Sura ya 13

Dhamira Zangu kadhaa zimefichwa ndani ya matamshi ya sauti Yangu. Ila mwanadamu hajui na hafahamu chochote kuhusu haya, huku akiendelea kuyapokea na kuyafuata maneno Yangu kutoka nje, bila kung’amua roho Yangu na kuelewa mapenzi Yangu kutoka ndani ya maneno Yangu. Hata ingawa Nimeyaweka maneno Yangu wazi, kuna yeyote aliyeelewa? Nilitoka Sayuni Nikaja miongoni mwa wanadamu. Kwa sababu Nimejivisha ubinadamu wa kawaida na ngozi ya mwanadamu, watu hulitambua umbo Langu tu kwa nje—ila hawatambui uhai uliomo ndani Yangu, wala hawatambui Mungu Roho, wanajua tu mtu wa mwili. Je, yawezekana kuwa Mungu halisi Mwenyewe hana thamani kwenu kujaribu kumfahamu? Yawezekana kuwa Mungu halisi Mwenyewe hana thamani kwenu kujaribu “kumhakiki kwa makini”? Nachukizwa na upotovu wa ukoo mzima wanadamu, lakini Nauonea imani unyonge wao. Vilevile Nashughulikia tabia ya zamani ya wanadamu. Kama mmoja wa watu Wangu katika Uchina, nyinyi si sehemu ya ukoo wa binadamu? Miongoni mwa watu Wangu wote, na miongoni mwa wanangu wote, yaani, miongoni mwa wale Niliowachagua kutoka kwa wanadamu wote, nyinyi ni wa kundi la chini zaidi. Kwa sababu hii, Nimegharamika kwa nguvu nyingi zaidi kwenu, na juhudi nyingi. Je, bado hamyathamini maisha ya baraka mnayofurahia leo? Je, bado mnafanya mioyo yenu kuwa migumu na kuasi dhidi Yangu na kuenenda katika mipangilio yenu wenyewe? Isingekuwa kwa ajili ya huruma na upendo Wangu, binadamu wote wangekuwa wameshakuwa mateka wa Shetani na kugeuka kuwa “mafunda matamu” katika kinywa chake. Leo hii, miongoni mwa binadamu wote, wale wanaotumia rasilimali kwa dhati kwa ajili Yangu na wale wanaonipenda kwa dhati ni adimu sana kiasi cha kuwahesabu kwa vidole vya mkono mmoja. Yawezekana kuwa jina “watu Wangu” limekuwa miliki yenu binafsi? Je, dhamiri yako imeingia ubaridi? Je, unafaa kweli kuwa mtu Ninayehitaji? Kwa kutafakari kuhusu zamani, halafu sasa, ni nani kati yenu ameufurahisha moyo Wangu? Ni nani kati yenu ameonyesha kutaka kujihusisha kwa kweli kwa nia Zangu? Kama Mimi Singewazindua, bado msingeamka, lakini, mngeendelea kuwa kama mlioganda, na tena, kana kwamba katika hali ya kubumbwaa.

Katikati ya mawimbi mabaya, mwanadamu huiona ghadhabu Yangu; katika dhoruba na mawingu meusi, wanadamu huogopeshwa kiasi cha kuwa na wazimu, wasijue pa kukimbilia, kana kwamba radi na mvua zitawasomba. Kisha, baada ya kupita kwa dhoruba ya theluji, hali zao zinakuwa tulivu na zenye furaha wanavyopendezwa na urembo wa mandhari ya asili. Lakini, katika wakati huo, ni nani kati yao amewahi kushuhudia mapenzi Yangu yasiyo na kikomo Niliyo nayo kwa binadamu? Katika mioyo yao ni umbo Langu tu, ila si kiini cha Roho Wangu: Yawezekana kwamba mwanadamu hanikatai hadharani? Tufani ikishapita wanadamu wote huwa kama walitengezwa upya, kana kwamba, kufuatia usafishaji kupitia taabu, wamepata mwangaza na uhai. Je, hamkuwa na bahati njema kufika leo baada ya kupitia mapigo yote Niliyowapa? Lakini leo ikiisha na kesho kuwadia, mtaweza kuendelea kudumisha utakatifu uliofuata mvua hiyo? Mtaweza kuendelea kuwa na moyo wa ibada uliofuata usafishaji wenu? Mtaendelea kuwa na utiifu wa leo? Ibada yenu yaweza kuendelea kuwa imara au kubadilika? Kwa hakika hili si sharti lililo nje ya uwezo wa mwanadamu. Ninaishi na wanadamu siku baada ya siku Nikitenda pamoja na wanadamu, miongoni mwa wanadamu, ila hapana hata mmoja aliyegundua hili. Isipokuwa uongozi wa Roho Wangu, ni nani kati ya ukoo mzima wa wanadamu bado angekuwepo katika enzi hii? Yawezekana Ninatia chuku Ninaposema kuwa Naishi na kutenda miongoni mwa wanadamu? Zamani Nilisema kuwa “Niliwaumba binadamu, na kuwaongoza binadamu wote, na kuwaamuru binadamu wote”; hili halikuwa kweli? Inawezekana kuwa uzoefu wenu wa haya mambo ni finyu? Kauli ya “mtendaji-huduma” inafaa kukutosha kugharamia juhudi zenu maishani mkieleza kwa undani. Bila uzoefu halisi, mwanadamu hawezi kunifahamu, hangeweza kuja kunifahamu kupitia katika maneno Yangu. Hata hivyo, leo Nimekuja mwenyewe miongoni mwenu—hili halitakuwa lenye manufaa kwa kuelewa kwenu? Yawezekana kwamba kupata mwili Kwangu vilevile si ukombozi kwenu? Nisingeshuka kuja kwa mwanadamu Mimi binafsi, ukoo wote wa binadamu ungekuwa umeingiliwa na Shetani na kuwa mali yake, kwa sababu unachokiamini ni sura ya Shetani na hakihusiani na Mungu Mwenyewe kwa njia yoyote. Si huu ni ukombozi Wangu?

Shetani anapokuja mbele Yangu, sitetemeki kwa kuuogopa ukali wake, wala kumuogopa kwa sababu ya ubaya wa sura yake; Ninampuuza tu. Shetani anaponijaribu, Ninauona ujanja wake na kumfanya atoweke kwa haya na aibu. Shetani anapopigana na Mimi na kujaribu kunipokonya wateule Wangu, Ninapigana vita na yeye katika mwili Wangu; na katika mwili Wangu Nawakimu na kuwaongoza watu Wangu ili wasianguke na kupotea, na Nawaongoza katika kila hatua ya safari. Na Shetani anapong’atuka kwa kushindwa, Nitakuwa nimetukuka na watu Wangu watakuwa wamenitolea ushuhuda mzuri na mkubwa. Kwa hivyo, Nitachukua ninavyotumia kama foili[a] katika mpango Wangu wa usimamizi na kuvitupilia mbali hatimaye katika shimo lisilo na mwisho. Huu ndio mpango Wangu; hii ndiyo Kazi Yangu. Katika maisha yenu, ipo siku itakuja ambayo utakumbana na hali kama hii: Je, utakubali bila kusita kushikwa mateka na Shetani, au utaniruhusu Nikuokoe? Haya ndiyo majaliwa yako mwenyewe, na sharti uzingatie kwa makini.

Maisha katika ufalme ni maisha ya watu na Mungu Mwenyewe. Binadamu wote wako katika ulinzi Wangu na wote wako vitani dhidi ya joka kuu jekundu. Ili kushinda hili pambano la mwisho, ili kulimaliza kabisa hili joka kuu jekundu ni sharti watu wote wajitolee asili zao kabisa Kwangu katika ufalme Wangu. “Ufalme” unaozungumziwa hapa unaashiria maisha ambayo mtu anaishi chini ya uongozi wa uungu, ambamo Mimi ni mchungaji wa wanadamu wote, ambao wanakubali mafundisho Yangu moja kwa moja ili kwamba maisha ya binadamu wote, ingawa yupo duniani, yawe kama yu mbinguni—utambuzi wa kweli wa maisha ya mbingu ya tatu. Ingawa Niko katika mwili Wangu, Sikumbani na upungufu wa kimwili. Mara nyingi Nimekuja miongoni mwa wanadamu kusikiliza maombi, na mara nyingi Nimefurahia sifa zao ninapotembea miongoni mwao; japo wanadamu hawajaugundua uwepo Wangu, bado Naendelea na kazi Yangu kwa njia hii. Katika makao Yangu, ambayo ni sehemu Nilipojificha, hata hivyo, katika haya makao Yangu, Nimewashinda maadui Wangu wote; katika makao Yangu, Nimepata uzoefu wa kuishi duniani; katika makao Yangu, Ninalichunguza kila neno na tendo la mwanadamu, na kuchungulia na kuongoza wanadamu wote. Binadamu wangejihusisha na dhamira Yangu, hivyo kuuridhisha moyo Wangu na kunifurahisha, kwa hakika Ningewabariki wanadamu wote. Hili silo Ninalolikusudia kwa binadamu?

Mwanadamu akiwa kwenye usingizi mzito, ni kwa mapigo ya radi Yangu tu ndipo wanaweza kuzinduka kutoka ndotoni mwao. Na wafunguapo macho yao, wengi huumizwa machoni na mwanga huu baridi, hadi kwa kiwango kwamba wanapoteza mwelekeo, na kushindwa kutambua watokako na waelekeako. Watu wengi hupigwa na mwale huu kama wa mshale na kama matokeo huanguka kwenye rundo chini ya dhoruba, na miili yao kusombwa na mafuriko, bila kuacha nyuma dalili yoyote. Katika mwangaza, manusura hatimaye huweza kuuona uso Wangu kwa uwazi zaidi, na hapo ndipo hugundua kitu kuhusu umbo Langu la nje, kwa kiasi kwamba wao hawawezi kuthubutu kuniangalia usoni ana kwa ana, wakihofu pakubwa kuwa Nitailetea tena miili yao kuadibu Kwangu na laana. Watu wengi sana hulia kwa sauti na kwa uchungu mwingi; wengi sana hukata tamaa; wengi sana husababisha mito na damu yao; wengi huwa miili inayoelea huku na kule bila mwelekeo; watu wengi sana, wanapopata sehemu yao katika mwangaza, huhisi uchungu wa mioyo yao ghafla na kulia machozi kwa ajili ya miaka yao ya kukosa furaha. Watu wengi sana, kwa msukumo wa mwangaza huu wa kuogofya hukiri uchafu wao na kuamua kujibadilisha; wengi kwa kuwa wamepofushwa wamepoteza hamu ya kuishi na hatimaye hawawezi kamwe kuuona huu mwangaza na kwa hivyo kukwama, wakisubiri mwisho wao. Na ni watu wengi sana huanza safari ya maisha yao na, chini ya uongozi wa mwanga huu, kwa bashasha wakitumainia kesho. … Leo hii ni nani miongoni mwa binadamu hayumo katika hali sawa na hii? Ni nani hayumo katika mwangaza Wangu? Hata kama wewe ni mwenye nguvu, au hata kama wewe ni mnyonge, unawezaje kuepuka ujio wa mwanga Wangu?

Machi 10, 1992

Tanbihi:

a. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.

Iliyotangulia: Sura ya 12

Inayofuata: Sura ya 14

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp