Sura ya 33

Katika nyumba Yangu, kulikuwapo wakati mmoja wale waliolisifu jina Langu takatifu, ambao walifanya kazi bila kuchoka ili utukufu Wangu duniani ungejaza anga. Kwa sababu ya hili, Nilifurahi sana, moyo Wangu ulijawa na furaha—lakini nani angeweza kufanya kazi badala Yangu, akiacha usingizi usiku na mchana? Azimio la mwanadamu mbele Yangu hunipa raha, lakini uasi wake huchochea hasira Yangu, na hivyo, kwa sababu mwanadamu hawezi kamwe kuzingatia wajibu wake, huzuni Yangu kwa ajili yake inakua kubwa zaidi. Kwa nini watu daima hawawezi kujitolea Kwangu? Kwa nini daima wao hujaribu kubishana na Mimi? Mimi ni msimamizi mkuu wa kituo cha biashara? Kwa nini Mimi hutimiza kwa moyo kamili kile ambacho watu hudai kutoka Kwangu, lakini Nitakacho kutoka kwa mwanadamu hakitimii? Inawezekana kuwa mimi Sina maarifa katika njia za biashara, lakini mwanadamu anayo? Kwa nini watu daima hunidanganya kwa mazungumzo ya ushawishi na ya kusifu mno? Kwa nini watu kila mara huja wakibeba “zawadi,” wakiomba njia ya kurudi ndani? Je, hili ndilo Nililomfundisha mwanadamu kufanya? Kwa nini watu hufanya mambo hayo haraka na kwa unadhifu? Kwa nini watu kila mara huhamasishwa kunidanganya? Ninapokuwa kati ya wanadamu, watu hunitazama kama kiumbe aliyeumbwa; Ninapokuwa katika mbingu ya tatu, wananiona kama Mwenyezi, Anayetawala vitu vyote; wakati Niko angani, wananiona kama Roho ambaye hujaza vitu vyote. Kwa jumla, hakuna mahali panaponistahili katika mioyo ya watu. Ni kama kwamba Mimi ni mgeni asiyekaribishwa, watu wananichukia sana, na hivyo wakati Ninachukua tiketi na kuchukua kiti Changu, wananifukuza nje, na kusema kwamba hakuna mahali pa Mimi kukaa hapa, kwamba Nimekuja mahali pabaya, na hivyo sina budi ila kuondoka kwa nguvu. Ninaamua kutoshirikiana na mwanadamu tena, kwa kuwa watu wana akili finyu, ukarimu wao ni haba sana. Sitakula kwenye meza moja nao tena, Sitazungumza nao tena duniani. Lakini Ninapozungumza, watu wanashangaa, wanaogopa kwamba Nitaondoka, na kwa hiyo wanaendelea kunikawisha. Nionapo upendo wao, mara moja Nahisi huzuni na upweke ndani ya moyo Wangu kwa kiasi fulani. Watu wanaogopa kwamba Nitawaacha, na hivyo wakati Ninapoachana nao, sauti ya kilio hujaza nchi, na nyuso za watu hufunikwa kwa machozi. Nafuta machozi yao, Nawainua juu tena, na wananitazama Mimi, macho yao ya kusihi inavyoonekana kwa nje ikiniomba Nisiende, na kwa sababu ya “unyofu” wao Niko nao. Lakini ni nani anayeweza kuelewa maumivu yaliyo ndani ya moyo Wangu? Ni nani anayezingatia mambo Yangu yasiyoelezeka? Kwa macho ya watu, ni kama kwamba Sina hisia, na hivyo daima tumekuwa katika familia mbili tofauti. Wangewezaje kuona hisia ya huzuni ndani ya moyo Wangu? Watu hutamani tu raha zao wenyewe, na hawajali mapenzi Yangu, kwa sababu, hadi sasa, watu bado hawajui lengo la mpango Wangu wa usimamizi, na hivyo leo bado husihi kimyakimya—na hili ni la faida gani?

Ninapoishi kati ya wanadamu, Nashikilia nafasi fulani katika mioyo ya watu; kwa kuwa Nimeonekana katika mwili, na watu wanaishi katika mwili wa zamani, wao kila mara hunishughulikia na mwili. Kwa sababu watu wana mwili tu, na hawana vijalizo vingine zaidi, wamenipa “yote waliyo nayo.” Lakini hawajui chochote, wao “hutoa ibada yao” tu mbele Yangu. Ninachovuna ni takataka isiyo na thamani—lakini watu hawafikiri hivyo. Ninapolinganisha “zawadi” walizotoa kwa vitu Vyangu, watu hutambua thamani Yangu mara moja, na wakati huo tu ndio wao huona kutopimika Kwangu. Sijivuni kwa sababu ya sifa zao, lakini Naendelea kuonekana kwa mwanadamu, ili watu wote waweze kunijua kwa ukamilifu. Nionyeshapo uzima Wangu kwao, wao hunitazama kwa macho yaliyokodoa, wakisimama mbele Yangu bila kujongea, kama nguzo ya chumvi. Na Ninapotazama kutokuwa kawaida kwao Mimi huwa na taabu kujizuia kucheka. Kwa sababu wananyosha mkono kuomba vitu kutoka Kwangu, Mimi huwapa vitu vilivyo mkononi Mwangu, nao huvikumbatia, wakivitunza kama mtoto aliyezaliwa hivi sasa, ishara waifanyayo tu mara moja. Ninapobadilisha mazingira ambamo wanaishi, mara moja wao humtupa “mtoto mchanga” upande mmoja na kukimbia na vichwa vyao mikononi mwao. Machoni pa watu, Mimi ni msaada ambao upo bila kujali muda au mahali, ni kama kwamba Mimi ni mhudumu ambaye huja mara tu anapoitwa. Hivyo, watu daima “wamenitegemea,” kama kwamba Nina uwezo usio na kipimo wa kupambana na janga, na hivyo kila mara wameushika mkono Wangu, wakiniongoza kwenye safari kutoka upande mmoja hadi mwingine wa nchi, ili vitu vyote viweze kuona kwamba vina Mtawala, ili mtu yeyote asithubutu kuvidanganya. Nimebaini tangu zamani hila za watu za “mbweha kuchukua utukufu wa chui mwenye milia,” kwa maana wote “wananing’iniza mbwe zao,” wakitaka kufaidika kwa njia ya udanganyifu. Nimebaini tangu zamani mpango wao wenye kudhuru kwa siri, wenye nia mbaya, na ni vile tu Sitaki kuumiza uhusiano wetu. Sileti taabu bila sababu yoyote—hakuna thamani au umuhimu katika hilo. Mimi hufanya tu kazi ambayo ni lazima kwa sababu ya udhaifu wa watu; kama sivyo, Ningewageuza majivu na kutowaruhusu kuwapo tena. Lakini kazi Nifanyayo ina maana, na hivyo Simwadibu mwanadamu kwa urahisi. Ni kwa sababu hii ndiyo watu daima wameipa miili yao uhuru. Hawafuati mapenzi Yangu, lakini wamenirairai daima mbele ya kiti Changu cha hukumu. Watu ni wajasiri sana: Wakati vifaa vyote vya mateso vinapowatishia, hawawi na shaka hata kidogo. Kabla ya ukweli, wanasalia kutoweza kutoa ukweli wowote, na hawafanyi chochote ila kwa ukaidi hunipinga. Ninapowauliza kuleta yote yaliyo na uchafu, bado wananionyesha mikono miwili mitupu—wengine wangewezaje kukosa kutumia hili kama “mfano”? Ni kwa kuwa imani ya watu ni kubwa mno ndio wao ni “wa kusifiwa.”

Nimeanza kazi Yangu kutoka upande mmoja hadi upande mwingine wa ulimwenguni; watu wa ulimwengu huamka ghafla, na kutembea wakizunguka kiini, ambayo ni kazi Yangu, na “Ninaposafiri” ndani yao, wote huepuka utumwa wa Shetani, na hawateswi katikati ya mateso ya Shetani. Kwa sababu ya majilio ya siku Yangu, watu hujaa furaha, huzuni ndani ya mioyo yao hutoweka, mawingu ya huzuni angani hugeuka kuwa oksijeni katika hewa na kuelea hapo, na wakati huu, Nafurahia furaha ya umoja na mwanadamu. Vitendo vya mwanadamu hunipa kitu cha kufurahia, na hivyo Sisikitishwi tena. Na, kuandamana na majilio ya siku Yangu, vitu vya dunia amabavyo vina nguvu, vitu vyote duniani huwa hai tena, na vinanikubali Mimi kama asili ya kuwepo kwao, kwa sababu Mimi Husababisha vitu vyote kuangaza na uzima, na hivyo, pia, Navisababisha kutoweka kimyakimya. Hivyo, vitu vyote husubiri amri kutoka kwa kinywa Changu, na hupendezwa na yale ambayo Ninafanya na kusema. Kati ya vitu vyote, Mimi ni Aliye Juu Zaidi—lakini Mimi pia Naishi miongoni mwa watu wote, na kutumia matendo ya watu kama maonyesho ya uumbaji Wangu wa mbingu na dunia. Wakati watu wanatoa sifa kubwa mbele Yangu, Mimi Husifiwa miongoni mwa vitu vyote, na hivyo maua duniani huwa mazuri zaidi chini ya jua kali, nyasi hustawi zaidi, na mawingu angani huonekana samawati zaidi. Kwa sababu ya sauti Yangu, watu hukimbia huku na kule; leo nyuso za watu katika Ufalme Wangu zimejaa furaha, na maisha yao yanakua. Ninafanya kazi miongoni mwa wateule Wangu wote, na Siruhusu kazi Yangu kutiwa doa na mawazo ya binadamu, kwani Mimi binafsi hutekeleza kazi Yangu Mwenyewe. Ninapofanya kazi, mbingu na dunia na kila kitu ndani yake hubadilika na kufanywa upya, na wakati Ninapokamilisha kazi Yangu, mwanadamu hufanywa upya kabisa, haishi tena katika huzuni kwa sababu ya kile Ninachouliza, kwani sauti za furaha zinaweza kusikika kutoka upande mmoja hadi upande mwingine wa dunia, na Mimi Huchukua nafasi hii kutoa miongoni mwa wanadamu baraka ambazo Mimi huwapa. Wakati Mimi ni Mfalme wa ufalme, watu huniogopa, lakini wakati Mimi ni Mfalme miongoni mwa wanadamu, na kuishi miongoni mwa wanadamu, watu hawafurahishwi nami, kwa maana dhana zao juu Yangu ni za kuhuzunisha sana, kiasi kuwa zimetiwa ndani sana kiasi cha kuwa ngumu kuondoa. Kwa sababu ya onyesho la mwanadamu, Nafanya Kazi Yangu, ambayo inafaa, na wakati Ninapoinuka juu mbinguni na kuachilia ghadhabu Yangu juu ya mwanadamu, maoni mbalimbali ya watu kunihusu mara moja hugeuka majivu. Nawaomba kunena dhana zao kadhaa zaidi Kwangu, lakini wamepigwa na bumbuwazi, kama kwamba hawana chochote, na kama kwamba wao ni wanyenyekevu. Kadri Ninavyoishi katika dhana za watu, ndivyo wanavyokuja kunipenda zaidi, na kadri Ninavyoishi nje ya dhana za watu, ndivyo wanavyozidi kunikwepa, na wana maoni zaidi kunihusu, kwani, tangu wakati Nilipoumba dunia mpaka leo, daima Nimeishi katika dhana za watu. Ninapokuja miongoni mwa wanadamu leo, Mimi huondoa dhana zote za watu, na hivyo watu hukataa tu—lakini Nina mbinu zinazofaa za kushughulikia dhana zao. Watu wasiwe na wahaka au wasiwasi; Nitawaokoa wanadamu wote kwa mbinu Zangu Mwenyewe, na kuwafanya watu wote wanipende, na kuwaruhusu kufurahia baraka Zangu mbinguni.

Aprili 17, 1992

Iliyotangulia: Sura ya 32

Inayofuata: Sura ya 34

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp