Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu Mwenye Mwili na Wajibu wa Mwanadamu

Ni lazima myafahamu maono ya kazi ya Mungu na mpate mwelekeo wa kazi Yake. Huku ni kuingia kwa njia nzuri. Punde unapong’amua ukweli wa maono kwa usahihi, kuingia kwako kutakuwa salama; bila kujali kazi Yake hubadilika kiasi gani, utaendelea kuwa imara moyoni mwako, utakuwa wazi kuhusu maono, na utakuwa na lengo la kuingia na kufuatilia kwako. Kwa njia hiyo, uzoefu na ufahamu ulio ndani yako utakua kwa kina na kutakaswa zaidi. Punde unapong’amua taswira nzima kwa ukamilifu, hutapoteza kitu maishani na hutapotea. Kama hutazijua hatua hizi za kazi, utapata hasara kwa kila mojawapo. Huwezi kugeuka baada ya siku chache tu na hutaweza kuipata njia mwafaka hata katika majuma machache. Je, si hili linakurudisha nyuma? Kuna zaidi katika kuingia kwa njia nzuri dhahiri na vitendo ambavyo mnapaswa kuving’amua, na vilevile unapaswa kuelewa mambo kadha katika maono ya kazi Yake kama vile umuhimu wa kazi Yake ya ushindi, njia ya kufanywa mkamilifu katika siku za usoni, kinachofaa kupatikana kupitia uzoefu wa majaribu na masaibu, umuhimu wa hukumu na kuadibu, kanuni za kazi ya Roho Mtakatifu, na kanuni za ukamilifu na ushindi. Huu wote ndio ukweli wa maono. Hayo mengine ni hatua tatu za kazi ya Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema na Enzi ya Ufalme pamoja na ushuhuda wa baadaye. Huu pia ni ukweli kuhusiana na maono, na ni wa msingi na muhimu sana pia. Kwa sasa, kuna mengi sana mnayopaswa kuingia kwayo na kutenda, na kwa sasa yana safu nyingi na maelezo ya kina. Kama huna ufahamu wa ukweli huu, ni thibitisho kwamba bado hujaingia. Mara nyingi, ufahamu wa mwanadamu kuhusu ukweli huwa wa juujuu; mwanadamu hushindwa kuweka ukweli wa kimsingi katika vitendo na hajui jinsi ya kushughulikia hata maswala madogo. Sababu ya mwanadamu kushindwa kutenda ukweli ni tabia yake ya uasi, na kwa sababu ufahamu wake kuhusu kazi ya sasa ni wa juu juu na wa kuegemea upande mmoja. Kwa hivyo, si kazi rahisi kwa mwanadamu kufanywa mkamilifu. Uasi wako ni wa hali ya juu sana, na unashikilia sana hali yako ya zamani; huwezi kusimama katika upande wa ukweli, na huwezi kutenda hata ukweli ulio wazi. Wanadamu kama hao hawawezi kuokolewa na ni wale ambao hawajashindwa. Kama kuingia kwako hakuna kina au malengo, kukua kwako kutakujia polepole. Kama kuingia kwako hakuna uhalisi hata kidogo, basi kufuatilia kwako kutakuwa bure. Kama hujui kiini cha ukweli, hutabadilishwa. Ukuaji katika maisha ya mwanadamu na mabadiliko katika tabia zake hupatikana kwa kuingia ndani ya ukweli na, zaidi ya hili, kwa kuingia katika uzoefu wa kina. Ukiwa na uzoefu wa kina katika wakati wa kuingia kwako, na ukiwa na ufahamu halisi kuhusu kuingia, tabia yako itabadilika haraka. Hata kama kwa sasa hujapata nuru sana katika vitendo, unafaa angalau upate nuru ya maono ya kazi. La sivyo utashindwa kuingia, na hutaweza kufanya hivyo isipokuwa uufahamu ukweli. Ni baada ya kuangaziwa nuru na Roho Mtakatifu katika uzoefu wako ndipo utakapopata ufahamu wa kina kuhusu ukweli na uingie kwa kina. Ni sharti uifahamu kazi ya Mungu.

Baada ya uumbaji wa mwanadamu hapo mwanzoni, Waisraeli ndio waliokuwa kielelezo cha kazi, na Israeli nzima ilikuwa ngome ya kazi ya Yehova duniani. Kazi ya Yehova ilikuwa imwongoze mwanadamu moja kwa moja na kumchunga kwa kuweka wazi sheria ili kwamba mwanadamu aweze kuishi maisha ya kawaida na kumwabudu Yehova kwa njia ya kawaida duniani. Katika Enzi ya Sheria Mungu alikuwa Asiyeonekana wala kuguswa na mwanadamu. Alikuwa tu Anawaongoza wanadamu waliokuwa mwanzo wamepotoshwa na Shetani, na Alikuwepo kuwaagiza na kuwaongoza wanadamu, kwa hivyo maneno yote Aliyoyanena yalikuwa ya kisheria, amri na maarifa ya kawaida ya kuishi maisha kama mwanadamu, na wala sio kuhusu ukweli unaomruzuku mwanadamu. Waisraeli chini ya uongozi Wake hawakuwa wale waliopotoshwa zaidi na Shetani. Kazi Yake ya sheria ilikuwa tu hatua ya kwanza kabisa katika kazi ya ukombozi, mwanzo hasa wa kazi ya wokovu, na haikuwa inahusiana kamwe na mabadiliko katika tabia za kimaisha za mwanadamu. Kwa hivyo, mwanzoni mwa kazi ya ukombozi hapakuwa na haja Kwake kuwa katika mwili kwa ajili ya kazi Yake katika Israeli. Ndiyo maana Alihitaji kiungo, yaani, chombo ambacho kwacho Angemfikia mwanadamu. Kwa hivyo kukazuka miongoni mwa viumbe waliozungumza na kufanya kazi kwa niaba ya Yehova, na hivi ndivyo wana wa wanadamu na manabii walikuja kufanya kazi miongoni mwa wanadamu. Wana wa Adamu walifanya kazi miongoni mwa wanadamu kwa niaba ya Yehova. Ili waitwe na Yeye inamaanisha kuwa hao watu walipanga sheria kwa niaba ya Yehova na walikuwa miongoni mwa watu wa Israeli; na watu kama hao walikuwa makasisi walioangaliwa na kulindwa na Yehova, na Roho wa Yehova alifanya kazi ndani yao; walikuwa viongozi miongoni mwa wanadamu na wahudumu wa Yehova wa moja kwa moja. Manabii kwa upande mwingine ndio waliokuwa na jukumu la kunena na mataifa na makabila yote kwa niaba ya Yehova. Ndio vilevile waliotoa unabii kuhusu kazi ya Yehova. Wawe wanadamu au manabii, wote waliinuliwa na Roho wa Yehova Mwenyewe na walikuwa na kazi ya Yehova ndani yao. Miongoni mwa wanadamu, walikuwa ndio wale waliomwakilisha Yehova moja kwa moja; walifanya kazi tu kwa kuwa waliinuliwa na Yehova wala si kwa kuwa walikuwa miili ambamo Roho mtakatifu Mwenyewe alikuwa kapata mwili. Kwa hivyo, ingawa wao walifanya kazi na kuongea kwa niaba ya Mungu, hao wana wa mwanadamu na manabii wa Enzi ya Sheria hawakuwa mwili wa Mungu mwenye mwili. Hii ilikuwa kinyume hasa katika Enzi ya Neema na hatua ya mwisho, kwani kazi ya ukombozi na hukumu ya mwanadamu vilifanywa na Mungu katika mwili Mwenyewe, na hapakuwa na haja ya kukuza manabii na wanadamu kufanya kazi kwa niaba Yake. Machoni pa mwanadamu, hamna tofauti kubwa kati ya kiini na mbinu za kazi zao. Ni kwa sababu hii ndiyo mwanadamu anachanganya kati ya kazi ya Mungu mwenye mwili na ile ya manabii na wanadamu. Kimsingi, umbo la Mungu mwenye mwili lilikuwa sawa na lile la manabii na wanadamu. Mungu mwenye mwili alikuwa wa kawaida na halisi zaidi kuliko manabii. Kwa hivyo mwanadamu anashindwa kabisa kuwatofautisha. Mwanadamu huangazia maumbile peke yake bila kugundua kuwa japo wote hufanya kazi na kuongea, kuna tofauti kubwa kati yao. Kwa sababu uwezo wa mwanadamu wa kung’amua ni duni, mwanadamu anashindwa kung’amua mambo ya kimsingi na hata zaidi hawezi kubainisha kitu changamano. Maneno na kazi za manabii na za wale waliotumiwa na Roho Mtakatifu zote zilikuwa zinafanya wajibu wa mwanadamu, kutekeleza jukumu lake kama kiumbe na kufanya ambacho mwanadamu anapaswa kufanya. Hata hivyo, maneno na kazi za Mungu mwenye mwili ilikuwa ni kuendeleza huduma Yake. Ingawa umbo Lake lilikuwa lile la kiumbe, kazi Yake haikuwa kutimiza majukumu Yake bali Huduma Yake. Dhana “wajibu” inarejelea viumbe ilhali “huduma” inarejelea mwili wa Mungu mwenye mwili. Kuna tofauti kubwa kati ya haya mawili, na haya mawili hayabadilishani nafasi. Kazi ya mwanadamu ni kufanya wajibu wake, ilhali kazi ya Mungu ni kusimamia, na kuendeleza huduma Yake. Kwa hivyo, ingawa mitume wengi walitumiwa na Roho Mtakatifu na manabii wengi wakajazwa na Yeye, kazi zao na maneno yao yalikuwa tu kutimiza wajibu wao kama viumbe. Ingawa unabii wao ungeweza kuwa mkubwa kuliko maisha kama yanavyozungumziwa na Mungu mwenye mwili, na hata ubinadamu wao ulikuwa wa hali ya juu kuliko wa Mungu kuwa mwenye mwili, walikuwa bado wanafanya wajibu wao na wala si kutimiza huduma yao. Wajibu wa mwanadamu unarejelea majukumu yake, na ni kitu kinachoweza kupatwa kwa mwanadamu. Hata hivyo, huduma ifanywayo na Mungu mwenye mwili inahusiana na usimamizi Wake, na haiwezi kufanikishwa na mwanadamu. Hata kama Mungu mwenye mwili hunena, kufanya kazi, au kutenda miujiza, Anafanya kazi kubwa katika usimamizi Wake, kazi ambayo haiwezi kufanywa na mwanadamu kwa niaba Yake. Kazi ya mwanadamu ni kufanya tu wajibu wake kama kiumbe katika hatua fulani ya usimamizi wa Mungu. Bila usimamizi kama huo, yaani, ikiwa huduma ya Mungu mwenye mwili itapotea, pia wajibu wa viumbe utapotea. Kazi ya Mungu kuendeleza huduma Yake ni kumsimamia mwanadamu, ilhali mwanadamu afanyapo wajibu wake ni kutimiza wajibu wake ili kuafikia masharti ya Muumba na haiwezi kwa vyovyote vile kuchukuliwa kwamba ameendeleza huduma ya mtu yeyote. Kwa kiini asili cha Mungu, yaani, Roho, kazi ya Mungu ni usimamizi wake, bali kwa Mungu mwenye mwili akiwa na umbile la nje la kiumbe, kazi yake ni kuendeleza huduma Yake. Kazi yoyote Aifanyayo ni ya kuendeleza huduma Yake, na mwanadamu anaweza tu kufanya awezalo ndani ya upeo Wake wa usimamizi na chini ya uongozi Wake.

Mwanadamu kufanya wajibu wake ni, kwa uhakika, kutimiza yote yaliyo ya asili yake, yaani, yale yawezekanayo kwa mwanadamu. Hapo ndipo wajibu wake hutimizika. Dosari za mwanadamu wakati wa huduma ya mwanadamu hupunguzwa taratibu kupitia kwa uzoefu uongezekao na mchakato wa uzoefu wake wa hukumu; hayazuii au kuathiri wajibu wa mwanadamu. Wanaoacha kutoa huduma au kuzalisha na kurudi nyuma kwa kuogopa makosa yanayoweza kuwepo katika huduma ndio waoga zaidi miongoni mwa wanadamu wote. Ikiwa mwanadamu haonyeshi anachopaswa kuonyesha wakati wa kutoa huduma au kutimiza kile kilicho katika uwezo wake kiasili, na badala yake huzembea na kufanya tu bila ari yoyote, atakuwa amepoteza majukumu yake ambayo kiumbe anapaswa kuwa nayo. Mwanadamu kama huyu anachukuliwa kuwa mtu hafifu na duni apotezaye nafasi; itakuaje kwamba mtu kama huyu aitwe kiumbe? Je, hao si ni vyombo vya upotovu ving’aavyo kwa nje ila vimeoza kwa ndani? Ikiwa mwanadamu atajiita Mungu lakini hawezi kuonyesha uungu na kufanya kazi ya Mungu Mwenyewe, au amwakilishe Mungu, bila shaka si Mungu kwani hana sifa za Mungu, na kile ambacho Mungu Anaweza kukitimiza hakimo ndani yake. Mwanadamu akipoteza kile ambacho chaweza kutimizwa kiasili, hawezi kamwe kuitwa mwanadamu, na hafai kusimama kama kiumbe aliyeumbwa au kuja mbele za Mungu na kumtolea huduma. Aidha, hafai kupokea neema ya Mungu au kutunzwa, kulindwa na kukamilishwa na Mungu. Wengi waliopoteza imani ya Mungu hatimaye hupoteza neema Yake. Si kwamba wanachukia makosa yao tu bali pia hueneza wazo kuwa njia ya Mungu si sahihi. Na wale waasi hupinga hata uwepo wa Mungu; itakuwaje watu wenye uasi kama huo waendelee kupata neema ya Mungu? Wanadamu walioshindwa kutekeleza wajibu wao wameasi sana dhidi ya Mungu na wanawiwa mengi na Yeye, lakini wanageuka na kumkong'ota Mungu kwamba ni mkosaji. Je, mwanadamu kama huyo anastahili vipi kufanywa mkamilifu? Je, si huyu ni mmoja wa wale watakaoondolewa na kuadhibiwa? Mwanadamu asiyefanya wajibu wake mbele za Mungu tayari ana hatia ya makosa mazito sana ambayo hata kifo si adhabu stahili, ila bado mwanadamu ana ufidhuli wa kubishana na Mungu na kujilinganisha na Yeye. Pana faida gani kumkamilisha mwanadamu sampuli hiyo? Kama mwanadamu ameshindwa kutekeleza wajibu wake, anafaa kujihisi mwenye hatia na mdeni; anapaswa kuudharau udhaifu wake na kukosa umuhimu, uasi na uharibifu wake, na zaidi ya hayo, anafaa kujitolea maisha na damu sadaka kwa ajili ya Mungu. Hapo tu ndipo atakapokuwa kiumbe ampendaye Mungu kwa kweli, na ni mwanadamu kama huyu tu anayestahili baraka na ahadi za Mungu, na kukamilishwa na Yeye. Na wengi wenu je? Mnamtendeaje Mungu aishiye miongoni mwenu? Mmefanyaje wajibu wenu mbele Zake? Je, mmefanya yote mliyoitwa kufanya, hata kwa gharama ya maisha yenu? Mmetoa sadaka gani? Je, hamjapokea mengi kutoka Kwangu? Mnaweza kuonyesha tofauti? Mna uaminifu kiasi gani Kwangu? Mmenitolea huduma vipi? Na kuhusu yote Niliyowapa na kuwafanyia je? Je, mmeyazingatia yote? Je, mmeyahukumu na kuyalinganisha haya yote kwa dhamiri yoyote ndogo mliyo nayo? Maneno na matendo yenu yanawezaje kuwa ya kustahili? Je, yawezekana hizo sadaka zenu kidogo zinalingana na yote Niliyowapa? Sina chaguo jingine na Nimejitolea kwenu kwa moyo wote, na bado mna nia zenye uovu kunihusu na hamnipendi kwa dhati. Huo ndio upeo wa wajibu wenu, jukumu lenu la pekee. Au sivyo? Hamjui kwamba hamjatimiza wajibu wa kiumbe aliyeumbwa hata kidogo? Mnawezaje kuchukuliwa kama kiumbe aliyeumbwa? Je, hamjui wazi mnachopaswa kuonyesha nakuishi kwa kudhihirisha katika maisha yenu? Mmeshindwa kutimiza wajibu wenu, ila mnataka mpate huruma na neema tele za Mungu. Neema hiyo haijaandaliwa kwa wasio na thamani na wa hali duni kama nyinyi, bali kwa wale ambao hawaombi kitu ila wanatoa kwa moyo wa dhati. Wanadamu kama nyinyi, watu duni, hawastahili kufurahikia neema ya mbinguni. Ni ugumu tu wa maisha na adhabu isiyokoma vitayaandama maisha yenu! Ikiwa hamwezi kuwa waaminifu Kwangu, majaaliwa yenu yatakuwa matatizo. Ikiwa hamwezi kuyawajibikia maneno Yangu na kazi Yangu, kundi lenu litakuwa la kuadhibiwa. Kamwe hamtapata neema, na hamtakuwa na baraka na maisha ya kupendeza katika ufalme. Hii ndiyo hatima na matokeo mnayostahili kupata kwa kujitakia! Hao watu wapumbavu na mafidhuli hawajafanya kila wawezalo wala kutimiza wajibu wao tu, bali wameinyoosha mikono yao wakitaka neema, kana kwamba wanastahili wanachoitisha. Na wakishindwa kupata wanachokiomba, wanakuwa wakosa imani zaidi. Watu kama hao wanawezaje kuchukuliwa kuwa wenye mantiki? Ninyi ni sampuli mbaya isiyokuwa na urazini, isiyoweza kabisa kutimiza wajibu mnaotakiwa kutimiza wakati wa kazi ya usimamizi. Thamani yenu tayari imeshuka pakubwa. Kushindwa kwenu kunilipa kwa kuwaonea imani tayari ni tendo la uasi mkuu litoshalo kuwahukumu na kuthibitisha uoga, uovu, uzembe na uduni wenu. Mnawezaje kuendelea kustahili kunyoosha mikono yenu? Hamwezi kuwa hata wa msaada kidogo kwa kazi Yangu, hamwezi kuahidi imani yenu, na hamwezi kunitolea ushuhuda. Tayari haya ni makosa na kushindwa kwenu, na bado mnanivamia, mnanisemea uongo na kulalama kuwa Mimi si mwenye haki. Je, huu ndio uaminifu wenu? Huu ndio upendo wenu? Ni kazi gani nyingine mnayoweza kufanya zaidi ya hii? Mmechangia vipi katika kazi yote ambayo imeishafanywa? Mmegharamia kiasi gani? Ni huruma kubwa tayari kwamba bado Sijawawekea lawama, na bado mnanipa visingizio na kulalama faraghani kunihusu. Kweli mna hata chembe ndogo ya ubinadamu? Ingawa wajibu wa mwanadamu umetiwa doa na fikira za mwanadamu na mitazamo yake, ni sharti ufanye wajibu wako na kuwa mwaminifu kwa imani yako. Uchafu katika kazi ya mwanadamu ni suala la ubora wa tabia yake, ilhali, ikiwa mwanadamu hafanyi wajibu wake, unajisi huu unaonyesha uasi wake. Hakuna uhusiano kati ya wajibu wa mwanadamu na endapo amebarikiwa au amelaaniwa. Wajibu ni kile ambacho mwanadamu anapaswa kutimiza; ni wajibu wake na hautegemei fidia, masharti, au sababu. Hapo tu ndipo huko kutakuwa kufanya wajibu wake. Mwanadamu aliyebarikiwa hufurahia wema baada ya kufanywa mkamilifu baada ya hukumu. Mwanadamu aliyelaaniwa hupokea adhabu tabia yake isipobadilika hata baada ya kutiwa adabu na kuhukumiwa, yaani, hajakamilishwa. Kama kiumbe, mwanadamu anapaswa kutimiza wajibu wake, afanye anachopaswa kufanya, na afanye anachoweza kufanya, bila kujali kama atabarikiwa au kulaaniwa. Hili ndilo sharti la msingi kwa mwanadamu, kama anayemtafuta Mungu. Usifanye wajibu wako ili ubarikiwe tu, na usikatae kutenda kwa kuogopa kupata laana. Acha Niwaambie hiki kitu kimoja: Ikiwa mwanadamu anaweza kufanya wajibu wake, inamaanisha kuwa anafanya anachopaswa kufanya. Ikiwa mwanadamu hawezi kufanya wajibu wake, inaonyesha uasi wake. Kila mara ni katika harakati ya kufanya wajibu wake ndipo mwanadamu polepole anabadilishwa, na ni katika harakati hii ndipo anapoonyesha utiifu wake. Kwa hivyo, kadiri uwezavyo kufanya wajibu wako, ndivyo ukweli utakaopokea unavyoongezeka, na vivyo hivyo mwonekano wako utakuwa halisi zaidi. Wale ambao hufanya tu mambo bila ari yoyote katika kufanya wajibu wao na hawautafuti ukweli mwishowe wataondolewa, kwani watu kama hao hawafanyi wajibu wao katika utendaji wa ukweli, na hawatendi ukweli katika kutekeleza wajibu wao. Watu kama hao ni wale wanaobaki bila kubadilika na watalaaniwa. Misemo yao haijajaa najisi tu, ila wakitamkacho si kingine bali ni uovu.

Katika Enzi ya Neema, Yesu pia Alinena mengi na kufanya kazi nyingi. Alikuwaje tofauti na Isaya? Alikuwaje tofauti na Danieli? Je, Alikuwa nabii? Ni kwa nini inasemekana kwamba Yeye ni Kristo? Kuna tofauti gani baina yao? Wote walikuwa wanadamu walionena maneno, na maneno yao yalionekana sawa kwa wanadamu. Wote walinena na kufanya kazi. Manabii wa Agano la Kale walitoa unabii, na vivyo hivyo, pia na Yesu. Ni kwa nini iwe hivi? Tofauti hapa inapatikana katika aina ya kazi zao. Ili kutambua suala hili, huwezi kuangazia asili ya mwili na hufai kuangazia upurukushani wa maneno ya mtu. Daima ni sharti kwanza uangazie kazi yake na athari ambayo kazi yake inafanikisha ndani ya mwanadamu. Unabii uliotolewa na manabii wakati ule, haukuyaruzuku maisha ya mwanadamu, na ujumbe uliopokelewa na watu kama Isaya na Danieli ulikuwa tu unabii na si njia ya uzima. Ingekuwa si kuonekana moja kwa moja kwa Yehova, hakuna ambaye angefanya hiyo kazi, ambayo haiwezekani kwa wanadamu. Yesu pia Alisema mengi, lakini maneno yake yalikuwa njia ya uzima ambayo kwayo mwanadamu angepata njia ya kutenda. Hii ni kusema kuwa, kwanza, Angeukimu uzima wa mwanadamu, kwa kuwa Yesu ni uzima; pili, Angeweza kuugeuza upotovu wa mwanadamu; tatu, kazi Yake ingeweza kuifuata ile ya Yehova ili kuendeleza enzi; nne, Angeweza kutambua mahitaji ya mwanadamu kwa ndani na kufahamu anachokosa mwanadamu; tano, Angeweza kuanzisha enzi mpya na kutamatisha enzi ya zamani. Ndiyo maana Anaitwa Mungu na Kristo; Yeye si tofauti na Isaya tu; bali pia na manabii wengine wote. Chukua Isaya kama ulinganisho wa kazi za manabii. Kwanza, asingeweza kuukimu uzima wa mwanadamu; pili, asingeweza kuanzisha enzi mpya. Alikuwa akifanya kazi chini ya uongozi wa Yehova wala si kuanzisha enzi mpya. Tatu, alichokizungumza yeye mwenyewe kilikuwa nje ya ufahamu wake. Alikuwa akipata ufunuo moja kwa moja kutoka kwa Roho wa Mungu, na wengine wasingeelewa hata baada ya kuusikiliza ufunuo huo. Haya machache yanatosha kuthibitisha kuwa kazi yake haikuwa zaidi ya unabii, si zaidi ya kazi iliyofanywa kwa niaba ya Yehova. Hata hivyo, asingeweza kumwakilisha Yehova kikamilifu. Alikuwa mtumishi wa Yehova, chombo katika kazi ya Yehova. Aidha alikuwa anafanya kazi katika Enzi ya Sheria tu na katika mawanda ya kazi ya Yehova; hakufanya kazi nje ya Enzi ya Sheria. Kinyume na haya, kazi ya Yesu ilikuwa tofauti. Alivuka mipaka ya kazi ya Yehova; Alifanya kazi kama Mungu mwenye mwili na kupitia mateso ili amkomboe mwanadamu. Hiyo ni kusema kuwa Alifanya kazi mpya nje ya ile iliyofanywa na Yehova. Huku kulikuwa kukaribisha kwa enzi mpya. Jambo jingine ni kuwa Aliweza kuyazungumzia mambo ambayo mwanadamu asingeweza kupata. Kazi Yake ilikuwa kazi ndani ya usimamizi wa Mungu na ilijumuisha wanadamu wote. Hakufanya kazi miongoni mwa watu wachache tu, na wala kazi yake haikuwa kuwaongoza watu wachache tu. Kuhusu jinsi Mungu alivyopata mwili kuwa mwanadamu, jinsi Roho alivyotoa ufunuo wakati ule, na jinsi Roho alivyomshukia mwanadamu kufanya kazi, haya ni mambo ambayo mwanadamu hawezi kuona au kugusa. Haiwezekani kabisa ukweli huu kuwa thibitisho kuwa Yeye ni Mungu mwenye mwili. Kwa sababu hii, tofauti inaweza kupatikana tu kwenye maneno na kazi ya Mungu ambayo ni mambo dhahiri kwa mwanadamu. Hili tu ndilo halisi. Hii ni kwa sababu masuala ya Roho hayaonekani kwako na yanafahamika wazi na Mungu Mwenyewe peke Yake, wala hata mwili wa Mungu haufahamu yote; unaweza kuthibitisha tu kama Yeye ni Mungu[a] kutokana na kazi Aliyoifanya tu. Kutokana na kazi Yake, inaweza kuonekana kuwa, kwanza, Anaweza kufungua enzi mpya; pili, Yeye ana uwezo wa kuyaruzuku maisha ya mwanadamu na kumwonyesha mwanadamu njia ya kufuata. Hii inatosha kuthibitisha kuwa Yeye ni Mungu Mwenyewe. Angalau kazi Aifanyayo yaweza kumwakilisha kikamilifu Roho Mtakatifu wa Mungu na kutokana na kazi hiyo inaonekana kuwa Roho wa Mungu yupo ndani Yake. Kwa kuwa kazi iliyofanywa na Mungu mwenye mwili ilikuwa kuanzisha enzi mpya, kuongoza kazi mpya, na kuanzisha na kufungua mazingira mapya, haya mambo machache tu yanatosha kuthibitisha kuwa Yeye ni Mungu Mwenyewe. Hili kwa hivyo linamtofautisha na Isaya, Danieli, na manabii wengine wakuu. Isaya, Danieli na wengine wote walikuwa ni watu walioelimika na kustaarabika vilivyo; walikuwa watu wa kipekee chini ya uongozi wa Yehova. Mwili wa Mungu mwenye mwili pia ulikuwa na maarifa na haukupungukiwa na akili ila ubinadamu Wake ulikuwa wa kawaida. Alikuwa mwanadamu wa kawaida na jicho la mwanadamu lisingeweza kubaini ubinadamu wowote wa pekee kumhusu au kugundua kitu chochote katika ubinadamu Wake tofauti na wa wale wengine. Kamwe hakuwa kabisa wa kimiujiza au wa kipekee na hakuwa na elimu ya juu, ujuzi au nadharia kupita kiasi. Maisha Aliyoyazungumzia na njia Aliyoenenda hakuipata kinadharia, kielimu, kitajriba au kupitia malezi ya kifamilia. Badala yake, ilikuwa kazi ya moja kwa moja ya Roho, ambayo ni kazi ya mwili. Ni kwa kuwa mwanadamu ana mawazo makuu kumhusu Mungu, na hasa kwa kuwa fikira hizi hutungwa kutokana na vipengele vingi visivyo yakini na vya kimiujiza hivi kwamba, katika macho ya mwanadamu, Mungu wa kawaida mwenye udhaifu wa kibinadamu, ambaye hawezi kutenda miujiza, kwa hakika si Mungu. Je, si hizi ni fikra potovu za mwanadamu? Mwili wa Mungu mwenye mwili usingekuwa wa kawaida, basi ingesemekanaje kwamba Alipata mwili? Kupata mwili ni kuwa mtu wa kawaida; iwapo angekuwa wa kupita uwezo wa binadamu, basi Asingeweza kuwa wa kimwili. Kuthibitisha kuwa Yeye ni wa kimwili, Mungu mwenye mwili alihitaji kuwa na mwili wa kawaida. Hili lilikusudiwa tu kutimiza umuhimu wa kupata mwili. Hata hivyo, mambo hayakuwa hivyo kwa manabii na wanadamu. Walikuwa wanadamu waliopewa vipawa na kutumiwa na Roho Mtakatifu; machoni mwa mwanadamu, ubinadamu wao ulikuwa wa hali ya juu, walitenda matendo mengi yaliyovuka mipaka ya ubinadamu wa kawaida. Kwa sababu hii mwanadamu aliwachukulia kama Mungu. Sasa ni sharti nyote mlione hili kwa uwazi zaidi, kwani limekuwa jambo ambalo liliwakanganya sana wanadamu wote katika enzi zilizopita. Aidha, kuwa mwili ndicho cha ajabu zaidi kwa vitu vyote, na Mungu mwenye mwili ni vigumu zaidi kukubaliwa na mwanadamu. Ninachokisema kinasaidia katika kutimiza majukumu yenu na kuelewa kwenu kwa fumbo la kupata mwili. Haya yote yanahusiana na usimamizi wa Mungu, kwa maono. Ufahamu wenu wa hili jambo utakuwa wa faida zaidi kwa kupata ufahamu wa maono, yaani kazi ya usimamizi. Kwa njia hii, mtafahamu zaidi pia wajibu ambao wanadamu mbalimbali wanafaa kutekeleza. Ingawa maneno haya hayawaonyeshi njia moja kwa moja, bado ni msaada mkubwa kwa kuingia kwenu, kwa kuwa maisha yenu ya sasa yamepungukiwa sana na maono na hili litakuwa kikwazo kikubwa kinachozuia kuingia kwenu. Kama hamjaweza kuyafahamu masuala haya, basi hakutakuwa na motisha ya kuchochea kuingia kwenu. Na kufuatilia kama huku kunawezaje kuwawezesha kutimiza wajibu wenu vyema zaidi?

Tanbihi:

a. Maandiko asili hayana kauli “kama Yeye ni Mungu.”

Iliyotangulia: Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake Ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu

Inayofuata: Mungu Ndiye Bwana wa Viumbe Vyote

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp