Mimi Si Mpuuzi Tena, Licha ya Ujana Wangu

05/11/2020

Ni kama maneno ya Mungu yasemavyo, “Ikiwa katika kupitia kazi ya Mungu, mtu anataka kubadilika awe yule aliye na mfano wa binadamu, lazima apitie ufunuo, kuadibiwa, na hukumu ya maneno ya Mungu, na hatimaye, ataweza kubadilika. Hii ndiyo njia. Kazi isingekuwa hivi, watu wasingekuwa na njia ya kubadilika. Lazima ifanywe hivi, kidogo kidogo. Watu lazima wapitie hukumu na kuadibiwa; na kupogolewa kwa mfululizo na kushughulikiwa. Vitu vilivyofunuliwa katika asili za watu ni lazima vifichuliwe. Watu wataweza kutembea kwenye njia inayofaa baada ya vitu hivi kufichuliwa na watu kuvielewa vizuri. Ni baada tu ya kipindi cha kupitia na kupata kuelewa baadhi ya ukweli ndipo watakapokuwa na uhakika kiasi wa kusimama(“Kuelewa Visawe na Tofauti katika Asili ya Binadamu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Sasa nitafanya ushirika kuhusu uzoefu na ufahamu wangu mwenyewe.

Nilianza kujifunza kucheza zitha nilipokuwa mwenye umri wa miaka 5, na nilitaalamikia kucheza zitha katika chuo cha muziki. Baada ya kuanza kumwamini Mungu, nilipoona kwamba nyumba ya Mungu ilikuwa na video ambazo zilihitaji wimbo wa ala ya muziki ya zitha, nilifurahi sana. Niliwaza, “Siku moja nikiweza kufanya wajibu huu, nitaweza kutumia vyema vipaji vyangu na kutunga muziki mzuri wa kumsifu Mungu.”

Mnamo Mei mwaka wa 2019, nilipata wajibu huu mwishowe. Nilipojiunga na kikundi hicho mara ya kwanza, nilikutana na kina dada wawili, na nikawaza, “Hawa ni watu ambao walichaguliwa kwa ajili ya vipaji vyao, lakini nina hakika kwamba ujuzi wangu bila shaka ni bora ukilinganishwa na wao.” Kisha, baada ya kuwajua, niligundua kwamba hakuna yeyote kati yao aliyekuwa amesomea nadharia ya kitaalamu ya muziki, na wote wawili walisema kwamba walitaka kujifunza zaidi kutoka kwangu. Niliposikia hayo, nilihisi vizuri. Niliwaza, “Nilichaguliwa miongoni mwa ndugu wengi ili kujiunga na kikundi hiki, na najua mengi zaidi kuwaliko dada ninaoshirikiana nao, kwa hivyo ujuzi wangu hakika ni bora!” Baada ya hayo, mmoja wa kina dada hao aliniambia, “Baada ya siku chache, dada mwingine atajiunga na kikundi, na nimesikia kwamba yeye ni mchezaji wa zitha wa kiwango cha 10, hivyo wewe ni wa kiwango gani?” Sikuvutiwa, na nikawaza, “Haijalishi hata kidogo wewe ni mchezaji wa kiwango gani. Nilitaalamikia zitha na ninaipenda sana. Ikiwa wewe ni mchezaji wa kiwango cha 10, kwa hiyo? Viwango havina maana yoyote kwa mtaalamu.” Kwa hivyo, nilimtangazia kwa majivuo, “mimi ni mtaalamu.” Siku chache baadaye, Dada Ming alifika. Alisema kuwa baada ya kupita mtihani wa kiwango cha 10, hakuwa amecheza zitha kwa zaidi ya muongo mmoja. Hiyo ilinifanya nifikiri, “Inaonekana kwamba mimi ndiye mtaalamu wa pekee katika kikundi. Katika siku zijazo, nitawaonyesha nyote jinsi nilivyo hodari sana.” Baada ya hapo, niliweza kumaliza kutunga wimbo kwa siku 2-3, lakini niligundua kwamba kina dada zangu bado walikuwa wakijifunza nadharia ya msingi ya muziki. Wakati mwingine walichanganyikiwa kabisa, na nilihisi kwamba nilikuwa bora kuwaliko. Nilihisi kana kwamba kujifunza maarifa ya kitaaluma kwa kweli kulinifanya niwe tofauti. Hasa nilipoona kwamba hawakuweza kutunga nyimbo, au walifanya makosa, nilihisi kwamba lilikuwa jambo la kawaida kwangu kuanza kujifanya mwalimu nilipokuwa nikiwafundisha.

Nakumbuka wakati mmoja nilipokuwa nikitunga wimbo, nilisikia ghafla mtu akicheza zitha kwenye chumba kilichofuata. Nilijua kwamba Dada Ming ndiye aliyekuwa akifanya mazoezi, lakini sikuweza kujizuia kuhisi chuki ikiibuka ndani yangu. Niliwaza, “Muda mrefu sana umepita tangu Dada Ming alipocheza. Anacheza vibaya sana ...” Nilijaribu kuvumilia kusikia sauti hiyo, lakini baada ya muda sikuweza kuvumilia tena kabisa, kwa hivyo nilimwendea na kusema, “Unacheza kwa kutofuata mfululizo wa noti! Je, ulipitaje mtihani wa kiwango cha 10?” Uso wake ulianza kuwa mwekundu mara moja kwa sababu ya aibu, halafu akaniambia kwa woga, “Muda mrefu sana umepita tangu nilipocheza, mimi si stadi. Unaweza labda kunifundisha jinsi ya kucheza wimbo huu?” Nilimtupia jicho na kusema, “Hakika muda mrefu sana umepita tangu ulipocheza!” Aliinamisha kichwa chake na hakusema lolote, na nilihisi hatia kidogo. Nilidhani kwamba pengine sikupaswa kumtendea dada yangu kwa namna hii. Lakini pia nilifikiria jinsi ambavyo, nilipokuwa bado shuleni, niliwanenea wenzangu waliokuwa wadogo kunizidi kwa ukali zaidi kuliko hivyo, kwa hivyo sauti yangu kwake haikuwa mbaya mno. Kwa hivyo, niliketi na kuicheza huku akitazama, kisha nikasema, “Cheza kama nilivyokuonyesha na utajua.” Baada ya hapo, alipoketi na kucheza, niliona kwamba mikono na vidole vyake vilishupaa, na alionekana kuwa na wasiwasi. Alicheza noti chache tu kisha akakosea, kwa hivyo nilimwonyesha mara nyingine chache. Lakini alipoendelea kufanya makosa, nilianza kumchukia. “Kule shuleni, nilipokuwa na matatizo na kuwaomba wenzangu msaada, nilijaribu mara kadhaa tu na nielewa. Nimekuonyesha mara kadhaa tayari, hivyo kwa nini huwezi kucheza? Wewe ni mpumbavu sana,” niliwaza. Kwa hivyo, nilimwambia, “Ikiwa bado huwezi kucheza baada ya mara zote ambazo nimekuonyesha, basi kusema ukweli, sitaki kukufundisha." Aliniangalia, na niliona masikitiko tu machoni mwake. Nilifadhaishwa sana na jinsi alivyoonekana. Niligundua kwamba alihisi kuwa alizuiwa nami. Niliwezaje kutenda hivi? Kwa nini sikuweza kuwa mvumilivu zaidi? Lakini nikawaza baadaye, “Ninarekebisha tu makosa yake. Huenda anateseka hivi sasa, lakini hiyo itamhimiza afanye vizuri haraka zaidi, kwa hivyo bado namsaidia mwishoni.” Mara nilipogundua hayo, sikuyafikiria sana. Lakini baadaye, niligundua kwamba shauku ya Dada Ming ya kucheza ilizidi kupungua, na akaacha kuniuliza maswali. Nilipomuuliza sababu, aliniambia, “Naogopa kwamba nikikuuliza, utanikosoa, kwa hivyo sithubutu kukuuliza yale ambayo siyajui. Afadhali nisubiri hadi utakapofanya mazoezi, nisikilize nikiwa katika chumba kifuatacho, nijifunze jinsi unavyocheza na niboreshe ujuzi wangu kwa njia hiyo.” Niliposikia hayo, niliumia moyoni kwa kweli. Kwa kweli sikuwahi kufikiri kwamba ningemfanya ahisi kwamba alizuiwa sana kiasi kwamba aliogopa kuniuliza maswali, au kwamba naweza kumuumiza vibaya. Nilihisi vibaya na nikawaza, “Nilichotaka kufanya tu ni kumsaidia kujifunza haraka zaidi. Je, mambo yaliishiaje kuwa hivi?” Kwa hivyo, nilimwomba Mungu, nikimsihi Anisaidie kuelewa matatizo yangu.

Na kisha nikasoma kifungu hiki cha maneno ya Mungu: “Je, tabia ya kiburi hutokeaje? Je, hiyo husababishwa na mtu kushauriana na wewe? (Hapana; hiyo hutokana na asili yangu). Je, basi, asili yako inawezaje kukuongoza kuwa na majibu na maonyesho ya aina hii? Inafichuliwaje? Punde mtu anaposhauriana na wewe kuhusu jambo fulani, mara moja unakuwa usiye na busara, unapoteza ubinadamu wako wa kawaida, na huwezi tena kufanya maamuzi sahihi. Wewe hufikiri, ‘Unaniuliza juu ya hili; ninaelewa! Najua kulihusu! Ninalifahamu! Mara nyingi mimi hukumbana na jambo hili, na ninalifahamu vizuri sana jambo hili; kwangu, si jambo kubwa.’ Unapofikiria namna hii, je, mantiki yako ni ya kawaida au siyo ya kawaida? Wakati ambapo tabia yoyote potovu inafichuliwa, mantiki ya mtu yanakuwa yasiyo ya kawaida. Kwa hivyo, haijalishi ni jambo gani unalokumbana nalo—hata mtu anaposhauriana na wewe—ni sharti usiwe na mtazamo wa kiburi; mantiki yako lazima yabaki kuwa ya kawaida(Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). “Usiwe mwenye haki wa kibinafsi; zichukue nguvu za wengine na kuzitumia kusawazisha na mapungufu yako mwenyewe, angalia jinsi wengine wanaishi kwa kutegemea maneno ya Mungu na uone kama maisha, vitendo na hotuba zao ni vya thamani ya kujifunza kutoka kwavyo au la. Ukiwaona wengine kuwa chini yako wewe basi ni mwenye haki binafsi, mwenye majivuno ya kibinafsi na huna manufaa kwa yeyote(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 22). Nilihisi vibaya na kutaabika niliposoma maneno ya Mungu. Maneno ya Mungu yalifunua kila moja ya matendo na mawazo yangu, na wakati huo tu ndipo nilipogundua kuwa tabia kama hiyo ilikuwa ufunuo wa tabia yangu ya kiburi. Nilidhani kwamba kwa sababu nilikuwa na elimu ya muziki na nilikuwa na maarifa kidogo ya kitaalamu, nilikuwa wa kipekee. Nilidhani kwamba nilikuwa mtu mwenye kipaji cha kitaalamu. Wakati ambapo dada zangu hawakuelewa kitu fulani na waliponiuliza, nilidhani hata zaidi kwamba katika ustadi na ujuzi wa kitaalamu, nilikuwa bora kuliko wote. Nilihisi kwamba nilikuwa bora, kwa hivyo nilijiweka katika nafasi ya mwalimu na nilitumia mtazamo na sauti ya cheo cha juu cha mwalimu nilipowafundisha kina dada zangu. Niliposikia kuwa Dada Ming hakucheza vizuri sana, mbali na kumdharau, pia nilimkaripia papo hapo. Sikuzingatia hisia zake hata kidogo. Nilimwonyesha jinsi ya kucheza mara kadhaa, lakini wakati ambapo bado nilimsikia akifanya makosa, nilimzungumzia kwa ukali sana kiasi kwamba alihisi kuwa alizuiwa sana na hakutaka kufanya mazoezi tena. Aliogopa sana kiasi kwamba aliona ni afadhali kujifumza kwa siri kuliko kuniuliza maswali. Je, nilianzaje kuwa mwenye kiburi sana na asiyekuwa na mantiki? Kwa kweli nilikuwa mwenye kiburi sana kiasi kwamba nilipoteza ubinadamu wote wa kawaida. Kwa kuzingatia kwamba hakuwa amecheza kwa zaidi ya miaka 10, ilikuwa kawaida kwake kutokuwa stadi kidogo na kujifunza polepole alipoanza tena. Lakini, ukweli kwamba alikuwa tayari kujifunza tena na kufanya kazi ngumu ya mazoezi ili kutimiza wajibu huu lilikuwa jambo la kusifiwa. Badala ya kuona hayo kutoka kwake, nilimdharau na kumdunisha kwa ajili ya kasoro zake, na kumkatisha tamaa ya kujaribu. Niliwezaje kuwa mwenye kiburi sana na kutokuwa na ubinadamu? Kadiri nilivyozidi kufikiria hayo, ndivyo nilivyozidi kugundua jinsi tabia yangu ya upotovu ilivyokuwa mbaya. Ilibidi nitubu kwa Mungu. Sikufaa kuendelea hivi. Kwa hivyo, nilimwomba Mungu, “Mungu, naishi katika tabia yangu ya kiburi, na kwa kumdharau na kumzuia dada yangu, nimemdhuru sana. Sasa, ninagundua yale ambayo nimeyafanya, na natamani kutubu Kwako. Nakusihi pia Uniongoze ili niache tabia yangu ya majivuno na kiburi, niingie katika ukweli, na niiishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida.”

Baada ya hapo, nilimwambia kwa dhati kila mtu aliyekuwa kwenye mkutano kuhusu upotovu niliokuwa nikionyesha, na nikamwomba Dada Ming msamaha. Nilisema, “Nilichukulia kwamba, kwa sababu nilisomea taaluma ya muziki, nilikuwa hodari kuliko ninyi nyote, kwa hivyo nilipokufundisha kucheza, nilitumia sauti ya kejeli, ya kudunisha, na ya kukaripia katika mtazamo wangu kwako. Nakuomba msamaha kwa uchungu niliokusababishia. Kuanzia leo, nataka kuingia katika ukweli wa kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida. Sitaki mhisi kwamba mmezuiwa nami tena, na mkiniona nikifichua upotovu, nataka mnisaidie kwa kunionyesha upotovu huo.” Baada ya kusema hayo, nilishangaa wakati ambapo, mbali na Dada Ming kunisamehe, pia alisema kwamba alitumaini kuwa nitamsaidia zaidi katika ustadi wake. Nilipoona kwamba, baada ya kumdhuru na kumzuia sana dada yangu, alinisamehe, niliaibika hata zaidi. Niliwaza, “Katika siku za baadaye, nataka kuwa mbia wake mzuri na kutimiza wajibu huu pamoja.” Baada ya hapo, nilipomwona Dada Ming akifanya makosa katika muziki wake, wakati mwingine bado nilimdharau, lakini niliweza kugundua mara moja kwamba nilikuwa nikionyesha tabia yangu ya majivuno. Kisha, niliweza kumwomba Mungu, kurekebisha mtazamo wangu, kuacha kujifanya mwalimu, na kumsaidia kujifunza kwa njia ya utulivu na ya kirafiki. Muda fulani ulipita, na nikagundua kuwa uhusiano wangu na yeye ulizidi kuwa wa kawaida, na kila nilichomfundisha, alikielewa haraka sana. Kulikuwa na nyimbo ambazo zilinichukua miezi mingi kujifunza shuleni, lakini yeye alijifunza kwa mwezi mmoja. Sote tulifurahi na tukamshukuru Mungu kwa mwongozo Wake.

Lakini, licha ya tukio hilo na ukweli kwamba hali yangu ilikuwa imeboreka, na kwamba kwa nje sikuwa mwenye kiburi kama hapo awali, bado sikuelewa au kuchukia sana tabia zangu za kishetani za kiburi na majivuno. Na kwa hivyo hali ambazo zilifaa zilipotokea, tatizo lile lile la zamani lilitokea tena. Baada ya hapo, kikundi chetu kilianza kujifunza jinsi ya kukokotoa tofauti ya sauti baina ya noti mbili. Usiku mmoja, niliona kwamba njia ya Dada Ming ya kukokotoa tofauti ilikuwa ya polepole sana, kwa hivyo nilitaka kumfundisha njia rahisi ya kufanya hivyo. Dada Han na Dada Xiaoyue pia walikuja kutusikiliza, na baada ya muda mfupi, Dada Xiaoyue na Dada Ming waliweza kukokotoa tofauti kwa kutumia mbinu niliyowafundisha. Sikuweza kujizuia kuridhika nilipoona kwamba waliweza kufanya hivyo. Niliwaza, “Kwa kweli mimi ni mweledi wa kipekee.” Nilihisi kana kwamba nilitaka tu kuendelea kuongea na kuwafundisha, lakini niligundua kwamba Dada Han hakuwa akikokotoa kwa kutumia mbinu yangu, na alikuwa akifanya hivyo polepole. Niliwaza “Ukifanya hivi peke yako, utaweza kukokotoa tofauti ngapi kwa saa moja? Unapoteza tu wakati. Wale wengine wanafanya vile nilivyowafundisha na wanafanya haraka zaidi.” Kwa hivyo basi, nilimwambia Dada Han, “Jaribu kufanya jinsi nilivyokufundisha.” Alionyesha sura ya mfadhaiko na akasema kwamba alijua jinsi ya kukokotoa tofauti kabla ya kusikia mbinu niliyofundisha kwa sababu alikuwa amejifunza mbinu nyingine. Lakini baada ya kusikia nilichofundisha, hakuweza kuifanya tena, na sasa alichanganyikiwa kabisa. Sikuweza kujizuia kumchukia. Niliwaza “Mbinu yangu ni rahisi sana, unawezaje kutoielewa? Nitakufundisha mbinu hii leo. Siamini kwamba huwezi kuielewa!” Kwa hivyo, nilivuta stuli na kuketi karibu naye, na nikaanza kutumia mikono yangu kueleza jinsi ya kukokotoa. Nilirudia mara kadhaa, lakini niliona tu kwamba alikuwa amekanganyikiwa, kwa hivyo nilizuia hasira yangu na kujaribu kuieleza kwa nusu saa nyingine. Lakini baada ya hapo, niliona jinsi alivyoonekana mwenye aibu na sikujua la kusema. Niliwaza, “Pegine muda umepita, labda amechoka sana kiasi kwamba hawezi kuelewa,” na hivyo nikamwacha apumzike.

Katikati ya usiku, niliamka na kumwona Dada Han bado akikokotoa tofauti. Nilishtuka. Nilimwuliza kwa nini bado alikuwa akishughulikia kazi hiyo, na alisema kwa sauti iliyokuwa na fadhaa, “Kwa kweli, bado sielewi mbinu uliyonifundisha. Naweza kukokotoa tofauti kwa kutumia mbinu yangu mwenyewe, lakini ni ya polepole kidogo. Nadhani kwamba pengine napaswa kutumia mbinu yangu mwenyewe kwa sasa.” Nilipoona kwamba dada yangu bado alikuwa akifanya kazi kwa bidii katikati ya usiku, na pia maneno yake ya tahadhari aliponizungumzia, nilihisi hatia kidogo, kwa sababu ni wakati huo ndipo nilipogundua, “Kwa mara nyingine tena, nimemzuia dada yangu, siyo?”

Kwa hivyo siku iliyofuata, kwenye mkutano wetu, nilimsihi kila mtu azungumze waziwazi juu ya kasoro zangu. Dada hawa walisema kwamba nilipenda kuzungumza kila wakati kutoka katika nafasi ya mtu mwenye mamlaka, kwamba nilikuwa mwenye kiburi mno, kwamba niliwafanya wahisi kila mara kuwa walizuiwa, na kwamba nilisisitiza kila wakati wafanye mambo kwa njia yangu. Dada mmoja alisema kwamba nilizungumza kila mara kwa ukali mno na niliwafanya wengine wawe na wasiwasi. Niliposikia dada zangu wakisema mambo haya, nilikanganyikiwa mara moja, na nilihisi joto usoni pangu. Ilikuwa vigumu sana kukubali. Sikuweza kujizuia kusikitika. Niliwaza, “Pengine mimi ni mwenye kiburi kidogo, lakini pia ninashughulikia jambo hilo. Hakika kiburi changu si kibaya sana kama wanavyodai.” Lakini niliwazia hilo zaidi, na ndipo nikagundua kwamba jambo hili lilikuwa likifanyika kwa sababu Mungu alikuwa Ameliruhusu, na sikuwa na haki ya kutoa visingizio au kubishana. Kufanya hivyo kungekuwa kukataa kukubali ukweli. Na zaidi ya hayo, mimi ndiye niliyewaomba kina dada zangu waseme kasoro zangu. Walizisema kwa kweli, na iwapo ningetaa kuzikubali, je, huo usingekuwa tu upumbavu? Mara nilipofahamu haya yote, nilimwomba Mungu kimyakimya nikimsihi Aniruhusu nikubali na kutii yale ambayo dada zangu walikuwa wameibua. Baada ya kuomba, nilihisi mwenye utulivu zaidi, na nikawaambia kina dada zangu kuwa nitatafakari juu ya matatizo yangu.

Baadaye, wakati wa ibada zangu, nilisoma kifungu hiki cha maneno ya Mungu: “Kama kwa kweli una ukweli ndani yako, njia unayotembea kiasili itakuwa njia sahihi. Bila ukweli, ni rahisi kufanya uovu na hutakuwa na budi kuufanya. Kwa mfano, kama ungekuwa na kiburi na majivuno, ungeona kwamba haiwezekani kuepuka kumwasi Mungu; ungehisi kulazimishwa kumwasi. Hutafanya hivyo kimakusudi; utafanya hivyo chini ya utawala wa asili yako ya kiburi na majivuno. Kiburi na majivuno yako vitakufanya umdharau Mungu na kumwona kuwa asiye na maana; vitakufanya ujiinue, vitakufanya kujiweka kila wakati kwenye maonyesho, na mwishowe vitakufanya ukae katika nafasi ya Mungu na kujitolea ushuhuda mwenyewe. Mwishowe utayabadilisha mawazo yako mwenyewe, fikira zako mwenyewe na dhana zako yawe ukweli wa kuabudiwa. Tazama ni kiasi gani cha uovu kinafanywa na watu chini ya utawala wa asili yao ya kiburi na majivuno!(“Ni Kwa Kufuatilia Ukweli Tu Ndiyo Unaweza Kupata Mabadiliko Katika Tabia Yako” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Nilipoona yaliyofichuliwa katika maneno ya Mungu, nilielewa mwishowe kwamba chanzo cha kiburi na majivuno niliyoonyesha na jinsi nilivyowazuia kina dada zangu ni kwamba bado nilikuwa na asili ya kiburi na ya kishetani ndani yangu. Kwa sababu ya kuishi kulingana na asili ya kiburi, nilifikiri kila mara kwamba nilikuwa bora kuwaliko wengine, kwa hivyo nilitaka kuwa na kauli ya mwisho katika kila kitu. Hasa nilipoona kwamba ujuzi wangu wa kitaalamu ulikuwa bora kuliko wa wengine, nilijikweza na kujifanya mwalimu, na nikadai kwamba kila mtu anisikilize na kunitii. Katika hali zilizofaa, nilionyesha maarifa na ujuzi wangu pasipo kutaka, nikatumia maoni yangu mwenyewe kama vigezo vya kufuatwa, na hata kuyachukulia kama ukweli na kudai wengine wanitii kikamilifu. Nilipoona kuwa Dada Han hakutumia mbinu yangu kukokotoa tofauti, nilikasirika papo hapo na kumlazimisha. Nilisisitiza kwamba abadilishe njia zake na anisikilize. Sikuheshimu hisia zake hata kidogo na sikuzingatia shida zake halisi. Hata sikuwapa kina dada nafasi yoyote ya kufanya ushirika au kujadili mambo. Nilikuwa mwenye kiburi sana kiasi kwamba nilipoteza mantiki yote. Mwishowe, sikuwasaidia kina dada zangu waliokuwa kwenye kikundi hata kidogo. Niliwaumiza na kuwazuia tu, nikiathiri utendaji wao wa wajibu wao na kuzuia kazi ya kila mtu. Wakati huo ndipo nilipogundua kwamba kuishi kulingana na tabia ya kiburi kulikuwa kukinizuia nisiishi kwa kudhihirisha mfano wa kibinadamu, na pia kuvuruga wajibu wa wengine na kuzuia kazi ya kanisa. Ningewezaje kusema kwamba nilikuwa nikitimiza wajibu wangu? Je, si wazi kwamba nilikuwa nikifanya maovu na kumpinga Mungu? Nisingetubu, Mungu angenikataa na kuniondoa siku moja! Kina dada zangu kuweza kunisaidia kwa kuonyesha mambo haya kulikuwa Mungu aliyekuwa Akinilinda. Bila wao, ningeendelea kuishi kulingana na tabia yangu ya kiburi, na sijui ni mambo mangapi maovu ambayo naweza kuyafanya.

Baada ya hapo, katika ibada zangu, niliona kifungu kingine cha maneno ya Mungu: “Mungu alimuumba binadamu, Akapumua maisha ndani yake, na pia Akampa baadhi ya werevu Wake, uwezo Wake, na kile Anacho na alicho. Baada ya Mungu kumpa binadamu mambo haya yote, binadamu aliweza kufanya baadhi ya mambo haya kwa uhuru na kufikiria pekee yake. Kama kile binadamu anaunda na kufanya ni kizuri machoni mwa Mungu, basi Mungu anakikubali na haingilii kati. Kama kile binadamu anafanya ni sahihi, basi Mungu atakiacha tu kiwe hivyo milele. Kwa hivyo kauli hii ‘chochote ambacho Adamu alikiita kiumbe hai, hilo ndilo likawa jina lake kuanzia hapo’ inaonyesha nini? Inaonyesha kwamba Mungu hakuona haja ya kufanya marekebisho kwa majina yoyote ya wale viumbe mbalimbali hai. Jina lolote lile ambalo Adamu alimwita, Mungu alisema ‘Ndiyo’ na akasajili jina hilo hivyo. Je, Mungu alionyesha maoni yoyote? La, hilo ni hakika. Kwa hivyo, mnaona nini hapa? Mungu Alimpa binadamu werevu naye binadamu akautumia werevu wake aliopewa na Mungu kufanya mambo. Kama kile binadamu anafanya ni kizuri machoni mwa Mungu, basi kinathibitishwa, kutambulika, na kukubalika na Mungu bila ya utathmini au upinzani wowote. Hili ni jambo ambalo hakuna mtu wala roho wa maovu, wala Shetani, anaweza kufanya(Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I). Nilitambua kwamba hakukuwa na kiburi, majikwezo, au majivuno hata kidogo katika kiini cha Mungu. Baada ya Adamu kuwapa wanyama wote majina, Mungu aliyakubali tu na kuyatumia bila kutokubaliana. Mungu ndiye Muumba, hekima ya Mungu haiwezi kulinganishwa na ya mwanadamu, na bado Mungu kamwe hajionyeshi au kuwalazimisha wengine wamsikilize. Badala yake, Yeye huwapa watu nafasi na Anatupa uhuru, na almradi tufanye mambo yanayojenga, Yeye haingilii. Nilipofikiria hayo, niliaibika. Mimi ni mdogo kuliko chembe ya vumbi machoni pa Mungu, lakini bado nilijaribu kutumia maarifa yangu ya kitaalamu na kipaji nilichopewa na Mungu kwa manufaa yangu, na nilijikweza, nikajionyesha na kuwadharau wengine. Pia nilisisitiza kwamba watu wengine wanisikilize, hadi kufikia wakati ambapo hata sauti yangu ilibadilika. Kwa kweli nilikuwa mwenye kiburi sana. Dada yangu angeweza kutekeleza wajibu wake vizuri sana kwa kutumia mbinu aliyojua, lakini nilimlazimisha atumie mbinu yangu na sikumpa nafasi yoyote ili afikirie kwa uhuru. Niliwashinikiza wengine na nilikuwa dikteta. Je, niliwezaje kutokuwa na mantiki hivyo? Niliishi kwa kudhihirisha tu tabia za kishetani, na hali hiyo ilikuwa mbaya sana. Niligundua kwamba bila kujali jinsi nilivyokuwa na uwezo au kipaji, nisingetenda ukweli au kubadilisha tabia zangu za kishetani, siku moja, ningekataliwa na kuondolewa na Mungu. Nilipofikiria hayo, niliogopa kidogo na pia nilijidharau na kujichukia. Nilimwomba Mungu, nikisema kwamba nitatubu na kutenda ukweli, na kwamba sitaishi tena kwa kufuata tabia yangu yenye kiburi.

Baada ya hapo, nilisoma vifungu viwili vya maneno ya Mungu ambavyo vilinipa njia ya jinsi ya kujikana na kuondokana na tabia yangu ya kiburi. “Usijifanye kuwa wewe ni bora kuliko wengine. Je, wewe peke yako unaweza kutekeleza kazi hiyo, hata ikiwa wewe ni stadi wa kitaalamu zaidi au unahisi kwamba ubora wako ndio mkubwa zaidi kuliko wa wale walio hapa? Je, wewe peke yako unaweza kutekeleza kazi hiyo hata ikiwa una hadhi ya juu zaidi? Huwezi, huwezi bila msaada wa kila mtu. Kwa hivyo, hakuna anayepaswa kuwa na kiburi na hakuna anayepaswa kutamani kutenda yeye peke yake; lazima mtu ajinyenyekeze, aachilie fikira na maoni yake mwenyewe, na afanye kazi kwa upatanifu na wafanyakazi wenzake. Hawa ndio watu ambao hutenda ukweli na wana ubinadamu. Watu kama hao wanapendwa na Mungu, na ni wao tu ndio wanaoweza kujitolea katika utekelezaji wa wajibu wao. Hili pekee ndilo dhihirisho la kujitolea(“Utimizaji Sahihi wa Wajibu Unahitaji Ushirikiano wa Upatanifu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). “Mungu humpa mwanadamu vipaji, akimpa ujuzi maalum na vile vile akili na busara. Je, mwanadamu anapaswa kutumiaje vitu hivi? Lazima uutoe kikamilifu ujuzi wako maalum, vipaji vyako, akili na busara yako kwa ajili ya wajibu wako. Lazima utumie moyo wako na kupiga bongo zako katika kutumia kila kitu unachojua, kila kitu unachoelewa, kila kitu unachoweza kufanikisha, na kila kitu unachofikiri kuhusu katika kufanya wajibu wako. Kwa kufanya hivyo, utabarikiwa(Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Kutafakari maneno ya Mungu kulinifanya nielewe kwamba Mungu alinipa kipaji na Akanijaalia nijifunze maarifa ya kitaalamu yanayohusu muziki, kwa hivyo napaswa kutumia vitu hivi kutimiza wajibu wangu, wala si kama mtaji wa kuwa na majivuno na kiburi. Niligundua kwamba kila mtu ana ustadi wake na kasoro zake, na bila kujali jinsi ninavyoweza kuwa hodari katika muziki, sitawahi kuwa hodari katika kila kitu wala haimaanishi kwamba nina uhalisi wa ukweli. Niligundua kwamba ilibidi nifanye kazi na kina ndugu ili tuweze kufidia kasoro za kila mmoja, na kufanya kazi kwa umoja nao ili kutunga kazi ambazo zilimshuhudia Mungu. Kufanya hivi pekee ndiko kunalingana na mapenzi ya Mungu.

Baada ya hapo, nilipocheza zitha na kujifunza ujuzi pamoja na dada zangu, nilipopata maeneo ambayo walihitaji kuboresha, nilimwomba Mungu kimakusudi uwezo wa kujikana na kuwafundisha kwa uvumilivu, na niliweza pia kujifunza kutokana na uwezo ambao walikuwa nao. Baada ya hapo, hawakuhisi tena kwamba walizuiwa nami na waliweza kutumia vipaji vyao katika wajibu wao, na baada ya muda walizidi kuhisi huru. Kwa sababu ya mwongozo wa Roho Mtakatifu, tulitunga nyimbo haraka zaidi kuliko hapo awali, na ubora ulizidi kuongezeka. Baadaye, dada mdogo ambaye hakuwa amesomea nadharia ya muziki alijiunga na kikundi chetu, kwa hiyo, ili kumsaidia kujifunza na kuwa mweledi haraka iwezekanavyo, nilimbunia kozi ambayo ilijumuisha masomo ya misingi na ya juu. Nilifikiri kwamba almradi afuate kozi yangu, ataweza kujifunza kila kitu haraka sana. Lakini siku moja, alikuja kuniuliza juu ya jambo ambalo hakuelewa, na nilipogundua kwamba swali lake halikuwa popote katika kozi niliyobuni, nilianza kuwa na wasiwasi sana na nikawaza, “Nilikubunia kozi nzuri sana lakini huifuati. Badala yake, unachunguza habari nyingine. Ukijifunza kwa njia hii, utaanza kufanya vyema lini? Je, si kwamba unatilia tu shaka utaalamu wangu?” Msururu wa mawazo ulipofikia hatua hii, niligundua mara moja kwamba tabia yangu ya kiburi ilikuwa ikiibuka tena, kwa hivyo nilimwomba Mungu mara moja na nikajikana. Nilikumbuka jinsi nilivyokuwa nimefanya mambo hapo awali kwa kutegemea tabia yangu ya kiburi na kusababisha kina dada waliokuwa katika kikundi changu wahisi kwamba walizuiwa sana. Wakati huu, nilijua kwamba sharti niheshimu maoni yake. Niliamua kumruhusu ajifunze kwa kasi yake mwenyewe na kwa njia yake mwenyewe badala ya kumlazimisha afanye kile nilichodhani kuwa bora. Baada ya hapo, mimi na yeye tulipokuwa tukitunga wimbo, kila tulipokuwa na maoni tofauti, nilijikana kwa makusudi na kisha nikajadili naye kuhusu mambo. Mwishowe, wiki moja baadaye, wimbo wetu ulikuwa umekamilika na nilijua kwamba huu kwa kweli ulikuwa mwongozo na baraka za Mungu. Ni kama maneno ya Mungu yasemavyo, “Kadiri unavyoweka ukweli katika vitendo, ndivyo unavyokuwa na ukweli; kadiri unavyoweka ukweli katika vitendo, ndivyo unavyokuwa na upendo wa Mungu; na kadiri unavyoweka ukweli katika vitendo, ndivyo unavyobarikiwa na Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wanaompenda Mungu Wataishi Milele Katika Mwangaza Wake).

Iliyotangulia: Masumbuko Makali ya Milele

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Jinsi ya Kuuchukulia Wajibu Wako

Na Zhongcheng, Uchina Mwenyezi Mungu anasema, “Mahitaji ya msingi ya imani ya mtu kwa Mungu ni kuwa ni sharti awe na moyo mwaminifu, na...

Ukweli Umenionyesha Njia

Na Shizai, Japani Mwenyezi Mungu anasema, “Kumtumikia Mungu si kazi rahisi. Wale ambao tabia yao potovu haibadiliki hawawezi kamwe...

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp