Sura ya 24

Kuadibu kwangu kunawajia watu wote, lakini pia kunakaa mbali na watu wote. Maisha yote ya kila mtu yamejaa upendo na pia chuki Kwangu, na hakuna mtu ambaye amewahi kunijua na kwa hivyo mtazamo wa mwanadamu Kwangu ni wa sitasita, na hauna uwezo wa kuwa kawaida. Lakini Nimekuwa Nikimlea na kumchunga mwanadamu na ni kwa sababu ya upumbavu wake ndiyo maana hana uwezo wa kuona matendo Yangu yote na kuelewa nia Zangu. Mimi Ndiye Ninayeongoza katika mataifa yote, na ndiye Mkubwa Zaidi kwa watu wote; kwa ufupi ni kwamba mwanadamu hanijui Mimi. Kwa miaka mingi Nimeishi na mwanadamu na kujionea Maisha katika dunia ya mwanadamu, lakini amekuwa Akinipuuza na kunichukulia kama kiumbe kutoka ulimwengu wa nje ya dunia. Kwa sababu hii, kutokana na tofauti za tabia na lugha, watu Hunichukulia Mimi kama mgeni barabarani. Nguo Zangu, huenda ikawa, pia ni za kipekee, hata kumfanya mwanadamu kukosa imani ya kunikaribia. Ni wakati huo ndio naona upweke wa maisha ya mwanadamu, na wakati huo tu ndio Ninapata ufafanuzi wa dhuluma katika dunia ya mwanadamu. Ninatembea katikati ya wapita njia, Nikiangalia nyuso zao zote. Ni kama kwamba wanaishi ndani ya maradhi, ambayo yanajaza nyuso zao na huzuni, na miongoni mwa adhabu, inayozuia kuachiliwa kwao. Mwanadamu hujitia pingu mwenyewe na kuonyesha adabu. Watu wengi hujenga hisia za uwongo juu yao mbele Yangu ili Niwaunge mkono, na watu wengi hujifanya makusudi kuwa wa kuhuzunisha mbele Yangu ili waweze kupata usaidizi Wangu. Nyuma Yangu, watu wote wananirairai na kuniasi. Je, Mimi sio wa kweli? Je, huu si mkakati wa mwanadamu ili aweze kuishi? Ni nani ambaye ameweza kuishi kwa kunidhihirisha katika Maisha yake? Nani ambaye ameweza kunitukuza miongoni mwa wengine? Nani amewahi kuwajibika mbele ya Roho? Nani ambaye amesimama imara kwa ushuhuda wake Kwangu mbele ya Shetani? Ni nani ameweza kuongezea ukweli kwa hulka ya “uaminifu” walio nao Kwangu? Ni nani amewahi kutupwa nje na joka kubwa jekundu kwa sababu Yangu? Watu wametupa kura zao kwa shetani na sasa wanatembea naye kwenye matope, wamekuwa wataalam kwa Kunipinga, na wamekuwa waanzilishi wa upinzani kuja Kwangu, na ni “wanafunzi waliobobea” katika njia zao zisizo za dhati katika kunishughulikia. Kwa ajili ya hatima yake mwenyewe, mwanadamu anatafuta hapa na pale duniani, na Ninapomwita, anabaki kutokuwa na uwezo wa kuhisi thamani Yangu kubwa na anaendelea kuwa na Imani katika kujitegemea, asiwe mzigo kwa wengine. “Matarajio” ya mwanadamu ni ya thamani, lakini hakujawahi kuwa na matarajio ya yeyote ambayo yametimiza alama zote. Yote yanabomoka mbele Yangu, na kuporomoka bila sauti.

Kila siku Ninaongea, na kila siku Nafanya mambo mapya pia. Ikiwa mwanadamu hawezi kutumia nguvu zake zote, basi atakuwa na ugumu kusikia sauti Yangu na atapata ugumu kuona uso wangu. Mpendwa Anaweza kuwa mzuri sana, na mazungumzo Yake kuwa yenye upole mkubwa sana, lakini mwanadamu hana uwezo wa kutazama kwa urahisi sura Yake tukufu na kusikia sauti Yake. Katika miaka yote, hakuna ambaye amewahi kuweza kutazama sura Yangu kwa urahisi. Niliwahi kuongea na Petro na Nikajitokeza kwa Paulo, na hakuna mwingine—isipokuwa Waisraeli—ambaye kweli amewahi kuona uso Wangu. Leo, nimekuja Mimi Mwenyewe kati ya mwanadamu kuishi pamoja na yeye. Je, hiki hakihisi kuwa kitu nadra na cha thamani kwenu? Je, hamtamani kufanya matumizi bora ya muda wenu? Je, mnataka jambo hili liwapite kwa njia hii? Inawezekana muda usimamishwe ghafula katika mawazo ya watu? Au inawezekana muda urudishwe nyuma? Au inawezekana mwanadamu awe kijana tena? Inawezekana maisha ya leo yenye baraka kuja tena? Simpatii mwanadamu “zawadi” sahihi kwa “ubadhirifu” wake. Mimi huendelea kufanya kazi Yangu tu, nimejitenga na mengine yote na sisimamishi mtiririko wa masaa kwa sababu mwanadamu ana shughuli, au kwa sababu ya sauti ya vilio vyake. Kwa miaka elfu kadhaa, hakuna ambaye ameweza kugawa nguvu Yangu, na hakuna ambaye ameweza kuharibu mpango Wangu wa asili. Nitavuka anga, na kuzunguka miaka, na kuanzisha kiini cha Mpango Wangu mzima juu na miongoni mwa vitu vyote. Hakuna mtu hata mmoja ambaye ameweza kupokea utunzaji maalum kutoka Kwangu au zawadi kutoka mikononi Mwangu, licha ya kwamba wanafungua vinywa vyao na kuomba ili wapate hivi vitu, licha ya kuwa wananyoosha mikono yao, huku wakisahau kila kitu kingine, wanataka hivi vitu kutoka Kwangu. Hakuna hata mmoja wa hawa watu amenisababisha kubadilisha nia Yangu, na wao wote wamesukumwa nyuma na sauti Yangu “isiyo na utu.” Watu wengi bado wanaamini kuwa wao ni “wachanga sana,” na hivyo wanasubiri Niwaonyeshe rehema kubwa, kuwa na huruma kwao kwa mara ya pili, na wanauliza Niwaruhusu kuchukua mlango wa nyuma. Hata hivyo ni jinsi gani Mimi Nitaufanyia mpango Wangu mzaha? Je, Ninaweza kusimasisha dunia isizunguke kwa ajili ya ujana wa mwanadamu, ili aweze kuishi miaka zaidi duniani? Akili ya mwanadamu ni tata, lakini inaonekana kwamba pia kuna vitu ambavyo inakosa. Kwa sababu hii, katika akili ya mwanadamu mara nyingi huonekana “njia za ajabu” za kupinga kazi Yangu kwa makusudi.

Ingawa ni mara nyingi Nimesamehe dhambi za mwanadamu, na kumwonyesha upendeleo wa pekee kwa sababu ya udhaifu wake, mara nyingi pia Nimempa utunzaji sahihi kwa sababu ya ujinga wake. Ni rahisi kuwa mwanadamu hajawahi kujua jinsi ya kufahamu wema Wangu, hadi amezama ndani ya yale anayopitia sasa: amefunikwa katika vumbi, nguo zake zikiwa matambara, nywele zake zimefunika kichwa chake kama magugu yanayokua, uso wake umepakwa masizi, miguu yake imevalishwa viatu valivyojitengenezea yaye mwenyewe, mikono yake kama makucha ya tai aliyekufa, yakining’inia kwa udhaifu katika pande zake. Nikifungua macho Yangu na kutazama, ni kama kwamba mwanadamu amepanda juu kutoka nje ya shimo lisilo na mwisho. Sina budi ila kuwa na hasira: Nimekuwa mvumilivu kwa mwanadamu, ni jinsi gani Nilimruhusu shetani kuja na kwenda kama atakavyo kutoka Ufalme Wangu mtakatifu? Ni jinsi gani nilimruhusu mwombaji kula bure katika nyumba Yangu? Ni jinsi gani nilivumilia kuwa na roho mchafu kama mgeni wa nyumba Yangu? Mwanadamu daima amekuwa “mkali kwake mwenyewe” na “mwenye upole kwa wengine,” ilhali hajawahi angalau hata kidogo kuwa na adabu kuelekea Kwangu, maana Mimi ni Mungu mbinguni, na hivyo Yeye hunichukulia Mimi kwa nia tofauti, na hajawahi kuwa na upendo hata kidogo Kwangu. Ni kama kwamba macho ya mwanadamu ni majanja: Mara tu anapokutana na Mimi, uso wake unabadilika mara moja na anaongeza hisia kidogo kwa uso wake baridi na usio na hisia. Mimi simtilii mwanadamu vikwazo vinavyofaa kwa sababu ya mtazamo wake kuelekea Kwangu, bali Naangalia tu angani kutoka juu ya ulimwengu na kutekeleza kazi Yangu hapa duniani. Katika kumbukumbu ya mwanadamu, sijawahi kuonyesha wema kwa mtu yeyote, lakini sijawahi pia kumtendea vibaya mtu yeyote. Kwa sababu mwanadamu hanihifadhii “kiti kitupu” ndani ya moyo wake, Nisipotahadhari na kukaa ndani yake, ananilazimisha Mimi Nitoke nje bila utaratibu, na kisha anatumia maneno ya kujipendekeza na ubembelezaji ili kufanya visingizio, akisema yeye hana uwezo wa kujitoa mwenyewe kwa ajili ya starehe Yangu. Anapoongea, uso wake mara nyingi hufunikwa na “mawingu ya giza,” kana kwamba madhara yatakuja miongoni mwa wanadamu wakati wowote. Hata hivyo, bado ananiambia Mimi niondoke, bila kuzingatia hatari zinazohusika. Hata kama ninampatia mwanadamu maneno Yangu na joto la kumbatio Langu, yeye anaonekana kuwa hasikii, na hivyo haipatii sauti Yangu muda hata kidogo, na badala yake anashikilia kichwa chake huku akiondoka upesi. Naondoka kwa mwanadamu Nikijihisi Nimesikitishwa kidogo, lakini pia nikiwa Nimeghadhabishwa. Mwanadamu wakati huo anatoweka huku kukiwa na shambulio la upepo mkubwa na mawimbi makuu. Baadaye, Ananililia Mimi, lakini ni jinsi gani yeye angebadili harakati ya upepo na mawimbi? Hatua kwa hatua, dalili zote za mwanadamu zinapotea, mpaka hapatikani mahala popote.

Kabla ya nyakati, Niliangalia nchi zote za ulimwengu kutoka juu mbinguni. Nilipanga shughuli kubwa duniani: uumbaji wa mwanadamu ambaye angependeza moyo Wangu, na ujenzi wa ufalme duniani kama ule wa mbinguni, Nikaruhusu uwezo Wangu kujaza anga na hekima Yangu kuenea kote ulimwenguni. Na hivyo leo, maelfu ya miaka baadaye, Mimi Naendelea na mpango Wangu, lakini hakuna anayejua mpango Wangu au usimamizi wa dunia, wala hawauoni ufalme Wangu duniani. Kwa hivyo, mwanadamu hukimbiza vivuli, na kuja mbele Yangu ili kujaribu kunidanganya, akitaka kulipa “gharama ya kimya” ili apate baraka Zangu za mbinguni. Kwa sababu hii, amechochea hasira Yangu na Ninamletea hukumu, lakini bado hana fahamu. Ni kana kwamba alikuwa anafanya kazi kichinichini, pasi na kutojua kabisa lililokuwa likiendelea katika ulimwengu huku akifuata ndoto na dhamira zake tu. Miongoni mwa watu wote, sijawahi kuona mtu yeyote ambaye anaishi chini ya mwanga Wangu. Wanaishi katika ulimwengu wa giza, na wanaonekana kuzoea kuishi ndani ya giza. Mwanga unapokuja wanakaa mbali, na ni kana kwamba mwanga umevuruga kazi zao; matokeo yake, wanaonekana kuudhika kidogo, ni kama mwanga umeathiri amani yao na kuwaacha bila uwezo wa kulala fofofo. Kwa sababu hii, mwanadamu anakusanya nguvu zake zote na kuuondoa mwanga. Mwanga, pia, unaonekana kukosa ufahamu, na hivyo unaamsha mwanadamu kutoka usingizini, na wakati mwanadamu anaamka, anafunga macho yake, akijawa na hasira. Kwa kiasi fulani ni kama hajafurahishwa na Mimi, lakini katika moyo Wangu najua lengo. Ninaendelea hatua kwa hatua kuimarisha mwanga, kusababisha watu wote kuishi katika mwanga Wangu, ili baada ya muda usiokuwa mrefu wazoee kujihusisha na mwanga, na, zaidi ya hapo, wote wathamini mwanga huo. Kwa wakati huu, ufalme Wangu umekuja miongoni mwa mwanadamu, watu wote wanacheza kwa shangwe na kusherehekea, ghafla dunia inajazwa na furaha, na kimya cha miaka elfu kadhaa chavunjwa kwa kuwasili kwa mwanga …

Machi 26, 1992

Iliyotangulia: Sura ya 23

Inayofuata: Sura ya 25

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp