Roho Yangu Yakombolewa
“Katika maisha yake, kama mwanadamu anatamani kutakaswa na kufikia mabadiliko katika tabia yake, kama anatamani kuishi kwa kudhihirisha maisha yenye maana, na kutimiza wajibu wake kama kiumbe, basi lazima akubali adabu na hukumu ya Mungu, na lazima asiruhusu nidhamu ya Mungu na kipigo cha Mungu kiondoke kwake, ili aweze kujiweka huru kutokana na kutawalwa na ushawishi wa Shetani na kuishi katika mwanga wa Mungu. Ujue kwamba adabu ya Mungu na hukumu ni mwanga, na mwanga wa wokovu wa mwanadamu, na kwamba hakuna baraka bora zaidi, neema au ulinzi bora kwa ajili ya mwanadamu” (“Kuadibu na Kuhukumu kwa Mungu Ndiko Mwanga wa Wokovu wa Mwanadamu” Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Maneno haya ya Mungu yananikumbusha tukio fulani lililopita.
Mnamo Oktoba 2016, video moja ya muziki ambayo nilishiriki katika kubuni miondoko yake iliwekwa mtandaoni. Kina ndugu waliipenda, na walipendekeza kwamba niongoze timu ya wacheza ngoma ya kanisa. Nilifurahi sana kiasi kwamba nilimwomba Mungu kwamba nitamshuhudia kwa kutekeleza wajibu wangu vizuri kanisani. Timu ya dansi ilianza kufanya kazi yao vizuri kwa haraka. Kina ndugu walinijia ili niwasaidie kutatua changamoto za kucheza ngoma. Na bila shaka jambo hili lilizidisha kiburi changu sana, na nilihisi kana kwamba nilikuwa mtu mwenye kipaji muhimu sana kanisani. Muda mfupi baadaye, Dada Ye alikuja kufanya kazi nami, kama ilivyopangwa na kiongozi wa kanisa. Hili lilinifurahisha sana na nikawaza, “Dada Ye ana uzoefu wa kitaalamu wa kucheza ngoma, na yeye hufanya vizuri katika mitindo tofauti ya dansi kunizidi. Tunaweza kusaidiana na kufanya vizuri katika wajibu wetu.” Baada ya muda fulani, tulikuwa tukijitayarisha kupiga picha za video ya muziki, na maoni ya Dada Ye ya koregrafia yalikuwa yenye utambuzi zaidi kuliko yangu. Kila mtu alionekana kuyapenda. Sikupendezwa sana na jambo hilo na nikawaza, “Je, wengine watanionaje sasa? Je, watafikiri kwamba sina uwezo sawa na wa Dada Ye? Je, akinishinda, wajibu wangu bado utakuwa muhimu katika timu hii?” Kisha wengine wakaanza kumwendea Dada Ye kila walipokuwa na tatizo, na jambo hilo lilinikera sana. Nilikuwa msimamizi lakini walimtafuta badala ya kunitafuta. Je, hiyo haikumaanishi kuwa walimpenda zaidi? Sikuhisi vizuri, kwa hivyo niliamua kufanya onyesho zuri sana ili nithibitishe kuwa nilikuwa hodari kama yeye.
Mimi na Dada Ye tuligawanya kazi zetu baadaye ili kutosheleza mahitaji ya kazi, mimi nikisimamia video ya muziki, na yeye akisimamia maonyesho ya jukwaa. Nilifurahishwa sana na haya. Tulipofanya kazi pamoja hapo awali, nilihisi kwamba nilipuuzwa. Nilitaka kuchukua fursa hiyo kumthibitishia kila mtu kwamba kuwa nilikuwa bora kumshinda. Nilitumia saa nyingi kutafiti miondoko na mitindo mipya ili nitengeneze video bora ya muziki, lakini nilipoona kwamba Dada Ye alikuwa karibu kumaliza utunzi wake wa dansi, ilhali koregrafia yangu haikuwa imealizika bado, nilihisi wasiwasi na mashaka. Kwa hivyo nilianza kuongeza kasi. Nilikuwa mkali kwa kina ndugu katika mazoezi yetu. Wakati mmoja nilimkemea ndugu fulani kwa sauti ya kukaripia, alipokuwa akicheza dansi vibaya. Niliogopa kwamba iwapo asingecheza vizuri, onyesho langu lisingekuwa zuri kama la Dada Ye. Kabla ya kupiga picha, ndugu moja alisema kwamba hakukuwa na uchezaji dansi wa kutosha katika utangulizi. Na alisema ukweli kabisa, lakini wakati huo nilikanganyikiwa, kwa hivyo alipendekeza nizungumze na Dada Ye. Sikufurahi kabisa niliposikia haya. Je, kumwendea ili kumwomba msaada kusingenifanya nionekane kana kwamba sikuwa na uwezo? Iwapo Dada Ye angehusika, basi asingepata sifa mwishoni? Nilikuwa nimetumia wakati wangu na nguvu yangu kuimarisha matokeo ya mwisho. Kwa hivyo la; sitamwomba msaada. Nilisema, “Hebu tusizingatie maelezo madogo. Itakapomalizika, tutaweza kuangalia matokeo ya mwisho.” Baadaye, kiongozi alitazama video yetu ya muziki na akasema kwamba haikumshuhudia Mungu na akatuambia tuitengeneze upya. Nilifadhaika sana na nikahisi kana kwamba moyo wangu ulichomwa. Niliwaza, “Sasa wengine wote wataniona jinsi nilivyo kwa kweli. Wataona kuwa mimi si hodari kama Dada Ye na kwamba sina uwezo. Sasa nitawezaje kushikilia nafasi ya kudumu katika timu?” Baada ya hapo, sikuweza kufikiria lolote ila sifa yangu. Sikuweza kulala usiku. Nilionekana kusingizia mikutanoni na kuzembea katika wajibu wangu.
Na kwa hivyo, kiongozi wangu alinijia. Alipoona kwamba sikujijua, alinifunua, akisema kwamba nilimwonea wivu Dada Ye kwa ajili ya umaarufu wangu mwenyewe, na sikuwa nimezingatia kazi ya kanisa, na kwamba nilikuwa mbinafsi. Aliniambia nitafakari, kisha akanisomea maneno ya Mungu: “Mara tu inapogusia cheo, sura au sifa, moyo wa kila mtu huruka kwa matazamio, na kila mmoja wenu daima hutaka kujitokeza, kuwa maarufu, na kutambuliwa. Watu wote hawataki kushindwa, bali daima wanataka kushindana—hata ingawa kushindana kunaleta fedheha na hakukubaliwi katika nyumba ya Mungu. Hata hivyo, bila kupinga, bado huridhiki. Unapomwona mtu fulani akitokeza, unahisi wivu, chuki, na kuwa hiyo si haki. ‘Mbona nisitokeze? Mbona kila mara ni mtu huyo anayetokeza, na hauwi wakati wangu kamwe?’ Kisha unahisi chuki fulani. Unajaribu kuizuia, lakini huwezi. Unamwomba Mungu na unahisi nafuu kwa muda, lakini punde unapokumbana na hali ya aina hii tena, huwezi kulishinda. Je, hii haionyeshi kimo kisicho komavu? Je, si mtu kuanguka katika hali hizi ni mtego? Hizi ndizo pingu za asili potovu ya Shetani ambazo huwafunga wanadamu. ... Kadiri unavyong’ang’ana, ndivyo giza litakuzingira zaidi, na ndivyo utakavyohisi wivu na chuki, na hamu yako ya kupata itaongezeka na kuongezeka tu. Kadiri hamu yako ya kupata ilivyo kuu, ndivyo utakaavyopunguza kuweza kufanya hivyo, na unapopata kidogo chuki yako itaongezeka. Chuki yako inapoongezeka, utakuwa mbaya zaidi. Kadiri ulivyo mbaya ndani yako, ndivyo utakavyotekeleza wajibu wako vibaya zaidi; kadri unavyotekeleza wajibu wako vibaya, ndivyo utakuwa mwenye manufaa kigogo zaidi. Huu ni mzunguko mwovu uliofungamana. Ikiwa huwezi kamwe kutekeleza wajibu wako vizuri, basi, utaondolewa polepole” (“Mpe Mungu Moyo Wako wa Kweli, Na Unaweza Kupata Ukweli” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Maneno haya ya Mungu yalikuwa pigo kali sana kwangu. Mungu alifichua hali yangu mwenyewe hasa. Nilionea wivu vipaji vya Dada Ye na nilifikiri tu kuhusu sifa yangu. Hali hiyo ilichukiza. Nilikumbuka jinsi nilivyokuwa na wivu kabisa tangu Dada Ye alipojiunga na timu na kuonyesha kipaji chake. Niliogopa kwamba wengine wangemstahi na hivyo ingehatarisha cheo changu. Nilitaka kuonyesha uwezo wangu na nilihisi kwamba sikuwa na budi kujipambanisha naye. Nilipogundua kwamba programu yake ya dansi ilikuwa ikiendelea haraka zaidi kuliko yangu, nilianza kuwa mkali na nilitaka mengi kutoka wengine ili nisishindwe naye. Ilikuwa dhahiri kwamba ingekuwa bora kama ningekwenda kuzungumza na Dada Ye. Lakini nilitafuta visingizio vya kujitenga naye, nikiogopa angejipatia sifa yote. Kwa hivyo, matatizo mengine hayakutatuliwa mapema, na hata baada ya kina ndugu kufanya kazi kwa bidii sana, kazi hiyo haikuridhisha vya kutosha kutumika kama ushuhuda kwa Mungu. Kiongozi wa kanisa alipompangia Dada Ye afanye kazi nami, ilikuwa ili tuweze kuleta uwezo wetu pamoja na kumshuhudia Mungu kupitia maonyesho hayo, lakini sikuwa nikizingatia mapenzi ya Mungu hata kidogo. Nilivuruga kazi ya kanisa kwa kushindania kupata sifa kila wakati. Nilikuwa nimempinga Mungu na nilifanya matendo maovu tu. Wazo hili lilinifanya nijutie yote. Nilimwomba Mungu na sikutaka kamwe kuonea wivu mafanikio ya wengine. Nilitaka kutubu, kufanya kazi vizuri na Dada Ye, kutimiza wajibu wetu na kufanya kazi vizuri pamoja.
Baada ya hapo, tulifanya kazi pamoja katika koregrafia, na mtazamo wangu ulianza kuwa bora kidogo. Kuna na nyakati ambapo bado nilimwonea wivu, lakini nilijua kwamba nilipaswa kuunga mkono kazi ya kanisa wala si maslahi yangu ya binafsi Niliukana mwili na kuacha ubinafsi wangu kwa makusudi, nikifirikia jinsi ya kufanya kazi na dada yangu ili kuboresha mpango ule. Tulipopata matatizo, tulifanya kazi pamoja mara nyingi, tukazungumza juu ya upotovu wetu na kutafuta ukweli ili kuutatua. Kisha Mungu alitubariki upesi na koregrafia ilifanya vizuri. Kutenda ukweli kulinifanya nihisi amani moyoni.
Miezi michache baadaye, mimi na Dada Ye tulikuwa tukishughulikia maonyesho pamoja. Mambo yalikwenda haraka sana mwanzoni, na wengine walipenda jinsi tulibuni miondoko ya dansi zile. Niliridhika sana. Halafu siku moja, kiongozi aliuliza jinsi mambo yalivyokuwa yakiendelea, na nikajibu, “Tunapiga hatua.” Kisha dada moja akaingilia, “Dada Ye ana mawazo mazuri, kazi inaendelea vizuri sana.” Hilo lilinikera sana kwa hivyo nikawaza, “Kwa nini unasema hivyo? Sasa kila mtu anajua mawazo ya dansi yalitoka kwa Dada Ye, na sitapata sifa yoyote. Sharti nitafute jinsi nitakavyofanikisha jambo fulani, vinginevyo, kila mtu atanionaje?” Wakati mmoja wa mazoezi, nilifikiri juu ya mwondoko mpya wa sarakasi. Na niliwaza huku nikisisimka, “Mimi ni hodari sana katika sarakasi. Almradi tufanye mazoezi haya vizuri, mbali na kuongeza thamani ya koregrafia, pia, kila mtu atatambua vyema uwezo wangu. Kisha hatimaye, kila mtu atasifu kazi yangu yote.” Lakini siku iliyofuata, nilipokuwa nikiwafundisha kina ndugu mwondoko huo, walitoa maoni kwamba mwendo ulikuwa wa haraka sana na kwamba mwondoko ule ulikuwa mgumu. Jioni hiyo, dada mmoja alinionya, “Watu wanaweza kujijeruhi kwa urahisi kutokana na mwondoko huo. Sidhani kwamba ni salama.” Nilikuwa na wasiwasi kwamba huenda wangebadilisha mwondoko wangu mpya na mwingine, kisha ningejilinganisha vipi na Dada Ye? Kwa hivyo nilimhimiza kila mtu ajaribu tena na niliacha tu wakati ambapo dada kadhaa walianguka na kujijeruhi. Nilifadhaika na kuhisi vibaya sana. Kwa hivyo niliomba timu msamaha na nikarekebisha mwondoko huo, lakini sikutafakari juu yangu mwenyewe licha ya kile kilichokuwa kimetokea. Muda mfupi baadaye, upigaji picha ulikuwa karibu kuanza. Mimi na Dada Ye tulifanya maonyesho. Wakati wa kupiga picha, sikufikiri kwamba nilicheza dansi vizuri katika video moja, kwa hivyo nilimsihi mwelekezi anipige tena picha. Lakini baadaye niliona kwamba kulikuwa na picha nyingi ambazo zilizonyesha uso wa Dada Ye, na kwamba picha zangu za karibu zilionyesha upande tu. Nilivunjika moyo. Katika vipindi vilivyofuata vya kupiga picha, sikuweza hata kutabasamu, na uchezaji ngoma wangu haukuvutia. Niliwaza sana na kufikiri: Naweza kucheza dansi vizuri zaidi kuliko Dada Ye. Sikuweza kutazama maonyesho ya dansi ambayo nilipaswa kukagua. Sikujali iwapo onyesho hilo lilimshuhudia Mungu au la. Na kwa hivyo, video hiyo ilipotokea, kila mtu alisema kwamba jinsi tulivyocheza ngoma kulikosa kuvutia. Mbali na kutomshuhudia Mungu, pia ilimwaibisha Mungu. Baadaye, kiongozi alisema kwamba nilikuwa nikishindania sifa na faida, na sikuwa nimefanya wajibu wangu, na akaamua kuniachisha wajibu wangu. Nilifadhaika sana. Mwanzoni, nilitaka tu kumridhisha Mungu, lakini baadaye nilishindania sifa. Programu zote ambazo nilikuwa nimebuni zilimwaibisha Mungu. Hili lilikuwa kosa. Nilikuwa nimepoteza fursa yangu ya kufanya wajibu wangu kupitia dansi. Nililia sana.
Nilifikiria tena na tena, “Najua kwamba kupigania sifa na faida si vizuri, hivyo basi kwa nini siwezi kujizuia kufuatilia mambo hayo? Sababu halisi ni ipi?” Wakati wa ibada, nilisoma maneno haya kutoka kwa Mungu. “Shetani hutumia umaarufu na faida kudhibiti fikira za mwanadamu hadi anachofikiria tu ni umaarufu na faida. Wanapambana kwa sababu ya umaarufu na faida, wanateseka matatizo kwa sababu ya umaarufu na faida, wanastahimili udhalilishaji kwa sababu ya umaarufu na faida, wanatoa kila kitu walichonacho kwa sababu ya umaarufu na faida, na watafanya maoni au uamuzi wowote kwa ajili ya umaarufu na faida. Kwa njia hii, Shetani humfunga mwanadamu kwa pingu zisizoonekana. Pingu hizi zinabebwa na watu, na hawana nguvu ama ujasiri wa kuzirusha mbali. Kwa hivyo, bila kujua, watu huvumilia pingu hizi na kutembea kwenda mbele kwa ugumu mkubwa. Kwa ajili ya umaarufu huu na faida hii, binadamu humwepuka Mungu na kumsaliti, na wanazidi kuwa waovu zaidi na zaidi. Kwa njia hii, hivyo kizazi kimoja baada ya kingine kinaharibiwa katika umaarufu na faida ya Shetani. Tukiangalia sasa vitendo vya Shetani, nia zake husuda ni za kuchukiza? Pengine leo bado hamwezi kuona kupitia nia husuda za Shetani kwa sababu mnafikiri hakuna maisha bila umaarufu na faida. Mnafikri kwamba, iwapo watu wataacha umaarufu na faida nyuma, basi hawataweza tena kuona njia mbele, hawataweza tena kuona malengo yao, siku zao za baadaye zawa giza, zilizofifia na za ghamu. Lakini, polepole, nyote siku moja mtatambua kwamba umaarufu na faida ni pingu za ajabu ambazo Shetani hutumia kumfunga mwanadamu. Hadi ile siku utakuja kutambua hili, utapinga kabisa udhibiti wa Shetani na utapinga kabisa pingu anazoleta Shetani kukufunga. Wakati utakapofika wa wewe kutaka kutupilia mbali vitu vyote ambavyo Shetani ameingiza ndani yako, utakuwa basi umejiondoa kwa Shetani na pia utachukia kwa kweli vyote ambavyo Shetani amekuletea. Hapo tu ndipo utakuwa na upendo na shauku ya kweli kwa Mungu” (Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI). Maneno ya Mungu yalifichua mbinu na nia mbaya za Shetani za kuwapotosha wanadamu. Yeye hutumia umaarufu na faida kuwadhibiti watu na kuwapotosha ili wakengeuke, wapotoke, wampinge Mungu na watende maovu. Nilikuwa nimeelimishwa na kushawishiwa na Shetani tangu nilipokuwa mdogo. “Mtu anapaswa kuleta heshima kwa wahenga wake,” na “Urithi wa mtu huonyesha jinsi maisha yake yalivyo” zilikuwa kanuni za kishetani zilizokita mizizi ndani yangu. Bila kujali nilikuwa katika kikundi kipi, nilitaka kuwa wa kipekee, nilitaka kupendwa na kusifiwa. Kumwona mtu mwingine akitia fora kulinifanya nione wivu, na nilifanya kila nililoweza kufaulu, nikijitahidi kila mara kwa ajili ya sifa na faida na kutaabishwa na hila za Shetani. Nilizidi pia kuwa na kiburi na ubinafsi. Nilitaka kumshinda Dada Ye kwa ustadi wangu wa ufundi, kuonyesha vipaji vyangu, na sikujali iwapo wacheza ngoma walikuwa na uwezo wa kimwili, jambo ambalo liliwasababisha dada kadhaa wajeruhiwe. Tulipokuwa tukipiga picha za video, nilitaka kutumia picha yangu ya karibu ya pekee kuonyesha kuwa nilikuwa ni bora kumzidi Dada Ye, na kwa sababu nilifikiri kwamba miondoko yangu ilikuwa na kasoro, nilimwamuru mwelekezi apige picha tena na tena, na nilichelewesha kazi. Na wakati ambapo upande wa uso wangu tu ndio ulioonekana katika video, ilhali picha ya Dada Ye ilionyesha uso wake, nilijawa na chuki na nikaishi katika hali hasi, na sikulenga kufanya wajibu wangu vizuri. Kama matokeo, uchezaji ngoma wangu ulimwaibisha Mungu. Koregrafia yangu haikuwa ya kumtumikia Mungu, bali ilikuwa ya kunitumikia. Pambano langu la umaarufu lilianza kuwa vizuizi vikubwa kwa kazi ya kanisa na pia liliwadhuru sana wale walionizingira. Tabia yangu ilimchukiza na kumkirihi Mungu sana! Kisha nikakumbuka maneno haya kutoka kwa Mungu: “Hii ‘njia ovu’ hairejelei kiasi kidogo cha vitendo viovu, lakini inarejelea chanzo cha maovu katika tabia ya watu” (Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II). Maneno ya Mungu yalinionyesha kwamba sikuwa nimeachishwa wajibu wangu kwa sababu nilikuwa nimefanya mambo machache mabaya. Niliachishwa kwa sababu njia niliyokuwa nikiitembea ilikuwa ovu na chanzo cha matendo yangu pia kilikuwa kiovu. Tangu nilipoanza kufanya kazi na Dada Ye, nilikuwa nikipigania masilahi yangu mwenyewe kila mara, na kutekeleza biashara ya kibinafsi. Kumaanisha kwamba nilikuwa nikimpinga Mungu. Nilihisi kama kwamba nilikuwa nimejawa na woga. Niliona kwamba nilikuwa nikimpinga Mungu kwa kufuatilia sifa na hadhi, na nisingetubu, ningeadhibiwa na kuondolewa mwishowe. Nilihisi hatia mbaya sana. Nililia na kumwomba Mungu. “Mungu! Nimepoteza wajibu wangu. Haki Yako inafichuliwa kwangu na najua kwamba Unanilinda. Asante sana kwa kukomesha njia zangu mbaya mapema. Natubu Kwako.”
Katika siku zilizofuata, nilihubiri injili kanisani na nikatafakari kujihusu. Kila nilipokumbuka mambo ambayo nilikuwa nimeyafanya kwa ajili ya sifa na faida, nilihisi majuto. Nilijichukia kwa kutothamini fursa ambayo Mungu alikuwa Amenipa. Nilipotazama tena video hizo za muziki, nilitaka sana kurudi, na kuanza upya. lakini bila shaka, hiyo haikuwezekana. Bila shaka, yote niliyoweza kufanya sasa ni kujifunza kutokana na makosa yangu na kufanya wajibu wangu mpya vizuri. Ajabu ni kwamba, mwezi mmoja baadaye, kiongozi wa kanisa aliniruhusu nijiunge na timu tena. Shukrani kwa Mungu! Niliguswa sana na habari hii kiasi kwamba sikuweza kabisa kuzuia machozi yangu, na nikaamua kuacha kufuatilia sifa na faida na kuthamini fursa hii, kulipa upendo wa Mungu na kufanya kazi na kila mtu, na kufanya wajibu wangu vizuri.
Wakati mmoja baada ya kujiunga tena na timu, Dada Ye alisema kwamba mwondoko wa dansi ambao nilikuwa nimewafunza wengine haukufikia kiwango kilichowekwa. Nilihisi aibu wakati huo, kisha nikawaza, “Unawezaje kunikosoa mbele ya wengine hivyo? Sasa hakika watafikiri kwamba wewe ni bora kunishinda. Siwezi kukubali wanidharau. Mimi pia ni mweledi. Unajua kwamba miondoko yako ya dansi pia ina kasoro.” Nilitaka kutupilia mbali miondoko aliyokuwa amebuni, na kisha nikagundua kwamba nilikuwa nikifikiri juu yangu tena, kwa hivyo nilimwomba Mungu moyoni mwangu. Nilifikiria maneno ya Mungu baada ya kuomba: “Kadiri wakati fulani ulivyo muhimu zaidi, ndivyo watu wanavyoweza kutii zaidi na kuachana na masilahi yao ya binafsi, majisifu, na kiburi, na watekeleze wajibu wao ipasavyo, na ni hapo tu ndipo watakapokumbukwa na Mungu. Hayo yote ni matendo mema! Bila kujali kile ambacho watu hufanya, ni kipi kilicho muhimu zaidi—majisifu na kiburi chao, au utukufu wa Mungu? (Utukufu wa Mungu.) Ni kipi kilicho muhimu zaidi—majukumu yako, au masilahi yako mwenyewe? Kutimiza majukumu yako ndilo jambo lililo muhimu zaidi, na unawajibikia majukumu hayo. … Utavipa kipaumbele wajibu wako mwenyewe, mapenzi ya Mungu, kumshuhudia Yeye, na majukumu yako mwenyewe. Hii ni njia nzuri sana ya kutoa ushuhuda, na inamwaibisha Shetani!” (Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Nilichangamka ndani yangu. Je, hali hii haikuwa njia ya Mungu ya kunijaribu? Kila kunapokuwa na mgongano kati ya masilahi yangu na ya kanisa, napaswa kulenga kuridhisha mapenzi ya Mungu, kutenda ukweli na kumwaibisha Shetani. Mara nilipotulia niliona kwamba sikuwa nimewafundisha mwondoko huo kwa usahihi. Dada Ye alikuwa amenikosoa waziwazi na jambo hilo liliniaibisha, lakini nilikubali maoni yake kwa sababu nilijua kwamba alikuwa amesema ukweli. Kwa hivyo baada ya hatimaye kuacha kujifikiria, tulifanya kazi haraka pamoja na kumaliza koregrafia hiyo. Nilihisi pia kwamba nilikuwa nikitimiza wajibu wangu kwa njia hiyo.
Tukio hili lilinionyesha kweli kwamba hukumu ya Mungu ni wokovu na upendo Wake kwangu. Hukumu ya Mungu kweli iliniamsha na ilinifanya nione hatari za kufuatilia sifa na faida. Hiyo ilisahihisha mtazamo wangu ambao haukuwa sahihi. Na nilianza kufanya wajibu wangu na kufuatilia ukweli kwa njia halisi. Shukrani kwa Mungu!
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?