Asili na Utambulisho wa Mwanadamu

Kwa kweli, Waisraeli hawajasikitika, wameing’amua kazi ambayo inafanywa na Mungu kwa miaka elfu sita, mpaka hivi sasa, kwa kuwa Sikuwaacha. Badala yake, kwa sababu mababu zao walikula tunda kutoka kwa mti wa ujuzi wa mema na maovu lililotolewa na yule mwovu, waliniacha kwa ajili ya dhambi. Mema ni Yangu, wakati maovu ni ya yule mwovu ambaye hunirairai kwa ajili ya dhambi. Mimi Simlaumu mwanadamu, wala Simwangamizi kwa ukatili au kumtolea kuadibu kusiko na huruma, kwani uovu haukuwa wa wanadamu kiasili. Kwa hivyo ingawa wale Waisraeli walinipigilia misumari msalabani hadharani, wao, ambao wamekuwa wanamngoja Masiha na Yehova na kumtamani sana Mwokozi Yesu, hawajasahau ahadi Yangu. Hii ni kwa sababu Sijawatelekeza. Hata hivyo, Nilikuwa nimechukua damu kama ushahidi wa agano Nililoanzisha na mwanadamu. Ukweli huu umekuwa agano la damu lililoandikwa katika mioyo ya watu wachanga na wasio na hatia, kana kwamba lilichapiliwa, na kama kuishi kwa pamoja kwa amani kwa mbingu na dunia milele. Sijawahi kuzidanganya nafsi hizo za huzuni Nilizoziokoa, kuzipata, na ambazo hunipenda zaidi ya yule mwovu baada ya Mimi kuzijaalia na kuzichagua. Kwa hiyo, kwa shauku zinatazamia kurudi Kwangu na kwa hamu zinatarajia kukutana na Mimi. Kwa kuwa Sijawahi kufuta agano Nililoanzisha nazo kwa damu, si ajabu kwamba zimekuwa zikisubiri kwa hamu. Nitawateka tena wanakondoo hawa ambao wamepotea kwa miaka, kwa maana siku zote Nimewapenda mwanadamu. Ni kwamba tu dalili za uovu zimeongezwa kwa wema katika wanadamu. Nitazipata zile nafsi hafifu ambazo zinanipenda na ambazo Nimezipenda tayari, lakini Nawezaje kuwaleta wale waovu ambao hawajawahi kunipenda na wametenda kama adui ndani ya nyumba Yangu? Sitawaleta wazawa wa Shetani na nyoka mwenye sumu kali ambao hunichukia, hunipinga, hunikataa, hunishambulia, na kunilaani ndani ya ufalme Wangu, hata ingawa Nimeanzisha agano la damu na mwanadamu. Unapaswa kujua kwa nini na kwa ajili ya nani Ninatekeleza kazi hiyo. Je, ni wema au uovu katika upendo wako? Je, kwa kweli unanijua kama vile walivyonijua Daudi na Musa? Je, kwa kweli unanihudumia kama vile alivyonihudumia Ibrahimu? Ni kweli kwamba unafanywa kamili na Mimi, lakini unapaswa kujua ni nani utakayemwakilisha na ni nani utakayekuwa na matokeo sawa na. Katika maisha yako, una mavuno ya furaha na mengi katika kupata uzoefu wa kazi Yangu? Je, ni mengi na yenye matokeo mazuri? Unapaswa kujichunguza mwenyewe. Kwa miaka umefanya kazi kwa bidii kwa ajili Yangu, lakini umewahi kupata chochote? Umebadili au kupata kitu chochote? Badala ya uzoefu wako katika shida, je, unakuwa kama Petro ambaye alisulubiwa, au kama Paulo ambaye alibwagwa na kupokea mwanga mkubwa? Unapaswa kuwa na ufahamu wa haya. Mimi sizungumzi siku zote juu ya, na kufikiria kuhusu maisha yako ambayo ni madogo kuliko mbegu ya haradali, ambayo ni ukubwa wa punje ya mchanga. Kusema kweli, ni mwanadamu ambaye Ninasimamia. Hata hivyo, Sifikirii maisha ya mwanadamu, ambaye wakati mmoja Nilimchukia lakini baadaye Nikamwinua tena, kama sehemu muhimu ya usimamizi Wangu. Unapaswa kuwa mwenye uhakika juu ya utambulisho wako wa zamani kwa kweli ulikuwa upi, na ni nani mliyemtumikia kama watumwa. Kwa hiyo, Situmii nyuso za wanadamu kama ya Shetani kama mali ghafi kuwasimamia, kwa kuwa wanadamu si vitu vya thamani. Mnapaswa kukumbuka mtazamo Wangu kwenu hapo mwanzoni, na hotuba Yangu kwenu wakati huo ambayo haikuwa bila umuhimu wa utendaji. Unapaswa kujua kwamba zile “kofia” juu ya vichwa vyenu zina msingi. Ninadhani kwamba nyote mnajua kwamba hamkuwa wa Mungu kwa asili, lakini mlikamatwa na Shetani zamani na kutumikia nyumbani kwake kama watumishi waaminifu. Mmenisahau kwa muda mrefu, kwani kwa muda mrefu mmekuwa nje ya nyumba Yangu lakini mikononi mwa yule mwovu. Wale ambao Mimi huokoa ni wale ambao Nimewaamulia kabla zamani na wamekombolewa na Mimi, wakati ninyi ni nafsi hafifu ambazo zimewekwa kati ya wanadamu kama jambo la pekee. Mnapaswa kujua kwamba nyinyi si wa nyumba ya Daudi au Yakobo, lakini ni wa nyumba ya Moabu, ambao ni wanachama wa kabila la Mataifa. Kwa maana Sikuanzisha agano na nyinyi, lakini Nilitekeleza tu kazi na kunena kati yenu, na kuwaongoza. Damu Yangu haikumwagika kwa ajili yenu. Nilitekeleza tu kazi kati yenu kwa ajili ya ushuhuda Wangu. Je, hamjajua hilo? Je, kazi Yangu kweli ni kama Yesu kumwaga damu hadi kufa kwa niaba yenu? Haikuwa na thamani kwamba Nilivumilia fedheha kubwa kwa ajili yenu. Mungu, ambaye hana dhambi kabisa, Alikuja moja kwa moja kwa pahali panapochukiza na kukirihi kabisa, dunia ya nguruwe na mbwa ambayo haikufaa kwa binadamu kuishi, lakini bado Nilivumilia hii aibu yote ya ukatili kwa ajili ya utukufu wa Baba Yangu na kwa ajili ya ushuhuda wa milele. Mnapaswa kujua mienendo yenu na kuona kwamba nyinyi si watoto waliozaliwa katika “familia tajiri na yenye nguvu” bali watoto fukara tu wa Shetani. Nyinyi si waanzilishi kati ya wanadamu, na hamna haki za kibinadamu au uhuru. Kwa asili, hamkuwa na mgao wowote kabisa la baraka kutoka kwa binadamu au ufalme wa mbinguni. Hili ni kwa sababu mko chini kabisa ya binadamu katika wanadamu, na Sijawahi kufikiria kuhusu wakati wenu ujao. Kwa hivyo, ingawa ilikuwa sehemu ya asili ya mpango Wangu kwamba leo Ningekuwa na imani kuwakamilisha, ni kazi ya pekee, kwa sababu hadhi yenu ni ya chini sana na kiasili hamkuwa na mgawo katika binadamu. Je, hii si baraka kwa wanadamu?

Wale Ninaowaokoa ni nafsi ambazo Nilizitoa kutoka toharani zamani, na waliochaguliwa ambao Nilitembelea zamani, kwa kuwa wametamani sana kuonekana Kwangu tena kati yao. Wamenipenda, na wameandika agano Langu ambalo Nilianzisha kwa damu katika mioyo yao, kwa sababu Nimewapenda. Wao ni kama kondoo waliopotea ambao wamekuwa wakinitafuta kwa miaka mingi, na wao ni wazuri, na kwa hivyo Ninawaita Waisraeli wazuri na malaika wadogo wanaopendeza. Singepitia aibu kama hii iwapo Ningekuwa miongoni mwao. Ni kwa sababu wananipenda zaidi kuliko wanavyopenda maisha yao wenyewe, na Ninawapenda kama kile ambacho ni kirembo zaidi kati ya vitu vyote. Ni kwa sababu waliumbwa na Mimi na ni Wangu; hawajawahi kunisahau. Upendo wao unazidi upendo wenu, na wananipenda kwa upendo mkubwa zaidi kuliko mnavyopenda maisha yenu wenyewe. Wananitii Mimi kama vile njiwa wadogo weupe hufanyia anga, na kwa upendo mkubwa zaidi kuliko mnavyonifanyia. Na ni kwa sababu wao ni wazawa wa Yakobo, watoto wa Adamu, na ni miongoni mwa wateule Wangu, kwa kuwa Nimewapenda zamani, na hata zaidi kuliko Ninavyowapenda, na kwa sababu nyinyi ni waasi sana, upinzani wenu ni mkubwa sana, mnaniangalia kwa dharau sana, hamnithamini hata kidogo Kwangu, mnanipenda kidogo sana, na mnanichukia sana. Mnadharau kazi Yangu, na kutweza vitendo Vyangu sana. Tofauti na wao, hamjawahi kuona matendo Yangu kuwa kitu cha thamani. Badala yake, mnayadharau na macho mekundu ya wasiwasi, kama tu Shetani. Utiifu wenu uko wapi? Tabia zenu ziko wapi? Upendo wenu uko wapi? Ni lini mmeonyesha wazi dalili ya upendo ndani yenu? Ni lini mmechukua kazi Yangu kwa uzito kabisa? Hurumia wale malaika wa kupendeza ambao kwa wasiwasi wananitazamia na kuteseka sana wakati wanaponisubiri kwa wasiwasi, kwani Ninawapenda kwa dhati. Hata hivyo, kile Ninachokiona leo ni ulimwengu usio wa kibinadamu sana ambao hauhusiani nao. Je, hamfikirii kuwa dhamiri zenu zilikuwa zisizojali na zisizo na huruma muda mrefu uliopita? Je, hamfikirii kuwa nyinyi ndio watu duni mnaozuia kurudiana Kwangu na malaika wa kupendeza? Ni lini hawajakuwa wakisubiri kurudi Kwangu? Ni lini hawajakuwa wakisubiri kuungana tena na Mimi? Je, ni lini hawajatarajia kushinda kwa siku nzuri na kula pamoja na Mimi? Je, mliwahi kutambua kile mfanyacho leo—yaani, kufanya ghasia ulimwenguni, kupanga njama dhidi ya nyinyi kwa nyinyi, kudanganyana, kutenda kwa uongo, kwa siri na kwa ukavu wa macho, kutojua ukweli, kuwa wasio waaminifu na wadanganyifu, kutenda ubembelezaji, nyinyi kujiona daima kuwa waadilifu na bora zaidi kuliko wengine, kuwa wenye kiburi, na kutenda kikatili kama wanyama wa mwitu milimani na kwa fujo kama mfalme wa wanyama—huu ndio mfano wa mwanadamu? Nyinyi ni fidhuli na wasio na busara. Hamjawahi kuliona neno Langu kuwa hazina, lakini badala yake mmechukua mtazamo wa dharau. Kwa njia hii, mafanikio, maisha ya kweli ya binadamu, na matumaini mazuri yangetoka wapi? Je, wazo lako badhirifu litakuokoa kwa kweli kutoka kwa kinywa cha chui? Kweli litakuokoa kutoka kwa moto unaowaka? Je, ungekuwa umeanguka hadi hapa iwapo kwa kweli ungeiona kazi Yangu kuwa kitu cha thamani kubwa mno? Inaweza kuwa kwamba majaliwa yako kweli hayawezi kubadilishwa? Je, uko tayari kufa na majuto kama haya?

Iliyotangulia: Kusudi la Kuwasimamia Binadamu

Inayofuata: Utambulisho wa Asili wa Mwanadamu na Thamani Yake: Je, Viko Namna Gani?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp