Kushikilia Wajibu Wangu

24/01/2021

Na Yangmu, Korea ya Kusini

Nilikuwa nikihisi wivu sana nilipowaona ndugu wakifanya maonyesho, wakiimba na kucheza kwa kumsifu Mungu. Niliwaza kuhusu siku ambayo ningeenda jukwaani kuimba na kumshuhudia Mungu. Nilidhani ingekuwa heshima kubwa sana! Siku hiyo iliwadia mapema kuliko vile nilivyofikiria.

Mnamo Mei 2018, nilijiunga na mazoezi ya Wimbo wa Ufalme, onyesho la kwaya. Sikuwa nimewahi kuhudhuria mafunzo ya kuimba au kucheza ngoma, kwa hivyo mazoezi yalikuwa magumu sana kwangu mwanzoni. Nilikuwa mwoga sana nilipoimba na nilikuwa na sura iliyokazika usoni mwangu, na daima sikuwa katika utaratibu na wengine nilipokuwa nikicheza dansi. Hata hivyo, bado sikufa moyo. Ningelifikiria Wimbo wa Ufalme kuwa ushuhuda wa binadamu wote kuhusu kuja kwa Mungu na mara moja ningehisi niliyetiwa msukumo sana hivi kwamba ningeendelea kuomba tu. Niliazimia kuweka nguvu zangu zote katika kuimba na kucheza vizuri. Mungu alinielekeza polepole, na baada ya miezi michache nilianza kuyazoea yote zaidi. Pia nilikuwa nikiwaongoza ndugu katika kufanya mazoezi ya sura zao. Nilianza kujisikia sana, nikiwaza, “Sura na miondoko Yangu kweli ni mizuri sasa. Hakika nitawekwa mbele tutakapopiga picha za sinema, na ndugu kutoka nyumbani watakaponiona katika filamu hiyo watashangilia sana, watafurahia sana. Nina hakika watakuwa na wivu pia, na wataniheshimu.” Nilijisikia vizuri sana kila nilipokifikiria hilo na nilikuwa na nguvu nyingi sana ya kufanya wajibu wangu. Hata tulipofanya mazoezi hadi nikalowa jasho na kuumwa, bado sikupumzika. Niliogopa kwamba kama ningezembea, singewekwa mbele na kisha ningekuwa na fursa ndogo ya kujionyesha. Nilijua nililazimika kufanya bidii bila kujali hali ingekuwa ngumu na ya kuchosha vipi. Mwelekezi alipanga nafasi zetu kwenye jukwaa muda wa kupiga picha za sinema ulivyokaribia. Nikiwa nimefurahi, nilifungua orodha ya waigizaji na kutafuta jina langu, kisha nikaona kwamba nilikuwa katika safu ya saba. Sikuamini macho yangu kwa muda. Kwa nini niliwekwa nyuma sana? Je, mwelekezi alikuwa amekosea? Sura na miondoko yangu ilikuwa sawa kabisa, na hata nilikuwa nikiwasaidia ndugu kufanya mazoezi. Nilidhani kwamba kweli nilipaswa kuwa kwenye safu za kwanza za mbele. Nawezaje kuwa nyuma? Kama singeonekana kwenye skrini, iwapo hakungekuwa na picha zinazonionyesha, wengine hata hawangeniona. Wazo hilo liliniacha nikiwa sijaridhika hata kidogo. Katika mazoezi baada ya hapo, sikuweza kuweka furaha yoyote katika uimbaji wangu au nguvu katika kucheza ngoma kwangu. Nilikuwa nikinuna kila wakati, hasa nilipoona kwamba sura na miondoko ya akina dada wengine ilikuwa ya kawaida tu, lakini walikuwa katika safu tatu za mbele. Kwa kweli sikuelewa. Walikuwaje bora kuniliko mimi? Je, kwa nini walikuwa wamewekwa mbele, wakati mimi nilikuwa nimewekwa nyuma? Nilijawa na wivu na sikuweza kukubali jambo hilo. Niliona kwamba ndugu wengine ambao kwa ujumla walikuwa bora katika mazoezi kuliko nilivyokuwa waliwekwa hata nyuma zaidi, lakini walionekana watulivu kabisa wakati wa mazoezi kana kwamba hilo halikuwa limewaathiri hata kidogo. Nilishangazwa: Hata wakiwa nyuma, walikuwa watiifu na walifanya wajibu wao kwa uchangamfu, hivyo kwa nini ilikuwa vigumu sana kwangu, na kwa nini sikuweza kutii? Je, nilikuwa bila busara kweli? Nilihisi kujilaumu kiasi wakati huo, lakini bado sikutafuta ukweli au kutafakari kujihusu. Bado sikuweza kukubali mahali nilipowekwa kwenye mpangilio.

Siku chache baadaye mwelekezi alifanya mabadiliko kadhaa kwa mpangilio. Nilihisi ongezeko la furaha ya siri na nikawaza iwapo ningesongeshwa mbele. Lakini nilipouona, nilitamani sana kulia. Niliwekwa kwenye safu ya mwisho kabisa na ukingoni kabisa ambako kamera haingeweza kuniangazia. Kile nilichoshindwa kuamini hata zaidi ni kwamba dada wengine ambao hawakuwa wamefanya mazoezi kwa muda mrefu waliwekwa mbele yangu. Nilisikitishwa kabisa na nilihisi kuchanganyikiwa. Nilikuwa nimejitahidi sana kufanya mazoezi ya sura na miondoko yangu ili niweze kuwa kwenye filamu, kwa hivyo kwa nini nilikuwa nimeshushwa hadi kwenye kona iliyofichika bila hata nafasi ndogo ya kuonyesha uso wangu? Ningekuwa tu kifaa cha kutumiwa jukwaani! Je, hata kuna haja gani ya kuwa katika onyesho hili? Kama ningejua hapo awali, singefanya bidii sana katika mazoezi. Nilihisi kama kwamba nilikuwa navurugika kimawazo na sikuweza kukubali ukweli huu kabisa. Kwa kweli, katika siku chache zilizofuata za mazoezi, niliishia kutenguka tindi ya mguu wangu. Niliwaza, "Ninaweza kupumzika sasa kwa kuwa tindi ya mguu wangu imetenguka, na hakuna haja ya kujichosha kila siku. Hata hivyo nimewekwa nyuma ambapo hakuna mtu anayeweza kuniona. Kwa nini nifanye bidii sana?" Nilianza kuja nikiwa nimechelewa na kuondoka mapema, na mazoezi yalipozidi kuwa makali, ningepumzika pembeni. Dada wachache walipoona hili walinikumbusha, "Tunakaribia kupiga picha za sinema. Usipotumia siku hizi kufanya mazoezi, hutakuwa katika utaratibu na kila mtu mwingine. Hatuwezi kuzembea." Kusikia hili kulinikasirisha kidogo na kweli nilihisi vibaya. Nilijua kuwa tulikuwa tupige picha za filamu ndani ya siku 20 tu, kwa hivyo kama singejibidiisha na kufanya mazoezi, mradi mzima ungecheleweshwa. Ningekuwa nasababisha usumbufu. Ghafla nilishikwa na woga. Je, ninawezaje kuwa mpotovu hivyo? Ni kupitia katika kutafakari tu ndiyo niligundua kwamba nilikuwa nikitoa visingizio na kupinga, na nilikuwa nimepoteza shauku yangu ya wajibu wangu tangu ule wakati nilipowekwa nyuma na sikuwa na nafasi ya kujionyesha. Nilikuwa nikitia bidii kidogo tu, nikifanya kwa uzembe. Nilikuwa nikimpinga Mungu na kuwa mpinzani. Jeraha langu la kutenguka pia lilikuwa linazidi kuwa baya, ambalo linaweza kuwa kwamba Mungu alikuwa Ananifundisha nidhamu. Kama ningeendelea kuwa mpinzani sana, haijalishi kama ningeweza kujionyesha au la, huenda nisiweze kupanda jukwaani, na kisha ningepoteza hata wajibu wangu. Katika uchungu na kujilaumu kwangu, nilipiga magoti mbele ya Mungu usiku huo kuomba. “Ee Mungu, nimekasirika sana tangu nilipoona kwamba niliwekwa nyuma na sijaweza kutii, nikiwa nimejaa malalamiko, na nimekuwa nikifanya wajibu wangu vibaya, nikizembea kazini. Ninaona jinsi nilivyo mwasi, jinsi ambavyo nimekuhuzunisha. Mungu, naomba Uniongoze kutoka katika hali hii.”

Kisha nilisoma maneno haya ya Mungu: “Mara tu inapogusia cheo, sura au sifa, moyo wa kila mtu huruka kwa matazamio, na kila mmoja wenu daima hutaka kujitokeza, kuwa maarufu, na kutambuliwa. Watu wote hawataki kushindwa, bali daima wanataka kushindana—hata ingawa kushindana kunaleta fedheha na hakukubaliwi katika nyumba ya Mungu. Hata hivyo, bila kupinga, bado huridhiki. Unapomwona mtu fulani akitokeza, unahisi wivu, chuki, na kuwa hiyo si haki. ‘Mbona nisitokeze? Mbona kila mara ni mtu huyo anayetokeza, na hauwi wakati wangu kamwe?’ Kisha unahisi chuki fulani. Unajaribu kuizuia, lakini huwezi. Unamwomba Mungu na unahisi nafuu kwa muda, lakini punde unapokumbana na hali ya aina hii tena, huwezi kulishinda. Je, hii haionyeshi kimo kisicho komavu? Je, si mtu kuanguka katika hali hizi ni mtego? Hizi ndizo pingu za asili potovu ya Shetani ambazo huwafunga wanadamu. Kama mtu ametupilia mbali tabia hizi potovu, basi yeye hayuko huru na aliyekombolewa? Fikiria hili: Ni mabadiliko ya aina gani ambayo mtu anapaswa kufanya iwapo anataka kujizuia kutegwa katika hali hizi, aweze kujinasua kutoka kwazo, na kukombolewa kutoka katika maudhi na utumwa wa mambo haya? Je, mtu anapaswa kupata nini kabla aweze kuwa huru na kukombolewa kwa kweli? Kwa upande mmoja, lazima ang’amue mambo: Umaarufu na faida na vyeo ni vifaa na mbinu tu ambazo Shetani hutumia kuwapotosha watu, kuwatega, kuwadhuru, na kusababisha mkengeuko wao. Kinadharia, lazima kwanza upate ufahamu wa wazi kuhusu hili. Aidha, lazima ujifunze kuacha mambo haya na kuyaweka kando. … Vinginevyo, kadiri unavyong’ang’ana, ndivyo giza litakuzingira zaidi, na ndivyo utakavyohisi wivu na chuki, na hamu yako ya kupata itaongezeka na kuongezeka tu. Kadiri hamu yako ya kupata ilivyo kuu, ndivyo utakaavyopunguza kuweza kufanya hivyo, na unapopata kidogo chuki yako itaongezeka. Chuki yako inapoongezeka, utakuwa mbaya zaidi. Kadiri ulivyo mbaya ndani yako, ndivyo utakavyotekeleza wajibu wako vibaya zaidi; kadri unavyotekeleza wajibu wako vibaya, ndivyo utakuwa mwenye manufaa kigogo zaidi. Huu ni mzunguko mwovu uliofungamana. Ikiwa huwezi kamwe kutekeleza wajibu wako vizuri, basi, utaondolewa polepole(“Mpe Mungu Moyo Wako wa Kweli, Na Unaweza Kupata Ukweli” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Haya yalinigutusha kidogo. Maneno ya Mungu hasa yaliifichua hali yangu mwenyewe. Baada ya kujiunga na kikundi cha kwaya na nikaona kwamba nilikuwa nazidi kuzoea utaratibu, na nilikuwa nikiwaongoza wengine kufanya mazoezi yao ya nyuso zao, nilianza kuhisi kana kwamba nilikuwa nikifanya maonyesho vizuri kuwaliko na kwamba ningekuwa mbele wakati wa upigaji picha za sinema. Nilikuwa nimejawa na nguvu ya wajibu wangu nilipofikiria kwamba ningepigwa picha za filamu, kamba ningeweza kujionyesha. Nilifurahia kufanya kazi kwa bidii na kujichosha, na nikalenga tu kufanya mazoezi ya sura na miondoko yangu. Lakini nafasi yangu ilipoishia kuwa nyuma zaidi, matumaini yangu ya kujionyesha yalivunjika. Nilipinga mipangilio ya mwelekezi na nikakataa kuwakubali wale waliokuwa mbele. Niliwaonea wivu. Niliwaelewa visivyo na kulalamika, nilihisi hilo halikuwa haki, nilijaribu kujieleza na kushindana na Mungu, na nikawa hasi na kuzembea katika wajibu wangu. Hata nilijuta juhudi ambayo nilikuwa nimeweka katika mazoezi. Nilipotafakari juu ya nia na tabia zangu, niliona kwamba sikuwa nikifanya wajibu wangu kwa kuzingatia mapenzi ya Mungu au ili kumshuhudia. Badala yake, nilitaka fursa hiyo ili nijitokeze, kuwafanya wengine waniheshimu. Sikuwa nikipigania tu sifa na hali yangu mwenyewe? Nilikuwa mbinafsi na mwenye kustahili dharau sana! Nafasi hiyo ya kujiunga na kikundi cha kwaya ilikuwa Mungu kuniinua, lakini, nikiwa bila dhamiri na mantiki, sikufikiria jinsi ya kutekeleza wajibu wangu vizuri na kumridhisha Mungu. Badala yake nilipambana kujionyesha. Nilikasirika na kulalamika wakati sikuweza kujionyesha. Nilizama katika hali ya giza zaidi na zaidi. Niliishia kufanya wajibu wangu vibaya, na hili lilimchukiza Mungu. Je, sikuwa nimeanguka katika utando wa Shetani? Niliwafikiria wale ndugu wote ambao walifanya wajibu wao bila kuonekana, ambao hawakupata nafasi ya kwenda jukwaani, lakini walijitahidi bila malalamiko, wakishikilia wajibu wao kwa uthabiti. Nilikuwa duni sana nikilinganishwa nao. Nilihisi kwamba sikujua tofauti ya mema na mabaya, na kwamba nilikuwa na deni kubwa la Mungu. Sikutaka kuendelea kuwa mwasi sana. Nilitaka kutubu kwa Mungu.

Baada ya hapo, nilisoma maneno haya kutoka kwa Mungu: “Lazima ujifunze kuacha na kuweka kando vitu hivi, kuwapendekeza wengine, na kuwaruhusu wengine kutokeza. Using’ang’ane au kukimbilia kujinufaisha punde unapopata nafasi ya kutokeza au kupata utukufu. Lazima ujifunze kujiondoa, lakini hupaswi kuchelewesha utekelezaji wa wajibu wako. Kuwa mtu anayefanya kazi kwa ukimya bila kuonekana, na ambaye hajionyeshi kwa wengine unapotekeleza wajibu wako kwa uaminifu. Kadiri unavyoacha ufahari na hadhi yako, na kadiri unavyoacha masilahi yako mwenyewe, ndivyo utakavyokuwa mwenye amani zaidi, na ndivyo nafasi itakavyofunguka zaidi ndani ya moyo wako na ndivyo hali yako itakuwa bora zaidi. Kadiri unavyopambana ana na kushindana zaidi, ndivyo hali yako itakuwa mbaya zaidi. Ikiwa huamini hili, jaribu na uone! Ikiwa unataka kugeuza hali hii, na usidhibitwe na vitu hivi, basi lazima uviweke kando kwanza na kuviacha(“Mpe Mungu Moyo Wako wa Kweli, Na Unaweza Kupata Ukweli” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Maneno ya Mungu yalinipa njia ya kutenda. Kila nilipotaka kujionyesha tena, ilinibidi nimwombe Mungu na nijikane, niache tamaa zangu mwenyewe na nifikirie zaidi juu ya jinsi ningeweza kutekeleza wajibu wangu kulingana na matakwa ya Mungu, na nishike miondoko yangu vizuri na niimbe nyimbo zangu vizuri. Hili ndilo nililohitaji kufanya. Niligundua kuwa fursa yangu ya kushiriki katika Wimbo wa Ufalme ilikuwa ni mimi kufanya wajibu wa kiumbe aliyeumbwa, iwe nilikuwa mbele au nyuma. Mungu haamui ikiwa watu wamejitolea katika wajibu wao kulingana na mahali wanaposimama kwenye mpangilio, bali kwa uaminifu wao, na kama wanatenda ukweli na wanamtii Mungu. Nilihisi utulivu zaidi baada ya kuelewa mapenzi ya Mungu, na nikasema sala hii: "Mungu, Sitaki kukuasi tena. Haijalishi mahali nafasi yangu iliko, hata kama iko nyuma kabisa ambapo hakuna mtu anayeweza kuniona, Nataka kufanya wajibu wangu vizuri ili nikuridhishe Wewe!"

Katika mazoezi baada ya hapo nilikuwa daima katika safu mbili za nyuma. Wakati mwingine ilinijia kwamba singewahi kuonekana katika filamu kwa njia hiyo, kwamba hakuna yeyote ambaye angeweza kuniheshimu, na ningehisi mwenye kuvunjika moyo kidogo. Lakini nyakati hizo nilisali kwa haraka sana kwa Mungu na kumwomba Autulize moyo wangu, na nikatafakari jinsi ya kudhihirisha kile ambacho Mungu anataka katika kila mstari nilioimba, na jinsi ya kucheza dansi kwa nguvu, kulingana na koregrafia. Nilipoanza kufanya vitu hivi kwa dhati, nilihisi kuwa karibu sana na Mungu na sikujali nilikowekwa. La kushangaza ni kwamba, tulipokaribia kupiga picha za sinema, niliendelea kusongeshwa mbele na pia nilipewa maonyesho mengine madogo ya kupiga picha. Nilimshukuru Mungu kwa kunipa nafasi hiyo ya kufanya mazoezi. Katika siku hizo kadhaa za kupiga picha maonyesho hayo, nilishikilia hisia yangu ya shukrani. Kwa kila upigaji picha, nililenga kuufanya kwa dhati ili nisije nikajuta katika wajibu wangu. Katika picha ya mwisho, niliwekwa kwenye safu ya kwanza kamera ikiwa karibu sana nami. Sikuweza kuamini jambo hilo hata kidogo. Nilihisi kwamba ilikuwa heshima kubwa. Nilimshukuru Mungu mara kwa mara na nilikuwa nimeazimia kufanya kazi nzuri. Nilipokuwa nikitembea tu kwa furaha kwenda kwenye safu ya kwanza, zile taa zote zilikuwa zinaniangazia na kamera zilielekezwa kwangu. Dada mmoja alikimbia kuja kunyoosha mavazi yangu, kutengeneza mapambo yangu, na kurekebisha nywele zangu. Ghafla nikawa na hisia kwamba nilikuwa kivutio, kwamba kila mtu alikuwa akiniangalia, na sikuweza kuficha furaha yangu. Hata katika ndoto zangu sikuwahi kufikiria ningekuwa katika safu ya kwanza. Ikiwa picha hiyo ingetokea vizuri, nilifikiria watu wengi wangeniona na ningejiundia sifa sana. Nilizidi kupendezwa na wazo hilo. Hisia hiyo haingeelezeka. Nikiwa na wazo hilo ghafla niligundua kwamba sikuwa katika hali sahihi, na kwamba nilikuwa nataka kujionyesha tena. Nilimwomba Mungu mara moja na huku nikijikana, lakini bado sikuweza kufuta fikira zangu zisizo sahihi na sikuweza kutulia. Tulipiga picha mbili au tatu za sinema moja baada ya nyingine, lakini sikuweza kujihusisha kikamilifu. Kisha mwelekezi alitukumbusha tuwe katika hali sahihi ya kiakili. Nilianza kuwa na wasiwasi kwamba mwelekezi alikuwa ameona kwamba sura yangu haikuwa sahihi na angeniweka nyuma tena. Nilikuwa na wasiwasi kuwa ningeipoteza nafasi hiyo ya kujionyesha Lakini niligundua kwamba sikupaswa kufikiria maslahi yangu mwenyewe kila wakati, na ilinibidi nizingatie jinsi ya kurekebisha hali yangu ili niweze kufanya wajibu wangu vizuri. Kulikuwa na vita hivi vikali vya ndani kati ya kutaka kufanya wajibu wangu vizuri na kuwa na wasiwasi juu ya kupoteza nafasi yangu ya kujionyesha. Viliniacha nikiwa na wasiwasi mkubwa. Tulichukua picha tano za sinema kwa mfululizo, lakini bado sikuweza kujihusisha kikamilifu, na nilionekana mgumu sana. Niliona wale akina dada wengine wote wakiongea kwa furaha juu ya yale waliyojifunza baada ya upigaji picha, na wengine waliguswa sana kiasi kwamba walikuwa wanalia, lakini sikuweza kupata msisimko. Nilihisi nimevunjika moyo sana na nikaondoka haraka.

Nilipokuwa nikitembea kurudi, nilihisi hatia sana kuhusu kufanya vibaya katika upigaji picha wa sinema. Hao wengine wote walikuwa wamempa Mungu mioyo yao ya uaminifu na tabasamu zisizo na hatia lakini mimi nilikuwa ninafikiria tu kujionyesha. Maonyesho yangu hayakuwa mazuri vya kutosha kumshuhudia Mungu hata kidogo, na Mungu hangekubali wajibu wangu. Wakati huo nilitaka kulia kweli. Nilimwambia Mungu, "Mungu, najuta huu upigaji picha uliopita. Kweli sitaki kujionyesha tena, na ningependa kuwa nyuma ya jukwaa, kwenye kona ambayo hakuna mtu anayeweza kuniona, ama hata kamera. Mradi nina moyo wa kawaida, wa kweli wa kukuimbia kwa dhati, nitahisi furaha na amani, na kamwe sitajisikia mtuhumiwa tena. Lakini nimeshachelewa sana, na siwezi kufidia deni langu." Kadiri nilivyofikiria zaidi juu ya hili ndivyo nilivyokasirika zaidi, nikihisi majuto sana katika jinsi nilivyotekeleza wajibu wangu.

Niliutuliza moyo wangu na nikaanza kulifikiria tena. Kwa nini tamaa yangu ya kujionyesha na kuonekana ni kubwa sana kiasi kwamba kuukana mwili na kutenda ukweli kumekuwa kugumu sana? Nilisoma haya katika maneno ya Mungu: “Kila unachopenda, kile unachozingatia, kile unachoabudu, kile unachohusudu, na kile unachofikiria ndani ya moyo wako kila siku vyote ni viwakilishi vya asili yako. Inatosha kuthibitisha kwamba asili yako inapenda udhalimu, na katika hali mbaya, asili yako ni mbovu na isiyotibika. Unapaswa kuichambua asili yako kwa njia hii; yaani, chunguza kile unachopenda na kile unachoacha katika maisha yako. Unaweza kuwa mzuri kwa mtu fulani kwa muda, lakini hili halithibitishi kwamba unampenda. Kile unachopenda sana kweli ndicho hasa kilicho katika asili yako; hata kama mifupa yako ingekuwa imevunjwa, bado ungekifurahia na hungeweza kukiacha. Hili si rahisi kubadilisha(“Unachopaswa Kujua Kuhusu Kuigeuza Tabia Yako” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). “Kuongezea kwa kufukua vitu ambavyo watu huvipenda sana ndani ya asili zao, vipengele vingine vinavyohusiana na asili zao vinahitaji kufukuliwa pia, Kwa mfano, mitazamo ya watu kuhusu vitu, mbinu na malengo ya watu katika maisha, maadili ya maisha na mitazamo kuhusu maisha ya watu, pamoja na mitazamo kuhusu vitu vyote vinavyohusiana na ukweli. Hivi ni vitu vyote vilivyo ndani kabisa ya nafsi za watu na vina uhusiano wa moja kwa moja na mgeuzo wa tabia(“Unachopaswa Kujua Kuhusu Kuigeuza Tabia Yako” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Maneno ya Mungu yalinisaidia nielewe kwamba mawazo, mapendeleo, na ufuatiliaji wa kibinadamu vyote hutoka katika asili yetu, na vinadhibitiwa na asili yetu pia. Kisha nilijiuliza, Je, nilikuwa nimelenga na kutafuta nini hasa wakati huo wote katika wajibu wangu? Nafasi yangu jukwaani ilipozidi kusongeshwa mbele na nilikuwa katika picha zaidi na zaidi, nilichofikiria zaidi kilikuwa nafasi ya kuwa mbele hatimaye, kujionyesha, na kupata husuda na heshima kutoka kwa wengine. Hasa kwa onyesho la mwisho nilipowekwa mbele, nilihisi kama kwamba nilikuwa mtu fulani mashuhuri. Nilihisi kuwa nimefanikiwa sana kiasi kwamba sikuweza kudhibiti hamu yangu ya kujionyesha, kuonyesha uso wangu bora zaidi kwa kamera, kuwashangaza ndugu walionijua, na kujipa kumbukumbu nzuri ambayo ingedumu milele. Niliona jinsi nilivyothamini sana sifa na hadhi, na kwamba ilikuwa imejikita sana moyoni mwangu, ikawa asili yangu mwenyewe. Baadaye, nilisoma haya katika maneno ya Mungu: “Tabia potovu ya kishetani imekita mizizi kabisa ndani ya watu; inageuka kuwa maisha yao. Je, ni nini hasa ambacho watu hutafuta na wanachotamani kupata? Huku wakidhibitiwa na tabia potovu ya kishetani, maadili, matumaini, matarajio, na malengo na mielekeo ya maisha ya watu ni yapi? Je, haviendi kinyume na mambo chanya? Kwanza, watu daima hutaka kuwa na sifa au kuwa watu mashuhuri; wanataka kupata umaarufu mkubwa na ufahari, na kuwaletea mababu zao heshima. Je, haya ni mambo chanya? Haya hayalingani hata kidogo na mambo chanya; zaidi ya hayo, yanapingana na sheria ya Mungu ya kutawala majaliwa ya wanadamu. Kwa nini niseme hivyo? Je, Mungu anamtaka mtu wa aina gani? Je, Anamtaka mtu mwenye ukuu, mtu mashuhuri, mtu mwenye cheo kikufu, au mtu muhimu sana? (La.) Kwa hivyo basi, Mungu anamtaka mtu wa aina gani? Anamtaka mtu aliye thabiti ambaye anatafuta kuwa kiumbe wa Mungu anayestahili, anayeweza kutimiza wajibu wa kiumbe, na anayeweza kusalia katika nafasi ya binadamu(“Ni Kutafuta Ukweli na Kumtegemea Mungu Pekee Ndiko Kunakoweza Kutatua Tabia Potovu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). “Wewe daima unatafuta ukuu, hadhi na heshima; wewe hutafuta kuinuliwa daima. Je, Mungu anahisije Anapoona hili? Analichukia, na hataki kuliangalia. Kadiri unavyozidi kufuatilia mambo kama ukuu; hadhi; na kuwa mkubwa kuliko wengine, mwenye kuheshimiwa, uliyejipambanua, na mwenye kutambulika, ndivyo ambavyo Mungu anachukizwa na wewe zaidi. Usiwe mtu ambaye Mungu anachukizwa na yeye! Kwa hivyo, hili linaweza kutimizwaje? Kwa kufanya vitu kwa njia ya unyenyekevu ukiwa umesimama katika nafasi ya mwanadamu. Usifikirie ndoto za bure, usitafute umaarufu au kujitokeza kwa wenzako, na zaidi ya hayo, usijaribu kuwa mtu mwenye ukuu anayewazidi wengine wote, ambaye ni mkuu kati ya wanadamu na huwafanya wengine wamwabudu. Hiyo ndiyo njia ambayo Shetani huitembea; Mungu hawataki viumbe kama hao. Mwishowe, kazi yote ya Mungu itakapokuwa imekamilika, iwapo bado kutakuwa na watu wanaofuatilia mambo haya, basi kuna tokeo moja tu kwao: kuondolewa(“Utimizaji Sahihi wa Wajibu Unahitaji Ushirikiano wa Upatanifu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Maneno ya Mungu kweli yalikuwa mwito wa kunigutusha. Nilitafakari kuhusu kwa nini nilipenda sana kujionyesha, kwa nini nilikuwa batili sana. Yote yalitokana na kuelimishwa na kupotoshwa na Shetani. Sumu zake kama vile na “Mtu hujitahidi kwenda juu; maji hububujika kwenda chini” zilikuwa zimeniingia sana, zikinipa mtazamo mbaya juu ya maisha. Niliona kutafuta sifa na hadhi na kuishi bora kuliko wengine kama vitu chanya. Nilivichukua kama malengo ya maisha. Haijalishi nilichokuwa nikifanya nilitaka kujionyesha, kuwataka wengine wananiheshimu na kunihusudu. Nilihisi kwamba huko kungekuwa kuishi vyema kuliko wengine, kwamba lingekuwa jambo la kuheshimiwa. Upendo huo wa sifa na hadhi ulikuwa umegeuka kuwa asili yangu mwenyewe. Nilifikiria jinsi ambavyo nilitamani zamani kufaulu nikiwa shuleni na katika miingiliano na wengine. Nilitaka kuwa mbele ya wengine, nilitaka kuangaziwa. Wakati wowote ambapo mtu alianza kunitambua nilifurahi sana. Wakati sikutambuliwa au sikuwa muhimu katika kikundi chochote cha watu, sikuweza kulivumilia hilo. Nilitaka kupigania nafasi, na kushindwa katika hilo kulikuwa kunasikitisha. Siku zote nilikuwa naishi kulingana na sumu hizi za kishetani, kila mara nikiwataka wengine waniheshimu. Vitu hivi vilikuwa kama minyororo iliyonifunga, ikiyadhibiti mawazo yangu, ikinifanya nione kwamba kuwa katika filamu ya kumshuhudia Mungu ni kama jukwaa langu binafsi la kujionyesha. Nilikuwa nikiuchukulia wajibu wangu kama ubao wa kuchupia kuridhisha matamanio yangu mwenyewe. Kila kilichokuwa moyoni mwangu kilikuwa tu jinsi ya kujionyesha, jinsi ya kung’aa zaidi. Sikufikiria jinsi ya kutekeleza wajibu wangu vizuri au kumridhisha Mungu. Niliona kwamba sumu na tabia zangu za kishetani zikisalia bila kutatuliwa, haingekuwa tu vigumu kwangu kutekeleza wajibu wangu vizuri na kumridhisha Mungu, lakini pia mwishowe ningeondolewa na Mungu kwa sababu nilimwasi na nikampinga.

Baadaye nilisoma hili katika maneno ya Mungu: “Kile ambacho Mungu anataka kutoka kwa watu sio uwezo wa kukamilisha kiwango fulani cha kazi au kukamilisha shughuli zozote kubwa, wala Yeye hawahitaji waanzishe shughuli zozote kubwa. Kile ambacho Mungu anataka ni watu waweze kufanya yote wawezayo kwa njia ya unyenyekevu, na waishi kulingana na maneno Yake. Mungu hakuhitaji uwe mkuu au mwenye kuheshimiwa, wala Hakuhitaji usababishe miujiza yoyote, wala Hataki kuona mambo mazuri yanayoshangaza kutoka kwako. Hahitaji vitu kama hivyo. Yote ambayo Mungu anahitaji ni wewe usikilize maneno Yake na baada ya kuyasikia, uyaweke moyoni mwako na uyatii unapotenda kwa njia ya unyenyekevu, ili maneno ya Mungu yaweze kuwa kile unachoishi kwa kudhihirisha, na yawe uzima wako. Hivyo, Mungu ataridhika(“Utimizaji Sahihi wa Wajibu Unahitaji Ushirikiano wa Upatanifu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Niliona kwamba mapenzi ya Mungu ni kwamba sisi tufuatilie ukweli na tuwe watu waaminifu kabisa, tutii utawala na mipango Yake, na kujitolea kikamilifu katika wajibu wetu. Kujitahidi kufikia malengo haya kutamridhisha Yeye. Sikuwahi kuelewa mapenzi ya Mungu hapo awali, lakini nilifuatilia tu sifa na hadhi kwa moyo wote. Kwa sababu hiyo, sikuweza kufanya wajibu wangu vizuri, jambo lililomsikitisha Mungu. Nilikuwa mpotovu sana, lakini bado Hakuniacha. Mara kwa mara, Alifichua mitazamo yangu isiyo sahihi juu ya ufuatiliaji kwa kurekebisha nafasi yangu kwenye jukwaa ili niweze kuona tabia yangu potovu ya kishetani, nigeuke kutoka katika mwelekeo wangu, na nibadilike. Upendo wa Mungu kweli ulinitia moyo. Nilimwomba sala hii: “Mungu, sitaki kutafuta kuonekana au kuheshimiwa tena. Ufuatiliaji huo huniletea tu uchungu na hunifanya nisiweze kukuridhisha katika wajibu wangu, ukiniacha nikiwa mwenye hatia sana. Kuanzia sasa kuendelea natamani tu kutenda kulingana na maneno Yako. Haijalishi nina nafasi gani, ikiwa naweza kujionyesha au la, ninachotaka tu ni kuimba ili nikusifu Wewe kwa moyo wa kweli wenye utiifu Kwako, kufanya wajibu wangu ili nikuridhishe.” Tulipochukua picha upya baada ya hapo, wakati mwingine nilisongeshwa nyuma, wakati mwingine nilisongeshwa mbele, na wakati mwingine nilihitajika katika mazoezi lakini sio kwa sababu ya upigaji picha za sinema. Hili liliniathiri kihisia, lakini niliweza kuacha matamanio yangu mwenyewe kwa kumwomba Mungu na kusoma maneno Yake ili kusimamia mawazo yangu. Wakati mwingine niliwaona akina dada wengine wakiathiriwa kwa kubadilishwa nafasi zao na hawakuwa wanafanya vizuri katika wajibu wao. Niliweza kupata baadhi ya maneno husika ya Mungu kwa wakati mzuri na kuunganisha hayo na uzoefu wangu mwenyewe ili niwasaidie. Kufanya wajibu wangu kwa njia hiyo kweli kulinituliza na kulizaa matunda sana! Baadaye, mwelekezi aliniambia niende kwenye safu ya mbele tena, lakini sikuwa najaribu kujionyesha kama awali. Nilihisi tu kwamba kamera kunilenga lilikuwa jukumu, kwamba ulikuwa ushahidi. Nililenga kuimba vizuri na kutekeleza wajibu wangu kama nilivyopaswa. Nakumbuka katika onyesho moja wakati nilikuwa nyuma kabisa, tuliimba wimbo huu kutoka katika maneno ya Mungu: “Inua bendera yako ya ushindi umsherehekee Mungu! Imba wimbo wako wa ushindi ili ulieneze jina takatifu la Mungu!” Nilifikiria kuhusu jinsi ambavyo nilikuwa nimepotoshwa sana na Shetani, nikitafuta sifa na hadhi, kwamba nilikuwa nimeshindwa kufanya wajibu wangu vizuri kumridhisha Mungu, jinsi ambavyo nilikuwa nimemuumiza sana. Siku hiyo, nilihisi kwamba nilipaswa kumsifu Mungu kwa dhati, nimtolee wimbo wangu bora ili Shetani aaibike na ashindwe! Nilipokuwa nikiimba kumsifu Mungu jukwaani nikiwa na mtazamo wa aina hiyo, nilihisi amani na raha ambayo sikuwa nimewahi kuhisi hapo awali. Pia nilihisi hali ya fahari na haki sana!

Wimbo wa Ufalme, kazi kubwa ya kwaya, ilikuwa mtandaoni kabla ya muda mrefu. Sote, ndugu, tuliitazama video hiyo kwa furaha. Kuwaona wateule wengi sana wa Mungu wakiwa wamesimama mbele ya Mlima wa Mizeituni wakiimba kwa fahari “Umati unamshangilia Mungu, umati unamsifu Mungu,” kulinishtua sana, na niliguswa sana kiasi kwamba singeweza kujizuia kulia machozi ya shukrani. Ninapokumbuka kila kitu kilichotokea, kuanzia na kuathiriwa sana na nafasi yangu mwanzoni kiasi kwamba sikuweza kufanya wajibu wangu kwa dhati, mpaka hatimaye kuweza kutoathiriwa na sifa na hadhi iwe nafasi yangu ilikuwa mbele au nyuma, lakini kuchukua tu nafasi ya kiumbe aliyeumbwa, kuimba kwa uhuru na kumshuhudia Mungu, hayo yote yalikuwa matunda ya kazi ya Mungu ndani yangu.

Iliyotangulia: Roho Yangu Yakombolewa

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Kuna Njia ya Kumaliza Kiburi

Xiaochen Jijini Zhengzhou, Mkoani Henan Kiburi ni dosari yangu ya mauti. Nilikuwa mara kwa mara nikifichua tabia yangu ya kiburi, kila...

Katikati ya Jaribu la Kifo

Na Xingdao, Korea ya Kusini Mwenyezi Mungu anasema, “Mungu amekuja kufanya kazi ulimwenguni ili kumwokoa mwanadamu aliyepotoka—hakuna uongo...

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp