Kuna Furaha Kubwa Katika Uaminifu

15/01/2018

Gan’en Mji wa Hefei, Mkoa wa Anhui

Katika maisha yangu, siku zote nimeongozwa na msemo, “Mtu hapaswi kuwa na moyo wa kuwadhuru wengine, lakini lazima awe macho ili asidhuriwe” katika uingiliano wa kijamii. Kamwe huwa siwaridhii wengine imani yangu kwa urahisi. Daima nimehisi kuwa katika hali ambapo hujui nia za kweli ya mtu, hupaswi kuonyesha nia yako punde sana. Kwa hiyo, inatosha kuweka mtazamo wa amani—kwa njia hii unajilinda na utafikiriwa na wenzako wa rika kama “mtu mzuri.”

Hata baada ya mimi kuikubali kazi ya Mungu katika siku za mwisho, nilishikilia kanuni hii katika kushughulikia kwangu wengine. Nilipoona kwamba Mungu huuliza kwamba tusiwe na hatia, tuwe wazi na waaminifu, nilikuwa wazi tu juu ya mambo madogo ambayo hayakuwa na manufaa binafsi kwangu. Karibu ningekosa kamwe kushiriki vipengele hivyo vya tabia yangu ambayo niliona ikiwa potovu kwa hakika, kwa hofu kwamba ndugu zangu wa kiume na wa kike wangeniangalia kwa dharau. Wakati kiongozi wangu alinibagua kwa ajili ya kufanya kazi yangu kwa njia isiyo ya dhati, nilikuwa nimejaa mashaka na tuhuma na nikafikiria mwenyewe, “Kwa nini kiongozi wangu daima hunibagua na kutoa maelezo marefu ya hali yangu mbele ya ndugu zangu wote wa kiume na wa kike? Je, si ni dhahiri kwamba hili litanifanya kupoteza heshima na kunitahayarisha mbele ya kila mtu? Labda kiongozi wangu hanipendi sana, kwa hiyo ameamua kunionea.” Lilikuwa jambo la kuumiza hasa na lisilovumilika kuona ndugu wengine wa kiume na wa kike wakipandishwa vyeo wakati nilibaki katika cheo kile kile. Nilidhani kwamba sikuwa nikipandishwa cheo kwa sababu sikuwa na thamani ya kufundishwa. Moyo wangu ulijaa suitafahamu na mashaka; nilihisi sikuwa na mustakabali, kwamba hapakuwa na maana katika kuendelea kwa njia hii. Kwa sababu siku zote nilikuwa nikijihadhari na mwenye shaka kuhusu wengine, zaidi na zaidi nilimwelewa Mungu visivyo na nilihisi kuwa kuunganika na Yeye kulipungua zaidi na zaidi. Hali yangu iliendelea kuwa hasi zaidi na zaidi na hatimaye nilipoteza mawasiliano na kazi ya Roho Mtakatifu na kutumbukia katika giza.

Katika lindi la mateso, nikiwa nimepotea na bila mwelekeo, nilipata kifungu hiki cha neno la Mungu: “Kama una udanganyifu mwingi, basi utakuwa na moyo wenye hadhari na mawazo ya shaka juu ya mambo yote na wanadamu wote. Kwa sababu hii, imani yako Kwangu inajengwa kwa msingi wa shaka. Imani kama hii ni moja ambayo kamwe Sitaitambua. Bila imani ya kweli, basi utakuwa mbali hata zaidi na upendo wa kweli. Na ikiwa unaweza kumshuku Mungu na kumkisia utakavyo, basi wewe bila shaka ni mdanganyifu zaidi kati ya wanadamu wengine(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani). Nilipokuwa nikilifikiria neno la Mungu, mara moja nilitafakari juu ya matendo yangu mwenyewe katika maisha ya kila siku. Kwa mshtuko, niliwaza: “Si nilikuwa nikiishi na ‘moyo wenye hadhari na mawazo ya shaka juu ya mambo yote na wanadamu wote’?” Hasa, si nilikuwa mtu mwenye hila machoni pa Mungu? Wakati huo, maneno “mtu wa hila” yalikata moyo wangu kama ubapa wenye makali, na kunisababishia maumivu yasiyovumilika. Daima nilikuwa nimefikiri kwamba mradi nilivyozingatia kanuni “Mtu hapaswi kuwa na moyo wa kuwadhuru wengine, lakini lazima awe macho ili asidhuriwe,” ningeonekana kuwa mtu mzuri na wenzangu wa rika, kwa hiyo nilikuwa nimeishi kwa maneno hayo katika kushughulika kwangu na watu wengine na katika kufanya biashara. Kamwe, katika miaka yangu yote, sikushuku kuwa kuishi kwa kanuni hii kungenigeuza kuwa mtu wa hila. Hii ilimaanisha kuwa “Mtu hapaswi kuwa na moyo wa kuwadhuru wengine, lakini lazima awe macho ili asidhuriwe,” kanuni ambayo niliunga mkono kwa muda mrefu, haikupatana na ukweli na ilikuwa katika ukinzani wa moja kwa moja na neno la Mungu. Nilishtuka kujua falsafa hii ya maisha ambayo nilikuwa nimeunga mkono kwa muda mrefu kama kadiri nilivyoweza kukumbuka ilikuwa imeshushwa na kukanwa na maneno ya Mungu yamkini kwa ghafla sana. Hata hivyo, vitu vikiwa kama vilivyokuwa, sikuwa na chaguo bali kukubali ukweli. Nilijituliza, nikawaza kiasi na kutathmini tena kanuni hii niliyokuwa nimeunga mkono kwa muda mrefu. Baada ya muda, kwa sababu ya kunurishwa na Mungu, hatimaye nilipata ufahamu mpya na utambuzi katika msemo huo. Kijuujuu, “Mtu hapaswi kuwa na moyo wa kuwadhuru wengine, lakini lazima awe macho ili asidhuriwe” linaonekana kuwa wazo la busara wa kutosha na linalokubaliana na dhana za watu wengi juu ya lililo sawa na lisilo sawa. Hakuonekani kuwa na kitu chochote kisicho sawa mwanzoni, kwa sababu linasema tu kwamba tunapaswa kujihadhari dhidi ya wengine, lakini halipangi kufanya madhara kwa wengine. Zaidi ya hayo, kuishi kwa kanuni hii kunatuzuia kuanguka katika mitego na wakati huo huo kukituwezesha kujifunza jinsi ya kuwa watu wema. Hata hivyo, tunapouchunguza msemo huu kikamilifu, inakuwa dhahiri kuwa huu ni utaratibu muovu hasa ambao Shetani hutumia kuwapotosha wanadamu. Msemo huu unatuambia kwa siri kwamba huwezi kumwamini mtu yeyote, kwamba mtu yeyote anaweza kukudhuru, hivyo katika shughuli zako na wengine, usiingilie kabisa kamwe. Kwa njia hii, ninajihadhari dhidi yako, unakuwa mwenye shaka nami na kwa kweli sote wawili hatuaminiani. Hili hutuongoza kwa njia ya suitafahamu, uadui, na kupanga njama, ambayo husababisha wanadamu kuwa wapotovu zaidi na zaidi, wadanganyifu, wenye hila na walaghai. Hata vibaya zaidi, usemi huu wa Shetani hutufanya tujihadhari, kuwa wenye shaka na wasioamini katika kukutana na Mungu wetu mwenye upendo na mwenye huruma. Tunaanza kufikiri kwamba Mungu, pia, ni mdanganyifu, mwenye hila na aliyejaa vitimbi—kwamba Mungu hafanyi kazi kwa manufaa yetu. Matokeo yake, bila kujali ni kiasi gani Mungu anatupenda na kutufikiria, hatutaki kuweka imani yetu Kwake, na ni vigumu sana kwetu kuthamini ni jitihada gani Yeye hufanya kwa ajili yetu. Badala yake, sisi hushuku kwa moyo wa hila kila kitu Anachofanya, na kughilibu suitafahamu zetu, mashaka, kutokuwa waaminifu na upinzani Kwake. Kwa njia hii, Shetani hutimiza lengo lake la kuwapotosha na kuwalisha sumu binadamu na kutufanya tugeuke nyuma au kumsaliti Mungu. Hata hivyo, nilikosa utambuzi na nilikosa kuelewa njama mbovu ya Shetani. Niliuchukua udanganyifu wake kuwa falsafa dhabiti ya maisha ya kuheshimiwa na kutetewa na hatimaye nikawa mwenye hila zaidi na zaidi, mwenye shaka na wa kujihadhari. Badala ya kusimama kwa upande wa Mungu, na kujongelea mambo kutoka kwa mtazamo mzuri, hali yoyote niliyokutana nayo, siku zote nilitumia mawazo yangu yenye udanganyifu. Nilimwelewa Mungu visivyo na kushuku nia Yake. Hatimaye, suitafahamu yangu kwa Mungu ilipokuwa dhahiri zaidi na zaidi, nilipoteza mawasiliano na kazi ya Roho Mtakatifu na kutumbukia katika giza. Kama ilivyo wazi sasa, msemo, “Mtu hapaswi kuwa na moyo wa kuwadhuru wengine, lakini lazima awe macho ili asidhuriwe” si zaidi ya udanganyifu uliobuniwa na Shetani kuwapotosha na kuwanasa wanaadamu. Kuishi kwa hiki kinachojulikana kama kanuni kutawaongoza watu kuwa wenye hila na walaghai zaidi, na kushuku bila haki na kujihadhari dhidi ya wengine wakati wote wakiwa na suitafahamu na kugeuka mbali na Mungu. Maisha yaliyoongozwa hivyo yatapata tu karaha ya Mungu na kumwongoza mtu kupoteza mawasiliano na kazi ya Roho Mtakatifu na kutumbukia gizani. Mwishowe, wafuasi wa kanuni hii watakuwa waathirika wa udanganyifu wao wenyewe—mustakabali wao mchangamfu ukizimwa. Wakati huu, hatimaye nilitambua kwamba msemo, “Mtu hapaswi kuwa na moyo wa kuwadhuru wengine, lakini lazima awe macho ili asidhuriwe” haukuwa falsafa halali ya maisha, lakini badala yake ilikuwa njama katili iliyopangwa na Shetani ili kuwahadaa na kuwatesa wanadamu. Msemo huu ulikuwa na uwezo wa kuwapotosha wanadamu, ukiwafanya kupoteza ubinadamu wao na kumpotea au kumsaliti Mungu. Kuishi kulingana na msemo huu kungemwongoza tu mtu kumpinga Mungu na hivyo achukiwe na kuchujwa na Mungu.

Baadaye, niliona kifungu kinachofuata cha neno la Mungu: “Mungu ana kiini cha uaminifu, na kwa hivyo neno Lake siku zote linaweza kuaminika. Aidha, matendo Yake hayana dosari wala hayajadiliwi. Hii ndiyo maana Mungu anawapenda wale walio waaminifu kabisa Kwake. Uaminifu unamaanisha kumpa Mungu moyo wako; kutomdanganya katu katika kitu chochote; kuwa wazi Kwake katika mambo yote, kutowahi kuficha ukweli; kutowahi kufanya kile kinachowadanganya wale walio juu na kuwafumba macho wale walio chini; na kutowahi kufanya kile ambacho kinakupendekeza kwa Mungu. Kwa ufupi, kuwa waaminifu ni kujizuia dhidi ya uchafu katika matendo na maneno yenu, na kutomdanganya Mungu wala binadamu. … Kama wewe una siri nyingi usizotaka kutoa, na kama huko radhi kabisa kuweka wazi siri zako—yaani, ugumu wako—kwa wengine ili uweze kutafuta njia ya mwangaza, basi Ninasema kwamba wewe ni mmoja ambaye hatapokea wokovu kwa urahisi na ambaye hataweza kuibuka kutoka gizani kwa urahisi. Kama kutafuta njia ya ukweli kunakufurahisha vyema, basi wewe ni yule anayeishi kila mara katika mwangaza. Kama wewe unafurahia kuwa mtoa huduma katika nyumba ya Mungu, ukifanya kazi kwa bidii na kwa makini bila kuonekana, siku zote ukitoa na katu hupokei, basi Nasema kwamba wewe ni mtakatifu mwaminifu, kwani hutafuti tuzo na unakuwa tu binadamu mwaminifu. Kama uko radhi kuwa wazi, kama uko radhi kutoa kila kitu ulichonacho, kama una uwezo wa kujitolea maisha yako kwa ajili ya Mungu na kuwa shahidi, kama wewe ni mwaminifu hadi kwa kiwango ambapo unajua tu kumridhisha Mungu na si kujifikiria au kuchukua chochote kwa ajili yako, basi Nasema kwamba watu kama hao ndio wanaostawishwa na mwangaza na wataishi milele katika ufalme(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maonyo Matatu). Kutoka kwa neno la Mungu nilikuja kutambua, Mungu huwapenda na kuwabariki watu waaminifu. Ni kwa kuwa mwaminifu tu ndio mtu anaweza kuishi kwa njia sahihi, kwa upatanifu na nia ya Mungu. Hivyo, ni watu waaminifu pekee wanaohitimu kuupokea wokovu wa Mungu. Pia nilikuja kuelewa jinsi ya kutenda kama mtu mwaminifu: Watu waaminifu husema kwa kawaida, waziwazi na bila udanganyifu—husema waziwazi. Watu waaminifu kamwe hawawadanganyi wengine, hawafanyi kazi kwa uzembe na kamwe hawamdanganyi au kusema uongo kwa Mungu. Moyo wa mtu mwaminifu ni mwaminifu na bila udanganyifu au upotovu. Katika kuzungumza na kutenda haweki kusudi au nia zilizojificha, hatendi kwa faida yake mwenyewe au kuridhisha mwili wake, lakini badala yake zaidi kwa kusudi la kuwa mtu wa kweli. Moyo wa mtu mwaminifu ni mkarimu, roho yake ni aminifu, na yuko radhi kutoa moyo na maisha yake kwa Mungu. Haulizi chochote kama malipo, lakini hujitahidi tu kutimiza matakwa ya Mungu. Ni wale tu wenye sifa hizi wanaoweza kuitwa watu waaminifu, watu wanaoishi katika mwanga.

Mara nilipoelewa kanuni zinazohusiana na kuwa mtu mwaminifu, nilianza kujaribu kuweka kanuni hizo katika vitendo. Katika kushughulika kwangu na watu wengine, kwa utambuzi nilijaribu kutokuwa mwenye hila, au kukosoa bila mpango na kuwa na tahadhari. Nilipofanikiwa, nilijihisi huru hasa na aliyekombolewa; lilionekana jambo la kuburudisha zaidi kuishi hivi. Nilipodhihirisha upotovu wakati ninapokuwa nikitimiza wajibu wangu, kwa kuamili ningemtafuta mwenzangu dada ili kufunua ufahamu wangu mpya kujihusu katika ushirika na huyu dada angefanya vivyo hivyo. Wakati wa mchakato huu, sio tu kuwa hatukukuza chuki kuelekea kila mmoja wetu, lakini kwa kweli tulikuja kuwa wapatanifu hata zaidi katika uratibu wetu. Nilipodondoa neno la Mungu kwa kufunua upotovu wangu wakati wa mikutano, ndugu zangu wa kiume na wa kike hawakunidunisha kama nilivyofikiria kwanza, lakini badala yake walikuchukua maelezo yangu kama mfano wa wokovu wa Mungu wenye upendo. Wakati, katika kutimiza wajibu wangu, sikufanya kazi kwa sifa na hadhi zangu mwenyewe lakini kutimiza matakwa ya Mungu, nilihisi Roho Mtakatifu akifanya kazi kupitia kwangu na kunipa mwongozo, ili nipate kuona lengo la Mungu katika kutimiza wajibu wangu. Matokeo yake, nilikuwa na ufanisi sana katika kutimiza wajibu wangu. Katika sala, nilijaribu kwa utambuzi kushiriki mawazo yangu ya ndani na Mungu na kusema kutoka kwa roho. Niligundua kwamba nilipofanya hivyo, nilikua karibu zaidi na zaidi na Mungu na niliona kwamba Mungu ni mzuri sana. Kwa kawaida, suitafahamu zote za zamani nilizokuwa nazo na Mungu ziliisha katika mchakato huo. Kupitia kwa mchakato huu wa kutenda uaminifu, nilipitia jinsi kuwa mwaminifu kunamruhusu mtu kuishi katika mwanga na kupokea baraka za Mungu. Kuwa mtu mwaminifu kwa hakika ni kwa maana na kwa thamani!

Katika kupitia faida za kuwa mtu mwaminifu, nilikuwa hata wazi kwamba kanuni ya Shetani, “Mtu hapaswi kuwa na moyo wa kuwadhuru wengine, lakini lazima awe macho ili asidhuriwe” huwapotosha na kuwatesa wanadamu. Mtu akiunga mkono kanuni hii, ataishi daima katika giza, upotovu na mateso. Ni kwa kuwa tu mtu mwaminifu tunapoweza kuishi katika mwanga, kulishwa na kupokea sifa za Mungu. Kuanzia sasa kwendelea, nimeahidi kuanza upya na kuiacha kabisa kanuni hii ya Shetani, “Mtu hapaswi kuwa na moyo wa kuwadhuru wengine, lakini lazima awe macho ili asidhuriwe.” Kuanzia sasa, uaminifu utakuwa kiwango ambacho nitaishi kwacho na nitajitahidi kumpendeza Mungu kwa uaminifu wangu.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Masumbuko Makali ya Milele

“Roho zote ambazo zimepotoshwa na Shetani ziko chini ya udhibiti wa miliki ya Shetani. Ni wale tu wanaomwamini Kristo ndio waliotengwa...

Kuinuka licha ya kushindwa

Na Fenqi, Korea ya Kusini Kabla ya kumwamini Mungu, nilifundishwa na CCP, na sikufikiria chochote ila jinsi ya kufaulu kutokana na juhudi...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp