Tuzo za Kutimiza Wajibu wa Mtu

24/01/2021

Na Yang Mingzhen, Kanada

Mwenyezi Mungu anasema, “Kujisalimisha kwa kazi ya Mungu lazima kugusike na kuishi kwa kudhihirishwa. Kujisalimisha kwa kiwango cha juu juu hakuwezi kupokea idhini ya Mungu, na kutii tu vipengele vya juujuu vya neno la Mungu bila kutaka mgeuzo wa tabia ya mtu, hakutaweza kuufurahisha moyo wa Mungu. Utiifu kwa Mungu na kujinyenyekeza kwa kazi ya Mungu ni kitu kimoja. Wale wanaomtii Mungu tu lakini hawatii kazi Yake hawawezi kudhaniwa kuwa watiifu, sembuse wale wasiotii kwa kweli na kwa nje hao ni wa kujipendekeza. Wale ambao kweli wanajinyenyekeza kwa Mungu wote wanaweza kufaidika kutokana na kazi na kupata ufahamu wa tabia na kazi ya Mungu. Wanadamu kama hawa tu ndio kweli wanajinyenyekeza kwa Mungu. Wanadamu kama hawa wanaweza kupata maarifa mapya kutokana na kazi mpya na kuwa na uzoefu wa mabadiliko mapya kutoka hayo. Wanadamu kama hawa tu ndio wana idhini ya Mungu; mwanadamu wa aina hii tu ndiye amekamilishwa, ndiye amepitia mabadiliko ya tabia yake. Wale wanaopokea idhini ya Mungu ni wale wanaojisalimisha kwa Mungu kwa furaha, na pia kwa neno na kazi Yake. Mwanadamu wa aina hii tu ndiye yuko sahihi; mwanadamu wa aina hii tu ndiye kweli anamtamani Mungu, na anamtafuta Mungu kwa dhati(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watapatwa na Mungu). Ningependa kushiriki uzoefu na ufahamu wangu wa kumtii Mungu kwa kuzingatia maneno haya.

Yote yalianza mnamo Machi 2016 wakati nilikimbia kutoka China ili kutoroka kukamatwa na kuteswa na CCP, ili niweze kufuata imani yangu kwa uhuru. Muda fulani baadaye, kiongozi wa kanisa Dada Zhang alinijia na kuuliza, “Je, ungependa kuchukua wajibu wa unyunyizaji?” Kwa furaha kubwa, nilijibu, “Hiyo itakuwa vyema! Nitaweza kuwasaidia kina ndugu waelewe ukweli na waweke msingi katika njia ya kweli. Nitakuwa nikifanya vitendo vyema sana!” Ndugu walionijua wangegundua kwamba nilikuwa nikifanya wajibu wa unyunyizaji, wangenistahi na kuniheshimu kweli. Jambo hilo lingenifanya nionekane mzuri sana. Hata hivyo, nilipokuwa tu nikiweka matumaini yangu juu, kiongozi huyo alikuja kuzungumza nami tena. Alisema kwamba kina dada fulani walilazimika kuhama kwa sababu za dharura, lakini hawakuwa wamepata mahali panapofaa. Alisema kwamba nyumba yangu ingefaa, na akaniuliza kama ningeweza kufanya wajibu wa mwenyeji. Nilihisi msukosuko sana ndani mwangu aliposema hivyo. Nilidhani kwamba nilikuwa nifanye wajibu wa unyunyizaji, lakini sasa nilikuwa nifanye wajibu wa mwenyeji? Je, sitakuwa nikishinda jikoni wakati wangu wote tu? Itakuwa kazi ngumu, lakini zaidi ya hiyo itakuwa kazi ya kuaibisha! Huko nje, nilikuwa nimefanya biashara kubwa na nilikuwa na kiwanda changu mwenyewe. Jamaa na marafiki wote waliniita mwanamke mwenye uwezo sana. Nyumbani, nilimfanya yaya afue, kupika na kusafisha. Sasa nilikuwa nichukue jukumu hilo na niwapikie wengine. Kwa kweli sikutaka kuifanya kazi hiyo. Lakini nilifikiria jinsi kina dada hao hawakuwa na mahali pa kuishi na hawangeweza kufanya wajibu wao kwa amani, Kweli. na kuongezea, nyumba yangu ilifaa kwa kuwakaribisha wageni, kwa hivyo nilikubali shingo upande.

Katika siku chache zilizofuata, nilikuwa nikifanya wajibu wangu wa mwenyeji kwa nje, lakini ndani mwangu nilikuwa na msukosuko, na nikaanza kupata tuhuma. Je, ndugu zangu walidhani sikufaa kufanya wajibu wa unyunyizaji? Je, kuna sababu gani nyingine ya wao kuniambia nifanye kazi ya mwenyeji? Ndugu walionijua wakigundua hili, je, watasema kwamba nilikosa uhalisi wa ukweli, na kwamba sikuweza kufanya wajibu mwingine, lakini niliweza tu kuwa mwenyeji? Wazo hili lilinikasirisha hata zaidi. Kisha nilifikiria uamuzi niliofanya mbele ya Mungu, kwamba haijalishi ni wajibu upi niliopewa, mradi uliinufaisha kazi ya kanisa, ningeufanya kikamilifu, na hata kama sikuupenda, bado ningetii ili kumridhisha Mungu. Kwa hivyo mbona sikuweza kutii sasa nilipokuwa nikiulizwa nifanye wajibu wa kuwa mwenyeji? Nilimwomba Mungu kimyakimya. Nilisema, “Ee Mungu, Umeamua na kunipangia nifanye wajibu wa mwenyeji, lakini daima mimi huhisi mwenye kutaka kuasi na kamwe siwezi kutii. Mungu, tafadhali nipe nuru na Uniongoze ili niweze kuelewa mapenzi Yako.”

Baadaye, nilisoma vifungu viwili vya maneno ya Mungu: “Katika kupima ikiwa watu wanaweza kumtii Mungu au la, jambo muhimu la kuangalia ni ikiwa wanatamani kitu chochote cha kupita kiasi kutoka kwa Mungu, na ikiwa wana nia mbaya au la. Ikiwa watu humdai Mungu kila wakati, inathibitisha kuwa wao sio watiifu Kwake. Chochote kinachotokea kwako, ikiwa huwezi kukipokea kutoka kwa Mungu, huwezi kutafuta ukweli, kila wakati wewe unazungumza kutoka kwa hoja yako ya dhahania na kuhisi kila wakati kuwa wewe tu ndiye uliye sahihi, na hata bado una uwezo wa kumshuku Mungu, basi utakuwa taabani. Watu kama hao ndio wenye kiburi na waasi zaidi kwa Mungu. Watu ambao daima humdai Mungu hawawezi kamwe kumtii kweli. Ukimdai Mungu, hii inathibitisha kwamba unafanya maafikiano na Mungu, kwamba unachagua mawazo yako mwenyewe, na kutenda kulingana na mawazo yako mwenyewe. Kwa kufanya hivi, unamsaliti Mungu, na huna utiifu(“Watu Wanafanya Madai Mengi Sana kwa Mungu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). “Kutii kwa kweli ni nini? Wakati wowote ambapo Mungu anafanya jambo lolote linalokuendea vizuri, na kukuruhusu uhisi kwamba kila kitu ni cha kiridhisha na kinachostahili, na umeruhusiwa kutokeza, unahisi kwamba hili ni jambo la fahari mno, na unasema, ‘Shukrani kwa Mungu’ na unaweza kutii utaratibu na mipango Yake. Hata hivyo, kila unapotumwa mahali pasiposifika ambapo huwezi kutokezea, na ambapo hakuna anayekutambua, basi unaacha kuhisi furaha na unaona vigumu kutii. … Kutii wakati hali zinafaa kwa kawaida huwa rahisi. Ikiwa unaweza pia kutii katika hali ngumu—zile ambazo mambo hayakwendei vizuri na unasononeshwa, ambazo hukufanya uwe dhaifu, ambazo zinakufanya uteseke kimwili na sifa yako iharibike, ambazo haziwezi kuridhisha majivuno na majisifu yako, na zinazokufanya uteseke kisaikolojia—basi kweli una kimo(Ushirika wa Mungu). Maneno ya Mungu yalinionyesha kwamba kutii kwa kweli siyo mabadilishano, na kwamba chaguo la kibinafsi halihusiki. Niwe ninaupenda au la, uwe unanisaidia au la, mradi unatoka kwa Mungu na unaisaidia kazi ya kanisa, basi lazima nitii kabisa. Lakini nilikuwa nikifanya nini badala yake? Nilipoulizwa nifanye wajibu wa kuwa mwenyeji, kuyadhukuru mapenzi ya Mungu au kuiunga mkono kazi ya kanisa hakukuwa akilini mwangu, lakini badala yake nilifikiria tu kuhusu iwapo ningeweza kuringa, kuwafanya wengine wanistahi, na ikiwa majisifu yangu yangeridhishwa. Je, huko kulikuwaje kumtii Mungu? Nilikumbuka wakati nilipokuwa kiongozi wa kikundi. Kiongozi wa kanisa daima alishiriki nami kwanza kuhusu kazi kanisani. Nilikuwa nikifikiria kiongozi aliniheshimu sana, na ndugu zangu walinistahi. Hakuna juhudi iliyokuwa kubwa sana katika wajibu wangu, na bila kujali ulikuwa mgumu au wa kuchosha namna gani, nilifurahia kuufanya. Lakini nilipokabiliwa na wajibu wa kuwa mwenyeji, nilikuwa hasi, nikifikiria ulikuwa duni. La muhimu zaidi, haijalishi jinnsi nilivyojaribu kutia bidii, bidii hiyo haingeonekana kwa wengine. Hiyo ndiyo maana niliuchukia wajibu huo, na sikutaka kuufanya. Ni wakati huo tu ndipo niliona kwamba niliweka bidii sana katika wajibu wangu wa zamani kwa sababu niliweza kuringa na kuwafanya wengine wanistahi. Hata hivyo, wajibu wa kuwa mwenyeji haukuweza kuridhisha tamaa yangu ya makuu hata kidogo, kwa hivyo sikuweza kutii. Kisha nilitambua kwamba kila mara nilikuwa na upendeleo na chaguo za kibinafsi katika wajibu wangu, na yote niliyowahi kufikiria yalikuwa sifa yangu, hadhi yangu, na jinsi yalivyonifaidi. Sikuwa nikifuatilia ukweli au kumtii Mungu hata kidogo!

Baadaye nilisoma maneno haya ya Mungu: “Wale ambao wanaweza kutia ukweli katika vitendo wanaweza kukubali uchunguzi makini wa Mungu katika matendo yao. Unapokubali uchunguzi makini wa Mungu, moyo wako unawekwa kuwa sawa. Ikiwa daima unafanya tu mambo kwa ajili ya wengine kuona na hukubali uchunguzi makini wa Mungu, je, una Mungu moyoni mwako? Watu kama hawa hawana moyo unaomcha Mungu. Usifanye mambo kwa ajili yako daima na usiyafikirie masilahi, hadhi na sifa yako mwenyewe kila wakati. Pia usiyafikirie masilahi ya mwanadamu. Lazima kwanza uyafikirie masilahi ya nyumba ya Mungu, na uyape kipaumbele. Unapaswa kuyafikiria mapenzi ya Mungu na uanze kwa kutafakari kama umekuwa mwenye najisi katika utimizaji wa wajibu wako au la, kama umefanya kila uwezalo kuwa mwaminifu, kama umefanya kila uwezalo kutimiza majukumu yako, na kufanya kadiri uwezavyo au la, na vile vile kama umefikiria wajibu wako na kazi ya nyumba ya Mungu kwa moyo wote au la. Lazima uyazingatie mambo haya. Yafikirie mara kwa mara, na itakuwa rahisi kwako kutekeleza wajibu wako(“Mpe Mungu Moyo Wako wa Kweli, Na Unaweza Kupata Ukweli” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Ndani ya maneno ya Mungu nilipata njia ya kutenda. Ilibidi nikubali uchunguzi wa Mungu katika wajibu wangu, niwe na moyo wa kumcha Mungu, niweze kuacha faida ya kibinafsi na kufanya tu chochote kilicholifaidi kanisa. Baada ya kuelewa mapenzi ya Mungu, niliomba ombi hili: “Ee Mungu, niko tayari kukubali uchunguzi Wako. Sitazingatia yale ambayo wengine wananifikiria tena. Nataka tu niweze kutii mipangilio Yako na nifanye wajibu wangu wa kuwa mwenyeji vizuri.” Katika siku zilizofuata, dada zangu wa kanisa walijua kwamba nilikuwa nimefika hivi karibuni katika nchi hii ya kigeni na ilikuwa vigumu kwangu kununua vitu, kwa hivyo walitenga muda ili kwenda pamoja nami kununua vitu muhimu. Walikuwa na shughuli nyingi sana katika wajibu wao, lakini walinisaidia na kazi ya nyumbani walipoweza. Wakati wowote nilipokuwa na shida, wangeshiriki nami juu ya maneno ya Mungu, na kufanya ushirika juu ya matukio yao wenyewe ili wanisaidie na kunihimili. Hakuna dada yeyote aliyenidharau au kuniepuka kwa sababu nilikuwa mwenyeji. Nilikuja kufahamu kwamba kweli hakuna wajibu wa juu au wa chini linapokuja suala la kufanya wajibu na kina ndugu. Tunatekeleza tu wajibu wetu mbele za Mungu. Baada ya tukio hili, nilifikiria niliweza kunyenyekea kidogo katika wajibu wangu, lakini kwa sababu sikuwa na ufahamu halisi wa asili na kiini changu, bado sikuwa nimeacha kabisa ufuatiliaji wa umaarufu na hadhi. Nilifunuliwa tena punde hali ambayo sikupenda iliibuka.

Wakati fulani baadaye, kiongozi wa kanisa alinipigia simu akisema kwamba Dada Zhou alikuwa na shughuli nyingi sana akihubiri injili, na aliuliza kama ningeweza kutenga nusu ya siku kila Jumamosi kumwangalia binti ya Dada Zhou wakati hakuwepo. Nilipinga wazo hili la kuwatunza watoto mara moja. Zamani nilikuwa na shughuli nyingi sana katika biashara yangu kiasi kwamba sikuweza hata kuwatunza watoto wangu mwenyewe. Kuwatunza watoto wa watu wengine kweli kungenifanya niwe kama yaya. Je, ndugu walionijua wangefikiria nini kama wangegundua hili? Ningewezaje kuonekana bila kuhisi aibu? Lakini nilifikiria matatizo ya kweli aliyokuwa nayo Dada Zhou, na nilijua kwamba kama singesaidia, jambo hili lingeisumbua dhamiri yangu. Nililifikiria kwa muda kisha nikakubali. Alasiri ya Jumamosi hiyo, nilienda nyumbani kwa Dada Zhou. Nilifanikiwa kushinda hadi jioni kwa shida tu wakati ambapo kwa ghafla mtoto huyo alianza kulia kwa sauti kubwa na kupiga kelele akimtaka mamake, na sikuweza kumtuliza. Nilikimbia huku na kule nikitafuta vitu vya kumpendeza nimpe ili nimfurahishe, nilimwambia hadithi na nikamwekea katuni kwenye televisheni, na mwishowe aliacha kulia. Nikiwa njiani kurudi nyumbani, nilitembea nikiwaza: “Kuwatunza watoto ni kazi ngumu sana. Hakuchoshi tu, bali pia ni kazi duni na isiyoonekana kabisa.” Kadiri nilivyofikiria zaidi, ndivyo nilivyohisi kusikitika zaidi. Nilipofika nyumbani, niliwaona kina dada hapo wakijadili kwa furaha kuhusu tuzo na uzoefu waliopata kutokana na wajibu wao. Nilihisi wivu na mfadhaiko. Niliwaza, “Nitaweza kufanya wajibu wa unyunyizaji lini kama kina dada zangu? Katika wajibu huu ninaofanya sasa, ninasugua vyombo vya kupika au kuwatunza watoto wadogo. Je, naweza kupata ukweli gani nikifanya haya? Je, watu watasema kwamba sina uhalisi wa ukweli, kwa hivyo ninaweza tu kufanya kazi za mtumishi wa nyumbani kama hii?” Wazo hili lilinifadhaisha hata zaidi. Usiku huo, nilijilaza kitandani nikigaagaa na kupinduka, nisiweze kulala hata chembe, kwa hivyo nilienda mbele za Mungu kuomba. Nilisema, “Ee Mungu, nimefadhaika sana hivi sasa. Siku zote ninataka kufanya wajibu unaonifanya nijitokeze, ambao huwafanya wengine wanistahi. Ee Mungu, najua kwamba ufuatiliaji huu unapingana na mapenzi Yako, lakini ninaona vigumu sana kutii. Mungu, tafadhali nielekeze na Uniongoze, na Unisaidie nijijue ili niweze kuiacha hali hii mbaya.”

Kisha nilisoma baadhi ya maneno ya Mungu: “Tabia potovu ya mwanadamu hujificha ndani ya kila wazo na fikira yake, ndani ya nia za kila kitendo chake; inajificha ndani ya kila mtazamo ambao mwanadamu anao juu ya chochote na ndani ya kila maoni, ufahamu, fikira na tamaa aliyo nayo katika mtazamo wake kwa yote ambayo Mungu hufanya. Imefichika ndani vitu hivi(“Kuwa Mtiifu Kwa Kweli Pekee Ndiyo Imani ya Kweli” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). “Tabia potovu ya kishetani imekita mizizi kabisa ndani ya watu; inageuka kuwa maisha yao. Je, ni nini hasa ambacho watu hutafuta na wanachotamani kupata? Huku wakidhibitiwa na tabia potovu ya kishetani, maadili, matumaini, matarajio, na malengo na mielekeo ya maisha ya watu ni yapi? Je, haviendi kinyume na mambo chanya? Kwanza, watu daima hutaka kuwa na sifa au kuwa watu mashuhuri; wanataka kupata umaarufu mkubwa na ufahari, na kuwaletea mababu zao heshima. Je, haya ni mambo chanya? Haya hayalingani hata kidogo na mambo chanya; zaidi ya hayo, yanapingana na sheria ya Mungu ya kutawala majaliwa ya wanadamu. Kwa nini niseme hivyo? Je, Mungu anamtaka mtu wa aina gani? Je, Anamtaka mtu mwenye ukuu, mtu mashuhuri, mtu mwenye cheo kikufu, au mtu muhimu sana? (La.) Kwa hivyo basi, Mungu anamtaka mtu wa aina gani? Anamtaka mtu aliye thabiti ambaye anatafuta kuwa kiumbe wa Mungu anayestahili, anayeweza kutimiza wajibu wa kiumbe, na anayeweza kusalia katika nafasi ya binadamu. … Hivyo basi, tabia potovu ya kishetani huwaletea watu nini? (Upinzani kwa Mungu.) Ni nini hutokana na watu kumpinga Mungu? (Uchungu.) Uchungu? Ni maangamizo! Uchungu sio hata nusu yake. Kile unachoona kwa dhahiri sasa ni uchungu, uhasi, na udhaifu, na ni upinzani na malalamiko—vitu hivi vitaleta matokeo yapi? Maangamizo! Hili silo jambo dogo na sio mchezo(“Ni Kutafuta Ukweli na Kumtegemea Mungu Pekee Ndiko Kunakoweza Kutatua Tabia Potovu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Baada ya kusoma maneno ya Mungu ya hukumu na ufunuo, nilihisi aibu sana. Nilianza kutafakari juu yangu: “Kwa nini siwezi kamwe kutii hali ambazo Mungu hupanga? Je, kwa nini daima huwa siko tayari kufanya wajibu huu usioonekana kuwa wa maana? Nahisi ni kama wengine hunidharau kwa sababu ya kufanya wajibu huu, kana kwamba mimi ni duni. Siwezi kujiamini, na nahisi kuwa mimi ni bure. Ninahisi kama kwamba ule wajibu muhimu unaoweza kufanya nijitokeze, na kuwafanya wengine wanistahi na kuniheshu pekee ndio unaofaa kufanywa.” Nilipokuwa nikitafakari juu mawazo haya, niligundua kwamba nilikuwa bado nikidhibitiwa na hamu yangu ya umaarufu na hadhi. Nilikuwa nikiishi kwa kufuata sumu za kishetani kama “Kama mti unavyoishi kwa ajili ya gomba lake, mtu huishi kwa ajili ya sifa yake,” “Mtu huacha urithi nyuma yake kama vile bata bukini anavyoacha sauti yake,” na “Mtu hujitahidi kupanda juu; maji hutiririka chini.” Sumu hizi kwa muda mrefu zilikuwa zimekita mizizi ndani mwangu na zikawa maisha yangu. Zilikuwa zimenifanya niwe mwenye kiburi na majivuno sana. Nilipenda kuwafanya wengine wanistahi. Nilipenda kuwa na sifa na hadhi, na niliyachukua mambo haya kama malengo ya maisha ya kufuatilia. Nilitambua kwamba haya yalikuwa malengo yale yale ambayo watu ulimwenguni walifuatilia. Hiyo ni kweli kabisa. Kabla nianze kumwamini Mungu, nilikuwa mwenye kupenda kushindana sana. Nilifanya kazi kutoka alfajiri hadi magharibi na kujichosha na kazi nikijaribu kufanya kiwanda changu kiendelee vizuri. Kila nilipotembelea mji wangu wa asili, na jamaa na marafiki zangu walinisalimia kwa uchangamfu na kuniita mwanamke mwenye uwezo sana, majisifu yangu yangeridhishwa, na ningekuwa tayari kulipa gharama yoyote. Bado niliishi kwa kufuata maoni haya baada ya kupata imani yangu. Kufanya wajibu wangu kwa ajili ya sifa na wadhifa kulinifanya niwe na wasiwasi kuhusu faida na hasara zangu. Nikiwa na wadhifa ambao wengine walistahi, nilikuwa na furaha. Bila wadhifa huo, wakati sikutokeza, nilikuwa hasi na nisiye na furaha, nilimpinga Mungu, na nilipinga hali ambayo Mungu alikuwa amenipangia. Kadiri nilivyofikiria zaidi juu ya hilo, ndivyo nilivyogundua zaidi kuwa sumu hizi zote za kishetani ziliniletea uchungu tu na zilinifanya nimwasi Mungu na kumpinga bila kutaka. Kama ningeendelea na ufuatiliaji wa aina hiyo, bila shaka ningeishia kumchukiza Mungu, na Angeniangamiza. Kadiri nilivyofikiria zaidi juu ya hilo, ndivyo nilivyoogopa zaidi kuhusu njia niliyokuwa nikiifuata. Nilikimbia kuomba na kutubu kwa Mungu. Sikutaka kufuatilia sifa na hadhi au kuwafanya wengine wanistahi tena, lakini nilitaka kutafuta kuwa kiumbe wa kweli aliyeumbwa anayepatana na maneno ya Mungu. Baada ya kuomba, moyo wangu ulitulia zaidi.

Wakati wa ibada zangu siku iliyofuata, nilisoma maneno haya ya Mungu: “Unamwamini Mungu na unafuata Mungu, na kwa hivyo moyoni mwako ni lazima umpende Mungu. Ni lazima uache tabia yako potovu, lazima utafute kutimiza mapenzi ya Mungu, na ni lazima utekeleze wajibu wako kama kiumbe wa Mungu. Kwa kuwa unamwamini na kumfuata Mungu, unapaswa kutoa kila kitu kwake, na hupaswi kufanya uamuzi au madai ya kibinafsi, na unapaswa kutimiza ukamilishaji wa mapenzi ya Mungu. Kwa kuwa uliumbwa, unapaswa kumtii Bwana aliyekuumba, kwa kuwa wewe huna mamlaka kiasili juu yako mwenyewe, na huna uwezo wa kudhibiti hatima yako. Kwa kuwa wewe ni mtu ambaye anamwamini Mungu, inapaswa utafute utakatifu na mabadiliko. Kwa kuwa wewe ni kiumbe wa Mungu, unapaswa kushika wajibu wako, na kuhifadhi nafasi yako, na ni lazima usivuke mpaka wa wajibu wako. Hii si kwa ajili ya kukuzuia, ama kukukandamiza kupitia mafundisho, bali ndiyo njia ambayo utaweza kutekelezea wajibu wako, na inaweza kufikiwa—na inapaswa kufikiwa—na wote wanaotenda haki(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea). Kusoma maneno ya Mungu kulinifanya nielewe kwamba kama kiumbe aliyeumbwa, napaswa kutii sheria na mipango ya Mungu. Napaswa kufuatilia ukweli na kufuatilia mbadiliko katika tabia yangu. Huu ndio wajibu wangu na ndicho ninachopaswa kufuatilia. Sikupenda hali ambayo Mungu alikuwa amenipangia, lakini ilikuwa kwa sababu ya nia njema za Mungu. Alikuwa amepanga yote hayo kwa uangalifu ili Anitakase na kunibadilisha. Sikupaswa kufuatilia sifa na wadhifa, au kuwa mwenye kuchagua wajibu wangu tena. Napaswa kulenga kufuatilia ukweli, na nikubali hukumu na kuadibiwa na maneno ya Mungu ili kutatua tabia yangu potovu. Napaswa kuweka juhudi zangu zote katika kufanya wajibu wangu vizuri.

Katika siku zilizofuata, niliacha kuzingatia yale ambayo wengine walinifikiria lakini nilifanya wajibu wangu mbele za Mungu. Wakati mwingine wakati ambapo ndugu walikuwa na shughuli nyingi katika wajibu wao na hawakuwa na wakati wa kuwatunza watoto wao, nilijitolea kusaidia. Nilipowaona kina ndugu wakihubiri injili na kuwaleta watu zaidi mbele za Mungu, nilihisi furaha moyoni mwangu. Hata ingawa sikuweza kutokeza katika wajibu wangu, niliweza kutuliza mawazo ya kina ndugu na kwa kimya kufanya wajibu wangu kwa sababu ya uenezaji wa injili ya ufalme. Hili lilikuwa jambo la maana pia. Wakati nilipokuwa nikifanya wajibu wa mwenyeji na kusaidia katika utunzaji wa watoto, ingawa majisifu na hamu yangu ya ufahari havikuridhishwa, niliuona wajibu huo ukiwa wenye kuridhisha sana. Nilijua kwamba kufuatilia sifa na wadhifa haikuwa njia sahihi. Kutii sheria na mipango ya Mungu na kufanya juhudi yangu yote katika wajibu wangu ndivyo nilivyopaswa kufuatilia. Kwa kweli nilikuja kutambua kwamba hakika hakuna wajibu wa juu au wa chini katika nyumba ya Mungu. Haijalishi ni wajibu upi ninaofanya, kila mara kuna mafunzo ya kujifunza na ukweli ninaopaswa kutenda na kuuingia. Mradi ninatii na kufuatilia ukweli, basi ninatuzwa. Hii ilinionyesha jinsi Mungu ni mwenye haki na jinsi ambavyo Hampendelei mtu yeyote. Kuwa na ufahamu na mabadiliko haya madogo ni zawadi niliyopewa na Mungu katika maisha yangu. Shukrani ziwe kwa Mungu!

Inayofuata: Kumpa Mungu Moyo Wangu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mabadiliko ya Mwigizaji

Mwenyezi Mungu anasema, “Kama mojawapo ya viumbe, lazima mwanadamu achukue nafasi yake mwenyewe, na ajiendeleze kwa uangalifu, na kulinda...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp