Maneno ya Mungu Yalinifanya Nijijue

05/11/2020

Maneno ya Mungu yanasema: “Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufichua kiini cha mwanadamu, na kuchangua maneno na matendo yake. Maneno haya yanajumuisha ukweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyofaa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na pia hekima na tabia ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yote yanalenga nafsi ya mwanadamu na tabia yake potovu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu humkataa Mungu kwa dharau yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu ya adui dhidi ya Mungu. … Kile ambacho kazi ya hukumu humletea mwanadamu ni ufahamu wa uso halisi wa Mungu na ukweli kuhusu uasi wake mwenyewe. Kazi ya hukumu humruhusu mwanadamu kupata ufahamu zaidi wa mapenzi ya Mungu, wa makusudi ya kazi ya Mungu, na wa mafumbo yasiyoweza kueleweka kwa mwanadamu. Pia inamruhusu mwanadamu kutambua na kujua asili yake potovu na asili ya upotovu wake, na pia kugundua ubaya wa mwanadamu. Matokeo haya yote huletwa na kazi ya hukumu kwa maana asili ya kazi ya aina hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli, njia, na uhai wa Mungu kwa wale wote walio na imani ndani Mwake(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli). Nikiwa nasoma maneno ya Mungu, naweza kuona kwamba kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho inafanywa kwa kuonyesha ukweli kutuhukumu na kututakasa, ili tuweze kujua asili zetu za kishetani kupitia maneno ya Mungu na kuona ukweli wa jinsi ambavyo tumepotoshwa sana na Shetani. Kisha tunaweza kuhisi majuto, kujichukia sisi wenyewe, na kutubu kwa kweli. Nilikuwa nikijiona daima kuwa mtu mwenye ubinadamu mzuri, kwamba nilikuwa mvumilivu na mstahimilivu kwa watu wengine, na nilipomwona mtu akipitia wakati mgumu, ningefanya chochote nilichoweza kusaidia. Nilidhani kwamba nilikuwa mtu mzuri. Lakini baada ya kuikubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho na kupitia hukumu na ufunuo wa maneno Yake, niliona kwamba hata ingawa nilionekana kutenda vyema kwa nje na sikutenda dhambi za wazi, ndani mwangu nilikuwa na tabia nyingi potovu—kiburi, udanganyifu, uovu. Sikuweza kujizuia kwenda kinyume cha ukweli na kumpinga Mungu. Niliona kwamba nilikuwa nimepotoshwa sana na Shetani na kwa kweli nilihitaji hukumu na utakaso wa maneno ya Mungu.

Nakumbuka mnamo Machi 2018 nilikuwa na wajibu wa kutengeneza video kanisani. Nilikuwa mgeni kwenye timu, na nilimsikia dada mmoja akisema kwamba Ndugu Zhao, kiongozi wa timu, alikuwa mkali sana na alikuwa na viwango vya shuruti vya kazi. Niliwaza, “Kuwa mkali ni kuwajibika na kunaweza kutusukuma tufanye wajibu wetu vyema zaidi. Hili ni jambo zuri.” “Aidha,” niliwaza, “mimi ni mtu anayepatana na wengine kwa urahisi na ninaweza kuelewana na mtu yeyote. Sidhani nitakuwa na shida yoyote nikifanya kazi na Ndugu Zhao.”

Ndugu Zhao alipakua video kadhaa ili tuzipite kutusaidia kufahamiana na kazi kwa haraka zaidi, tukipitia mambo kama mapambo, muundo wa picha, mwangaza, na uratibu wa rangi. Kujifunza juu ya yote haya kulinichosha kiasi na umakini wangu uliendelea kutangatanga. Niliwaza, “Kuna habari nyingi sana, nitaisahau baada ya mfupi tu. Nitaelewa polepole kupitia mazoezi. Kwa wakati huu itakuwa bora kujifunza kutengeneza video bora kwa kutumia programu mpya, kutusaidia kujifunza na kuongeza mvuto wetu.” Niliibua wazo langu, nikidhani kwamba Ndugu Zhao angelizingatia, lakini nilishangaa wakati alinisikiliza kisha akasema kwa ukali sana, “Kujifunza ustadi huu wa kitaalamu ni muhimu sana. Lazima tuuelewe ili tutengeneze video nzuri. Lazima tujifahamishe na tuende hatua kwa hatua. Tusichukue mzigo tusioweza kubeba. Kujifunza yote haya ni ili tufanye wajibu wetu vizuri. Kwa kurekebisha mawazo yetu, tutakuwa na motisha zaidi ya kujifunza na halitaonekana kuwa jambo la kuchosha.” Mara tu baada ya yeye kusema hivyo ndugu wengine waliniangalia. Uso wangu mzima na shingo langu viligeuka kuwa rangi nyekundu. Nilishikwa na aibu sana. Niliwaza, “Watafikiria nini kunihusu ukiniongelesha namna hiyo? Je, watafikiria kwamba mimi nazembea tu katika wajibu wangu? Nitawezaje kuonyesha uso wangu baada ya hili?” Lakini kisha nikawaza, “Sipaswi kuwa mwenye mawazo finyu sana. Ndugu Zhao anasema haya ili kutusaidia sisi. Je, nitawezaje kushirikiana katika wajibu huu ikiwa ninafuatilia mambo madogo madogo katika kila kitu?” Kuanzia wakati huo nilianza kujifunza ustadi huu kwa bidii na nikapata ufahamu wa kimsingi juu ya vipengele vingine haraka sana. Baada ya muda mfupi nilikuwa najisikia vizuri sana, nikidhani kuwa nilikuwa mwenye ubora mzuri wa tabia na ningeweza kujifunza vitu haraka.

Siku moja Ndugu Zhao alitufundisha jinsi ya kutumia programu mpya. Niliikumbuka mara moja, lakini ndugu wengine walilazimika kuipitia tena mara moja zaidi. Ndugu Zhao aliifundisha kwa uvumilivu mara mbili, lakini sikuwa mvumilivu. Niliwaza, “Ni nini kigumu sana? Nimeielewa, hakuna haja ya kurudia tena.” Nilianza kupekuapekua vitu vingine. Alipoona kwamba sikuwa nazingatia sana kazi iliyokuwa ikiendelea, Ndugu Zhao alisema, “Dada, tayari umeielewa hii? Njoo ujaribu kuifanya.” “Kuna nini hata cha kufanya?” Niliwaza. “Ni kwamba tu huniamini, sivyo?” Nilijaribu, nikiwa nimejiamini kabisa, lakini nilikwama nikiwa katikati tu. Sikujua la kufanya baada ya hapo. Ndugu wengine walikuwa tu pembeni wakitazama. Uso wangu ulianza kuwasha. Nilitamani sana nipate shimo nijifiche. Akiwa na sura kali usoni, Ndugu Zhao alisema, “Dada, wewe ni mwenye kiburi na majivuno sana, na kwa jumla hauko makini katika chochote unachojifunza. Unawezaje kufanya wajibu wako vizuri ukiwa hivyo?” Sikukubaliana hata kidogo na kile alichosema. “Wewe hunipendi tu, sivyo?” Niliwaza. “Humuulizi mtu mwingine yeyote, ni mimi tu. Sio kwa sababu unataka kunifanya nionekane mjinga? Na ulinikaripia mbele ya kila mtu; hiyo haikuwa kwa sababu ulitaka kumfanya kila mtu afikirie mimi ni mwenye kiburi? Nitawezaje kuelewana na kila mtu baada ya hili?” Kadiri nilifikiria zaidi juu ya hili, ndivyo nilivyohisi kwamba Ndugu Zhao alikuwa akitafuta ugomvi na mimi makusudi, kwamba alitaka tu kunifanya nionekane mbaya kwa kila namna. Bila kukusudia, nilianza kuhisi chuki dhidi yake. Kuanzia wakati huo kuendelea, nilianza tu kumuepa bila kujua kikamilifu. Aliponiuliza chochote juu ya wajibu wangu, nilimtambua kwa nadra sana, nikisema tu hili au lile. Niliogopa kwamba angenikaripia kama angegundua shida zozote nyingine katika kazi yangu. Lakini kadiri nilivyojaribu kumwepa, ndivyo nilivyokumbwa na shida zaidi na makosa zaidi. Nilikuwa nikipata ukumbusho na uelekezi kila mara kutoka kwake. Hii iliniacha nikiwa mwenye kukasirika sana, na niliyezidi kutokuwa na furaha na Ndugu Zhao. Niliwaza, “Wewe huniaibisha kila wakati. Wakati ujao nitakapoona dosari kwako nitaikosoa mbele ya kila mtu pia, ili uweze kuhisi ninavyohisi unaponifanyia hivi.”

Muda mfupi baadaye dada mwingine alijiunga na kikundi chetu. Nilimpa maelekezo ya kimsingi, na ilipofika kwa Ndugu Zhao, nilitoa maoni na chuki yangu yote kwa dada huyo. Nilihisi wasiwasi kidogo baada ya hapo, nikijiuliza kama nilikuwa nikimhukumu pasi na yeye kujua. Lakini kisha nililitazama jambo hilo kwa njia nyingine. Nilikuwa nikimpa maoni yangu ya kweli ili aweze kujua jambo fulani kumhusu na aweze kushughulikia uwezo na udhaifu wake ipasavyo. Sikufikiria chochote zaidi kuhusu hilo.

Haikuchukua muda mrefu kabla nisikie kwamba dada mmoja alikuwa amemwambia kiongozi fulani wa kanisa kuhusu baadhi ya matatizo ya Ndugu Zhao katika wajibu wake. Niliwaza, “Hii ni fursa nzuri kwangu kushiriki maoni yangu pia. Pengine kiongozi atamshughulikia Ndugu Zhao kulingana na kile tunachosema, kwa hivyo wakati huu atajua inavyohisi. Na labda baada ya kushughulikiwa hata pia ataondolewa kutoka katika wajibu wake, na hivyo sitalazimika kuonana naye tena siku baada ya siku.” Nikiwa na hili akilini, nilishiriki na kiongozi upotovu na makosa yake. Nilidhani kwamba angebadilishwa, lakini cha kushangaza ni kwamba siku chache baadaye kiongozi alipojumuisha tathmini za kila mtu, alisema kuwa Ndugu Zhao alifichua upotovu kiasi lakini pia alijitambua kiasi, na kwamba aliwajibikia kazi yake na aliweza kufanya kazi ya vitendo. Aliruhusiwa kuendelea na wajibu wake kama kiongozi wa timu. Nilisikitishwa sana niliposikia hivyo. Baadaye, kiongozi alinitafuta ili tufanye ushirika. “Dada, tulipokuwa tukijadili matatizo ya Ndugu Zhao, ulitaja tu upotovu wake na makosa yake. Je, unamchukia bila sababu? Yeye ni mtu wa moja kwa moja kabisa, kwa hivyo anapomwona mtu akifanya kitu kibaya, au kitu kilicho kinyume na kanuni za ukweli, yeye hazungumza moja kwa moja. Wakati mwingine yeye husema kwa uzito kiasi, lakini anataka tu kuwasaidia ndugu na kuitetea kazi ya kanisa. Hatuwezi kuchukua mwelekeo usio sahihi hapa. Tukimbadilisha tumweke katika wajibu mwingine, hilo litavuruga kazi ya kanisa. Tunapozungumza kuhusu matatizo ya Ndugu Zhao, lazima tuchunguze kama kile tulichokuwa tunasema na kufanya kilikuwa kinaambatana na ukweli, kama nia zetu zilikuwa sawa, na ni upotovu upi uliochanganywa humo….” Ukumbusho wa kiongozi ulinifanya nifikirie huenda nina tatizo kubwa. Nilifikiria nyuma kuhusu jinsi nilivyokuwa nimetenda katika muda ambao nilikuwa nimefanya wajibu wangu na Ndugu Zhao, na nikahisi wasiwasi kiasi. Niliichukua hali yangu mbele za Mungu katika maombi

na baadaye nikasoma maneno haya ya Mungu: “Wale miongoni mwa ndugu ambao daima hueneza ubaya wao ni vibaraka wa Shetani na hulivuruga kanisa. Watu hawa lazima siku moja wafukuzwe na kuondolewa. Katika imani yao kwa Mungu, ikiwa watu hawana moyo wa kumcha Mungu ndani yao, ikiwa hawana moyo ambao ni mtiifu kwa Mungu, basi sio tu kwamba hawatashindwa kufanya kazi yoyote ya Mungu, lakini kinyume na hayo watakuwa watu wanaovuruga kazi ya Mungu na wanaomwasi Mungu. Wakati ambapo mtu anayeamini Mungu hamtii Mungu ama kumcha Mungu lakini badala yake anamwasi, basi hii ndiyo aibu kuu zaidi kwa muumini. … Mungu daima yumo mioyoni mwa wale wanaomwamini Mungu kwa kweli na daima wana moyo wa kumcha Mungu, moyo wa kumpenda Mungu. Wale wanaomwamini Mungu lazima wayafanye mambo kwa moyo wa uangalifu na wenye busara, na yote wanayoyafanya yanapasa kulingana na matakwa ya Mungu na yaweze kuuridhisha moyo wa Mungu. Hawapaswi kuwa wabishi, wakifanya watakavyo, hayo hayafai katika utaratibu mtakatifu. Watu hawawezi kuipunga bendera ya Mungu kwa madaha na kucharuka kila mahali, wakienda kwa mikogo na kutapeli kotekote; kutenda haya ni tendo la uasi la juu zaidi. Familia zina masharti zao na mataifa yana sheria zao; je, hali sio hivi hata zaidi katika nyumba ya Mungu? Je, matarajio sio makali hata zaidi? Je, hakuna amri nyingi hata zaidi za utawala? Watu wana uhuru wa kutenda watakayo, lakini amri za usimamizi za Mungu haziwezi kubadilishwa kwa hiari. Mungu ni Mungu asiyewaruhusu watu kumkosea Yeye…(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Onyo kwa Wale Wasiotenda Ukweli). Maneno ya Mungu yalinifadhaisha sana. Niliweza kuona kwamba tabia ya Mungu haistahimili kosa lolote, kwamba kuna amri za utawala katika nyumba ya Mungu, na kwamba Ana masharti. Mtu akinena na kutenda bila kumcha Mungu, akiropokwa kama mtu asiyeamini, akiwahukumu wengine kwa siri, akipanda mbegu ya chuki, akitengeneza vikundi, na kuvuruga kazi ya kanisa, basi mtu huyo ni mtumishi wa Shetani. Mungu kamwe hawezi kumruhusu mtu kama huyo abaki kanisani. Niliifikiria tabia yangu mwenyewe na kile nilichokuwa nimefichua katika wajibu wangu na Ndugu Zhao. Nilikuwa namwonea tu kwa sababu alikuwa ameitaja dosari yangu mbele ya wengine, na kunifedhesha. Pia nilimweleza dada mpya waziwazi juu ya chuki yangu kwa ndugu huyo na kumhukumu bila yeye kujua, nikijaribu kumvuta dada huyo upande wangu na kumtenga ndugu huyo. Niliposikia kwamba mtu mwingine alikuwa ameripoti juu ya matatizo kadhaa katika wajibu wake niliidakia fursa hiyo kumwelekezea kidole, nikiwa na hamu kiongozi wa kanisa ambadilishe na kumtimua. Je, sikuwa nikionyesha tabia yenye nia mbaya, ya kishetani? Je, huo ulikuwaje mfano wa mtu wa imani? Niligundua kuwa, kwa kutaja makosa na dosari zangu katika wajibu wangu, Ndugu Zhao alikuwa akiwajibikia kazi ya nyumba ya Mungu, na alifanya hivyo ili kunisaidia mimi. Lakini nikawa na chuki dhidi yake kwa sababu iliumiza fahari yangu. Nilikuwa nikijaribu kila mara kupata makosa kwake, kumuhukumu, na kuunda mizozo, nikitazamia kumwondoa. Nilikuwa nimechukua kazi gani? Je, sikuwa nikiivuruga na kuihujumu kazi ya nyumba ya Mungu? Je, sikuwa mtumishi wa Shetani? Mawazo haya yaliniogofya. Kama kiongozi wa kanisa hangechunguza hili kwa kuzingatia kanuni za ukweli na kumwacha ndugu aendelee na wajibu wake, kazi ya timu ingeathirika. Nilijuta na kujisuta, na nilihisi hatia kiasi kumhusu Ndugu Zhao. Niliona kwamba nilikosa ubinadamu kabisa. Isingekuwa hukumu kali na ufunuo wa maneno ya Mungu, basi nikiwa baridi kama nilivyokuwa, nisingetafakari kujihusu au kujijua mwenyewe hata kidogo. Ningeendelea kutenda uovu na kuvuruga kazi ya kanisa, na Mungu angenichukia na kuniondoa. Mwishowe nilitambua jinsi ambavyo ingekuwa hatari ikiwa tabia yangu yenye nia mbaya ya kishetani haingetatuliwa. Nilianza kutafakari juu ya mambo, nikijiuliza chanzo halisi cha tabia ya kishetani ambayo nilikuwa nimeifichua kilikuwa nini.

Baadaye nilisoma maneno haya ya Mungu: “Kwa sababu ya kuzaliwa katika nchi ya uchafu vile, mwanadamu ameangamizwa kabisa na jamii, amekuwa akishawishiwa na maadili ya kikabaila, na amefundisha katika ‘taasisi za elimu ya juu.’ Fikra zilizo nyuma kimaendeleo, maadili potovu, mtazamo mbaya juu ya maisha, falsafa za kudharauliwa za kuishi, uwepo usio na thamani, na hali ya maisha potovu za maisha na desturi— mambo yote haya yameuingilia moyo wa mwanadamu, na kudhoofisha na kushambuliwa dhamiri yake pakubwa. Matokeo yake, mwanadamu kamwe yuko mbali kutoka kwa Mungu, na kila mara anampinga. Tabia ya mwanadamu inakuwa matata zaidi kila siku, na hakuna hata mmoja ambaye kwa hiari yake atatoa chochote kwa ajili ya Mungu, hakuna hata mmoja ambaye kwa hiari atamtii Mungu, wala, zaidi ya hayo, mwanadamu mmoja ambaye kwa hiari yake atatafuta uso wa Mungu. Badala yake, chini ya umiliki wa shetani, mwanadamu hafanyi kitu ila kukimbiza anasa, kujitoa mwenyewe kwa upotovu wa mwili katika nchi ya matope. Hata wanaposikia ukweli, wale wanaoishi gizani hawafikiri kuuweka katika vitendo, na wala kuelekea kumtafuta Mungu hata kama wameuona mwonekano Wake. Jinsi gani wanadamu wapotovu kiasi hiki wawe na nafasi yoyote ya wokovu? Jinsi gani wanadamu waovu kiasi hiki kuishi katika mwanga?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu). “Watu hufikiria namna hii: ‘Kama hutakuwa mwenye fadhila, basi sitakuwa mwenye haki! Ukiwa mwenye kiburi kwangu, basi nitakuwa mwenye kiburi kwako pia! Usiponitendea kwa heshima, kwa nini nikutendee kwa heshima?’ Hii ni fikira ya aina gani? Je, fikira ya aina hiyo si ya kulipiza kisasi? Katika maoni ya mtu wa kawaida, si mtazamo wa aina hii unawezekana? ‘Jicho kwa jicho, na jino kwa jino’; ‘hapa onja dawa yako mwenyewe’— miongoni mwa wasioamini, huu wote ni urazini wenye busara na unakubaliana kabisa na mawazo ya wanadamu. Hata hivyo, kama mtu anayemwamini Mungu— kama mtu anayetafuta kuelewa ukweli na kutafuta mabadiliko katika tabia— je, unaweza kusema kwamba maneno kama hayo ni sahihi au si sahihi? Unapaswa kufanya nini ili kuyatambua? Je, Mambo kama hayo hutoka wapi? Yanatoka katika asili ovu ya Shetani; yana sumu, na yana sura ya kweli ya Shetani yenye uovu na ubaya wake wote. Yana kiini halisi cha asili hiyo. Je, hulka ya mitazamo, mawazo, maonyesho, usemi, na hata vitendo ambavyo vina kiini cha asili hiyo ni ipi? Je, si hulka ya Shetani? Je, vipengele hivi vya Shetani vinapatana na ubinadamu? Je, vinapatana na ukweli, au na uhalisi wa ukweli? Je, ni vitendo ambavyo wafuasi wa Mungu wanapaswa kufanya, na mawazo na mitzamo wanayopaswa kuwa nayo?(Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Nilielewa kutoka katika maneno ya Mungu kwamba kufichua tabia hii yenye nia mbaya ya kishetani na kufanya kitu kikatili cha aina hii hakukuwa kuonyesha upotovu wa muda mfupi tu, lakini kulikuwa ni kwa sababu nilidhibitiwa na sumu na asili ya Shetani. Kupitia elimu ya kitaifa na mafunzo ya kijamii, Shetani huwaloweza watu katika sumu zake nyingi, kama vile “Hatutashambulia isipokuwa tukishambuliwa; tukishambuliwa, hakika tutajibiza,” “Jicho kwa jicho, na jino kwa jino,” na “Hiki hapa kionjo cha dawa yako mwenyewe.” Wakiwa wamepotoshwa na kutiwa sumu na falsafa hizi za kishetani, watu wanakuwa wenye kiburi, wabinafsi, wadanganyifu, na watapeli zaidi na zaidi, na wanakuwa tayari kufanya chochote ili kulinda masilahi na heshima yao. Watu hawawezi kuingiliana vizuri, hawana ufahamu, sembuse uvumilivu wowote. Mara tu maneno au vitendo vya mtu mwingine vinapoathiri masilahi yao wenyewe wanakuwa na chuki dhidi yake, wakimdharau na kumtenga, au hata kulipiza kisasi. Ni kama tu CCP. Ili kudumisha udikteta wake na kulinda taswira yake kama “kubwa, tukufu na sahihi,” hakuna mtu anayeruhusiwa kufichua matendo yake maovu, bila kujali ni mangapi. Watu wanaweza tu kuisifia sana. Yeyote anayesema ukweli na kukifunua Chama cha Kikomunisti, akiichafua taswira yake “tukufu”, hakika ataadhibiwa. Chama hicho huwafunga watu kwa sababu ya kila aina ya mashtaka yaliyobuniwa, hata kuwauwa ili kuwanyamazisha. Joka kubwa jekundu ni katili sana! Nimetiwa sumu za joka kubwa jekundu tangu nilipokuwa mchanga na nimejaa tabia za kishetani. Mimi ni mwenye kiburi sana, sikubali ukweli, na siwaachi wengine wafunue upotovu wangu. Siwezi kupatana na mtu yeyote ambaye anatishia masilahi yangu mwenyewe, na hata mimi humchukulia kama adui mbaya. Ndugu Zhao alipothubutu kuwa mkweli, kutaja dosari zangu halisi, sikukosa tu kulishughulikia jambo hili vizuri, kukubali msaada wake kwa unyenyekevu, lakini nilikuza chuki dhidi yake kwa sababu liliathiri sifa na hadhi yangu. Nilisema udaku, nikamdhoofisha, na nilimtaka abadilishwe sana. Nilikuwa nikitenda kama kikaragosi wa Shetani bila hata kufahamu, nikiivuruga kazi ya kanisa. Ni hapo tu ndipo niliona jinsi Shetani alivyokuwa amenipotosha sana. Nilikuwa mwenye kiburi, mdanganyifu, mbinafsi, na mbaya kiasili. Nilifichua tu tabia yangu ya kishetani bila mfano wowote halisi wa binadamu. Niliona kwamba ikiwa tabia yangu ya kishetani haingetatuliwa, ningeishia kuangamizwa na Mungu. Sasa najua kwamba, nilipokuwa nimejiona kuwa mvumilivu, mstahimilivu kwa wengine, na mwenye ubinadamu mzuri hapo awali, ilikuwa ni kwa sababu masilahi yangu ya kibinafsi hayakuwa yameathiriwa, lakini punde tu kitu kilipoathiri masilahi yangu, asili yangu ya kishetani ilijidhihirisha. Nilianza kujichukia zaidi na zaidi. Sikutaka kuishi ndani ya tabia yangu ya kishetani na kumpinga Mungu tena. Kisha nilimwomba Mungu sala ya toba, nikiwa radhi kufuatilia ukweli, kukubali hukumu na utakaso wa maneno ya Mungu, na kutupilia mbali tabia yangu ya kishetani haraka iwezekanavyo.

Muda mfupi baadaye, nilisoma haya katika maneno ya Mungu: “Ikiwa, katika imani yao katika Mungu, watu mara nyingi hawaishi mbele Yake, basi hawataweza kuwa na uchaji wowote Kwake, na hivyo hawataweza kuepukana na uovu. Mambo haya yanahusiana. Ikiwa moyo wako huishi mara nyingi mbele za Mungu, utazuiwa, na utamcha Mungu katika mambo mengi. Hutavuka mipaka, au kufanya chochote kilicho kiovu. Hutafanya kile kinachochukiwa na Mungu, wala hutasema maneno ambayo hayana maana. Ukikubali uchunguzi wa Mungu, na kukubali nidhamu ya Mungu, utaepuka kufanya mambo mengi maovu. Hivyo, si utakuwa umeepukana na uovu?(“Ukiiishi mbele ya Mungu Kila Wakati tu Ndio Unaweza Kuitembea Njia ya Wokovu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Niliona kutoka katika maneno ya Mungu kwamba kumcha Mungu katika imani ya mtu ni jambo lenye umuhimu mkubwa. Lazima tuishi mbele za Mungu kila wakati na tukubali uchunguzi wa Mungu katika maneno na matendo yetu. Hata ingawa ni vigumu kukubali au tunaweza kuhisi upinzani jambo fulani linapogusa masilahi yetu, kwa moyo unaomcha Mungu, kupitia maombi, tunaweza kujitelekeza, tutafute ukweli, tulenge kazi ya nyumba ya Mungu na wajibu wetu, na tusifanye chochote kumwasi au kumpinga Mungu. Mara tu nilipoanza kutenda kulingana na maneno ya Mungu, niliacha chuki yangu dhidi ya Ndugu Zhao polepole na nikahisi kwamba yeye kutaja shida zangu kungeweza kunisaidia kujiboresha, na kwamba alifanya hivyo ili kutimiza matokeo bora katika wajibu wetu. Sasa ninapokumbana na shida, ninaweza kutafuta ushauri kutoka kwake nikiwa na mtazamo sahihi, na kupitia maoni na msaada wake, nimejiboresha katika sehemu zangu dhaifu. Nimeanza kufanya vyema zaidi katika wajibu wangu, na ninahisi utulivu na amani. Ilikuwa ni kupitia hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu tu ndiyo niliweza kupitia mabadiliko haya. Niliona jinsi kazi ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu ilivyo ya vitendo.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Kupima kwa Sura Ni Upuuzi Tu

Yifan Jiji la Shangqiu, Mkoa wa Henan Katika siku za nyuma, mimi mara nyingi niliwapima watu kwa sura zao, nikiwachukua watu wachangamfu,...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp