68 Furaha Katika Nchi ya Kanaani

1

Kurudi nyumbani kwa Mungu,

nahisi furaha na msisimko.

Nina bahati kuona hatimaye

Mwenyezi Mungu wa vitendo.

Maneno Yake huwaongoza watu kuingia

katika Enzi ya Ufalme.

Maneno Yake yananionyesha njia,

na naielewa njia

ninayopaswa kuchukua kama mtu.

Nchi ya Kanaani ni ufalme wa Kristo.

Upendo wetu Kwake ni mtamu,

pendo hili linatufanya tucheze kwa furaha.

Katika nchi ya Kanaani,

watu wa Mungu watamwabudu milele.


2

Sitafutitafuti tena,

ndoto yangu ya ufalme wa mbinguni

hatimaye imetimia.

Nimenyunyiziwa na Mungu

kwa maji yaishiyo ya uzima.

Kuwa ana kwa ana na Yeye ni starehe,

starehe isiyo na kifani.

Nchi nzuri ya Kanaani

ndiyo dunia ya maneno ya Mungu.

Nchi ya Kanaani ni ufalme wa Kristo.

Upendo wetu Kwake ni mtamu,

pendo hili linatufanya tucheze kwa furaha.

Katika nchi ya Kanaani,

watu wa Mungu watamwabudu milele.

Nimehudhuria karamu ya Mwanakondoo,

na maisha ndani ya upendo wa Mungu ni raha.

Nimekubali mafunzo ya vitendo

ya ufalme wa Kristo.

Ingawa nimepitia bonde la machozi,

upendo ambao Mungu alinipa ni halisi sana.

Moyo wangu unatakaswa na shida na majaribu.

Hayo hufanya upendo wangu Kwake kuwa safi.

Unakua siku baada ya siku.


3

Upendo kwa Mungu huujaza moyo wangu kwa shangwe.

Mungu ni mwaminifu na mwenye haki sana,

anayenipendeza na kunivutia.

Jinsi inavyopendeza sana

tabia ya Mungu!

Imewekwa kwa uthabiti moyoni mwangu.

Siwezi kupenda kwa nguvu ya kutosha

utakatifu na uzuri wa Mungu.

Kwa hivyo nimejaa nyimbo zinazomsifu.

Nchi ya Kanaani ni ufalme wa Kristo.

Upendo wetu Kwake ni mtamu,

pendo hili linatufanya tucheze kwa furaha.

Katika nchi ya Kanaani,

watu wa Mungu watamwabudu milele.


4

Nyota zinanitabasamia kutoka angani.

Mwangaza wa jua unaangaza kote duniani.

Umande hufanya kila kitu kiwe kilowe.

Maneno ya Mungu, ya fahari yasiyo na kifani,

yako nami kunisaidia nikue na nguvu.

Karamu yetu ni tamu sana,

Ruzuku tele ya Mungu hutuletea utajiri.

Maisha duniani ni kama mbinguni tu,

watu wote wa Mungu wanaishi kando Yake.

Katika nchi ya Kanaani,

hakuna huzuni au machozi.

Hayo ni maisha yetu milele,

maisha yetu mbele za Mungu.

Hatutawahi kutengana naye!

Mpendwa wangu, siwezi kusema vya kutosha

juu ya kupendeza Kwako.

Hukumu Yako ni yenye haki na takatifu,

hutakasa na kuusafisha moyo wangu.

Maneno Yako ni matamu sana, sana,

huchangamsha moyo wangu, hulichochea pendo langu.

Sasa maisha yangu ni mazuri sana.

Kwa sababu naweza kukupenda sasa,

moyo wangu unafurahia siku nzima.

Naomba niwe nawe katika maisha haya.

Nchi ya Kanaani ni ufalme wa Kristo.

Upendo wetu Kwake ni mtamu,

pendo hili linatufanya tucheze kwa furaha.

Katika nchi ya Kanaani,

watu wa Mungu watamwabudu milele.

Nchi ya Kanaani ni ufalme wa Kristo.

Upendo wetu Kwake ni mtamu,

pendo hili linatufanya tucheze kwa furaha.

Katika nchi ya Kanaani,

watu wa Mungu watamwabudu milele.

Iliyotangulia: 67 Imba na Kucheza katika Sifa kwa Mungu

Inayofuata: 70 Msifu Mungu Kwa Moyo Mmoja

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

137 Nitampenda Mungu Milele

1Ee Mungu! Maneno Yako yananiita nirudi Kwako.Nakubali kufundishwa katika ufalme Wako mchana na usiku.Mara nyingi sana nilikuwa dhaifu na...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki