Sura ya 36

Kila kitu kinapangwa kwa mkono Wangu. Nani anathubutu kufanya anavyopenda? Nani anayeweza kukibadilisha kwa urahisi? Watu huelea hewani, wakienda mbele kama vumbi linavyokwenda, nyuso zao zimejaa uchafu, kuwafanya wasivutie kutoka utosini hadi wayoni. Mimi huangalia kutoka miongoni mwa mawingu na moyo mzito: Kwa nini mwanadamu, ambaye wakati mmoja alijaa uhai, amegeuka kuwa namna hii? Na kwa nini hajui jambo hili, na kutohisi jambo hili? Kwa nini “anajiachilia” na kujiruhusu kufunikwa kwa uchafu? Huo ndio ukosefu wake wa upendo na heshima kwake. Kwa nini mwanadamu daima huepuka Ninachouliza? Je, Mimi ni mkatili na mnyama kwake kweli? Je, Mimi kweli ni dhalimu na Asiye na huruma? Hivyo kwa nini watu daima hunitazama kwa macho makali? Kwa nini daima wao hunichukia? Je, Nimewaleta mpaka ukingoni? Mwanadamu hajawahi kugundua chochote katika kuadibu Kwangu, kwani hafanyi chochote ila kushika nira inayozunguka shingo kwa mikono miwili, macho yake mawili yakiwa yamekodolewa Kwangu, kana kwamba anamwangalia adui kwa makini—na wakati huu tu ndio Nahisi vile amedhoofishwa. Ni kwa sababu ya hili ndio Nasema hakuna yeyote aliyewahi kusimama imara katikati ya majaribio. Je, kimo cha mwanadamu hakiko hivyo kabisa? Je, Nahitaji kumwambia tarakimu za “vipimo” vyake? “Urefu” wa mwanadamu sio mkubwa zaidi kuliko ule wa mnyoo mdogo anayejinyonganyonga juu ya ardhi, na “kifua” chake ni upana sawa tu na wa nyoka. Katika hili, mimi Simdunishi mwanadamu—je, hizi sizo tarakimu kamili za kimo chake? Je, Nimemshusha daraja mwanadamu? Mwanadamu ni kama mtoto anayechezacheza. Kuna hata nyakati ambapo anacheza na wanyama, lakini bado anabaki na furaha; na yeye ni kama paka, akiishi maisha bila kujali au wasiwasi. Labda ni kwa sababu ya mwelekeo wa Roho, au jukumu la Mungu mbinguni, ndio Najisikia mchovu sana kuhusu maisha ya ubadhirifu ya watu duniani. Kwa sababu ya maisha ya mwanadamu—ambayo ni kama ya kupe—“Shauku” Yangu katika maneno “maisha ya binadamu” imeongezeka kwa kiasi fulani, na hivyo Nimekuwa “mwingi wa heshima” zaidi kidogo kwa maisha ya binadamu. Kwa maana inaonekana kwamba mwanadamu pekee ndiye anaweza kuunda maisha ambayo yana maana, wakati ambapo Siwezi kufanya hivyo. Kwa hivyo Naweza tu kwenda kwenye “milima,” kwa maana Siwezi kupitia na kuchunguza shida miongoni mwa wanadamu. Lakini mwanadamu ananishurutisha kwa haraka—Sina budi! Ninaweza tu kutii mipango ya mwanadamu, kufupisha uzoefu pamoja naye na kupitia maisha ya binadamu pamoja naye. Mbinguni, wakati mmoja Nilitalii jiji lote, na chini ya mbinguni, wakati mmoja Nilitalii nchi zote. Lakini hakuna mtu aliyewahi kunitambua, walisikia tu sauti ya mwendo Wangu Nilipokuwa Natembea kote. Machoni pa watu, Mimi huja na kwenda Nisionekane tena. Ni kama kwamba Nimekuwa sanamu isiyoonekana ndani ya mioyo yao, lakini watu hawaamini hivyo. Yawezekana kuwa yote haya si ukweli uliokiriwa na kinywa cha mwanadamu? Wakati huu, ni nani asiyekubali kwamba anapaswa kuadibiwa? Je, watu bado wangejiamini kabla ya ushahidi thabiti?

Nafanya mapatano ya biashara miongoni mwa wanadamu, Naufuta uchafu wake wote na udhalimu wake, na hivyo “Namtengeneza” ili apate kuupendeza moyo Wangu. Lakini ushirikiano wa mwanadamu ni wa lazima kwa hatua hii ya kazi, kwa sababu yeye daima huchupa na kuruka kote kama samaki ambaye amevuliwa hivi sasa. Kwa hiyo ili kuzuia ajali zozote, Niliwaua samaki wote waliokuwa wamevuliwa, baada ya hilo samaki hao wakawa watiifu, na hawakuwa na malalamiko hata kidogo. Ninapomhitaji mwanadamu, daima huwa amejificha. Ni kana kwamba hajawahi kamwe kuona maonyesho ya kustaajabisha, kana kwamba alizaliwa mashambani na hajui chochote kuhusu mambo ya mjini. Naongeza hekima yangu kwa sehemu za mwanadamu ambazo zina upungufu, na kumfanya anijue Mimi; kwa sababu mwanadamu ni maskini sana, Mimi binafsi huja miongoni mwa wanadamu na kuwapa “njia ya kupata utajiri,” na kumfanya afumbue macho yake. Katika hili, je, Simwokoi? Je, hii si huruma Yangu kwa mwanadamu? Je, upendo ni kutoa bila masharti? Je, basi chuki ni kuadibu? Nimemwelezea mwanadamu kwa taswira tofauti, lakini analichukulia hili kama maneno na kanuni tu. Ni kama maneno Yangu ni bidhaa za daraja la pili, ambazo huuzwa kama vitu visivyo na thamani tena katika mikono ya mwanadamu. Hivyo, wakati Ninapowaambia watu kuwa dhoruba kubwa inakuja kumeza kijiji cha mlima, hakuna mtu anayefikiri chochote juu yake, ni wachache tu wanaohamisha nyumba zao, mioyo yao ikiwa na shaka. Wengine hawahami, kama kwamba hawajali, kama kwamba Mimi ni mbayuwayu kutoka angani—hawaelewi chochote kati ya yale Nisemayo. Ni wakati ambapo tu milima hupinduliwa na dunia kutenganishwa mbalimbali ndio watu hufikiria kuhusu maneno Yangu, wakati huo tu ndio wao huamshwa kutoka kwa ndoto zao, lakini wakati umefika tayari, wamemezwa katika mafuriko makuu, maiti yao yaelea juu ya maji. Kuona taabu ulimwenguni, Nashusha pumzi kwa msiba wa mwanadamu. Nilitumia muda mwingi, na kulipa gharama kubwa, kwa ajili ya majaliwa ya mwanadamu. Katika mawazo ya watu, Sina michirizi ya machozi—lakini Mimi, “dubwasha” huyu asiye na michirizi ya machozi, Nimelia machozi mengi kwa ajili ya mwanadamu. Mwanadamu, hata hivyo, hajui lolote kuhusu hili, anacheza tu na vidude vya kuchezea watoto mikononi mwake duniani, kama kwamba Siishi. Hivyo, katika hali za leo, watu hubakia sugu na wajinga, bado “wameganda” katika sehemu za nyumba zilizo chini ya ardhi, kama kwamba bado wanalala pangoni. Kuona vitendo vya mwanadamu, chaguo Langu la pekee ni kuondoka …

Machoni pa watu, Nimefanya mengi ambayo ni mazuri kwa mwanadamu, na hivyo wananitazama kama mfano mwema wa enzi ya sasa. Lakini hawajawahi kamwe kunifikiria kama Mtawala wa majaliwa ya mwanadamu na Muumba wa vitu vyote. Ni kama kwamba hawanielewi. Ingawa wakati fulani watu walitangaza “Ufahamu udumu,” hakuna yeyote ambaye ametumia muda mwingi kuchambua neno ‘ufahamu,’ kuonyesha kwamba watu hawana hamu ya kunipenda. Katika nyakati za leo, watu hawajawahi kunithamini, Sina nafasi ndani ya mioyo yao. Je, wataweza kuonyesha upendo wa kweli Kwangu katika siku zijazo za mateso? Haki ya mwanadamu inabaki kitu bila umbo, kitu ambacho hakiwezi kuonekana wala kuguswa. Nitakacho ni moyo wa mwanadamu, kwa kuwa katika mwili wa mwanadamu moyo ndio wa thamani sana. Je, matendo Yangu hayafai kulipwa kwa moyo wa mwanadamu? Kwa nini watu hawanipi mioyo yao? Kwa nini daima huikumbatia kwa vifua vyao wenyewe, wasitake kuiwacha? Je, moyo wa mwanadamu unaweza kuhakikisha amani na furaha katika maisha yote ya watu? Kwa nini, wakati Ninapotaka vitu kutoka kwa watu, wao daima kiasi kidogo cha vumbi kutoka ardhini na kulirusha Kwangu? Je, huu ni mpango wa hila wa mwanadamu? Ni kama kwamba anajaribu kumdanganya mpita njia ambaye hana mahali popote pa kwenda, akimshawishi arudi nyumbani kwake, ambako anageuka kuwa mbaya na kumuua. Watu wametaka pia kufanya mambo kama hayo Kwangu. Ni kama kwamba wao ni chakari ambaye atamuua mtu bila kujali, kama kwamba wao ni mfalme wa pepo, ambaye asili yake ya pili ni kuua watu. Lakini sasa watu huja mbele Yangu, bado wakitaka kutumia njia hizo—lakini wana mipango yao, na Nina mipango Yangu ya kupinga. Ingawa watu hawanipendi, Ningewezaje kukosa kuifanya mipango yangu ya kupinga wazi kwa mwanadamu wakati huu? Nina ujuzi usio na kikomo, usiopimika katika kumshughulikia mwanadamu; kila sehemu yake Hushughulikiwa binafsi na Mimi, na kutengenezwa binafsi na Mimi. Hatimaye, Nitamfanya mwanadamu avumilie maumivu ya kujitenga na kile anachopenda, na kumfanya atii mipango Yangu, na wakati huo, watu watalalamikia nini? Je, yote Nifanyayo si kwa ajili ya mwanadamu? Katika nyakati zilizopita, Sikuwahi kumwambia mwanadamu hatua za kazi Yangu—lakini leo, katika wakati usiofanana na uliopita, kwa sababu maudhui ya kazi Yangu ni tofauti, Nimewaambia watu juu ya kazi Yangu mapema ili kuwazuia kuanguka chini kutokana na hili. Je, hii siyo chanjo ambayo Nimeidunga sindano ndani ya mwanadamu? Kwa sababu yoyote ile, watu hawajawahi kuzingatia maneno Yangu kwa makini; ni kama kwamba kuna njaa ndani ya matumbo yao na si wagumu kupendeza kuhusu kile wanachokula, ambacho kimefanya matumbo yao kuwa dhaifu. Lakini watu huchukua “gimba yao bora” kuwa rasilimali na hawatambui maonyo ya “daktari.” Kwa kuona ukaidi wao, Najikuta Nikisikitika kwa ajili ya mwanadamu. Kwa sababu watu si wakomavu, na bado hawana uzoefu wa maisha ya binadamu, hawana hofu; mioyoni mwao, maneno “maisha ya binadamu” hayapo, hawayajali, na huchoka tu na maneno Yangu, kama kwamba Nimekuwa mwanamke mzee mwenye kuparaganyaparaganya. Kwa jumla, kwa vyovyote vile, Natumai kwamba watu wanaweza kuelewa moyo Wangu, kwa maana Mimi Sina hamu ya kumtuma mwanadamu katika nchi ya kifo. Natumai kwamba mwanadamu anaweza kuelewa ni nini hisia Zangu kwa wakati huu, na kujali mzigo Ninaobeba hasa wakati huu.

Aprili 26, 1992

Iliyotangulia: Sura ya 35

Inayofuata: Sura ya 37

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp