Sura ya 112

Kwamba “maneno na uhalisi huendelea kwa pamoja” ni sehemu ya tabia Yangu ya haki na, kutoka kwa maneno haya, bila shaka Nitamwacha kila mtu aone tabia Yangu yote. Watu hufikiri hili haliwezi kutimizwa, lakini Kwangu ni rahisi na linafurahisha, na halitumii juhudi yoyote. Wakati ambapo maneno Yangu yanatoka mara moja kuna uhalisi ambao kila mtu anaweza kuuona. Hii ndiyo tabia Yangu. Kwa kuwa Nasema kitu kinakamilishwa kwa lazima, vinginevyo Singezungumza. Katika dhana ya binadamu neno “wokovu” linasemwa kwa ajili ya watu wote, lakini hili halilingani na nia Zangu. Zamani Nilisema “Daima Mimi huwaokoa wale ambao ni wajinga na ambao wanatafuta kwa ari” ambapo neno “okoa” lilisemwa kuhusu wale wanaonitolea huduma, na lilimaanisha kwamba Ningewatendea kwa upekee watendaji huduma kama hawa. Kwa maneno mengine, Ningepunguza adhabu kwa watu hao. Hata hivyo, hawa watendaji huduma wasio waaminifu na walio wadanganyifu wangekuwa miongoni mwa walengwa wa uangamizaji, yaani, Ningewapa adhabu kali. (Ingawa wao ni miongoni mwa walengwa wa uangamizaji, ni tofauti sana kuliko wale wanaoangamizwa: Watapokea adhabu kali ya milele, na adhabu ambayo watu hao watapokea ni adhabu ya ibilisi, Shetani. Hii pia ndiyo maana ya kweli ya kile Nilichosema, kwamba watu wale ni uzao wa joka kubwa jekundu.) Lakini Situmii maneno ya aina hizi kuhusu wazaliwa Wangu wa kwanza; badala yake Nasema kwamba Nitawapata tena wazaliwa Wangu wa kwanza na watarudi Sayuni. Kwa hivyo Nimesema daima kwamba wazaliwa Wangu wa kwanza ni waliojaaliwa na waliochaguliwa Wangu. Wazaliwa Wangu wa kwanza walikuwa Wangu mwanzoni, walitoka Kwangu, kwa hivyo lazima warudi hapa Kwangu. Na kulinganisha wana na watu kwa wazaliwa wa kwanza, kweli ni tofauti kati ya mbinguni na dunia: Ingawa wana na watu ni bora zaidi kuwaliko watendaji huduma, wao sio wale walio Wangu hata kidogo. Inaweza kusemekana pia kwamba wana na watu wanachaguliwa kwa kuongezea kutoka miongoni mwa wanadamu. Kwa hivyo daima Nimelenga nguvu Yangu kwa wazaliwa wa kwanza, na kisha Nitawaacha wazaliwa wa kwanza wawakamilishe hawa wana na watu. Hizi ndizo hatua za baadaye za kazi Yangu. Sasa hakuna haja kuwaambia, kwa hivyo Nimelitaja mara chache kwa wana na watu, lakini ni kwa wazaliwa wa kwanza pekee ndiyo Nimesema kwa kurudia na kutaja mambo haya kwa kurudia. Hivi ndivyo Ninavyosema na kufanya kazi. Hakuna mtu anayeweza kubadili hili—Mimi pekee ndiye Nina uamuzi wa mwisho kuhusu kila kitu.

Kila siku Narudisha mapigo dhidi ya dhana zenu, kila siku Namchambua kila mmoja wenu. Wakati ambapo Nimesema hadi mahali fulani, mnarudia hali mbaya na tena mnatenganisha ubinadamu Wangu kutoka kwa uungu Wangu. Wakati huu muda umefika wa watu kufichuliwa: Watu hufikiri kwamba bado Naishi katika nyama na Mimi si Mungu Mwenyewe hata kidogo, kwamba Mimi bado ni mwanadamu na Mungu bado ni Mungu, na kwamba Mungu hana uhusiano wowote na mtu Niliye Mimi. Binadamu hawa ni wapotovu jinsi gani! Nimezungumza awali maneno mengi sana, ambayo mmechukulia kutoka kitambo kama kwamba hayakuwepo, kiasi kwamba linanifanya kuwachukia sana, linanifanya kuwakirihi! Mimi—Mungu Mwenyewe kamili—ubinadamu Wangu pamoja na uungu Wangu kamili, nani anayethubutu kunikosea kwa kawaida? Nani anathubutu kunipinga katika mawazo yake? Baada ya maafa Yangu makuu kuanza kushuka Nitawaadhibu mmoja mmoja, Sitamsamehe yeyote, ila badala yake kuwaadhibu wote vikali. Roho Wangu anafanya kazi binafsi. Hili halimaanishi kwamba Mimi si Mungu Mwenyewe; kinyume chake kabisa, linamaanisha zaidi kwamba Mimi ni Mungu Mwenyewe mwenye uweza. Watu hawanijui—wote wananipinga na hawatazami kudura Yangu kutoka kwa maneno Yangu, lakini badala yake wanajaribu kupata kitu katika maneno Yangu ambacho wanaweza kutumia dhidi Yangu na kupata makosa Kwangu. Wakati ambapo siku moja Naonekana na wazaliwa Wangu wa kwanza Sayuni, Nitaanza kushughulikia mambo haya. Katika kipindi hiki Nafanya kazi hii kimsingi. Wakati ambapo Nimezungumza hadi kiwango fulani, idadi kubwa ya watendaji huduma itakuwa imerudi nyuma, na wazaliwa wa kwanza watakuwa pia wamepitia kila aina ya taabu. Kwa kuendelea kwa hatua hizi mbili za kazi, kazi Yangu itafika tamati. Wakati huo huo Nitawarudisha wazaliwa Wangu wa kwanza Sayuni. Hizi ndizo hatua za kazi Yangu.

Wazaliwa Wangu wa kwanza ni sehemu muhimu ya ufalme Wangu, ambayo kutoka kwayo kunaweza kuonekana kwamba nafsi Yangu ni ufalme—ufalme Wangu unazaliwa na kuzaliwa kwa wazaliwa Wangu wa kwanza. Kwa maneno mengine, ufalme Wangu umekuwepo tangu uumbaji wa dunia, na kuwapata wazaliwa Wangu wa kwanza (kumaanisha kuwapata tena wazaliwa Wangu wa kwanza) ni kufanya upya ufalme Wangu. Kutoka kwa hilo unaweza kuona kwamba wazaliwa wa kwanza ni wa umuhimu maalum. Kama tu kuna wazaliwa Wangu wa kwanza, hapo ndipo kutakuwa na ufalme, basi uhalisi wa kutawala katika mamlaka utatimia, basi kutakuwa na maisha mapya, na basi enzi nzima nzee inaweza kukamilishwa. Mwelekeo huu hauepukiki. Kwa sababu wazaliwa wa kwanza wako katika nafasi hii—kwa sababu wazaliwa wa kwanza wanaashiria uharibifu wa dunia, uangamizaji wa Shetani, kufichuliwa kwa tabia halisi ya watendaji huduma, kwamba joka kubwa jekundu halitakuwa na uzao na liashuka katika ziwa la moto na kibiriti—kwa hivyo wale wanaoshikilia madaraka na wale ambao ni uzao wa joka kubwa jekundu wanazuia kwa kurudia, wanapinga kwa kurudia, na wanaharibu kwa kurudia. Lakini Nawapandisha cheo kwa kurudia, Nawashuhudia kwa kurudia, na kuwafichua wazaliwa Wangu wa kwanza kwa kurudia. Kwa kuwa wale tu ambao wametoka Kwangu ndio wanafaa kunitolea ushuhuda; ni wao pekee ndio wana sifa zinazostahili kuishi kwa kunidhihirisha, na ni wao pekee ndio wana msingi wa kupigana vitani na kushinda ushindi mzuri kwa ajili Yangu. Wale ambao wametengana na Mimi ni udongo mdogo wa mfinyanzi mkononi Mwangu pekee—viumbe walioumbwa, kila moja wavyo. Wale ambao ni wana na watu ni walio bora waliochaguliwa kutoka kwa viumbe wa uumbaji, lakini si Wangu. Kwa hivyo, kuna tofauti kubwa kati ya wazaliwa wa kwanza na wana. Wana hawastahili kulinganishwa na wazaliwa wa kwanza hata kidogo—wanatawaliwa na kuongozwa na wazaliwa wa kwanza. Sasa mnapaswa kuwa wazi kabisa kuhusu hili! Kila neno ambalo Nimesema ni kweli, na si uongo hata kidogo. Yote haya ni sehemu ya maonyesho ya nafsi Yangu, na ni tamko Langu.

Nimesema Siongei mambo matupu, na Sifanyi makosa, ambalo linatosha kuonyesha uadhama Wangu. Lakini watu hawawezi kujua tofauti kati ya mema na mabaya, na ni wakati kuadibu Kwangu kunawafikia tu ambapo wanaridhishwa kikamilifu; vinginevyo wanabaki waasi na wakaidi, kwa hivyo hii ndiyo maana Natumia kuadibu kurudisha mapigo dhidi ya wanadamu wote. Katika dhana ya binadamu, kwa kuwa kuna Mungu Mwenyewe pekee, kwa nini kuna wazaliwa wengi wa kwanza wanaotoka Kwangu? Naweza kulisema kwa njia hii: Kutokana na shughuli Zangu mwenyewe, Nasema kile Nilicho tayari kusema, kwa hivyo watu wanaweza kunifanyia nini? Naweza pia kulisema kwa njia hii: Ingawa Mimi na wazaliwa wa kwanza si wa mfano mmoja, sisi ni wa Roho mmoja, kwa hivyo wote wanaweza kufanya kazi kwa pamoja nami. Sisi si wa mfano mmoja ili kuruhusu watu wote kuweza kuona kila sehemu ya nafsi Yangu kwa uwazi usio wa kawaida kabisa, kwa hivyo Nawaacha wazaliwa Wangu wa kwanza wawe na mamlaka pamoja na Mimi juu ya mataifa yote na watu wote. Huu ndio mfumo wa amri Zangu za utawala (mfumo Ninaozungumzia unamaanisha kwamba sauti Yangu ni pole na Naanza kuzungumza kwa wana na watu). Watu wengi wana mashaka kuhusu kipengele hiki, lakini hawapaswi kuwa na shaka sana. Nitafichua fikira zote za watu moja baada ya nyingine, kwa nia ya kuwafanya watu wahisi aibu wasiwe na pahali pa kujificha. Nasafiri kote ulimwenguni hadi miisho ya dunia na kutazama uso mzima wa ulimwengu. Nachunguza kila aina ya mtu—hakuna mtu ambaye anaweza kuhepa udhibiti Wangu. Nashiriki katika kila aina ya kitu, na hakuna kitu ambacho Sishughulikii binafsi. Nani anayethubutu kukana kudura Yangu? Ni nani anayethubutu kutoridhika kikamilifu kunihusu? Nani anayethubutu kutosujudu kikamilifu mbele Yangu? Mbingu zote zitabadilika kwa sababu ya wazaliwa Wangu wa kwanza, na hata zaidi, dunia nzima itatetemeka kwa nguvu nyingi kwa sababu ya Mimi na wazaliwa Wangu wa kwanza. Watu wote watapiga magoti mbele ya nafsi Yangu, na vitu vyote hakika vitakuja katika udhibiti wa mikono Yangu—bila kosa hata kidogo. Kila mtu lazima aridhike kikamilifu na kila kitu kitakuja nyumbani Mwangu na kunitolea huduma. Hii ndiyo sehemu ya mwisho ya amri Zangu za utawala. Kuanzia sasa kuendelea kila makala ya amri Zangu za utawala, kikilenga watu tofauti, kitaanza kuzaa matunda? (Kwa sababu amri Zangu za utawala zinatolewa kwa umma kikamilifu, na kwa kila aina ya mtu na kila kitu matayarisho ya kufaa yamefanywa. Watu wote watakuwa katika mahala pao pa kufaa na tabia halisi ya kila aina ya mtu itafichuliwa kwa sababu ya amri Zangu za utawala). Huku ndiko kufika kwa amri za utawala zilizo kweli na halisi.

Sasa, kwa mujibu wa hatua za kazi Yangu, Ninasema ninachotaka kukisema, na kila mtu lazima akichukulie kwa uzito. Kotekote katika enzi, kinywa cha kila mtakatifu kimetaja “Yerusalemu Mpya,” na kila mtu anaujua, lakini hakuna mtu anaelewa maana ya kweli ya neno hili. Kwa kuwa kazi ya leo imeendelea hadi kwa hatua hii, Nitafichua maana ya kweli ya neno hili kwenu kuwafanya mlielewe. Lakini Nina mpaka—bila kujali jinsi Ninavyolielezea na bila kujali jinsi Ninavyolisema kwa uwazi, hamwezi kulielewa kabisa kwa sababu hakuna mtu anayeweza kupata uhalisi wa neno hili. Zamani kile ambacho Yerusalemu ilirejelea kilikuwa makao Yangu duniani, yaani, mahali ambapo Natembea na kusonga. Lakini neno “mpya” linabadilisha neno hili na si sawa hata kidogo. Watu hawawezi kulielewa hata kidogo. Watu wengine wanafikiri linarejelea ufalme Wangu; watu wengine wanafikiri ni mwanadamu Niliye; watu wengine wanafikiri ni mbingu mpya na dunia mpya; na watu wengine wanafikiri ni dunia mpya baada ya Mimi kuharibu dunia hii. Hata kama akili ya mtu inafikiri kwa wingi, na hata kama akili ya mtu ni changamani mno, bado hawezi kuelewa chochote kulihusu. Kotekote katika enzi, watu wamekuwa wakitumaini kujua au kuona maana ya kweli ya neno hili, lakini matamanio yao hayajawahi kutimizwa—wote wamevunjika matumaini na wamefariki, wakiacha matumaini yao nyuma; kwa sababu wakati Wangu ulikuwa haujafika bado Singeweza kumwambia mtu yeyote kwa urahisi. Kwa kuwa kazi Yangu imefanywa hadi kwa hatua hii Nitawaambia kila kitu. Yerusalemu Mpya unajumuisha haya mambo manne: ghadhabu Yangu, amri Zangu za utawala, ufalme Wangu na baraka zisizoisha Ninazowapa wazaliwa Wangu wa kwanza. Sababu ya Mimi kutumia neno “mpya” ni kwa sababu hizi sehemu nne ni sehemu zilizofichwa. Kwa sababu hakuna mtu anayejua ghadhabu Yangu, hakuna mtu anayejua amri Zangu za utawala, hakuna mtu ambaye ameona ufalme Wangu, na hakuna mtu ambaye amefurahia baraka Zangu, “mpya” linarejelea kile ambacho kimefichwa. Hakuna mtu anayeweza kuelewa kikamilifu kile ambacho Nimesema, kwa sababu Yerusalemu Mpya umeshuka duniani lakini hakuna mtu amepitia uhalisi wa Yerusalemu Mpya mwenyewe. Bila kujali jinsi Ninavyouzungumzia kwa ukamilifu, watu hawataelewa kwa ukamilifu. Hata kama mtu anaelewa, ni maneno yake, ni akili yake, na ni dhana zake. Huu ni mwelekeo usioepukika, ni njia ya pekee, ambayo hakuna mtu anaweza kuhepa.

Iliyotangulia: Sura ya 111

Inayofuata: Sura ya 113

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp