Mchakato wa Mbadiliko wa Muumini Mwenye Kiburi

16/01/2018

Zhang Yitao, Mkoa wa Henan

“Ee Mungu! Hukumu Yako ni ya kweli kabisa, imejaa haki na utakatifu. Ufunuo Wako kuhusu ukweli wa upotovu wa wanadamu umenifichua kabisa. Nafikiri juu ya jinsi nilivyojitumia na kujishughulisha kwa miaka mingi ili tu kupata baraka Zako. Nilimwiga Paulo, kufanya kazi kwa bidii, ili niweze kujitokeza kwa umati. Maneno Yako ya hukumu yalinifanya nione jinsi nilivyokuwa mbinafsi na wa kudharauliwa. Ninaanguka chini nikiwa na aibu na fedheha, sistahili hata kuutazama uso Wako. Mara nyingi nimekumbuka njia ambayo nimeitembea. Ni Wewe uliyenitunza na kunilinda, Ukiniongoza katika kila hatua ya njia hadi kufikia sasa. Naona jinsi inavyokugharimu kuniokoa, yote ni upendo Wako. Ee Mungu! Kwa kupitia hukumu Yako, nimeonja upendo Wako wa kweli. Ni hukumu Yako ambayo huniruhusu kujijua mwenyewe na kutubu kwa kweli. Mimi ni mpotovu sana kiasi kwamba nahitaji sana Unihukumu na kunitakasa Bila hukumu Yako, ningetapatapa gizani tu. Ni maneno Yako ambayo yameniongoza kwenye njia ya maisha ya nuru. Nahisi kuwa kukupenda na kuishi kwa ajili Yako ni ufuatiliaji wa maana zaidi. Mara nyingi sana nimekumbuka njia ambayo nimeitembea. Hukumu Yako na kuadibu Kwako ni baraka Zako na upendo wa kweli. Nitaelewa ukweli na kufikia mapenzi halisi zaidi Kwako. Niko tayari bila kujali nitateseka kiasi gani” (“Mungu Amenipa Upendo Mwingi Sana” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Kila wakati ninapoimba wimbo huu, mimi hufikiria juu ya wokovu wa Mungu kwangu kupitia miaka hii yote, na nimejaa shukrani Kwake. Ilikuwa ni hukumu ya Mungu na kuadibu vilivyonibadilisha. Lilinifanya—kuwa mwana mwenye kiburi, kutaka makuu, mwasi—kuonekana kidogo zaidi kama mwanadamu. Kwa kweli ninatoa shukrani kwa ajili ya wokovu wa Mungu kwangu!

Nilizaliwa mashambani. Kwa sababu familia yangu ilikuwa maskini na wazazi wangu walikuwa waaminifu, mara nyingi walikuwa wakidanganywa. Kuanzia wakati nilipokuwa mdogo watu waliniangalia kwa dharau, na kupigwa na kudhulumiwa kulikuwa matukio ya kawaida. Hili mara nyingi lilinifanya kuhuzunika kiasi cha kutokwa na machozi. Niliweka kila kitu nilichokuwa nacho katika masomo yangu ili kwamba nisingelazimika kuishi maisha ya aina hiyo tena, ili wakati wa baadaye ningepata kazi kama afisa wa serikali, kuwa mtu mwenye madaraka, na kila mtu angeweza kunipa heshima kubwa. Lakini mara tu nilipomaliza shule ya kati na nilikuwa nikijiandaa kwa mtihani wa kuingia shule ya sekondari, Mapinduzi ya Kitamaduni yakaanza. Kundi la wanafunzi lenye hadhi ya kijeshi la Red Guards likaasi, wafanyakazi wakagoma, wanafunzi wakagoma. Kila siku ilihusika katika mapinduzi. Ilikuwa vurumai, watu walikuwa na hofu, na mfumo wa mtihani wa kuingia chuo ulipigwa marufuku. Kwa hivyo, nilipoteza fursa ya kutahiniwa kuingia shuleni. Nilihangaika—nilihisi vibaya kana kwamba nilikwisha kuwa mgonjwa kwa uzito kabisa. Baadaye, nilifikiria: Ingawa siwezi kutahiniwa kuingia shuleni au kuwa afisa wa serikali, nitafanya kazi kwa bidii ili kupata pesa. Almradi nina pesa, watu wataniheshimu sana. Kuanzia hapo kuendelea, nilikuwa natafuta njia za kutengeneza pesa kila mahali. Kwa kuwa familia yangu ilikuwa masikini, sikuwa na fedha zozote za kuanza kufanya biashara. Kupitia kwa jamaa na marafiki, niliweza kukopa Yuan 500 ili kuanzisha duka la kuuza nyama ya nguruwe iliyopikwa kwa mvuke. Wakati huo nyama iligharimu senti sabini tu kwa ratili moja, lakini baada ya kununua vifaa nilivyohitaji, kile kilichobaki kutoka kwa hiyo Yuan 500 hakikuwa cha kutosha hasa. Kila wakati nilipokuwa na mapato kiasi yalikwenda moja kwa moja kwa ufadhili wa biashara hiyo. Mara nilipokuwa nimepata pesa zozote ningelipa deni langu. Nilivumilia shida nyingi ili niweze kuishi maisha bora zaidi kuliko wengine. Kutoka asubuhi hadi mwishoni mwa siku, sikuwa na wakati wa ziada. Baada ya miaka kadhaa ya kazi ngumu, ujuzi wangu ukawa mzuri zaidi na zaidi, na biashara yangu ilikuwa inasitawi zaidi na zaidi. Familia yangu kwa haraka ikawa na mali zaidi, na watu wengi wananiangalia kwa wivu.

Katika majira ya kuchipua ya mwaka wa 1990, kulikuwa na mtu fulani katika kijiji chetu ambaye alizungumza nami kuhusu kumwamini Yesu. Nilisikiliza mahubiri machache kwa kutaka kujua, na nikaona kwamba wakati ndugu huyu wa kiume aliyekuwa akihubiri alikuwa akizungumza, watu wengi walimheshimu. Nilikuwa na wivu usioaminika kuhusu tukio hilo la yeye kuzungukwa na kupendwa na umati. Nilifikiria mwenyewe: Kama ningeweza kuwa mtu kama huyo, sio tu kuwa kila mtu angenipenda mno, lakini ningeweza kupata neema ya Bwana na kupewa thawabu na Yeye. Hilo lingekuwa jambo la ajabu sana! Kutokana na mawazo haya, nilianza kumwamini Bwana Yesu Kristo, na nilijiunga na kanisa la nyumbani. Baada ya hilo, nilifanya kazi kwa bidii kujifunza Biblia, hasa kutafuta maarifa ya Biblia, nikizingatia kukariri vifungu fulani, na kwa haraka sana nilijua sura nyingi maarufu na aya kwa moyo. Niliisoma sura ya 16, aya ya 26 ya Injili ya Mathayo ambapo Bwana Yesu alisema: “Kwani mwanadamu atafaidika na nini, ikiwa ataupata ulimwengu mzima, na apoteze nafsi yake mwenyewe? au mwanadamu atabadilisha nafsi yake na nini?” Kisha nikasoma pia juu ya Bwana Yesu akimwita Petro, na mara moja alizitupa nyavu zake za uvuvi na kumfuata Kristo. Nikafikiria mwenyewe: Kuwa na pesa za kutosha ili kuishi ni vyema; nikichuma zaidi, itakuwa na faida gani nitakapokufa? Nikitaka kupata sifa za Bwana, ni lazima nifuate mfano wa Petro. Kwa hiyo nikaacha biashara yangu, na kuanza kujishughulisha kanisani muda wote. Nilikuwa na shauku sana wakati huo, na kwa kupitia kwa jamaa na marafiki zangu nilikuwa nimehubiri kwa watu 19 kwa muda mfupi, na kisha hiyo idadi ilipanuliwa hadi watu 230 kupitia hao 19. Kisha, nikasoma maneno ya Bwana Yesu: “Siye kila mmoja ambaye aliniambia, Bwana, Bwana, ataingia ufalme wa mbinguni, ila yeye atendaye mapenzi ya Baba yangu ambaye yuko mbinguni(Mathayo 7:21). Nikajihisi mwenye kukinai hata zaidi. Kwa msingi wa kile nilichoelewa kutoka kwa maana halisi ya maneno Yake, niliamini kwamba nilikuwa tayari naifuata njia ya Bwana, kwamba nilikuwa kwa njia ya kuyafuata mapenzi ya Baba wa mbinguni, na katika enzi yenye kufuata wakati ufalme wa Mungu umefanikishwa, ningetawala kama mfalme duniani. Chini ya utawala wa lengo la aina hii, shauku yangu ikawa hata zaidi. Niliweka azimio langu kwamba nilipaswa kufuata maneno ya Yesu kwa uthabiti ya “Mpende jirani yako kama unavyojipenda” na “kuwa na uvumilivu na subira,” na vile vile kuongoza kwa mfano, na kutoogopa kustahimili shida. Wakati mwingine nilipoenda nyumbani kwa ndugu zangu wa kiume na wa kike, ningewasaidia kubeba maji, kuwasha mioto, na kufanya kazi ya shamba. Walipokuwa wagonjwa ningeenda kuwatembelea. Walipokuwa hawana pesa za kutosha ningewasaidia kutoka kwa akiba yangu mwenyewe; ningemsaidia yeyote aliyekuwa anapitia shida. Kwa haraka nilipata sifa ya ndugu zangu wote wa kiume na wa kike na vilevile ya viongozi wa ngazi za juu katika kanisa. Mwaka mmoja baadaye nilipandishwa cheo kuwa kiongozi wa kanisa, kuyaongoza makanisa 30. Nilikuwa nimesimamia waumini takriban 400. Mara nilipokuwa nimepata cheo hiki, nilijihisi mashuhuri. Nilihisi kuwa kazi yangu yote ngumu na jitihada hatimaye zilikuwa zimezaa matunda, lakini wakati huo huo niliunda msimamo wa juu zaidi katika moyo wangu: kufuatilia cheo cha juu zaidi, kupata sifa na upendo wa watu hata wengi zaidi. Kupitia mwaka mwingine wa kazi ngumu, nikawa kiongozi wa ngazi ya juu wa kanisa, nikiongoza wafanyakazi wenzangu katika wilaya tano, nikiongoza makanisa 420. Baada ya hapo nilikuwa na woga zaidi wa kuzembea, kwa hiyo nilizingatia hasa tabia yangu nzuri kijuujuu, na kuanzisha taswira yangu miongoni mwa wafanyakazi wenzangu na ndugu wa kiume na wa kike. Kwa kibali cha wafanyakazi wenzangu na ili ndugu zangu wa kiume na wa kike wangeniheshimu, nilikataa chakula badhirifu katika kanisa, na nikapiga marufuku mawasiliano yote baina ya washiriki wa jinsia tofauti na matendo ya hatari. “Uadilifu wangu na hisia za haki” zilipata uungwaji mkono na kibali kutoka kwa wafanyakazi wenzangu na ndugu wengine wa kiume na wa kike. Asili yangu ya kiburi pia ilituna na kufika kiasi cha kutoweza kudhibitika. Juu ya hayo, nilijua vizuri baadhi ya vifungu vya kawaida zaidi vya Biblia, na wakati nilipokuwa nikikutana na kuhubiri kwa baadhi ya viongozi wa kanisa wa ngazi za chini na wafanyakazi wenzangu, ningeweza kuvitongoa vifungu bila kutazama Biblia yangu kwa msingi wa sura na nambari za mstari tu. Ndugu zangu wa kiume na wa kike kwa kweli walinipenda sana, kwa hiyo siku zote nilikuwa na kauli ya mwisho katika kanisa. Kila mtu alinisikiliza. Siku zote nilifikiri kwamba niliyoyasema yalikuwa sahihi, kwamba nilikuwa na ufahamu wa juu. Kama ulikuwa ni utawala wa kanisa, kuainisha makanisa, au kuwakuza viongozi wa kanisa na wafanyakazi wenzangu, sikujadiliana mambo na wengine. Nilichokisema daima kilikuwa na thamani; kwa kweli nilikuwa na utawala wa mfalme. Wakati huo hasa nilifurahia kusimama kwa mimbari, nikinena kwa umbuji na bila kukoma, na kila mtu alipokuwa akinitazama kwa upendezewaji, hiyo hisia ya kufurahi sana ilikuwa ya kunipendeza mno na ilinifanya kusahau kila kitu. Mimi hasa nilihisi hili wakati niliposoma sura ya 3, mstari wa 34 katika Injili ya Yohana: “Kwani yeye ambaye Mungu amemtuma huyasema maneno ya Mungu: kwa kuwa Mungu hampi Roho kwa kipimo.” Kwa kweli nilifurahia hili, na kwa kujipujua niliamini kwamba nilikuwa nimetumwa na Mungu, kwamba Mungu alikuwa amenipa Roho Mtakatifu, na mapenzi ya Mungu yalionyeshwa kunipitia. Niliamini kwamba kwa sababu ningeweza kufafanua maandiko, ningeweza kuyaelewa “mafumbo” ambayo wengine hawakuweza kuyaelewa, kwamba ningeona vidokezo ambavyo wengine hawangeweza kuviona. Nilijali tu kuhusu kujitosa mwenyewe katika furaha iliyoletwa na cheo changu, na nilikuwa nimesahau kabisa kwamba nilikuwa kiumbe tu, kwamba nilikuwa tu chombo cha neema ya Bwana.

Kanisa lilipoendelea kukua, sifa yangu pia ilikua, na kila mahali nilikoenda nilifuatiliwa na polisi kwa kushiriki katika shughuli zisizoruhusiwa za kidini. Kutokana na mateso haya kutoka kwa serikali, sikuthubutu kurudi nyumbani. Ningeweza kujificha kwa muda, lakini sio milele, na wakati mmoja nilishikwa na polisi wakati niliporudi kuchukua nguo. Nilihukumiwa miaka mitatu ya ufundishwaji tena kwa njia ya kufanya kazi. Katika kipindi hicho cha miaka mitatu nilipitia kila aina ya mateso na maumivu makali ya ukatili. Siku hizo kwa kweli nilihisi zilikuwa kama miaka, na ilihisika kama safu ya ngozi ilikuwa imeambuliwa kutoka kwa kichwa hadi kwa vidole. Lakini baada ya kuachiliwa, bado niliendelea kuhubiri injili kwa ujasiri mkubwa, sawa tu na wakati wowote, na pia nilirudishiwa nafasi yangu ya kazi ya asili. Baada ya miezi sita mingine, niliwekwa kizuizini tena na serikali ya mitaa na kuhukumiwa miaka mitatu ya ufundishwaji tena kwa njia ya kufanya kazi. Baada ya kunitesa kwa kila njia iliyowezekana, waliniweka kwa kituo cha kizuizi kwa siku zingine 70. Baada ya hapo, niliwekwa katika kambi ya kazi ambapo nilikuwa nikibeba matofali. Wakati huo ulikuwa ni mwezi wa saba unaofuata kuandama kwa mwezi na hali ya hewa ilikuwa ya joto ya kumfanya mtu kujisikia vibaya. Halijoto katika tanuru lilikuwa takriban nyuzi 70 sentigredi na nililazimika kutengeneza matofali zaidi ya 10,000 kila siku. Njaa yangu ikichanganywa na mateso yaliyotangulia ya kikatili yalikuwa yameufanya mwili wangu kuwa dhaifu mno. Sikuweza kuvumilia aina hiyo ya kazi katika joto, lakini walinzi wenye dhuluma hawakujali kuhusu yoyote ya hayo. Wakati sikuweza kuzikamilisha kazi zangu, walinifunga pingu mikononi mwangu nyuma yangu, walinilazimisha kupiga magoti, na kuniweka chupa katika makwapa yangu na nyuma ya magoti yangu. Kisha wakanipiga na midukuo ya umeme mpaka pingu zikachimba ndani ya mwili wangu. Ulikuwa uchungu usiofikirika. Nikitolewa mhanga kwa kikatili, nilikuwa nimekamilisha siku saba tu za kazi nilipozirai ndani ya tanuru. Sikuokolewa hadi baada ya saa 52, lakini nilikaribia kuwa punguani. Mbali na kuwa na fahamu na kuweza kuona na kusikia, sikuweza kufanya chochote. Sikuweza kula, kuzungumza, kutembea, au hata kwenda msalani. Baada ya kuharibiwa jinsi hii na Chama cha Kikomunisti, asili yangu ya kiburi ilikuwa imeshindwa kwa kiasi kikubwa. Hiyo nguvu ya uwezo na kiburi niliyokuwa nayo katika kanisa ilikuwa imetoweka tu. Nilikwisha kuwa mwenye huzuni na kukosa rajua; nilikuwa nikiishi katikati ya mateso yasiyo na mipaka na hali ya kutokuwa na msaada. Baadaye watu katika kituo cha kizuizi walikuja na wazo lililopindika na kupata daktari kutengeneza taarifa za udanganyifu zikisema kwamba nilikuwa na “maradhi ya kinasaba.” Walimwita mke wangu na wakamwambia anichukue na kunipeleka nyumbani. Ili kuitibu hali yangu, kila kitu nyumbani mwetu kiliuzwa, na wakati jamaa zangu walipokuja kuniona walipiga kijembe, wakawa fidhuli na kufanya mzaha. Nikikabiliwa na hali hii, nilivunjika moyo na nilihisi kwamba dunia ilikuwa yenye uovu sana, kwamba hapakuwa na upendo wa familia au mapenzi kati ya watu, kwamba kulikuwa tu na mateso ya kikatili na shutuma…. Nikikabiliwa na mateso ya ugonjwa huu wa kuumiza, hakukuwa na matumaini katika maisha yangu na sikujua jinsi ningeweza kuendelea.

Nilivyokuwa tu nikizama katika kukata tamaa, Mwenyezi Mungu akaninyoshea mkono wa wokovu. Nilipokuwa nimerejea nyumbani kwa zaidi ya mwezi mmoja, ndugu wawili wa kiume walikuja kunihubiria injili ya Mungu ya siku za mwisho na kwamba Alikuwa akishughulikia hatua mpya ya kazi, kupata mwili Kwake kwa mara ya pili ili kuwaokoa wanadamu. Wakati huo sikuamini yote kabisa, lakini kwa sababu sikuweza kuzungumza, nikatafuta vifungu fulani vya Biblia kuwaonyesha. Hivi ndivyo nilivyowakanusha. Walinijibu kwa upole: “Ndugu, wakati unamwamini Mungu unapaswa kuwa na moyo wa utafutaji wa unyenyekevu. Kazi ya Mungu ni mpya daima; daima inasonga mbele, na hekima Yake haiwezi kueleweka na wanadamu, kwa hiyo hatuwezi kushughulika mno katika siku za nyuma. Ikiwa unashikilia kazi ya Mungu katika Enzi ya Neema utaweza kuingia katika Enzi ya Ufalme? Licha ya, yale Bwana Yesu aliyoyasema katika Biblia yote yana maana yake na muktadha.” Kisha, walinifungulia maneno ya Mwenyezi Mungu ili niyasome, na baada ya hapo wakapata unabii mwingi katika Biblia ili nisome juu ya kazi ya Mungu katika siku za mwisho. Kwa njia ya maneno ya Mungu na ushirika na ndugu zangu wa kiume, nilikuja kuelewa maana ya jina la Mungu, ukweli wa ndani katika hatua Zake tatu za kazi, kusudi Lake katika usimamizi Wake wa wanadamu, siri za kupata Kwake mwili, ukweli wa ndani katika Biblia, na zaidi. Hivi ni vitu ambavyo sikuwahi kusikia kuvihusu katika maisha yangu, na pia vilikuwa mafumbo na ukweli ambavyo sikuwa msikivu kwavyo wakati nilipokuwa ninajitahidi sana kujifunza Biblia kwa miaka yote hiyo. Niliisikiliza kwa furaha; niliridhishwa kabisa. Baada ya hayo, ndugu zangu walinipa kitabu cha maneno ya Mungu, wakisema: “Baada wewe kuwa bora wa afya, unaweza kuhubiri injili kwa wafanyakazi wenzako na ndugu wa kiume na wa kike.” Kwa furaha sana nilikubali kitabu cha maneno ya Mungu. Wakati huo, niliweza tu kulala kitandani siku nzima na kusoma maneno ya Mungu. Nilihisi hamu na furaha kama ya samaki akirudi kwa maji. Nilifurahia na nikaidhinisha. Baada ya muda mfupi, afya yangu ilikuwa ikiboreka hatua kwa hatua. Ningeweza kutoka nje ya kitanda na kutembea huku na kule kiasi, na niliweza kujitegemea zaidi katika maisha yangu. Baada ya hapo nilikuwa nikiishi maisha ya kanisa nyumbani mwangu, na nilikuwa na mikutano mara mbili kila juma.

Sikuwa nimefikiria kuwa katika maisha yangu ya baadaye ya kanisa tabia yangu ya kiburi ingefunuliwa kabisa. Kupitia Maneno Yake na watu mbalimbali, masuala na mambo, kupitia hukumu Yake na kuadibu, ushughulikiaji Wake kwangu na upogoaji wa vipengele fulani vyangu, Mungu alisababisha moyo wangu wa kiburi, mkaidi kushushwa kidogo kidogo. Wakati mmoja kanisa lilimpangia msichana mdogo wa miaka 17 au 18 kuja kukutana nami. Alikuwa binti ya ndugu fulani wa kiume kutoka dhehebu langu la awali, na awali nilipokuwa kiongozi wa kanisa nilikuwa nimekwenda nyumbani kwake mara kwa mara. Nikafikiria mwenyewe: Ni nini kibaya na mipango ya kiongozi wa kanisa? Kufanya mtoto aje kuniongoza—wananiangalia kwa dharau? Chini ya kanuni ya asili yangu ya kiburi, nikasema kwa dharau: “Nimemwamini Mungu kwa miaka mingi zaidi ya umri wako. Nilipokuwa nikienda nyumbani kwenu ulikuwa na miaka michache tu. Ningecheza nawe wakati huo, lakini sasa unakuja kunielekeza….” Dada yangu mdogo alikasirika kutokana na kile nilichokisema, na hakuthubutu kuja tena. Wiki iliyofuata dada tofauti mdogo alikuja. Alikuwa mdogo sana pia na alitoka kwa kijiji jirani. Sikusema chochote, lakini niliwaza: Ikiwa ni idadi ya miaka au sifa za kumwamini Mungu, elimu ya Biblia, au uzoefu katika uongozi wa kanisa, mimi ni bora zaidi kukuliko katika kila kipengele! Kutokana na umri wako, naweza kuona kwamba umekuwa muumini kwa miaka mitatu au minne na si zaidi. Nimeamini kwa miaka 21. Je, unawezaje kuwa na sifa zinazostahili kunielekeza? … Lakini ni nani angeweza kujua kwamba huyu dada mdogo alikuwa akieleza kwa ufasaha mno—alizungumza kwa uwazi na kwa ukali. Wakati tukikutana, mara moja alifungua matamshi ya Mungu na kusoma kwa sauti: “watu wengine hususan humpenda Paulo sana. Wanapenda kwenda na kuhutubu na kufanya kazi, wanapenda kukutana pamoja na kuzungumza; wanapenda watu kuwasikiza, kuwaabudu, na kuwazingira. Wanapenda kuwa na hadhi katika mawazo ya wengine, na wanafurahia wakati wengine wanathamini mifano yao. … Kama kweli wanatenda kwa njia hii, basi hilo linatosha kuonyesha kuwa wao ni fidhuli na wenye majivuno. Hawamwabudu Mungu hata kidogo; wanatafuta hadhi ya juu zaidi, na wangependa kuwa na mamlaka juu ya wengine, kuwamiliki, na kuwa na hadhi akilini mwao. Huu ni mfano bora wa Shetani. Vipengele vya asili yao vinavyojitokeza ni ufidhuli na majivuno, kutokuwa radhi kumwabudu Mungu, na tamaa ya kuabudiwa na wengine. Tabia kama hizi zinaweza kupa mtazamo dhahiri sana juu ya asili yao(“Jinsi ya Kujua Asili ya Mwanadamu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Maneno ya Mungu yaliuchoma moyo wangu kama upanga wa makali kuwili, yakinijeruhi moja kwa moja. Ulikuwa ni ufunuo mkali wa malengo yangu yenye kustahili dharau na utendaji mbaya katika vitendo vyangu vya kumwamini Mungu, na pia kiini cha kweli cha asili yangu. Nilikuwa nimejaa aibu na sikutaka chochote zaidi ya kutoweka tu. Juu ya kile kilichofichuliwa katika maneno ya Mungu, nilipofikiria juu ya kile nilichofichua, ni hapo tu nilipotambua kwamba asili yangu ilikuwa ya kiburi sana na kwamba kimsingi nilikuwa nikiwa na uhasama kwa Mungu. Katika siku za nyuma, ili watu wanistahi na kunipenda, kuwa mtu aliye na mamlaka juu ya wengine, kuwa katika daraja la juu, nilifanya bidii kwa kusoma Biblia na kutia kila kitu katika kujiandaa na elimu ya Biblia. Kwa sababu ya hili, nilipata hadhi na cheo ambavyo nilikuwa nimeviota tu pamoja na uungwaji mkono na kila mtu. Nilipata raha kutokana na kupendwa na wengine, na nilihubiri ili kuridhisha majivuno yangu mwenyewe. Kupitia kwa ukiritimba wangu wa mamlaka, nilijifichua na kujionyesha. Nilikuwa naridhika daima kufaidika na hisia ya kuwa na furaha sana nilipokuwa nikisimama kwa mimbari, na hata kwa kujipujua niliitumia aya kutoka kwa Biblia kujishuhudia na kujiinua mwenyewe. Niliamini kwamba nilikuwa nimetumwa na Mungu. Nilikuwa na kiburi dhalimu. Siku hiyo, nilimwangalia huyo dada mdogo kwa dharau, nikitumia miaka yangu mingi ya kuhubiri kwa manufaa yangu. Niliamini kwamba kwa sababu nilikuwa nimemwamini Mungu kwa miaka mingi zaidi na nilikuwa na elimu kubwa zaidi ya Biblia, uzoefu mkubwa zaidi katika uongozi wa kanisa, nilikuwa bora zaidi kuliko kila mtu. Sikumchukua yeyote kuwa muhimu, na niliwakadiria kwa upungufu na kuwadharau hao dada wawili. Nilipozungumza niliwaudhi wengine, na kwa kiburi nilipoteza hisi yangu na ubinadamu wa kawaida. Ni hapo tu nilipotambua kwamba ufuatiliaji wangu ulikuwa katika upinzani kwa Mungu na kumpinga Yeye. Nilikuwa nikishindana na Mungu kwa hadhi. Kiini cha asili yangu kilikuwa ni mfano bora kabisa wa Shetani. Nikikabiliana na maneno ya Mungu, singeweza kutoridhishwa. Nilimwomba Mungu, nikisema, “Ee Mungu, nina kiburi sana. Nilipokuwa na hadhi nilikuwa mwenye majivuno sana, na wakati nilipokuwa sina hadhi bado sikumsikiliza yeyote. Nilitumia sifa zangu za zamani na mamlaka kuwatawala watu, kuwaangalia kwa dharau. Mimi nina utovu wa haya sana! Leo nilipokea wokovu Wako. Niko radhi kukubali ufichuzi na hukumu katika maneno Yako.”

Baada ya hapo, huyo dada tena alifungua kifungu cha maneno ya Mungu ili nisome. Yalikuwa: “… Hisia ya mwanadamu imepoteza kazi yake ya awali, na kwamba dhamiri ya mwanadamu, pia, imepoteza kazi yake ya awali. Mwanadamu Ninayemtazamia ni mnyama katika mavazi ya binadamu, yeye ni nyoka mwenye sumu, haijalishi jinsi anavyojaribu kuonekana mwenye kuhurumiwa machoni Pangu, Sitawahi kamwe kuwa na huruma kwake, kwa kuwa mwanadamu hana ufahamu wa kutofautisha kati ya nyeusi na nyeupe, tofauti kati ya ukweli na yasiyo ya kweli. Hisia ya mwanadamu ni usiohisi chochote, ilhali bado anataka apate baraka; ubinadamu wake si wa kuheshimika lakini bado anataka kumiliki ukuu wa mfalme. Ataweza kuwa mfalme wa nani, na hisia kama hiyo? Jinsi gani yeye na ubinadamu kama huo ataweza kukaa kwenye kiti cha enzi? Mwanadamu kwa kweli hana aibu! Yeye ni mdhalili wa kujivuna tu! Kwa wale kati yenu mnaotaka kupokea baraka, Ninawashauri kwanza mtafute kioo na kuangalia picha zenu mbaya—je, una kile kinachohitajika kuwa mfalme? Je, una uso wa mwanadamu ambaye anaweza kupata baraka? Hakujawa mabadiliko hata madogo katika tabia yako na wewe hujaweka ukweli wowote katika vitendo, ilhali bado unatamani kuona siku ifuatayo ikiwa ya ajabu. Unajihadaa mwenyewe!(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu). Baada ya kuyasikia maneno ya Mungu, sikuweza kuyazuia machozi kutiririka usoni mwangu. Nilihisi kwamba kila sentensi ya maneno ya Mungu ilinyakua moyo wangu, kwa ukali nilihisi hukumu Yake, na nilihisi aibu hasa. Tukio baada ya tukio la ukimbizaji wangu wa aibu wa kutawala kama mfalme katika kanisa langu la zamani lilionekana mbele yangu: Miongoni mwa ndugu zangu wa kiume na wa kike nilikuwa mwenye majivuno sana, niliwaamrishaamrisha watu, nilitaka kudhibiti kila kitu, na sikukosa tu kuwaleta ndugu zangu wa kiume na wa kike mbele ya Mungu na kuwasaidia kumjua Yeye, lakini niliwafanya wanitendee kana kwamba nilikuwa juu sana, mkuu sana …. Jinsi nilivyozidi kufikiri juu ya hilo, ndivyo nilivyozidi kuhisi kwamba matendo yangu yalimchukiza Mungu, kwamba nilikuwa wa kuchosha, nisiyestahili, na kwamba niliwasikitisha ndugu zangu wa kiume na wa kike. Wakati huo nilihisi aibu kupita kadiri. Niliona kuwa gharama niliyokuwa nimelipa kwa ajili ya tamaa zangu za kutaka makuu haikuwa na thamani yoyote. Ukimbizaji wangu mbaya wa hadhi na kupewa heshima na wengine ulikuwa wa upuuzi. Nilikuwa nakurupuka pote mchana na usiku; nilistahimili shida, nilifanya kazi kwa bidii, na nikaenda jela. Niliadhibiwa na kuteswa, na nilikuwa karibu kufa. Haikunifanya kuwa na ufahamu wa Mungu; kinyume chake, asili yangu ya kiburi iliongezeka zaidi na zaidi, kumweka Mungu karibu yangu kulipungua zaidi na zaidi kiasi kwamba nilifikiri kwa kujidanganya kwamba ningetawala kama mfalme wakati Ufalme wa Mungu umefanikishwa. Wakati huo huo, nilitambua pia kwamba wakati nilipokuwa nimeteswa na Chama cha Kikomunisti katika kanisa langu la awali, Mungu alikuwa akitumia hilo ili kunifanya niweze vyema zaidi kuikubali kazi Yake katika siku za mwisho. Vinginevyo, kulingana na fahari kuu na hadhi yangu katika kanisa langu la awali, kwa msingi wa ukweli kwamba sikumweka Mungu karibu nami na tabia yangu ya kujivuna, singeweza kabisa kuiachilia hali yangu kwa urahisi na kumkubali Mwenyezi Mungu. Bila shaka ningekuwa mtumishi mwovu aliyezuia kurudi kwa wengine kwa Mungu, aliyempinga Mungu na hatimaye angepata adhabu Yake! Sikuweza kujizuia kumshukuru Mungu kwa dhati kwa ajili ya wokovu Wake, na msamaha Wake mkubwa kwangu. Kwa hiyo nikawa bila makeke zaidi kwa sababu ya kile kilichofichuliwa kupitia kwa maneno ya Mungu, na sikuthubutu tena kuwa mfidhuli na muhali na ndugu zangu wa kiume na wa kike.

Chini ya utunzaji na ulinzi wa Mungu ugonjwa wangu ukapungua hatua kwa hatua. Ingawa sikuweza kuzungumza vizuri, ningeweza kuendesha baiskeli na kufanya kazi kidogo katika mambo ya kawaida. Hata hivyo, kwa sababu asili yangu ya kiburi ilikuwa madhubuti mno, Mungu mara nyingine tena alinipangia watu wapya na mambo ya kunihukumu na kunibadilisha. Siku moja, kiongozi wa kanisa alinipangia wajibu wa kukaribisha. Baada ya kusikia hili nilihisi kutotaka sana kulifanya hilo. Niliamini kuwa kutenda kazi ya kukaribisha ilikuwa ni kutumia vibaya uwezo wangu, lakini sikuweza kukataa, kwa hiyo nilikubali shingo upande. Nilipokuwa nikikaribisha, baadhi ya ndugu wa kiume na wa kike walikuwa wakikutana nyumbani kwangu na kunifanya kulinda mlango ili kulinda mazingira yetu. Mara nyingine tena mawazo yangu ya ndani yalitokea: kutenda tu kama mwenyeji, kulinda mlango—nitapata nini kutoka hili? Nilifikiria wakati wa nyuma. Niliposimama nyuma ya mimbari nilikuwa na majivuno sana, lakini katika kazi yangu leo sikuwa na ujasiri wowote au hadhi yoyote. Cheo changu kilikuwa cha chini sana! Hivyo baada ya muda fulani, upinzani wangu wa ndani ukawa mkubwa zaidi na zaidi, nilihisi kukosewa zaidi na zaidi, na sikuwa radhi tena kutimiza wajibu huo. Kiongozi wa kanisa alipopitia wakati fulani baadaye, sikuweza kulizuia tena. Nikasema: “Unahitaji kunipa wajibu mwingine wa kutekeleza. Ninyi nyote mnahubiri injili na kulitunza kanisa, lakini mimi niko nyumbani nikitenda kama mwenyeji na kulinda mlango—nitapata nini wakati wa baadaye?” Huyo dada akatabasamu na kusema: “Umekosea. Mbele ya Mungu, hakuna wajibu mkubwa au mdogo, hakuna hadhi kubwa au ndogo. Bila kujali ni wajibu gani tunaotekeleza, kila mmoja wetu ana kazi. Kanisa ni kitengo kimoja chenye kazi tofauti, lakini ni mwili mmoja. Hebu tuangalie kifungu kimoja cha maneno ya Mungu.” Kisha akanisomea kifungu hiki: “Katika mkondo wa sasa, kila mtu anayempenda Mungu kwa kweli ana fursa ya kukamilishwa na Yeye. Bila kujali kama yeye ni kijana au mzee, mradi tu anatazamia kwa hamu kumtii Mungu na kumheshimu Yeye, wataweza kukamilishwa na Yeye. Mungu huwakamilisha watu kulingana na kazi zao tofauti. Mradi tu umefanya yote kwa nguvu yako na kuitii kazi ya Mungu utakuwa na uwezo wa kukamilishwa na Yeye. Kwa sasa hakuna hata mmoja wenu aliye mkamilifu. Wakati mwingine mnaweza kutekeleza aina moja ya kazi na wakati mwingine mnaweza kutekeleza mbili; mradi tu mnatoa nguvu zenu zote kujitumia kwa ajili ya Mungu, hatimaye mtafanywa wakamilifu na Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Kila Mmoja Kutekeleza Wajibu Wake). Baada ya kusikiliza maneno haya ya Mungu na ushirika wa huyu dada, moyo wangu ukatulia na kuchangamka. Niliwaza: Huwa kwamba Mungu huwakamilisha watu kulingana na kazi tofauti ya kila mmoja. Yeye haangalii kama watu wana hadhi au la ama ni wajibu upi wao hutekeleza, kile ambacho Mungu hukamilisha ni mioyo ya watu na utii wao. Kile Anachoangalia ni kama wao huishia kupata mabadiliko katika tabia. Bila kujali wao hutekeleza wajibu upi, almradi wao huufanya kwa moyo wao wote na ni wacha Mungu kabisa, na wakitupilia mbali tabia yao potovu wao wenyewe wanapotekeleza wajibu wao, wanaweza kukamilishwa na Mungu. Ingawa watu hufanya kazi mbalimbali katika kanisa, lengo daima ni kumridhisha Mungu. Wote wanatimiza wajibu wa uumbaji. Kama watu wanaweza kumtazama Mungu na kutimiza wajibu wao bila nia za kibinafsi au uchafu, hata kama wengine huuangalia kwa dharau wajibu wanaoutimiza na kufikiri si wa thamani sana, machoni mwa Mungu unatunzwa na kuthaminiwa. Watu wakitekeleza wajibu wao ili kuridhisha nia zao wenyewe na tamaa zao, bila kujali ukubwa wa kazi yao na ni wajibu gani wao hutimiza, hautampendeza Mungu. Baada ya hapo, niliona maneno haya kutoka kwa Mungu: “Kama kiumbe, mwanadamu anapaswa kutimiza wajibu wake, afanye anachopaswa kufanya, na afanye anachoweza kufanya, bila kujali kama atabarikiwa au kulaaniwa. Hili ndilo sharti la msingi kwa mwanadamu, kama anayemtafuta Mungu. Usifanye wajibu wako ili ubarikiwe tu, na usikatae kutenda kwa kuogopa kupata laana(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu Mwenye Mwili na Wajibu wa Mwanadamu). Nilielewa kutoka kwa maneno haya ya Mungu kwamba kama kiumbe, ibada ya Mungu ni sawa na sahihi. Sistahili kuwa na chaguo langu mwenyewe, na sifai kabisa kujadili masharti ama kufanya shughuli na Mungu. Kama imani yangu kwa Mungu na utimizaji wa wajibu wangu ni ili kupata baraka ama taji, aina hii ya imani haiko katika dhamiri na maana nzuri. Imetoka kwa mtazamo usiofaa. Nilisita kufanya “kazi ndogo” na kutimiza “wajibu mdogo”—si huko bado ni kuwa chini ya utawala wa matarajio ya kiburi kufuatilia baraka na kupewa heshima na wengine? Katika mawazo yangu, niliamini kwamba nikiwa na hadhi na mamlaka ningeweza kuongoza, na kwamba jinsi nilivyofanya kazi zaidi ndivyo Mungu angezidi kufurahi, na ndivyo ningepokea sifa ya Mungu na kutuzwa na Yeye. Hivyo bado singetaka kuachana na hadhi, na daima nilikuwa nikitafuta kufanya kazi kubwa na kutekeleza majukumu makubwa ili mwishowe ningepokea taji kubwa. Vilevile nilielewa visivyo mapenzi ya Mungu na sikuridhishwa na wajibu uliopangwa na kanisa. Nililalamikia juu ya jambo hilo na hata niliamini kuwa kutimiza wajibu wa mwenyeji kulikuwa ni kutumia vibaya ujuzi wangu, kwamba ilikuwa ni njia ya kuniangalia kwa dharau. Nilikuwa na kiburi sana na mjinga! Chini ya hukumu ya maneno ya Mungu, mimi kwa mara nyingine tena niliona aibu. Na pia kwa sababu ya kupata nuru kutoka kwa maneno ya Mungu, nilielewa mapenzi Yake. Nilijua ni mtu wa aina gani Mungu humpenda, na ni mtu wa aina gani Yeye hukamilisha, na ni mtu wa aina gani humchukiza Yeye. Nilipata moyo wa utii kwa Mungu. Baada ya hapo niliweka mapenzi yangu mbele ya Mungu na nilikuwa radhi kuwa mdogo kabisa, mtu asiyejitanguliza kabisa katika kanisa, ili kuukamilisha wajibu wangu kama mwenyeji, kuyalinda mazingira yetu, kuwaruhusu ndugu zangu wa kiume na wa kike kukutana katika nyumba yangu kwa amani bila kusumbuliwa. Ningeufariji moyo wa Mungu kwa njia hii.

Kwa njia ya uzoefu huu, niligundua jinsi maneno ya Mungu yalivyo makubwa, kwamba Yeye amenyesha ukweli na mapenzi Yake yote ili kuwaokoa wanadamu. Tunahitaji tu kusoma kwa bidii maneno Yake ili kuufahamu ukweli katika mambo yote, kuyaelewa mapenzi Yake, kutatua mawazo yetu wenyewe na imani. Kutoka hapo na kuendelea, nilikuza kiu zaidi ya maneno Yake, na nikaanza kuamka saa kumi au saa kumi na moja kila asubuhi kusoma maneno Yake. Baada ya muda fulani, niliweza kukumbuka sehemu moja ya maneno Yake, nikapata ufahamu wa mapenzi Yake, na kweli niliyafurahia moyoni mwangu. Baadaye, kulikuwa na ndugu wa kiume aliyekuwa na wajibu wa kazi ya injili ambaye alikaa nyumbani yangu mara nyingi. Mara nyingi alipokuwa akihubiri injili na kukabiliwa na matatizo, aliniulizwa kutafuta maneno ya Mungu ili kuyatatua. Aliona kwamba mimi ningeweza kuyapata haraka sana, na mara tu alipojipata katika matatizo angeniuliza kumsaidia kupata baadhi ya maneno kutoka kwa Mungu. Alinipenda kweli. Bila kukusudia, asili yangu ya kiburi ilianza kujifaragua mara nyingine tena. Nilifikiria mwenyewe: licha ya ukweli kwamba una wajibu wa kuhubiri injili, bado inabidi nikusaidie kutatua masuala. Hujasoma neno la Mungu kama vile nimesoma, na hulielewi jinsi ninavyolielewa. Mimi tayari nimepata ukweli. Kama ningekuwa na madaraka ya kuhubiri injili, waziwazi ningekuwa bora katika hilo kuliko ulivyo. Hivyo katika moyo wangu nilianza kumwangalia kwa dharau huyu ndugu yangu, na baada ya muda hata nilianza kutomthamini. Baadaye, kiongozi wa kanisa alikuja nyumbani kwangu na kuniuliza: “Umekuwa ukiendeleaje hivi karibuni?” Kama nimejaa imani, nilimjibu: “Nimekuwa mwema. Mimi husoma maneno ya Mungu na kuomba kila siku. Yule ndugu ameona kwamba ninaelewa neno la Mungu kiasi, kwa hiyo yeye daima hutaka nimsaidie kutafuta maneno kutoka kwa Mungu ya kutatua masuala….” Kiongozi wa kanisa alisikia kiburi katika kile nilichokisema, na akachukua kitabu cha maneno ya Mungu na kusema: “Hebu tusome vifungu vichache vya maneno Yake” Mungu anasema: “Kwa sababu hadhi yao ilivyo kubwa zaidi, ndivyo tamaa yao ya makuu ilivyo kubwa zaidi; kadiri wanavyofahamu mafundisho zaidi, ndivyo tabia zao zinavyokuwa zenye majivuno zaidi. Kama, katika kumwamini Mungu kwenu, humwufuati ukweli, na badala yake mnaifuata hadhi, basi ninyi mko hatarini(“Watu Wanafanya Madai Mengi Sana kwa Mungu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). “Bila kujali ni kipengele kipi cha uhalisi wa ukweli umesikia, ukikitumia kama kigezo, utayatekeleza haya maneno katika maisha yako mwenyewe, na kuyashirikisha katika matendo yako mwenyewe, kwa hakika utapata kitu, na kwa hakika utabadilika. Ukiingiza maneno haya ndani ya tumbo lako, na kuyakariri katika ubongo wako, basi hutawahi badilika. … lazima uweke msingi mzuri. Kama, kule mwanzoni kabisa, uliweka msingi wa barua na mafundisho, basi utakuwa katika shida. Ni kama wakati watu hujenga nyumba ufuoni: Nyumba hiyo itakuwa katika hatari ya kuanguka bila kujali umeijenga kwa urefu gani, na haitadumu sana(“Vitendo vya Msingi Kabisa vya Kuwa Mtu Mwaminifu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Baada ya kusikia maneno haya ya Mungu, niliona aibu kabisa. Nikagundua kuwa asili yangu mwenyewe ya kiburi ilikuwa inaibuka tena. Katika imani yangu kwa Yesu katika siku za nyuma, nilikuwa nimezingatia kupata elimu ya kina na kuelewa nadharia katika Biblia, na nilitumia hilo kama msingi wa kuwa mtu mwenye majivuno sana, kwa kuwa na kiburi zaidi na zaidi. Sasa nilikuwa na bahati niliweza kusoma ukweli mwingi katika maneno ya Mungu, lakini nilikuwa nimeirudia njia yangu ya zamani na nilikuwa nikitegemea akili yangu. Nilikuwa nimekariri sentensi kadhaa kutoka kwa maneno Yake na niliamini kuwa nilikuwa nimepata ukweli; mara nyingine tena nikawa mwenye kiburi na singemsikiliza mtu yeyote. Nilichuana na wengine kwa ajili ya hadhi na nilishindana nao. Kwa kweli ilikuwa ni aibu sana! Kuelewa nadharia katika maneno inaweza tu kuwafanya watu kuwa na kiburi, lakini ni wale tu wanaojua ukweli wa maneno ya Mungu watakaoweza kubadilisha tabia zao na kuishi kama binadamu. Ndugu huyo wa kiume alikuwa amemwamini Mungu kwa muda mrefu kuniliko, na alelewa mengi kuniliko, lakini aliweza kuomba msaada wangu kwa unyenyekevu. Hii kwa kweli ilikuwa ni nguvu yake, na lilikuwa ni tunda lililotokana na uzoefu wake wa kazi na neno la Mungu. Si kwamba tu sikujifunza kutoka kwake na kuzingatia kuweka neno la Mungu katika matendo maishani mwangu, na kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu sahihi, lakini nilimwangalia kwa dharau na kutomthamini. Kwa kweli nilikuwa na kiburi, kipofu, na mjinga! Moyo wangu wakati huo ulikuwa na maumivu sana. Nilihisi kwamba asili hii yangu ya kiburi ilikuwa ya aibu na mbaya kwa kweli. Ilikuwa ya kuchukiza mno! Na aina hii ya kiburi kwa kiasi kilichokosa mantiki yote huichukiza tabia ya Mungu kwa urahisi sana. Bila kujibadilisha, bila kufuatilia ukweli kwa ukweli ningekuwa tu nimejiangamiza mwenyewe. Nilipotambua yote haya, nilihisi kwa kweli kuwa hukumu na kuadibu katika maneno ya Mungu yalikuwa kweli upendo Wake na wokovu kwangu. Hili lilinisababisha kuhisi chuki kwa asili yangu ya kiburi, na nilielewa kwamba katika imani yangu katika Mungu, napaswa kutembea njia sahihi ya kufuatilia ukweli na kufuatilia mabadiliko katika tabia.

Hilo lilipokuwa limepita, nilianza kujiangalia ndani kwa ajili ya mizizi ya kiburi changu na ukosefu wa mantiki, kwa kile kilichokuwa kikiyaongoza mawazo yangu, kile kilichonifanya mara kwa mara kufichua asili yangu ya kishetani ya kiburi. Siku moja, niliona maneno haya kutoka kwa Mungu: “Kila kitu ambacho Shetani hufanya ni kwa ajili yake. Anataka kumpita Mungu, kujiondoa kwa Mungu na kushika mamlaka mwenyewe, na kumiliki vitu vyote ambavyo Mungu ameumba. Baada ya mwanadamu kupotoshwa na Shetani, alikuwa mwenye kiburi na majivuno, mchoyo na mwovu, na alijishughulisha na faida zake pekee. Kwa hivyo, asili ya mwanadamu ni asili ya Shetani. … Asili ya kishetani ya mwanadamu ina kiwango kikubwa cha falsafa. Wakati mwingine wewe mwenyewe huna hata habari ya hilo na hulielewi, ilhali kila muda wa maisha yako unategemea hilo. Isitoshe, unafikiri kuwa falsafa hii ni sahihi sana, yenye mantiki na isiyo na kosa. Falsafa ya Shetani imekuwa ukweli wa watu, na wanaishi kulingana na falsafa ya Shetani kabisa, bila kumpinga hata kidogo. Kwa hivyo, kila mara wanaonyesha asili yao ya kishetani. mwanadamu daima hufichua asili ya Shetani, na katika vipengele vyote, wanaishi daima kulingana na falsafa ya ya kishetani. Asili ya Shetani ni maisha ya mwanadamu(“Jinsi ya Kuitembea Njia ya Petro” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Nikitafakari maneno haya ya Mungu, moyo wangu ulichangamka zaidi na zaidi. Niliwaza: Inatukia kwamba baada ya wanadamu kupotoshwa na Shetani, asili yetu pia ilikuwa ya kiburi vilevile, kaidi vilevile, na bila ya ibada ya Mungu kama Shetani mwenyewe, na sisi hufuatilia wengine kutuheshimu na kutuabudu kana kwamba sisi ni Mungu. Kupitia ushawishi wa kijamii na maneno maarufu kutoka kwa watu mashuhuri, Shetani ameweka kufikiri kwake, falsafa yake ya maisha na sheria zake za kudumu ndani ya moyo wa binadamu, kikiwa kitu ambacho watu hutegemea katika maisha yao; hivi vinayaongoza mawazo ya wanadamu, vikitawala matendo yao, na vikiwasababisha wawe na kiburi na muhali zaidi na zaidi. Nilitafakari juu ya ukweli kwamba tangu nilipokuwa mtoto nilionewa na kubaguliwa na nilianza kuwahusudu wale waliokuwa na mamlaka na hadhi. Aidha, sheria za kishetani za kudumu za “Watu hupambana kwenda juu, lakini maji hutiririka kwenda chini,” “Mimi ni bwana wangu mwenyewe kote mbinguni na duniani,” “kuinuka juu ya wengine,” na “Mtu anafaa kuwaletea mababu zake sifa njema” vilikuwa vimepandwa kwa udhabiti katika moyo wangu kuanzia umri mdogo, vikiyatawala maisha yangu. Kama ilikuwa nje katika ulimwengu au katika kanisa, nilikuwa nafanya kila linalowezekana kufuatilia hadhi na sifa; nilikuwa natafuta kuwa na kimo cha juu kuliko wengine, kuwa mwenye madaraka juu ya wa wengine. Nikiwa nimetiwa sumu na mambo haya, nikawa mwenye kiburi zaidi na zaidi kiasi kwamba nilikuwa na majivuno na daima neno langu lilikuwa ni kauli ya mwisho. Nilikuwa na kiburi kiasi kwamba niliamini kwamba nilikuwa nimetumwa na Mungu, na nilifikiri kwamba ningetawala kama mfalme pamoja na Mungu. Kwa sababu ya sumu hizi, nilijiona mwenye hadhi ya juu sana; nilijiona kama mkubwa kwa kweli. Daima ningeweka sifa zangu za kuwa muumini wa muda mrefu nilipokabiliwa na ndugu zangu wa kiume na wa kike na kulinganisha nguvu zangu na udhaifu wa watu wengine. Ningewadunisha na kuwaangalia kwa dharau. Sikuweza kuwatendea kwa haki, na sikuwa na ufahamu wa asili na ukweli wa upotovu wa Shetani kwangu. Sumu ya Shetani ilikuwa imenifanya kuwa na kiburi kiasi kwamba nilikuwa nimepoteza mantiki yangu ya binadamu. Kama Shetani tu, nilitaka kutwaa mamlaka katika kila kitu. Nilitaka cheo kilichoinuliwa ili kuwatawala wanadamu. Hizi sumu za Shetani zilinidhuru vibaya mno, kwa kina sana, hivi kwamba kile nilichokuwa nikiishi kwa kudhihirisha kilikuwa ni mfano wa shetani, ibilisi! Nilimwomba Mungu, nikisema, “Ee Mungu, siko radhi tena kuishi kwa msingi wa mambo haya. Nimeteseka mno kwa sababu ya mambo hayo, nimekuwa nikiishi katika ubaya usiostahimilika na nimekuchukiza Wewe. Ee Mungu, niko radhi kufanya kila linalowezekana kufuatilia ukweli, kuwa mtu ambaye kwa hakika ana dhamira na mantiki, kuishi kwa kudhihirisha mwenendo wa mtu wa kweli, kuufariji moyo Wako. Ee Mungu, nakuomba Usichukue hukumu na kuadibu Kwako mbali na mimi, naomba kazi yako initakase. Mradi inawezekana kunibadilisha, kunifanya nikue na kuwa Wako hivi karibuni, niko radhi kukubali hata hukumu kali zaidi na kuadibu kutoka Kwako na kuadibiwa kwa nidhamu Yako.”

Siku moja, nilisoma maneno ya Mungu yakisema: “Mungu hana mambo ya ukamilifu wa kibinafsi na umuhimu wa kibinafsi, au yale wa kujiona na kiburi; Hana mambo yasiyo aminifu. Yote yanayomuasi Mungu yanatoka kwa Shetani; Shetani ni chanzo cha ubaya na uovu wote. Sababu kwamba mwanadamu anayo sifa sawa na zile za Shetani ni kwa sababu mwanadamu amelaghaiwa na kushughulikiwa na Shetani. Kristo hajawahi kupotoshwa na Shetani, hivyo Anazo tu tabia za Mungu na hakuna hata moja ya Shetani(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni). Moyo wangu ulisisimuliwa mara nyingine tena. Mungu ni wa fahari sana na mkuu, lakini mnyenyekevu sana na aliyejificha. Kamwe huwa Hajishaui, na Yeye kamwe hawi na kiburi katika kazi Yake miongoni mwa wanadamu. Yeye daima hufanya kazi yote inayohitajika na mwanadamu kimya kimya, Akivumilia fedheha kubwa na maumivu bila kuiona kama ni shida. Badala yake, Yeye huteseka na huzunishwa kutokana na binadamu kuishi chini ya miliki ya shetani na kufungwa kwa falsafa zake. Yeye hutumia juhudi zote iwezekanavyo ili tu kuwaokoa wanadamu kutoka kwa ushawishi wa Shetani ili watu waweze kupata uzima, waishi kwa uhuru na bila vizuizi, na wanaweza kuzikubali baraka Zake. Mungu ni mkuu sana, mtakatifu sana, na katika maisha Yake hakuna vipengele vya kujidai na majisifu, Kwa sababu Kristo Mwenyewe ni ukweli, njia, na uzima. Yeye ni mkuu na vilevile mnyenyekevu na mzuri. Kuona kile Kristo alicho nacho na alicho, nilihisi hata zaidi kwamba nilikuwa na kiburi na mtovu wa haya, na nilitamani kufuata mfano wa Kristo, ili kufuatilia kuishi kulingana na mwenendo wa mtu sahihi ili kumridhisha Mungu. Baada ya hapo, nikifuata mfano wa Kristo na kuishi kulingana na mwenendo wa mtu wa kweli likawa ndilo lengo nililofuatilia.

Baadaye, kulikuwa na wakati ambapo nilisoma kifungu cha maneno ya Mungu na sikuweza kukielewa. Sikujua kilimaanisha nini, lakini kwa ajili ya kujiepusha na aibu, sikuwa radhi kujiweka kando na kutafuta ushirika na ndugu zangu wa kiume na wa kike. Nilihofia kuwa wangeniangalia kwa dharau kwa sababu nilikuwa nimezoea kutatua masuala ya watu wengine na kamwe sikuwa nimetaja matatizo yangu mwenyewe ili kutafuta msaada kutoka kwa wengine. Baadaye, nilitambua kwamba kutotaka kwangu kukubali ushirika bado ulikuwa ni utawala wa asili yangu ya kiburi na kutotaka kuangaliwa kwa dharau na wengine. Niliasi dhidi ya mwili ili kutafuta ushirika na ndugu zangu wa kiume na wa kike. Sikuwa nimewahi kudhania kwamba hawakukosa tu kuniangalia kwa dharau, lakini kwa subira waliwasiliana nami mapenzi ya Mungu, na shida yangu ilitatuliwa kwa haraka sana. Kulikuwa na wakati mwingine ambapo ndugu mmoja alinituma nipeleke barua iliyohusiana na kazi ya kanisa. Kwa sababu ya kiburi changu na kwamba nilikamilisha kazi hiyo kwa msingi wa mawazo yangu mwenyewe, haikuwasilishwa kwa wakati wake. Alipoona kuwa ingechelewesha kazi, huyu ndugu akawa na wasiwasi sana. Alinishughulikia na kunifichua. Wakati huo nilikuwa na wasiwasi sana na niliona aibu, lakini nilijua pia kwamba hili lilikuwa ni Mungu akinishughulikia na kuvipogoa vipengele vyangu. Ilikuwa ni Mungu akipima kama nilikuwa na utii au la, na kama ningeweka ukweli katika matendo au la. Nilimwomba Mungu: “Ee Mungu, leo nilishughulikiwa na ndugu yangu, niliona wasiwasi. Nilitaka pia kulipinga kwa sababu katika siku za nyuma, daima nilikuwa katika cheo cha juu na nikiwakaripia wengine, na sikuwa nimewahi kutii ukweli. Daima niliishi kwa kudhihirisha sura ya Shetani. Sasa, nina uzoefu mwingi sana wa kazi ya Mungu na ninaelewa kwamba mtu ambaye anaweza kukubali kushughulikiwa na kupogolewa ndiye wa maana zaidi. Huyu ni mtu ambaye ni mtiifu kwa Mungu na anayemwogopa Mungu. Ni mtu wa aina hii tu aliye na uadilifu na mwenendo wa binadamu. Sasa niko radhi kuunyima mwili wangu mwenyewe na moyo wa kumpenda Mungu. Niko radhi Wewe uusisimue moyo wangu, ulikamilishe azimio langu.” Baada ya maombi hayo, nilihisi sana amani na utulivu katika moyo wangu. Niliona kuwa lile Mungu alilolifanya lilikuwa kubwa, na kwamba kupitia kwa watu, matukio, na mambo, Alinisaidia kujitambua ili niweze kubadilika haraka iwezekanavyo. Kuanzia sasa kwendelea, niko radhi kumtafuta Mungu zaidi, kumtegemea Mungu ili kutimiza wajibu wangu vizuri iwezekanavyo. Baada ya hapo, ndugu yangu alikuwa na wasiwasi kwamba ningekuwa sitaki kukubali yote haya, hivyo aliwasiliana nami juu ya mapenzi ya Mungu. Niliongea kuhusu utambuzi wangu juu ya uzoefu wangu mwenyewe. Tulicheka pamoja kuhusu hilo, na kutoka moyoni mwangu nilitoa shukrani kwa wokovu wa Mungu, kwa Yeye kunibadilisha. Utukufu wote uwe kwa Mungu!

Kwa hiyo, kupitia muda baada ya muda wa hukumu na kuadibu kwa Mwenyezi Mungu, tabia yangu ya kiburi ilibadilika hatua kwa hatua. Ningeweza kuwa mtu asiye makeke, ningeweza kwa subira kuwasikiliza wengine wakiongea, na ningeweza kutilia maanani mapendekezo ya wengine. Ningeweza kukusanya maoni ya ndugu zangu wa kiume na wa kike juu ya masuala fulani, na ningeweza kushirikiana kwa upatanifu nao. Chochote kilichotokea, sikuwa tena na kauli ya mwisho, na sikuwa tena na kiburi na kutokuwa radhi kuwasikiliza wengine. Hatimaye nilikuwa nimepata ubinadamu kidogo. Tangu wakati huo, nahisi kwamba nimekuwa mtu wa kawaida zaidi. Mimi huishi maisha bila shida, kwa furaha sana. Naushukuru wokovu wa Mwenyezi Mungu kwangu. Bila wokovu Wake, bado ningekuwa napambana kwa uchungu katikati ya giza na dhambi bila kuweza kamwe kutoka kwa upotovu. Bila wokovu ya Mungu, asili yangu ingekuwa imekuwa tu ya kiburi zaidi na zaidi, hata nikiwafanya watu kuniabudu kama Mungu, kiasi cha kuikasirisha tabia ya Mungu na kupata adhabu Yake lakini bila mimi kulitambua. Kupitia muda baada ya muda wa hukumu na kuadibu kwa Mungu, niliona kwamba upendo Wake ni halisi sana, na kwamba daima Ametumia upendo Wake kunishawishi, akinisubiri ili nijigeuze. Bila kujali ni jinsi gani nilivyokuwa muasi, bila kujali ni jinsi gani nilivyokuwa mgumu kushughulikiwa, ni malalamiko mangapi na suitafahamu nilizokuwa nazo za Mungu, Hakuwa amewahi kamwe kulifanya kuwa suala kubwa. Bado kwa bidii Alikuwa ameanzisha kila aina ya mazingira ili kuuamsha moyo wangu, kuiamsha roho yangu, kuniokoa kutoka kwa mateso ya Shetani, kuniruhusu niishi katika mwanga wa Mungu, kutembea njia ya kweli ya maisha ya binadamu. Mungu kwa subira alingoja zaidi ya miaka 20 na kulipa gharama isiyo kifani kwa ajili yangu—Upendo wa Mungu kweli ni mkubwa na hauna mwisho! Sasa, hukumu na kuadibu kwa Mungu vimekuwa hazina yangu; pia ni chanzo cha thamani cha utajiri kutoka kwa uzoefu wangu na ni kitu ambacho sitaweza kukisahau kamwe. Mateso haya yalikuwa na thamani na maana. Ingawa bado sijafikia matakwa ya Mungu, ningali naufuatilia kwa matumaini mabadiliko katika tabia, na niko radhi kwa kina sana kupitia uzoefu wa hukumu ya Mungu na kuadibiwa. Naamini kuwa kwa hakika Anaweza kunigeuza kuwa mtu wa kweli anayeweza kukubaliana na mapenzi Yake.

Inayofuata: Kuzaliwa Upya

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Kuripoti Au Kutoripoti

Na Yang Yi, Uchina Mwenyezi Mungu anasema, “Kwa minajili ya majaliwa yenu, mnastahili kutafuta kuidhinishwa na Mungu. Hii ni kusema kwamba,...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp