Sura ya 8

Ufunuo Wangu unapofika upeo wake, na hukumu Yangu inapomalizika, utakuwa wakati ambapo watu Wangu wote wanafichuliwa na kufanywa wakamilifu. Ninasafiri kila pembe ya ulimwengu dunia katika hali ya kutafuta wale wanaolingana na nia Yangu na wanastahili kwa matumizi Yangu. Nani anaweza kusimama na kushirikiana na Mimi? Upendo wa mwanadamu Kwangu ni mdogo mno na imani yake Kwangu ni ndogo ajabu. Kama sehemu kubwa ya maneno Yangu haingeelekezwa kwa udhaifu wa mwanadamu, angejigamba na kutia mambo chumvi, na angehubiri na kubuni nadharia zenye kuvutia, kana kwamba ni mwenye maarifa yote na anayejua yote kuhusu mambo ya ulimwengu. Kati ya wale waliokuwa “waaminifu” Kwangu hapo awali, na wale “wanaosimama imara” leo Yangu, ni nani anayethubutu kuongea kwa kujigamba? Nani asiyefurahia matarajio yake mwenyewe kisiri? Wakati Sikufichua waziwazi, mwanadamu hakuwa na mahali pa kujificha na aliteswa na aibu. Ingekuwa mbaya zaidi kiasi gani wakati Mimi ninapozungumza kupitia mbinu nyingine? Wanadamu wangekuwa na hisia hata kubwa zaidi za kuwa wadeni, wangeamini kwamba hakuna kitu ambacho kingeweza kuwatibu, na wote wangefungwa vizuri na kutokuwa na hisia kwao. Mwanadamu anapopoteza matumaini, saluti ya ufalme husikika rasmi, ambayo ni “wakati ambapo Roho aliyeongezwa nguvu mara saba Huanza kufanya kazi,” kama ilivyosemwa na mwanadamu, kwa maneno mengine, wakati maisha ya ufalme huanza kwa urasmi duniani, yaani, wakati uungu Wangu huja kufanya kazi moja kwa moja (bila kufikiriwa na ubongo). Watu wote wanakuwa na shughuli nyingi kama nyuki; inaonekana ni kana kwamba wamefufuliwa, kana kwamba wameamshwa kutoka ndotoni, na punde wanapoamka, wanapigwa na butwaa kwa kujikuta katika hali kama hizo. Katika siku za awali, Nilisema mengi kuhusu ujenzi wa kanisa, Nilifichua siri nyingi, na wakati ujenzi wa kanisa ulifika kilele chake, ulifika kikomo cha ghafla. Hata hivyo, ujenzi wa ufalme ni tofauti. Wakati vita katika ulimwengu wa kiroho vinapofika hatua yake ya mwisho tu ndipo Nianzapo upya duniani. Yaani, ni wakati tu mwanadamu anapokaribia kurudi nyuma ndipo Ninaanza rasmi na kuinua kazi Yangu mpya. Tofauti kati ya ujenzi wa ufalme na ujenzi wa kanisa ni kwamba, katika ujenzi wa kanisa, Nilifanya kazi katika ubinadamu ulioongozwa na uungu. Nilishughulika moja kwa moja na asili ya zamani ya mwanadamu, Nilifichua nafsi mbaya ya mwanadamu moja kwa moja, na kuweka wazi kiini cha mwanadamu. Kwa sababu hii, mwanadamu alikuja kujijua mwenyewe kwa msingi huu, na hivyo waliridhishwa moyoni mwao na katika neno. Katika ujenzi wa ufalme, Natenda moja kwa moja katika hali ya uungu Wangu, na kuruhusu watu wote kujua kile Nilicho nacho na Nilicho kwa msingi wa maarifa ya maneno Yangu, hatimaye kuwaruhusu kutimiza ufahamu kunihusu Mimi kama mwili halisi. Hivyo hukamilisha ufuatiliaji wote wa binadamu wa Mungu asiye dhahiri, na hivyo basi huacha kushikilia nafasi ndani ya nyoyo zao ya Mungu aliye mbinguni; yaani, Ninamruhusu mwanadamu ajue matendo Ninayotenda Nikiwa mwenye mwili, na hivyo nitahitimisha wakati Wangu duniani.

Ujenzi wa ufalme unalenga ulimwengu wa kiroho moja kwa moja. Kwa maneno mengine, vita vya ulimwengu wa kiroho vimewekwa wazi moja kwa moja miongoni mwa watu Wangu wote, na kutoka kwa hii inaweza kuonekana kwamba watu wote daima wamo vitani, sio tu katika kanisa, lakini hata zaidi katika Enzi ya Ufalme, na kwamba hata ingawa mwanadamu yuko katika mwili, ulimwengu wa kiroho unafichuliwa moja kwa moja, na mwanadamu anajihusisha na maisha ya ulimwengu wa kiroho. Hivyo, mnapoanza kuwa waaminifu, lazima mjiandae vizuri kwa ajili ya sehemu inayofuata ya kazi Yangu. Mnapaswa kutoa moyo wenu wote, na ni kwa kufanya hivi tu ndio mnaweza kukidhi moyo Wangu. Sijali kuhusu chochote ambacho mwanadamu alifanya hapo awali katika kanisa; leo, ni katika ufalme. Katika mpango Wangu, Shetani amewahi kushindana na kila hatua, na, kama foili[a] ya hekima Yangu, amejaribu siku zote kutafuta njia na namna za kuvuruga mpango Wangu wa awali. Lakini Ningeweza kushindwa na njama zake danganyifu? Vyote mbinguni na duniani vinanitumikia—njama danganyifu za Shetani zingeweza kuwa tofauti? Huku ndiko hasa kukutana kwa hekima Yangu, ndiyo hasa yaliyo ya ajabu kuhusu matendo Yangu, na ni kanuni ya utendaji ya mpango Wangu mzima wa usimamizi. Katika enzi ya ujenzi wa ufalme, bado Mimi siepuki njama danganyifu za Shetani, ila Naendelea kufanya kazi ambayo lazima Nifanye. Kati ya ulimwengu na vitu vyote, Nimechagua matendo ya Shetani kama foili Yangu. Je, hii si hekima Yangu? Je, si haya ndiyo hasa yaliyo ya ajabu kuhusu kazi Yangu? Wakati wa kuingia katika Enzi ya Ufalme, mabadiliko makubwa mno hutokea katika vitu vyote mbinguni na duniani, na wao husherehekea na kufurahia. Je, nyinyi mna tofauti yoyote? Ni nani asiyejisikia mtamu kama asali katika moyo wake? Ni nani asiyebubujikwa na furaha katika moyo wake? Ni nani asiyecheza kwa furaha? Ni nani asiyesema maneno ya sifa?

Katika yote Niliyonena na kusema kuhusu hapo juu, je, mnafahamu malengo na asili ya matamko Yangu, au la? Kama Singeuliza swali hili, watu wengi wangeamini kuwa Ninabubujikwa na maneno tu, na hawangeweza kutambua chanzo cha maneno Yangu. Mkiyatafakari kwa makini, mtajua umuhimu wa maneno Yangu. Ungefanya vyema kuyasoma kwa karibu: Ni yapi yasiyo ya faida kwako? Ni yapi yasiyo kwa ajili ya ukuaji wa maisha yako? Ni yapi yasiyozungumzia hali halisi ya ulimwengu wa kiroho? Watu wengi sana wanaamini kwamba hakuna maana katika maneno Yangu, ya kuwa hayana maelezo na tafsiri yoyote. Je, maneno Yangu kweli ni ya dhahania na yasiyoeleweka sana? Je, mnatii maneno Yangu kwa kweli? Je, mnayakubali maneno Yangu kwa kweli? Je, hamyachukulii kama kidude cha watoto kuchezea? Je, huyatumii kama mavazi ya kuficha sura yako mbaya? Katika dunia hii kubwa, ni nani amechunguzwa na Mimi binafsi? Ni nani ameyasikia maneno ya Roho Wangu mwenyewe? Watu wengi sana hututusa na kutafuta gizani; wengi sana huomba wakiwa kwenye shida; wengi sana, wakiwa na njaa na baridi, wengi sana wamefungwa na Shetani, ilhali wengi sana hawajui pa kugeukia, wengi sana hunisaliti wakiwa katika furaha, wengi sana hawana shukrani, na wengi sana ni waaminifu kwa njama danganyifu za Shetani. Nani kati yenu ni Ayubu? Nani ni Petro? Kwa nini Nimetaja mara kwa mara jina la Ayubu? Na mbona Nimemtaja Petro mara nyingi? Je, mmewahi kufahamu matumaini Yangu kwenu? Mnapaswa kuchukua muda zaidi kuwaza mambo ya aina hii.

Petro alikuwa mwaminifu Kwangu kwa miaka mingi, lakini hakunung’unika wala kuwa na moyo wa kulalamika kamwe, na hata Ayubu hakuwa sawa na yeye. Katika enzi zote, watakatifu wote, pia, hawajamfikia hata kidogo. Yeye hakufuatilia kunijua Mimi tu, lakini pia alipata kunijua wakati ambapo Shetani alikuwa anatekeleza njama zake danganyifu. Hii ilisababisha miaka mingi ya huduma iliyoupendeza nafsi Yangu, na kwa sababu hii Shetani hakumnyonya kamwe. Petro alitumia imani ya Ayubu, ilhali yeye pia alifahamu wazi upungufu wake. Ingawa Ayubu alikuwa na imani kubwa, alikosa ufahamu wa masuala katika ulimwengu wa kiroho, na hivyo alisema maneno mengi ambayo hayakulingana na hali halisi; hii inaonyesha kwamba ufahamu wake bado haukuwa wa kina, na haukuwa na uwezo wa kufanywa kuwa kamilifu. Na hivyo, Petro siku zote alitazamia kufahamu roho, na daima alilenga kuchunguza mienendo ya ulimwengu wa kiroho. Kwa sababu hii, hakuwa tu na uwezo wa kutambua matakwa Yangu kiasi, lakini pia alielewa kidogo juu ya njama danganyifu za Shetani, na hivyo ufahamu wake kuhusu Mimi ulikuwa mkubwa zaidi kuliko mwingine wowote katika enzi zote.

Kutokana na matukio ya Petro si vigumu kuona kwamba mtu akitaka kunijua, lazima awe makini kwa kuzingatia kwa uangalifu katika roho. Sikuombi kwamba utoe kiasi kikubwa Kwangu kwa nje; hili ni la umuhimu wa ziada. Iwapo hunijui, basi imani, upendo na uaminifu wote unaozungumzia ni ndoto tu, ni upuuzi, na wewe hakika utakuwa mtu ambaye ana majivuno makubwa mbele Zangu lakini hajijui mwenyewe, na hivyo wewe utanaswa tena na Shetani na hutaweza kujinasua; utakuwa mwana wa kuteseka milele, na utakuwa mlengwa wa maangamizi. Lakini kama wewe huna hisia na hujali kuhusu maneno Yangu, basi bila shaka unanipinga Mimi. Huu ni ukweli, na ingekuwa vyema utazame kupitia lango la ulimwengu wa kiroho uone roho nyingi na tofautitofauti zilizoadibiwa na Mimi. Ni wapi kati yao hawakukaa tu na hawakujali, na hawakuyakubali maneno Yangu? Ni wapi kati yao hawakuwa na shaka kwa maneno Yangu? Ni yupi kati yao hakujaribu kutafuta makosa katika maneno Yangu? Ni wapi kati yao hawakuyatumia maneno Yangu kama silaha ya kujikinga itakayotumiwa kujilinda? Wao hawakutafuta kunijua kwa njia ya maneno Yangu, lakini waliyatumia kama vitu vya kuchezea tu. Katika hili, je, si wao walinipinga moja kwa moja? Nani ni maneno Yangu? Nani ni Roho Wangu? Mara nyingi Mimi nimeyanena maneno haya kwenu, lakini maono yenu yamewahi kuwa ya kiwango cha juu na yenye uwazi? Matukio yenu yamewahi kuwa ya kweli? Nawakumbusha mara nyingine: Iwapo hamyajui maneno Yangu, hamyakubali, na hamyaweki katika matendo, basi bila shaka mtaadibiwa na Mimi! Nyinyi kwa hakika mtakuwa waathirika wa Shetani!

Februari 29, 1992

Tanbihi:

a. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.

Iliyotangulia: Sura ya 7

Inayofuata: Sura ya 9

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp