binafsi, lakini kama wajibu wako. Je, watu wanapaswa kuelewaje wajibu wao? Ni wakati ambapo Muumbaji—Mungu—anampa mtu kazi ya kufanya, na wakati huo, wajibu wa mtu huyo unatokea. Kazi ambayo Mungu anakupa, agizo ambalo Mungu anakupa—huu ni wajibu wako. Unapoyafuatilia kama malengo yako, na kwa kweli una moyo wa kumpenda Mungu, je, bado unaweza kukataa? Hupaswi kuyakataa. Unapaswa kuyakubali. Hii ndiyo njia ya kutenda(“Ni kwa Kuwa Mtu Mwaminifu tu Ndiyo Mtu Anaweza Kuwa na Furaha Kweli” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Niligundua kwamba wajibu wangu ulikuwa agizo la Mungu kwangu, na iwapo ningeweza kujionyesha au la, nilipaswa kuacha nia zangu za kibinafsi, kulichukulia kama wajibu wangu na kufanya vizuri zaidi kama Mungu anavyohitaji. Katika namna yoyote ya mpangilio, watu wengine huwa mbele na wengine huwa nyuma, lakini bila kujali walipo, wanafanya wajibu wao. Mungu huangalia nia na mitazamo yetu kwa wajibu wetu, iwapo tunaufanya kwa bidii, na iwapo tunatenda ukweli ili kumridhisha Mungu. Nilifikiria jinsi ambavyo sikuwa na kipaji kama waimbaji wengine, lakini bado Mungu alinipa nafasi hiyo ya kujifundisha ili niweze kupiga hatua katika ustadi wangu na kuingia kwangu katika uzima. Huo ni upendo wa Mungu! Nilijua kwamba sikupaswa kuwa mbinafsi na mkatili kama zamani na kuuvunja moyo wa Mungu na kumsikitisha. Iwapo ningekuwa mbele au nyuma, iwapo ningeonekana au la, ningechukua nafasi yangu kama kiumbe ili nitekeleze tu wajibu wangu na kulipa upendo wa Mungu.

Nilihakikisha kwamba nilimwomba na kumtegemea Mungu na nilijitahidi bila kujali tulichojizoeza. Tuliposoma maneno ya Mungu kabla ya kufanya mazoezi, nilifikiri kuhusu matakwa ya Mungu na nikatia maneno Yake katika vitendo nikiwa mazoezini. Mwalimu alipotaja matatizo yangu, nilisikiliza na kuyashirikisha katika mazoezi yangu. Nilizingatia kasoro zangu na kutumia wakati ambapo sikuwa na kazi kufanya mazoezi. Niliacha kutia juhudi ndogo kabisa. Nilipokuwa na nia zilizofaa za mazoezi, niliridhika kila siku. Niliweza kuhisi kabisa mwongozo wa Mungu katika wajibu wangu na sikuchoka sana. Baada ya muda kiasi, miondoko na hisia nilizoonyesha viliboreka, na kina dada walisema kwamba uwezo wangu ulikuwa umeboreka sana. Nilihisi jinsi ilivyo muhimu kuchukulia wajibu wangu kwa moyo mwaminifu. Wakati ambapo Wimbo wa Ufalme ulikuwa ukimalizika, Mungu alisema kwamba mtoto mchanga mwenye sauti safi alipaswa kuimba mstari wa mwisho: “Wanamwimbia Mungu nyimbo nzuri sana!” Niliguswa sana na hayo. Niliona kwamba Mungu anatarajia kupata moyo wenye uaminifu. Anatumaini kwamba tutamgeukia na kuwa safi kama watoto, kwamba tutatoa mioyo yetu na kumtolea sehemu yetu bora. Azimio langu la kutenda ukweli na kumridhisha liliimarika.

Wakati mwingi wa upigaji picha za filamu bado niliwekwa nyuma, na wakati mwingine sikutaka kufanya vizuri zaidi kadiri nilivyoweza. Kwa hivyo nilimwomba Mungu na kufikiria jinsi ya kuzingatia mapenzi Yake na jinsi ya kujitumia. Jabo hilo lilichukua muda, lakini mtazamo wangu uliboreka. Nilipokuwa nyuma, niliwaombea kina ndugu zangu waliokuwa mbele. Wakati ambapo sikuwa nikipigwa picha, niliwasaidia kina dada zangu kwa kuwatengenezea mavazi yao na nywele zao, na kufanya kile nilichoweza kwa ajili ya wajibu wangu. Nilipowaona kina dada wengine wakianza kuwa hasi kwa sababu walikuwa nyuma, nilitoa ushirika wangu juu ya mapenzi ya Mungu. Kufanya wajibu wangu kwa njia hiyo kulinipa amani na hali yangu ikaboreka. Kuacha heshima na hadhi yangu na kutenda ukweli kulitokana na mwongozo wa maneno ya Mungu.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mbona Ujihusishe na Hila Unapomtumikia Mungu

Ee Mungu! Asante kwa kufunua asili yangu ya kiburi na majivuno. Kuanzia siku hii na kuendelea, hakika nitachukulia hili kama onyo na kuweka juhudi zaidi katika kujua asili yangu. Nitafanya kazi hasa kulingana na mipangilio ya kazi. Kwa kweli nitakuwa mtu mwenye mantiki, anayezingatia kanuni, na aliye na moyo wa uchaji Kwako.

Nilifurahia Karamu Kubwa

Xinwei Mkoa wa Zhejiang Juni 25 na 26, mwaka wa 2013 zilikuwa siku zisizosahaulika. Eneo letu lilipata tukio kubwa, viongozi wengi na...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp