Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (3)

Matokeo ya kutimizwa kutoka kwa kazi ya kushinda kimsingi ni kwa ajili ya mwili wa mwanadamu kuacha kuasi, yaani, ili fikira za mwanadamu zipate ufahamu mpya wa Mungu, moyo wake umtii Mungu kabisa, na aamue kuwa wa Mungu. Watu hawahesabiwi kuwa walioshindwa wakati ambapo ambapo mwenendo ama mwili wao unapobadilika; wakati ambapo fikira, ufahamu, na utambuzi wa mwanadamu unabadilika, ambayo ni kusema, wakati ambapo mwelekeo wako wote wa akili unabadilika—huo utakuwa wakati ambapo umeshindwa na Mungu. Ukiamua kutii na kupata fikira mpya, pale ambapo huingizi mawazo na nia zako katika maneno na kazi ya Mungu, na wakati ubongo wako unaweza kufikiri kwa njia ya kawaida, yaani, unapoweza kujitolea kwa Mungu kwa moyo wako wote—huyu ni mtu aliyeshindwa kabisa. Katika ulimwengu wa dini, watu wengi huteseka pakubwa maishani mwao mwote, kwa kuihini miili yao au kuubeba msalaba wao, au hata kuteseka na kustahimili hadi pumzi zao za mwisho! Wengine huwa wanafunga hadi siku ya kifo chao. Katika maisha yao yote wanajinyima chakula kizuri na mavazi mazuri, wakisisitiza mateso tu. Wanaweza kuihini miili yao na kuinyima miili yao. Uwezo wao wa kustahimili mateso unastahili sifa. Ila fikira zao, mawazo yao, mielekeo yao ya kiakili, na kwa hakika asili yao ya kale, havijashughulikiwa hata kidogo. Hawana ufahamu wowote wa kweli kujihusu. Picha ya Mungu akilini mwao ni ile ya kijadi na ya kidhahania, Mungu asiye yakini. Uamuzi wao wa kuteseka kwa ajili ya Mungu unaletwa na azma na asili yao chanya. Hata ikiwa wanamwamini Mungu, hawamfahamu Mungu wala kuyafahamu mapenzi Yake. Wanamfanyia Mungu kazi na kumtesekea Mungu kama vipofu. Hawawekei utambuzi thamani yoyote na hawajishughulishi na jinsi ambayo huduma yao inatimiza mapenzi ya Mungu kwa kweli. Aidha hawajui jinsi ya kutimiza ufahamu kuhusu Mungu. Mungu wanayemhudumia si Mungu katika sura Yake ya asili, ila ni Mungu waliyejifikiria, Mungu waliyemsikia, au Mungu wa kihadithi wanayemsoma katika maandiko. Kisha wanatumia mawazo yao dhahiri na mioyo yao ya kiungu kumtesekea Mungu na kuifanya kazi ambayo Mungu anapaswa kufanya. Huduma yao haiko sahihi, kiasi kwamba hakuna yeyote kati yao anayeweza kuhudumu kulingana na mapenzi ya Mungu. Haijalishi wako radhi kiasi gani kuteseka, mitazamo yao asilia ya huduma na picha ya Mungu akilini mwao havibadiliki kwani hawajapitia hukumu ya Mungu na kuadibu na usafishaji Wake na ukamilifu, na kwa sababu hakuna yeyote aliyewaongoza na ukweli. Japo wanasadiki kwa Yesu Mwokozi, hamna kati yao aliyewahi kumwona Mwokozi. Wamemsikia tu kwa hadithi na uvumi. Hivyo huduma yao ni sawa na kuhudumu mara mojamoja macho yao yakiwa yamefungwa kama kipofu anayemhudumia baba yake. Ni nini kinaweza kupatikana kutokana na huduma kama hiyo? Na ni nani anaweza kuikubali? Huduma yao haibadiliki kamwe toka mwanzo hadi mwisho. Wanapokea mafunzo ya kibinadamu na kukita huduma yao katika uasili wao na kile wanachokipenda wao. Hili laweza kuzalisha faida gani? Hata Petro, aliyemwona Yesu, hakujua jinsi ya kumhudumia Mungu kwa njia inayotimiza mapenzi ya Mungu. Ni katika uzee wake ndipo alipopata ufahamu. Hili linaonyesha nini kuhusu wanadamu vipofu ambao hawajapitia ushughulikiaji na hawana upogoaji na ambao hawajawahi kupata yeyote wa kuwaongoza? Je, si huduma ya wengi miongoni mwenu leo ni kama ile ya vipofu? Wale wote ambao hawajapokea hukumu, hawajapokea upogoaji na ushughulikiaji, na hawana mabadiliko—je, wao si waliokosa kushindwa kabisa? Wana manufaa gani watu kama hao? Ikiwa fikira zako, ufahamu wako wa maisha, na ufahamu wako wa Mungu hauonyeshi mabadiliko mapya na hautoi faida hata kidogo, hutatimiza chochote kizuri katika huduma yako. Bila maono na bila ufahamu mpya wa kazi ya Mungu, huwezi kuwa mtu aliyeshindwa. Njia yako ya kumfuata Mungu itakuwa kama ile ya wale wanaoteseka na kufunga—itakuwa ya thamani ndogo! Hii ni kwa sababu kuna ushuhuda kidogo katika yale wayafanyayo ndipo Nasema huduma yao ni bure! Wanashinda maisha yao wakiteseka na kukaa gerezani; ni wastahimilivu, wenye upendo daima na wao daima hubeba msalaba, wao hukejeliwa na kukataliwa na dunia, wao hupitia kila aina ya ugumu, na ingawa wao ni watiifu hadi mwisho kabisa, bado hawajashindwa, na hawawezi kutoa ushuhuda kuhusu kushindwa. Wameteseka si haba, ila kwa ndani hawamfahamu Mungu kabisa. Hakuna fikira zao za zamani, mawazo ya zamani, vitendo vyao, uelewa wa wanadamu, na mawazo ya wanadamu yaliyoshughulikiwa. Kamwe hakuna uelewa mpya ndani yao. Hakuna hata chembe ya ufahamu wao wa Mungu ambao ni wa kweli au ni sahihi. Wamekosa kuyaelewa mapenzi ya Mungu. Je, huku kwaweza kuwa kumhudumia Mungu? Japo ulimfahamu Mungu zamani, tuseme umeudumisha ufahamu huo hadi leo na kuendelea kukita ufahamu wako kuhusu Mungu kwenye fikira na mawazo yako bila kujali Mungu anafanya nini. Yaani, ikiwa huna ufahamu mpya na wa kweli kuhusu Mungu na ukose kutambua sura na tabia ya kweli ya Mungu. Ikiwa ufahamu wako wa Mungu bado unaongozwa na fikira za uhasama na ushirikina na bado una mawazo na fikira za mwanadamu. Ikiwa hii ndiyo hali, basi hujashindwa. Lengo langu la kukwambia maneno haya yote sasa ni kukupa fursa ya kufahamu na kutumia utambuzi huu kukuongoza katika ufahamu sahihi na mpya. Aidha yanalengwa kukuondolea mawazo ya zamani na utambuzi wa zamani ulio nao ili uweze kuwa na ufahamu mpya. Ikiwa unakula na kunywa matamshi Yangu kweli, basi ufahamu wako utabadilika kwa kiwango kikubwa. Bora tu udumishe moyo mtiifu kwa kula na kunywa matamshi ya Mungu, mtazamo wako utabadilika. Bora tu unaweza kukubali kuadibu kwa kila mara, fikira zako za zamani zitabadilika taratibu. Bora tu fikira zako za zamani zimebadilishwa kabisa na kuwa mpya, vitendo vyako vitabadilika ipasavyo. Kwa njia hii, huduma yako itaendelea kuwa yenye malengo zaidi, na itaweza kutimiza mapenzi ya Mungu. Kama unaweza kubadilisha maisha yako, ufahamu wako wa maisha ya binadamu, na mawazo yako mengi kuhusu Mungu, basi uasili wako utadidimia taratibu. Hili, na hakuna jingine ila hili, ndilo tokeo baada ya Mungu kumshinda mwanadamu; haya ndiyo mabadiliko yatakayoonekana ndani ya mwanadamu. Ikiwa katika kumwamini Mungu, yote ujuayo ni kuutiisha na kuuhini mwili wako na kustahimili na kuteseka, na hujui wazi ikiwa unachokifanya ni sawa au la, bila kujali unamfanyia nani kazi, basi vitendo kama hivi vitaletaje mabadiliko?

Mnapaswa kufahamu kuwa Ninachokitarajia kutoka kwenu si kwamba miili yenu iwekwe katika kifungo au bongo zenu zitawaliwe na kuzuiwa kufikiria mawazo dhahania. Hili si lengo la kazi wala kazi inayopaswa kufanywa hivi sasa. Hivi sasa mnahitaji kuwa na ufahamu kutoka kwa mtazamo chanya ili muweze kubadilika wenyewe. Kile mnachohitaji kufanya zaidi ni kujiandaa wenyewe na maneno ya Mungu, kumaanisha kujiandaa kwa ukamilifu na ukweli na maono yaliyo mbele yenu sasa, na kisha mwende mbele na kuyatia katika vitendo. Hili ni jukumu lenu. Siwaambii mtafute na kupata hata mwangaza mkuu zaidi. Kwa sasa ninyi hamna kabisa kimo cha hilo. Kinachohitajika kutoka kwenu ni kufanya yote muwezayo ili kula na kunywa maneno ya Mungu. Mnatakiwa kufahamu kazi ya Mungu na mjue asili yenu, uwezo wenu, na yale maisha yenu ya zamani. Hususan mnapaswa kujua kuhusu vile vitendo vyenu vyenye makosa vya zamani na mienendo yenu ya kibinadamu. Ili Kubadilika, mnapaswa kuanza kwa kubadilisha fikira zenu. Kwanza, badilisha fikira zenu za zamani kwa fikira mpya, na mruhusu fikira zenu mpya ziongoze maneno na matendo yenu na maisha yenu. Hili ndilo ombi kwa kila mtu sasa hivi. Msitende kama kipofu au kufuata kama kipofu. Ni sharti muwe na msingi na lengo. Msijidanganye. Mnapaswa mjue kabisa imani yenu kwa Mungu ni kwa ajili ya nini, ina faida gani, na kitu gani mnachopaswa kuingia kwacho sasa hivi. Ni muhimu kwamba uyafahamu haya yote.

Kile mnachopaswa kuingia ndani sasa hivi ni kuyainua maisha yenu na kukweza uhodari wenu. Kuongezea, mnahitaji kubadilisha hiyo mitazamo ya zamani kutoka kwa siku zenu za zamani, mbadilishe kufikiri kwenu, na mbadilishe fikira zenu. Maisha yenu yote yanahitaji kufanywa upya. Ufahamu wako wa matendo ya Mungu unapobadilika, unapokuwa na ufahamu mpya wa ukweli wa kila anachokisema Mungu, na ufahamu wako wa ndani unapoinuliwa, maisha yako yanabadilika na kuwa bora. Kila kitu kinachofanywa na kusemwa na mwanadamu sasa ni cha utendaji. Haya si mafundisho ya dini, ila kile ambacho watu wanahitaji kwa ajili ya maisha yao na kile wanachopaswa kumiliki. Hili ndilo badiliko linalotokea kwa mwanadamu wakati wa kazi ya kushinda, badiliko ambalo mwanadamu anapaswa kupitia, na ndiyo matokeo baada ya mwanadamu kushindwa. Ukishabadilisha fikira zako, uchukue mwelekeo mpya wa kimawazo, ubadilishe mawazo yako na nia zako na mantiki yako ya zamani, uache mambo yaliyokita mizizi ndani yako, na kupata ufahamu mpya wa imani kwa Mungu, basi, ushuhuda unaotoa utainuliwa na uwepo wako mzima, kwa kweli utakuwa umebadilika. Yote haya ndiyo ya kiutendaji zaidi, halisi zaidi, na vitu vya kimsingi kabisa—vitu vilivyokuwa vigumu kwa mwanadamu kuelewa hapo zamani, na hawakuweza kushughulika navyo. Ndiyo kazi ya kweli ya Roho. Ni vipi hasa ulivyoelewa Biblia zamani? Ulinganishi wa haraka leo utakwambia. Zamani ulikweza Musa, Petro, Paulo, au kauli na mitazamo hiyo yote ya biblia. Sasa, kama ungeambiwa uikweze Biblia, ungefanya hivyo? Ungeona kwamba Biblia ina rekodi nyingi sana zilizoandikwa na mwanadamu na kwamba Biblia ni maelezo tu ya hatua mbili za kazi ya Mungu. Ni kitabu cha historia. Je, hili halina maana kwamba ufahamu wako kuihusu umebadilika? Kama ungeangalia sasa ukoo wa Yesu uliotolewa katika Injili ya Mathayo, ungesema, “Ukoo wa Yesu? Upuuzi! Huu ni ukoo wa Yusufu, si wa Yesu. Hakuna uhusiano kati ya Yesu na Yusufu.” Unapoiangalia Biblia sasa, ufahamu wako kuihusu ni tofauti, kumaanisha mtazamo wako umebadilika, na unaleta ufahamu wa kiwango cha juu zaidi kwayo kuliko wasomi wa dini wa zamani. Mtu fulani anaposema kwamba kuna kitu katika ukoo huu, ungejibu, “Ni nini kiko hapo? Endelea na ufafanue. Yesu na Yusufu hawana uhusiano. Je, hulijui hilo? Je, Yesu anaweza kuwa na ukoo? Yesu anawezaje kuwa na mababu? Anawezaje kuwa uzao wa mwanadamu? Mwili wake ulizaliwa na Maria; Roho Wake ni Roho wa Mungu, si roho ya mwanadamu. Yesu ni Mwana mpendwa wa Mungu, kwa hiyo anaweza kuwa na ukoo? Wakati alipokuwa duniani Hakuwa mshirika wa wanadamu, kwa hiyo Anawezaje kuwa na ukoo?” Unapochambua ukoo na kufafanua ukweli kwa dhahiri, ukishiriki kile ambacho umeelewa, mtu huyo ataachwa ameduwaa. Watu wengine watarejelea Biblia na kukuuliza, “Yesu alikuwa na ukoo. Je, Mungu wako wa leo ana ukoo?” Wewe basi utawaambia ufahamu wako wenye uhalisi zaidi. Kwa njia hii, ufahamu wako utakuwa umepata matokeo. Kwa kweli, Yesu hana uhusiano na Yusufu kabisa na hata zaidi hana uhusiano na Abrahamu. Ni kwamba tu Yesu alizaliwa Israeli. Lakini Mungu si Mwisraeli au uzao wa Waisraeli. Kwa vile tu Yesu alizaliwa Israeli, haimaanishi Mungu ni Mungu wa Waisraeli pekee. Ilikuwa tu kwa kusudi la kazi Yake ndio Alichukua hii hatua ya kupata mwili Mwenyewe. Mungu ni Mungu wa viumbe vyote ulimwenguni. Ni vile tu kwanza Alifanya hatua moja ya kazi katika Israeli na kisha, baadaye, Akaanza kufanya kazi katika nchi za Mataifa. Lakini watu walimdhania Yesu kuwa Mungu wa Waisraeli na zaidi ya hayo walimweka miongoni mwa Waisraeli na miongoni mwa vizazi vya Daudi. Biblia inasema kwamba mwishoni mwa siku, jina la Yehova litakuwa kuu miongoni mwa nchi za Mataifa, kumaanisha Mungu atakuwa akifanya kazi ndani ya nchi za Mataifa katika siku za mwisho. Kwamba alipata mwili Uyahudini wakati huo wa zamani hakuashirii kwamba Mungu anawapenda Wayahudi pekee. Hilo lilitendeka tu kwa sababu kazi ililihitaji. Haiwezi kusemwa kwamba Mungu alitakiwa kupata mwili ndani ya Israeli (kwa sababu Waisraeli walikuwa wateule Wake). Je, wateule wa Mungu hawapatikani katika nchi za Mataifa, pia? Ni baada ya Yesu kumaliza kufanya kazi Uyahudi ndiyo kazi ikapanuka hadi kwa nchi za Mataifa. (Waisraeli waliziita nchi zote nje ya Israeli “nchi za Mataifa.”) Kwa kweli, hizo nchi za Mataifa zilijazwa wateule wa Mungu vilevile; ni kwamba tu hakuna kazi iliyokuwa ikifanywa huko wakati huo. Watu hutilia mkazo kama huo kwa Israeli kwa sababu hatua mbili za kwanza za kazi zilifanyika Israeli ilhali hakuna kazi iliyokuwa ikifanyika katika nchi za Mataifa. Kazi katika nchi za Mataifa inaanza tu leo, na ndiyo maana watu wanaona ugumu kuikubali. Kama unaweza kuelewa kwa dhahiri haya yote, uyakubali sawasawa na kuyatazama mambo haya yote kwa sahihi, utakuwa na ufahamu sahihi wa Mungu wa leo na wa zamani, na utakuwa wa juu zaidi kuliko ufahamu wa Mungu uliomilikiwa na watakatifu kotekote katika historia. Kama wewe hupitia kazi ya leo na kusikia matamko ya Mungu binafsi leo, lakini huna ufahamu kabisa wa ukamili wa Mungu; ukimbizaji wako ukibaki kama ulivyokuwa daima na usibadilishwe na kitu chochote kipya; na hasa ukipitia kazi hii yote ya kushinda, lakini hatimaye hakuna mabadiliko yoyote yanaweza kuonekana ndani yako, basi imani yako si kama ile ya wale ambao hutafuta tu mkate kushibisha njaa yao? Kwa hiyo, kazi ya kushinda haitakuwa imetimiza matokeo yo yote ndani yako. Basi wewe hutakuwa mtu wa kutolewa?

Katika hitimisho la kazi yote ya kushinda, ni muhimu kwamba nyinyi nyote mfahamu kwamba Mungu si Mungu wa Israeli tu, ila ni Mungu wa kila kiumbe. Aliumba wanadamu wote wala si Waisraeli tu. Ukisema kuwa Mungu ni Mungu wa Israeli tu au kwamba haiwezekani Mungu kupata mwili katika taifa lolote lililo nje ya Israeli, basi bado hujafikia ufahamu wowote katika harakati ya kazi ya kushinda na hutambui kamwe kwamba Mungu ni Mungu wako. Kile unachokitambua ni kuwa Mungu alitoka Israeli Akaenda Uchina na Analazimishwa kuwa Mungu wako. Iwapo huu ndio mtazamo wako wa vitu, basi kazi Yangu haijazaa matunda ndani yako na hujaelewa chochote Nilichokisema. Hatimaye, ikiwa utaandika ukoo Wangu, sawa na Mathayo, Nitafutie babu afaaye na Nitafutie mizizi sahihi—ili kwamba Mungu ana koo mbili kwa sababu ya kupata Kwake mwili mara mbili—je, huo hautakuwa mzaha mkubwa zaidi duniani? Wewe “mtu mwenye nia njema” uliyenipatia ukoo, je, huwezi kuwa mtu uliyemgawa Mungu? Je, uko tayari kuubeba mzigo huu wa dhambi? Baada ya hii kazi yote ya kushinda, ikiwa huamini kwamba Mungu ni Mungu wa viumbe wote, ikiwa bado unadhani kwamba Mungu ni Mungu wa Waisraeli tu, je, wewe si mtu anayemkana Mungu waziwazi? Kusudi la kukushinda leo ni kukufanya utambue kuwa Mungu ni Mungu wako, na Mungu wa wengine, na muhimu zaidi ni Mungu wa wote wanaompenda, na Mungu wa viumbe wote. Ni Mungu wa Israeli na Mungu wa Misri. Ni Mungu wa Waingereza na Mungu wa Wamarekani. Si Mungu wa Adamu na Hawa tu, bali pia Mungu wa kizazi cha Adamu na Hawa. Ni Mungu wa kila Kitu mbinguni na duniani. Familia ya Waisraeli na familia zote za Mataifa zimo mikononi mwa Mungu. Hakufanya kazi katika nchi ya Israeli pekee kwa miaka elfu kadhaa na kuzaliwa Uyahudi, ila leo Anashuka Uchina, nchi hii ambapo joka kuu jekundu limejikunja. Ikiwa kuzaliwa Uyahudi kunamfanya Mfalme wa Wayahudi, basi si kushuka kwake miongoni mwenu leo kunamfanya Mungu wenu? Aliwaongoza Waisraeli na alizaliwa Yudea na vilevile amezaliwa katika nchi ya Mataifa. Je, kazi Yake yote haifanywi kwa ajili ya wanadamu wote Aliowaumba? Je, Anawapenda Waisraeli mara mia moja na kuwachukia Mataifa mara elfu moja? Je, hayo siyo mawazo yenu? Ni ninyi ambao hamtambui Mungu; si kwamba Mungu Hakuwa Mungu wenu. Ni ninyi mnaomkataa Mungu; si kwamba Mungu hapendi kuwa Mungu wenu. Ni nani kati ya walioumbwa hayuko mikononi mwa mwenye Uweza? Kwa kuwashinda leo, je, lengo si kuwafanya mtambue kuwa Mungu ni Mungu wenu? Iwapo bado mnashikilia kuwa Mungu ni Mungu wa Waisraeli tu, na kuendelea kushikilia kuwa nyumba ya Daudi huko Israeli ni asili ya uzao wa Mungu na kuwa hakuna taifa tofauti na Israeli limewezeshwa “kumzaa” Mungu, na hata zaidi kuwa hakuna familia ya Mataifa yenye uwezo wa kupokea kazi ya Yehova—ikiwa bado unafikiria hivi, je, haikufanyi kuwa mshikiliaji wa ukaidi? Usikazie macho Israeli kila wakati. Mungu Yuko hapa miongoni mwenu leo. Vilevile msitazamie mbingu tu. Acheni kutamani Mungu wenu Aliye mbinguni! Mungu ametua miongoni mwenu, basi Anawezaje kuwa mbinguni? Hujaamini katika Mungu kwa muda mrefu, ilhali una mawazo mengi kuhusu Mungu, kiasi kwamba unathubutu kutofikiri hata kwa sekunde moja kuwa Mungu wa Waisraeli Anaweza kuwatunukia na uwepo wake. Wala hamthubutu kufikiri jinsi mnavyoweza kumwona Mungu Akijitokeza binafsi, ikitiliwa maanani jinsi mlivyo wachafu. Aidha hamjawahi kufikiri jinsi Mungu anavyoweza kushuka miongoni mwa Mataifa. Anapaswa kushuka juu ya Mlima Sinai au Mlima wa Mizeituni na kuonekana kwa Waisraeli. Je, si watu wa Mataifa (yaani watu wa nje ya Israeli) ndio walengwa wa chuki Yake? Anawezaje kufanya kazi miongoni mwao? Haya yote ni mawazo yaliyokita mizizi ndani yenu ambayo mmeyakuza kwa miaka mingi. Kusudi la kuwashinda leo ni kuyaharibu haya mawazo yenu. Kwa njia hiyo mmeweza kumwona Mungu akijionyesha Mwenyewe miongoni mwenu—si katika Mlima Sinai au Mlima wa Mizeituni, bali miongoni mwa watu ambao Hajawahi kuwaongoza hapo awali. Baada ya Mungu kufanyia hatua mbili za kazi Yake Israeli, Waisraeli na watu wa Mataifa walishikilia wazo hili: Japo ni kweli Mungu aliumba viumbe wote, yuko radhi kuwa Mungu wa Waisraeli tu, si Mungu wa Mataifa. Waisraeli wanaamini yafuatayo: Mungu anaweza tu kuwa Mungu wetu, sio Mungu wenu Mataifa, na kwa sababu humchi Yehova, Yehova—Mungu wetu—Anawachukia. Zaidi, Wayahudi hao huamini hili: Bwana Yesu alichukua sura yetu Wayahudi na ni Mungu aliye na alama ya Wayahudi. Mungu anafanyia kazi miongoni mwetu. Sura ya Mungu na sura zetu zinafanana; sura zetu na sura ya Mungu zinakaribiana. Bwana Yesu ni Mfalme wetu Wayahudi; watu wa Mataifa hawajawezeshwa kupokea wokovu mkubwa kiasi hicho. Bwana Yesu ni sadaka ya dhambi kwetu Wayahudi. Ni kwa misingi ya hatua hizi mbili za kazi ndipo Waisraeli na Wayahudi walijijengea haya mawazo mengi. Wanamdai Mungu kuwa wao tu, bila kukubali kwamba Mungu vilevile ni Mungu wa Mataifa. Kwa njia hii, Mungu alikuwa pengo katika mioyo ya watu wa Mataifa. Hii ni kwa sababu kila mtu aliamini kuwa Mungu hataki kuwa Mungu wa watu wa Mataifa na kuwa Anawapenda tu Waisraeli—Wateule wake—na Anawapenda Wayahudi hasa wafuasi waliomfuata. Je, wajua kuwa kazi aliyoifanya Yehova na Yesu ilikuwa ni kwa ajili ya uzima wa wanadamu wote? Je, sasa unatambua kuwa Mungu ni wa wale wote waliozaliwa nje ya Israeli? Je, Mungu Hayumo miongoni mwenu leo? Hii haiwezi kuwa ndoto, ama vipi? Je, hamkubali uhalisi huu? Mnathubutu kutoamini au kulifikiria. Licha ya jinsi mnavyolitazama, je, Mungu hayumo miongoni mwenu? Je, bado mnaogopa kuyaamini maneno haya? Kuanzia leo, je, wote walioshindwa, na wale wote wanaotaka kuwa wafuasi wa Mungu, si wateule wa Mungu? Je, nyote mlio wafuasi leo, si wateule nje ya Israeli? Je, nafasi yenu si sawa na ya Waisraeli? Je, hili silo mnalopaswa kutambua? Je, hili si lengo la kazi ya kukushinda? Kwa kuwa mwaweza kumwona Mungu, basi Atakuwa Mungu wenu milele, tangu mwanzo hadi siku za baadaye. Hatawaacha, mradi tu nyinyi nyote mko radhi Kumfuata na kuwa viumbe Wake waaminifu na watiifu.

Haijalishi azimio lao la sasa la kumpenda Mungu ni imara vipi, mwanadamu kwa jumla amekuwa mtiifu na kufuata mpaka siku hii. Si mpaka mwisho, wakati ambapo hatua ya kazi hii itahitimishwa, ndiyo mwanadamu atatubu kabisa. Huo ndio wakati ambapo watu watashindwa kweli. Hivi sasa wako tu katika mchakato wa kushindwa. Wakati ambapo kazi itahitimishwa, watashindwa kabisa, lakini sio hivyo sasa hivi! Hata kama kila mtu ataridhika, hilo halina maana kwamba wameshindwa kabisa. Hii ni kwa kuwa kwa sasa watu wameona maneno pekee na sio matukio yenye ukweli, na wao bado hujiona wasio na hakika haijalishi vile wanavyoamini kwa kina. Ndiyo maana ni kwa hilo tukio lenye ukweli la mwisho, maneno kuwa hakika, ndiyo watu watashindwa kabisa. Hivi sasa watu hawa wanashindwa kwa sababu wanasikia kuhusu mafumbo mengi ambayo hawakuwahi kusikia kabla. Lakini ndani ya kila mmoja wao, wao bado wanatafuta na kungoja matukio fulani yenye ukweli yanayowaruhusu kuona kila neno la Mungu likitimilizwa. Ni wakati huo tu ndiyo wataridhishwa kabisa. Wakati ambao tu, mwishowe, wote wameona uhalisi huu wenye ukweli uliotimilizwa, na uhalisi huu umewasababisha kuwa na uhakika, ndiyo wataonyesha kusadiki sana ndani ya mioyo yao, kunena kwao, na macho yao, na ndiyo wataridhishwa kabisa kwa dhati. Hii ni asili ya mwanadamu. Mnahitaji kuona maneno yote yakitokea kuwa kweli, mnahitaji kuona baadhi ya matukio yenye ukweli yakitendeka na kuona msiba ukiwafika baadhi ya watu, na kisha mtaridhishwa kabisa ndani yenu. Kama Wayahudi, mnaendelea kutilia maanani sana kuona ishara na miujiza. Lakini mnaendelea kukosa kuona kwamba kuna ishara na miujiza na kwamba uhalisi unatendeka ambao unatakiwa kuyafungua macho yenu sana. Kama ni mtu fulani anayeshuka kutoka angani, au mhimili wa mawingu ukinena kwenu, au Mimi kutekeleza upungaji pepo kwa mmoja wenu, au sauti Yangu kunguruma kama radi kati yenu, ninyi daima mmetaka na daima mtataka kuona aina hii ya tukio. Mtu anaweza kusema kwamba katika kumwamini Mungu, matakwa yenu makuu zaidi ni kumwona Mungu akija na kuwaonyesha binafsi ishara. Kisha mtaridhika. Ili kuwashinda ninyi watu, lazima Nitekeleze kazi iliyo sawa na uumbaji wa dunia na kisha kuongeza ishara. Halafu, mioyo yenu itashindwa kabisa.

Iliyotangulia: Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (2)

Inayofuata: Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (4)

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp