Hukumu ni Mwanga

16/01/2018

Zhao Xia Mkoa wa Shandong

Jina langu ni Zhao Xia. Nilizaliwa katika familia ya kawaida. Kutokana na ushawishi wa misemo kama “Kama vile mti huishi kwa sababu ya ganda lake, mtu huishi kwa sababu ya uso wake,” na “Mtu huacha jina lake nyuma popote akaapo, kama vile bata bukini hutetea popote arukapo,” sifa na heshima zikawa muhimu sana kwangu. Kila kitu nilichofanya kilikuwa ili kupata sifa, pongezi, na upendezwaji wa watu wengine. Baada ya kuolewa, malengo niliyojiwekea yalikuwa: Nitaishi maisha ya kitajiri zaidi kuliko wengine; Ni lazima nisiruhusu mtu yeyote kusema mambo hasi kuhusu jinsi ninavyowatendea wazee au kuhusu tabia na mwenendo wangu; na nitahakikishia mtoto wangu ataingia katika chuo kikuu cha kifahari na ana matarajio mazuri, ili kuongeza fahari zaidi katika heshima yangu. Kwa hivyo, sikuwahi kugombana na wakwe wangu. Mara nyingine, wakati walisema maneno makali kwangu, ningehisi nimekerwa mno mpaka ningejificha na kulia badala ya kuwapa uhasi. Wakati niliona wengine wakiwanunulia wazazi wao nguo wakati wa Mwaka Mpya wa Kichina na sikukuu zingine, ningeenda mara moja kumnunulia mama mkwe wangu baadhi, na ingekua pia ya ubora wa hali ya juu. Wakati jamaa walikuja kunitembelea, ningesaidia kununua vyakula na kupika. Hata wakati ilikuwa ngumu na ya kuchosha kiasi bado ningekuwa radhi kabisa. Nikihofia kuwa ningekuwa na utajiri kiasi kuliko wengine, niliacha mtoto wangu wa kike nyuma mwezi mmoja baada ya kumzaa na kurudi mara moja kazini. Matokeo yake yakawa, binti yangu alipata maumivu ya utapiamlo na akawa tu ngozi na mifupa kwa sababu hangeweza kunywa maziwa ya matiti yangu. Hali yake iliimarika tu baada ya sindano 100 za lishe, ilhali nilikuwa nimechoka sana kiasi kwamba nilikuwa na maumivu ya mgongo kila siku. Ingawa ilikuwa ngumu na yenye kuchokesha, nilivumilia shida hizo na nilijitolea kwa bidii kwa ajili ya kupata sifa nzuri. Katika miaka michache tu, nikawa mkwe maarufu katika kijiji, na familia yangu ikawa tajiri na kuonewa kijicho na watu walio karibu nasi. Matokeo yake yakawa, wakwe zangu, majirani, jamaa na marafiki wote walinisifu sana. Katika kukabiliwa na sifa na taadhimu kutoka kwa wale walio karibu nami, kiburi changu kilitoshelezwa sana. Nilihisi shida zangu wakati wa kipindi cha miaka michache iliyopita hazikuwa za bure, na nilikuwa nimefurahishwa sana kindani. Hata hivyo, maisha yangu ya utulivu yalikatishwa baada ya shemeji wangu kuolewa. Mke wake alinena nami kwa kejeli daima, akisema kuwa nilikuwa na nia fiche kwa kumtendea mama mkwe wetu vyema kwa sababu nilikuwa nataka tu mali yake. Yeye alikuwa akisema kila mara kuwa mama mkwe wetu alikuwa na upendeleo kwani alitupa sisi vitu vingi zaidi kuliko alivyowapa wao, na mara nyingi tulikuwa tukigombana kwa sababu ya haya. Nilihisi kuudhika mno na nilitaka kubishana naye hadharani ili kulalamika kutokuwa na hatia kwangu, lakini ingeweza kuharibu picha nzuri niliyokuwa nimejenga ndani ya mioyo ya watu. Kwa hivyo, ningejizuia kwa lazima, na wakati singeweza kuvumilia tena ningekuwa na kilio kikubwa kwa faragha. Baadaye, wifi huyo alisukuma bahati yake kwa kumiliki ardhi iliyosambazwa kwa upande wangu wa familia, iliyonifanya nitingike kwa hasira na nisikule au kunywa kwa masiku. Nilitaka hata pia kupambana naye hadi suluhu ipatikane. Hata hivyo, nikifikiria kwamba ingeweza kunifanya kupoteza heshima, kuharibu sifa yangu, na kufanya wale walio karibu nami kunidharau, nilimeza hayo yote, lakini ndani nilihisi nimekazwa mno kiasi kwamba nilikuwa na maumivu. Nilionekana mwenye majonzi na nilitanafusi siku nzima, nikihisi kama ilikuwa chungu sana na ya kuchosha kuishi na kutojua wakati kungekuwa na mwisho kwa maisha kama hayo.

Mwisho wa binadamu kweli ndio mwanzo wa Mungu. Pindi wakati nilikuwa na maumivu na kuhisi mnyonge, Mwenyezi Mungu alinyoosha mikono Yake ya wokovu kwangu. Siku moja, jirani yangu aliniuliza: “Unaamini katika uwepo wa Mungu?” Nilijibu: “Nani asiye? Ninaamini Mungu yupo.” Kisha akasema kwamba Mungu anayeamini ndiye Mungu pekee na wa kweli aliyeumba ulimwengu na vitu vyote, na kwamba mwanzoni, binadamu waliishi katika baraka za Mungu kwa sababu walimwabudu Mungu, lakini baada ya wao kupotoshwa na Shetani, hawaabudu tena Mungu na ndivyo basi wanaishi chini ya laana na maumivu kwa Mungu. Mwenyezi Mungu wa siku za mwisho alikuja kuwapa watu ukweli na kuwaokoa kutoka kwenye lindi kuu la taabu. Kwa kuongezea, pia aliwasiliana uzoefu wake mwenyewe wa kumwamini Mungu. Baada ya kusikiza mawasiliano yake, nilihisi kuwa nimepata msiri wangu wa karibu sana, na singeweza kujizuia kuelezea maumivu yote moyoni mwangu. Baadaye, alinisomea kifungu cha neno la Mungu: “Unapokuwa umechoka na unapoanza kuhisi huzuni kubwa ya ulimwengu huu, usipotoke, usilie. Mwenyezi Mungu, Mlinzi, atakaribisha kuwasili kwako wakati wowote. Yuko kandokando yako akiangalia, akikusubiri urudi. Anasubiri siku ambayo utarudisha ghafla kumbukumbu yako: ukitambua ukweli kwamba ulitoka kwa Mungu, lakini wakati fulani usiojulikana ukapoteza mwelekeo wako, wakati fulani usiojulikana ukaanguka barabarani ukiwa hujitambui na tena wakati fulani usiojulikana ukampata ‘baba.’ Isitoshe, unagundua kuwa Mwenye uweza amekuwa hapo muda huo wote, akiangalia, akisubiri kurejea kwako, kwa muda mrefu sana(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kutanafusi kwa Mwenye Uweza). Maneno ya Mungu yalitiririka ndani ya moyo wangu kama mkondo wenye joto, yakituliza moyo wangu wenye uchungu na huzuni, na singeweza kuzuia machozi yangu kumwagika. Wakati huo huo, nilihisi kama mtoto aliye na mateso aliyepotea na aliyerudi kwa ghafla katika kumbatio la mama yake. Kulikuwa na msisimko usioweza kusemeka na mhemuko katika moyo wangu. Niliendelea kumshukuru Mungu, kwa sababu alinichukua katika nyumba Yake na kunijalia wakati sikuwa na pengine pa kwenda. Nitafuata Mungu kwa moyo na roho yangu! Tangu wakati huo, nilisoma maneno ya Mungu, nikamwomba Mungu, na niliimba nyimbo za kumsifu Mungu kila siku, mambo yalilonifanya kutulia hasa katika moyo wangu. Kwa kuhudhuria mikutano, niliona kuwa ndugu walikuwa kama familia kubwa, ingawa wao hawana uhusiano wa damu. Uingiliano wao ulikuwa wa kawaida na wazi, ulikuwa umejaa uelewa, ustahamilivu, na uvumilivu, na haukuwa na wivu, mgongano na kupanga njama au kisingizio na unafiki. Hawakuwadhulumu maskini ilhali wakipenda matajiri, na wote waliweza kutendea kila mtu na unyofu na usawa. Moyo wangu ungehisi huru hasa wakati tuliimba nyimbo za kumsifu Mungu pamoja. Kwa sababu hiyo nilipendezwa na maisha haya ya kanisa yenye upendo na ukunjufu, ya haki na yenye furaha. Nilisadiki kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Mungu pekee wa kweli na nilifanya uamuzi wangu kuwa ningemfuata hadi mwisho.

Kupitia kusoma maneno ya Mungu, nilielewa hamu ya haraka ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu kwa kiwango kikubwa kiwezekanavyo, na kuona kwamba ndugu wengi walikuwa wakifanya kila liwezekanalo kujitoa na kujitumia kwa ajili ya kueneza injili ya ufalme. Hivyo basi pia nikajihusisha kikamilifu katika kuhubiri injili. Ili kunitakasa na kunibadili mimi, Mungu alilenga asili yangu mbovu na alitekeleza adabu na hukumu Yake juu yangu mara kwa mara. Wakati mmoja, nilikwenda kuhubiri injili kwa aliyeweza kuwa mwaminifu. Ilikuwa msimu wa kilimo wenye shughuli nyingi wakati huo. Baada ya kuona jinsi alivyokuwa na shughuli nyingi za kilimo, nilienda kufanya kazi pamoja naye huku nikimpa ushuhuda wa kazi ya Mungu ya siku za mwisho. Nani angejua ya kwamba baada ya kuzungumza naye kwa siku tatu mtawalia angekuwa hana nia ya kuukubali tu na badala yake angenikaripia: “Wewe huna haya hata! Mimi tayari nilisema siyaamini haya, na bado huachi kuhubiri.” Maneno yake yaliniumiza sana. Uso wangu ulichomeka ni kama nilikuwa nimechapwa makofi mara kadhaa hadharani, wakati moyo wangu uliuma na wimbi baada ya wimbi la maumivu hafifu yasiyo makali. Nilifikiria: Nilikuja kukuhubiria kwa nia njema na nilijichokesha nilipokusaidia na kazi yako hadi mgongo wangu ulipata maumivu, na bado badala ya kukubali hayo, ulinitendea hivi. Wewe ni katili kweli! Nilihisi nimeaibishwa mno na sikutaka kuzungumza naye tena, lakini pia nilihisi kuwa hii haikuwa inaambatana na nia za Mungu, kwa hivyo niliomba kwa ukimya moyoni mwangu na nilizuia maumivu yangu ya kindani ili kuendelea kuongea naye nilipokuwa nikimsaidia na kazi yake. Hata hivyo, haidhuru kwa bidii gani niliwasiliana sikuweza bado kumfikia. Niliporomoka kama mpira uliotolewa upepo niliporudi nyumbani. Maneno ya mlengwa wa mahubiri yangu yaliendelea kujitokeza kichwani mwangu. Nilivyofikiria zaidi kuhusu hayo ndivyo nilivyoteseka zaidi: Mbona ninajisumbua? Yote niliyoyapata kama malipo ya nia yangu njema yalikuwaa kuzomewa, kukashifiwa, na kunyanyaswa. Kwa kweli hii sio haki kabisa! Hakuna mtu aliyewahi kunitenda namna hii. Kueneza injili ni uchungu na ngumu kabisa! Hapana, siwezi kwenda nje kuhubiri injili tena! Ikiwa nitaendelea kuhubiri sitabaki na heshima yoyote ya kuona mtu yeyote. Wakati tu nilipohisi nimekosewa sana na mwenye maumivu kiasi kwamba sikuwa na hiari tena ya kuhubiri injili, maneno ya Mungu yalinipatia nuru: “Je, unajua mzigo ulio begani mwako, kazi yako na majukumu yako? Hisia yako ya kihistoria ya mwito iko wapi? … Wao ni masikini, wa kuhurumiwa, vipofu na waliopotea na wanalia gizani, ‘Njia iko wapi?’ Jinsi gani wanatamani mwangaza, kama nyota iangukayo kutoka angani, ianguke ghafla na kutawanya nguvu za giza zilizowakandamiza wanadamu kwa miaka mingi. Ni nani anayeweza kujua jinsi wanavyotumaini kwa hamu, na wanavyotamani hili usiku na mchana? Wanadamu hawa wanaoteseka mno wamebaki wafungwa katika jela za giza, bila tumaini la kuwachiliwa huru, hata ile siku ambayo mwanga utaonekana; ni lini hawatalia kwa uchungu tena? Roho hizi dhaifu ambao kamwe hazijapewa pumziko kwa hakika zinateseka na bahati hii mbaya. Kwa muda mrefu wamefungiwa nje na kamba zisizo na huruma na historia iliyokwama katika wakati. Ni nani amewahi kusikia sauti ya vilio vyao? Ni nani amewahi kuona nyuso zao zenye taabu? Umewahi kufikiria jinsi moyo wa Mungu ulivyosononeka na ulivyo na wasiwasi? Anawezaje kustahimili kuona mwanadamu asiye na hatia, Aliyemuumba kwa mikono Yake Mwenyewe akiteswa na makali? Mwishowe, wanadamu ndio wasio na bahati na waliopewa sumu. Hata ingawa wamenusurika mpaka siku hii, ni nani angefikiri kuwa wamepewa sumu na yule mwovu kwa muda mrefu? Je, umesahau kuwa wewe ni mmoja wa waathiriwa? Kwa ajili ya upendo wako kwa Mungu, una nia ya kufanya kila uwezalo kuwaokoa walionusurika? Je, huna nia, ya kutumia nguvu zako zote kulipiza Mungu anayempenda binadamu kama nyama na damu Yake Mwenyewe?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kushughulikiaje Wito Wako wa Baadaye?). Mistari katikati ya maneno ya Mungu yote yalifichua hangaiko Lake na huzuni Yake yenye masikitiko na ya kuwajali watu wasio na hatia. Mungu hawezi kuvumilia kuona watu walioumbwa kwa mikono Yake mwenyewe wakidanganyika na kuumizwa na Shetani. Mungu anaendelea kusubiri kwa hamu sana kwa wanadamu kurudi katika nyumba Yake hivi karibuni ili wapokee wokovu mkubwa amewafadhili. Ilhali wakati nilipopatwa na maneno machache makali kutoka kwa mlengwa wangu wa mahubiri, nilihisi nimekosewa na kuteswa na nililalamika kuhusu shida na mateso hayo. Nilikuwa hata tena sina radhi ya kushirikiana kwa sababu nilikuwa nimefedheheka. Dhamiri na mantiki yangu ilikuwa wapi? Ili kutuokoa sisi watu potovu katika siku za mwisho, Mungu ameendelea kuwindwa na kuteswa na serikali kwa kila mara, kutelekezwa, kushutumiwa, kukufuriwa na kukashifiwa na jamii ya dini, na kuelewa visivyo na kupingwa na sisi wafuasi wa Mungu. Yale machungu na aibu Mungu amepitia ni mengi sana, ni mengi kabisa! Hata hivyo, Mungu hakuachana na wokovu Wake wa wanadamu, na aliendelea kutoa mahitaji ya wanadamu katika utulivu. Upendo wa Mungu ni mkubwa sana! Nafsi yake ni nzuri sana na yenye ukarimu! Taabu zangu leo haziwezi kulinganishwa na mateso ambayo Mungu amepitia kwa ajili ya kuokoa mwanadamu! Nilikumbuka kuwa mimi nilikuwa pia mwathiriwa, mtu yule aliyekuwa amedhuruiwa na Shetani kwa miaka. Kama Mungu hangekuwa amenyoosha mikono Yake ya wokovu kwangu, ningekuwa bado ninang’ang’ana kwa uchungu katika giza, nisiweze kupata mwanga na matumaini ya kuishi. Kwa kufurahia wokovu wa Mungu, ninapaswa kuubeba aibu na maumivu ili kufanya lote liwezekanalo kushirikiana na Mungu, kutekeleza wajibu wangu vizuri, na kuleta watu wale wasio na hatia na bado wanadhuruiwa na Shetani mbele za Mungu. Hii ni ya thamani na ya maana zaidi kuliko kazi yoyote duniani, na ni ya kufaa haijalishi ni mateso ngapi yanapaswa kuvumiliwa! Nilipofikiria juu ya haya, sikuhisi tena kwamba kuhubiri kwa injili ni kitu chenye uchungu, na badala yake nilihisi mwenye bahati kuwa na uwezo wa kuratibu na injili ya ufalme. Huu ulikuwa heshima yangu na pia kuinuliwa na Mungu. Nilifanya uamuzi wangu: Bila kujali aina gani ya shida nitakayopatana nayo katika kazi yangu ya injili, nitajitolea yangu yote na kumtegemea Mungu kuwaleta watu zaidi na zaidi wenye shauku ya Mungu mbele Yake ili kufariji moyo Wake! Baadaye, nilijirusha mwenyewe tena katika kazi ya injili tena.

Kufuatia kipindi cha mafunzo, kila nilipokutana na mlengwa wa mahubiri ambaye alikuwa na mtazamo mbaya au aliyeninenea maneno makali wakati wa kutekeleza wajibu wangu, ningekuwa na uwezo wa kukabiliana na hilo kwa njia sahihi na kuendelea kushirikiana na moyo wa upendo. Kwa sababu ya haya, nilihisi nilikuwa nimebadilika na sikuwa ninajali tena kuhusu heshima na hadhi. Lakini wakati Mungu aliweka mazingira mengine ya kunijaribu kulingana na kile nilichohitaji katika maisha, nilifichuliwa kabisa tena. Siku moja, kiongozi wa kanisa alinijulia hali hivi karibuni na pia alizungumzia nia za Mungu za wakati uliopo na njia ya utendaji. Wakati niligundua wakati wa mazungumzo kuwa alikuwa anahamishwa katika kanisa lingine ili kutimiza wajibu wake, singeweza kujisaidia kuhisi wimbi la msisimko: Kuna uwezekano kuwa nitafanywa kuwa kiongozi wa kanisa baada ya yeye kuondoka. Ikiwa ndivyo, ni lazima kabisa nishirikiane vizuri! Wakati tu nilipokuwa ninahisi furaha kisiri, dada huyo alisema kuwa dada mwingine katika kijiji changu angetutembelea kesho. Nilikuwa na wasiwasi mara tu niliposikia hayo: Anakujia nini? Yeye ndiye atafanywa kuwa kiongozi mpya wa kanisa? Singeweza kujizuia kuwa na wasiwasi: Hajakuwa akimwamini Mungu kwa muda mrefu kama vile nimefanya, na pia anakuja kutoka kijiji hicho kama mimi. Ikiwa yeye atafanywa kiongozi, basi heshima yangu itakuwa aje? Ndugu wataniona namna gani? Kwa hakika watasema kuwa mimi huwa sifuatilii ukweli kwa kiwango chake. Sikuweza kuacha kufikiria juu ya hayo. Niligaagaa na kugeuka kitandani usiku, nisiweze kulala. Wakati wa mkutano siku iliyofuata, nilitia makini mara kwa mara sauti na mtazamo wa kile kiongozi alikuwa akisema kwa sababu nilitaka kujua kwa hamu ni nani angechaguliwa kuwa kiongozi mpya wa kanisa. Kila wakati kiongozi huyo aliniangalia alipozungumza, nilihisi tumaini la kufanywa kuwa kiongozi. Sura yangu ingejawa na furaha na ningekubali kwa kichwa na kukubaliana na chochote alichosema. Kwa upande huo mwingine, wakati wowote kiongozi huyo alitazama dada huyo mwingine alipokuwa akizungumza, ningekuwa na uhakika kuwa dada huyo angetajwa kama kiongozi, na ningehisi huzuni na kuwa na masumbuko makali kwa sababu ya hilo. Wakati wa siku hizo chache, nilikuwa nimeteseka kwa ajili ya heshima na hadhi sana hadi nikawa na wasiwasi na kuchanganyikiwa. Nilipoteza hamu yangu ya kula na hata nikahisi kama muda ulikuwa unapita hasa polepole, ni kama ulikuwa umeganda. Kiongozi wa kanisa aliweza kuona hali niliyokuwa katika, kwa hivyo alipata kifungu cha neno la Mungu niweze kusoma: “Sasa nyinyi ni wafuasi, na mmepata ufahamu fulani wa hatua hii ya kazi. Hata hivyo, bado hamjaweka kando tamaa yenu ya hadhi. Wakati hadhi yenu iko juu mnatafuta vizuri, lakini wakati hadhi yenu iko chini hamtafuti tena. Baraka za hadhi daima ziko katika fikira zenu.” “Ingawa mmewasili kwenye hatua hii leo, bado hamjaacha hadhi lakini mnapambana bila kukoma kuuliza kuihusu, na mnaichunguza kila siku…. Kadiri unavyotafuta zaidi kwa njia hii, ndivyo utakavyovuna kidogo zaidi. Kadiri ilivyo kubwa zaidi tamaa ya mtu ya hadhi, ndivyo itabidi washughulikiwe kwa uzito zaidi na ndivyo watakavyozalimika kupitia usafishaji mkubwa. Watu kama hao hawana thamani kabisa! Lazima wshughulikiwe na wahukumiwe vya kutosha ili waachane na mambo haya kabisa. Mkifuatilia kwa njia hii mpaka mwisho, hamtavuna chochote. Wale ambao hawafuatilii uzima hawawezi kubadilishwa, na wale ambao hawana kiu ya ukweli hawawezi kupata ukweli. Hulengi kufuatilia mabadiliko ya kibinafsi na uingiaji, lakini badala yake unalenga tamaa badhirifu na vitu vinavyozuia upendo wako kwa Mungu na kukuzuia kumkaribia Yeye. Je, vitu hivyo vinaweza kukubadili? Je, vinaweza kukuleta katika ufalme?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mbona Huna Hiari ya Kuwa Foili?). Kila mstari wa maneno ya Mungu uligonga moyo mwangu, ukinifanya nihisi kuwa Mungu alikuwa kando yangu, akifuatia kila neno na mwenendo wangu. Singeweza kujizia ila kujitafakari kwa mawazo na utendaji wangu siku hizi mbili zilizopita. Niligundua kuwa mtazamo wangu wa ufuatiliaji ulikuwa mbovu sana na uliathiriwa na misemo kama “Kama vile mti unavyoishi kwa sababu ya gome lake, mtu huishi kwa sababu ya uso wake,” na “Mtu huacha jina lake nyuma mahali popote anapoishi, kama vile bata bukini hunena kilio chake popote anapoburuka.” Siku zote nilitaka hadhi ili nipate kushinda sifa zaidi kutoka kwa wengine, kilichosababisha mimi kuteseka kwa ajili ya heshima na hadhi kiasi kwamba nilikuwa na wasiwasi na kuchanganyikiwa, nilipoteza hamu yangu ya kula na singeweza kulala, na nilijifanya kuonekana mpumbavu. Hali kama hiyo ilitengenezwa na Mungu kulingana na hali yangu. Ilikuwa upendo wa Mungu ukiniangukia. Kazi ya Mungu leo ilikuwa ya kuniokoa, kunisaidia kuepuka ushawishi wa giza wa Shetani ili nipate kupata wokovu. Njia niliyokuwa nikifuatilia ilikinzana na mapenzi ya Mungu. Singekuwa na uwezo wa kupokea idhini ya Mungu hata kama ningemwamini hadi mwisho. Ningeachwa bila chochote! Kwa hivyo nilimwomba Mungu kwa ukimya: “Ewe Mungu! Niko radhi kutii kazi Yako, kutembea katika njia sahihi ya kuamini Mungu kwa mujibu wa mahitaji Yako, na kutia juhudi kwa neno Lako ili kufikia kuelewa ukweli na kuachana na tabia yangu mbovu. Bila kujali kama nimefanywa kiongozi, nitafuatilia ukweli na kutia makini kwa kubadili mambo yangu ambayo hayakidhi malengo Yako.” Baada ya kuelewa makusudi ya Mungu, nilihisi hasa utulivu moyoni mwangu na nilifurahia kuwasiliana bila kujali maudhui yalikuwa gani. Baada ya mkutano, kiongozi wa kanisa alisema kuwa, kulingana na mapendekezo ya wengi wa ndugu, dada huyo angekuwa kiongozi mpya wa kanisa, na kuwa ningeweza kuratibu na kazi yake. Nilikuwa na utulivu sana ndani na kukubali bila kusita, kukubali kufanya kazi kwa upatanifu na dada huyo ili kutimiza wajibu wetu.

Baada ya kupitia adabu na hukumu ya Mungu wakati huu, nilipata ujuzi fulani juu ya mwelekeo wangu wa kuzingatia heshima na hadhi, na nilikuwa radhi kuachana na mwili wangu na kumwamini Mungu na kutekeleza wajibu wangu kulingana na mahitaji Yake. Hata hivyo, uchafu wangu uliotokana na sumu za Shetani zilikuwa zimezama sana. Kina cha nafsi yangu bado kilikuwa kinatawaliwa na ushawishi wa Shetani. Ili kuniokoa vyema kutoka kwa madhara ya Shetani, Mungu aliinyoosha mikono Yake ya wokovu kwangu tena. Siku moja, niliambiwa kuwa kulikuwa na dada katika kanisa ambaye hakuwa katika hali nzuri, kwa hiyo nilishauriana na dada niliyeshirikishwa naye kuhusu jinsi ya kutatua shida hii. Kwa sababu dada niliyeshiriki naye hakuhisi vizuri, nilikwenda peke yangu kutatua tatizo hilo baada ya majadiliano yetu. Nilimtafuta dada huyo usiku uo huo ili kuwasiliana naye, na tatizo hilo lilitatuliwa haraka sana. Moyo wangu ulibubujikwa kwa furaha wakati huo, nikifikiri kuwa kiongozi wa ngazi ya juu angenisifu kwa hakika kwa sababu nilikuwa nimetia jitihada nyingi sana. Hata hivyo, wakati tu nilipokuwa nikisubiria habari njema, kiongozi wa ngazi ya juu aliandika barua akitaka kuelewa hali ya dada huyo. Nilifikiria ilikuwa ni kunisifu, kwa hiyo niliifungua kwa furaha na kuisoma. Lakini nilipoona kuwa kile kilichokuwa ndani ya barua kilikuwa hasa cha kuuliza dada mwenzi vile alivyoshughulikia tatizo hilo, mara moja nikawa mwenye uchungu: Kwa uwazi ni mimi niliyeshughulikia suala hilo. Mbona usiniandikie kuniuliza juu ya hilo? Inaonekana mimi sina nafasi katika moyo wa kiongozi na ninadharauliwa. Mimi ni msichana wa kibaraka tu. Haijalishi jinsi ninavyofanya vyema sipati sifa njema yoyote kwa sababu hakuna mtu anayelizingatia kwa makini. Nilivyofikiria zaidi juu ya hilo, ndivyo nilihisi zaidi nilikuwa nimekosewa na kuhuzunika. Nilihisi nimefedheheshwa. Wakati huu, dada yangu mwenzi alikuwa na barua mkononi mwake na alikuwa karibu kuzungumza nami. Singeweza kuzuia hisia zilizokuwa ndani yangu na nikampigia kelele: “Kiongozi wa ngazi ya juu hajui jinsi suala hili lilivyotatuliwa. Hujaelewa haya? Nililifanya kazi kwa bidii kwa muda mrefu lakini hakuna hata mmoja aliyesema neno jema kulihusu, na hatimaye wewe bado ulipata sifa zote. Mbele ya kila mtu, mimi ni mtu tu wa kutumwa na kusaidia. Haijalishi ninaliwekea jitihada gani, hakuna mtu atakayelifurahia.” Baada ya kusema haya, nilihisi mwenye kudhulumiwa sana hadi nikaangua kilio. Wakati huo, maneno ya Mungu yalirudiarudia katika masikio yangu: “3. Ikiwa bado Ninakudharau sana licha ya wewe kutumia bidii nyingi, je, utaweza kuendelea kunifanyia kazi katika mashaka? 4. Ikiwa, baada ya wewe kufanya matumizi kwa ajili Yangu, Siyaridhishi mahitaji yako madogo, je, utavunjika moyo na kusikitishwa na Mimi, au hata ukasirike na kunitukana kwa sauti kubwa?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tatizo Zito Sana: Usaliti (2)). Maneno ya kushutumu ya Mungu yalinituliza polepole, na mawazo yangu yalifumbuka sana pia. Tukio ambalo lilikuwa limetoka kutokea liliendelea kucheza tena katika mawazo yangu kama sinema. Ufunuo wa Mungu ulinifanya kuona kwamba asili yangu ni ya kutisha na ya hatari sana, na kwamba imani yangu kwa Mungu na kutekeleza kwa wajibu wangu haukuwa wa kuridhisha Mungu au kupokea idhini Yake, mbali kupokea sifa na taadhimu kutoka kwa watu wengine. Mara tu matamanio yangu hayakuwa yakitoshelezwa, ningekuwa mwenye kujaa chuki; asili yangu ya unyama ungejitokeza, na kumsaliti Mungu ikawa jambo rahisi sana kufanya hata zaidi. Wakati huu, niliona kuwa nimevuka mipaka sana na kwamba nilikuwa mkatili. Maumivu niliyoyahisi yalikuwa ya kuhuzunisha sana. Nilipotubu, nikamwomba Mungu: “Ewe Mungu, nilifikiri nilikuwa nimebadilika na sikuwa ninaishi tena kwa sababu ya heshima na hadhi, na pia ningeweza kushirikiana na dada huyo. Lakini katika ufunuo Wako leo, kwa mara nyingine tena nimeweza kufunua ubaya wangu wa kishetani, daima nikihisi kuwa sikuwa na hadhi kati ya watu na kuteseka kwa sababu jitihada zangu hazikusifiwa na wengine. Ee Mungu, Shetani kweli alikuwa amenidhuru sana. Hadhi, sifa, na majivuno yote yakawa pingu zangu. Ninaomba kuwa Unaweza kuniongoza kutoka kwa ushawishi wa Shetani tena.” Baadaye, niliona kati ya maneno ya Mungu yafuatayo: “Kila mmoja wenu amepanda vilele vya juu zaidi vya umati; ninyi mmepanda kuwa mababu wa umati. Ninyi ni wadhalimu mno, na mnacharuka miongoni mwa mabuu wote, mkitafuta mahali pa amani na mkijaribu kuwameza mabuu walio wadogo kuwaliko ninyi. Ninyi ni wenye kijicho na wa husuda katika mioyo yenu, kuwashinda wale pepo ambao wamezama chini ya bahari. Mnaishi chini ya samadi, mkiwasumbua mabuu kutoka juu hadi chini ili wasiwe na amani, mkipigana wenyewe kwa wenyewe kwa muda mfupi na kisha kutulia. Ninyi hamjui hali yenu wenyewe, ilhali bado ninyi hupigana wenyewe kwa wenyewe ndani ya samadi. Ni nini ambacho mnaweza kupata kutokana na mapambano hayo? Kama ninyi kweli mngekuwa na moyo wa kunicha Mimi, mngewezaje kupigana wenyewe kwa wenyewe bila Mimi kujua? Haijalishi vile hali yako ilivyo juu, je, bado wewe si mnyoo mdogo mwenye uvundo ndani ya samadi? Utaweza kuota mbawa na kuwa njiwa angani?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Majani Yaangukayo Yatakaporudi kwa Mizizi Yake, Utajuta Maovu Yote Ambayo Umefanya). Kila neno la hukumu ya Mungu lilinidunga kwa uchungu ndani ya moyo wangu kama upanga mkali, likichangamsha roho yangu na kunifanya kutambua kwamba nilitekeleza wajibu wangu sio ili kumtukuza Mungu na kumshuhudia, lakini kwa sababu daima nilitaka kujionyesha, kujishuhudia mwenyewe, na nilikuwa na ndoto ya kuwa bora kuliko watu ili waweze kunienzi na kuniheshimu. Kulikuwa na uchaji wowote wa Mungu ndani ya moyo wangu? Nilichofuatilia hakikuwa sawa na kile cha malaika mkuu aliyemsaliti Mungu? Mimi ni kiumbe kilichoumbwa kilichopotoshwa kabisa na Shetani. Mbele ya Mungu, mimi ni kama uchafu, funza. Ninatakiwa kuwa ninamwabudu Mungu na kutimiza wajibu wangu nikiwa na uchaji moyoni mwangu wakati wote, lakini sikushughulika na kazi ya uaminifu, na nilitaka daima kutumia kutekeleza wajibu wangu kama fursa ya kujionyesha na kujishuhudia mwenyewe. Mungu angewezaje kutochukia na kusinywa na haya? Mungu ni mtakatifu sana na mkuu, amejaa mamlaka na uongozi, na bado anabaki kuwa mnyenyekevu na kujisetiri, hafichui utambulisho Wake kamwe ili kuwafanya watu kumtazamia na kumstahi. Badala yake, Anaendelea kwa ukimya kujitolea Kwake kote ili kuwaokoa wanadamu, kamwe hajitetei Mwenyewe au kudai sifa njema, na kamwe hadai chochote kutoka kwa wanadamu. Unyenyekevu, uadilifu, na kutokuwa na ubinafsi kwa Mungu kulinifanya nione kiburi, kuwa duni, na ubinafsi wangu, sikuwa na budi ila kuhisi aibu, kana kwamba sikuwa na mahali pa kujificha, na nilihisi kwamba nilikuwa nimepotoshwa sana na Shetani na nilihitaji sana wokovu wa hukumu, adabu, jaribio na usafishaji wa Mungu. Kwa hivyo nilianguka tena mbele ya Mungu: “Ewe, Mwenyezi Mungu! Kupitia uadibu na hukumu Yako ninaweza kuona uasi wangu, pamoja na uadilifu Wako na ukuu. Kuanzia sasa kuendelea, wakati ninapotekeleza wajibu wangu ninatumaini tu kutenda kama mwanadamu wa adabu aliye na moyo unaokuogopa Wewe, na kutupa tabia yangu ya kishetani kwa kutegemea maneno Yako.”

Baada ya kupitia adabu na hukumu ya Mungu mara kwa mara tena, maoni yangu juu ya ufuatiliaji yamebadilika hatua kwa hatua, lakini tabia ya maisha yangu haikuwa bado imepata mabadiliko kweli. Ili kunitakasa kabisa zaidi na kunisababisha kutembea kwenye njia ya sahihi ya uzima, Mungu mara nyingine tena alinipa wokovu Wake. Baadaye, nilichaguliwa kuwa kiongozi wa kanisa, nikishirikiana na dada mwingine kutekeleza wajibu wetu. Kutokana na kushindwa kwangu kwa awali, niliendelea kujikumbusha kila wakati kwamba nilihitaji kukubaliana na dada huyo ili kufanya kazi ya kanisa vizuri. Mwanzoni, ningekuwa nikijadili kila kitu na dada huyo na kufuatilia mwongozo wa Mungu pamoja, kwa hivyo tulifanikisha matokeo katika vipengele vyote vya kazi. Lakini baada ya muda fulani, niligundua kuwa dada huyo alikuwa na tabia nzuri za asili, mawasiliano yake ya ukweli yalikuwa wazi na ya kuangaza, na uwezo wake wa kikazi ulikuwa sawa kuliko wangu. Wakati wa mikutano, ndugu walikuwa wote radhi kusikiliza mawasiliano yake na wote walitafuta ushauri wake walipopatwa na shida. Nilipokabiliwa na mazingira kama hayo, nilikuwa tena nimetegwa katika mtego wa Shetani na kupumbazwa nayo: Dada huyo ni bora zaidi kuliko mimi kwa kila namna na anapendwa na ndugu bila kujali mahali anaenda. Hapana! Ni lazima nimpite kwa vyovyote vile, na niache ndugu waone kwamba mimi niko chini yake. Kwa sababu hii, nilijishughulisha kanisani kila siku mtawalia, nikipanga mikutano ya ndugu na haijalishi ni nani aliyepata matatizo ningekimbia kwao kuwasaidia kutatua suala hilo. … Inawezekana kuwa nilionekana kuwa mwaminifu na mtiifu kutoka nje, lakini malengo yangu ya ndani ingewezaje kuepuka macho ya Mungu? Uasi wangu ulifufua hasira ya Mungu, na kama matokeo nilianguka katika giza. Sikupata nuru niliposoma maneno ya Mungu, sikuwa na cha kusema wakati wa kuomba, niliwasiliana bila kusisimua wakati wa mikutano, na hata niliogopa mikutano na ndugu zangu. Nilikuwa nimefungwa kabisa na heshima na hadhi. Nilipitia kila siku bila kidokezo, ni kama nilikuwa nimebeba mzigo mkubwa mgongoni mwangu na singeweza kupumua kutokana na kubanwa. Singeweza pia kubaini tena baadhi ya masuala ya kanisa, na utendaji bora wangu wa kazi yangu ukashuka kwa kasi. Nilipokabiliwa na ufunuo kama huo kutoka kwa Mungu, sikujaribu kujijua na pia sikuwa radhi kuzungumza kwa nyofu kwa ndugu kuhusu hali yangu na kutafuta ukweli ili kuutatua, kwa hofu kuwa wangenidharau. Baadaye, kuadibu na nidhamu ya Mungu ikaniangukia. Tumbo yangu ilianza kwa ghafla kuniuma sana hadi singeweza kukaa au kusimama kwa amani. Mateso ya magonjwa na kutoridhika kutokana na kutopata hadhi kuliniacha nikizungukazunguka katikati ya maisha na kifo. Kutokana na kukataa kwangu kuyakubali matatizo yangu na kushindwa kwangu kushirikiana kwa kazi ya kanisa, kanisa halikuwa na budi ila kunibadilisha na kunituma nyumbani ili ibada ya kiroho na kujitafakari. Baada ya kupoteza hadhi yangu, nilihisi kama nilikuwa nimehukumiwa jehanamu. Kihisia, nilizama hadi katika kiwango changu cha chini kabisa na kuhisi kuwa nilikuwa nimeaibika kabisa. Niliteseka hata zaidi ndani hasa wakati nilipowaona ndugu wote wakitekeleza kikamilifu wajibu wao, wakati nilikuwa nimepoteza kazi ya Roho Mtakatifu na sikuwa na uwezo wa kutekeleza wajibu wowote. Kwa uchungu, sikuweza kujisaidia ila kujiuliza: Mbona kuna wengine wanaamini Mungu na wanaelewa ukweli zaidi na zaidi, ilhali ninaendelea kumuasi na kumpinga Mungu mara kwa mara tena kwa sababu ya heshima na hadhi? Nilimsihi Mungu mara nyingi anielekeze nipate chanzo cha kufeli kwangu. Siku moja, niliona yafuatayo kati ya maneno ya Mungu: “… watu wengine hususan humpenda Paulo sana. Wanapenda kwenda na kuhutubu na kufanya kazi, wanapenda kukutana pamoja na kuzungumza; wanapenda watu kuwasikiza, kuwaabudu, na kuwazingira. Wanapenda kuwa na hadhi katika mawazo ya wengine, na wanafurahia wakati wengine wanathamini mifano yao. Hebu tuchanganue asili yao kutoka kwa tabia hizi: Je, asili yao ni ipi? Kama kweli wanatenda kwa njia hii, basi hilo linatosha kuonyesha kuwa wao ni fidhuli na wenye majivuno. Hawamwabudu Mungu hata kidogo; wanatafuta hadhi ya juu zaidi, na wangependa kuwa na mamlaka juu ya wengine, kuwamiliki, na kuwa na hadhi akilini mwao. Huu ni mfano bora wa Shetani. Vipengele vya asili yao vinavyojitokeza ni ufidhuli na majivuno, kutokuwa radhi kumwabudu Mungu, na tamaa ya kuabudiwa na wengine. Tabia kama hizi zinaweza kupa mtazamo dhahiri sana juu ya asili yao(“Jinsi ya Kujua Asili ya Mwanadamu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Kwa kuongezea, inasema katika “Mahubiri na Ushirika kuhusu Kuingia Katika Maisha”: “Kiini na asili ya Shetani ni usaliti. alimsaliti Mungu tangu mwanzo kabisa, na baada ya kumsaliti Mungu alidanganya, akapotosha, akachezea, na akatawala wanadamu duniani walioumbwa na Mungu, akijaribu kuwa sawa na Mungu kama na kuanzisha ufalme tofauti. … Unaona, asili ya Shetani sio ile inayosaliti Mungu? Kutoka kwa yote ambayo Shetani amefanyia wanadamu, tunaweza kuona wazi kwamba Shetani ni kwa kweli pepo mbaya anayepinga Mungu na kwamba asili ya Shetani ni ile inayomsaliti Mungu. Haya yote ni kamili” (“Jinsi ya Kupata Ujuzi wa Asili Yako Potovu” katika Mahubiri na Ushirika juu ya Kuingia Katika Maisha I). Nikizingatia haya maneno, singeweza kujizuia kutetemeka na hofu. Niliona kwamba yale niliyoyaishi kwa kudhihirisha yalikuwa kwa sura ya Shetani kabisa, na nilikuwa mwenye kiburi na mwenye majivuno, na asiyemwabudu Mungu hata kidogo. Mungu aliniinua ili nitekeleze wajibu wangu kanisani, ili nipate kuwaleta ndugu mbele za Mungu nikiwa na uchaji Kwake moyoni mwangu, na kuwafanya watu wawe na nafasi ya Mungu katika mioyo yao, na pia kuwa na uchaji na kumtii Mungu. Lakini nilipokabiliwa na kuinuliwa na Mungu, sikutia maanani nia ya Mungu katika kutekeleza wajibu wangu, na sikuhisi mzigo kuwasaidia ndugu kuingia katika maisha. Badala yake, nilitaka kila mara kuwafanya watu waniangalie kwa makini na kunisikiliza, na kwa ajili ya matamanio yangu, nilijaribu kila mara kujiinua bila kujalisha popote nilipoenda. Nilikuwa hata mwenye wivu kwa waliokuwa wazuri na mwenye husuda kwa wakakamavu, na nilishindana kwa ukaidi na wengine kwa ajili ya ukuu. Kutoka nje, nilikuwa ninashindana na wanadamu, lakini kwa kweli nilikuwa nikipigana dhidi ya Mungu. Hili ni jambo ambalo huudhi sana tabia ya Mungu. Alinihukumu na kuniadibu, kunirudia na kunifundisha nidhamu, na kuninyang’anya hadhi ili kunifanya nijitafakari na kutubu. Niliona kwamba mapenzi ya Mungu kwangu yalikuwa ya kina sana na makubwa sana! Singeweza kujizuia kuhisi majuto na kujilaumu ndani, na hata zaidi nilichukia ya kwamba upotovu wangu ulikuwa wa kina sana. Nilifuata Mungu lakini sikufuatilia ukweli, na badala yake nilifanya kazi kwa bidii bila kufikiri tu kwa sababu ya hadhi na heshima. Nilikuwa nimeshindwa kabisa kuishi kulingana na mapenzi na wokovu wa Mungu. Kadri nilivyojichungua, ndivyo nilivyoona wazi zaidi kuwa misemo niliyoishi kulingana nayo, kama vile “Kama vile mti huishi kwa sababu ya ganda lake, mtu huishi kwa sababu ya uso wake,” na “Mtu huacha jina lake nyuma popote akaapo, kama vile bata bukini hutetea popote arukapo,” yalikuwa uongo yaliyotumiwa na Shetani ili kuwapotosha na kuwadhuru wanadamu. Nilitambua kwamba Shetani alitumia mambo haya kuduwaza nafsi za watu, kupotosha mawazo yao, na kuwafanya kukuza mitazamo mbaya kuhusu maisha, kuwafanya wajitahidi kwa vyovyote vile kufuatilia vitu bure kama vile hadhi, umaarufu, utajiri na heshima, na hatimaye kupotea kutoka kwa na kumsaliti Mungu, ili waweze wote kuzingatia uwongo wake na kuifanyia kazi na kuangamizwa na kudhuruiwa kwa hiari. Nilikuwa mmoja wa watu hao ambao walikuza mtazamo mbaya wa maisha kwa msingi wa udanganyifu wa Shetani, nikawa mwenye kiburi, majivuno, dharau, na asiyekuwa na mahali pa Mungu moyoni mwangu. Niliishi katika upotovu na kumtendea Mungu kama adui. Sasa, sipaswi tena kuenda kinyume na Mungu wakati ninafurahia rehema Yake. Nitajirekebisha kabisa, nitaacha Shetani kabisa, nitampa Mungu moyo wangu kabisa, na kuishi kwa kudhihirisha mtu wa kweli ili kufariji moyo wa Mungu. Baada ya hapo, nilitaka kujua jinsi ya kuendelea na njia yangu ya baadaye, na jinsi ya kufuatilia ukweli ili kukidhi mapenzi ya Mungu. Asante kwa Mungu kwa kuniongoza tena. Kisha niliona maneno ya Mungu: “Leo, hata kama wewe si mfanyikazi, unapaswa kuwa na uwezo wa kutekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu, na kutafuta kujiwasilisha kwa mipango yote ya Mungu. Unapaswa kuwa na uwezo wa kutii chochote Mungu anachosema, na upitie kila aina ya madhila na usafishaji, na ingawa wewe ni dhaifu, moyoni mwako unapaswa bado uwe na uwezo wa kumpenda Mungu. Wale ambao huchukua jukumu katika maisha yao wako tayari kutekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu, na mtazamo wa watu kama hawa kuhusu harakati ni ule sahihi. Hawa ndio watu ambao Mungu anahitaji. … Kama kiumbe wa Mungu, mwanadamu anapaswa kutafuta kutekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu, na kutafuta kumpenda Mungu bila kufanya chaguo lingine kwa kuwa Mungu anastahiki upendo wa mwanadamu. Wale ambao wanatafuta kumpenda Mungu hawapaswi kutafuta faida zozote za kibinafsi au lile ambalo wanatamani binafsi; hii ndiyo njia sahihi kabisa ya ufuatiliaji(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea). Kama kioleza, maneno ya Mungu yalinipa nuru moyoni mwangu, yakinionyesha njia ambayo ninapaswa kuchukua. Mungu anatarajia kuwa watu, bila kujali kama wana hadhi na wamefikwa na hali gani, wanaweza kufanya kila wawezavyo kufuatilia ukweli, na wanaweza kutii upangaji na utaratibu wa Mungu na kutafuta kupenda na kumtosheleza Mungu. Hii ndiyo njia sahihi zaidi ya ufuatiliaji na pia ni njia ya ukweli ya uzima ambayo kiumbe kilichoumbwa kinapaswa kupitia. Hivyo basi niliamua mbele ya Mungu: Ee Mungu, asante kwa kunionyeshea njia ya ukweli ya uzima. Hadhi yangu ya awali ilikuwa kutokana na kuinuliwa na Wewe. Kutokuwa na hadhi leo pia ni kwa sababu ya haki Yako. Mimi ni kiumbe kidogo tu kilichoumbwa. Kuanzia sasa kuendelea, ninataka tu kufuatilia ukweli na kutii mipango Yako yote.

Baadaye, hali yangu ikarudi kawaida haraka kutokana na kusoma maneno ya Mungu na kuishi maisha ya kanisa. Kanisa tena lilinipangia kazi linalonifaa. Pia, nilizingatia kufuatilia ukweli katika kutekeleza wajibu wangu, wakati wowote kitu kilifanyika ningetafuta nia ya Mungu, ningejaribu kujijua mwenyewe, na kupata maneno yanayoambatana na ya Mungu ili kukitatua. Nilipokabiliwa na vitu vilivyohusisha heshima na hadhi, hata ingawa ningekuwa na mawazo fulani katika akili yangu, kwa kupitia maombi na neno la Mungu ningetafuta ukweli na kujitelekeza mwenyewe, na polepole niliweza kuwa na uwezo wa kutodhibitiwa na mambo haya na ningetekeleza wajibu wangu nikiwa na utulivu wa akili. Wakati niliona baadhi ya ndugu ambao hawakuwa wamemwamini Mungu kwa muda mrefu kama mimi wakiaminishwa na agizo, ningeweza, kwa kutafuta ukweli, kuelewa kwamba wajibu ambao unatekelezwa na mtu umejaaliwa na Mungu, na kwamba ninapaswa kutii mipango ya Mungu. Matokeo yake yakawa, niliweza kuwa na uwezo wa kuichukulia kwa njia sawa. Wakati ndugu walinishughulikia na kufichua asili yangu na kiini, ingawa nilihisi nimepoteza heshima, niliweza kuwa mtiifu kutumia sala. Hii ni kwa sababu upendo wa Mungu umeniangukia, na umefaidika sana katika kubadilisha tabia yangu ya maisha. Hapo awali, nilitia maanani katika heshima yangu sana kupindukia na sikuwa radhi kufichulia yeyote, kwa hofu kwamba wengine wangenidharau. Sasa, ninafanya mazoezi ya kuwa mtu mwaminifu kwa mujibu wa mahitaji ya Mungu, na kama nina shida yoyote nitafungua roho yangu kwa ndugu, jambo ambalo hunifanya kuhisi hasa nimefarijika na mwenye furaha katika kina cha roho yangu. Nikiyaona haya mabadiliko ndani yangu, singeweza kujisaidia ila kumshukuru na kumsifu Mungu, kwa maana mabadiliko haya yanaletwa kwangu na kazi ya adabu na hukumu ya Mungu ya siku za mwisho.

Nimemfuata Mwenyezi Mungu kwa miaka kadhaa sasa. Nikifikiria awali, ilikuwa ni sumu za Shetani ambazo zilikuwa zimemomonyoa nafsi yangu. Nilikuwa nimeishi chini ya miliki ya Shetani na niliangamizwa na kupumbazwa naye kwa miaka mingi. Sikujua thamani na maana ya maisha. Sikuweza kuona mwanga, wala sikuweza kupata furaha ya ukweli na shangwe. Nilizama katika dimbwi la simanzi na sikuweza kujinasua. Sasa, ni kupitia adhabu na hukumu ya mara kwa mara niliweza kuachana na madhara ya Shetani na kufikia faraja na uhuru. Nimepata tena dhamiri na mantiki yangu, na pia nina lengo sahihi la kufuatilia, kufuata Mungu katika njia ya ukweli na yenye kung’aa ya uzima. Kupitia adabu na hukumu ya Mungu, kwa kweli nilipitia upendo wa Mungu usio na ubinafsi na wa kweli, na kufurahia baraka na kupokea upendo ambao ulimwengu wa mwanadamu hauwezi kufurahia. Ni Mungu pekee anayeweza kumwokoa mwanadamu kutokana na bahari ya mateso ya Shetani, na ni kazi ya adabu na hukumu tu ya Mungu inayoweza kuwatakasa wanadamu kutokana na sumu za Shetani ndani yao na kuwafanya waishi kulingana na mfano wa mtu wa kweli na watembee katika njia ya ukweli ya uzima. Adabu na hukumu ya Mungu ni nuru. Ni rehema kubwa kabisa, ulinzi bora kabisa, na utajiri wenye thamani zaidi ya maisha ambayo Mungu amewapa watu. Kama vile maneno ya Mwenyezi Mungu yanasema: “… adabu na hukumu ya Mungu ndio uliokuwa ulinzi bora zaidi wa mwanadamu na neema kubwa. Ni kwa njia ya adabu na hukumu ya Mungu ndipo mwanadamu angeweza kugutuka, na kuchukia mwili, na kumchukia Shetani. Nidhamu kali ya Mungu inamweka huru kutokana na ushawishi wa Shetani, inamweka huru kutokana na dunia yake ndogo, na inamruhusu kuishi katika mwanga wa uwepo wa Mungu. Hakuna wokovu bora zaidi kuliko adabu na hukumu!(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu). Asante kwa adhabu na hukumu ya Mungu kwa kuniokoa na kuniruhusu kuzaliwa upya! Katika njia yangu ya baadaye ya kumwamini Mungu, nitajizatiti kufuatilia ukweli, kupokea zaidi adhabu na hukumu zaidi ya Mungu, na kutoa kabisa sumu za Shetani ili kupata utakaso, kupata ujuzi wa kweli wa Mungu, na kuwa mtu ambaye kwa kweli anampenda Mungu.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Baada ya Kupoteza Hadhi Yangu

Huimin Mji wa Jiaozuo, Mkoa wa Henan Kila wakati nilipoona au kusikia kuhusu mtu aliyekuwa amebadilishwa kama kiongozi naye kujisikia...

Mbona Ujihusishe na Hila Unapomtumikia Mungu

Ee Mungu! Asante kwa kufunua asili yangu ya kiburi na majivuno. Kuanzia siku hii na kuendelea, hakika nitachukulia hili kama onyo na kuweka juhudi zaidi katika kujua asili yangu. Nitafanya kazi hasa kulingana na mipangilio ya kazi. Kwa kweli nitakuwa mtu mwenye mantiki, anayezingatia kanuni, na aliye na moyo wa uchaji Kwako.

Uzoefu wa Kutenda Ukweli

Hengxin Jiji la Zhuzhou, Mkoa wa Hunan Sio muda mrefu mno uliopita, nilisikia “Mahubiri na Ushirika juu ya Kuingia Katika Maisha,” jambo...

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp