Niliona Kimo Changu cha Kweli kwa Dhahiri

14/01/2018

Ding Xiang Jijini Tengzhou, Mkoa wa Shandong

Katika mkutano wa viongozi wa kanisa niliowahi kuhudhuria, kiongozi wa kanisa aliyekuwa amechaguliwa hivi karibuni alisema: “Sina kimo cha kutosha. Mimi ninahisi sifai kuutimiza wajibu huu. Mimi ninahisi kushinikizwa na vitu vingi sana, kwa kiwango kwamba mimi sijaweza kupata usingizi kwa siku na usiku kadhaa mtawalia….” Wakati huo, mimi nilikuwa nimebeba mizigo katika kumfuatilia Mungu, kwa hivyo niliwasiliana naye: “Kazi zote hufanywa na Mungu; mwanadamu hushirikiana kidogo tu. Ikiwa tunahisi kulemewa, kuja mbele za Mungu mara nyingi na kumtegemea Mungu bila shaka kutatufanya tuone uweza wote na hekima ya Mungu. Kuhisi mzigo kutokana na kazi zetu ni kitu kizuri. Lakini ikiwa mzigo unageuka kuwa mfadhaiko, huo utakuwa kizuizi, na utasababisha uhasi na hata kutoelewana kuhusiana na Mungu.” Chini ya mwongozo wa Mungu, nilihisi mawasiliano yangu yalikuwa hasa yenye mwanga. Dada pia alitambua ya kwamba alikuwa katika hali ambapo Mungu hakukuwa na nafasi katika moyo wake, na kwamba alikuwa akijifanyia mwenyewe badala ya kumtegemea Mungu, na hivyo akapata njia ya kuingia. Mimi nilikuwa na furaha sana wakati huo kwa sababu nilidhani ningeweza kutatua shida ya yule dada, kudhibitisha kwamba nilimiliki uhalisi wa sehemu hii ya ukweli.

Miezi miwili baadaye, kanisa lilinibadilisha kazi hadi kukusanya hati fulani. Nilipojihusisha na kazi hii mara ya kwanza, kwa kuwa sikuelewa kanuni zinazohusika, sikuwa na budi ila kujipata katika hali ya uhasi na mapigano nilipokabiliwa na hati zote zilizohitaji kukusanywa: Sikuelewa chochote, na bado nililazimika sio tu kutimiza wajibu huu lakini hata nilipewa jukumu la kutafuta upungufu ulio katika hati. Ilikuwa kuuliza mengi kupita kiasi kutoka kwangu! Nilihisi tu shinikizo nyingi na nisingeweza kutulia, na pia sikujua jinsi ya kumtegemea Mungu. Nilikuwa na wasiwasi mwingi nisingeweza kulala kwa siku na usiku tatu mtawalia. Nilikuwa nimechanganyikiwa mno katika nikikabiliana na hali yangu Nilipomsaidia yule kiongozi mpya wa kanisa kutatua shida yake, nilijihisi kana kwamba nilielewa kabisa kipengele hiki cha ukweli. Lakini iweje kwamba nilipopatana na shida kama hiyo sasa, sikujua namna ya kukabiliana na tukio kama hili. Nilikuja mbele za Mungu nikiwa nimebeba kuchanganyikiwa na mshangao wangu.

Baadaye, niliyaona maneno ya Mungu katika “Kazi na Kuingia (2)”: “Mwanadamu anapofanya kazi na kuzungumza, au wakati mwanadamu anapofanya maombi katika shughuli zake za kiroho, ndipo ukweli utawekwa wazi kwao. Hata hivyo, katika uhalisi, kile ambacho mwanadamu anakiona ni nuru tu iliyoangaziwa na Roho Mtakatifu (kwa kawaida, hii inahusiana na ushirikiano kutoka kwa mwanadamu) na sio kimo halisi cha mwanadamu. Baada ya kipindi cha kupitia ambapo mwanadamu anakabiliwa na shida na majaribu fulani, kimo cha kweli cha mwanadamu hudhihirika katika mazingira kama hayo. … Ni baada tu ya mizunguko kadhaa ya uzoefu kama huo ndipo wengi wa jinsi hiyo ambao wameamshwa ndani ya roho zao watatambua kwamba haukuwa uhalisi wao hapo nyuma, bali ni mwangaza wa muda tu kutoka kwa Roho Mtakatifu, na mwanadamu alipokea nuru tu. Roho Mtakatifu anapompa mwanadamu nuru ili aelewe ukweli, mara nyingi inakuwa katika namna ya wazi na tofauti, bila kueleza jinsi ambavyo mambo yalitokea au kule yanakoenda. Yaani, Hayajumuishi matatizo ya mwanadamu katika ufunuo huu, na badala yake Anatoa ufunuo moja kwa moja. Mwanadamu anapokabiliana na matatizo katika kuingia, basi mwanadamu anaijumuisha nuru ya Roho Mtakatifu, na huu unakuwa uzoefu halisi wa mwanadamu(Neno Laonekana katika Mwili). Nilipokuwa nautafakari fungu hili, nilielewa: Ukweli niliouelewa nilipomsaidia yule dada kutatua shida yake ulikuwa umetoka kwa kuangaziwa kwa Mungu. Ilikuwa kwa sababu ya ushirika wangu wakati huo ndiyo nilipokea kupata nuru kwa Roho Mtakatifu. Lakini hakikuwa kimo changu cha kweli na pia sikuonyesha ya kwamba nilikuwa nimepokea kipengele hicho cha ukweli. Roho Mtakatifu alinipa nuru ili nielewe ukweli wakati huo kwa sababu ulikuwa unahitajika katika kazi yangu, na kupitia ushirika wangu Alinisaidia kutatua shida na ugumu katika kazi yangu. Lakini kabla sijapata ujuzi halisi kuhusiana na hili, kimo changu bado kilikuwa kidogo hivi tu. Kwa hivyo ninapokumbana na ugumu katika kuingia, ni kupitia kushirikisha nuru ya Roho Mtakatifu pekee ndio ukweli unaweza kuwa uzima wangu.

Chini ya kupewa nuru na mwelekezo wa neno la Mungu, niliutuliza moyo wangu na nikamtazamia na kumtegemea Mungu, na kupitia ulinganisho wa makini na kuzingatia kanuni zinazohusu kukusanya hati, nilipata nuru na mwelekezo wa Mungu bila kujua, kuniwezesha kubaini matatizo katika hati hatua kwa hatua, na kupata uwazi mwingi mno katika kuwaza kwangu nilipokuwa nikizibadilisha hati hizo. Niliweza pia kutoka nje ya uhasi na kutoelewa kwangu hatua kwa hatua.

Shukrani ziwe kwa Mungu. Kupitia uzoefu huu niliweza kuona kimo changu halisi kwa wazi, nikibadilisha kukengeuka katika kuelewa kwangu. Ilinifanya nigundue kwamba kuelewa kwangu kwa ukweli unaopewa nuru na Roho Mtakatifu hakukumaanisha kwamba nilimiliki hali halisi ya kipengele hiki cha ukweli. Kutoka sasa kuendelea, niko radhi zaidi kuleta kupata nuru kwa Roho Mtakatifu katika maisha halisi kutenda na kuingia, ili kwamba ukweli huu uweze kuwa hali halisi ya maisha yangu kwa kweli.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Katikati ya Jaribu la Kifo

Na Xingdao, Korea ya Kusini Mwenyezi Mungu anasema, “Mungu amekuja kufanya kazi ulimwenguni ili kumwokoa mwanadamu aliyepotoka—hakuna uongo...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp