Sura ya 19

Ni wajibu wa mwanadamu kuchukua maneno Yangu kama msingi wa maisha yake. Mwanadamu lazima aanzishe fungu lake binafsi katika kila sehemu ya maneno Yangu; kutofanya hivyo kutakuwa kujiletea maangamizo na kujiletea dharau. Binadamu haunijui, na kwa sababu ya hili, badala ya kuleta maisha yake Kwangu badala, anachofanya ni kujipanga tu mbele Yangu na takataka mikononi mwake, na hivyo kujaribu kuniridhisha. Lakini, mbali na kuridhishwa na mambo yalivyo, Naendelea kutoa matakwa kwa binadamu. Napenda michango ya mwanadamu, lakini Nachukia madai yake. Wanadamu wote wana mioyo iliyojaa ulafi; ni kama moyo wa binadamu unadhibitiwa na Shetani, na mwanadamu hawezi kuponyoka na kutoa moyo wake Kwangu. Ninapozungumza, watu husikiliza sauti Yangu kwa makini sana; Ninaponyamaza kimya, hata hivyo, wao huanza “shughuli” zao wenyewe na kuacha kabisa kusikiliza maneno Yangu, kana kwamba maneno Yangu yalikuwa tu kijalizo cha “shughuli” zao. Sijawahi kuwa mzembe kwa binadamu, na bado Nimekuwa pia mwenye subira na mvumilivu kwa binadamu. Na hivyo, kwa sababu ya huruma Yangu, binadamu wote hujiinua na wanakosa maarifa na kujitafakari; wanatumia vibaya uvumilivu Wangu ili kunidanganya. Hakuna mmoja kati yao anayenijali kwa dhati, na hakuna mmoja kweli ananithamini kama kitu apendacho moyoni mwake; ni wakati tu walipo na wakati wa ziada ndipo wanaponitambua kwa kiwango duni. Juhudi ambazo Nimetumia kwa mwanadamu tayari ni zaidi ya kipimo. Ninamfanyia mwanadamu aina ya pekee ya kazi, na mbali na haya, Nimempaa mzigo wa ziada, ili, ndani ya kile Ninacho na kile Nilicho, mwanadamu anaweza kupata maarifa na kupitia mabadiliko. Siwataki watu wawe ‘watumiaji’ tu; pia Nawataka wawe ‘wazalishaji’ wanaomshinda Shetani. Ingawa Sidai chochote kutoka kwa mwanadamu, hata hivyo Nina viwango vya matakwa Ninayoyatoa, kwani kuna madhumuni kwa yale Ninayoyafanya, na vile vile msingi wa matendo Yangu: Sichezi kiholela, anavyodhani mwanadamu, wala Siundi mbingu na dunia na mambo mengi ya uumbaji kwa ghafla na bila mpango. Kwa kazi Zangu, mwanadamu anapaswa kuwa na uwezo wa kuona kitu, kupata kitu. Hapaswi kutumia vibaya uchangamfu wa ujana wake, ama kutunza maisha yake kama vazi ambalo linakusanya vumbi; badala yake, anapaswa kujilinda vikali, kuchukua kutoka kwa fadhila Yangu kwa ajili ya starehe yake mwenyewe, hadi, kwa sababu Yangu, hawezi kumrudia Shetani, na kwa sababu Yangu anamshambulia Shetani. Si Ninachomwulizia mwanadamu ni rahisi hivi?

Mwangaza hafifu unapoanza kuonekana Mashariki, watu wote ulimwenguni wanautilia maani zaidi kidogo. Bila kujawa na usingizi, binadamu wanasonga mbele kuchunguza chanzo cha mwangaza huu wa mashariki. Kwa sababu ya uwezo wao finyu, hakuna yeyote ambaye ameweza kuona mahali unapotokea mwangaza. Wakati yote yaliyo ulimwenguni yameangaziwa kabisa, binadamu watazinduka kutoka usingizini na ndotoni, na ni hapo tu ndipo wanapotambua pole pole kwamba siku Yangu inawajia. Binadamu wote wanasherehekea kwa sababu ya ujio wa mwangaza, na kwa sababu ya haya hawalali tena, na si wapumbavu tena. Chini ya mng’aro wa mwangaza Wangu, binadamu wote wanakuwa na uwazi wa akili na mtazamo, na ghafla wanakuwa na furaha ya maisha. Chini ya kifuniko cha ukungu, Naulinda ulimwengu. Wanyama wote wako katika mapumziko; kwa sababu ya ujio wa mwangaza hafifu, kila kitu katika uumbaji kinafahamu kwamba maisha mapya yanakaribia. Kwa sababu hii, wanyama pia wanatoka nje ya mapango yao, kutafuta chakula. Mimea, bila shaka, si tofauti, na kwa mng’aro wa mwangaza majani yao ya kijani yanang’aa, yakisubiri kutakasa sehemu yao binafsi Kwangu wakati Niko duniani. Wanadamu wote wanataka ujio wa mwangaza, lakini bado wanahofia ujio wake, na wasiwasi kwamba ubaya wao hutafichika tena, kwani mwanadamu yu uchi kabisa, na hajafunikwa. Watu wangapi wanahofia, kwa sababu ya ujio wa mwangaza, na kwa sababu mwangaza umetokea, wako katika hali ya mshtuko? Watu wengi, baada ya kuuona mwangaza, hujawa na majuto yasiyo na mipaka, wakichukia uchafu wao, ilhali, bila uwezo wa kubadilisha ukweli, hawana budi ila kunisubiri Nitoe hukumu. Watu wangapi, wakisafishwa na mateso gizani, wanapoona mwangaza wanapigwa ghafla na umuhimu wake mkubwa, na hatimaye kukumbatia mwangaza karibu na vifua vyao, wakiogopa sana kuupoteza tena. Watu wengi sana, badala ya kutupwa nje ya uzingo na kutoka kwa ghafla kwa mwanga, wanaendelea tu na kazi ya kila siku, kwa sababu wamekuwa vipofu kwa miaka mingi, na hivyo hawana habari kwamba mwangaza umekuja, wala hawaridhishwi nao. Katika mioyo ya binadamu, Mimi daima si wa juu, wala duni. Kulingana na wao, haijalishi kama Nipo au la; ni kama kwamba maisha ya mwanadamu hayawezi kuwa na upweke zaidi iwapo Sipo, na iwapo Nipo, hayatafaidika na furaha. Kwa sababu wanadamu hawanithamini, raha Ninayowapa ni chache. Lakini punde tu binadamu unaponiabudu kidogo, basi pia Nitafanya mabadiliko kwa mtazamo Wangu kwa binadamu. Kwa sababu hii, wakati tu binadamu unapofahamu sheria hii, ndipo tu wanadamu watakapokuwa na bahati ya kujitolea Kwangu na kudai vitu vilivyo mikononi Mwangu. Hakika pendo la mwanadamu Kwangu halifungwi tu na maslahi yake mwenyewe? Hakika imani yake Kwangu haifungwi tu kwa mambo Ninayompa? Inaweza kuwa kwamba, isipokuwa tu yeye kuona mwangaza Wangu, mwanadamu hawezi kunipenda kwa dhati kwa njia ya imani yake? Hakika nguvu za mwanadamu na afya hazizuiliwi na hali ya leo? Inaweza kuwa kwamba mwanadamu anahitaji ujasiri ili anipende?

Kutegemea kuwepo Kwangu, mambo mengi ya uumbaji yanakubali kwa utiifu mahali yanamoishi, na katu, bila ya nidhamu Yangu, hayajihusishi na uasherati bila kujali. Kwa hiyo, milima inakuwa mipaka kati ya mataifa ulimwenguni, maji yanakuwa vikwazo vya kuwatenga watu wa nchi tofauti mbali mbali, na hewa inapuliza kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine katika nafasi zilizo juu ya dunia. Binadamu tu ndio hawawezi kweli kutii matakwa ya mapenzi Yangu; hii ndiyo maana Nasema kwamba, kwa viumbe vyote, mwanadamu pekee ni ndiye wa kundi la wasiotii. Mwanadamu hajawahi kweli kunitii, na kwa sababu hii wakati wote Nimemweka chini ya nidhamu kali. Iwapo katikati ya binadamu, itakuja kuwa kwamba utukufu Wangu umetandaa ulimwengu nzima, basi hakika Nitachukua utukufu Wangu wote na kuufanya uwe wazi mbele ya mwanadamu. Kwa sababu katika uchafu wake mwanadamu hafai kutazama utukufu Wangu, kwa maelfu ya miaka Sijawahi kujitokeza hadharani, lakini Nimebakia mafichoni; kwa sababu hii utukufu Wangu hujawahi kuwa wazi mbele ya mwanadamu, na mwanadamu daima amezama kwa shimo la kina la dhambi. Nimeusamehe udhalimu wa binadamu, lakini wanadamu hawajui jinsi ya kujihifadhi, na badala yake daima wanajiweka wazi kwa dhambi, kuruhusu dhambi kuwajeruhi. Huu si ukosefu wa mwanadamu wa kujiheshimu na kujipenda? Katikati ya binadamu, kuna kweli yeyote anayeweza kupenda? Ibada ya mwanadamu inaweza kuwa na uzito wa wakia ngapi? Hakuna bidhaa safi zilizochanganywa na kinachoitwa uhalisi wake? Si ibada yake imeungana kabisa na mkanganyiko? Ninachohitaji ni upendo wa mwanadamu usiogawanyika. Mwanadamu hanijui, na ingawa anaweza kupata kunijua, hatanipa moyo wake wa ukweli na dhati. Kwa mwanadamu, Sidai kile asichotaka kupeana. Akinipa ibada yake, Nitaikubali bila pingamizi; lakini asiponiamini, na kukataa kujitoa hata kidogo Kwangu, badala ya kukasirika juu ya hayo, Nitamwondoa tu kwa njia ingine na kumpangia hatima inayomfaa. Radi, inayovingirika angani, itawaangusha binadamu; milima ya juu, inapoanguka, itawazika; wanyama pori kwa njaa yao watawala; na bahari, zinapobingirika, zitawagubika. Binadamu wanapojishughulisha na migogoro ya mauaji ya jamii, binadamu wote watatafuta maangamizo yao katika majanga yatokayo katikati yao.

Ufalme unapanuka miongoni mwa binadamu, unachipua miongoni mwa binadamu, unasimama miongoni mwa binadamu; hakuna nguvu inayoweza kuharibu ufalme Wangu. Kwa watu Wangu walio katika ufalme wa leo, nani kati yenu si mwanadamu miongoni mwa wanadamu? Nani kati yenu yu nje ya hali ya ubinadamu? Wakati hatua Yangu ya kwanza mpya itatangazwa kwa wengi; binadamu utaguswa vipi? Mmeona na macho yenu hali ya mwanadamu; hakika bado hamna matumaini ya kudumu milele kwa dunia hii? Sasa Natembea ng’ambo katikati ya watu Wangu, Naishi katikati ya watu Wangu. Leo, walio na pendo la kweli Kwangu, watu kama hawa wamebarikiwa; wamebarikiwa wanaonitii, hakika watabaki katika ufalme Wangu; wamebarikiwa wanaonijua, hakika watakuwa na mamlaka katika ufalme Wangu; wamebarikiwa wanaonitafuta, hakika watatoroka vifungo vya Shetani na kufurahia baraka ndani Yangu; wamebarikiwa wanaoweza kujiacha, hakika wataingia katika milki Yangu, na kurithi fadhila ya ufalme Wangu. Wanaokimbia kimbia kwa ajili Yangu Nitawakumbuka, wanaopata gharama kwa ajili Yangu Nitawakumbatia kwa furaha, wanaonitolea sadaka Nitawapa starehe. Wanaopata raha ndani ya maneno Yangu, Nitawabariki; hakika watakuwa nguzo zinazoshikilia mwamba kwa ufalme Wangu, hakika watakuwa na fadhila isiyo na kifani kwa nyumba Yangu, na hakuna anayeweza kulinganishwa nao. Mmewahi kuzikubali baraka mlizopewa? Mmewahi kuzitafuta ahadi mlizofanyiwa? Hakika, chini ya mwongozo wa mwangaza Wangu, mtapenya katika utawala wa nguvu za giza. Hakika, katikati ya giza, hamtaupoteza mwangaza unaowaongoza. Hakika mtakuwa bwana wa viumbe vyote. Hakika mtakuwa washindi mbele ya Shetani. Hakika, wakati wa maangamizi ya ufalme wa joka kubwa jekundu, mtasimama miongoni mwa umati mkubwa kushuhudia ushindi Wangu. Hakika mtasimama imara na thabiti katika nchi ya Sinimu. Kupitia katika mateso mnayoyavumilia, mtarithi baraka zinazotoka Kwangu, hakika mtaonyesha utukufu Wangu katika ulimwengu mzima.

Machi 19, 1992

Iliyotangulia: Sura ya 18

Inayofuata: Sura ya 20

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp