Sura ya 1

Je, wale wanaoshuhudia maneno Yangu huyakubali kwa kweli? Je, mnanijua kwa kweli? Mmejifunza utiifu kweli? Ninyi hutumia rasilimali kwa ajili Yangu kwa uaminifu? Mmekuwa na ushuhuda thabiti, usiokubali kushindwa Kwangu mlipokabiliwa na joka kuu jekundu? Je, moyo wenu wa ibada hulifedhehesha kweli joka kuu jekundu? Ni kupitia tu kwa jaribio la maneno Yangu ndipo Naweza kutimiza lengo Langu la kulitakasa kanisa na kuwachagua wale wanaonipenda Mimi kweli. Nisingetenda kwa njia hii, kuna yeyote angenijua Mimi? Ni nani angeweza kujua uadhama Wangu, ghadhabu Yangu, na hekima Yangu kupitia kwa maneno Yangu? Nitakamilisha Nilichoanza, lakini bado ni Mimi nipimaye mioyo ya wanadamu. Kwa kweli, hakuna mwanadamu anayenielewa Mimi kwa ukamilifu, kwa hiyo Ninamwongoza kwa maneno, na kumwongoza katika mwongo mpya kwa njia hii. Mwishowe Nitatumia maneno kukamilisha kazi Yangu yote, Nikiwafanya wale wote wanaonipenda kwa dhati kurudi kwa ufalme Wangu kwa utiifu, kuishi mbele ya kiti Changu cha enzi. Hali sio kama ilivyokuwa wakati fulani, na kazi Yangu imeingia katika kiwango kipya cha kuanza. Hilo likiwa hivyo, kutakuwa na njia mpya: Wale wanaolisoma neno Langu na kulikubali kama uzima wao kabisa ndio watu wa ufalme Wangu. Kwa vile wako katika ufalme Wangu, wao ni watu Wangu katika ufalme. Kwa sababu wanaongozwa na maneno Yangu, ingawa wanatajwa kama watu Wangu, jina hili si la chini ya kuitwa “wana” Wangu. Baada ya kufanywa kuwa watu wa Mungu, wote ni lazima wawe waaminifu katika ufalme Wangu na kutimiza majukumu yao, na wale wanaokosea amri Zangu za usimamizi lazima wapate adhabu Yangu. Hili ni onyo Langu kwa wote.

Kwa sasa njia mpya inatumika, yale yote kutoka wakati uliopita hayahitaji kusemwa tena. Hata hivyo, Nimeyasema maneno haya: Kile Nilichosema lazima kihesabiwe, kile kilichohesabiwa lazima kikamilishwe, na hili haliwezi kubadilishwa na yeyote; hili ni thabiti. Kama ni kile Nilichosema katika wakati uliopita au Nitakachosema katika siku za usoni, yote yatatimia, na wanadamu wote wataliona hili. Hii ni kanuni inayoelekeza maneno na kazi Yangu. Tangu ujenzi wa kanisa tayari umetimizwa, sasa sio tena enzi ya ujenzi wa kanisa, lakini badala yake ni enzi ambayo kwayo ufalme unajengwa kwa ufanisi. Hata hivyo, kwa vile bado mko duniani, makusanyiko yenu yatabaki kujulikana kama “kanisa.” Hata hivyo, kiini cha kanisa sio kama kilivyokuwa wakati fulani, na kimeonyesha ufanisi wa kweli. Kwa hivyo, Nasema kwamba ufalme Wangu umeshuka duniani. Hakuna anayeweza kuelewa kiini cha maneno Yangu, wala hawezi kufahamu kusudi la maneno hayo. Ninapozungumza leo, mnaweza kupitia epifania. Labda wengine wataangua kilio; baadhi huenda wakahisi woga kwamba hivi ndivyo Mimi huzungumza. Baadhi huenda wakashikilia maoni ya mtindo wa zamani wanapotazama kila hatua Yangu; baadhi huenda wakajuta kwa baada ya kueleza malalamiko yao au kunipinga Mimi wakati ule. Kwangu; wengine huenda wakafurahia kimoyomoyo, kwani hawajawahi kupotea kutoka kwa jina Langu, na sasa leo wamehuishwa; labda watu wengine waliochacharishwa na maneno Yangu zamani sana, na wanakaribia kifo, wamevunjika moyo na ni wenye huzuni, hawana tena moyo wa kuyasikia maneno Niyazungumzayo, hata Nikichagua njia tofauti ya kueleza. Huenda kuna wengine ambao wamejitolea sana Kwangu hata hawajawahi kulalamika, wasioshuku kamwe, leo wana bahati sana kupata kufunguliwa na kuhisi shukrani isiyoelezeka ndani ya mioyo yao Kwangu. Hali hizi zote zilizotajwa zinaweza kutumika kwa viwango tofauti tofauti, kwa kila binadamu. Lakini kama vile wakati uliopita ni wakati uliopita, na sasa ni wakati uliopo, hakuna haja ya kutamani tena wakati uliopita, au kuwa na wasiwasi kuhusu siku za usoni. Miongoni mwa wanadamu, wale wanaoenda kinyume cha uhalisi na hawafanyi mambo kulingana na uongozi Wangu hawatakuwa na mwisho mzuri, na watajiletea tu matatizo. Kwa kila kitu kinachotokea ulimwenguni, hakuna kitu Nisichokuwa na usemi wa mwisho kukihusu. Ni kitu gani kilichopo ambacho hakiko mikononi Mwangu? Chochote Nisemacho hufanyika, na miongoni mwa wanadamu, ni nani aliyepo anayeweza kuyabadilisha mawazo Yangu? Yaweza kuwa agano Nililofanya juu ya dunia? Hakuna chochote kinachoweza kuuzuia mpango Wangu; Mimi huwepo wakati wote katika kazi Yangu na vilevile katika mpango wa usimamizi Wangu. Ni mwanadamu gani anaweza kuingilia? Je, sio Mimi binafsi Niliyetengeneza mipango hii? Kuingia katika hali hii leo, bado haipotei kutoka kwa mpango Wangu au Nilichoona mbele; yote iliamuliwa Nami zamani sana. Ni nani miongoni mwenu anaweza kufahamu mpango Wangu wa hatua hii? Watu Wangu wataisikiliza sauti Yangu, na kila mmoja wa wale wanaonipenda kwa kweli atarudi mbele ya kiti Changu cha enzi.

Februari 20, 1992

Iliyotangulia: Utangulizi

Inayofuata: Sura ya 2

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp