Ninapata njia ya kumjua Mungu

13/01/2018

Xiaocao Mji wa Changzhi, Mkoa wa Shanxi

Siku moja, niliona kifungu hiki kifuatacho cha neno la Mungu kwa maandishi “Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu”: “Katika kipindi kile alichomfuata Yesu, Petro alitazama na kutia moyoni kila kitu kuhusu maisha Yake: Matendo Yake, maneno Yake, mwendo Wake na maonyesho Yake. … Tangu wakati huo akiwa na Yesu, Petro alitambua pia kwamba hulka Yake ilikuwa tofauti na ile ya binadamu wa kawaida. Siku zote alikuwa na mwenendo dhabiti na hakuwahi kuwa na haraka, hakupigia chuku wala kupuuza chochote, na aliyaishi maisha Yake kwa njia iliyofichua hulka iliyokuwa ya kawaida na ya kuvutia. Katika mazungumzo, Yesu alikuwa mwenye madaha na uzuri, mwenye uwazi na mchangamfu ilhali pia mtulivu, na Hakuwahi kupoteza heshima Yake katika utekelezaji wa kazi Yake. Petro aliona kwamba Yesu wakati mwingine alikuwa mnyamavu, ilhali nyakati nyingine alizungumza kwa mfululizo. Wakati mwingine Alikuwa na furaha sana kiasi kwamba alionekana kuwa njiwa anayerukaruka na kuchezacheza, na ilhali nyakati nyingine Alihuzunika sana kiasi cha kwamba hakuzungumza kamwe, ni kana kwamba alikuwa mama aliyechoka sana. Nyakati nyingine Alijawa na hasira, kama askari jasiri anayefyatuka kuwaua adui, na wakati mwingine hata kama simba anayenguruma. Nyakati nyingine Alicheka; nyakati nyingine aliomba na kulia. Haijalishi ni vipi Yesu alivyotenda, Petro alizidi kuwa na upendo na heshima isiyokuwa na mipaka Kwake. Kicheko cha Yesu kilimjaza kwa furaha, huzuni Yake ikamtia simanzi, hasira Yake ikamtetemesha, huku huruma Zake, msamaha na madai makali Aliyotoa kwa watu yalimfanya aje kumpenda Yesu kwa kweli, na akaweza kumcha na kumtamani kwa kweli. Bila shaka, Petro alikuja kutambua haya yote kwa utaratibu baada ya kuishi kando yake Yesu kwa miaka michache(Neno Laonekana katika Mwili). Baada ya kusoma kifungu hiki nilifikiri: Haishangazi kwamba Petro angeweza kufikia ujuzi wa Mungu! Yaonekana kuwa ilikuwa kwa sababu wakati aliishi pamoja na Yesu usiku na mchana, yeye binafsi alishuhudia kila neno na kila tendo la Yesu, na kutoka kwa hayo akagundua zaidi kuhusu kupendeza kwa Mungu. Sasa pia ni enzi ya wakati Mungu anakuwa mwili ili yeye mwenyewe ashuke katika ulimwengu wa mwanadamu kufanya kazi. Kama mimi pia ningekuwa na bahati ya kuweza kukutana na Mungu na kuwa na muda pamoja naye kama Petro alivyokuwa, basi si mimi pia ningemjua Mungu vizuri zaidi? Oo! Inasikitisha kwamba sasa ninaweza kusoma tu neno la Mungu lakini siwezi kuuona uso wa Kristo. Basi ningewezaje kupata ujuzi wa kweli kumhusu Mungu?

Wakati tu nilipokuwa na huzuni na kusikitishwa juu ya hili, maneno ya Mungu yalinipa nuru: “Kumjua Mungu kunapaswa kutimizwa kupitia kwa kusoma na kuyaelewa maneno ya Mungu. Wengine husema: ‘Sijamwona Mungu mwenye mwili, hivyo ningewezaje kumjua Mungu?’ Kwa kweli, maneno ya Mungu ni maonyesho ya tabia Yake. Kutoka kwa maneno ya Mungu unaweza kuuona upendo Wake na wokovu kwa wanadamu, na vile vile mbinu Yake ya kuwaokoa…. Hii ni kwa sababu maneno ya Mungu yanaonyeshwa na Mungu Mwenyewe bali hayajaandikwa na mwanadamu. Yameonyeshwa na Mungu binafsi- Yeye; Mungu mwenyeweAnaeleza maneno Yake mwenyewe na sauti Yake ya ndani. Kwa nini yanaitwa maneno kutoka moyoni? Ni kwa sababu hayo hutolewa kutoka ndani kabisa, na yanaonyesha tabia Yake, mapenzi Yake, mawazo Yake, upendo Wake kwa wanadamu, wokovu Wake wa wanadamu, na matarajio Yake ya wanadamu…. Matamshi ya Mungu yanajumuisha maneno makali, na maneno ya upole na yenye kuzingatia, na vile vile maneno mengine ya ufunuo ambayo hayalingani na matakwa ya binadamu. Ikiwa unayaangalia tu maneno ya ufunuo, unaweza kuhisi kwamba Mungu ni mkali. Ikiwa unaangalia maneno ya upole tu, utaweza kuhisi kuwa Mungu sio mweneye mamlaka sana. Hivyo basi hupaswi kuyachukua nje ya muktadha; badala yake yaangalie kutoka kila pembe. Wakati mwingine Mungu huzungumza kwa mtazamo mpole na wenye huruma, na hivyo basi watu wanauona upendo Wake kwa wanadamu; wakati mwingine Yeye huzungumza kwa mtazamo mkali sana, na hivyo basi watu wanaona tabia Yake ambayo haitavumilia kosa lolote. Mwanadamu ni mchafu kwa njia ya kusikitisha, na hastahili kuuona uso wa Mungu au kuja mbele Zake. Kuwa watu sasa wanaweza kukubaliwa kuja mbele Zake ni kwa neema Yake tu. Hekima ya Mungu inaweza kuonekana kutokana na jinsi Yeye anavyofanya kazi na kwa umuhimu wa kazi Yake. Watu bado wanaweza kuona mambo haya katika maneno ya Mungu hata bila mwingiliano wa moja kwa moja kutoka Kwake(“Jinsi ya Kumjua Mungu Mwenye Mwili” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Maneno ya Mungu kwa ghafla yalinifanya kuona mwanga. Ndiyo! Mungu katika mwili wa siku za mwisho tayari Ametumia neno Lake kuonyesha tabia Yake kwa mtu, Akimruhusu mtu kuona nguvu Zake kuu kwa njia ya neno la Mungu, mamlaka Yake ya juu kabisa, unyenyekevu Wake na kujificha kwake, na kupendeza Kwake, na zaidi ya hayo kuelewa furaha Yake na huzuni, na kujua chote Anacho Yeye na alicho. Hii inatosha kuonyesha kwamba kusoma neno la Mungu na kupitia neno la Mungu ndiyo njia ya pekee ya kumjua Mungu. Nikiliondokea neno la Mungu, halafu nini hata nikimwona Mungu katika mwili? Si Mafarisayo pia walimuona Yesu wakati huo wa nyuma? Kwa hivyo mbona walimtundika Yesu msalabani? Si ni kwa sababu hawakusikiliza maneno ya Yesu, walijigamba na kwa ukaidi wakashikilia dhana zao wenyewe na mawazo yao, na kumpinga na kumshutumu Bwana Yesu kwa msingi wa maandiko kidogo waliyoyaelewa? Kwa upande mwingine, Petro aliweza kumjua Yesu kwa sababu angeachilia mawazo na dhana zake mwenyewe, kusikiliza kwa makini maneno ya Bwana Yesu, na alikuwa mzuri kwa kutafakari kwa uangalifu kila neno na sentensi zilizotamkwa na Yesu. Kwa njia ya matamshi na kazi ya Bwana Yesu alipata kujua tabia ya Mungu na chote Anacho Yeye na alicho, hatimaye akipata maarifa ya kweli ya Mungu. Si ukweli huu dhabiti unaeleza kwa utoshelevu kwamba mtu anaweza tu kumjua Mungu kupitia kwa neno Lake? Zaidi ya hayo, kutokana na kwamba kazi kuu ya Mungu katika mwili wa siku za mwisho ni kazi ya neno, si hili linanifaidi kwa kupata kumjua Mungu?

Jinsi nilivyofikiria nyuma kwa mawazo yangu ya mantiki zaidi ndivyo nilivyohisi unyonge wangu mwenyewe zaidi, ujinga, na utoto. Kila siku nilishikilia neno la Mungu mikononi mwangu, nikala na kunywa neno la Mungu, kusoma neno la Mungu, na kuwa na uzoefu wa neno ya Mungu, lakini sikulipenda neno la Mungu kwa dhati, nikifikiri kwamba ningemjua Mungu tu kwa kuona uso wa Kristo. Kwa kweli nilikuwa ninaishi maisha ya heri bila kuyafurahia! Ee Mungu! Asante kwa kufichua na kugeuza njia yangu mbaya ya kujua na kunifanya kuona njia ya kumjua Mungu. Kuanzia sasa kuendelea, nitatamani kusoma neno Lako, kutafakari neno Lako, kutafuta kuelewa furaha na huzuni Zako kwa njia ya neno Lako, na kwa kutambua zaidi kupendeza kwako nipate kukujua Wewe hata zaidi.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp