7 Ufalme Mtakatifu Umeonekana

1

Mungu mwenye mwili amewasili kati ya wanadamu,

na hukumu imeanza na nyumba ya Mungu.

Tunainuliwa mbele ya kiti Chake kuhudhuria

karamu ya harusi ya Kristo, Mwenyezi Mungu.

Hukumu inatutakasa, hubadilisha tabia yetu.

Tumezaliwa upya na kuwa watu wapya.

Kwa kumcha Mungu, tunasujudu mbele Yake,

tukisifu utakatifu na haki Yake.

Tukiwa tayari kutii na kutoa uaminifu wetu,

tunatimiza wajibu wetu kwa uaminifu.

Mungu, tunakupenda kwa mioyo yetu yote,

na milele tunakuimbia sifa zetu.

Ufalme mtakatifu umeonekana

Ufalme mtakatifu umeonekana.

2

Mungu anaonyesha ukweli kuuhukumu ulimwengu

na kufichua kikamilifu haki Yake.

Nguvu mbaya zinazompinga Mungu,

zitaangamizwa na majanga makubwa.

Sasa Mungu amefanya kila kitu kipya

kwa matumizi na starehe Yake.

Hii siyo tena nchi chafu, ya uasherati,

bali ni ufalme mtakatifu milele.

Neno la Mungu limekamilisha kila kitu,

Mungu anatawala kama Mfalme ulimwenguni.

Mungu amepata utukufu Wake kikamilifu

Ufalme wa Kristo umeonekana duniani.

Ufalme mtakatifu umeonekana.

Ufalme mtakatifu umeonekana.

3

Jua la haki linang'aa juu ya nchi nzima,

na vitu vyote vinafufuliwa.

Watu wa Mungu wakusanyika kwa furaha,

wakiimba na kucheza katika ushindi Wake.

Wote wasifu mafanikio Yake makubwa.

Ulimwengu wote umejawa shangwe na kicheko.

Kila kitu chenye pumzi kinaimba sifa za Mungu,

kwa kuwa Amerudi kwa ushindi kamili.

Ulimwengu mzima umefanywa upya,

na tunasherehekea siku ya utukufu wa Mungu.

Sauti za sifa zinaipasua anga,

tunamwimbia Mungu sifa bila kukoma.

Ufalme mtakatifu umeonekana.

Ufalme mtakatifu umeonekana.

Iliyotangulia: 6 Kristo wa Siku za Mwisho, Wokovu wa Mwanadamu

Inayofuata: 8 Ufalme wa Kristo Umeshuka Duniani

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp