Kuishi Mbele za Mungu

24/01/2021

Na Yongsui, Korea ya Kusini

Mwenyezi Mungu anasema, “Ili kuingia katika uhalisi, mtu lazima apindue vitu vyote kuelekea maisha halisi. Iwapo waumini katika Mungu, watu hawawezi kuja kujijua kupitia kuingia katika maisha halisi, na ikiwa hawawezi kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida katika maisha halisi, watashindwa. Wale wanaomkaidi Mungu wote ni watu ambao hawawezi kuingia katika maisha halisi. Wote ni watu wanaozungumza kuhusu ubinadamu lakini wanaishi kwa kudhihirisha asili ya pepo mbaya. Wote ni watu wanaozungumza kuhusu ukweli lakini wanaishi kwa kudhihirisha kanuni badala yake. Wale wasioweza kuishi kwa kudhihirisha ukweli katika maisha halisi ni wale wanaoamini katika Mungu lakini wanachukiwa na kukataliwa na Yeye. Lazima ufanye mazoezi ya kuingia kwako katika maisha halisi, ujue upungufu wako mwenyewe, ukaidi na upumbavu, na ujue ubinadamu wako usio wa kawaida na udhaifu. Kwa njia hiyo, ufahamu wako wote utaambatanishwa ndani ya hali yako halisi na ugumu. Ni aina hii ya ufahamu pekee ndiyo ya kweli na inaweza kukufanya ushike kwa hakika hali yako mwenyewe na ufanikishe mabadiliko ya tabia yako(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kujadili Maisha ya Kanisa na Maisha Halisi). “Katika kutafuta kuingia katika uzima, mtu lazima achunguze maneno, vitendo, mawazo na maoni yake katika kila jambo ambalo anakumbana nalo katika maisha ya kila siku. Mtu lazima afahamu hali zake mwenyewe, na kisha azichunguze dhidi ya ukweli, atafute ukweli, na aingie katika uhalisi wa ukweli anaouelewa. Wakati wa mchakato wa kuingia katika uhalisi wa ukweli, mtu lazima afahamu hali zake mwenyewe, na aje mbele za Mungu mara kwa mara kumwomba na kumsihi. Mtu lazima pia afanye ushirika mara kwa mara na ndugu wengine kwa uaminifu, atafute njia ya kuingia katika uhalisi wa ukweli, na atafute kanuni za ukweli. Mwishowe, mtu huyo atakuja kujua ni tabia zipi ambazo yeye hufichua katika maisha ya kila siku, ikiwa Mungu anazifurahia au la, ikiwa njia ambayo mtu huyo anatenda ni sahihi au la, ikiwa mtu huyo amehakiki hali zinazopatikana ndani yake kupitia kujichunguza mwenyewe dhidi ya Maneno ya Mungu au la, ikiwa hizi zimehakikiwa kwa usahihi au la, ikiwa zinakubaliana na maneno ya Mungu au la, na ikiwa kwa kweli mtu huyo amepata mafanikio na kweli amepata kuingia kuhusu zile hali ambazo zinakubaliana na maneno ya Mungu au la. Unapoishi mara kwa mara katika hali hizi, mazingira kama haya, basi polepole, utakuja kuwa na ufahamu wa kimsingi wa ukweli fulani na wa hali zako halisi(“Kujua Tabia ni Msingi wa Kubadili Tabia” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Maneno ya Mungu yanatuonyesha njia ya kuingia katika uzima, ambayo ni kuchunguza fikira na matendo yetu yote katika kila kitu kinachotendeka katika maisha halisi, na kisha kuvilinganisha na ufunuo wa maneno ya Mungu, kutafakari na kufahamu tabia zetu potovu na kutafuta kutumia ukweli kuzitatua. Hii ndiyo njia pekee ya kujifahamu kwa kweli na kuingia katika uhalisi wa maneno ya Mungu. Ningependa kushiriki baadhi ya matukio niliyopitia. Vyema.

Ndugu Cheng alishiriki mojawapo ya matukio yaliyompata kwenye mkutano mmoja miezi sita iliyopita. Alipomaliza, niliwaza kuwa alikuwa mkaidi katika wajibu wake na alikuwa ametenda kinyume na kanuni, na kwa hivyo alikuwa amepogolewa na kushugulikiwa. Alikuwa amejidhibiti tu kwa kiasi fulani bila kutoa visingizio, na alikuwa ameonekana kutii. Lakini kuhusu ni kwa nini alikuwa amekuwa mkaidi katika kazi yake, ni tabia zipi potovu zilizokuwa zikimdhibiti au sababu kuu ilikuwa nini, hakuwa kweli ametafakari au kujaribu kufahamu mambo haya, wala hakuwa ametafuta ukweli ili kuyatatua. Utiifu wake ulikuwa tu yeye kufuata sheria. Haungeweza kuitwa utiifu wa kweli. Nilijiuliza, “Je, ninapaswa kumtajia kasoro hii?” Lakini kisha nikawaza, “Ndugu Chen amekuwa muumini kwa muda mrefu kuniliko, na ufahamu na uzoefu wake umeshinda wangu. Nikimtolea pendekezo, je, nitakuwa kama mtoto anayejaribu kujigamba? Je, jambo hilo litanifanya nionekane mwenye kujisifu? Afadhali nisiseme chochote.” Alipomaliza ushirika wake, alituomba tutaje dosari zozote tulizoziona kwake. Nilitaka kutaja tatizo lake, lakini sikuweza hata kidogo. Niliwaza, “Ana umri mkubwa zaidi kuniliko. Nikisema hajatii kwa kweli na kwamba anafuata tu sheria, ataadhirika sana na nitakuwa nikimwingiza matatani. Asipokubali jambo hilo na kusema kwamba mimi ni mwenye majivuno sana na asiye na uzoefu, nitaaibika sana. Simjui vizuri, na sistahili kumpa picha mbaya kunihusu.” Nilisita kwa muda mrefu, kisha nikasema, “Una uzoefu mwingi na ufahamu fulani wa utendaji.”

Nilihisi wasiwasi baada ya kusema hivi. Niliweza kuona matatizo yake waziwazi lakini sikumwambia chochote kuyahusu. Badala yake, nilisema tu jambo zuri ambalo lilikuwa kinyume na dhamiri yangu. Hakukuwa na lolote la ukweli au la uaminifu kuhusu jambo hilo. Kisha nikawaza kuhusu mikutano yetu katika kipindi hicho cha wakati ambapo kila mtu alishiriki ushirika. Tulitakiwa kutafakari na kujifahamu sisi wenyewe kila siku, kuona tulikuwa tumesema uwongo au kuficha ukweli kiasi gani, ni mambo mangapi tulikuwa tumeyasema yaliyosababishwa na malengo ya kibinafsi, na ni mambo gani tuliyokuwa tumeyasema au kuyafanya ambayo yalikuwa kinyume na ukweli. Niligundua kuwa nilikuwa nimemdanganya tu Ndugu Chen. Nilijua kuwa Mungu hutusihi tena na tena tuwe waaminifu, tuseme waziwazi, na kusema ukweli bila kuficha chochote kibaya. Na bado, sikuweza kutenda masharti haya ya msingi kabisa. Kufikia wakati huo, nilianza kukasirika. Nilikwenda mbele za Mungu bila kupoteza wakati kumwomba Aniongoze ili nijifahamu. Kisha nikasoma maneno haya ya Mungu: “Ninyi nyote mna elimu nzuri. Ninyi nyote hutilia maanani kusafishwa na mnajizuia katika kusema, na vilevile kwa namna ambavyo mnazungumza: Ninyi ni wenye busara, na mmejifunza kutoathiri kujiheshimu kwa wengine na hadhi yao. Katika maneno na vitendo vyenu, mnawaachia watu nafasi ya kusonga. Mnafanya kila muwezalo ili kuwatuliza watu. Hamfunui makovu au mapungufu yao, na mnajaribu msiwaumize au kuwaaibisha. Watu wengi hutenda kulingana na kanuni kama hizi. Na hii ni kanuni ya aina gani? Ni kula njama, ujanja, ulaghai, na kudhuru kwa siri. Mambo maovu, ya kudhuru kwa siri na ya kustahili dharau yamefichwa nyuma ya nyuso za watu zenye tabasamu. Kwa mfano, wanapoingiliana na wengine, mara tu wanapoona kwamba mtu huyo mwingine ana hadhi kiasi, baadhi ya watu wataanza kuzungumza kwa njia nyororo, yenye sauti nzuri, yenye kujipendekeza ili kumfanya mtu huyo mwingine aridhike. Lakini, je, kweli hilo ndilo wanalofikiria? Bila shaka wameficha dhamira na nia mbaya. Watu kama hao wana uovu mioyoni mwao na ni wenye kustahili dharau sana. Njia ambayo watu kama hao hutenda maishani ni ya kuudhi na kuchukiza(“Ishara Sita za Ukuaji katika Maisha” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Maneno ya Mungu yalifichua hali halisi niliyokuwamo. Sikuwa mwaminifu katika maneno yangu hata kidogo, bali nilikuwa mjanja sana. Nilizungumza kwa kuzungukazunguka ili nisije kuwasononesha watu, na nilisema mambo mazuri daima. Kutoka nje, ilionekana kana kwamba nilikuwa nikiwajali wengine, lakini nia zangu halisi zilikuwa kuwafanya wengine wanisifu na kulinda heshima na hadhi yangu. Kutokana na kusikiliza aliyoyapitia, nilijua vyema kwamba Ndugu Chen alikuwa akifuata sheria kupita kiasi, na nilijua kuwa jambo hili halikusaidia katika kuingia kwake katika uzima. Lakini nilifikiri kwamba kutaja jambo hili kungemwaibisha na kumpa picha mbaya kunihusu, kwa hivyo nilinyamaza. Hata aliponiomba mapendekezo, bado sikuwa wazi. Badala yake nilimsifu mno na kumdanganya tu. Nilikuwa mjanja na mdanganyifu mno! Ndugu Chen alitusihi tutaje dosari zake kwa kuwa alitaka kufidia upungufu wake na dosari zake, lakini mbali na kushindwa katika jukumu langu kumsaidia, pia nilimsifu tu ili kumdanganya na kumhadaa. Wakati huo tu ndipo nilipogundua, kuwa nilionekana mzuri na mwenye busara, na hakuna aliyekosewa, lakini nilipokabiliwa na tatizo sikutenda ukweli. Hiyo kwa kweli haikuwa kuwa mtu mzuri hata kidogo, bali ilikuwa kuwa mjanja na mdanganyifu. Nilikuwa nikifikiri kuwa nilikuwa mchanga na asiye na uzoefu, kwamba sikujua njia za ulimwengu. Ni wakati tu ambapo nilifunuliwa na ukweli ndipo niliona kwamba kwa kweli nilikuwa mjanja sana, na nikaanza kujichukia. Sikutaka kuwa mdanganyifu sana na asiye mwaminifu tena. Kisha nikamwomba Mungu, nikiwa tayari kutubu, kusema ukweli na kuwa mtu mwaminifu kama Anavyotaka.

Nilipanga kuandika matatizo niliyokuwa nimegundua kwa Ndugu Chena na kumtumia, lakini nilipokuwa nikiandika nilisita tena. Nilikuwa na wasiwasi kwamba sikuwa nikieleza mambo kwa maneno yanayofaa, kwamba hangeyapenda, na kwamba angedhani kwamba nilikuwa nikisisitiza tofauti ndogondogo sana. Zaidi ya hayo, kwa kuwa sikuwa nimetaja jambo hilo wakati huo, iwapo ningelalamika sasa, je, angedhani kuwa nilikuwa nikilalamika bure? “Labda sipaswi kufanya chochote wakati huu,” niliwaza, “lakini wakati ujao nitoe mawazo bila kusita.” Lakini wazo hilo liliniacha nikiwa nimekasirika tena. Mungu hakuwa amepanga hali hii kwa ajili tu ya ufahamu wangu mwenyewe pekee. Alikuwa akitarajia kwamba nitakubali maneno Yake na kuyatia katika vitendo. Kama tu ningekubali kushindwa na kuacha mambo yaliyvo, je, huko hakungekuwa kumdanganya Mungu? Nilimwomba Mungu tena, nikisema “Sitaki kuwa na wasiwasi juu ya majisifu ya Ndugu Chen tena, au kuwazia kile ambacho wengine wanaweza kufikiri kunihusu. Tafadhali Mungu, niongoze nitende ukweli.” Baadaye, nilitafakari kuhusu tukio la Ndugu Cheng na kuliunganisha na maneno ya Mungu. Niliandika matatizo ambayo nilikuwa nimeyaona na ufahamu wangu mdogo na kuyatuma kwa Ndugu Chen. Nilitulia zaidi nilipotenda kwa njia hiyo. Nilipokea jibu kutoka kwa Ndugu Chen siku iliyofuata. Alisema kuwa aliguswa sana aliposoma barua yangu, na kuwa kumwandikia kuhusu matatizo yake kulikuwa kumetokana na upendo wa Mungu. Aligundua kuwa hakuwa amelenga kutafuta ukweli maswala yalipoibuka, na kuwa alipopogolewa na kushughulikuwa, alikuwa tu amepitia hayo kwa kubahatisha. Aliandika kwamba alikuwa tayari kurekebisha makosa yake katika jinsi alivyopitia mambo. Nilipomaliza kusoma jibu lake, niliguswa sana. Nilihisi kuwa sikuhitaji kuwa na wasiwasi sana katika mwingiliano wangu na kina ndugu. Nilipaswa tu kuwa na nia sahihi kama chanzo cha kutaja tatizo, na kisha watakuwa tayari kulikubali. Wasiwasi wangu wote ulikuwa wazo langu, na nilikuwa nimedhibitiwa na tabia yangu potovu. Pia nilikuja kuelewa kwamba mahusiano katika kanisa hayategemei falsala za kuishi au hila danganyifu, lakini yanajengwa kwa kutia maneno ya Mungu katika vitendo na uaminifu wa pande mbili.

Lakini nilikuwa nimepotoshwa sana na Shetani na tabia yangu potovu ilikuwa imekita mizizi kabisa kiasi kwamba hadhi yangu na masilahi yangu yalipohatarishwa, niliona vigumu kutenda ukweli.

Muda fulani baadaye, niligundua kuwa dada mmoja mdogo alisoma riwaya za mtandaoni mara kwa mara. Nilisisimka na kuwaza, “Hizi riwaya nyingi za mtandaoni ni hadithi tu za kubuniwa na wanadamu. Zikijaa akilini mwake, hatataka kusoma maneno ya Mungu au kutekeleza wajibu wake. Kisha, atapoteza kazi ya Roho Mtakatifu, na hilo litakuwa hasara kubwa sana katika maisha yake. Lazima nimwambie kuhusu suala hilo.” Lakini nilipokuwa tu karibu kuzungumza, nilisita: “Je, atafadhaika na kufikiri kuwa ninaingilia mambo yasiyonihusu? Asipokubali ninachokisema, basi litakuwa jambo la kufedhehesha kuonana kila siku. Labda ninapaswa kuripoti jambo hili kwa kiongozi wa kanisa na kumwacha kiongozi huyo ashiriki kuhusu jambo hilo pamoja naye.” Lakini nilijua kuwa wazo hili halikuwa sahihi. Nilikuwa na jukumu la kushiriki pamoja naye kuhusu jambo hili kwa sababu mimi ndiye niliyekuwa nimeligundua. Sikupaswa tu kukwepa wajibu na kumpa mtu mwingine. Nilifikiria kumdakizia suala hilo mara kadhaa baada ya hapo, lakini kila wakati sikuweza kuzungumza, na sikujua pa kuanzia. Hili liliendelea siku baada ya siku hadi siku moja kiongozi wa kanisa akaniuliza kuhusu hali ya dada huyo. Ni wakati huo tu ndipo nilimweleza kiongozi huyo kuhusu jambo hili. Kwa mshangao wangu, kiongozi huyo alisema kuwa alikuwa akishughulikia jambo lingine na aliniomba nishiriki pamoja na dada huyo. Niligundua kuwa Mungu alikuwa Akipanga hali hii kwa ajili yangu ili Aone iwapo nitaukana mwili wangu na kutenda ukweli. Niliwaza kuhusu jinsi nilivyokuwa na wasiwasi kwa muda. Hususa nilipomwona dada huyo, nilisumbuka kwa ajili ya kutozungumza naye. Sikuwa nimemwonyesha upendo au kuchukua jukumu, na dhamiri yangu ilikuwa ikiteseka. Nilifahamu vizuri sana hatari za kupenda sana riwaya za mtandaoni. Ibilisi Shetani hutumia mitindo hii miovu kuwadanganya na kuwapotosha watu, kudhibiti mawazo yao na kuwafanya wamwepuke Mungu, ili kwamba wazidi kupotoka na kuvunjwa moyo, hadi mwishowe awaangamize. Sikuwa nimetafakari hata kidogo jinsi maisha ya dada huyo yangeweza kuharibika, au kuhusu jinsi kukanganywa kwake katika wajibu wake kungesababisha madhara makubwa katika kazi ya kanisa. Niliogopa kutaja jambo hilo na kumkosea, na nilikuwa mwangalifu katika matamshi yangu ili nidumishe uhusiano wetu. Nilikuwa mbinafsi na mwenye kustahili dharau sana!

Kisha nikasoma maneno haya ya Mungu: “Watu wengi huamini kwamba kuwa mtu mzuri ni rahisi kweli na kunahitaji tu kusema machache na kufanya mengi, kuwa na moyo mzuri na kutokuwa na nia yoyote mbaya. Wanaamini kwamba hili litahakikisha kwamba watafanikiwa popote waendapo, kwamba watu watawapenda, na kwamba kuwa mtu wa aina hiyo tu kunatosha. Hata wanafika kiwango cha kutotaka kufuatilia ukweli; wanaridhika na kuwa watu wazuri tu. Wanafikiri kwamba suala la kufuatilia ukweli na kumtumikia Mungu ni tata mno; wanafikiri linahitaji kuelewa ukweli mwingi, na ni nani anayeweza kufanikisha hilo? Wanataka tu kuchukua njia rahisi zaidi—kuwa watu wazuri na kufanya wajibu wao—na wanafikiri kwamba hilo litatosha. Je, hali hii inaweza kutimizwa? Je, kwa kweli ni rahisi sana kuwa mtu mzuri? Mtawapata watu wengi wazuri katika jamii wakizungumza kwa njia ya kujidai sana, na hata ingawa kwa nje wanaonekana kutofanya uovu wowote mkubwa, mioyoni mwao, wao ni wadanganyifu na walaghai. Hasa, wanaweza kuona mambo yalivyo kwa kweli, na lugha yao ni nyororo na ya kidunia. Kama Nionavyo, ‘mtu mzuri’ kama huyu ni wa uongo, mnafiki; mtu kama huyu anajifanya tu kuwa mzuri. Wale wote ambao hushikilia furaha ya kati ndio waovu zaidi. Wao hujaribu kutomkosea yeyote, ni watu wa kuwafurahisha watu, wanafuata mambo, na hakuna mtu anayeweza kuwaelewa. Mtu kama huyo ni Shetani aliye hai!(“Ni kwa Kuweka Ukweli Katika Vitendo Tu Ndipo Unaweza Kutupa Minyororo ya Tabia Potovu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Maneno ya Mungu yalipenya moyoni mwangu kwa kuwa niliona kwamba nilikuwa mtu “mzuri” ambaye daima alikubaliwa na wengi, hajawahi kumkosea yeyote, na hajawahi kutaja tatizo lolote la mtu yeyote, na ni hasa kile ambacho maneno ya Mungu yalifichua. Iwapo ningesema chochote, ingenilazimu nizingatie ni nani niliyekuwa nikizungumza naye na hali ilivyokuwa. Sikuwahi kudhuru urafiki au kumruhusu yeyote kupata dosari kwangu. Nilikuwa nimeona kwamba dada huyu alikuwa na tatizo na nilitaka kumwambia kuhusu jambo hilo, lakini mara nilipofikiri kuwa hilo lingemkosea, niliepa kufanya hivyo mara kwa mara, badala yake nikakwepa wajibu na kumpa kiongozi wa kanisa. Niligundua kuwa nilikuwa nikijijali tu, kwamba niliwatwisha wengine kazi za kuleta ugomvi, na kwamba sikutaka masilahi yangu yadhuriwe kwa vyovyote vile. Hivyo ndivyo nilivyokuwa nikiwatendea ndugu zangu. Wakati mwingine nilipoona kwamba mtu fulani alikuwa katika hali mbaya au alifichua upotovu, nilijifanya kutoona, na nikakosa kulitaja au kushiriki kulihusu. Kijuujuu, nilionekana kuelewana vyema na kila mtu. Nilionekana mwenye kuwajali wengine sana. Lakini yote yalikuwa uongo, yalikuwa kujifanya. Nilificha maneno yangu ya kweli na ya dhati, kwa kuvalia tu sura ya kinafiki. Nilikuwa mnafiki sana! Niliwadanganya ndungu zangu waziwazi na bado niliwataka waniheshimu. Sikuwa na haya kabisa! Niliona kwamba nilikuwa tu bwana ndiyo mwenye kudhuru kwa siri na wa kudanganya, na mtu bandia.

Kisha nikasoma maneno mengine zaidi ya Mungu: “Mpaka watu wawe wamepitia kazi ya Mungu na kupata ukweli, ni asili ya Shetani inayotwaa madaraka na kuwatawala kwa ndani. Ni nini, hasa, kilicho ndani ya asili hiyo? Kwa mfano, kwa nini wewe ni mchoyo? Kwa nini wewe hulinda nafasi yako mwenyewe? Kwa nini una hisia kali sana namna hiyo? Kwa nini unafurahia hivyo vitu visivyo vya haki? Kwa nini unapenda maovu hayo? Msingi wa kupenda kwako vitu hivi ni upi? Mambo haya hutoka wapi? Kwa nini unafurahia sana kuyakubali? Kufikia sasa, nyote mmekuja kuelewa kwamba sababu kuu ya mambo haya yote ni kwamba sumu ya Shetani iko ndani yenu. Kuhusu sumu ya Shetani ni nini, inaweza kuelezwa kwa ukamilifu kwa maneno. Kwa mfano, ukiwauliza baadhi ya watenda maovu kwa nini walitenda jinsi walivyotenda, watajibu, ‘Kwa sababu kila mwamba ngoma huvutia upande wake.’ Msemo huu mmoja unaonyesha asili ya shida. Mantiki ya Shetani imekuwa maisha ya watu. Wanaweza kutenda mambo kwa ajili ya madhumuni fulani au mengine, lakini wanajifanyia tu. Kila mtu hudhani kwamba kwa kuwa ni kila mwamba ngoma huvutia upande wake, watu wanafaa kuishi kwa sababu yake mwenyewe tu, na kufanya kila awezalo kupata wadhifa mzuri kwa ajili ya chakula na mavayi mazuri. ‘Kila mwamba ngoma huvutia upande wake’—haya ndiyo maisha na falsafa ya mwanadamu, na pia inawakilisha asili ya binadamu. Maneno haya ya Shetani ni sumu ya Shetani hasa, na watu wanapopoiweka moyoni, inakuwa asili yao. Asili ya Shetani hufunuliwa kupitia maneno haya; yanamwakilisha yeye kabisa. Sumu hii inakuwa maisha ya watu pamoja na msingi wa kuwepo kwao; na wanadamu waliopotoshwa wametawaliwa kwa uthabiti na sumu hii kwa maelfu ya miaka(“Jinsi ya Kuitembea Njia ya Petro” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Maneno haya yalinipa ufahamu fulani kuhusu sababu kuu ya kuwa bwana ndiyo, ambayo ilikuwa hasa kwamba falsafa na sumu za Shetani zilikuwa zimefanywa madhubuti ndani yangu kabisa. Baada ya kupotoshwa na mambo kama vile “Kila mtu ajali maslahi yake kwanza, bila kuwafikiria wengine.” “Kufumbia macho kasoro za marafiki hudumisha urafiki” na “Zungumza maneno mazuri kwa kuambatana na hisia na mantiki ya wengine, kwa kuwa kusema ukweli huwaudhi wengine,” Nilifikiri tu kuhusu sifa yangu njema na hadhi yangu. Niliwataka wengine waseme mazuri kunihusu katika kila jambo nililolifanya na nikawa mbinafsi, mjanja, na mdanganyifu sana. Tangu nilipokuwa mchanga mama na baba yangu waliniambia kila mara kwamba nisikilize zaidi kuliko kuzungumza, na kadiri nilivyosema machache, ndivyo ilivyokuwa vyema. Waliniambia nisiwe mnyoofu sana kwa wengine kwa kuwa hawatapenda. Nilikuwa nikiishi kulingana na falsafa hizi za kishetani na nilikuwa mnyoofu na mwaminifu kwa watu wengine mara chache sana. Hata kwa rafiki yangu mkubwa. nilitoa hisia zangu waziwazi kutaja makosa yao mara chache sana, nikiogopa kuwakasirisha na kuharibu taswira waliyo nayo kunihusu. Badala yake, niliona heri nifuatane na walichohisi na kuwasifu, lakini yote yalikuwa uwongo, yote yalikuwa unafiki! Niligundua kuwa kuishi kulingana na falsafa hizi za kishetani maishani mwote kunaweza tu kunifanya niwe mwongo, mjanja, mbinafsi na mbaya sana. Nilijali tu kuhusu masilahi yangu na sikujali kuhusu wengine hata kidogo. Sikuwa mnyofu kwa watu na sikuwapenda. Mtu kama mimi hangeweza kumsaidia au kumnufaisha yeyote katika njia yoyote kabisa, na sikufaa kabisa kuhusiana na yeyote. Niliona kwamba falsafa hizi za kishetani zilikuwa za kipumbavu kwa kweli na kwamba hazikupaswa kamwe kuwa kanuni za mwenendo. Niliona kwamba kuishi kulingana na falsafa hizi za kishetani maishani mwote kunaweza kutufanya tuwe wapotovu zaidi, na wenye kukosa ubinadamu zaidi. Niliwaza jinsi ambavyo kila mara nilipoona tatizo sikusema lolote, nilihisi mwenye hatia baadaye, na kana kwamba kulikuwa na jiwe moyoni mwangu ambalo sikuweza kuondoa. Nilihisi kama nilijua ukweli lakini sikuweza kuutia katika vitendo. Nilikuwa mwoga sana, bila heshima au uaminifu wowote. Katika umri wangu, bado sikuweza kuwa mtu wa heshima, na sikujua kanuni za mwingiliano wa wanadamu. Badala yake, nilifuatilia njia za kidunia zinazofunzwa na kuenezwa na Shetani. Nilijichukia sana wakati huo. Sikutaka kuishi kulingana na falsafa hizi za kishetani tena. Nilitaka tu kufanya na kutenda kulingana na maneno ya Mungu.

Kisha nikasoma maneno haya ya Mungu: “Je, kitendo kipi ndicho muhimu zaidi cha kuwa mtu mwaminifu? Ni kwamba moyo wako lazima uwe wazi kwa Mungu. Namaanisha nini kwa kusema ‘uwe wazi’? Inamaanisha kumwonyesha Mungu mtazamo dhahiri kabisa wakila kitu unachofikiria, dhamira zako ni zipi, na ni nini kinachokudhibiti. Ikiwa kile unachosema ni kile kilicho moyoni mwako, bila tofauti hata kidogo na bila kuficha chochote, bila uovu wowote, bila wengine kulazimika kukisia au kuchunguza zaidi kwa kuuliza maswali, na bila wewe kuhitaji kusema kwa njia isiyo ya moja kwa moja, badala yake kusema tu kile unachofikiria, bila dhamira nyingine yoyote, basi hili linamaanisha kuwa moyo wako uko wazi. Wakati mwingine unyofu wako unaweza kuwaumiza wengine na kuwakera. Hata hivyo, kuna yeyote anayeweza kusema, ‘Unazungumza kwa njia ya uaminifu sana na umeniumiza sana; siwezi kukubali uaminifu wako’? Hapana; hakuna anayeweza kusema hivyo. Hata ikiwa unawumiza watu mara kwa mara, kama unaweza kuwazungumzia kwa wazi na uwaombe msamaha, ukubali kwamba ulizungumza bila hekima na hukujali udhaifu wao, wataona kuwa huna chuki, kwamba wewe ni mtu mwaminifu, na kwamba wewe tu hutilii maanani namna unavyozungumza na wewe ni mnyofu tu; hakuna atakayekulaumu kwa sababu ya hili. … Sehemu muhimu zaidi ya kuwa mtu mwaminifu ni kwamba moyo wako lazima uwe wazi kwa Mungu. Baadaye, unaweza kujifunza kujiweka wazi kwa watu wengine, kuzungumza kwa uaminifu na kwa kweli, kusema kilicho moyoni mwako, kuwa mtu mwenye heshima, uadilifu, na unyoofu, na kutozungumza maneno matupu au uwongo au kutumia maneno kujificha au kuwadanganya wengine(Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Nilipokuwa nikitafakari maneno ya Mungu, niliguswa sana. Nilihisi kwamba Mungu alikuwa amenichukua kwa mkono ili Anifunze jinsi ya kutenda kama mwanadamu. Kuwa mtu mwaminifu, kuzungumza na kutenda kwa uaminifu, kutoa hisia zangu kabisa kwa Mungu, kuwa mnyoofu kwa kina ndugu, na kutolazimika kuwa namna fulani au kucheza shere—kuishi kwa njia hii hakuchoshi. Nilimtajia dada huyo tatizo lake baadaye. na kushiriki naye kuhusu hatari za kupenda sana riwaya za mtandaoni. Mwanzoni, alionekana mwenye huzuni sana, na hali ilikuwa ngumu kiasi tu. Lakini kwa kutoa hisia zangu na kushiriki naye, alikuja kugundua kuwa alikuwa katika hali hatari. Alisema kwamba hatasoma riwaya za mtandaoni tena na atamakinikia wajibu wake. Nilipomsikia akiyasema haya, hatimaye niliweza kushusha pumzi, lakini pia nilijilaumu. Kama ningezungumza mapema basi pengine hali yake ingerekebishwa mapema. Ilikuwa tu kwa sababu nilitaka kuwa wa maridhia kila mara kwamba sikuwa nimeukana mwili wala kutenda ukweli, na mambo yalikuwa yameendelea vivyo hivyo. Kuwa bwana ndiyo kunadhuru sana. Baada ya hayo, nilipoona tatizo katika wajibu wa kina ndugu, wakati mwingine bado niliona wasiwasi kuhusu kuwakosea, lakini kwa kumwomba Mungu, kutenda ukweli kwa uzingatifu na kuwa mtu mwaminifu, niliweza kila mara kutaja tatizo kwa kweli baadaye. Ni kwa mwongozo tu wa maneno ya Mungu ndiyo niliweza kujifunza jinsi ya kutenda na kuingiliana na kina ndugu. Nilitambua hasa jinsi maneno ya Mungu yalivyo ya thamani. Hayo ndiyo kanuni za mwenendo wetu na matendo yetu. Ikiwa ni katika wajibu au mwenendo wetu, tutahitaji maneno ya Mungu yatuongoze kila mara. Mradi tutafute ukweli tatizo linapoibuka, basi tutapata njia ya kufuata.

Nikikumbuka hapo nyuma, nilikuwa nikikubali katika nadharia kwamba nilikuwa bwana ndiyo na kwamba nilikuwa mdanganyifu, lakini sikuwahi kujilinganisha na maneno ya Mungu kwa dhati ili kuchunguza na kuchambua tabia yangu potovu. Pia nilitafuta njia ya kutenda au kanuni kutoka kwa maneno ya Mungu mara chache sana, kwa hivyo tabia yangu ya ubinafsi na ya udanganyifu haikubadilika hata kidogo. Ingawa nimepitia tu baadhi ya masuala madogo maishani, ninapolenga kujichunguza na kutafuta ukweli katika maneno ya Mungu, mimi huvuna na kupata ufahamu fulani. Pia mimi huhisi amani halisi ya nafsi na kupata njia kidogo ya kuingia katika uzima. Kupata ufahamu huu na kuvuna mavuno haya ni kwa sababu tu ya mwongozo wa maneno ya Mungu!

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mimi Sistahili Kumwona Kristo

Huanbao Mji wa Dalian, Mkoa wa Liaoning Tangu kwanza nianze kumwamini Mwenyezi Mungu, daima nimewapenda wale ndugu wa kiume na wa kike...

Kuibuka Kutoka Kwenye Ukungu

Zhenxi Jijini Zhenzhou, Mkoani Hena Miaka kumi iliyopita, nikiendeshwa na asili yangu ya kiburi, sikuweza kamwe kutii kikamilifu...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp