Kwa Nini Sijabadilika Baada ya Miaka Mingi ya Imani

14/01/2018

Jinru Mji wa Nanyang, Mkoa wa Henan

Wakati ndugu wa kiume au wa kike alipoonyesha dosari zangu au hakusikiza kauli yangu ama sikuhisi kushawishika au nilibishana nao. Nilijutia vitendo vyangu baadaye, lakini nilipokabiliwa na mambo haya, sikuweza kujizuia mwenyewe kuifichua tabia yangu potovu. Nilisumbuliwa na hili kwa kina, na nikafikiri: Kwa nini maneno ya wengine yanaweza kuniaibisha hadi kukasirika? Na kwa nini sijabadilika hata kidogo licha ya miaka minane ya kumfuata Mungu? Nilikuwa na wasiwasi na tena na tena nilitafuta kutoka kwa Mungu, nikimuuliza kunipa nuru ili niweze kujua chanzo cha mbona tabia yangu potovu haikuwa imebadilika.

Siku moja, wakati wa ibada zangu, niliona kifungu cha mahubiri: “Kila mtu huyachukia majisifu na majivuno yake mwenyewe, uhalifu wake na udanganyifu. Watu wengi hubadilika kwa kiasi fulani; watu fulani, wenye kiburi na majivuno na hawana mantiki, na ambao ni wahalifu na wadanganyifu kwa asili, hubadilika kidogo tu na hivyo maneno na tabia zao hubakia karibu kutobadilika: Kiburi chao, majivuno, uhalifu na udanganyifu hubakia dhahiri. Hili linahusiana na uzoefu wao. Kutoka mwanzo hadi mwisho huwa hawafuatilii mabadiliko katika tabia yao, ila wao huangalia tu jinsi wengine wanavyoingia katika maisha. Matokeo yake, wao hujizuia. Kwa maana wao huona tu kiburi na majivuno ya wengine, na kuamini kuwa ni wengine tu wanaopaswa kuhukumiwa na kuadibiwa na Mungu. Wao hufikiri wenyewe hawajampinga Mungu, na hukumu ya Mungu na kuadibiwa ni kwa wengine tu. Kusoma neno la Mungu kutoka kwa mtazamo huu wa kipekee, si ajabu kuwa hawabadiliki” (Ushirika Kutoka kwa wa Juu). Wakati huu nilikuwa na mwamko. Niligundua sababu nilikuwa sijabadilika licha ya kumfuata Mungu kwa miaka mingi ni kwa sababu nilikuwa nimemwamini Mungu lakini sikuwa nimetafuta kubadilisha tabia yangu; nilikuwa nimezingatia tu jinsi wengine walivyoingia katika maisha na sio kuingia kwangu mwenyewe katika maisha. Na wakati huu sikuweza kujizuia kufikiria matukio yangu nikikurupuka kwa haraka “nikifanya kazi”: Wakati wa kula na kunywa maneno ya Mungu sikuwahi kutumia haya kamwe ili kufikiria hali zangu. Daima niliwafundisha wengine na kuwapima dhidi ya maneno ya Mungu. Katika mikutano nilipopitisha ukweli ilikuwa tu kutatua shida na matatizo ya wengine, na sikuwahi kamwe kutafuta kile ambacho mimi mwenyewe ni lazima nikiingie. Nilipopitisha maneno ya ufunuo wa Mungu wa kiini kipotovu cha binadamu, mifano yangu ilikuwa ya ndugu wengine wa kiume na wa kike, nikitumia wengine kama onyo wakati mimi chache sana nilitumia maneno ya Mungu kuzielewa hali zangu mwenyewe na kupata kuingia kwangu. … Na hivyo mwaka baada ya mwaka ilipita na kuingia kwangu mwenyewe katika maisha kukabaki karibu kutupu. Lakini bado nilifikiria nilikuwa mtu mwenye huruma, kwamba nilikuwa nikibeba mzigo wa maisha ya ndugu zangu wa kiume na wa kike. Hasa kuanzia mwaka jana hadi sasa, kanisa lilinipangia kushirikiana na dada mdogo kutimiza majukumu yetu pamoja, na nikaendelea kuubeba “mzigo” wangu na kuzingatia kuingia kwake katika maisha. Huyo dada alipojifichua kuwa mwenye kiburi na mwenye kushikilia maoni yake ningeharakisha kutumia neno la Mungu ili kuwasiliana naye, lakini nilijifikiria mwenyewe: Wewe una kiburi sana tu. Wakati dada huyo hakuweza kujiepusha na uhasi kwa sababu alizuiliwa na wasiwasi wake kuhusu mustakabali na majaaliwa yake, nilitafuta maneno sahihi ya Mungu ili kula na kunywa pamoja naye na kumpitishia kuwa Mungu anataka kutuokoa, lakini ndani nilimdharau: Kuna muda mchache uliobaki na bado unatafuta baraka kwa bidii sana? Wakati dada huyo alitoa hisia zake na kuniambia jinsi mara nyingi alivyokuwa na shaka kwa watu, nilizungumza juu ya ukweli wa kuwa mtu mwaminifu, lakini ndani alinikasirisha: Wewe ni msumbufu mno. Wakati dada huyo alikuwa katika hali mbaya lakini hakuweza kusema ni kwa nini, nilimwambia ajichunguze, aichangue asili yake, lakini ilipofika kwangu sikuzingatia kutumia neno la Mungu kujielewa na kujichanganua kutoka kwa kile nilichokifichua. … Si ni kweli kwamba nilifikiria kuwa ni wengine tu waliokuwa wapotovu mno na wangepaswa kuhukumiwa na kuadibiwa na Mungu, huku nikijiweka nje ya neno la Mungu? Si nilikuwa nazingatia tu kuingia katika maisha kwa wengine na kujiacha nyuma? Ni wakati huo tu nilipokuja kutambua kuwa nilikuwa maskini na wa kusikitisha kama maskini na mwombaji wa mtaani asiye na pesa, na moyo wangu ulijazwa na majuto.

Chini ya mwongozo wa Mungu, niliona kwamba neno Lake linasema: “Watu husema mambo kama haya: Acha matarajio yako, kuwa wa kweli. Unataka watu waachane na mawazo ya kubarikiwa—lakini wewe je? Wewe hukanushi mawazo ya watu ya kubarikiwa na wewe mwenyewe unatafuta baraka? Huwaruhusu wengine kupokea baraka lakini wewe unazifikiria kwa siri—hilo linakufanya kuwa nini? Tapeli? Unapofanya hivyo, dhamiri yako haishutumiwi? Ndani ya moyo wako, huhisi kuwa na deni? Je, wewe si mdanganyifu? Unachimbua maneno yaliyo ndani ya mioyo ya wengine, lakini husemi lolote kuhusu yaliyo moyoni mwako—wewe kweli ni kipande cha takataka kisicho na thamani!(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufafanuzi wa Mafumbo ya “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima”, Sura ya 42). Neno la Mungu liliuchoma moyo wangu na kuniacha na aibu ya kina. Niliyafikiria yote niliyoyafanya. Si nilikuwa laghai, kama Mungu alivyofichua? Kijuujuu nilikuwa ninafanya kazi yangu, lakini kwa kweli nilikuwa nikitumia shauku yangu kumlaghai Mungu uaminifu Wake. Kijuujuu nilikuwa nikiwasaidia ndugu zangu wa kiume na wa kike, lakini kwa kweli nilikuwa nikitumia maneno na mafundisho ya kidini kuwalaghai heshima yao na upendezwaji, kwa lengo la kuwa na nafasi katika moyo wao. Niliwaambia wengine wasiwe na tamaa ya hadhi, wasiwe na kiburi, lakini daima niliwaangalia wengine kwa dharau na sikuweza kuangalia kwa usahihi dosari za ndugu zangu wa kiume na wa kike na hata nilikataa kumtii mtu yeyote. Niliwafanya wengine waache nia zao za kupata baraka, wasiongozwe na kesho zao na jaala, wakati mimi daima nilifanya mipango ya kesho yangu na hata nilikuwa na wasiwasi sana kuhusu hili. Nilikasirishwa na ujanja na tuhuma za wengine, wakati mimi mara nyingi niliangalia maonyesho yao na nikawa na wasiwasi jinsi walivyonifikiria. Niliwaambia wengine kujielewa wenyewe, kuelewa mawazo yao ya ndani zaidi ili kuichangua asili yao, wakati mimi nilificha malengo yangu maovu, na maneno na matendo yangu hayakusimamiwa na Mungu. … Kwa miaka mingi nilikuwa nikizungumza maneno makubwa na niliridhika kububujika kanuni halisi, lakini sikuwa nimezingatia kuingia katika uhalisi na kuishi kwa kudhihirisha maneno ya Mungu. Kwa sababu ya hiyo, bado sikuwa na ufahamu wowote kujihusu mwenyewe, wala tabia yangu ya maisha haikuwa imebadilika sana. Bali, ilikuwa ya kiburi zaidi na zaidi. Kama tu Mungu anavyosema: “… kadiri wanavyofahamu mafundisho zaidi, ndivyo tabia zao zinavyokuwa zenye majivuno zaidi(“Watu Wanafanya Madai Mengi Sana kwa Mungu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Niliona mafundisho niliyokuwa nayo kama rasilmali yangu, lakini sikuzingatia kujielewa mwenyewe, kutafuta kuingia, kupata ukweli. Na hivyo ningewezaje kuwa na mabadiliko yoyote katika tabia yangu ya maisha? Kazi na maneno ya vitendo ya Mungu hutupa ukweli wote tunaouhitaji na Yeye hutaka tuuelewe huo ukweli, na kupitia kutimiza wajibu wetu kuleta mwanga na upataji wa nuru tuliopata katika uzoefu wetu wa kila siku na kuingia, na kutoa hayo kwa ndugu zetu wa kiume na wa kike. Lakini nililenga tu kujitayarisha na mafundisho, na niliona kuzungumza juu ya mafundisho kuwa wajibu wangu, kuwapa wengine nuru ya Roho Mtakatifu bila ubinafsi, kuwafanya wengine watende ukweli, wakati mimi mwenyewe sikuingia. Na kwa sababu hiyo nilijiacha nyuma na pia nikawadhuru ndugu zangu wa kiume na wa kike. Mimi ni Paulo wa kweli wa kisasa!

Mungu, asante kwa kupata nuru Yako na mwanga, ambazo zimeniwezesha kuona kuwa kushindwa kubadili tabia yangu licha ya miaka mingi ya kumwamini Mungu ilikuwa tu ni kutokana na kuzingatia kazi, kujitayarisha na mafundisho na kujionyesha badala ya kuzingatia kuingia kwangu katika maisha. Ninachukia kwamba mimi nina kiburi sana na mjinga, kwamba siupendi ukweli, na hivyo nimepoteza fursa nyingi za kuingia katika ukweli na kutafuta mabadiliko. Niko tayari sasa kuuelewa ukweli vyema kupitia maneno Yako, kutafuta kujifahamu kwa kina, kwa bidii na kwa vitendo kutenda neno la Mungu na kuingia katika ukweli, kutumia vitendo ili kuishi kwa kudhihirisha na kukulipa Wewe.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Masumbuko Makali ya Milele

“Roho zote ambazo zimepotoshwa na Shetani ziko chini ya udhibiti wa miliki ya Shetani. Ni wale tu wanaomwamini Kristo ndio waliotengwa...

Kuona Uhalisi Wangu Kwa Dhahiri

Xiaoxiao Jijini Xuzhou, Mkoani Jiangsu Kwa sababu ya mahitaji ya kazi ya kanisa, nilihamishwa mpaka mahali pengine ili kutimiza wajibu...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp