Sura ya 18

Katika mwako wa umeme, kila mnyama hufichuliwa katika hali yake halisi. Hivyo pia, kama wameangaziwa na mwanga Wangu, mwanadamu amepata tena utakatifu aliokuwa nao wakati mmoja. Eh, dunia potovu ya zamani! Mwishowe, imeanguka na kutumbukia ndani ya maji machafu na, imezama chini ya maji, na kuyeyuka na kuwa tope! Ah, ya kwamba binadamu wote Niliouumba hatimaye umerudiwa na uhai tena katika mwanga, kupata msingi wa kuwepo, na kuacha kupambana katika tope! Ah, Mambo mengi ya uumbaji Ninayoyashikilia mikononi Mwangu! Wanawezaje, kukosa kufanywa upya, kupitia maneno Yangu? Wanawezaje, katika mwanga, kukosa kuendeleza kazi zao? Dunia si kimya cha mauti na nyamavu tena, mbingu si ya ukiwa na yenye huzuni tena. Mbingu na nchi, bila kutenganishwa na utupu tena, zimeungana kama kitu kimoja, kamwe kutotenganishwa tena. Katika wakati huu wa shangwe, wakati huu wa nderemo, haki Yangu na utakatifu Wangu umeenea katika kila pembe ya ulimwengu, na binadamu wote wanavisifu bila kikomo. Miji yote ya mbingu inacheka kwa furaha, na falme zote za nchi zinacheza kwa shangwe. Ni nani wakati huu ambaye haonyeshi furaha? Na ni nani wakati huu ambaye halii? Nchi katika hali yake ya asili ni miliki ya mbingu, na mbingu imeungana na nchi. Mwanadamu ni ugwe unaounganisha mbingu na nchi, na kwa sababu ya utakatifu wa mwanadamu, kwa ajili ya kufanywa upya kwa mwanadamu, mbingu haijafichwa tena kutoka kwa nchi, na nchi haiko kimya tena kwa mbingu. Nyuso za binadamu zimezingirwa na tabasamu za shukurani, na nyoyo zao zinadondokwa na utamu usiokuwa na kifani. Mwanadamu hagombani na mwanadamu, wala binadamu kupigana wenyewe kwa wenyewe. Kunao wale ambao, katika mwanga Wangu, hawaishi kwa furaha na wenzao? Kunao wale ambao, katika siku Yangu, hulifedhehesha jina Langu? Watu wote huelekeza macho yao ya heshima Kwangu, na wao hunililia kwa siri katika nyoyo zao. Nimechunguza kila kitendo cha binadamu: Miongoni mwa wanadamu waliotakaswa, hakuna yeyote aliye mkaidi Kwangu, hakuna anayenielekezea hukumu. Binadamu wote umejawa na tabia Yangu. Kila mtu anakuja kunijua, ananijongelea, na ananiabudu. Msimamo wangu ni mmoja katika roho ya mwanadamu, Nimetukuzwa kwa kiwango cha juu zaidi kwa macho ya mwanadamu, na hububujika katika damu ya mishipa yake. Nderemo za furaha katika nyoyo za wanadamu huenea kila sehemu ya uso wa nchi, hewa ni ya kuchangamsha na bichi, ukungu mzito hauitandai ardhi tena, na mwangaza wa jua huvutia.

Sasa, ona ufalme Wangu, ambamo Mimi ni mfalme juu ya vyote, na Ninamotawala juu ya vyote. Tangu mwanzo wa uumbaji hadi sasa, wana wangu, wakiongozwa na Mimi, wameyapitia matatizo mengi sana ya maisha, dhuluma nyingi za ulimwengu, mageuko mengi sana ya ulimwengu wa binadamu, lakini sasa huishi katika nuru Yangu. Je, ni nani asiyelia kwa ajili ya dhuluma za jana? Je, ni nani ambaye hatokwi na machozi juu ya dhiki za kuifikia leo? Na tena, kuna wowote ambao hawaichukui fursa hii kujitolea kwa dhati kwa ajili Yangu? Je, kuna wowote ambao hawachukui fursa hii kuonyesha uchu unaochipuka mioyoni mwao? Je, kuna wowote ambao, wakati huu, hawaongei juu ya yale waliyoyapitia? Wakati huu, binadamu wote wanaziweka wakfu sehemu zao zilizo bora zaidi kwa ajili Yangu. Ni wangapi wanateseka na majuto kwa upumbavu wa giza wa jana, ni wangapi wanajichukia kwa sababu ya malengo ya jana. Binadamu wote wamepata kujijua, wote wameona matendo ya Shetani na maajabu Yangu, ndani ya nyoyo zao, sasa kuna nafasi kwa ajili Yangu. Sitakumbana tena na chuki na kukataliwa miongoni mwa wanadamu, kwani kazi Yangu kubwa imekwisha tekelezwa, na haizuiliwi tena. Leo, miongoni mwa wana Wangu, kunao wowote ambao hawajatafakari kwa niaba yao wenyewe? Kunao wowote ambao hawadhukuru zaidi kwa ajili ya njia ambazo kwazo kazi Yangu ilifanywa? Kunao wowote ambao wamejitolea kwa kweli kwa ajili Yangu? Uchafu ulio ndani ya mioyo yenu umepungua? Ama umeongezeka? Iwapo sehemu chafu katika nyoyo zenu hazijapungua, na wala hazijaongezeka, basi bila shaka Nitawatupa watu kama hao. Wale Ninaowataka ni watu watakatifu wanaoupendeza moyo Wangu, sio ibilisi wachafu wanaoniasi. Hata ingawa matakwa Yangu kwa binadamu si ya juu, ulimwengu wa ndani wa nyoyo za watu una changamano kiasi kwamba binadamu hauwezi kuafikiana na mapenzi Yangu bila kusita ama mara moja kutosheleza mahitaji Yangu. Wengi wa wanadamu wanaweka jitihada kisiri kwa matumaini ya kuweza kupata laurusi ya kuvishwa taji hatimaye. Idadi kubwa ya wanadamu wanajitahidi kwa nguvu zao zote, bila kuzembea hata kidogo, wakiogopa sana kutekwa nyara na Shetani tena. Hawathubutu tena kuwa na manung’uniko juu Yangu, lakini daima huonyesha utiifu wao Kwangu. Nimesikia maneno ya dhati yakinenwa na watu wengi, simulizi kutoka kwa watu wengi sana kuhusu matukio machungu ya mateso waliyopitia; Nimeona wengi sana, katika dhiki kubwa sana, wakinipa utiifu wao bila kukosa, na Nimewatazama wengi sana, wakitembea kwenye njia yenye mabonde, wakitafuta suluhisho. Katika hali hizi, hawajawahi kulalamika; hata wakati, wakishindwa kupata mwanga, walijipata kuwa wenye huzuni kidogo, hawajawahi kulalamika hata mara moja. Lakini pia Nimesikia watu wengi sana wakitoa mawazo yao bila woga kwa maapizo kutoka kwa vina vya nyoyo zao, wakiilaani Mbingu na kuishutumu nchi, na Nimeona, vilevile, watu wengi sana wakijiruhusu kukata tamaa katikati ya dhiki yao, wakijitupa mbali kama taka kwa jaa, halafu kufunikwa kwa uchafu na masizi. Nimesikia watu wengi sana wakigombana baina yao, kwa sababu mabadiliko katika cheo, pamoja na mabadiliko ya mwonekano wa nyuso zao yanayoandamana nayo, yamesababisha mabadiliko katika uhusiano wao na binadamu wenzao, hivi kwamba marafiki wanaacha kuwa marafiki na kuwa maadui, huku wakishambuliana kwa midomo. Wengi wa watu hutumia maneno Yangu kama risasi kutoka kwa bombomu, wakiwafyatulia wengine kwa ghafla, hadi ulimwengu wa waume umejawa kila mahali na makelele yanayoharibu kimya kitulivu. Kwa bahati nzuri, sasa ni leo; ama sivyo ni nani anayejua ni wangapi wangekuwa wamekufa kupitia kwa mfululizo usio na huruma wa moto huu wa bombomu.

Kufuatia maneno yanayotoka Kwangu, na kwenda sambamba na hali za binadamu wote, ufalme Wangu, hatua kwa hatua, hushuka duniani. Mwanadamu hahodhi tena fikira zenye wasiwasi, ama “kuzingatia” mambo ya watu wengine, au “kutafakari” kwa niaba yao. Na hivyo, migogoro yenye ubishi duniani haipo tena, na, kufuatia kutolewa kwa maneno Yangu, ‘silaha’ mbali mbali za enzi ya sasa zimeondolewa. Binadamu hupata amani na binadamu, moyo wa binadamu hunururisha roho ya uwiano tena, hakuna yeyote mwenye mwelekeo wa kujikinga dhidi ya mashambulizi ya siri. Binadamu wote wamerudi katika hali ya kawaida na kuanza maisha mapya. Wakiishi katika mazingira mapya, idadi kubwa ya watu huangalia kandokando yao, wakihisi kana kwamba wameingia katika ulimwengu mpya kabisa, na kwa sababu ya hili, wanashindwa kubadilika mara moja katika mazingira yao ya sasa ama kuingia mara moja kwenye njia nyofu. Na kwa hivyo linakuwa ni jambo la “roho iko radhi, lakini mwili ni dhaifu” kwa kadiri binadamu unavyohusika. Ingawa Mimi, kama mtu, sijaonja machungu ya mashaka Mwenyewe, Nayajua yote ya kujulikana kuhusu upungufu wa mwanadamu. Ninayaelewa kwa undani mahitaji ya mtu, na uelewa Wangu wa udhaifu wake ni mtimilifu. Kwa sababu hii, Simfanyii mzaha binadamu kwa dosari zake; Mimi husimamia tu, kulingana na udhalimu wa mwanadamu, kipimo mwafaka cha ‘elimu,’ bora zaidi ili kumwezesha kila mtu kushika njia nyofu, ili kwamba binadamu waache kuwa mayatima wanaozurura na badala yake wawe watoto wachanga walio na makao. Hata hivyo, matendo Yangu yanaelekezwa na kanuni. Kama wanadamu hawataki kufurahia upeo wa furaha iliyo ndani Yangu, Ninaweza kukubaliana tu na kile ambacho mioyo yao inatamani kufanya na kuwatupa katika shimo lisilo na mwisho. Katika hatua hii, hakuna anayestahili kuyahodhi malalamiko moyoni mwake tena, ila wote wanapaswa kuona haki Yangu katika mipango ambayo Nimeifanya. Siulazimishi binadamu kunipenda Mimi, wala Sitampiga mwanadamu yeyote kwa kunipenda Mimi. Ndani Yangu ni uhuru kamili, ufunguliwaji kamili. Ingawa majaliwa ya mtu yamo mikononi Mwangu, Nimempa binadamu hiari ambayo haitegemei uongozi Wangu. Kwa njia hii, wanadamu hawatabuni njia za kuingia katika matatizo kwa sababu ya amri Zangu za kiutawala, bali, kwa kutegemea ukarimu Wangu, watajipatia ufunguliwaji. Na kwa hivyo watu wengi, bila kufungiwa katika kizuizi Kwangu, huenda kutafuta njia yao wenyewe ya kutoka, katika tendo la kupata ufunguliwaji.

Daima Mimi huushughulikia binadamu kwa mkono mkarimu, bila kusababisha matatizo yasiyoweza kutatulika, bila kuweka mtu yeyote katika shida; je, si hivi ndivyo? Ingawa watu idadi kubwa hawanipendi, bila kukasirishwa na mtazamo wa aina hii, Nimewapa wanadamu uhuru, kuwaruhusu hiari kiasi kwamba nimewaacha kuogelea pote katika bahari chungu. Kwa kuwa mtu ni chombo na hastahili kudhaminiwa: Ingawa yeye huona baraka Ninayoibeba mkononi Mwangu, hana shauku ya kuifurahia, ila angefurahia kuchomoa mjeledi kutoka kwa mkono wa Shetani matokeo yake yakiwa ni kujihukumu mwenyewe kumung’unywa na Shetani kama “chakula”. Bila shaka, kuna wengine ambao wameiona nuru Yangu kwa macho yao, na kwa hivyo, hata kama wao wanaishi katika ukungu wa wakati huu, hawajapoteza imani katika mwanga kwa ajili ya ukungu huu wenye giza, lakini wameendelea kupapasa na kutafuta kupitia kwa ukungu—ijapokuwa katika njia ilichozagazwa vikwazo. Mwanadamu anaponiasi, Mimi humwelekezea hasira Zangu zenye ghadhabu, na kwa hivyo mwanadamu anaweza kuangamia kwa ajili ya kutotii kwake. Anaponitii, Mimi hubaki nimejificha kutoka kwake, kwa njia hii nikiamsha pendo katika kina cha moyo wake, pendo ambalo halinuii kunibembeleza, ila kunipa raha. Ni mara nyingi sana, katika uchunguzi wa mwanadamu kunipata, Nimefunga macho Yangu na kukaa kimya, kwa kusudi la kuvuta imani yake ya kweli. Lakini wakati Nimekosa kuongea, imani ya mwanadamu hubadilika ghafula, na hivyo kile Ninachokiona tu ni “mali” ghushi, kwa sababu mwanadamu hajawahi kunipenda kwa dhati. Ni wakati tu Ninapojidhihirisha Mwenyewe ndiyo kwamba binadamu wote hufanya onyesho kubwa la “imani”; lakini wakati Nimejificha katika pahali Pangu pa siri, wanakua dhaifu na kudhoofika moyo, kama kwamba wanahofia kunikosea; kuna hata baadhi ambao, kwa kuwa hawawezi kuuona uso Wangu, “wananipitisha katika mchakato mkubwa” hivyo kukanusha ukweli wa kuwepo Kwangu. Watu wengi hubaki katika hali hii; watu wengi wana fikira za aina hii. Ni upendeleo tu wa wanadamu wote kuficha yale mabaya ndani yao. Kwa sababu ya hili, hawako radhi kutangaza dosari zao wenyewe, na hukubaliana na ukweli wa maneno Yangu tu shingo upande na kwa nyuso zilizofichwa.

Machi 17, 1992

Iliyotangulia: Sura ya 17

Inayofuata: Sura ya 19

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp