Enzi ya Ufalme Ni Enzi ya Neno

Katika Enzi ya Ufalme, Mungu hutumia maneno kuikaribisha enzi mpya, kubadilisha njia ambayo kwayo Yeye hufanya kazi, na kufanya kazi ya enzi nzima. Hii ndiyo kanuni ambayo kwayo Mungu hufanya kazi katika Enzi ya Neno. Alikuwa mwili ili Anene kutoka katika mitazamo tofauti, ili mwanadamu aweze kumwona Mungu kweli, ambaye ni Neno kuonekana katika mwili, na angeweza kuona hekima na ajabu Yake. Kazi kama hiyo inafanywa ili kufikia malengo ya kumshinda mwanadamu, kumkamilisha mwanadamu, na kumwondoa mwanadamu vyema zaidi, ambayo ndiyo maana ya kweli ya matumizi ya maneno kufanya kazi katika Enzi ya Neno. Kupitia katika maneno haya, watu huja kuijua kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, kiini cha mwanadamu, na kile ambacho mwanadamu anapaswa kuingia katika. Kupitia katika maneno, kazi ambayo Mungu anataka kufanya katika Enzi ya Neno inafanikiwa kwa ukamilifu. Kupitia katika maneno haya, watu wanafunuliwa, kuondolewa, na kujaribiwa. Watu wameyaona maneno ya Mungu, kuyasikia maneno haya, na kutambua uwepo wa maneno haya. Kama matokeo, wameamini katika uwepo wa Mungu, katika kudura na hekima ya Mungu, na pia katika upendo wa Mungu kwa mwanadamu na tamanio Lake la kumwokoa mwanadamu. Neno "maneno" linaweza kuwa rahisi na la kawaida, lakini maneno yanayonenwa kutoka katika kinywa cha Mungu mwenye mwili yanautikisa ulimwengu, kuibadilisha mioyo ya watu, kubadilisha fikira zao na tabia zao za zamani, na kubadilisha jinsi ambavyo ulimwengu wote ulikuwa ukionekana. Katika enzi zote, ni Mungu wa leo tu ndiye Aliyefanya kazi kwa njia hii, na ni Yeye Anayezungumza kwa namna hii na kuja kumwokoa mwanadamu hivi. Kuanzia wakati huu na kuendelea, mwanadamu anaishi chini ya mwongozo wa maneno ya Mungu, akichungwa na kuruzukiwa na maneno Yake. Watu wanaishi katika ulimwengu wa maneno ya Mungu, kati ya laana na baraka za maneno ya Mungu, na kuna hata watu wengi zaidi ambao wamekuja kuishi chini ya hukumu na kuadibu kwa maneno Yake. Maneno haya na kazi hii vyote ni kwa sababu ya wokovu wa mwanadamu, kwa sababu ya kutimiza mapenzi ya Mungu, na kwa sababu ya kubadilisha kuonekana kwa asili kwa ulimwengu wa uumbaji wa zamani. Mungu aliuumba ulimwengu kwa kutumia maneno, Anawaongoza watu ulimwenguni kote kutumia maneno, na Anawashinda na kuwaokoa kutumia maneno. Hatimaye, Atatumia maneno kuutamatisha ulimwengu mzima wa zamani, hivyo kuukamilisha mpango Wake mzima wa usimamizi. Katika Enzi nzima ya Ufalme, Mungu hutumia maneno kufanya kazi Yake, na kufikia matokeo ya kazi Yake. Hatendi maajabu au kufanya miujiza, lakini hufanya kazi Yake kupitia katika maneno tu. Kwa sababu ya maneno haya, mwanadamu hulishwa na kuruzukiwa, na hupata maarifa na uzoefu wa kweli. Katika Enzi ya Neno, mwanadamu amebarikiwa kwa njia ya pekee. Hapitii uchungu wa mwili na hufurahia tu ruzuku nyingi ya maneno ya Mungu; bila kuhitaji kwenda kutafuta bila kufikiri au kusafiri mbele bila kufikiri, kutoka katikati ya utulivu wake, huiona sura ya Mungu, humsikia Akinena kwa kinywa Chake mwenyewe, hupokea kile ambacho Yeye hutoa, na humtazama Akifanya kazi Yake binafsi. Hivi ni vitu ambavyo watu wa enzi zilizopita hawakuweza kufurahia, na ni baraka ambazo hawangeweza kupokea kamwe.

Mungu ameamua kumfanya mwanadamu mkamilifu, na bila kujali mtazamo ambao Ananena kutoka, yote ni kwa sababu ya kuwafanya watu wawe wakamilifu. Maneno yanenwayo kutoka katika mtazamo wa Roho ni magumu kwa watu kuelewa; hawana namna ya kupata njia ya kutenda, kwa kuwa uwezo wao wa kuelewa ni finyu. Kazi ya Mungu inafikia matokeo tofauti, na katika kuchukua kila hatua ya kazi Ana kusudi Lake. Aidha, ni muhimu kwamba Azungumze kutoka katika mitazamo tofauti, kwa kuwa ni kwa kufanya hivyo tu ndipo Anaweza kumkamilisha mwanadamu. Kama Angetamka sauti Yake kutoka katika mtazamo wa Roho tu, hakungekuwa na njia yoyote ya kukamilisha hatua hii ya kazi ya Mungu. Kutoka katika sauti Anayozungumza nayo, unaweza kuona kwamba Amedhamiria kulifanya kundi hili la watu kamilifu. Kwa hivyo, hatua ya kwanza kwa kila anayetamani kukamilishwa inapasa kuwa ipi? Zaidi ya yote, lazima uijue kazi ya Mungu. Leo, njia mpya imeanza katika kazi ya Mungu; enzi imebadilika, namna ambavyo Mungu hufanya kazi pia imebadilika, na njia ambayo Mungu huzungumza ni tofauti. Leo, sio tu kwamba njia ya kazi Yake imebadilika, lakini pia enzi imebadilika. Sasa ni Enzi ya Ufalme. Pia ni Enzi ya kumpenda Mungu. Ni kionjo cha Enzi ya Ufalme wa Milenia—ambayo pia ni Enzi ya Neno, na ambayo Mungu hutumia njia nyingi za kunena ili kumkamilisha mwanadamu, na Ananena kutoka katika mitazamo tofauti ili kumruzuku mwanadamu. Baada ya kuingia katika Enzi ya Ufalme wa Milenia, Mungu ataanza kutumia maneno kumfanya mwanadamu awe mkamilifu, Akimruhusu mwanadamu aingie katika uhalisi wa maisha na kumwongoza kwenye njia sahihi. Mwanadamu amepitia hatua nyingi sana za kazi Yake na ameona kuwa kazi ya Mungu haibaki vile vile, lakini inageuka na kuongezeka kwa kina bila kukoma. Baada ya watu kuipitia kwa muda mrefu sana, kazi imebadilika kwa kurudia rudia, ikibadilika tena na tena. Hata hivyo, bila kujali kiasi inachobadilika, kamwe haikengeuki kutoka kwa kusudi la Mungu la kuwaletea binadamu wokovu. Hata kupitia katika mabadiliko elfu kumi, kamwe haipotei kutoka kwa kusudi lake la asili. Bila kujali jinsi mbinu ya kazi ya Mungu inavyoweza kubadilika, kazi hii kamwe haiuachi ukweli au uzima. Mabadiliko katika njia ambayo kazi hufanywa inahusisha mabadiliko katika muundo wa kazi tu, na mtazamo ambao kwao Mungu ananena; hakuna mabadiliko katika kusudi kuu la kazi ya Mungu. Mabadiliko katika toni ya sauti ya Mungu na njia ya kazi Yake hufanywa ili kufikia matokeo. Mabadiliko katika toni ya sauti hayamaanishi mabadiliko katika madhumuni au kanuni ya kazi hiyo. Watu wanamwamini Mungu hasa ili kutafuta uzima; ikiwa unaamini katika Mungu lakini hutafuti uzima au hufuatilii ukweli au maarifa ya Mungu, basi hii siyo imani katika Mungu! Na, je, bado ni jambo lenye uhalisi kutafuta kuingia katika ufalme kuwa mfalme? Kufanikisha upendo wa kweli kwa Mungu kupitia kutafuta uzima—huu pekee ndio uhalisi; ufuatiliaji na utendaji wa ukweli—hivi vyote ni uhalisi. Kusoma maneno ya Mungu, na kuyapitia maneno haya, utakuja kufahamu maarifa ya Mungu katika uzoefu halisi, na hii ndiyo maana ya kufuatilia kweli.

Sasa ni Enzi ya Ufalme. Ikiwa umeingia katika enzi hii mpya inategemea ikiwa umeingia katika uhalisi wa maneno ya Mungu, ikiwa maneno Yake yamekuwa uhalisi wa maisha yako. Maneno ya Mungu yanafahamishwa kwa kila mtu ili, mwishowe, watu wote wataishi katika ulimwengu wa maneno ya Mungu, na maneno Yake yatampa nuru na kumwangazia kila mtu kutoka ndani. Ikiwa, wakati huu, wewe ni mzembe katika kusoma maneno ya Mungu, na huna shauku ya maneno Yake, basi hili linaonyesha kuwa hali yako ni mbaya. Ikiwa huwezi kuingia katika Enzi ya Neno, basi Roho Mtakatifu hafanyi kazi ndani yako; ikiwa umeingia katika enzi hii, Atafanya kazi Yake. Je, unaweza kufanya nini mwanzoni mwa Enzi ya Neno ili upate kazi ya Roho Mtakatifu? Katika enzi hii, na miongoni mwenu, Mungu atatimiza ukweli ufuatao: kwamba kila mtu ataishi kwa kuyadhihirisha maneno ya Mungu, ataweza kuuweka ukweli katika vitendo, na atampenda Mungu kwa dhati; kwamba watu wote watatumia maneno ya Mungu kama msingi na kama uhalisi wao, na watakuwa na mioyo inayomcha Mungu; na kwamba, kupitia kutenda maneno ya Mungu, mwanadamu kisha atashikilia mamlaka ya kifalme pamoja na Mungu. Hii ndiyo kazi inayopaswa kufanikishwa na Mungu. Je, unaweza kuishi bila kusoma maneno ya Mungu? Leo, kuna wengi ambao wanahisi kuwa hawawezi kuishi hata siku moja au mbili bila kusoma maneno Yake. Lazima wayasome maneno Yake kila siku, na ikiwa muda hauruhusu, kuyasikiza kutatosha. Hii ndiyo hisia ambayo Roho Mtakatifu huwapa watu, na ndiyo njia ambayo Anaanza kuwagusa. Yaani, Yeye huwatawala watu kupitia maneno, ili kwamba waweze kuingia katika uhalisi wa maneno ya Mungu. Ikiwa, baada ya siku moja tu bila kula na kunywa maneno ya Mungu, unahisi giza na kiu, na huwezi kustahimili hali hiyo, hili linaonyesha kwamba umeguswa na Roho Mtakatifu, na kwamba Hajakukuacha. Wewe basi, ni mtu aliye kwenye mkondo huu. Hata hivyo, ikiwa baada ya siku moja au mbili bila kula na kunywa maneno ya Mungu, huhisi kitu, ikiwa huna kiu, na hujaguswa hata kidogo, hili linaonyesha kwamba Roho Mtakatifu amekuacha. Hili linamaanisha, basi, kwamba kuna kitu kibaya na hali yako; hujaingia katika Enzi ya Neno, na wewe ni mmoja wa wale ambao wamebaki nyuma. Mungu hutumia maneno kuwatawala watu; unahisi vizuri ukila na kunywa maneno ya Mungu, na usipokula na kunywa maneno ya Mungu, huna njia ya kufuata. Maneno ya Mungu huwa chakula cha watu, na nguvu inayowaendesha. Biblia inasema “Mwanadamu hataishi kwa mkate pekee, lakini kwa kila neno linalotoka kinywani mwa Mungu”. Leo, Mungu ataikamilisha kazi hii, naye Ataukamilisha ukweli huu ndani yenu. Ni vipi kwamba hapo zamani, watu wangeweza kwenda siku nyingi bila kusoma maneno ya Mungu na bado waweze kula na kufanya kazi kama kawaida, lakini hivi sivyo ilivyo leo? Katika enzi hii, Mungu haswa hutumia maneno kutawala vyote. Kupitia katika maneno ya Mungu, mwanadamu anahukumiwa na kukamilishwa, kisha hatimaye kupelekwa katika ufalme. Maneno ya Mungu tu ndiyo yanayoweza kuyaruzuku maisha ya mwanadamu, na ni maneno ya Mungu tu yanayoweza kumpa mwanadamu mwangaza na njia ya kutenda, hasa katika Enzi ya Ufalme. Alimradi hupotei kutoka katika ukweli wa maneno ya Mungu, kula na kunywa maneno Yake kila siku, Mungu ataweza kukufanya mkamilifu.

Ufuatiliaji wa maisha si jambo ambalo linaweza kuharakishwa; ukuaji wa maisha haufanyiki kwa siku moja au mbili. Kazi ya Mungu ni ya kawaida na ya vitendo, na kuna mchakato ambao lazima ipitie. Ilimchukua Yesu mwenye mwili miaka thelathini na mitatu na nusu kukamilisha kazi Yake ya kusulubiwa—sembuse kazi ya kumtakasa mwanadamu na kuyabadilisha maisha yake, kazi ngumu zaidi? Sio kazi rahisi kumfanya mwanadamu wa kawaida ambaye anamdhihirisha Mungu. Hili ni hivyo hasa kwa watu ambao wamezaliwa katika taifa la joka kubwa jekundu, ambao ni wenye ubora duni wa tabia na wanahitaji muda mrefu wa maneno na kazi ya Mungu. Kwa hivyo usiwe bila subira kutaka kuona matokeo. Lazima uwe mwenye kujitolea katika kula na kunywa maneno ya Mungu, na uweke bidii zaidi katika maneno ya Mungu. Unapomaliza kusoma maneno Yake, lazima uweze kuyaweka katika vitendo halisi, ukikua katika maarifa, ufahamu, utambuzi, na hekima katika maneno ya Mungu. Kupitia katika hili, utabadilika bila kufahamu. Ikiwa unaweza kuchukua kula na kunywa maneno ya Mungu kama kanuni yako, ukiyasoma, ukija kuyajua, kuyapitia, na kuyatenda, utakuwa mkomavu bila kufahamu. Kuna wale ambao wanasema kuwa hawawezi kuyaweka maneno ya Mungu katika vitendo hata baada ya kuyasoma. Haraka yako ni nini? Utakapofikia kimo fulani, utaweza kuyaweka maneno Yake katika vitendo. Je, mtoto wa umri wa miaka minne au mitano anaweza kusema kuwa hawezi kuwasaidia au kuwaheshimu wazazi wake? Unapaswa kujua jinsi kimo chako cha sasa kilivyo kikubwa. Weka katika vitendo kile unachoweza kuweka katika vitendo, na uepukane na kuwa mtu ambaye anasumbua usimamizi wa Mungu. Kula na kunywa maneno ya Mungu tu, na ulichukue hilo kama kanuni yako kuanzia sasa kuendelea. Usijali, kwa wakati huu, kuhusu ikiwa Mungu anaweza kukufanya mkamilifu. Usilichunguze hilo kwa sasa. Kula na kunywa maneno ya Mungu tu yanavyokujia, na Mungu hakika Atakufanya mkamilifu. Hata hivyo, kuna kanuni ambayo kwayo lazima ule na kunywa maneno Yake. Usifanye hivyo tu bila kufikiria. Katika kula na kunywa maneno ya Mungu, kwa upande mmoja, yatafute maneno ambayo unapaswa kuyajua—yaani, yale yanayohusiana na maono—na kwa upande mwingine, tafuta kile unachopaswa kuweka katika vitendo halisi—yaani, kile unachopaswa kuingia ndani. Kipengele kimoja kinahusiana na maarifa, na kingine kinahusiana na kuingia. Mara unapovifahamu vyote viwili—wakati umeshaelewa kile unachopaswa kujua na kile unachopaswa kutenda utajua jinsi ya kula na kunywa maneno ya Mungu.

Kuanzia sasa kuendela, mazungumzo ya maneno ya Mungu yanapaswa kuwa kanuni ambayo kwayo unazungumza. Kwa kawaida, mnapojumuika pamoja, mnapaswa kushiriki katika ushirika kuhusu maneno ya Mungu, mkiyachukua maneno ya Mungu kama maudhui ya mwingiliano wenu, mkiongea juu ya yale mnayojua kuhusu maneno haya, jinsi mnavyoyaweka katika vitendo, na jinsi Roho Mtakatifu afanyavyo kazi. Alimradi unashiriki maneno ya Mungu, Roho Mtakatifu atakupa nuru. Kufanikisha ulimwengu wa maneno ya Mungu kunahitaji ushirikiano wa mwanadamu. Usipoingia katika hili, Mungu hatakuwa na njia ya kufanya kazi; ukiufunga mdomo wako na usizungumze kuhusu maneno Yake, Hatakuwa na njia ya kukuangazia. Wakati wowote ambapo huna shughuli nyingine, zungumza juu ya maneno ya Mungu, na usijishughulishe na mazungumzo yasiyo na maana! Acha maisha yako yajazwe na maneno ya Mungu—ni hapo tu ndipo utakapokuwa mwumini mwenye kumcha Mungu. Haijalishi ikiwa ushirika wako ni wa juu juu. Bila ujuu juu hakuwezi kuwepo kina kirefu. Lazima kuwe na mchakato. Kupitia mafunzo yako, utafahamu kuangaziwa kwako na Roho Mtakatifu, na jinsi ya kula na kunywa maneno ya Mungu kwa matokeo yanayotarajiwa. Baada ya muda wa uchunguzi, utaingia katika ukweli wa maneno ya Mungu. Ni ukiamua kushirikiana tu ndipo utaweza kupokea kazi ya Roho Mtakatifu.

Kati ya kanuni za kula na kunywa maneno ya Mungu, moja inahusiana na maarifa, na nyingine inahusiana na kuingia. Ni maneno yapi unayopaswa kujua? Unapaswa kujua maneno yanayohusiana na maono (kama vile, yale yanayohusiana na ni enzi ipi ambayo kazi ya Mungu imeingia sasa, kile ambacho Mungu anataka kufanikisha sasa, kupata mwili ni nini, na kadhalika; haya yote yanahusiana na maono). Je, njia ambayo mwanadamu anapaswa kuingia katika inamaanisha nini? Hii inahusu maneno ya Mungu ambayo mwanadamu anapaswa kutenda na kuingia ndani. Yaliyo hapo juu ni vipengele viwili vya kula na kunywa maneno ya Mungu. Kuanzia sasa, kula na kunywa maneno ya Mungu kwa njia hii. Ukiwa na ufahamu wazi wa maneno Yake kuhusu maono, basi hakuna haja ya kuendelea kusoma kila wakati. Jambo la umuhimu wa msingi ni kula na kunywa maneno zaidi ya kuingia, kama vile kuugeuza moyo wako kwa Mungu, jinsi ya kuutuliza moyo wako mbele za Mungu, na jinsi ya kuunyima mwili. Hivi ni vitu ambavyo unapaswa kuweka katika vitendo. Bila kujua jinsi ya kula na kunywa maneno ya Mungu, ushirika wa kweli hauwezekani. Mara tu unapojua jinsi ya kula na kunywa maneno Yake, wakati ambapo umeelewa kile kilicho muhimu, ushirika utakuwa wazi, na suala lolote liibuliwalo, utaweza kushirikiana na kufahamu uhalisi. Ikiwa, wakati unashiriki kuhusu maneno ya Mungu, huna uhalisi wowote, basi hujaelewa kile kilicho cha muhimu, ambalo linaonyesha kuwa hujui jinsi ya kula na kunywa maneno ya Mungu. Watu wengine wanaweza kupata kusoma maneno ya Mungu kuwa jambo la kuchosha, ambayo sio hali ya kawaida. Kilicho cha kawaida ni kamwe kutochoka kuyasoma maneno ya Mungu, kuwa na kiu ya maneno hayo kila wakati, na daima kuyaona maneno ya Mungu kuwa mazuri. Hivi ndivyo mtu ambaye ameingia kwa kweli hula na kunywa maneno ya Mungu. Unapohisi kuwa maneno ya Mungu ni ya vitendo sana na ndiyo mwanadamu anapaswa kuingia katika hasa; unapohisi kuwa maneno Yake ni ya msaada mkubwa na yenye faida kwa mwanadamu, na kwamba ni riziki ya maisha ya mwanadamu—ni Roho Mtakatifu anayekupa hisia hii, na Roho Mtakatifu anayekugusa. Hii inathibitisha kuwa Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yako na kwamba Mungu hajakuacha. Watu wengine, wakiona kuwa Mungu huzungumza kila wakati, huchoka na maneno Yake, na hufikiria kwamba haina athari wakiyasoma au la—ambayo si hali ya kawaida. Wanakosa moyo ambao unatamani kuingia katika uhalisi, na watu kama hao hawana kiu wala hawaoni umuhimu wa kukamilishwa. Kila unapopata kuwa huna kiu ya maneno ya Mungu, hii inaonyesha kuwa hauko katika hali ya kawaida. Hapo zamani, ikiwa Mungu angekuwa Amekuacha kungeweza kuamuliwa na ikiwa ulikuwa na amani ndani yako, na ikiwa uliona furaha. Sasa cha muhimu ni ikiwa una kiu ya maneno ya Mungu, ikiwa maneno Yake ni uhalisi wako, ikiwa wewe ni mwaminifu, na ikiwa unaweza kumfanyia Mungu yote uwezayo. Kwa maneno mengine, mwanadamu anahukumiwa na uhalisi wa maneno ya Mungu. Mungu huelekeza maneno Yake kwa binadamu wote. Ikiwa uko tayari kuyasoma, Atakupa nuru, lakini ikiwa hauko tayari, Hatafanya hivyo. Mungu huwapa nuru wale ambao wana njaa na kiu ya haki, na Huwapa nuru wale wanaomtafuta. Wengine husema kwamba Mungu hakuwapa nuru hata baada ya kusoma maneno Yake. Lakini uliyasoma maneno haya kwa njia gani? Ukiyasoma maneno Yake kama ambavyo mtu asiye ba shauku, na usiweke umuhimu katika uhalisi, Mungu angewezaje kukupa nuru? Mtu ambaye hayathamini maneno ya Mungu anawezaje kufanywa mkamilifu na Yeye? Ikiwa huyathamini maneno ya Mungu, basi hutakuwa na uhalisi wala ukweli. Ikiwa unayathamini maneno Yake, basi utaweza kuuweka ukweli katika vitendo, na ni hapo tu ndipo utakapomiliki uhalisi. Hii ndiyo maana lazima ule na kunywa maneno ya Mungu wakati wote, iwe una shughuli nyingi au la, hali iwe mbaya au la, na iwe unajaribiwa au la. Kwa jumla, maneno ya Mungu ndiyo msingi wa kuwepo kwa mwanadamu. Hakuna anayeweza kuyaepuka maneno Yake, lakini lazima ale maneno Yake kama anavyokula milo mitatu ya siku. Je, kufanywa mkamilifu na kupatwa na Mungu kunaweza kuwa rahisi vile? Ikiwa wewe unaelewa kwa sasa au la, na ikiwa una utambuzi juu ya kazi ya Mungu au la, lazima ule na kunywa maneno mengi ya Mungu iwezekanavyo. Huku ni kuingia kwa njia ya vitendo. Baada ya kusoma maneno ya Mungu, harakisha kutia katika vitendo kile unachoweza kuingia katika, na uweke kando kwa sasa kile ambacho huwezi. Kunaweza kuwa na maneno mengi ya Mungu ambayo huwezi kuelewa mwanzoni, lakini baada ya miezi miwili au mitatu, pengine hata mwaka, utayaelewa. Je, hili linawezekanaje? Ni kwa sababu Mungu hawezi kuwafanya watu wawe wakamilifu kwa siku moja au mbili. Wakati mwingi, unaposoma maneno Yake, huenda usielewe papo hapo. Wakati huo, yanaweza kuonekana kama maandishi tu; lazima uyapitie kwa muda kabla ya kuyaelewa. Mungu akiwa Amezungumza mengi sana, unapaswa kufanya kila uwezalo kula na kunywa maneno Yake, kisha, bila ya wewe kutambua, utakuja kuelewa, na bila wewe kutambua, Roho Mtakatifu atakupa nuru. Roho Mtakatifu anapompa mwanadamu nuru, mara nyingi huwa bila ufahamu wa mwanadamu. Yeye hukupa nuru na kukuongoza unapoona kiu na kutafuta. Kanuni ambayo kwayo Roho Mtakatifu hufanya kazi ina msingi katika maneno ya Mungu ambayo wewe hula na kunywa. Wale wote ambao hawaweki umuhimu katika maneno ya Mungu na daima huwa wenye mtazamo tofauti kwa maneno Yake—wakiamini, katika fikira zao zilizochanganyikiwa, kuwa ni jambo lisilo na athari yoyote wakisoma maneno Yake au la—ni wale ambao hawana uhalisi. Kazi ya Roho Mtakatifu wala utoaji nuru Wake haviwezi kuonekana ndani ya mtu kama huyo. Watu kama hawa wanasairi tu, wanaojifanya na wasio na sifa za kweli, kama Bwana Nanguo wa mfano.[a]

Bila maneno ya Mungu kama uhalisi wako, huna kimo halisi. Wakati utakapofika wa wewe kujaribiwa, bila shaka utaanguka, na kisha kimo chako cha kweli kitafichuliwa. Lakini wale ambao hutafuta kuingia katika ukweli mara kwa mara, watakapokumbwa na majaribu, watapata kuelewa madhumuni ya kazi ya Mungu. Mtu aliye na dhamiri, na mwenye kiu ya Mungu, anapaswa kuchukua hatua za matendo kumlipa Mungu kwa sababu ya upendo Wake. Wale ambao hawamiliki ukweli hawawezi kusimama imara hata katika mambo madogo. Hiyo ndio tofauti kati ya wale walio na kimo cha kweli na wale wasio na kimo halisi. Je, ni kwa nini kwamba, ingawa wote wanakula na kunywa maneno ya Mungu, wengine wanaweza kusimama imara katika majaribu, huku wengine wanakimbia? Tofauti ya wazi ni kwamba wengine hawana kimo cha kweli; hawana maneno ya Mungu kutumika kama ukweli wao, na maneno Yake hayajakita mizizi ndani yao. Punde tu wanapojaribiwa, wao hufika mwisho wa njia yao. Je, basi ni kwa nini kwamba fulani wanaweza kusimama imara katikati ya majaribu? Ni kwa sababu wanaelewa ukweli na wana maono, na wanaelewa mapenzi ya Mungu na mipango Yake, na hivyo wanaweza kusimama imara katika majaribu. Hiki ni kimo cha kweli, na haya pia ni maisha. Wengine wanaweza pia kusoma maneno ya Mungu, lakini hawayaweki katika vitendo, hawayachukulii kwa uzito; wale ambao hawayachukulii kwa uzito hawaweki umuhimu wowote katika kutenda. Wale ambao hawana maneno ya Mungu kutumika kama ukweli wao hawana kimo cha kweli, na watu kama hao hawawezi kusimama imara katika majaribu.

Maneno ya Mungu yanapotokea, unapaswa kuyapokea mara moja, na kuyala na kuyanywa. Haijalishi wewe unaelewa kiasi gani, mtazamo mmoja ambao lazima ushikilie imara ni kula na kunywa, kujua, na kutebda maneno Yake. Hiki ni kitu ambacho unapaswa kuweza kufanya. Kamwe usijali kuhusu jinsi kimo chako kinavyoweza kuwa kikubwa; lenga tu kula na kunywa maneno Yake. Hiki ndicho mwanadamu anapaswa kushiriki katika. Maisha yako ya kiroho hasa ni kujaribu kuingia katika ukweli wa kula na kunywa maneno ya Mungu na kuyaweka katika vitendo. Sio shughuli yako kulenga juu ya kitu kingine chochote. Viongozi wa kanisa wanapaswa kuwaongoza ndugu zao wote ili wajue jinsi ya kula na kunywa maneno ya Mungu. Hili ndilo jukumu la kila kiongozi wa kanisa. Wawe wachanga au wazee, wote wanapaswa kuzingatia kula na kunywa maneno ya Mungu kama jambo lenye umuhimu mkubwa na wanapaswa kuwa na maneno Yake mioyoni mwao. Kuingia katika ukweli huu kunamaanisha kuingia katika Enzi ya Ufalme. Leo, watu wengi wanahisi kuwa hawawezi kuishi bila kula na kunywa maneno ya Mungu, na wanahisi kuwa maneno Yake ni mapya bila kujali wakati. Hii inamaanisha kuwa wanaanza kwenda katika njia sahihi. Mungu hutumia maneno kufanya kazi Yake na kumruzuku mwanadamu. Wakati kila mtu anatamani na kuwa na kiu ya maneno ya Mungu, binadamu wataingia katika ulimwengu wa maneno Yake.

Mungu amezungumza mengi sana. Je, ni kiasi gani ambacho wewe umepata kujua? Umeingia kwa kiasi gani? Kama kiongozi wa kanisa hajawaongoza ndugu zake kuingia katika ukweli wa maneno ya Mungu, basi atakuwa hajatimiza wajibu wake, na atakuwa ameshindwa kutekeleza majukumu yake! Ufahamu wako uwe wa kina au wa juu juu, bila kujali kiwango cha ufahamu wako, lazima ujue jinsi ya kula na kunywa maneno Yake, lazima uyazingatie kwa makini sana maneno Yake, na uelewe umuhimu na haja ya kuyala na kuyanywa. Kwa kuwa Mungu amezungumza sana, usipokula na kunywa maneno Yake, au kujaribu kutafuta, au kuyaweka maneno Yake katika vitendo, huku hakuwezi kuitwa kumwamini Mungu. Kwa kuwa unamwamini Mungu, basi lazima uyale na kuyanywa maneno Yake, uyapitie maneno Yake, na uishi kwa kuyadhihirisha maneno Yake. Hii tu ndiyo inayoweza kuitwa imani katika Mungu! Ukisema kwa mdomo wako kwamba unamwamini Mungu lakini huwezi kuyaweka maneno Yake yoyote katika vitendo au kutoa ukweli wowote, huku hakuitwi kumwamini Mungu. Badala yake, ni "kutafuta mkate ili kumaliza njaa." Kuzungumza tu kuhusu ushuhuda mdogo, vitu visivyo na maana, na mambo ya juujuu, bila kuwa hata na ukweli mdogo kabisa: hivi havijumuishi imani katika Mungu, na hujafahamu tu njia sahihi ya kuamini katika Mungu. Kwa nini lazima ule na kunywa maneno mengi ya Mungu iwezekanavyo? Usipokula na kunywa maneno Yake lakini utafute tu kupaa mbinguni, je, huko ni kumwamini Mungu? Je, hatua ya kwanza ambayo mtu amwaminiye Mungu anapaswa kuchukua ni ipi? Ni kwa njia gani ndiyo Mungu humkamilisha mwanadamu? Je, unaweza kukamilishwa bila kula na kunywa maneno ya Mungu? Je, unaweza kuchukuliwa kama mtu wa ufalme bila ya maneno ya Mungu kutumika kama ukweli wako? Je, ni nini hasa maana ya imani katika Mungu? Waumini katika Mungu wanapaswa, angalau, kuwa na tabia njema kwa nje; la muhimu zaidi ni kuwa na maneno ya Mungu. Bila kujali chochote, kamwe huwezi kuyaacha maneno Yake. Kumjua Mungu na kutimiza nia Zake vinafanikishwa kupitia katika maneno Yake. Katika siku zijazo, kila taifa, dhehebu, dini, na sehemu zitashindwa kwa njia ya maneno ya Mungu. Mungu atazungumza moja kwa moja, na watu wote watashikilia maneno ya Mungu mikononi mwao, na kwa njia hii, binadamu watakamilishwa. Ndani na nje, maneno ya Mungu yanapenyeza kotekote: Binadamu watazungumza maneno ya Mungu kwa vinywa vyao, watende kulingana na maneno ya Mungu, na kuweka maneno ya Mungu ndani, wakisalia wamelowa na maneno ya Mungu ndani na nje. Hivi ndivyo binadamu watakamilishwa. Wale wanaotimiza nia za Mungu na wanaweza kumshuhudia, hawa ni watu wanaomiliki maneno ya Mungu kama ukweli wao.

Kuingia katika enzi ya Neno—Enzi ya Ufalme wa Milenia—ni kazi ambayo inatimizwa leo. Kuanzia sasa kuendelea, fanya mazoezi ya ushirika kuhusu maneno ya Mungu. Ni kwa njia ya kula na kunywa na pia kupitia maneno ya Mungu ndiyo utaweza kuishi kwa kuyadhihirisha maneno ya Mungu. Lazima uwe na uzoefu wa vitendo ili uwashawishi wengine. Ikiwa huwezi kuishi kwa kuudhihirisha ukweli wa maneno ya Mungu, hakuna atakayeshawishika! Wale wote wanaotumiwa na Mungu wanaweza kuishi kwa kuudhihirisha ukweli wa maneno ya Mungu. Ikiwa huwezi kutoa ukweli huu na kumshuhudia Mungu, hii inaonyesha kwamba Roho Mtakatifu hajafanya kazi ndani yako, na kwamba wewe hujakamilishwa. Huu ndio umuhimu wa maneno ya Mungu. Je, wewe una moyo wenye kiu ya maneno ya Mungu? Wale ambao wana kiu ya maneno ya Mungu wana kiu ya ukweli, na watu tu kama hawa tu ndio ambao hubarikiwa na Mungu. Katika siku zijazo, kuna maneno mengi zaidi ambayo Mungu atanena kwa dini zote na madhehebu yote. Kwanza Ananena na kutamka sauti Yake kati yenu ili Awakamilishe kabla ya kusonga mbele kunena na kutamka sauti Yake kati ya watu wa Mataifa ili Awashinde. Kupitia katika maneno Yake, wote watashawishika kwa dhati na kikamilifu. Kupitia katika maneno ya Mungu na ufunuo Wake, tabia potovu ya mwanadamu inapungua, anapata kuonekana kwa mwanadamu, na tabia yake ya uasi inapungua. Maneno hayo hufanya kazi kwa mwanadamu kwa mamlaka na humshinda mwanadamu katika nuru ya Mungu. Kazi ambayo Mungu hufanya katika enzi ya sasa, na vile vile mabadiliko ya kazi Yake, yote yanaweza kupatikana ndani ya maneno Yake. Usiposoma maneno Yake, hutaelewa chochote. Kupitia kula kwako na kunywa maneno Yake, na kupitia kushiriki katika ushirika na ndugu na uzoefu wako halisi, utapata ufahamu kamili wa maneno ya Mungu. Ni hapo tu ndipo utaweza kweli kuishi kwa kudhihirisha ukweli wake.

Tanbihi:

a. Maandishi ya asili hayana maneno “wa mfano.”

Iliyotangulia: Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watapatwa na Mungu

Inayofuata: Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp