Utendaji Wangu wa Utukuzaji na Ushuhuda kwa Mungu Ulikuwa wa Kipumbavu Mno

18/10/2019

Na Zhang Cheng, Mkoa wa Shandong

Kila mara nilipowaona baadhi ya viongozi na wafanyikazi wenza kanisani wakigeuka na kuwa wapinga Kristo, na kuondolewa na Mungu, kwa sababu kila wakati walijishuhudia na kuwaleta ndugu mbele yao, nilijionya: Lazima nihakikishe nimemtukuza na kumshuhudia Mungu katika mambo yote; Sipaswi kuringa au kujitukuza kamwe, nisije nikaingia kwenye njia ya washinde. Na kwa hivyo, kila wakati nilipofanya ushirika, nililenga tu kufichuliwa kwa upotovu wangu mwenyewe na kamwe sikuongea kuhusu utendaji au kuingia kutoka kwa mwelekeo unaosaidia. Wengine waliposema kulikuwa na kuingia au mabadiliko kidogo ndani yangu, nilikana hilo papo hapo. Kwa hiyo nikitenda, niliamini, nilikuwa nikimtukuza na kumshuhudia Mungu.

Siku moja, nilisikia maneno haya kutoka kwa ushirika: “Maarifa ya watu wengine kuhusu kumtukuza na kumshuhudia Mungu hayajakamilika, kwa hivyo wanachotenda si sahihi kabisa. Wanafikiri kuwa kuzungumza kuhusu kupitia kazi ya Mungu kimsingi kunamaanisha kuongea kuhusu kujua upotovu wao wenyewe, kufunua upotovu wao wenyewe, na kujizoesha kuelezea hisia zao, na kuchangua kufunuliwa kwa upotovu wao wenyewe—kwamba huku tu ndiko kumtukuza na kumshuhudia Mungu. Kuzungumza juu ya vipengele kama hivi vya uzoefu na ushuhuda kama mabadiliko ndani ya mtu na mchakato ambao kwao mtu hubadilika, au kuingia kwa mtu katika uhalisi, ni kana kwamba unajishuhudia, si Mungu. Je, maarifa kama haya ni sahihi? Je, kuzungumza kuhusu mchakato ambao uliupitia ili kupata mabadiliko ni sawa na kujishuhudia? Si sawa. ... Tunachohitajika kuelewa ni kwamba ili kuwa na matokeo yanayofaa zaidi katika kuwaleta watu mbele za Mungu, unapoongea tu kuhusu uzoefu mbaya, na kutosema chochote kuhusu kuingia halisi, matokeo ni madogo, na si bora, na watu bado hawatakuwa na njia. Wakati wa ushirika wenu, watu wengine wanaona tu jinsi unavyoelezea hisia zako, jinsi unavyojichangua, na jinsi unavyojifichua. Je, vipi kuhusu kuingia kwako halisi, vipi kuhusu utendaji wako? Unawapa watu njia gani ya kutenda? Hujawaambia watu jinsi wanavyopaswa kutenda kuanzia sasa na kuendelea. ... Watu wengine hawaelewi kujishuhudia ni nini. Wanafikiri kuwa kuzungumza kuhusu vipengele halisi na kuhusu kipengele cha kuingia kwao katika uhalisi, ni kujishuhudia—lakini kwa kweli huu ni ushuhuda bora zaidi kwa Mungu, ushuhuda mkamilifu zaidi kwa Mungu. Kwamba tunaweza kuwa na uhalisi kidogo, kuhusu matendo mema kiasi, uaminifu kiasi katika kutekeleza wajibu wetu—je, si huu ni upendo wa Mungu? Je, hii si neema ya Mungu? Je, haya si matokeo ya kazi ya Roho Mtakatifu? Kwa kufanya ushirika juu ya mambo kama haya, unaweza kushuhudia uweza wa Mungu zaidi, jinsi ambavyo kazi ya Mungu ni kazi ya wokovu wa mwanadamu, jinsi maneno ya Mungu yanavyoweza kuwabadilisha watu, na kuwakamilisha, na kuwaokoa. Kwa hivyo, ushuhuda kwa kazi ya Mungu pia unahitaji kuzunguma kuhusu kuingia kwako halisi, kuhusu jinsi ulivyotoka katika hali ya kutoweza kuingia hadi hatimaye kuweza kuingia; kuhusu jinsi ulivyotoka katika hali ya kutoweza kujijua hadi hatimaye kuweza kujijua, na kuweza kujua kiini cha asili yako; kuhusu jinsi ulivyotoka katika hali ya kupinga na kuasi dhidi ya Mungu hadi kuweza kumtii, kumridhisha, na kumshuhudia. Ikiwa unaweza kufanya ushirika kuhusu uzoefu na ushuhuda kama huu kwa ukamilifu, basi ushuhuda wako kwa Mungu ni mtimilifu na mkamilifu. Huku pekee ndiko kumtukuza na kumshuhudia Mungu kwa maana ya kweli. ... Ikiwa unachozungumzia kwa kirefu ni upotovu wako na ubaya wako mwenyewe tu, na ikiwa, baada ya muongo mmoja au zaidi, huwezi kusema chochote kuhusu mabadiliko ndani yako, je, huku ni kumtukuza na kumshuhudia Mungu? Je, huku ni kumfaharisha Mungu? Je, jambo hili linaweza kushuhudia uweza wa kazi ya Mungu? ... Ikiwa ushuhuda wako unawasababisha watu kuwa hasi na kupotea kutoka kwa Mungu, basi si ushuhuda. Kazi yako inampinga Mungu, ni kazi ya Shetani; ni kazi inayompinga Mungu”. (“Maswali na Majibu” katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha III). Niliposikia haya niligundua ghafla kuwa kujifunua kwa ukakamavu na kuongea juu ya ufunuo wa upotovu wangu mwenyewe hakukuwa kumtukuza na kumshuhudia Mungu; ushuhuda wa kweli na utukuzaji wa Mungu hauhusishi tu kuongea juu ya kujua kiini chako potovu unapokuwa ukipitia kazi ya Mungu ya hukumu na kuadibu; kilicho muhimu zaidi ni kusema kitu kuhusu kutenda kwako na kuingia kwako halisi. Kwa mfano: Ni ukweli upi ambao umekuja kujua, ni nini ambacho umejua kumhusu Mungu, kazi ya Mungu imekuwa na matokeo gani ndani yako, kumekuwa na mabadiliko yapi katika tabia yako ya zamani, na kadhalika. Ukizungumza kwa kweli kuhusu vipengele hivi vya uzoefu na maarifa, kupitia uzoefu halisi ambao unafanya ushirika kuuhusu utawawezesha ndugu kupata maarifa ya Mungu, na kuona kwamba kazi ya Mungu kweli inaweza kuwaokoa watu na kuwabadilisha, na hivyo kuzalisha ndani yao imani ya kweli kuhusiana na Mungu, na, wakati huo huo, kuwapa njia ya kutenda na kuingia, na kuwajulisha jinsi ya kumridhisha Mungu, na jinsi ya kuingia katika uhalisi wa maneno ya Mungu. Huku pekee ndiko kumtukuza na kumshuhudia Mungu kwa kweli, na ushuhuda kama huo tu ndio unaoweza kumwaibisha Shetani. Ufahamu wangu kuhusu kumtukuza na kumshuhudia Mungu, kwa upande mwingine, ulikuwa wa upande mmoja sana, upuuzi mtupu. Nilidhani kwamba kusema zaidi juu ya upotovu wangu mwenyewe mbele ya ndugu, ili wasiniheshimu, kulikuwa kumtukuza na kumshuhudia Mungu. Nilidhani kwamba kuzungumza juu ya vipengele vyangu halisi vya kuingia kulikuwa kujitukuza na kujishuhudia. Nilikuwa mjinga sana! Kwa wakati huu, sina budi kufikiri juu ya utendaji wangu na matokeo ya kumtukuza na kumshuhudia Mungu.

Wakati mmoja, nakumbuka jinsi dada mmoja aliyekuwa akinikaribisha alivyosema, “Ninyi viongozi mmeziacha familia na kazi zenu ili kutekeleza wajibu wenu mbali na nyumbani, mmepitia shida nyingi, mmepitia mambo mengi, na mmekuja kuelewa ukweli mwingi. Katika ninyi nyote, kumekuwa na kuingia na mabadiliko kiasi fulani. Lakini ninapokaa nyumbani, ninazuiwa sana na mwili, nyakati ambazo moyo wangu una amani mbele za Mungu ni chache mno, na hakujakuwa na mabadiliko ndani yangu. Ningependa kuwa kama ninyi.” Niliposikia haya, nilijiambia, “Lazima nimtukuze na kumshuhudia Mungu, lazima nifanye ushirika kuhusu upotovu wangu mwenyewe, na nisizungumze kuhusu mabadiliko yangu mwenyewe, vinginevyo dada huyu ataniheshimu sana.” Hivyo, nilihakikisha nimezungumza juu ya jinsi, hapo zamani, nilivyokuwa na kiburi na uasi kwa mipangilio ya kanisa nilipokuwa nikitekeleza wajibu wangu, juu ya jinsi ambavyo sikuweza kuelewana na ndugu zangu, juu ya kiasi gani cha yale niliyoyasema kilikuwa kimetiwa doa na uwongo, juu ya jinsi ambavyo nilijaribu kudanganya na kuficha tuhuma juu ya watu…. Baada ya kusikia ushirika wangu, dada huyo alisema, “Nilidhani nyote mlikuwa mmebadilika kabisa—lakini imetokea kwamba ninyi pia hamjabadilika. Eeh! Hakuna yeyote kati yenu aliyebadilika, ambayo inanifanya mimi kuwa mbaya zaidi.” Baada ya hayo, ingawa dada huyo hakuniheshimu tena sana na hakunitegemea, kwa hiyo aligeuka na kuwa hasi, na akafikiria hakuwa na tumaini la wokovu. Wakati mmoja, wakati wa mkutano, niliwazungumzia ndugu kuhusu kipengele kimoja cha upotovu wangu: jinsi nilivyokuwa na dhana kumhusu Mungu. Nilizungumza tu juu ya jinsi nilivyokuwa na dhana juu ya Mungu, si kuhusu jinsi nilivyotatua dhana hizi, na ilitukia kwamba ndugu hao hawakuwa wamekuwa na dhana kama hizo, lakini walikuwa nazo baada ya kusikia ushirika wangu. Na kadhalika. Hayo yalikuwa matokeo ya kutukuza na kushuhudia kwangu kwa Mungu kulikodhaniwa. Kutukuza na kushuhudia kwa Mungu ambako nilitenda hakukukosa kushudia mamlaka na uadhama wa maneno ya Mungu tu, lakini badala yake kuliwapatia ndugu mashaka na dhana juu ya kazi ya Mungu ya kuwaokoa, kuwabadilisha, na kuwakamilisha watu; walipoteza imani katika wokovu, wala hawakuwa na motisha ya kuufuatilia ukweli au azimio la kushirikiana kikamilifu. Kutukuza na kushuhudia kwa Mungu ambako nilitenda hakukushuhudia kwa watu kuhusu wema, uzuri, na haki ya Mungu, hakukushuhudia kuhusu nia njema ya Mungu ya kumwokoa mwanadamu, kuwaonyesha watu upendo wa Mungu, na kuwawezesha wamjue Mungu; badala yake, ndani ya ndugu kulibuniwa dhana na kutokuelewa kuhusu Mungu, na waliishi katika hali mbaya. Nilikuwa nikimtukuza na kumshuhudia Mungu vipi? Nilikuwa tu nikieneza uhasi na kuachilia kifo. Kimsingi, nilikuwa nikiwaumiza watu na kuleta uharibifu juu yao. Ingawa, kutoka nje, haikuonekana kana kwamba nilikuwa nimefanya kitu chochote kiovu, kiini cha vitendo vyangu kilikuwa kinapingana na Mungu, kilikuwa kinapanda kukosa imani katika uhusiano wa watu na Mungu, lilikuwa shambulio kwa hali nzuri ya ndugu, na hilo lilisababisha kupotea kutoka kwa Mungu. Nilikuwa nikitenda uovu tu! Jambo hili linadharauliwa na kuchukiwa na Mungu kweli!

Shukrani kwa Mungu kwa kunielimisha kuhusu kumtukuza na kumshuhudia Mungu kwa kweli ni nini, kwa kuniwezesha nijue jinsi ufahamu wangu mwenyewe wa utukuzaji na ushuhuda kwa Mungu ulivyokuwa wa upuuzi, kwa kuniwezesha nione kwamba kimsingi, kutukuza kwangu na kushuhudia kwangu kwa Mungu nilikodhania kulikuwa upinzani mkali sana kwa Mungu. Kama ningeendelea hivyo, mwishowe yote ambayo yangenitokea ni kwamba ningekuwa nimeondolewa na kuadhibiwa kwa sababu nilikuwa nimemtumikia Mungu lakini nikamkana. Kuanzia siku hiyo, nilitamani kugeuza njia zangu za kutenda za kipuuzi; niliposhiriki juu ya kujijua, lazima nizungumze zaidi juu ya njia ya kuingia halisi, na juu ya ushuhuda wa kupitia na kutenda maneno ya Mungu. Lazima nishuhudie yote ambayo nimekuja kujua—ili, kwa msaada wa uzoefu na maarifa yangu, ndugu waweze kuyaelewa mapenzi ya Mungu, waweze kupata uzoefu wa kazi ya Mungu, na kupata maarifa kumhusu Mungu, nikiwaleta mbele za Mungu kwa kweli.

Inayofuata: Utajiri wa Maisha

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Uzoefu wa Kutenda Ukweli

Hengxin Jiji la Zhuzhou, Mkoa wa Hunan Sio muda mrefu mno uliopita, nilisikia “Mahubiri na Ushirika juu ya Kuingia Katika Maisha,” jambo...

Kuishi Mbele za Mungu

Na Yongsui, Korea ya Kusini Mwenyezi Mungu anasema, “Ili kuingia katika uhalisi, mtu lazima apindue vitu vyote kuelekea maisha halisi....

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp