Njia … (6)

Tumeletwa hadi siku ya leo kwa sababu ya kazi ya Mungu, na kwa hiyo sisi ndio waliosalia katika mpango wa Mungu wa usimamizi. Kwamba tumebaki leo ni kuinuliwa pakubwa na Mungu, kwani kulingana na mpango wa Mungu, nchi ya joka kubwa jekundu inapaswa kuangamizwa. Lakini Nadhani kwamba huenda Ameanzisha mpango mwingine, ama Anataka kutekeleza sehemu nyingine ya kazi Yake, kwa hiyo hata leo, Siwezi kueleza hili vizuri—ni kama fumbo lisiloweza kufumbulika. Lakini kwa jumla, hili kundi letu limeamuliwa kabla na Mungu, na Ninaendelea kuamini kwamba Mungu ana kazi nyingine ndani yetu. Nasi sote tusihi Mbingu hivi: “Mapenzi Yako yatimie, na Utuonekanie tena na Usijifiche ili tuweze kuona utukufu Wako na uso Wako vizuri zaidi.” Kila wakati Nahisi kwamba njia ambayo Mungu hutuelekezea siyo nyoofu, ila ni njia iliyopinda ambayo imejaa mashimo; aidha, Mungu husema kwamba kadiri njia ilivyo yenye miamba zaidi, ndivyo inavyoweza kufichua mioyo yetu ya upendo zaidi. Lakini hakuna kati yetu anayeweza kuifungua njia kama hii. Katika yale Niliyoyapitia, nimezitembea njia nyingi ngumu zenye miamba na Nimevumilia mateso makubwa; nyakati nyingine Nimekuwa na huzuni nyingi sana kiasi kwamba Nimetaka kulia, lakini Nimeitembea njia hii hadi wa leo. Naamini kwamba hii ndiyo njia inayoongozwa na Mungu, kwa hiyo Navumilia maumivu makali ya dhiki yote na Ninaendelea kusonga mbele. Kwani hili ndilo ambalo limeamuliwa na Mungu, kwa hiyo ni yupi anayeweza kuliepuka? Sitaki kupata baraka zozote; Ninachotaka tu ni kwamba Niweze kuitembea njia Ninayopaswa kuitembea kulingana na mapenzi ya Mungu. Sitaki kuwaiga wengine, Nikiitembea njia wanayoitembea; Nitakacho tu ni kwamba Niweze kutimiza kujitoa Kwangu katika kuitembea njia Niliyochaguliwa hadi mwisho. Siwataki wengine wanisaidie; kusema ukweli, Siwezi kumsaidia mwingine yeyote pia. Inaonekana kwamba Mimi ni mwepesi sana wa kuhisi kuhusiana na jambo hili. Sijui wanachofikiria watu wengine. Hii ni kwa sababu daima Nineamini kwamba kiasi ambacho mtu lazima ateseke na umbali ambao lazima autembee kwenye kinjia yake yameamuliwa na Mungu, na kwamba hakuna yeyote anayeweza kumsaidia mwingine kweli. Ndugu zetu wengine wenye ari wanaweza kusema kwamba Sina upendo, lakini hiki ndicho Ninachoamini tu. Watu wanazitembea njia zao wakitegemea mwongozo wa Mungu, na Ninaamini kwamba ndugu Zangu wengi watauelewa moyo Wangu. Natumai pia kwamba Mungu atatupa nuru kubwa zaidi katika kipengele hiki, ili upendo wetu uweze kuwa safi zaidi na urafiki wetu uwe wa thamani zaidi. Naomba tusikanganywe kuhusu mada hii, ila tupate ufahamu mkubwa zaidi tu, ili mahusiano baina yetu yaweze kujengwa juu ya msingi wa uongozi wa Mungu.

Mungu amefanya kazi katika bara China kwa miaka kadhaa, na Amelipa gharama kubwa kwa wanadamu wote ili atufikishe tulipo leo. Nadhani kwamba ili kuwaongoza watu wote kwenye njia sahihi, kazi hii lazia ianze kwenye udhaifu wa kila mtu; hapo tu ndipo wanaweza kukishinda kikwazo cha kwanza na kuendelea kusonga mbele. Si hilo ni bora? Taifa la China, likiwa limepotoshwa kwa miaka mingi, limesalia hadi leo, kila aina ya “virusi” vikizidi bila kikomo, vikienea kila mahali kama pigo; inatosha tu kuangalia mahusiano ya watu ili kuona jinsi “vijidudu” vingi vimejificha ndani ya watu. Ni vigumu sana kwa Mungu kukuza kazi Yake katika eneo lililobanwa sana na kujawa virusi. Hulka za watu, tabia, jinsi wanavyofanya mambo, kila kitu wanachoonyesha katika maisha yao na mahusiano baina yao—yote yameharibika, kufikia kiwango ambapo ufahamu na utamaduni wa kibinadamu yote yamehukumiwa kufa na Mungu. Sembuse uzoefu mbalimbali waliojifunza kutoka kwa familia na jamii zao—hawa wote wamepatikana kuwa na hatia machoni pa Mungu. Hii ni kwa sababu wale wanaoishi katika nchi hii wamevila virusi vingi sana. Ni kama mambo hayajabadilika kwao, hawajali hili. Kwa hiyo, kadiri watu walivyo wapotovu mahali fulani, ndivyo mahusiano baina yao yanavyozidi kuwa yasiyo ya kawaida. Mahusiano ya watu yamejaa njama, wanakuliana njama na kuuana kana kwamba wako katika ngome ya mapepo ambapo watu hulana. Katika mahali palipojaa hofu kama hapa, ambapo mazimwi wamejaa, ni vigumu sana kutekeleza kazi ya Mungu. Namwomba Mungu bila kukoma inaponibidi Nikutane na watu, kwani Ninahofia kukutana nao, na kuogopa sana kwamba Nitaikosea “heshima” yao na tabia Yangu. Moyoni Mwangu, daima Naogopa kwamba roho hizi chafu zitatenda bila kujali, kwa hiyo daima Namwomba Mungu anilinde. Kila namna ya mahusiano yasiyo ya kawaida yako dhahiri miongoni mwetu, na Nionapo haya yote, kuna chuki moyoni Mwangu, kwani miongoni mwao, watu daima wanajihusisha katika “biashara” ya mwanadamu, na kwamwe hawamfikirii Mungu hata kidogo. Nadharau tabia yao kabisa. Kinachoweza kuonekana ndani ya watu wa bara China ni tabia potovu za kishetani pekee, kwa hivyo katika kazi ya Mungu ndani ya hawa watu, ni vigumu sana kupata chochote cha thamani ndani yao; kazi yote inafanywa na Roho Mtakatifu, na ni kwamba tu Roho Mtakatifu anawagusa watu zaidi, na kufanya kazi ndani yao. Ni vigumu sana kuwatumia watu hawa; yaani, kazi ya Roho Mtakatifu kuwagusa watu pamoja na ushirika wa watu hayawezi kufanyika. Roho Mtakatifu anafanya tu kazi kwa bidii ili kuwagusa watu, lakini hata hivyo, watu wanabakia wenye ganzi na wasiohisi na hawajui anachofanya Mungu hata kidogo. Kwa hiyo, kazi ya Mungu huko bara China inalingana na kazi Yake ya kuumba mbingu na dunia. Anawafanya watu wote wazaliwe tena, na kubadili kila kitu kuwahusu, kwani hakuna kilicho cha thamani ndani yao. Ni jambo la kuhuzunisha sana. Mara nyingi huwa Ninawaombea watu hawa kwa huzuni: “Mungu, nguvu Yako kuu na ifichuliwe ndani ya watu hawa, ili Roho Wako aweze kuwaguza sana, na ili watu hawa wenye ganzi na wajinga ambao wanateseka waweze kuzinduka, kamwe wasiwe katika hali ya usingizi mzito, na waone siku ya utukufu Wako.” Na sote tuombe mbele za Mungu na kusema: Ee Mungu! Na Utuhurumie na kututunza tena ili mioyo yetu iweze kukugeukia kikamilifu, na ili tuweze kuikimbia nchi hii chafu, tusimame na kukamilisha kile Ulichotuaminia nacho. Natumai kwamba Mungu ataweza kutugusa tena ili tuweze kupata nuru Yake, na Natumai kwamba Anaweza kutuhurumia ili mioyo yetu iweze kumrudia polepole na Aweze kutupata. Hili ndilo tamanio letu sote.

Njia tuitembeayo imeamuliwa kikamilifu na Mungu. Kwa ufupi, Naamini kwamba hakika Nitaitembea njia hii hadi mwisho kabisa, kwani Mungu daima ananipa tabasamu, na ni kana kwamba daima Naongozwa na mkono Wake. Hivyo moyo Wangu hauchafuliwi na chochote kingine, na hivyo daima Naizingatia kazi ya Mungu. Natekeleza yote ambayo Mungu ananiagiza kwa uwezo Wangu wote na kwa moyo, na kamwe Siingilii kazi ambazo Sijatengewa, wala Sijihusishi na yule anayezifanya—kwa kuwa Naamini kwamba kila mtu lazima aitembee njia yake mwenyewe, na asiingilie ya wengine. Nayaona mambo hivi. Huenda hii ni kwa sababu ya hulka Yangu mwenyewe, lakini Ninatumai kwamba ndugu Zangu wanaelewa na kunisamehe kwa sababu kamwe Sithubutu kuzipinga amri za Baba Yangu. Sithubutu kuyaasi mapenzi ya Mbinguni. Je, Umesahau kwamba “mapenzi ya Mbinguni hayawezi kuasiwa”? Watu wengine wanaweza kunifikiria kuwa mwenye kujifikiria tu, lakini Naamini kwamba Nimekuja hasa ili kutekeleza sehemu moja ya kazi ya Mungu ya usimamizi. Sijaja ili kujihusisha na mahusiano baina ya watu; kamwe Sitajifunza jinsi ya kuelewana na wengine. Hata hivyo, katika agizo la Mungu, Nina mwongozo wa Mungu, na Nina imani na uthabiti wa kutimiza kazi hii. Labda “Najifikiria mwenyewe tu” sana, lakini Natumai kwamba kila mtu atachukua jukumu la kujaribu kuhisi upendo wa Mungu ulio wa haki na usio na ubinafsi, na ajaribu kushirikiana na Mungu. Usisubiri kuja kwa mara ya pili kwa uadhama wa Mungu; hilo halimfaidi yeyote. Daima Nafikiri kwamba kile tunachopaswa kuzingatia ni hiki: “Lazima tufanye kila kiwezekanacho kutenda kile tupaswacho ili kumridhisha Mungu. Agizo la Mungu kwa kila mmoja wetu ni tofauti; tunapaswa kulitimizaje?” Lazima utambue njia uitembeayo ni ipi hasa—ni muhimu kwamba uelewe hili. Kwa kuwa nyote mngependa kumridhisha Mungu, mbona msijikabidhi Kwake? Mara ya kwanza Nilipomwomba Mungu, Nilimpa moyo Wangu wote. Watu walio karibu nami—wazazi, ndugu na wafanyakazi wenza—wote walipuuzwa na kile Nilichokuwa nimeazimia, ilikuwa kana kwamba Kwangu hawakuweko hata kidogo. Kwani kila wakati Nilimfikiria Mungu, ama maneno ya Mungu, ama hekima Yake; mambo haya yalikuwa moyoni mwangu daima, na yalishikilia sehemu yenye thamani zaidi moyoni Mwangu. Kwa hiyo, kwa watu waliojaa falsafa za kuishi, Mimi ni mtu katili na asiyehisi. Mioyo yao inaumizwa na jinsi Ninavyojiheshimu, na jinsi Nifanyavyo mambo, na kila kitendo Changu. Wananiangalia kwa namna ya ajabu, kana kwamba mtu Niliye ni fumbo lisiloweza kufumbulika. Akilini mwao, wananipima kwa siri, wakipima kwa mizani ya mtu niliye wasijue Nitakachofanya baada ya hapo. Chochote wafanyacho kinawezaje kunizuia? Pengine wana wivu, ama wametishika, ama wananidhihaki; bila kujali, Naomba mbele za Mungu kila wakati kana kwamba Nina njaa na kiu kubwa, kana kwamba ni Mimi na Yeye tu katika dunia moja, na hakuna mtu mwingine yeyote. Nguvu za dunia ya nje hujazana zikinikaribia kila wakati—lakini pia hisia ya kuguswa na Mungu inajaa ndani Yangu. Nikiwa nimekabiliwa na mtanziko huu, Niliinama mbele za Mungu: “Ee Mungu! Ninawezaje kutotaka mapenzi Yako? Unanitazama kama aliye mwenye heshima, kama dhahabu iliyofuliwa, lakini Siwezi kuepuka nguvu za giza. Naweza kuteseka kwa ajili Yako maisha Yangu yote, Naweza kufanya kazi Yako iwe kazi ya maisha Yangu, na Nakuomba unipe mahali panapofaa pa pumziko ili Nijitolee Kwako. Ee Mungu! Ningependa kujitolea Kwako. Unajua udhaifu wa mwanadamu vizuri, kwa hiyo mbona Unajificha kutoka Kwangu?” Papo hapo, ilikuwa kana kwamba Nilikuwa yungiyungi la milimani wasilolijua watu, harufu yake nzuri ikisisimuliwa na upepo mwanana. Hata hivyo, Mbingu ililia, na moyo Wangu uliendelea kulia; Nilihisi kana kwamba kulikuwa na uchungu mkubwa hata zaidi moyoni Mwangu. Nguvu zote na kuzungukwa kwa mwanadamu—yalikuwa kama radi katika siku shwari. Ni nani angeweza kuuelewa moyo Wangu? Na kwa hiyo Nilikuja mbele za Mungu tena na kusema, “Ee Mungu! Hakuna namna ya kutekeleza kazi Yako katika nchi hii yenye uchafu? Mbona wengine hawawezi kuzingatia moyo Wako kwa mazingira ya kustarehesha, ya fadhila ambayo hayana mateso? Nataka kutandaza mabawa Yangu, lakini kwa nini ni vigumu sana kuondoka kwa kupuruka? Je, huliidhinishi?” Nililia kwa sababu ya hili kwa siku kadhaa, lakini daima Niliamini kwamba Mungu angeuletea moyo Wangu wenye huzuni faraja. Hakuna mtu ambaye amewahi kuelewa wasiwasi Wangu. Huenda ni utambuzi wa moja kwa moja kutoka kwa Mungu—Mimi daima Nimekuwa na shauku ya kazi Yake ndani Yangu, na Sijapata hata muda wa kupumua. Hadi leo, bado Naomba na kusema, “Ee Mungu! Ikiwa ni mapenzi Yako, Naomba Uniongoze kutekeleza kazi Yako hata kubwa zaidi ili iweze kuenea ulimwenguni kote, na ili iweze kufunuliwa kwa kila taifa na dhehebu, ili moyo Wangu uwe na amani kidogo, na ili Niweze kuishi mahali pa pumziko kwa ajili Yako, na Niweze kukufanyia kazi bila kukatizwa, na Niweze kukutumikia, moyo Wangu ukiwa na amani, kwa maisha Yangu yote.” Hili ndilo tamanio la moyo Wangu. Huenda ndugu watasema kwamba Mimi ni mwenye majivuno na Anayejipenda; nami pia Nakiri hili, kwani ni ukweli—vijana ni wenye majivuno kabisa. Kwa hiyo Nasema mambo kama yalivyo, bila kupinga ukweli. Huenda ukaona hulka zote za kijana ndani Yangu, lakini pia unaweza kuona Niliko tofauti na vijana wengine. Utulivu na ukimya Wangu. Siyazungumzii haya kwa undani; Naamini kwamba Mungu ananijua vyema kuliko Nijijuavyo. Haya ni maneno yatokayo moyoni Mwangu, na Natumai kwamba ndugu hawatachukizwa. Tuyazungumzie maneno yaliyo mioyoni mwetu, tuangalie ni kipi ambacho kila mmoja wetu anakifuatilia, tulinganishe mioyo yetu ya upendo kwa Mungu, tuyasikilize maneno tunayomnong’onezea Mungu, tuziimbe nyimbo nzuri zaidi mioyoni mwetu, na tudhihirishe fahari iliyo mioyoni mwetu, ili maisha yetu yaweze kuwa mazuri zaidi. Tuyasahau yaliyopita na tuyaganje yajayo. Mungu atatufungulia njia!

Iliyotangulia: Njia … (5)

Inayofuata: Njia … (7)

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp