88 Nashukuru kwa Upendo wa Mungu

1

Nani aonyeshaye ukweli,

akifichua upendo wa Mungu,

kumwezesha mwanadamu aone tumaini?

Nani afanyaye kazi ya hukumu ya siku za mwisho,

akileta njia ya uzima wa milele?

Kazi ya Mungu mwenye mwili

yasababisha ulimwengu wote kutikisika.

Mbele ya kiti cha enzi tunainuliwa

na karamu ya Mwanakondoo tunahudhuria.

Upendo wa Mungu kwetu ni halisi sana.

Kwamba hukumu Yake twaweza kuipata

ni kwa neema Yake kabisa.

Kwa ukweli na uzima atoao Mungu,

tunatoa shukrani na tunatoa sifa.

Tutatafuta ukweli, tufanye wajibu vizuri,

ili upendo wa Mungu tuulipe.

2

Tunafurahia maneno ya Mungu;

tunapata ukweli mwingi.

Kwa kupitia maneno ya Mungu,

kupitia jinsi yanavyohukumu,

tunaona wazi binadamu ni mpotovu.

Tumepitia hukumu, majaribu;

upotovu wetu umetakaswa.

Tunapata ukweli na tunapata uzima,

na kama watu wapya tunaishi.

Upendo wa Mungu kwetu ni halisi sana.

Kwamba hukumu Yake twaweza kuipata

ni kwa neema Yake kabisa.

Kwa ukweli na uzima atoao Mungu,

tunatoa shukrani na tunatoa sifa.

Tutatafuta ukweli, tufanye wajibu vizuri,

ili upendo wa Mungu tuulipe.

3

Nani anayetembea kando yetu,

kutuongoza katika nyakati ngumu?

Nani anayeongoza kwa maneno kumpiga Shetani,

kulishinda joka kubwa jekundu?

Maneno ya Mwenyezi Mungu hutupa nguvu,

kwa hivyo tunasimama wakati nyakati ni ngumu.

Pamoja na Mungu tunaweza kushinda.

Maneno ya Mungu hutusaidia kukimbia

kutoka kwa vifungo vya Shetani.

Na tumehisi binafsi

mamlaka ya maneno ya Mungu,

nguvu yake isiyo na kifani.

Na tuonapo kupendeza kwa Mungu,

tunampenda na kutoa ushuhuda.

Bila hofu ya hatari,

injili ya ufalme twaieneza.

Upendo wa Mungu kwetu ni halisi sana.

Kwamba hukumu Yake twaweza kuipata

ni kwa neema Yake kabisa.

Kwa ukweli na uzima atoao Mungu,

tunatoa shukrani na tunatoa sifa.

Tutatafuta ukweli, tufanye wajibu vizuri,

ili upendo wa Mungu tuulipe.

Iliyotangulia: 87 Upendo wa Mungu Unasambaa Duniani

Inayofuata: 89 Kazi ya Mungu Hakika ni ya Ajabu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp