Mabadiliko ya Mwigizaji

25/08/2020

Mwenyezi Mungu anasema, “Kama mojawapo ya viumbe, lazima mwanadamu achukue nafasi yake mwenyewe, na ajiendeleze kwa uangalifu, na kulinda kwa wajibu kile ambacho ameaminiwa na Muumba. Naye binadamu lazima asitende mambo nje ya mipaka yake au kufanya mambo zaidi ya uwezo wake au kufanya mambo ambayo ni ya kuchukiza Mungu. Binadamu ni lazima asijaribu kuwa mkubwa, au wa kipekee, au zaidi ya wengine, wala asitafute kuwa Mungu. Hivi ndivyo watu hawafai kutamani kuwa. Kutamani kuwa mkubwa au wa kipekee ni jambo la upuuzi. Kutafuta kuwa Mungu ndilo hata jambo la aibu zaidi; linaudhi na linastahili kudharauliwa. Kile cha kupongezwa, na ambacho viumbe vinastahili kushikilia kuliko chochote kile ni kuwa viumbe vya kweli; hii ndiyo shabaha pekee ambayo watu wote wanafaa kufuatilia(Neno Laonekana katika Mwili).

Mnamo Mei 2016, nilikuwa nikiigiza katika filamu ya kanisa. Niliheshimiwa sana kupangiwa dhima ili nifanye wajibu wangu katika filamu za kanisa ili kusaidia kueneza maneno ya Mungu na kushuhudia kazi Yake kwa njia hiyo ili wale wanaomtamani Mungu sana waweze kusikia sauti Yake na kuokolewa. Nilipopata nafasi ya mhusika mkuu katika filamu fupi niliyokuwa nimeifanyia majaribio, nilifurahia na nilisisimka sana. Ilikuwa mara yangu ya kwanza kuwa mhusika mkuu. Nilijua kwamba kama ningekuwa hodari, kila mtu kanisani angeanza kunistahi. Huku nikiazimia kufanya vyema kadiri nilivyoweza, nilianza kufanya kazi mara moja. Nilipokuwa na tatizo kuuigiza mstari fulani, nilimwambia mwigizaji mwenye uzoefu zaidi ausome, kisha nilirudia alichosema. Wakati ambapo mwondoko wangu haukuwa sawa, nilimwambia mtu mwingine anionyeshe, halafu nilifanya mazoezi tena na tena. Wakati mwingine hata nilikaa macho usiku kucha na sikuchoka. Nilijitahidi sana, halafu kina ndugu wengine wakanijia wakaniambia baada ya onyesho la awali la filamu, “Ulifanya kazi nzuri katika filamu hiyo fupi.” Waliposema hayo, yalizidisha majisifu yangu kweli. Karibu nihisi kama kwamba nilikuwa maarufu, kana kwamba nilikuwa mtu fulani mashuhuri. Lakini nilishangaa mwelekezi aliponiambia kwamba upigaji picha ulihitaji kufanywa upya kwa ajili ya sababu mbalimbali. Nili nilivunjika moyo sana. “Kufanywa upya? Sasa mimi ni mwigizaji wa ziada katika filamu tofauti ya kanisa, filamu ya injili. Mswada wa filamu hiyo fupi ukihaririwa na ratiba zigongane, bado nitaigiza kama mhusika mkuu?” Lakini nikawaza baadaye kwamba kwa kuwa kila mtu alipenda uigizaji wangu, ni mimi tu ndiye niliyefaa kuigiza nafasi hiyo. Siku chache zilipita na nikasikia kwamba mswada ule ulikuwa umesahihishwa, lakini hakuna mtu aliyenialika kwenye mandhari ya upigaji picha za filamu. Nilikuwa na wasiwasi sana. Niliangalia simu yangu ili kuona ujumbe mara nilipofungua macho yangu kila asubuhi, nikitumaini kwamba mtu fulani alikuwa amenitumia ujumbe. Lakini pia niliogopa kuwa ningefungua simu yangu na kusoma kwamba walimpangia dhima mhusika mwingine. Kila nilipopata ujumbe, nilifadhaika sana, nikiogopa kuwa nitabadilishwa na mwigizaji mwingine. Katika siku hizo kadhaa, sikuweza kulenga chochote nilichokuwa nikifanya na sikuweza kuzingatia upigaji picha wa filamu hiyo ambayo tayari nilikuwa nikiigiza. Sikuweza kabisa kungojea tena na sikujali jinsi filamu hiyo ya injili ilivyokuwa ikiendelea. Niliwasiliana na msimamizi wa wahusika wa filamu fupi, nikisema kwamba ningeweza kufanya hivyo. Lakini siku chache baadaye alinitumia ujumbe kwamba walikuwa wamempangia Dada Zhao awe mhusika mkuu kwa hivyo filamu ya injili ambayo nilikuwa nikiigiza haikuhitaji kusitishwa. Nilihisi kwamba nilikuwa nimekosewa sana. Nilitia juhudi zangu zote katika kuigiza nafasi hiyo na nilitumia muda wangu mwingi sana kwa ajili ya filamu hiyo. Kwa nini nilinyang’anywa, wakati ambapo mswada uliosahihishwa ulikuwa hapo na karibu nafasi hiyo iwe yangu? Sikuweza kabisa kukubali hayo. Nilijificha bafuni kwa muda mrefu na kulia. Kisha wazo baya likanijia akilini: “Dada Zhao asipoweza kuigiza nafasi hiyo, basi ninaweza kupata nafasi” Nilijua kwamba kufikiri hivyo hakukuwa sawa, lakini sikuweza kujizuia. Nilihisi vibaya sana. Walimaliza kupiga upya picha za filamu baada ya muda mfupi. Na kila mtu akasema kwamba filamu hiyo mpya ilikuwa bora zaidi. Kiongozi alisema kwamba ilikuwa yenye uhalisi zaidi na ilijawa na mwongozo wa Mungu, na alitaka sote tujifunze mambo kutokana nayo. Sikuweza kujizuia kujilalamikia, “Kwa nini upigaji picha wao ulienda vizuri sana, lakini wangu ulikuwa na matatizo? Kwa nini hawakuweza kupanga ratiba ili niweze kuwa mhusika mkuu katika filamu hiyo?” Niliona wivu sana na nikamkasirikia Dada Zhao. Sikutaka kumwona. Nilihisi kana kwamba alikuwa ameniibia sifa yangu. Niliteswa na umaarufu na kuutamani sana kiasi kwamba nilihisi kama kwamba sikuweza kupumua. Nilikuwa mwenye wasiwasi mno. Nilimwomba Mungu kila siku, nikimsihi Anisaidie ili niweze kushinda maumivu yote na ukataji tamaa.

Wakati mmoja, nilisoma kifungu cha maneno ya Mungu katika ibada zangu ambacho kilinigusa na kunifadhaisha. Maneno ya Mungu yanasema, “Mara tu inapogusia cheo, sura au sifa, moyo wa kila mtu huruka kwa matazamio, na kila mmoja wenu daima hutaka kujitokeza, kuwa maarufu, na kutambuliwa. Watu wote hawataki kushindwa, bali daima wanataka kushindana—hata ingawa kushindana kunaleta fedheha na hakukubaliwi katika nyumba ya Mungu. Hata hivyo, bila kupinga, bado huridhiki. Unapomwona mtu fulani akitokeza, unahisi wivu, chuki, na kuwa hiyo si haki. ‘Mbona nisitokeze? Mbona kila mara ni mtu huyo anayetokeza, na hauwi wakati wangu kamwe?’ Kisha unahisi chuki fulani. Unajaribu kuizuia, lakini huwezi. Unamwomba Mungu na unahisi nafuu kwa muda, lakini punde unapokumbana na hali ya aina hii tena, huwezi kulishinda. Je, hii haionyeshi kimo kisicho komavu? Je, si mtu kuanguka katika hali hizi ni mtego? Hizi ndizo pingu za asili potovu ya Shetani ambazo huwafunga wanadamu. … Ikiwa unataka kugeuza hali hii, na usidhibitwe na vitu hivi, basi lazima uviweke kando kwanza na kuviacha. Vinginevyo, kadiri unavyong’ang’ana, ndivyo giza litakuzingira zaidi, na ndivyo utakavyohisi wivu na chuki, na hamu yako ya kupata itaongezeka na kuongezeka tu. Kadiri hamu yako ya kupata ilivyo kuu, ndivyo utakaavyopunguza kuweza kufanya hivyo, na unapopata kidogo chuki yako itaongezeka. Chuki yako inapoongezeka, utakuwa mbaya zaidi. Kadiri ulivyo mbaya ndani yako, ndivyo utakavyotekeleza wajibu wako vibaya zaidi; kadri unavyotekeleza wajibu wako vibaya, ndivyo utakuwa mwenye manufaa kigogo zaidi. Huu ni mzunguko mwovu uliofungamana. Ikiwa huwezi kamwe kutekeleza wajibu wako vizuri, basi, utaondolewa polepole(Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Maneno ya Mungu yalinionyesha jinsi nilivyohisi hasa. Nilikuwa nikijaribu tu kuwa mashuhuri sana tangu nilipokuwa mwigizaji wa filamu za kanisa. Mara nilipopata nafasi ya mhusika mkuu katika filamu hiyo fupi nilitaka tu kuwa maarufu, kwa hivyo sikuwahi kulalamika, bila kujali mambo yalikuwa magumu kiasi gani. Nilipoambiwa kwamba upigaji picha ungerudiwa, niliogopa kwamba ningebadilishwa na mwigizaji mwingine, na niliishi katika woga na wasiwasi kila wakati. Sikuwa na shauku ya kufanya wajibu wangu tena. Nilipopoteza fursa yangu ya kuigiza nafasi hiyo, na ndoto yangu ya umaarufu ikavunjika, sikuweza kabisa kukubali hayo na nilimlaumu Mungu na mwanadamu. Nilimwoea wivu sana mhusika aliyechukua nafasi yangu na nilimwazia mabaya mengi sana. Nilitumaini asiweze kuigiza filamu hiyo ili niweze kuwa mhusika mkuu tena. Kila mtu alifurahia marudio ya upigaji picha na jinsi filamu hiyo ilivyotokea, lakini sikuweza kabisa kukubali hayo yote, na niliwazia hayo sana na nikawa mwenye wivu, uchungu na hasira hata zaidi. Sikuwa nikifanya wajibu wangu ili kuwa mzingatifu kwa mapenzi ya Mungu na kumshuhudia bali nilitaka tu kuwa maarufu na kupendwa na kila mtu. Nilikuwa tayari hata kuchelewesha upigaji picha za filamu ili bado niweze kuwa mhusika mkuu. Sikumheshimu Mungu hata kidogo. Mpaka maneno ya Mungu yaliponifanya nitambue jinsi nilivyostahili dharau, yote kwa ajili ya umaarufu na faida. Nilipoteza ubinadamu wangu, na jambo hili lilikuwa baya sana kwa Mungu. Nisingetubu kwa Mungu, nilijua kwamba Angeniondoa.

Baadaye, nilisoma maneno haya kutoka kwa Mungu: “Hisia za wanadamu ni za ubinafsi na zinamilikiwa na ulimwengu wa giza. Hisia hizo hazipo kwa ajili ya mapenzi, sembuse mpango wa Mungu, na kwa hiyo mwanadamu na Mungu hawawezi kamwe kuzungumziwa hapohapo. Mungu siku zote anayo mamlaka ya juu zaidi na ni mwenye heshima kila wakati, ilhali mwanadamu siku zote ni wa chini, siku zote asiye na thamani. Hii ni kwa sababu Mungu siku zote anajitolea mhanga na kujitoa Mwenyewe kwa wanadamu; mwanadamu, hata hivyo, siku zote huchukua na kujitahidi kwa ajili yake pekee. Siku zote Mungu anashughulikia kwa dhati kuendelea kuishi kwa wanadamu, ilhali mwanadamu kamwe hachangii kitu kwa ajili ya mwangaza au haki. Hata kama mwanadamu anajitahidi sana kwa muda, ni dhaifu sana kiasi cha kutoweza kustahimili dhoruba hata kidogo, kwani jitihada za mwanadamu siku zote ni kwa ajili yake mwenyewe na wala si kwa ajili ya wengine. Mwanadamu siku zote ni mbinafsi, huku naye Mungu siku zote si mwenye ubinafsi. Mungu ndiye chanzo cha vyote vilivyo vya haki, vyema, na vya uzuri, huku naye mwanadamu ni yule anayerithi na kudhihirisha vyote vyenye sura mbaya na vyenye maovu. Mungu hatawahi kubadilisha dutu Yake ya haki na uzuri, ilhali mwanadamu anaweza kabisa, wakati wowote, kusaliti haki na kupotoka kutoka kwa Mungu(Neno Laonekana katika Mwili). Niliposoma maneno haya kutoka kwa Mungunilifadhaika sana. Niliona jinsi nilivyokuwa mbinafsi na mbaya kiasili. Mawazo yangu ya pekee yalinihusu mimi pekee. Nilitaka sana upigaji picha wa filamu iyo usifaulu, kwa sababu tu sikuweza kuwa mhusika mkuu katika filamu hiyo. Nilitumaini isionyeshwe. Hata kiongozi alipotusihi tujifunze jambo fulani kutokana nayo, hata sikujisumbua kuitazama. Mungu hujawa na furaha kanisa linapotoa filamu nzuri kwa sababu ukweli uliofanyiwa ushirika katika kila filamu unaweza kuwasaidia wale wanaotafuta njia ya kweli wapate njia ya kweli na kutatua matatizo yao. Unaweza kuwaletea mwangaza wale ambao wamenaswa gizani. Filamu zote zinasaidia sana. Mungu hufurahishwa na mambo mazuri ya kila aina. Sikuweza kupenda yale ambayo Mungu aliyapenda. Nilichukia kila kitu ambacho Alipenda, na nilipenda kila kitu ambacho Alichukia. Je, sikuwa basi nikimpinga Mungu? Je, nilikuwa hata muumini? Nilikuwa tu ibilisi aliyejificha ndani ya nyumba ya Mungu. Mtu asiyeamini. Nilichukia kwamba nilikuwa mbaya sana na niliomba maombi haya: “Ee Mungu, nilikosea. Nilitaka kusimamisha kazi Yako ili niwe maarufu. Mimi ni mwasi sana. Nataka kutubu, kuacha kujaribu kutafuta umaarufu na kuvuta nadhari. Nataka kutii mpango Wako na kufanya wajibu wangu vizuri.” Baadaye, nilisoma maneno kadhaa ya Mungu yaliyozungumza juu ya yale niliyokuwa nikiyapitia na nilielewa kwamba wajibu wetu ni jukumu tulilo nalo. Si fursa yetu ya kujionyesha au hata kuzidisha majisifu yetu, bali uko kwa ajili ya kutukumbusha tuwe wanyenyekevu na tumfanyie Mungu kazi kwa bidii. Iwapo kanisa litanipangia niwe mhusika mkuu au wa ziada, sharti nifanye kila niwezalo, bila kujali ni nafasi ipi, ili nisaidie kueneza ujumbe wa kazi ya Mungu ya siku za mwisho. Nilihisi uhuru nilipogundua haya yote. Nilifanya majaribio ya nafasi nyingine zaidi za mhusika mkuu katika filamu za kanisa, na sikupata yoyote, lakini niliyakubali yote bila taabu, na nikaigiza nafasi zangu vizuri.

Mara baada ya hapo, nilipata nafasi nyingine ya mhusika mkuu katika filamu ya kanisa. Nilishukuru sana na nilijiahidi kutotafuta umaarufu na kumfanyia Mungu wajibu wangu kwa utiifu. Mara nilipopata mswada hatimaye, nilianza kufanya kazi papo hapo, nikichambua mhusika huyo na kujifunza mistari yangu. Kisha ndugu zangu wakaniambia nijaribu mavazi kadhaa ya kuigiza na nionyeshe mitindo ya mavazi hayo. Nilipomwona kila mtu akinizingira, nilihisi kama kwamba nilikwezwa sana. Niliwaza “Kuwa mhusika mkuu ni kitu cha kipekee sana. Nikiigiza nafasi hiyo katika filamu hii vizuri, watu wengi zaidi watajua mimi ni nani na watanipenda sana.” Lakini nilipofikiria hayo niligundua kwamba nilianza tena kutamani sana umaarufuna hadhi yangu tena, kwa hivyo nilimwomba Mungu ili niyaache mawazo yangu ya ubinafsi. Lakini kwa kuwa sikuwa nimeelewa kikamilifu chanzo cha tatizo hilo bado sikuweza kujizuia kuwaza juu ya kuwa mashuhuri. Wakati huo huo, nilikuwa na wasiwasi sana. Sikuwa nimeigiza kama mhusika mkuu hapo awali, kwa hivyo uigizaji wangu haukuwa mzuri. Sikujua ningefanya nini iwapo ningebadilishwa na mwigizaji mwingine kwa sababu ya uigizaji mbaya. Hakuna mtu ambaye angetaka niigize tena. Ilinibidi nitie bidii ili kujifunza ujuzi wa kimsingi ili nifanye kazi nzuri katika filamu hiyo. Sikupaswa kupoteza nafasi yangu. Nilianza kwenda mtandaoni kila siku kutafuta video za uigizaji ili nitazame na kozi za mtandaoni ambazo ningejifunza kutokana nazo, na nilifanya kazi kwa bidii iliniweze kuwa mwigizaji bora na mhusika mkuu aliyefaa. Nilijaribu sana na nilitia juhudi nyingi sana lakini baada ya kumaliza maonyesho machache niliona kwamba uigizaji wangu haukulingana kabisa na mhusika niliyeigiza. Kujieleza kwangu hakukuwa na uhalisi. Mwelekezi alisema kwamba macho yangu hayakuvutia na maneno yangu kamwe hayakulingana na onyesho hilo. Niliona wasiwasi sana niliposikia haya yote kutoka kwake. Niligundua kwamba nilikuwa na kazi nyingi ya kufanya, na nisingeifanya kwa haraka, bila shaka ningebadilishwa na mwingine. Nilijaribu hata zaidi kufanya mazoezi, lakini kadiri nilivyozidi kujaribu, ndivyo nilivyozidi kuanza kuwa na matatizo. Niliigiza kila onyesho polepole sana. Nilipowaona wengine wote wakinitazama na niliposikia kushusha pumzi kwa mwelekezi nilihisi kama kwamba kulikuwapo na uzito ulionigandamiza na nilipumua kwa shida. Siku moja mwelekezi aliniambia, “Wajua, Dada Liu anafaa sana kucheza nafasi ya mhusika huyu.” Tazama anachofanya na ujaribu kumwiga.” Niliwaza, “Imekwisha. Nina hakika kwamba mwelekezi wangu anafikiria kwamba angeigiza vyema zaidi nafasi hii. Nisipofanya vizuri zaidi, atanibadilisha naye. Siwezi kabisa siwezi kupoteza nafasi hii. Nikishindwa wakati huu, kila mtu kanisani atajua kuwa mimi si mwigizaji hodari, kisha nitaigizaje tena nafasi ya mhusika mkuu? Nitakuwa tu mhusika wa ziada na sitawahi kuwa mashuhuri.” Nilizidi kuhisi kana kwamba nilikuwa karibu kupoteza kila kitu, na sikuweza kujizuia kuanza kujionyesha kwa mwelekezi wangu. Sikula chakula cha mchana, lakini badala yake, nilisoma vitabu vilivyohusu uigizaji na nilikaa mahali ambapo mwelekezi aliniona, na nikasoma mswada wangu. Nilimtupia jicho wakati ambapo hakuwa akitazama, na alipoonekana kuwa na furaha, nilitulia. Wakati ambapo sikuweza kujua mawazo yake, nilianza kujiuliza iwapo angenibadilisha na mwigizaji mwingine. Sikufikiria hata kumwambia kwamba sikuweza kufahamu kikamilifu hisia za mhusika nikiogopa kuwa angeniondoa kama angegundua kilichokuwa kikiendelea. Nilikuwa nikizidi kusogea mbali na Mungu. Nilikuwa nikianguka gizani. Nilijikaza kisabuni tu na kuendelea.

Wakati mmoja, kabla ya kwenda kupiga picha za onyesho fulani katika kituo cha treni, mwelekezi wangu alinieleza tukio hilo mara nyingi na akanifanya hata niliigize. Nilielewa onyesho hilo kidogo lakini sikuweza kuelewa hisia za mhusika niliyeigiza. Kwa kuwa niliogopa kwamba mwelekezi wangu angefikiria sikuweza kuelewa, nilijifanya tu kwamba nilielewa. Tulipoanza kupiga picha za filamu, sikuweza kabisa kuonyesha hisia zilizofaa. Baada ya saa mbili na nusu za upigaji picha za filamu, hatukuwa tumemaliza maonyesho yoyote yaliyopigwa picha za filamu. Kulikuwa na wakati mwingine ambapo tulikuwa tukienda kupiga picha za filamu kwenye bustani, na tulikuwa na ratiba iliyojaa shughuli nyingi. Niliwaza, “Lazima nimalize onyesho hili haraka,” lakini kadiri nilivyozidi kujaribu kufanya kazi nzuri, ndivyo nilivyozidi kuwa na wasiwasi. Sikuweza kabisa kuigiza onyesho hilo vizuri. Tulipiga picha za filamu kuanzia adhuhuri hadi magharibi na kamwe hatukupiga picha nzuri. Watu wote walikata tamaa lakini hawakuweza kufanya chochote. Mwelekezi alipoona kwamba sikuwa nikifanya vizuri, alijaribu kunisaidia, lakini nilitoa visingizio vingi ili kukwepa hayo, nikiogopa kwamba ningepoteza wajibu wangu iwapo ningemwambia ukweli. Katika hizo siku hizo chache, nilihisi hatia sana na vibaya sana kila nilipowaza juu ya jinsi ambavyo nilikuwa nimechelewesha sana upigaji picha za filamu. Nilijiambia mara nyingi kwamba nirekebishe nia zangu na kufanya wajibu wangu na kuacha kufikiria kuhusu umaarufu na hadhi. Lakini sikuweza kufanya hivyo kabisa. nilishikilia sana jinsi ya kuigiza nafasi hiyo vizuri ili niweze kuitunza. Hata ndoto zangu zilihusu tu upigaji wa picha za filamu. Nilikuwa na wasiwasi kila wakati na nilizidi kukosa usingizi Kila mtu aliniuliza, “Kwa nini umebadilika sana hivi karibuni? Kila wakati unaonekana mwenye taabu sana.” Niliogopa kwamba wangenidharau kama ningewaambia ukweli, kwa hivyo sikuzungumza na mtu yeyote juu ya hilo.

Nilikuwa nimekwama katika tamaa yangu hatari ya umaarufu na hadhi. Sikuweza kabisa kujizuia kufikiria juu hayo. Nilikuwa nikimwomba Mungu mara nyingi kila siku nikimsihi Anisaidie kuondoka katika hali hiyo haraka. Katika mikutano ya kanisa, kila mtu alizungumza juu ya uzoefu mzuri ambao alikuwa akipitia, lakini nilikaa tu hapo bila kusema lolote, nisijue la kusema. Dada mmoja aliniuliza wakati mmoja, “Je, unaweza kushiriki kuhusu matukio ambayo umepitia? Hakika una mengi kutokana na filamu zote ambazo umeigiza.” Nilijawa tu na hofu. Sikujua la kusema. Ilibidi nitafakari yote ambayo nilikuwa nimeyapitia. Je, nilikuwanimejifunza chochote kutokana na kuigiza katika filamu za kanisa wakati wote huo? Kwa nini nilihisi kama kwamba sikuwa nimejifunza lolote? Nilikuwa nimelenga tu sifa na hadhi nikipoteza kabisa nafasi zote hizo za kupitia kazi ya Mungu. Kwa nini sikujali hayo yote? Wakati huo ndipo nilipoanza kujichukia kwa kutotafuta ukweli. Nilikuja mbele za Mungu kuomba na kutubu.

Baadaye, nilipata maneno kadhaa ya Mungu ambayo yalifichua chanzo cha tamaa yangu ya umaarufu na hadhi, na nikayafikiria tena. Nilisoma katika maneno ya Mungu: “Shetani hutumia umaarufu na faida kudhibiti fikira za mwanadamu hadi anachofikiria tu ni umaarufu na faida. Wanapambana kwa sababu ya umaarufu na faida, wanateseka matatizo kwa sababu ya umaarufu na faida, wanastahimili udhalilishaji kwa sababu ya umaarufu na faida, wanatoa kila kitu walichonacho kwa sababu ya umaarufu na faida, na watafanya maoni au uamuzi wowote kwa ajili ya umaarufu na faida. Kwa njia hii, Shetani humfunga mwanadamu kwa pingu zisizoonekana. Pingu hizi zinabebwa na watu, na hawana nguvu ama ujasiri wa kuzirusha mbali. Kwa hivyo, bila kujua, watu huvumilia pingu hizi na kutembea kwenda mbele kwa ugumu mkubwa. Kwa ajili ya umaarufu huu na faida hii, binadamu humwepuka Mungu na kumsaliti, na wanazidi kuwa waovu zaidi na zaidi. Kwa njia hii, hivyo kizazi kimoja baada ya kingine kinaharibiwa katika umaarufu na faida ya Shetani(Neno Laonekana katika Mwili). Nilipokuwa nikifikiria haya yote, nilielewa kwamba Shetani alikuwa akitumia umaarufu na faida kunidhibiti. Nilikuwa nimeshawishiwa na Shetani tangu nilipokuwa mdogo. “Jitokeze kuwashinda wengine wote,” “Mtu huacha urithi nyuma yake kama vile bata bukini anavyoacha sauti yake,” Na “Kama mti unavyoishi kwa ajili ya gomba lake, mtu huishi kwa ajili ya sifa yake.” Falsafa ya Shetani yenye sumu ilikuwa ikiyadhibiti mawazo na matendo yangu yote, kwa hivyo sikuweza kujizuia kufuatilia umaarufu na hadhi. Nilidhani kuwa maisha yangekuwa tu na maana iwapo kila mtu angenijua, na watu hao wote ambao walikuwa mashuhuri na walipendwa na watu wengi sana, pekee ndio walioishi maisha yenye maana. Nilipoanza kuwa mwigizaji katika filamu za nyumba ya Mungu, nilianza kuzidisha ndoto yangu ya kuwa mashuhuri, ya kuwa maarufu na kupendwa sana siku moja. Nilipopata nafasi yoyote, nilijaribu kuonyesha uso wangu kwenye kamera nikifurahia kujihimiza kufika kiwango chochote. Nilipopangiwa tena kuwa mhusika mkuu, tamaa yangu kuu ya kujipatia sifa ilirudi. Kwa kuwa sikutaka kupoteza nafasi yangu tena, sikuulizia mambo ambayo sikuyaelewa na sikumwambia mtu yeyote nilipokuwa taabani. Nilivalia sura ya kinafiki. Nilikuwa nikitazama pande zote kila wakati, nikiangalia ni nani aliyekuwa karibu nami. Niliogopa kwamba wengine wangeona kuwa sikuweza kuigiza, na kwamba ningepokonywa nafasi hiyo. Niliona kwamba ni afadhali niendelee kuchelewesha maendeleo ya upigaji filamu, kuliko kuacha kile nilichotaka, kuwafungulia moyo wengine au kutafuta ukweli. Sikufikiri juu ya kazi ya Mungu nilipotafuta umaarufu na hadhi. Sikuzingatia jukumu langu Kwake. Nilikuwa mbinafsi na mbaya sana kiasi kwamba sikuwa nikifanya wajibu wangu kwa Mungu. Nilikuwa nikifanya maovu tu! Je, bidii yangu yote ya umaarufu na hadhi ilinipa nini mwishowe? Nilianza kuwa mbinafsi, mkaidi, na mkatili hata zaidi na nilipoteza heshima yangu yote. Niligundua kwamba umaarufu ni mtego tu uliowekwa na Shetani, na kwamba nilikuwa nimenaswa nao. Wakati ambapo sikuweza kupokea sifa au heshima, nilijaribu sana kupata mambo hayo, na wakati ambapo niliyapata, nilifanya juu chini kuyashikilia. Kwa ajili ya umaarufu na hadhi, nilianza kukosa mantiki, nikapoteza uaminifu wangu na maadili yangu yote ya kimsingi. Nilikwenda kinyume na Mungu mara nyingi, na hakukuwa na chochote moyoni mwangu isipokuwa mateso. Nilitambua kwamba Shetani hutumia umaarufu kuwapotosha, kuwadanganya watu na hata kuwameza, na kutafuta mambo haya kunaweza tu kutushawishi na kutupotosha na kututenganisha na Mungu. Kama ningeendelea kutembea kwenye njia hii, ningeishi maisha ya uchungu na mwishowe ningeangamia kwa sababu ya kumpinga Mungu. Nilipogundua haya yote, nilipiga magoti mbele za Mungu na kuomba. “Ee Mungu Sitaki tena kuficha yule niliye. Hata ndugu zangu wakijua ukweli juu ya uwongo na ulafi wangu wote, na wanipokonye wajibu wangu kama mhusika mkuu, lazima niseme ukweli na nitubu Kwako.” Katika mkutano uliofuata, nilimweleza kila mtu kuhusu upotovu wote ambao nilifichua. Mwishowe nilihisi utulivu zaidi na kwa mara ya kwanza nilihisi amani. Hakuna hata mmoja wao aliyenihukumu hata kidogo, bali walishiriki nami juu ya mapenzi ya Mungu. Niliguswa sana.

Baadaye, nilisoma maneno haya kutoka kwa Mungu: “Kama mojawapo ya viumbe, lazima mwanadamu achukue nafasi yake mwenyewe, na ajiendeleze kwa uangalifu, na kulinda kwa wajibu kile ambacho ameaminiwa na Muumba. Naye binadamu lazima asitende mambo nje ya mipaka yake au kufanya mambo zaidi ya uwezo wake au kufanya mambo ambayo ni ya kuchukiza Mungu. Binadamu ni lazima asijaribu kuwa mkubwa, au wa kipekee, au zaidi ya wengine, wala asitafute kuwa Mungu. Hivi ndivyo watu hawafai kutamani kuwa. Kutamani kuwa mkubwa au wa kipekee ni jambo la upuuzi. Kutafuta kuwa Mungu ndilo hata jambo la aibu zaidi; linaudhi na linastahili kudharauliwa. Kile cha kupongezwa, na ambacho viumbe vinastahili kushikilia kuliko chochote kile ni kuwa viumbe vya kweli; hii ndiyo shabaha pekee ambayo watu wote wanafaa kufuatilia(Neno Laonekana katika Mwili). Kupitia maneno ya Mungu, nilielewa kwamba mapenzi ya Mungu ni kwamba niwe kiumbe aliyetosheleza viwango Vyake. Badala yake, nilikuwa nimeenda kinyume kabisa na Mungu, nikitaka tu kuwa mwigizaji maarufu. Nilitaka kuwa mashuhuri na sikutaka lolote ila kupendwa na kuhesimiwa sana. Ilikuwa tu kama Shetani alipojiamini kuwa mkuu kuliko Mungu. Niliikosea sana tabia Yake na nilikuwa katika njia ya maangamizo. Mimi ni kiumbe tu aliyepotoshwa sana na Shetani, na asiyefaa kabisa sifa na upendo mkuu wa wengine. Nilijua kwamba nilipaswa kutekeleza jukumu langu kama kiumbe na kufanya wajibu wangu ili kumfurahisha Mungu. Uigizaji wangu ulikuwa na nafasi kubwa ya ukuaji na uendeleaji kiasi. Lakini nilijiapia kwamba sitatafuta umaarufu au hadhi tena. Nitafanya kazi ili niwe bora zaidi na kujiimarisha katika wajibu wangu. Nililenga juhudi zangu zote katika uigizaji wangu, na nikaacha kufikiria iwapo nitakuwa mashuhuri. Niliweza kuelewa huyo mhusika kwa urahisi, na kisha nikaelewa maonyesho niliyoigiza haraka sana. Hatimaye, upigaji picha za filamu uliendelea haraka sana kuliko hapo zamani. Kufanya wajibu wangu hatimaye ndiko kulinipa utulivu. Wengine waliendelea kuniambia kwamba mwenendo wangu wote ulibadilika kabisa. Sikukanganyikiwa na uigizaji wangu pia ulianza kuboreka. Nilimshukuru Mungu mara nyingi.

Jambo la muhimu sana ambalo nilijifunza kutokana na tukio hili lote lilikuwa kuelewa kwamba kufanya kitu chochote kwa ajili ya nyumba ya Mungu hakupaswi kuwa kwa ajili yako mwenyewe. Ni kwa ajili ya kueneza maneno ya Mungu na kushuhudia. Hili ndilo jukumu la kila kiumbe. Sikufikiria mambo yajayo hapo awali na sikuelewa ukweli. Nilitaka mambo ya kidunia kama umaarufu na hadhi, na niliteseka na Shetani hadi nikakosa ubinadamu hata kidogo. Pia, niliharibu kazi ya Kanisa. Hukumu ya maneno yote ya Mungu ilinifanya niondokane na dhambi zangu, na kuniokoa mara nyingine tena kutoka kwa Shetani, ikinionyesha njia sahihi. Sasa nimerudi mahali pangu panapofaa kama kiumbe na ninafanya wajibu wangu vizuri. Mwishowe nahisi kwamba maisha yangu yana amani. Huu ulikuwa wokovu na upendo wa Mungu. Shukrani kwa Mwenyezi Mungu!

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Hili Jaribu Langu

Na Zhongxin, Uchina Mwenyezi Mungu anasema, “Matendo Yangu ni mengi zaidi kwa kuhesabiwa kuliko chembechembe za changarawe kwenye ufuo na...

Katikati ya Jaribu la Kifo

Na Xingdao, Korea ya Kusini Mwenyezi Mungu anasema, “Mungu amekuja kufanya kazi ulimwenguni ili kumwokoa mwanadamu aliyepotoka—hakuna uongo...

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp