Amri za Enzi Mpya

Katika kupitia kazi ya Mungu, ninyi lazima msome maneno ya Mungu kwa makini na mjiandae na ukweli. Lakini kuhusu kile mnachotaka kufanya au jinsi mnavyotaka kukifanya, hakuna haja ya maombi au dua yenu ya dhati, na kwa kweli mambo haya hayana maana. Ilhali kwa sasa, shida zinazowakabili hivi sasa ni kwamba hamjui jinsi ya kupitia kazi ya Mungu, na kwamba kuna ubaridi mwingi ndani mwenu. Mnajua mafundisho mengi, lakini hamna uhalisi mwingi. Je, hii si ishara ya makosa? Makosa mengi yanaonekana ndani yenu, kundi hili. Hivi leo, hamna uwezo wa kutimiza majaribu kama vile “watendaji huduma,” na hamwezi kutafakari au kutimiza majaribu na usafishaji mwingine unaohusiana na maneno ya Mungu. Lazima mzingatie mambo mengi ambayo mnapaswa kuweka katika matendo. Ambayo ni kusema kuwa watu lazima wafuate majukumu mengi wanayostahili kuyatekeleza. Hili ndilo watu wanalopaswa kufuata, na wanalostahili kufanya. Mruhusu Roho Mtakatifu afanye linalostahili kufanywa na Roho Mtakatifu; mwanadamu hawezi kulichangia lolote. Mwanadamu sharti ashike yale ambayo lazima yatendwe na mwanadamu, ambayo hayana uhusiano na Roho Mtakatifu. Si lolote bali lile ambalo lazima litendwe na mwanadamu, na lazima lifuatwe kama amri, kama ufuasi wa sheria za Agano la Kale. Ingawa sasa si Enzi ya Sheria, bado kuna maneno mengi yanayolingana na Enzi ya Sheria ambayo yanahitaji kufuatwa, na hayatendwi tu kwa kutegemea kuguswa na Roho Mtakatifu, lakini ni yale yanayostahili kufuatwa na wanadamu. Kwa mfano: Hupaswi kuihukumu kazi ya Mungu wa vitendo. Hupaswi kumpinga mtu anayeshuhudiwa na Mungu. Mbele za Mungu, utahifadhi nafasi yako, na hutakuwa mwovu. Matamshi yako yanapaswa yawe wastani, na maneno yako na matendo yako yanapaswa kufuata mpangilio wa mwanadamu aliyeshuhudiwa na Mungu. Unapaswa kuheshimu ushuhuda wa Mungu. Usipuuze kazi ya Mungu wala maneno kutoka kinywa chake. Usiige sauti na malengo ya matamshi ya Mungu. Kwa nje, usifanye lolote linalodhihirisha kumpinga mtu anayeshuhudiwa na Mungu. Na mengineyo. Haya ndiyo yanayopaswa kufuatwa na kila mmoja. Katika kila enzi, Mungu hutaja amri nyingi zinazoambatana na amri na zinazopaswa kufuatwa na mwanadamu. Kupitia hili, anazuia tabia ya mwanadamu, na kugundua ukweli wake. Tazama maneno “Onyesha heshima kwa baba na mama yako” kutoka kwa nyakati za Agano la Kale, kwa mfano. Maneno haya hayatumiki hivi leo; wakati huo, yalizuia tabia zingine za mwanadamu tu, yalitumika kuonyesha uaminifu wa imani ya mwanadamu kwa Mungu, na yalikuwa alama ya wale waliomwamini Mungu. Ingawa sasa ni Enzi ya Ufalme, bado kuna amri nyingi ambazo mwanadamu lazima azifuate. Amri za kale hazitumiki; leo, kuna mazoea mengi, mwafaka kwa mwanaadamu kutekeleza, na ambayo ni muhimu. Hayahusiani na kazi ya Roho Mtakatifu na lazima yatendwe na mwanadamu.

Katika Enzi ya Neema, mazoea mengi ya Enzi ya Sheria yaliondolewa kwa sababu sheria hizi hazikufaa hasa kazi ya wakati huo. Baada ya kuondolewa, mazoea mengi yaliwekwa ambayo yalifaa enzi hiyo, na ambayo yamekuwa amri nyingi za sasa. Mungu wa leo alipokuja, kanuni hizi zilitupiliwa mbali, na hazikuhitajika kufuatwa tena, na mazoea mengi ambayo yalifaa kazi ya wakati huu yakawekwa. Leo, mazoea haya si kanuni, lakini ili kuwa na athari; ni mazuri kwa ajili ya leo—na kesho, pengine, yatakuwa kanuni. Kwa ujumla, unafaa kufuata yale ambayo yatafanikisha kazi ya leo. Usizingatie kesho: Yanayofanywa leo ni kwa ajili ya leo. Pengine kesho kutakuwa na mazoea mazuri ambayo utahitajika kutekeleza—lakini usizingatie hayo sana, yafuate yanayofaa kufuatwa leo ili uepuke kumpinga Mungu. Leo, hakuna lolote muhimu analopaswa kufuata mwanadamu zaidi ya yafuatayo: Usijaribu kumbembeleza Mungu anayesimama mbele ya macho yako, au kumficha jambo lolote. Usizungumze uchafu ama matamshi ya kiburi mbele ya Mungu aliye mbele yako. Usimdanganye Mungu mbele ya macho yako kwa maneno mazuri wala kwa maneno ya kuridhisha ili uweze kujipatia uaminifu Wake. Usitende bila heshima mbele za Mungu. Tii yote yatokayo kinywani mwa Mungu, wala usikatae, usipinge, ama kusaili maneno Yake. Usitafsiri unavyoona kuwa sawa, maneno yanayonenwa kutoka kinywani mwa Mungu. Chunga ulimi wako ili usikutie katika mtego wa hila danganyifu za yule mwovu. Unapaswa kulinda nyayo zako ili kuepuka kupita mipaka uliyowekewa na Mungu. Kufanya hivyo kutakufanya uzungumze maneno ya majivuno na yenye fahari kuu kulingana na mtazamo wa Mungu, na hivyo kufanya uchukiwe na Mungu. Usieneze maneno kutoka kinywa cha Mungu ovyo ovyo, usije ukadhihakiwa na wengine na kufanywa kuwa mjinga na mapepo. Tii kazi yote ya Mungu wa leo. Hata ikiwa hauifahamu, usiihukumu; unachoweza kufanya ni kutafuta na kushiriki. Hakuna mtu atapatendea dhambi mahali pa Mungu pa asili. Huwezi kufanya lolote ila kumhudumia Mungu wa leo kwa mtazamo wa mwanadamu. Huwezi kumfunza Mungu wa leo kwa mtazamo wa mwanadamu—kufanya hivyo ni kupotoka. Hakuna anayeweza kusimama kwa niaba ya mtu aliyeshuhudiwa na Mungu; katika maneno yako, matendo, na mawazo yako ya ndani, unasimama katika nafasi ya mwanadamu. Hili ni la kufuatwa, ni wajibu wa mwanadamu, hakuna anayeweza kulibadilisha, na kufanya hivyo ni ukiukaji wa amri za utawala. Inapaswa kukumbukwa na kila mtu.

Muda mrefu ambao Mungu ametumia kuzungumza na kutamka kumemfanya mwanadamu kufikiria kusoma na kukariri maneno ya Mungu kuwa ndio wajibu wake wa kimsingi. Hakuna anayezingatia kutenda, na hata yale mnayopaswa kufuata hamyafuati, kwa hivyo hili limeleta ugumu na matatizo mengi kwa huduma yenu. Ikiwa, kabla ya kutenda maneno ya Mungu, hujayafuata yale unayopaswa kuyafuata, basi wewe ni mmoja wa wale wanaochukiwa na kukataliwa na Mungu. Kwa kufuata matendo haya, unapaswa kuwa na bidii na uaminifu. Hufai kuyachukua kuwa kama minyororo, ila uyafuate kama amri. Leo, hupaswi kuzingatia athari ambazo zinatarajiwa kufikiwa; kwa ufupi, hivi ndivyo Roho Mtakatifu anavyofanya kazi, na yeyote atakayefanya kosa lazima aadhibiwe. Roho Mtakatifu hana hisia, na hazingatii ufahamu wako wa sasa. Ukimkosea Mungu leo, basi Atakuadhibu. Ukimkosea ndani ya wigo wa mamlaka Yake, basi Hatakuachilia bure. Hajali jinsi gani ulivyo makini katika kufuata maneno ya Yesu. Ukikiuka amri za Mungu za leo, Atakuadhibu; Atakushutumu hadi kifo. Je, itakubalika vipi kwako wewe kutozifuata? Lazima ufuate—hata kama itamaanisha kupitia uchungu mdogo! Bila kujali ni dini, kundi, taifa, ama dhehebu gani, katika siku zijazo lazima yote yafuate mazoea haya. Hakuna yaliyosamehewa, na hakuna yatakayoachwa! Kwa sababu ndiyo yatakayotekelezwa na Roho Mtakatifu leo, na hayawezi kukosewa kwa wote. Ingawa si mambo makuu, lazima yatendwe na kila mtu, na ni amri zilizowekwa kwa mwanadamu na Yesu, aliyefufuka na kupaa mbinguni. Je, “Njia … (7)” haisemi kuwa ufafanuzi wa Yesu, wa kama wewe ni mwenye haki au mwenye dhambi, ni kwa mujibu wa mtazamo wako kwa Mungu leo? Hakuna anayekubaliwa kupuuza suala hili. Katika Enzi ya Sheria, kizazi baada ya kizazi cha Mafarisayo kilimwamini Mungu, lakini kwa ujio wa Enzi ya Neema, hawakumfahamu Yesu, na walimpinga. Hivyo basi, yote waliyoyafanya yakawa hayana maana na yalikuwa bure na Mungu hakuyakubali. Ukiweza kuelewa hili basi hutakuwa mwepesi wa kutenda dhambi. Watu wengi, pengine, wamejipima dhidi ya Mungu. Je, kumpinga Mungu kuna ladha ipi, chungu au tamu? Unapaswa kuelewa hili—usijifanye kuwa hujui. Mioyoni mwao, pengine, wengine wamesalia kutoshawishika. Bali Nakushauri, ulijaribu na kuona—hisi jinsi ladha yake ilivyo. Hili litawazuia wengi kuwa na shaka kulihusu siku zote. Watu wengi husoma maneno ya Mungu lakini wanampinga mioyoni mwao kwa siri. Baada ya kumpinga hivi, je, huhisi kama kisu kimepindwa moyoni mwako? Kama si utengano wa familia, basi ni usumbufu wa mwilini, ama mateso ya wana wa kiume na mabinti. Ingawa mwili wako umeepushwa na kifo, mkono wa Mungu kamwe hautakuacha. Je, unafikiri linaweza kuwa rahisi hivyo? Hasa, ni muhimu hata zaidi kwa wengi waliomkaribia Mungu kuzingatia hili. Muda unapoendelea, utalisahau, na, pasipo kujua, utaingia majaribuni, utaacha kujali kila kitu, na huu utakuwa mwanzo wako wa kutenda dhambi. Je, hili linaonekana duni kwako? Ikiwa utaweza kufanya hili vyema, basi una nafasi ya kufanywa mkamilifu—kupokea mwongozo kutoka kwa kinywa cha Mungu mwenyewe mbele za Mungu. Ikiwa wewe ni mzembe, itakuwa taabu kwako—utamwasi Mungu, maneno yako na matendo yatakuwa maovu, na punde au baadaye, utabebwa na dhoruba kubwa na mawimbi makuu. Kila mmoja wenu anapaswa kuzingatia amri hizi. Mkizikiuka, mtu aliyeshuhudiwa na Mungu anaweza akakosa kuwalaani, lakini Roho wa Mungu hajamalizana na wewe. Hatakuhurumia. Je, unadhania kwamba una uwezo wa kufanya makosa? Kwa hivyo, lolote Asemalo Mungu, lazima utie katika vitendo maneno Yake, na kuyafuata kwa njia zozote unazoweza. Hili si jambo rahisi!

Iliyotangulia: Kuhusu Mungu Kumtumia Mwanadamu

Inayofuata: Ufalme wa Milenia Umewasili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp