Kuhusu Mungu Kumtumia Mwanadamu
Watu hawawezi kuishi kwa kujitegemea, isipokuwa wale wanaopewa mwelekeo na mwongozo maalum na Roho Mtakatifu. Wote wanahitaji huduma na uchungaji wa wale wanaotumiwa na Mungu, kwa hivyo katika kila enzi Mungu huwainua watu tofauti ambao hujishughulisha huku na kule kwa ajili ya kazi Yake ili kuchunga makanisa. Yaani, kazi ya Mungu lazima ifanywe kupitia wale ambao Yeye anawatazama kwa upendeleo na kuwaona kuwa wanastahili; Roho Mtakatifu lazima afanye kazi kupitia sehemu iliyo ndani yao inayostahili kutumiwa, na wanafanywa kufaa kutumiwa na Mungu kupitia kufanywa kuwa watimilifu na Roho Mtakatifu. Kwa sababu uwezo wa kufahamu wa mwanadamu ni wenye upungufu sana, lazima achungwe na wale wanaotumiwa na Mungu; hii ni sawa tu na jinsi Mungu alivyomtumia Musa, ambaye ndani yake Alipata mengi yaliyofaa kutumiwa wakati huo, na ambayo Yeye aliyatumia kufanya kazi ya Mungu katika hatua hiyo. Katika hatua hii, Mungu anamtumia mwanadamu huku pia akitumia fursa ya sehemu yake inayoweza kutumiwa na Roho Mtakatifu ili kufanya kazi, na Roho Mtakatifu anamwelekeza na wakati huo huo anaifanya kuwa timilifu sehemu iliyosalia, isiyoweza kutumiwa.
Kazi inayofanywa na yule anayetumiwa na Mungu ni ili kushirikiana na kazi ya Kristo au Roho Mtakatifu. Mtu huyu anainuliwa na Mungu miongoni mwa wanadamu ili kuwaongoza watu wote wateule wa Mungu, na pia anainuliwa na Mungu ili kufanya kazi ya ushirikiano wa kibinadamu. Kukiwa na mtu kama huyu, ambaye anaweza kufanya kazi ya ushirikiano wa kibinadamu, matakwa mengi zaidi ya Mungu kwa mwanadamu, na kazi ambayo Roho Mtakatifu lazima afanye miongoni mwa wanadamu, inaweza kutimizwa kupitia kwake. Njia nyingine ya kusema hili ni kama hivi: lengo la Mungu katika kumtumia mtu huyu ni ili wale wote wanaomfuata Mungu waweze kuelewa nia za Mungu vyema zaidi, na waweze kufikia matakwa ya Mungu kwa kiwango kikubwa zaidi. Kwa sababu watu hawawezi kuelewa moja kwa moja maneno ya Mungu au nia za Mungu, Mungu amemwinua mtu ambaye anatumiwa kutekeleza kazi kama hiyo. Mtu huyu anayetumiwa na Mungu pia anaweza kuelezwa kama chombo ambacho kwacho Mungu anawaongoza watu, kama "mkalimani" anayewasilisha maelezo kati ya Mungu na mwanadamu. Hivyo, mtu kama huyo ni tofauti na mfanyakazi au mtume yeyote katika nyumba ya Mungu. Wote wanaweza kusemwa kuwa watu wanaomhudumia Mungu, lakini katika kiini cha kazi yake na usuli wa yeye kutumiwa na Mungu, mtu huyu anatofautiana sana na wafanyakazi na mitume wengine. Kwa upande wa kiini cha kazi yake na usuli wa kutumiwa kwake, mtu anayetumiwa na Mungu anainuliwa na Yeye, anatayarishwa na Mungu kwa ajili ya kazi ya Mungu, na anashirikiana na kazi ya Mungu Mwenyewe. Hakuna mtu ambaye anaweza kufanya kazi yake badala yake—ni ushirikiano wa kibinadamu ambao ni wa lazima kabisa pamoja na kazi ya kiungu. Wakati huo huo, kazi inayofanywa na wafanyakazi au mitume wengine, ni uwasilishaji na utekelezaji tu wa vipengele vingi vya mipango kwa ajili ya makanisa katika kila kipindi, au vinginevyo kazi ya ugavi rahisi wa uzima ili kudumisha maisha ya kanisa. Wafanyakazi na mitume hawa hawateuliwi na Mungu, sembuse wao kuitwa wale wanaotumiwa na Roho Mtakatifu. Wanachaguliwa kutoka miongoni mwa makanisa na, baada ya wao kufunzwa na kustawishwa kwa kipindi cha muda fulani, wale wanaofaa kutumiwa wanabakizwa, huku wale wasiofaa wakirudishwa kule walikotoka. Kwa sababu watu hawa wanachaguliwa kutoka miongoni mwa makanisa, wengine huonyesha tabia zao halisi baada ya kuwa viongozi, na wengine hata hufanya mambo mengi mabaya na kuishia kuondoshwa. Kwa upande mwingine, mtu anayetumiwa na Mungu, ni mtu ambaye ametayarishwa na Mungu, na ambaye ana ubora fulani wa tabia, na ana ubinadamu. Ametayarishwa na kufanywa kuwa mtimilifu kabla na Roho Mtakatifu, na anaongozwa kikamilifu na Roho Mtakatifu, na, hasa linapokuja suala la kazi yake, anaelekezwa na kutawaliwa na Roho Mtakatifu—kutokana na hili, njia anayowaongoza watu wateule wa Mungu kuifuata haina mkengeuko, kwa maana hakika Mungu anawajibikia kazi Yake Mwenyewe, na Mungu hufanya kazi Yake Mwenyewe nyakati zote.