Kuripoti Au Kutoripoti

24/01/2021

Na Yang Yi, Uchina

Mwenyezi Mungu anasema, “Kwa minajili ya majaliwa yenu, mnastahili kutafuta kuidhinishwa na Mungu. Hii ni kusema kwamba, kwa sababu mnatambua kwamba nyinyi mmehesabiwa miongoni mwa wale walio katika nyumba ya Mungu, basi mnastahili kumletea Mungu utulivu wa akili katika mambo yote na kumtosheleza katika kila jambo. Kwa maneno mengine, lazima muwe wenye maadili katika matendo yenu na kutii ukweli katika mambo kama hayo. Kama hali hii inazidi uwezo wako, basi utachukiwa na kukataliwa na Mungu na vilevile kukataliwa kwa dharau na kila mwanadamu. Punde utakapokuwa katika hali mbaya kama hii, basi hauwezi kuhesabiwa miongoni mwa wale walio kwenye nyumba ya Mungu. Hii ndiyo maana ya kutoidhinishwa na Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maonyo Matatu). Mungu anataka kwamba tufanye vitu kulingana na kanuni, na kufuatana na ukweli. Ni jukumu letu pia kama waumini. Hatuwezi kupata kibali cha Mungu bila kufikia kiwango hiki. Hapo zamani, siku zote nilizuiliwa na tabia yangu potovu. Sikuzungumza au kutenda kwa maadili. Nilipowagundua viongozi au wafanyakazi waongo wa kanisa, sikuthubutu kuwafukuza au kuwaripoti na hili lilichelewesha kazi ya nyumba ya Mungu. Nilijifunza kupitia uzoefu jinsi ilivyo muhimu kufanya mambo kwa maadili.

Kiongozi wetu wa kanisa aliniweka kufanya wajibu wa kuandika katika msimu wa joto uliopita ili nimsaidie kiongozi wa timu kufanya kazi ya timu. Nilikuwa nimefukuzwa kutoka katika wajibu wangu wa awali miezi mitatu kabla ya hapo, kwa hivyo nilimshukuru Mungu kwa dhati kwa kunipa nafasi nyingine. Niliithamini sana nafasi hii na nilitaka kumtegemea Mungu katika kuifanya kazi hii. Nilielezewa juu ya kazi ya timu na kiongozi wa timu, na nikaona kwamba hawakuwa na watu wa kutosha kuhariri hati. Hili liliathiri sana maendeleo yao. Niliwapendekeza kina ndugu kadhaa ili tuweze kujadili ni nani aliyefaa kufanya wajibu upi. Lakini jibu lake lilikuwa, “Hakuna haraka. Acha tusiwe na haraka—wewe andika makala machache kwanza, kisha tutaona.” Kuona jinsi alivyokuwa mtepetevu kulinifanya niwe na wasiwasi. Hakukuwa na watu wa kutosha katika timu ambao walielewa ukweli na waliokuwa na ubora mzuri wa tabia, na hii tayari ilikuwa imeathiri kazi. Angewezaje kusema, “Tusiwe na haraka”? Je, huko hakukuwa kutowajibika? Nilihisi kwamba ilinilazimu nijadiliane naye kulihusu. Lakini kisha nikawaza, “Yeye ndiye anayesimamia. Amekuwa akifanya wajibu huu kwa muda mrefu kuliko mimi na anaelewa kanuni zaidi. Anapaswa kuwa na ufahamu mzuri wa jinsi ya kupanga mambo. Nilijiunga na timu hivi karibuni tu na kila kitu kipya ni kwangu. Nikizungumza sana, je, hatasema kuwa mimi nimevuka mpaka? Haidhuru. Nitangoja nione.”

Baada ya muda kidogo niligundua kwamba alikuwa mzembe sana kuhusu kuwafundisha washiriki wa timu na hakuwa mwenye maadili katika kuwapa watu kazi. Kina ndugu wengine wanaweza kuwa walikuwa wakifanya wajibu fulani, na bila kufikiri kuhusu hali ilivyo kwa jumla, au uwezo wa mtu binafsi, au alifaa kufanya wajibu upi, Aliwatuma katika timu nyingine bila msingi maalum. Hii iliathiri kazi ya nyumba ya Mungu na kuchelewesha maendeleo yetu. Nilimgusia kwamba mipango yake haikuwa na maadili na haikufaa, lakini aliendelea hata hivyo. Nilitaka kufanya ushirika na yeye kuchangua na kufichua asili ya kile alichokuwa akifanya. Lakini kisha niliwaza, “Mimi ni mgeni kwenye timu. Nikipendekeza mambo kila wakati, je,atasema kwa mimi ni mwenye kuwaamrisha wengine na sina mantiki?” Sikuthubutu kutaja jambo hilo tena.

Muda si muda, nilipokea barua kutoka kwa kiongozi mmoja wa kanisa akiniuliza ikiwa tulikuwa tumepata mtu yeyote wa kuhariri hati na kama mimi na kiongozi wa timu tulikuwa tukifanya kazi vizuri pamoja. Hili lilinitia wasiwasi kidogo. Sikujua jinsi ya kujibu. Kiongozi wa timu akigundua kwamba nilikuwa nimemwambia kiongozi wa kanisa kwamba yeye hakufanya kazi ya vitendo, tutawezaje kuendelea kufanya kazi pamoja? Aidha, sikujua kile ambacho wengine kwenye timu walimfikiria. Ikiwa maoni yangu hayakuwa yanayofaa, kiongozi wa kanisa angesema kwamba nilikuwa nikifuatilia mambo madogo madogo, kwamba nilikuwa na upendeleo? Lakini ikiwa singeongea, ningehisi kwamba sikuwa mwaminifu au sikulinda masilahi ya nyumba ya Mungu. Baada ya kuwaza kwa muda, niliamua kutafuta nijue wale wengine walifikiria nini kumhusu kwanza. Niliamua kuijibu barua hiyo baadaye.

Nilimwona Ndugu Yang katika mkutano. Alisema kwamba alikuwa katika timu kwa miezi kadhaa na kiongozi wa timu hakuwa mwenye kuwajibika sana. Hakufuatilia kujua kuhusu kazi au kufuatilia kwa wakati unaofaa, na hakuwaongoza kina ndugu au kuwasaidia kuingia katika kanuni. Kulikuwa pia hati fulani za dharura ambazo hakuwa amewapa watu wazishughulikie kwa wakati, na kweli alikuwa asiyejali kuhusu masuala ambayo watu wengine waliibua. Ndugu Yang pia alisema kwamba alimsikia akitoa ushirika katika mikutano kwa nadra sana kuhusu kutafakari na kujijua mwenyewe, na jinsi ya kutenda maneno ya Mungu alipokumbwa na shida, lakini alifoka tu baadhi ya mafundisho. Alikuwa mzungumzaji mzuri, lakini hakufanya kazi yoyote halisi hata kidogo. Nilijiwazia, “Inaonekana anaboronga tu bila kufanya kazi yoyote halisi. Hakubali ukweli au maoni kutoka kwa wengine. Je, huo si ufafanuzi wa kiongozi au mfanyakazi wa uwongo? Akiendelea kufanya wajibu huu, akiwajibikia kazi muhimu kama hiyo katika nyumba ya Mungu, hiyo inaweza kuiharibu kazi ya nyumba ya Mungu kweli.” Hili lilinifanya nigundue jinsi tatizo hilo lilivyokuwa kubwa na kwamba nilipaswa kumwambia kiongozi wa kanisa bila kuchelewa. Lakini kisha niliwaza, “Nikiripoti jambo hili na akose kubadilishwa, anaweza kufanya mambo yawe magumu kwangu au hata kuniachisha wajibu wangu. Nilikuwa nikifanya ibada na kujitafakari kwa miezi mitatu. Sijakuwa katika wajibu huu kwa muda mrefu. Nikifukuzwa, je, nitapata nafasi katika wajibu mwingine tena? Msemo wa zamani husema, ‘Msumari unaojitokeza hugongwa kwanza.’ Sipaswi kusema chochote. Nitasubiri hadi mtu mwingine atakapomripoti kisha nitaingilia mazungumzo hayo kuchangia. Hivyo sitakuwa nimejionyesha.”

Nilitaka tu kuboronga nikijifanya sioni kinchoendelea huku nikifanya wajibu wangu, lakini Mungu huona ndani ya mioyo yetu. Nilikuwa na hisia fulani ya wasiwasi njiani nikirudi nyumbani. Dhamiri yangu ilikuwa ikichomwa. Nilihisi kwamba ni Roho Mtakatifu aliyekuwa akinisukuma. Nilimwomba Mungu na kumuuliza Anitie nuru ili nijijue. Baada ya maombi yangu, nilikumbuka maneno haya ya Mungu: “Wote wamesema kwamba wangeweza kuudhukuru mzigo wa Mungu na kutetea ushuhuda wa kanisa. Ni nani ambaye kweli amefikiri kwa makini kuhusu mzigo wa Mungu? Jiulize: Je, wewe ni mtu ambaye ameonyesha nadhari kwa mzigo wa Mungu? Je, unaweza kutenda haki kwa ajili ya Mungu? Je, unaweza kusimama na kuzungumza kwa ajili Yangu? Je, unaweza bila kusita kuweka ukweli katika vitendo? Je, wewe ni jasiri vya kutosha kupambana dhidi ya matendo yote ya Shetani? Je, unaweza kuwa na uwezo wa kuweka hisia zako kando na kufichua Shetani kwa sababu ya ukweli Wangu? Je, unaweza kuyaruhusu mapenzi Yangu yatimizwe ndani yako? Je, umejitolea moyo wako wakati muhimu unapowadia? Je, wewe ni mtu ambaye hufanya mapenzi Yangu?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 13). Sikuwa na jibu kwa hili. Nilikasirika sana. Siku zote nilikuwa nikiongea kuhusu kuyadhukuru mapenzi ya Mungu na kuitetea kazi ya kanisa, lakini wakati kitu fulani kilitokea ambacho kilikiuka ukweli na kuliumiza nyumba ya Mungu, niliyatetea tu masilahi yangu mwenyewe. Nilijua kwamba kiongozi wa timu alikuwa hobelahobela katika wajibu wake na hakufanya kazi yoyote halisi, kwamba tayari ilikuwa imeathiri kazi ya kanisa na nilipaswa kumwambia kiongozi wa kanisa. Lakini nilijilinda tu, nikiogopa kwamba angelipiza kisasi kwangu au kwamba hata ningepoteza wajibu wangu. Nilirudi nyuma katika wakati muhimu, nikipuuza, nikijifanya kutojua kilichokuwa kikiendelea. Sikuwa nikiyatetea masilahi ya nyumba ya Mungu hata kidogo. Nilikuwa mbinafsi na mwenye kustahili dharau, bila ubinadamu au mantiki yoyote!

Nilipofika nyumbani, nilimwomba Mungu nikitafuta: “Ni kitu gani hasa kilichonifanya nisitende ukweli, na nisiitetee kazi ya kanisa?” Baadaye nilisoma kifungu hiki cha maneno ya Mungu: “Watu wengi hutamani kutafuta na kutenda ukweli, lakini wakati mwingi wao huwa tu na azimio na tamaa ya kufanya hivyo; hawana uzima wa ukweli ndani yao. Kama matokeo, wanapokumbana na nguvu za uovu au wanapokutana na watu waovu na wabaya wakifanya vitendo viovu, au viongozi wa uwongo na wapinga Kristo wakifanya vitu kwa namna inayokiuka kanuni—hivyo kuisababisha kazi ya nyumba ya Mungu kupata hasara, na kuwadhuru wateule wa Mungu—baadaye watu hukosa ujasiri wa kusimama na kuzungumza. Maana ya kukosa ujasiri nini? Je, inamaanisha kwamba wewe ni mwoga au huwezi kuzungumza kwa ufasaha? Au ni kwamba huelewi jambo hilo kabisa, na kwa hivyo huna ujasiri wa kuzungumza? Si lolote kati ya haya; ni kwamba unadhibitiwa na aina kadhaa za tabia potovu. Mojawapo ya tabia hizi ni ujanja. Unajifikiria kwanza, ukiwaza, ‘Nikizungumza, litanifaidi namna gani? Nikizungumza na nimchukize mtu, tutawezaje kuhusiana katika siku za usoni?’ Haya ni mawazo ya ujanja, siyo? Je, haya si matokeo ya tabia ya ujanja? ... Tabia yako potovu ya kishetani inakudhibiti; mdomo wako unasonga bila wewe kukusudia. Hata ikiwa unataka kunena maneno ya uaminifu, huwezi kuyanena na unaogopa kuyasema. Huwezi kutekeleza hata kimoja kati ya vitu elfu kumi ambavyo unapaswa kufanya, vitu ambavyo unapaswa kusema, na jukumu ambalo unapaswa kuchukua; mikono na miguu yako imefungwa na tabia yako ya kishetani. Huna udhibiti hata kidogo. Tabia yako potovu ya kishetani inakwambia jinsi ya kuzungumza na kwa hivyo wewe unazungumza hivyo; inakwambia kitu cha kufanya na kwa hivyo wewe unakifanya. … Wewe hutafuti ukweli, sembuse kutenda ukweli, ilhali unaendelea kuomba, ukiikuza dhamira yako, ukifanya maazimio, na kula viapo. Na matokeo ya haya yote ni nini? Wewe bado ni bwana ndiyo: ‘Sitamchokoza mtu yeyote, wala sitamkosea mtu yeyote. Ikiwa jambo halinihusu, basi nitakaa mbali nalo; siwezi kusema chochote juu ya mambo ambayo hayanihusu, na hili ni bila ubaguzi. Ikiwa kitu chochote ni chenye kuyadhuru masilahi yangu mwenyewe, fahari yangu, au kujiona kwangu, bado sitajali kwa vyovyote kukihusu, na nitakichukulia kwa uangalifu; Sipaswi kutenda kwa pupa. Msumari unaojitokeza hugongwa kwanza, na mimi si mpumbavu hivyo!’ Kikamilifu, wewe uko chini ya udhibiti wa tabia zako potovu za uovu, ujanja, ugumu, na kuchukia ukweli. Zinakubomoa, na zimekuwa ngumu sana kwako kuvumilia hata kuliko kile Kiduara cha Dhahabu ambacho Mfalme wa Nyani alivaa. Kuishi chini ya udhibiti wa tabia potovu ni jambo la kuchosha na chungu sana!(“Ni Wale tu Wanaotenda Ukweli Ndio Wacha Mungu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Maneno ya Mungu yalizifichua tabia zangu za kishetani za ujanja na mbovu. Nilipoibua ukosefu wa watu katika timu mara ya kwanza na kuona kwamba kiongozi wa timu hakujali kabisa na hakuwajibika, nilijua vizuri kabisa kwamba jambo hili litaiathiri kazi ya kanisa. Lakini sikuthubutu kusema zaidi, nikiogopa kwamba angesema nilikuwa nikivuka mipaka na angeanza kunichukia. Baadaye, niliona kwamba aliwabadilisha watu huku na kule bila maadili yoyote, kumwibia Petro amlipe Paulo na kuharibu kazi yetu. Bado nilitaja jambo hilo kwa nadra, lakini nililigusia tu kwa juu juu. Nilijua hakuna kilichotokana na hilo, lakini niliogopa kumshughulikia au kumfunua. Ndugu Yang aliponiambia zaidi kumhusu, sikuwa na shaka kwamba alikuwa hafanyi kazi ya vitendo na hakukubali ukweli, kwamba alikuwa kiongozi wa uwongo na nilipaswa kuripoti jambo hilo kwa kiongozi wa kanisa mara moja. Bado, nilihofu kwamba angeninyang’anya wajibu wangu, kwa hivyo nilikunja mkia na nikakimbia tena, ili kulinda tu cheo na matarajio yangu. Nilikuwa mbinafsi na mjanja! Kila wakati nilipoona mojawapo ya shida zake sikuthubutu kumfunua au kumwambia kiongozi yeyote wa kanisa. Kama matokeo, kazi ya nyumba ya Mungu ilivurugika. Nilikuwa nikiishi kwa kufuata sumu za kishetani kama “Kila mwamba ngoma huvutia upande wake,” “Msumari unaojitokeza hugongwa kwanza,” “Nguvu husababisha usahihi,” na “Ofisa wa kaunti hawezi kuwaamuru watu huku na kule kama vile wa mtaa awezavyo.” Mtazamo wangu ulikuwa wa kipuuzi sana, na nilianza kuwa mbinafsi na mjanja zaidi. Nilijichunga na kuwa mwangalifu katika kila kitu nilichofanya, nikiyalinda masilahi yangu mwenyewe kila mara, nikiogopa kuwajibikia shida yoyote iliyosababishwa. Sikuweza kuvumilia wazo la kutoweza kujieleza. Ilikuwa vigumu sana kwangu kutamka neno la kweli, kusema kile kilichokuwa kikiendelea kweli. Sikuwa na ujasiri wa kumripoti na kumfunua kiongozi wa uwongo. Nilikuwa nimefungwa na kudhibitiwa kabisa na hizi tabia na sumu za kishetani kimwili na kiakili. Sikuweza kusema ukweli, na sikuwa na haki hata kidogo. Ilikuwa njia ya woga sana ya kuishi. Niliona kweli jinsi sumu hizi za kishetani zilivyo za kipumbavu na nilipoishi kwa kuzifuata, kila kitu nilichofanya kilikwenda kinyume na ukweli na kilimpinga Mungu. Sikuwa na mfanano wowote wa binadamu.

Wakati huo tu, ulifika wakati wa kanisa kutoa mpangilio wake wa kazi. Tuliambiwa tena kwamba ikiwa waovu na wapinga Kristo wowote, au viongozi au wafanyakazi wowote wa uwongo ambao hawakufanya kazi ya vitendo walikuwa wamegunduliwa, walipaswa kuripotiwa ili kulinda masilahi ya nyumba ya Mungu. Hilo ni jukumu la kila mmoja wa watu wateule wa Mungu. Nilihisi vibaya sana wakati mahitaji haya kutoka kwa nyumba ya Mungu yaliwekwa mbele yangu. Nilikuwa najua vizuri kwamba tulikuwa na kiongozi wa uwongo katika timu yetu, lakini sikuwa nimethubutu kumripoti. Je, nilistahili vipi kuwa mmoja wa wateule wa Mungu? Nilitafuta maneno fulani ya Mungu yaliyohusiana na hali yangu na nikapata haya: “Je, ni mtazamo upi ambao watu wanapaswa kuwa nao katika suala la jinsi ya kumtendea kiongozi au mfanyakazi? Ikiwa kile anachofanya ni sawa, basi unaweza kumtii; ikiwa kile anachofanya ni kibaya, basi unaweza kumfunua, na hata kumpinga na kutoa maoni tofauti. Ikiwa hawezi kufanya kazi ya vitendo, na afichuliwe kuwa kiongozi wa uwongo, mfanyakazi wa uwongo au mpinga Kristo, basi unaweza kukataa kukubali uongozi wake na pia unaweza kumripoti na kumfunua. Hata hivyo, baadhi ya watu wateule wa Mungu hawaelewi ukweli na ni waoga hasa, na kwa hivyo hawathubutu kufanya chochote. Wao husema, ‘Kiongozi akinitimua, basi mimi nimeisha; akimfanya kila mtu anifunue au kunitelekeza, basi sitaweza tena kumwamini Mungu. Nikiondoka kanisani, basi Mungu hatanitaka na hataniokoa. Kanisa linamwakilisha Mungu!’ Je, njia hizi za kufikiri haziathiri mtazamo wa mtu kama huyo kuhusu vitu hivyo? Je, inaweza kuwa kweli kwamba kiongozi akikufukuza, huwezi tena kuokolewa? Je, suala la wokovu wako linategemea mtazamo wa kiongozi wako juu yako? Kwa nini watu wengi sana wana kiwango kama hicho cha hofu? Punde tu mtu ambaye ni kiongozi wa uwongo au mpinga Kristo anapokutishia, ikiwa huthubutu kuripoti jambo hili kwa walio juu na hata uhakikishe kwamba kuanzia wakati huo kuendela, utakuwa mwenye mawazo sawa na kiongozi, basi wewe hujaangamia? Je, huyu ni aina ya mtu anayetafuta ukweli? Si tu kwamba huthubutu kuifunua tabia mbovu kama inayoweza kutendwa na wapinga Kristo wa kishetani, lakini kinyume chake, unawatii na hata kuyachukua maneno yao kama ukweli, ambayo unayatii. Je, huu sio ujinga wa juu zaidi?(Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Kusoma maneno haya kutoka kwa Mungu kuliuangaza moyo wangu. Niliogopa kumripoti kiongozi wa timu hasa kwa sababu ya hofu yangu kwamba angefanya mambo yawe magumu kwangu ikiwa ningemkosea, au kwamba ningepoteza wajibu wangu. Ilikuwa ni kama kwamba nilidhani angeweza kuamua wajibu wangu au hatima yangu. Ilikuwa njia ya kipumbavu ya kulichukulia jambo hilo. Iwe ningefukuzwa kutoka kazini au hatima yangu ilikuwa ipi yote yalikuwa mikononi mwa Mungu. Hakuna mwanadamu aliyekuwa na kauli ya mwisho. Viongozi wa uwongo na wapinga Kristo hawawezi kudhibiti jambo hilo. Nyumba ya Mungu si kama ulimwengu. Hapa, ukweli na haki vinatawala. Viongozi wa uwongo na wapinga Kristo hawawezi kupata mahali pa usalama katika nyumba ya Mungu. Wanaweza kushikilia mamlaka kwa muda, lakini mwishowe, wote watafunuliwa na kuondolewa. Kanisa lilikuwa limewafukuza na kuwaondoa viongozi wengi kiasi wa uwongo na wapinga Kristo hapo zamani. Niliona hilo waziwazi kabisa, lakini wakati mmoja wa hao alipoonekana katika kikundi changu na nilipaswa kumripoti ili nilinde masilahi ya nyumba ya Mungu, nilirudi nyuma. Niliona afadhali kuwa mtumishi wa Shetani. Nilikuwa dhaifu na mwoga. Sikuelewa tabia ya haki ya Mungu, na kweli sikuona kwamba Yeye anatawala na Anaona kila kitu. Niliogopa kumkosea mwanadamu, lakini sikuogopa kumkosea Mungu. Huko kulikuwaje kuwa na nafasi ya Mungu moyoni mwangu?

Nilisoma kifungu kingine cha maneno ya Mungu baada ya hapo. “Ikiwa hakuna mtu yeyote kanisani aliye radhi kuutenda ukweli, hakuna yeyote anayeweza kuwa shahidi kwa Mungu, basi kanisa hilo linapasa kutengwa kabisa, miunganisho yao na makanisa mengine kukatizwa. Hili linaitwa ‘kuzika kifo’; hii ndiyo maana ya kumfukuza Shetani. Iwapo kanisa lina waonevu kadhaa wa hapo, na wanafuatwa na ‘nzi wadogo’ wasio na ufahamu kabisa, na ikiwa washiriki wa kanisa, hata baada ya kuona ukweli, bado hawawezi kukataa vifungo na kuchezewa na hawa waonevu—basi hawa wajinga wataondolewa mwishoni. Ingawa nzi hawa wadogo wanaweza kuwa hawajafanya lolote baya, wao ni wenye hila hata zaidi, wadanganyifu hata zaidi na wenye kukwepa hata zaidi na kila mtu aliye namna hii ataondolewa. Hakuna yeyote atakayeachwa! Wale walio wa Shetani watarudishwa kwa Shetani, ilhali wale walio wa Mungu hakika watakwenda kutafuta ukweli; hili linaamuliwa na asili zao. Acheni wale wote wanaomfuata Shetani waangamie! Hakuna huruma watakayoonyeshwa watu hawa. Acheni wale wanaofuata ukweli wapate utoaji na muwakubalie kufurahia neno la Mungu hadi mioyo yao itosheke. Mungu ni mwenye haki; Yeye hawatendei watu kwa udhalimu. Ikiwa wewe ni ibilisi basi hutakuwa na uwezo wa kuutenda ukweli. Ikiwa wewe ni mtu anayetafuta ukweli basi ni wazi kuwa hutatekwa nyara na Shetani—hili halina tashwishi yoyote(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Onyo kwa Wale Wasiotenda Ukweli). Niliposoma maneno Yake, niliweza kweli kuihisi tabia takatifu, adilifu, na isiyokosewa ya Mungu. Hatavumilia viongozi wa uwongo na wapinga Kristo kuvuruga kazi ya nyumba Yake na kuwaumiza wateule Wake. Pia Anawachukia wale wasiotenda ukweli, wasiolinda masilahi ya nyumba ya Mungu watu hao wanapoonekana. Wasipotubu, wote wataishia kuondolewa na kuadhibiwa pia. Nilifikiri kuhusu jinsi nilivyojua kwamba kiongozi wa timu alikuwa kiongozi wa uwongo, lakini sikutenda ukweli wala kuwa na ujasiri wa kumripoti. Yote yalikuwa kwa ajili ya masilahi yangu mwenyewe. Nilimsujudia Shetani muda baada ya muda, nikisimama upande wake, nikimdekeza na kumlinda kiongozi huyo wa uwongo huku kazi ya nyumba ya Mungu ikiathirika. Nilishiriki katika maovu ambayo alikuwa akifanya. Nilikuwa nikifurahia ukweli ambao Mungu hutoa na kula na kunywa kutoka kwenye meza Yake. Lakini katika wakati muhimu wakati ambapo Shetani alikuwa akifanya uharibifu kwa fujo katika nyumba ya Mungu, sikuweza kulinda masilahi ya nyumba ya Mungu. Badala yake, niliuuma mkono ulionilisha na nikampendelea adui. Huko kulikuwa kumsaliti Mungu, na jambo hilo liliikosea sana tabia Yake. Kufikiria maneno haya ya Mungu, “Acheni wale wote wanaomfuata Shetani waangamie!” kuliniacha nikiwa na hofu sana. Nilijua kwamba kama singetubu, bila shaka ningeondolewa na Mungu, pamoja na kiongozi huyo wa uwongo. Niliona asili na matokeo makubwa ya kukosa kumripoti kiongozi wa uwongo na nilijichukia kwa kuwa mbinafsi na mwenye kustahili dharau. Sikuwa nimelinda masilahi ya nyumba ya Mungu hata kidogo. Nilikosa ubinadamu kabisa. Kisha nilikuja mbele za Mungu katika maombi. “Ee Mungu, mimi ni mbinafsi na mjanja sana. Nilimwona kiongozi wa uwongo kanisani ambaye sikuwahi kumripoti au kumfunua. Nilimtetea na nikamuendekeza na nikawa kama mtumishi wa Shetani ili kulinda masilahi yangu mwenyewe. Ninapaswa kuadhibiwa. Mungu, kamwe sitafanya kitu kama hicho tena. Ningependa kutubu. Tafadhali nipe nguvu ili niweze kutenda ukweli, nimripoti na kumfunua kiongozi huyo wa uwongo na niitetee kazi ya kanisa.”

Nilisoma maneno haya kutoka kwa Mungu katika ibada zangu siku iliyofuata: “Wewe lazima ujifunze jinsi ya kuchangua mawazo na maoni yako. Vitu vyovyote unavyoweza kuwa ukifanya vibaya, na tabia zako zozote ambazo Mungu hawezi kupenda, unapaswa kuweza kuzibadilisha mara moja na kuzirekebisha. Kusudi la kuzirekebisha ni nini? Ni kukubali na kuchukua ukweli, huku ukikataa vitu vilivyo ndani yako ambavyo ni vya Shetani na kuvibadilisha na ukweli. Ulikuwa ukitegemea tabia zako potovu, kama ujanja na udanganyifu, lakini sasa huzitegemei; sasa, unapofanya mambo, wewe hutegemea mitazamo, hali, na tabia ambazo ni za kweli, safi, na zilizo wazi. … Punde ukweli unapokuwa maisha yako, mtu akimkufuru Mungu, akiwa hamchi Yeye, ni mzembe na anafanya tu mambo kwa njia isiyo ya dhati ili kutimiza wajibu wake, au huvuruga au kuisumbua kazi ya nyumba ya Mungu, basi punde unapoona hili, utaweza kulichukulia kulingana na kanuni za ukweli kwa kutambua kile kinachopaswa kutambuliwa na kufunua kile kinachopaswa kufunuliwa(“Ni Wale tu Wanaotenda Ukweli Ndio Wacha Mungu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Maneno ya Mungu yalinionyesha kwamba kipengele cha msingi cha imani ni kuwa na moyo mwaminifu, kutenda ukweli, kulinda masilahi ya nyumba ya Mungu, na kufanya vitu kwa kufuata kanuni. Hivyo ndivyo tunavyoweza kumletea Mungu furaha. Nilijua kwamba ilinilazimu nitende ukweli na nimripoti kiongozi wa timu yetu kulingana na kanuni. Na kwa hivyo, niliandika kila kitu alichokuwa amefanya, kwa usahihi na kwa utondoti, na nikaikabidhi kwa kiongozi wa kanisa. Baada ya kuhakiki kila kitu, kiongozi wa kanisa alithibitisha kwamba alikuwa akifanya wajibu wake kwa uzembe na hakuwa amefanya kazi yoyote halisi. Kwa kweli alikuwa kiongozi wa uwongo na alifukuzwa kutoka katika wajibu wake. Nilihisi amani nilipoarifiwa kuhusu hilo. Tukio hilo lilinionyesha jinsi Mungu ni mwenye haki, na kwamba katika nyumba Yake, Kristo anatawala na ukweli unatawala. Haijalishi cheo cha mtu ni cha juu vipi, madaraka yake ni makubwa vipi, lazima atii ukweli na maneno ya Mungu. Wale wasiotenda ukweli hawataweza kusimama imara katika nyumba ya Mungu. Wataondolewa mwishowe. Ni kuwa mtu mwaminifu, kutenda maneno ya Mungu na kufanya vitu kwa njia ya uadilifu pekee ndiko kunakolingana na mapenzi ya Mungu na hupata kibali Chake. Hicho ndicho nilichojifunza kutoka katika tukio langu la kumripoti mtu.

Iliyotangulia: Ukweli Umenionyesha Njia

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Jaribu la Uzao wa Moabu

Na Zhuanyi, Uchina Mwenyezi Mungu anasema, “Kazi yote ifanywayo siku hii ya leo ni ili mwanadamu afanywe msafi na kubadilika; kupitia...

Masumbuko Makali ya Milele

“Roho zote ambazo zimepotoshwa na Shetani ziko chini ya udhibiti wa miliki ya Shetani. Ni wale tu wanaomwamini Kristo ndio waliotengwa...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp