Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe”
Kwa milenia kadhaa, mwanadamu ametamani kushuhudia kuwasili kwa Mwokozi. Mwanadamu ametamani kumtazama Yesu Mwokozi akiwa juu ya wingu jeupe Anaposhuka, yeye binafsi, kati ya wale ambao wamemtamani sana na kumtumainia kwa maelfu ya miaka. Mwanadamu pia ametamani sana Mwokozi arejee na kuungana na yeye, yaani, amemtamani sana Yesu Mwokozi, ambaye ametenganishwa na watu kwa maelfu ya miaka, arudi, na Atekeleze tena kazi ya ukombozi Aliyoifanya kati ya Wayahudi, kuwa na huruma na mwenye upendo kwa mwanadamu, kusamehe dhambi za mwanadamu na kujitwika dhambi za mwanadamu, na hata kujitwika makosa yote ya mwanadamu na kumwokoa mwanadamu kutoka dhambini. Kile ambacho mwanadamu anatamani sana ni Yesu Mwokozi awe jinsi Alivyokuwa hapo awali—Mwokozi ambaye anapendeka, mwema na mwenye kuheshimika, ambaye hana hasira kamwe kwa mwanadamu, na Asiyemkaripia mwanadamu, bali Anayesamehe na kubeba dhambi zote za mwanadamu, na ambaye hata, kama awali, atakufa msalabani kwa ajili ya mwanadamu. Tangu Yesu aondoke, wanafunzi waliomfuata, na vilevile watakatifu wote waliookolewa katika jina Lake, wamekuwa wakimtamani sana na kumtarajia. Wale wote waliookolewa kwa neema ya Yesu Kristo katika Enzi ya Neema wamekuwa wakiitamani siku hiyo ya shangwe katika siku za mwisho wakati ambapo Yesu Mwokozi atashuka juu ya wingu jeupe ili aonekane kati ya watu wasiohesabika. Bila shaka, hili pia ni tumaini la pamoja la wale wote wanaolikubali jina la Yesu Mwokozi leo. Kila mtu ulimwenguni anayejua kuhusu wokovu wa Yesu Mwokozi amekuwa akimtamani kwa hamu sana Yesu Kristo arejee kwa ghafla ili kutimiza kile ambacho Yesu alisema akiwa duniani: “Nitarejea tu jinsi Nilivyoondoka.” Mwanadamu anaamini kuwa, kufuatia kusulubishwa na kufufuka, Yesu alirudi mbinguni juu ya wingu jeupe kuchukua mahali Pake katika mkono wa kuume wa Aliye Juu. Vivyo hivyo, Yesu atashuka tena juu ya wingu jeupe (wingu hili linarejelea lile wingu ambalo Yesu alipaa juu yake Aliporudi mbinguni), miongoni mwa wale ambao wamemtamani sana kwa maelfu ya miaka, na Atachukua mfano na kuvalia mavazi ya Wayahudi. Baada ya kuwatokea, Atawapa chakula, na kuwamwagia maji yaliyo hai, naye Ataishi miongoni mwa wanadamu, akiwa Amejawa na neema na wema, hai na halisi. Ni fikira za aina hii ndizo watu huamini. Lakini Yesu Mwokozi hakufanya hivi; Alichofanya kilikuwa kinyume hasa na fikira za mwanadamu. Hakuwasili miongoni mwa wale waliokuwa wametamani sana kwa shauku kurejea Kwake, na Hakuwaonekania watu wasiohesabika akiwa juu ya wingu jeupe. Ameshafika tayari, lakini mwanadamu hamjui Yeye, na bado hajui hili. Mwanadamu anamngoja tu bila mwelekeo—hajui kabisa kwamba Ameshuka tayari juu ya “wingu jeupe” (wingu jeupe ambalo ni Roho Wake, maneno Yake, na tabia Yake yote na kila Alicho), na sasa yuko kati ya kikundi cha washindi ambacho Atakitengeneza katika siku za mwisho. Mwanadamu angewezaje kujua kwamba ingawa mtakatifu Mwokozi Yesu amejawa na wema na upendo kwa mwanadamu, haingewezekana Kwake kufanya kazi katika “mahekalu” hayo yaliyojaa uchafu na yaliyo na roho wachafu? Ingawa mwanadamu amekuwa akingoja kufika Kwake, Angewezaje kuwaonekania wale wanaokula mwili wa wasio na haki, wanaokunywa damu ya wasio na haki, na kuvaa mavazi ya wasio na haki, wanaomwamini na bado hawamfahamu na wanadai kwa nguvu kutoka Kwake kila wakati? Mwanadamu anajua tu kwamba Yesu Mwokozi amejawa na wema na rehema iliyofurika, na kwamba Yeye ni sadaka ya dhambi, iliyojawa na ukombozi. Hata hivyo mwanadamu hana habari kwamba Yeye ni Mungu Mwenyewe, ambaye Amejawa na haki, uadhama, ghadhabu, na hukumu, Aliye na mamlaka, na Aliyejawa na hadhi. Kwa hiyo, hata ingawa mwanadamu anatamani sana kwa hamu na kuonea shauku kurudi kwa Mkombozi, na hata ingawa maombi yake yanaigusa “Mbingu” Yesu Mwokozi hawaonekanii wale wanaomwamini ilhali hawamfahamu.
“Yehova” ndilo jina ambalo Nilichukua wakati wa kazi Yangu katika Israeli, na linamaanisha kwamba Mungu wa Waisraeli (watu wateule wa Mungu) Anayeweza kumwonyesha mwanadamu rehema, kumlaani mwanadamu, na kuyaongoza maisha ya mwanadamu; Mungu anayemiliki nguvu kuu na Amejawa na hekima. “Yesu” ni Imanueli, linalomaanisha sadaka ya dhambi iliyojaa wema, iliyojaa rehema, na inayomkomboa mwanadamu. Alifanya kazi ya Enzi ya Neema, na Anawakilisha Enzi ya Neema, na Anaweza tu kuwakilisha sehemu moja ya kazi ya mpango wa usimamizi. Yaani, Yehova pekee ndiye Mungu wa watu wateule wa Israeli, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, Mungu wa Musa, na Mungu wa watu wote wa Israeli. Na hivyo, Waisraeli wote wa wakati huo, ikiwemo Wayahudi, walimwabudu Yehova. Walimtolea dhabihu kwa madhabahu na walimtumikia hekaluni wakiwa wamevalia mavazi ya kikuhani. Kile walichotumainia kilikuwa kuonekana tena kwa Yehova. Yesu pekee ndiye Mkombozi wa wanadamu, na Yeye ndiye sadaka ya dhambi ambayo ilimkomboa mwanadamu kutoka dhambini. Yaani, jina la Yesu lilitoka katika Enzi ya Neema na lilikuja kuwepo kwa ajili ya kazi ya ukombozi katika Enzi ya Neema. Jina la Yesu lilikuja kuwepo ili kuwawezesha watu wa Enzi ya Neema wazaliwe upya na kuokolewa, nalo ni jina mahususi la ukombozi wa binadamu wote. Hivyo, jina Yesu linawakilisha kazi ya ukombozi, nalo linaashiria Enzi ya Neema. Jina Yehova ni jina mahsusi walilomwita Waisraeli walioishi chini ya sheria. Katika kila enzi na kila hatua ya kazi, jina Langu haliko bila msingi, lakini lina maana wakilishi wa kuwa muhimu: Kila jina linawakilisha enzi moja. “Yehova” linawakilisha Enzi ya Sheria nalo ni jina la heshima ambalo watu wa Israeli walimwita Mungu waliyemwabudu. “Yesu” linawakilisha Enzi ya Neema, nalo ni jina la Mungu wa wale wote waliokombolewa katika Enzi ya Neema. Iwapo mwanadamu bado anatamani kuwasili kwa Yesu Mwokozi katika siku za mwisho, na bado anamtarajia Afike katika mfano aliochukua kule Yudea, basi mpango wote wa usimamizi wa miaka elfu sita ungekomea katika Enzi ya Ukombozi, nao haungeweza kuendelea zaidi. Siku za mwisho, hata zaidi, zisingeweza kufika, nayo enzi isingekomeshwa. Hii ni kwa sababu Yesu Mwokozi ni kwa ajili ya ukombozi na wokovu wa wanadamu peke yake. Nilichukua jina la Yesu kwa ajili tu ya wenye dhambi wote katika Enzi ya Neema, lakini si jina ambalo kwalo Nitawafikisha wanadamu wote mwisho. Ingawa Yehova, Yesu, na Masihi yote yanawakilisha Roho Wangu, majina haya yanaashiria tu enzi tofauti za mpango Wangu wa usimamizi, nayo hayaniwakilishi katika ukamilifu Wangu. Majina wanayoniita watu duniani hayawezi kumaliza kwa ukamilifu tabia Yangu nzima na kila kitu Nilicho. Ni majina tofauti tu ambayo Ninaitwa katika enzi tofauti. Na hivyo, enzi ya tamati—enzi ya mwisho—itakapofika, jina Langu litabadilika tena. Sitaitwa Yehova, au Yesu, wala Masihi—Nitaitwa Mungu Mwenyewe mwenye nguvu na mwenyezi, na chini ya jina hili Nitaitamatisha enzi nzima. Niliitwa Yehova wakati mmoja, Nilijulika na watu pia kama Masihi, na wakati mmoja watu waliniita Yesu Mwokozi kwa upendo na heshima. Leo hii, Mimi si yule Yehova au Yesu tena ambaye watu walimfahamu nyakati zilizopita. Badala yake, Mimi ni Mungu ambaye Amerejea katika siku za mwisho, Mungu ambaye Ataitamatisha enzi; Mimi ndiye Mungu Mwenyewe ambaye Anainuka kutoka miisho ya dunia, Nimejawa na tabia Yangu nzima, na Nimejawa na mamlaka, heshima na utukufu. Watu hawajawahi kuwasiliana na Mimi, hawajawahi kunifahamu, na daima hawaijui tabia Yangu. Tangu uumbaji wa dunia hadi leo, hakuna mtu yeyote ambaye ameniona. Huyu ndiye Mungu anayemtokea mwanadamu katika siku za mwisho lakini Amejificha miongoni mwao. Anaishi kati ya watu, ni wa kweli na halisi, kama jua liwakalo na moto uwakao, Aliyejaa nguvu na kujawa mamlaka. Hakuna mtu au kitu chochote ambacho hakitahukumiwa kwa maneno Yangu, na mtu au kitu chochote ambacho hakitatakaswa kupitia moto unaowaka. Mwishowe, mataifa yasiyohesabika yatabarikiwa kwa sababu ya maneno Yangu, na pia kupondwa na kuwa vipande vipande kwa sababu ya maneno Yangu. Kwa njia hii, watu wote katika siku za mwisho wataona kwamba Mimi ndiye Mwokozi aliyerejea, na kwamba Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, ambaye Anawashinda binadamu wote. Na wote wataona kwamba wakati mmoja Nilikuwa sadaka ya dhambi kwa mwanadamu, lakini katika siku za mwisho Nimekuwa miale ya jua liwakalo linalochoma vitu vyote, na pia Jua la haki linalofunua vitu vyote. Hii ndiyo kazi Yangu katika siku za mwisho. Ninalichukua jina hili na Ninaibeba tabia hii ili watu wote wapate kuona kwamba Mimi ndimi Mungu mwenye haki, jua linalochoma, moto unaowaka, na kwamba wote waweze kuniabudu, Mungu pekee wa kweli, na ili waweze kuuona uso Wangu wa kweli: Mimi si Mungu wa Waisraeli tu, na Mimi si Mkombozi tu, badala yake Mimi ni Mungu wa viumbe vyote katika mbingu na ardhi na bahari.
Mwokozi angefika katika siku za mwisho na bado Awe anaitwa Yesu, na Azaliwe Yudea kwa mara nyingine na Afanye kazi Yake huko, basi hili lingethibitisha kwamba Niliwaumba watu wa Israeli pekee yao na Niliwakomboa watu wa Israeli pekee yao, na kwamba Sina uhusiano wowote na Mataifa. Je, hili halingekinzana na maneno Yangu kwamba “Mimi ni Bwana aliyeumba mbingu na ardhi na vitu vyote”? Nilitoka Yudea na Ninafanya kazi Yangu kati ya Mataifa kwa sababu Mimi si Mungu wa Waisraeli tu, bali ni Mungu wa viumbe wote walioumbwa. Ninaonekana kati ya Mataifa katika siku za mwisho kwa sababu Mimi si Yehova, Mungu wa Waisraeli tu, lakini, hata zaidi, Mimi ndimi Muumba wa watu Wangu wote wateule kati ya Mataifa. Sikuumba Israeli, Misri, na Lebanoni pekee, lakini pia Mataifa yote nje ya Israeli. Kwa sababu ya hili, Mimi ni Bwana wa viumbe wote walioumbwa. Nilitumia tu Israeli kama mahali pa kuanzia kazi Yangu, Nikatumia Yudea na Galilaya kama ngome za kazi Yangu ya ukombozi, na sasa Ninaitumia nchi ya Mataifa kama msingi ambao Nitatumia kuitamatisha enzi nzima. Nilifanya hatua mbili za kazi huko Israeli (hatua hizi mbili za kazi zikiwa Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema), na Nimekuwa Nikitekeleza hatua mbili zaidi za kazi (Enzi ya Neema na Enzi ya Ufalme) katika nchi nyingine zote nje ya Israeli. Nitafanya kazi ya ushindi kati ya Mataifa, na hivyo kuitamatisha enzi. Mwanadamu akiniita Yesu Kristo kila wakati, lakini hajui kuwa Nimeianza enzi mpya katika siku za mwisho na Nimeanza kazi mpya, na mwanadamu akiendelea kungoja kwa upumbavu kuwasili kwa Yesu Mwokozi, basi Nitawaita watu kama hao wale wasioniamini; wao ni watu wasionijua Mimi, wanaojifanya kuwa waumini. Je, watu kama hao wanaweza kushuhudia kufika kwa Yesu Mwokozi kutoka mbinguni? Wanachongoja si kufika Kwangu, bali ni kufika kwa Mfalme wa Wayahudi. Hawatamani sana Mimi niiangamize kabisa dunia hii chafu ya zamani, lakini badala yake wanatamani sana kurudi kwa Yesu kwa mara ya pili, ambapo watakombolewa—wanamtazamia Yesu kuwakomboa wanadamu wote mara nyingine kutoka nchi hii iliyochafuliwa na isiyo na haki. Watu kama hao watawezaje kuwa wale wanaoikamilisha kazi Yangu katika siku za mwisho? Matamanio ya mwanadamu hayawezi kutimiza mapenzi Yangu ama kutimiza kazi Yangu, kwani mwanadamu huheshimu au kuthamini tu kazi ambayo Nimeifanya hapo awali, bila kujua ya kwamba Mimi ni Mungu Mwenyewe ambaye ni mpya siku zote na si mzee kamwe, na anajua tu kwamba Mimi ni Yehova, na Yesu, bila habari yoyote kwamba Mimi ndimi Yule wa siku za mwisho ambaye Atawatamatisha binadamu. Yote ambayo wanadamu anatamani na kujua yanatoka katika dhana yake mwenyewe, na ni yale tu ambayo anaweza kuyaona kwa macho yake mwenyewe. Hayako sambamba na kazi Ninayoifanya, bali hayatangamani nayo. Kama kazi Yangu ingefanywa kulingana na mawazo ya mwanadamu, basi ingeisha lini? Mwanadamu angeingia katika pumziko lini? Nami Ningewezaje kuingia katika siku ya saba, Sabato? Ninafanya kazi kulingana na mpango Wangu na kulingana na kusudi Langu—si kulingana na nia za mwanadamu.