Ubora Duni wa Tabia Sio Kisingizio

24/01/2021

Na Zhuiqiu, China

Hapo zamani, kila wakati nilipokabiliwa na shida fulani wakati wa kutekeleza wajibu wangu, au nilifanya kazi yangu vibaya, nilidhani ilikuwa ni kwa sababu ubora wa tabia yangu ulikuwa duni sana. Kama matokeo, mimi mara nyingi niliishi katika hali hasi ya kukaa tu. Mara nyingi ningetumia ubora duni wa tabia yangu kama kisingizio cha kuwaachia watu wengine wajibu niliohisi kuwa mgumu, na nilihisi kuwa hakukuwa na chochote kibaya na hili, kwamba nilikuwa nikifikiria kuhusu kazi ya kanisa nilipowauliza watu wengine wafanye kitu fulani kwa sababu ubora wa tabia yangu ulikuwa duni, na singeweza kukifanya vizuri. Ilikuwa tu kwa sababu ya kusoma maneno ya Mungu ndiyo niliugeuza mtazamo huu mbaya, nikigundua kuwa nilikuwa nikiyatazama mambo kupitia dhana na mawazo yangu mwenyewe. Pia nilijifunza jambo kuhusu tabia yangu mwenyewe potovu.

Siku moja, kiongozi alituitaji kuandika barua kumsaidia dada. Dada niliyeshirikishwa naye alikuwa akishughulikia kitu kingine, kwa hivyo aliniomba niishughulikie. Nilianza kutoa visingizio haraka: “Ubora wa tabia yangu ni duni sana. Mimi siko bora katika kuandika na kuhariri maandishi. Ingekuwa bora kama ungeishughulikia.” Hivyo, nilikuwa nikisukuma moja kwa moja chochote kigumu kwa mwenzangu. Baadaye, aliniambia, “Tangu tulipokutana, umekuwa ukisema ubora wa tabia yako ni mbaya. Lakini baada ya kuwa na wewe kwa siku chache nimegundua kuwa una uwezo wa kugundua matatizo katika kazi. Sidhani kuwa ubora wa tabia yako ni mbaya, lakini kila unapokabiliwa na ugumu wowote katika kutekeleza wajibu wako, kila wakati unasema ubora wa tabia yako ni duni, na wakati mwingine hata unausukuma wajibu wako kwa mtu mwingine. Sijui nia yako ya kuendelea kuzungumza kila wakati juu ya jinsi ubora wako wa tabia ni duni ni ipi—inanionekania kana kwamba unabuni haya tu!” Nilipomsikia akisema haya, sikuwa na la kusema, lakini moyo wangu ulijawa na chuki: “Ninaposema ubora wa tabia yangu ni mbaya, nasema ukweli. Hujui ukweli, na umenielewa visivyo.” Baada ya hapo, nilitafakari kuhusu kwa nini dada huyo alisema hivyo. Sikuwa nasema uongo niliposema kuwa ubora wa tabia yangu ulikuwa duni—angewezaje kusema kuwa nilikuwa na nia? Moyoni mwangu, sikuweza tu kuelewa jambo hilo.

Wakati mmoja, katika mkutano na wafanyikazi wenzangu, niliwaambia ndugu zangu wengine kuhusu mkanganyiko niliokuwa nao. Nilipitia sababu za kwa nini nilidhani ubora wa tabia yangu ulikuwa duni, moja baada ya nyingine: Kwa mfano, nilipiga chapa polepole sana, mtindo wangu wa uandishi haukuwa mzuri sana. Nilipokuwa nikifanya kazi ya maandishi na mwenzangu, alifanya uchapaji na uhariri zaidi, na alipokuwa akishunghulika na kazi ya kanisa, aligundua matatizo kwa haraka sana, ilhali mimi nilikuwa nafanya pole pole, na kadhalika. Baada ya kunisikia nikishiriki, kiongozi wetu Ndugu Liu alisema, “Dada, ni kulingana na vitu hivi ndiyo tunapima ikiwa ubora wa tabia wa mtu ni mzuri au mbaya? Je, hili linaambatana na ukweli? Je, linaambatana na mapenzi ya Mungu? Sote tunajua kuwa watu ulimwenguni wanathamini kipaji na ubongo sana. Wote walio wepesi wa akili haraka, wanaojieleza kwa wazi zaidi, na wanaoeweza kushughulikia mambo ya ulimwengu wa nje kwa ustadi ni watu wenye ubora mzuri wa tabia, ilhali wale ambao ni holela katika maongezi, wasiojua na wasio na elimu nzuri wanaonekana kama wasio na ubora wowote wa tabia; hivyo ndivyo wasioamini wanavyoliona. Sisi tunaomwamini Mungu tunapaswa kuangalia mambo kulingana na maneno ya Mungu. Je, tumetafuta mapenzi ya Mungu katika jambo hili? Je, ni kwa msingi upi ambao Mungu hupima ikiwa ubora wa tabia wa watu ni mzuri au mbaya? Na ubora mzuri na mbaya wa tabia ni upi hasa?” Nilikuwa nikitikisa kichwa changu, na Ndugu Liu aliendelea kushiriki: “wacha tusome kifungu cha mahubiri ya Mungu: “Tunapimaje kiwango cha tabia ya watu? Njia sahihi zaidi ni kupima ubora wa tabia yao kulingana na kiwango ambacho wanaelewa ukweli. Watu wengine wanaweza kujifunza utaalam haraka sana, lakini wanaposikia ukweli, wanachanganyikiwa na wanalala, huwashangaza, hakuna chochote wanachosikia kinaingia, na hawaelewi wanachosikia—huu ndio ubora duni tabia. Kwa watu wengine, unawaambia wao ni wenye tabia duni na hawakubaliani. Wanafikiri kwamaba kuwa na elimu kubwa na ujuzi ina maana wao wana ubora sawa wa tabia. Je! Elimu bora inaonyesha ubora sawa wa tabia? Haimaanishi hivyo. Ubora wa tabia wa watu hupimwa kulingana na kiwango ambacho wanaelewa maneno ya Mungu na ukweli. Hii ndio njia ya kawaida zaidi, sahihi zaidi ya kuifanya. Hakuna matumizi katika kujaribu kupima ubora wa tabia wa mtu kwa njia nyingine yoyote. Watu wengine wana lugha ya fedha na wana akili ya haraka, na ni wazuri sana kuendelea na wengine—lakini wanaposoma maneno ya Mungu na kusikiliza mahubiri, hawaelewi chochote. Wanapozungumza juu ya uzoefu wao wenyewe na ushuhuda, wanajidhihirisha kuwa ni wapenda kazi tu, na wote wanaweza kuhisi kuwa hawana uelewa wa kiroho. Hawa sio watu wenye ubora wa tabia sawa(“Kuelewa Ukweli Ni Muhimu Kutimiza Wajibu Wa Mtu Vizuri” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Kutoka kwa maneno ya Mungu tunaona kwamba ikiwa ubora wa tabia ya mtu ni mzuri au mbaya inategemea uwezo wake wa kuelewa maneno ya Mungu. Hiki sicho kile wasioamini wanamaanisha wanaposema mtu ana ubora mzuri wa tabia au ana kipaji na mwerevu. Watu walio na ubora mzuri wa tabia wanaweza kuelewa mapenzi ya Mungu wanapomaliza kusoma maneno Yake, wanaweza kupata njia ya kutenda na kuingia katika ukweli, na wanaweza kutenda kulingana na kile ambacho Mungu anataka. Kwa upande mwingine, kuna wale ambao wanaonekana kuwa watu werevu sana na ni wastadi katika kushughulikia mambo ya ulimwengu wa nje—lakini wanachanganyikiwa mara tu wanapokabiliwa na ukweli wa maneno ya Mungu. Watu kama hao hawawezi kusemwa kuwa wenye ubora mzuri wa tabia. Ni kama tu jinsi watu wengine wenye maarifa, walioelimika wanaonekana kuwa na vipaji na wenye busara kwa nje, lakini hawawezi kuelewa ukweli wa maneno ya Mungu. Wengine wao hata wana mtazamo wa kipuuzi kuhusu mambo. Na kwa hivyo, kuwa mwenye elimu ya juu, mwepesi wa akili, na mwenye uwezo hakuwakilishi ubora mzuri wa tabia, na wala hivi sivyo viwango ambavyo hutumiwa kupima ubora wa tabia wa mtu. Cha muhimu ni ikiwa watu wanaelewa roho, ikiwa wana uwezo wa kuelewa ukweli. Hatuwezi kutegemea dhana na mawazo yetu wenyewe kupima ikiwa ubora wa tabia ya mtu ni mzuri au mbaya!” Baada ya kusikia haya, ghafla nilielewa: Ilitukia kwamba imani zangu zilikuwa tu dhana na mawazo—hazikulingana na ukweli.

Kisha, dada mmoja alipata vifungu viwili vya maneno ya Mungu na akaniomba nivisome. Maneno ya Mungu yanasema: “Jinsi Mungu anavyowatendea watu haitegemei umri wao, mazingira gani waliozaliwa, au wana talanta gani. Badala yake, Yeye huwatendea watu kulingana na mtazamo wao juu ya ukweli, na kutendea huku kunahusiana na tabia zao. Ikiwa una mtazamo sahihi wa kuukabili ukweli, una mtazamo wa kuukubali ukweli, na uchukue mtazamo wa unyenyekevu, basi hata ikiwa wewe ni mwenye ubora duni wa tabia, Mungu bado atakupa nuru na kukuruhusu upate kitu. Ikiwa wewe ni mwenye ubora mzuri wa tabia lakini daima ni mwenye kiburi, ukifikiria kila wakati kuwa wewe uko sahihi na daima kutokuwa radhi kukubali chochote ambacho wengine wanasema, na unapinga kila wakati, basi Mungu hatafanya kazi ndani yako. Mungu atasema kwamba tabia yako ni mbaya na hustahili kupokea chochote, na hata Mungu atakupokonya kile ulichokuwa nacho. Huku ndiko kunakojulikana kama kufunuliwa(“Mtu Akitenda Ukweli Tu Ndipo Anaweza Kuwa na Ubinadamu Wa Kawaida” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). “Wakati mtu anachukulia mambo kwa uzito, anawajibika, ni mwenye kujitolea, na anayefanya kazi kwa bidii, kazi itafanywa vizuri. Wakati mwingine, huna moyo kama huo, na huwezi kupata au kugundua kosa ambalo ni wazi kama mchana. Ikiwa mtu angekuwa na moyo kama huo, basi, kwa msukumo na mwongozo wa Roho Mtakatifu, wangeweza kutambua suala hilo. Lakini ikiwa Roho Mtakatifu alikuongoza na kukupa ufahamu kama huo, hukuruhusu kuhisi kuwa kuna kitu kibaya, lakini haukuwa na moyo kama huo, bado ungeweza kutambua shida. Kwa hivyo, hii inaonyesha nini? Inaonyesha kuwa ushirikiano wa watu ni muhimu sana, mioyo yao ni muhimu sana, na mahali wanapoelekeza mawazo na maoni yao ni muhimu sana. Kuhusu makusudi yao ni yapi na ni kiasi kipi cha juhudi wanaweka katika kutekeleza wajibu wao, Mungu huchunguza na anaweza kuona. Ni muhimu kwamba watu waweke mioyo na nguvu zao zote katika kile wanachofanya. Ushirikiano wao ni muhimu pia. Kujitahidi kutokuwa na majuto juu ya wajibu ambao mtu amekamilisha na juu ya vitendo vya zamani vya mtu, na kufika mahali ambapo mtu hana deni la Mungu—hii ndiyo maana ya kutoa moyo na nguvu zote za mtu(“Jinsi ya Kusuluhisha Shida ya Kuwa Mvivu na Mzembe Wakati wa Kutekeleza Wajibu Wako” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Baada ya kusoma maneno ya Mungu Dada huyo alisema, “Maneno ya Mungu yanaonyesha kwamba mtazamo wetu wakati tunatekeleza wajibu wetu ni muhimu sana—ni muhimu sana. Kama tuna fikira zinazofaa, kama tunaweza kuitoa mioyo na nguvu zetu zote katika kutekeleza wajibu wetu, Mungu ataona, na atatutendea kulingana na mtazamo wetu kwa wajibu wetu. Hata kama sisi ni wenye ubora duni wa tabia, Mungu bado atatupa nuru na kutuongoza. Ikiwa tuna ubora sawa lakini hatuna fikira sahihi, na hatuko tayari kulipa gharama na kushirikiana na Mungu, au ikiwa tuna kiburi na tunajishikilia wenyewe, au kufanya tu ili kupata umaarufu na jina basi hatutakosa tu kutekeleza wajibu wetu vizuri, lakini pia tutakataliwa na Mungu. Hii ni tabia ya haki ya Mungu. Tukiwaangalia ndugu walio karibu nasi kupitia katika maneno ya Mungu, tunaona kwamba wengine ni wenye ubora wa kawaida wa tabia lakini wana nia sahihi katika kutekeleza wajibu wao; wanapokabiliwa na ugumu, wanawajibika wenyewe kutafuta ukweli, na kulenga kuingia katika kanuni, na wanazidi kufanikiwa katika kutekeleza wajibu wao. Ilhali kuna ndugu wengine wanaoonekana kwetu kuwa hasa wenye ubora mzuri wa tabia, na walio na ufahamu safi wa maneno ya Mungu, lakini ni wenye majivuno, walioridhika, hawasikilizi ushauri wa watu wengine, na hujichukulia utukufu wa Mungu kila wanapokuwa na mafanikio kidogo katika kutekeleza wajibu wao. Wanajionyesha katika nafasi wanayopata, wakihangaika kupata faida na umaarufu. Wengine huivuruga kazi ya kanisa na hunyang'anywa ustahilifu wao wa kutekeleza wajibu wao; wengine wao huwa wapinga-kristo baada ya kutenda maovu mengi na hufukuzwa kutoka kanisani. Ukweli huu hutuonyesha kwamba kama ubora wa tabia ya mtu ni mzuri au mbaya hauamui ikiwa atasifiwa na Mungu; kilicho muhimu ni ikiwa anafuatilia ukweli na kutekeleza wajibu wao kwa moyo na akili zao zote.”

Kisha, ndugu walitumia uzoefu wao wenyewe kuzungumza kuhusu hatari na matokeo ya kujielezea kulingana na dhana na mawazo yao wenyewe. Hapo tu ndipo niligundua jinsi kutoelewa ukweli kulivyokuwa kujinga; sikuwa nimetafuta ukweli, na badala yake nilikuwa nimejieleza kuwa mwenye ubora duni wa tabia kwa kuishi katika dhana na fikira zangu, kiasi kwamba mara nyingi niliwasukumia watu wengine wajibu mgumu. Sikujaribu kujiboresha, wala sikumtegemea Mungu au kwa kweli kulipa gharama ya kuvunja vizuizi hivi, jambo ambalo hata lilinifanya nisiweze kutekeleza wajibu niliokuwa na uwezo wa kutekeleza. Sikuweza tu kupata mafunzo halisi, au kukua katika ukweli na maisha, lakini hili liliathiri moja kwa moja ufanisi wangu katika kutekeleza wajibu wangu. Nilifikiria juu ya jinsi yule dada niliyefanya naye kazi alivyoweza kupata matatizo kwa haraka. Ingawa hili lilihusika na tabia yake ya asili, la muhimu zaidi lilikuwa kwamba, kwa sababu ya mtazamo wake wa kuwa makini na kuwajibika katika wajibu wake, aliweza kumtegemea Mungu na kupambana na matatizo moja kwa moja alipokumbana nayo. Ni hapo tu ndipo alipopata nuru na mwangaza na Roho Mtakatifu. Mimi, kwa upande mwingine, nilijaribu kukwepa matatizo nilipokumbana nayo, na nikatumia ubora duni wa tabia kama kisingizio cha kujiondoa kwenye wajibu. Sikumtegemea Mungu na kuwajibika mwenyewe kujaribu kutatua tatizo kwa kutafuta ukweli unaofaa, ambayo ilimaanisha sikuweza kuipata kazi ya Roho Mtakatifu. Kutokana na hili, niliona kuwa Mungu yuko na usawa na ni mwenye haki kwa wote. Kupitia kwa ushirika, niligundua pia kuwa Mungu anataka kutoka kwetu kulingana na kile tunachoweza. Sio suala la Yeye kumsukuma mtu afanye jambo asiloweza. Napaswa kujitendea haki mimi mwenyewe; badala ya kuzingatia ubora wa tabia yangu, napaswa kulenga tu kuweka nguvu zangu zote katika kutekeleza wajibu wangu. Napaswa kutafuta na kutafakari kanuni za ukweli, nijifunze kutokana na uwezo wa wengine, nisikilize ushauri wa watu wengine, na kuushirikisha katika kile nilichotenda kwa kweli—na baada ya muda, ningekuwa na uhakika wa kufaidika na kukua.

Baadaye, ukosoaji wa dada huyo ulisikika masikioni mwangu: “Sijui nia yako ya kuendelea kila wakati kuzungumza juu ya jinsi ubora wako wa tabia ni duni ni ipi.” Alikuwa sahihi—kila wakati nilikuwa mwepesi wa kusema kuwa ubora wa tabia yangu ni mbaya. Je, ni nia na tabia gani potovu ambazo zilikuwa zikinidhibiti kwa siri?

Siku moja, nilisoma maneno haya ya Mungu: “Lazima ujichunguze mwenyewe kwa makini ili kuona kama wewe ni mtu sahihi. Je, malengo yako hufanywa Nami katika mawazo? Je, maneno na matendo yako husimama mbele Yangu? Mimi huchunguza fikira na mawazo yako yote. Je, si unajihisi mwenye hatia? Unajitwika sura ya bandia ili wengine waone na wewe kwa upole unajifanya kujidai; hili hufanyika ili ujikinge mwenyewe. Wewe hufanya hili ili kuyaficha maovu yako, na hata kutafuta njia za kuusukuma huo uovu kwa mtu mwingine. Ni hila gani hukaa ndani ya moyo wako!” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 13). Baada ya kusoma maneno ya Mungu nilianza kutafakari kujihusu: Ninapokabiliwa na wajibu ambao sikuwa nimewahi kufanya hapo awali, jambo la kwanza kufanya lingekuwa kuwaambia wale ndugu wengine kuwa ubora watabia yangu ni duni, kwa sababu nilihofu kuwa wangenidharau kama ningeufanya wajibu huo vibaya. Nilifanya hivyo kwa sababu ya heshima na hadhi yangu mwenyewe. Nilifanya hivi ili isiwe kosa langu ikiwa nitaufanya vibaya; sio kwamba sijaweka nguvu zangu zote ndani ya wajibu huo, lakini ni kwamba umezidi ubora wangu wa tabia. Kila nilipokumbana na ugumu wowote katika kutekeleza wajibu wangu, sikuwa tayari kuteseka na kulipa gharama ya kuukabili ana kwa ana. Niliogopa uwajibikaji, pia. Kwa hivyo nilitumia tu ubora duni wa tabia yangu kama kisingizio cha kuusukuma wajibu wangu kwa mtu mwingine, kumfanya afikirie kwamba nilikuwa mwenye busara na ninajitambua. Karibu kila wakati nilipopitia matatizo na nililazimika kulipa gharama au kulazimika kuwajibikiajambo fulani, nilikuwa nikirudi nyuma. Kwa kweli, nilikuwa nikiishi kulingana na falsafa ya uhusiano wa binadamu ya kishetani ya “kaa kimya kwa ajili ya kujilinda na utafute tu kuitoroka lawama.” Lilionekana kama jambo la busara sana—kutumia njia zangu mwenyewe za ujanja kuzuia uwajibikaji—lakini kwa kweli nilikuwa nimekosa fursa nyingi za kutafuta na kuelewa ukweli. Kwa kweli, ubora wa tabia ambao Mungu humpa kila mmoja wetu unafaa kwa kusudi; lakini sikuwa nimeuweka moyo na nguvu zangu zote katika kwa msingi wa kile nilichoweza kufanikisha, ili niipate kazi ya Roho Mtakatifu na kuboresha ubora wa tabia yangu; badala yake, kila wakati nilitumia ubora wangu duni wa tabia kama kisingizio cha kutotenda ukweli, ili kujaribu kumhadaa na kumdanganya Mungu. Je, huu sio ujanja, uwovu sana? Na ningewezaje kuongozwa na Mungu hivyo?

Maneno ya Mungu yanasema, “Nawathamini sana wale wasio na shaka kuhusu wengine na pia nawapenda sana wale wanaokubali ukweli kwa urahisi; kwa aina hizi mbili za wanadamu Ninaonyesha utunzaji mkubwa, kwani machoni Pangu wao ni waaminifu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani). “Katika mstari unaofuata, ‘Ingawa ubora wangu wa tabia ni duni, nina moyo mwaminifu.’ Watu wengi wanaposikia mstari huu, wanahisi vizuri, sivyo? Jambo hili linahusisha mahitaji ya Mungu kwa watu. Mahitaji yapi? Ikiwa watu wamepungukiwa katika ubora wa tabia, sio mwisho wa dunia, lakini lazima wawe na moyo mwaminifu na, kwa hivyo, wataweza kupokea sifa za Mungu. Haijalishi hali yako ni ipi, lazima uwe mtu mwaminifu, uzungumze kwa uaminifu, utende kwa uaminifu, uweze kutekeleza wajibu wako kwa moyo na akili yako yote, na uwe mwaminifu, na lazima usiikwepe kazi yako, usiwe mjanja au mdanganyifu, usiwe mjanja, usijaribu kuwalaghai wengine, au kuzungumza bila uwazi; lazima uwe mtu anayependa ukweli na anayefuatilia ukweli. … Unasema, ‘Ubora wangu wa tabia uko chini, lakini moyoni mimi ni mwaminifu.’ Wakati wajibu unakuangukia, hata hivyo, unaogopa kuteseka au kuwa unaweza kuwa usipoutimiza vizuri, utalazimika kuuwajibikia, kwa hivyo unatoa visingizio kuukwepa. Je, haya ni maonyesho ya mtu mwaminifu? Ni wazi kuwa siyo. Hivyo basi, mtu mwaminifu anapaswa kutendaje? Anapaswa kukubali na kutii, na kisha kujitolea kabisa katika kutekeleza wajibu wake kadiri ya uwezo wake, akijitahidi kuridhisha mapenzi ya Mungu. Hili linaonyeshwa kwanjia kadhaa. Njia moja ni kwamba unapaswa kukubali wajibu wako kwa uaminifu, kutofikiria kuhusu kitu kingine chochote, na usiwe shingo upande kulihusu. Usipangie kufaidika kwako mwenyewe, Haya ni maonyesho ya uaminifu. Njia nyingine ni kuweka nguvu zako na moyo wako wote katika hilo. Unasema, ‘Hiki ndicho kila kitu ninachoweza kufanya; nitaanza kukifanya chote, na kukikitoa kwa Mungu kabisa.’ Je, si haya ni maonyesho ya uaminifu? Unatoa kila kitu ulicho nacho na kila unachoweza kufanya—haya ni maonyesho ya uaminifu(“Ni kwa Kuwa Mtu Mwaminifu tu Ndiyo Mtu Anaweza Kuwa na Furaha Kweli” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Maneno ya Mungu yalinipa njia ya kutenda: Mungu hajali ikiwa ubora wa tabia ya watu ni mzuri au mbaya; kilicho muhimu ni ikiwa wana moyo ambao ni mwaminifu, ikiwa wanaweza kukubali ukweli, na kuuweka katika vitendo. Ingawa ubora wa tabia yangu ni duni, na mimi ni mpole kidogo katika kuelewa ukweli, na wakati mwingine nafuata mafundisho, kama moyo wangu ni mwaminifu, na mimi hufuatilia ukweli kila wakati ili nitatue tabia yangu potovu wakati natimiza wajibu wangu, ikiwa nafanya yote niwezayo kutekeleza yale ambayo Mungu anahitaji, basi nitapokea mwongozo na baraka za Mungu, na hatua kwa hatua nitaweza kuelewa ukweli. Ninapoingia katika ukweli nitaweza kufidia upungufu wangu kuhusu ubora wangu duni wa tabia, na nitakua bora zaidi na zaidi katika kuelewa na kuona mambo. Baada ya kuelewa mapenzi ya Mungu, nilianza kumtegemea Mungu ili niwe bora zaidi nilipotimiza wajibu wangu. Sikuwa navitoa tena vitu ambavyo havikuwa wazi kwangu, ambavyo sikuelewa, kwa watu wengine, lakini nilijaribu sana kutafuta na kuvisuluhisha mwenyewe. Shukrani ziwe kwa Mungu! Nilipotenda kama anavyohitaji Mungu, mimi pia niliweza kuona matatizo katika wajibu wangu—na ingawa kulikuwa na nyakati ambazo masuala kadhaa magumu yalisalia kuwa magumu kwangu, kwa kutafuta kanuni za ukweli pamoja na ndugu, polepole yalionekana wazi kwangu, na nilihisi mwepesi na huru zaidi nilipotekeleza wajibu wangu.

Kwa sababu ya kupitia mazingira niliyowekewa na Mungu, nilipata ufahamu fulani wa upotovu na upungufu wangu, na nikajua jinsi ya kukabiliana na maswala yanayohusiana na ubora wa tabia yangu. Nilipokuwa nikitekeleza wajibu wangu hapo zamani, sikuzingatia kutafuta ukweli, wala sikujaribu kushughulikia tabia yangu potovu. Siku zote niliona mambo kupitia dhana na mawazo yangu mwenyewe, ambayo yalinisababisha kujieleza kinaganaga mara nyingi, na kujaribu kujiondoa katika vitu kwa kusema ubora wa tabia yangu ulikuwa duni. Utendaji wangu wa wajibu ulikuwa umejaa uzembe, niliichelewesha kazi ya kanisa, na nikapata hasara katika maisha yangu mwenyewe. Sasa naelewa kuwa ubora wa tabia wa kila mtu umeshapangiwa kabla na Mungu na ni sehemu ya malengo matukufu ya Mungu. Sipaswi kuwekewa mipaka na ikiwa ubora wa tabia yangu ni mzuri au mbaya. Katika siku zijazo, nitajaribu kutafuta ukweli katika kila jambo, kutenda kwa maadili, na kuwa mtu mwaminifu ili nimridhishe Mungu.

Inayofuata: Baada ya Uwongo

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Baada ya Kupoteza Hadhi Yangu

Huimin Mji wa Jiaozuo, Mkoa wa Henan Kila wakati nilipoona au kusikia kuhusu mtu aliyekuwa amebadilishwa kama kiongozi naye kujisikia...

Kushikilia Wajibu Wangu

Na Yangmu, Korea ya Kusini Nilikuwa nikihisi wivu sana nilipowaona ndugu wakifanya maonyesho, wakiimba na kucheza kwa kumsifu Mungu....

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp